Script
Save and edit this resource as a Word document.
Utangulizi
Kwanini mada hii ni muhimu kwa msikilizaji?
Kwa sababu wakulima wa maembe wanafaa kujua:
- Wadudu wanaoadhiri matunda ya maembe na athari zao.
- Jinsi ya kutambua wadudu wa maembe.
- Jinsi ya kusimamia na kulinda bustani ili kupunguza mara ambazo wadudu wanavamia bustania la maembe.
- Jinsi ya kuzuia kusambaa kwa wadudu kati ya miembe kwenye bustani.
- Chaguzi zilizopo kati ya madawa ya kemikali na yasiyo ya kemikali zinazotumika kuthibiti wadudu.
- Magonjwa yanayosambazwa na wadudu wanaoshambulia maembe.
- Madhara ya wadudu kwa mazao ya maembe.
Ni ukweli gani muhimu kuhusu kuthibiti wadudu katika maembe?
- Wakulima ni sharti waondoe maembe yaliyoiva zaidi—yanaleta mazingara mazuri kwa wadudu kuzaana.
- Kusanya na uondoe maembe yaliyoanguka na kuharibika kando, lisha mifugo, au zika kwa shimo la urefu wa mita tatu na ufunike na karatasi ya plastiki nyeusi, kwa sababu maembe yaliyoanguka na kuharibika hugeuka kuwa maazingara mazuri kwa wadudu kuzaana.
- Tunda matunda yako wakati yanapokomaa wala sio wakati zimeiva zaidi. Katika hatua hii haziko katika hadhari ya kushambukiwa na wadudu.
- Chaza miti ya maembe hadi takribani mita 3.5 ili kuhakikisha matawi yote yanafika kwa magoto (mita 0.5). Kuhudumisha urefu huo unarahisisha kuangamiza wadudu na magonjwa.
- Chaza matawi yaliyovamiwa na wadudu na utupe mbali na bustani.
- Changanya maembe na, mananasi, mimea ya mbegu kama maharagwe, na manyasi ya mifugo. Hii inapunguza wadudu kwenye bustani. Lakini, mimea hii inaweza kuwa chanzo cha Wadudu Wabaya, kwa hivyo wakulima lazima wawe waangalifu sana.
- Funika kwa neti maembe yanayokomaa ili kuyakinga na wadudu wanaoruka na wadudu wengine.
- Fuatilia mara kwa mara miembe inapochipuka ili kuikinga na wadudu wanaovamia shina.
- Weka alama inayozunguka mmea kwa kutumia dawa ya wadudu. Alama hii inafaa kuwa na upana wa futi moja na iwe futi mbili kutoka kwa mchanga. Hii inazuia wadudu wasipande mti.
Ni changamoto zipi kubwa katika kuthibiti wadudu wa maembe?
- Kutozingatia usafi katika bustani la maembe inaongeza mkusanyiko wa wadudu kama nzi wa matunda.
- Miembe iliyokuwa zaidi au hazijachazwa hufanya kazi ya kuangamiza wadudu iwe ngumu.
- Kukosa kuchaza na kutupa matawi zilizovamiwa na wadudu.
- Kutunda maembe yako vibaya na kutoyahudumia ipasavyo baada ya kutunda.
- Kutokuwa na ujuzi wa kuzuia na kuangaia wadudu.
- Mabadiliko ya Hali ya anga huongeza uwepo wa wadudu.
- Wakulima kukosa kufuatilia na kuangalia miti yao mara kwa mara.
Athari ya utabiri wa mabadiliko ya hali ya hewa kwa uvamizi wa wadudu kwa maembe
- Utafiti umeonyesha ya kuwa mabadiliko ya hali ya hewa, pamoja na ongezeko la kaboni kwenye hewa, inaweza kuongeza mabuu yanayovamia mbegu za maembe na aphid.
- Ongezeko la joto kwenye hewa inongeza kusambaa kwa wadudu kama wadududu wa maembe kwenye maeneo ambayo hapo awali hayakuwa, na mahali kama matunda yanakuwa.
- Ongezeko la joto linaongeza idadi ya wadudu.
- Kugeuka kwa wadudu pia kunaweza kusababisha wadudu kutoangamizwa na njia zilizopo za kuangamiza wadudu.
Njia za ujumla za kuangamiza na kuzuia wadudu wa maembe
- Zingatia usafi kwenye bustani la maembe kwa kutupa mbali maembe yaliyooza na yaliyoanguka kwa sababu yanabeba wadudu kama wadudu wa maemb).
- Chaza sehemu za maembe ambayo zimeshambuliwa na wadudu. Zichome mbali na bustani.
- Angalia maembe mara kwa mara kwa ajili ya wadudu kama mango twig borer, ambazo hujulikana kwa matawi yaliyokauka.
- Kupalilia bustani la maembe baada ya kuvuna maembe inasaidia kuanika mabuu kwa jua na kupunguza uvamizi wa fukusi kwenye jiwe na inflorescence midge.
Kwa maelezo zaidi, soma 1-15.
Habari muhimu kuhusu kuthibiti wadudu wa maembe
Kuna baadhi ya wadudu sugu wanaoadhiri maembe.
1. Inzi wa matunda
Kulingana na mazingara, nzi wa matunda wanaeza wakaishi siku 12-28.
- Baadhi ya aina ya nzi wa matunda hushambulia maembe yanayoiva na yanaweza kusababisha hasara ya asilimia 50% ya mazao.
- Nzi wa matundas wa kike hutaga mayai ndani ya matunda yaliyoiva au yanayoanza kuiva, ndani karibu na ngozi. Mayai yanapasuka kati ya siku 2-4 na mabuu yanakula nyama ya matunda, na kusabababisha matunda kuiva kabla ya wakati wake na kuanguka.
- Mabuu yanapokula nyama, sehemu iliyoadhiriwa inaanza kuwa majimaji alafu rangi ya maembe inaanza kugeuka kabla ya wakati wake.
- Wadudu hawa huanguka chini karibu na mwembe alafu wanageuka kuwa wadudu waliokomaa baada ya siku kumi.
Kuthibiti nzi wa matunda
Kufunika
Kufunika hufanywa siku 55-60 baada ya maua kutokea, ama wakati matunda zimefika ukubwa wa mayai ya kuku. Funika na ufinge maembe na karatasi iliyopakwa nta. Kufunika matunda inazuia matunda yasiharibiwe na wadudu wanaoruka, wanaovamia shina la mwembe, thrips, na leafhoppers/ wadudu wakuruka, na inapunguza kushikwa na wadudu kama anthracnose. Wakulima pia wanaweza wakafunika matunda na magazeti kuukuu yaliyoshonwa pamoja ili kutengea shepu ya pembe tatu. Funga sehemu ya juu na Kamba au waya. Mara nyengine kufunika imekuwa bora kuliko kunyunyiza dawa mara mbili.
Unapotumia karatasi ya plastiki, toboa mashimo ili hewa isambae. Njia nyengine pia ni kutumia matawi. Baada ya kuvuna, haribu mifuko hiyo.
Mitego ya nzi wa matunda
Mitego ya chupa: Wakulima wanaweza kutumia chupa ya 500ml ama lita moja na kuweka kitu cha kuwavutia ndani ili kutega wadudu wa maembe. Tumia chuma moto ili kutengeza shimo kwa shingo ya chupa na kwenye kifuniko alafu pitisha waya ama uzi kwa hizo shimo kwenye kifuniko alafu anika baada ya kuweka kitu wapendacho ndani. Anika chupa kwenye kivuli chini ya tawi. Mtego huu utavutia nzi wa matunda ambao watashindwa kutoka kwa chupa na hatimaye watakufa. Mtego huu utauwa wadudu wa kike, wa kiume au wote kulingana na kile kilichowekwa ndani ya chupa Mitego pia inasaidia wakulima kujua idadi ya wadudu kwenye bustani ili kujua kama anafaa kuwanyunyizia dawa au la.
Vitu vya kuweka ndani y mtego wa chupa : Wakulima wanaweza kuweka vitu vifuatavyo kwenye mtego:
- Maganda ya ndizi zilizoiva zilizokatwa ndogondogo na kuchanganywa na sukari, unga na maji.
- Mchanganyiko wa lita mbili za maji, kijiko kimoja cha chai cha vanilla, vijiko viwili vya ammonia, na kikombe nusu cha sukari.
- Mchanganyiko wa vikombe viwili vya maji, kijiko kimoja cha asali, na kikombe kimoja cha vinegar.
- Mchanganyiko wa sukari, soya na ammonia.
- Badilisha mitego hii baada ya kila wiki mbili kwa sababu mitego Misafi inavutia wadudu zaidi.
- Anika mitego kwa kivuli juu ya majani yaliyo chini ambapo wadudu wanapenda na kuhakikisha mtego haifungamani na matawi.
- Mtego mmoja unatoshea miti miwili. Kama mkulima anamiti 40, kwa mfano, basi anahitaji mitego 20.
Mitego ya Vijiti vya manjano vinavvongata
Mitego ya vijiti vya manjano vinavyongata ni mitego iliyo na mchanganyiko wa nusu maji na nusu ammonia. Rangi hiyo ya manjano inavutia Wadudud wa membe, thrips, wadudu weupe, leaf miners, na aphids, ambao wanawama kwenye mtego na kufa. Mitego ya vijiti vya manjano vimegunduliwa kufanya kazi bora kuliko mitego ya rangi zengine.
Kunyunyizia dawa
Kama mitego haifanyi kazi vizuri dhidi ya wadudu wa maembe, mkulima wa maembe anaweza kuongezea kunyunyizia dawa inayotengezwa na majani ya basil au mbegu za mwarubaini.
- Siaga gramu 50 ya majani ya basil na uloweshe kwa maji littre 2-3 usiku kucha. Chunga alafu uongeze mililita 8-12 ya samuni ya maji na ukoroge. Majani ya basil pia inaweza kutumika kuamgamiza Viwavi, vipeo, ngozi nyekundu, Madodoa ya uyoga na mangonjwa kama nematode.
- Ponda kilo 3-5 za mbegu za mwarubaini zilizototewa maganda, weka kwenya chungu na uongeze lita 10 za maji. Funika chungu hicho na nguo na uweke kwa siku 3, alafu chunga. Changanya kila lita moja ya mchanganyiko huo na lita tisa ya maji, alafu ongeza mililita 100 ya sabuni na ukoroge.
- Nyunyiza kutoka ndani ya matawi ya mti (juu ya mti na matawi). Chagua sehemu tatu pembeni mwa mti na unyunyize lakini usinyunyize ukilenga matunda au sehemu zote za mti.
- Kumbuka ya kuwa dawa zilizo tengenezwa kutokana na mimea hufanya kazi wakati zinapokutana na wadudu.
Fruit Fly Mania
Fruit Fly Mania ni dawa inayonunuliwa na ni changanyiko wa mtego ulio na rotini iliyotengezwa na Amira ambayo inavutia wadudu wa kike na kwa idadi kidogo pia wadudu wa kiume, na ni sumu inayowaua. Dawa hii ilitengezwa na International Centre of Insect Physiology and Ecology (ICIPE) na inatengezwa kwa wingi, idadi ya kuuza hapa kenya na Kenya Biologics.
Jinsi ya kutumia
Nyunyiza kwenye doa: Changanya Fruit Fly Mania na sumu na unyunyize kwa bustani la maembe. Takriban lita 10 ya Fruit Fly Mania inatosha hekari moja.
Mtego: Mkulima naweza kuongeza Fruit Fly Mania kwa mtego ili kuvutia wadudu, ambao watakwama na wafe. Wakulima wanaweza kutumia mitego 30 kwa kila hekari kutega wadudu.
Usafi wa bustani
Mitego na sumu haziwezi kuangamiza wadudu wa maembe kama bustani ni chafu. Uchafu unaweza kusababishwa na mabuu kuishi ndani ya maembe yanayooza kwenye mchanga. Mabuu hayo hukuwa na kugeuka kuwa wadudu amabao wanataga mayai ndani ya maembe. Mayai haya baadaye. Mayai haya baadaye hugeuka mabuu eamabayo inakula matunda na kuyaharibu.
- Wakulima wanaweza kugeuza mtindo huu wa kuvamiwa na wadudud wa maembe kwa kukusanya maembe yaliyo oza na kuweka kwa karatasi nyeusi ya plastiki na kuianika kwa jua ili kuuwa wadudu hawa. Alafu, zika maembe hizo zilizooza.
- Wakulima wanaweza kutumia adui hawa wa wadudu wa maembe, pamoja na siafu amabao wanakula watoto wa fruit fly larvae na parasitoid wasps amabao wanataga mayai yao kwa Mabuu. Hawa wadudu na parasitoids hutokea kiasili, kwa hivyo wakulima wanafaa kuwacha miche kiasi kati ya miti ili ziishi. bizari, parsley, yarrow, zinnia, koti, alfalfa, parsley, cosmos, sunflower/alizeti, na marigold ni miti inayotoa maua ambayo yanavutia wasp na kuwapa makao mazuri.
- Mara mbili kwa wiki kwenye msimu wote, toa matunda zilizo na alama mbaya, zinazotoa maji, toa maji yanayotoka kwa miti na matunda iliyooza kwa mchanga, zitupe.
Kwa maelezo Zaidi tazama hati zifuatazo 1, 2, 3, 5, 10, na 12.
2. Mbegu za maembe/fukusi la jiwe
Fukusi za mbegu ya maembe zinasambazwa na maembe zilizoadhiriwa. Fukusi wanakua ndani ya mbegu na si rahisi kuzigundua; maembe zilizoathirika zinakaa tu sawa lakini zinaoza kutoka ndani. Fukusi la jiwe wa kikehutaga mayai kwa muda wa kati ya wiki 3 hadi 5 juu ya matunda kabla ziwe kubwa. Mayai hizo hupasuka baada ya siku 3-5. Wadudu hao ambao bado ni mabuu wanatoboa matunda, wanakula na kuwa wadudu wazima. Wanaharibu sehemu ya ndani ya mbegu na kuiwacha ikiwa nyeusi, yenye jivu linalokaa linalokaa vibaya amabayo inasabababisha kuoza. Wevil wazima hutoka nje ya matunda kupitia kwa maganda. Wakishaondoka huwa wanaishi chini ya magamba ya mwembe kwenye bustani.
Jinsi ya kuzuia na kuangamiza fukusi la maembe
Fykusi la maembe zinaweza kuishi kwa maembe zilizoanguka kwa muda wa siku 300. Ili kuangamiza fukusi kwenye mbegu, mkulima anapaswa:
- Aondoe na kuharibu takataka zinazozunguka mwembe kwenye bustani kila mwisho wa msimu wa kuvuna.
- Nyunyiza dawa zilizopendekezw na watafiti ma afisa wa ukulima wakati mti unapoanza kutoa maua. Hii inasaidia kuuwa fukusi ama mayai yake yaliyo kwenye matunda kisha kuangamiza idadi yao. Lowesha miti na matawi yake vyema wakati unaponyunyizia dawa au unapotumia kifagio kupaka dawa.
- Kusanya na uharibu maembe yote yaliyoanguka kila wiki hadi siku ya kuvuna. Maembe yaliyoanguka mara nyingi huvamiwa na Fukusi.
- Palilia maembe baada ya kuvuna ili kufunua fukusi la mbegu na kupunguza idadi yao na kadiri ya uvamizi.
- Haribu mbegu za maembe zilizobaki kwenye bustani na kwenye viwanda vya usindikaji.
- Weka bendi inayongata upande wa juu wa mti mti unapoanza kutoa maua ili kupunguza fukusi kutaga mayai kwa matawi.
3. Vidungati vya maembe
Dalili za mwembe kuvamiwa na vidungati ni majani kugeuka kuwa manjano, kutoongezeka ukubwa na kujikunja. Uvamizi ukizidi, matawi na maua huanguka alafu matunda hayamei. Matunda yaliyovamiwa na vidungati huanguka yakiwa machanga. Wadudu hawa hutoa finyaga iliyo na moshi amabayo inasababisha majani, matunda na shina kuwa nyeusi. Mayai ya vidungati ni manjano na yale zimekomaa huwa na rangi nyeupe.
Jinsi ya kuthibiti Vidungati vya maembe
Wakulima wanaweza kuthibiti vidungati vya maembe kwa njia zifuatazo:
- Nyunyizia miembe na dawa kwa kutumia mvuke au kushinikiza maji ili kuangusha wadudu kutoka kwa majani na matawi. Wadudu hao wanapoanguka kwa mchanga watakulwa na wadudu wengine kisha kupunguza idadi yao. Mealy bugs walio na unyevu huwa na pathojeni ya kuvu.
- Mealy bugs pia wanaweza kuokotwa na mikono ili kupunguza idadi yao. Unapotoa wadudu hawa na mkono, wanatoa kemikali ambayo inaambia wenzake waanguke kwenye mchanga.
- Chaza matawi zilizovamiwa na wadudu hao kupunguza mazingara zinazowasaidia kuzaana na kupunguza idadi yao.
- Tengeneza mchanganyiko wa pilipili kwa kuchemsha vikombe vinne vya pilipili kwenye chungu na vikombe tano vya mbegu za pilipili pamoja na maji kwa dakika 15 to 20. Toa chungu kwa moto, ongeza lita tatu za maji, wacha ipoe alafu uchunge na kichungi na uongeze gram 30 za sabuni. Mchanganyiko huu unaangamiza na kufukuza wadudu wa maembe.
- Changanya kijiko kimoja cha sabuni ya kuosha viombi na kikombe kimoja cha mafuta ya kupika. Ongeza vijiko tano au nane vya mchanganyiko huu kwa mtungi wa maji na unyunyizie mimea.
- Palilia mchanga unaozunguka miembe ili kufunua mayai ya mealy bug zilizofunikwa na mchanga ili zichomwe na jua.
- Nyunyizia miti na dawa ya wadudu iliyopendekezwa na maafisa wa utafiti na afisa wa ukulima, Kuzingatia miti inayoanza kumea kwa sababu wadudu wanazipenda.
4. Dumuzi
Mabuu wa dumuzi ambao ni kijani kibichi hula matunda machanga na yanayotokea. Mabuu haya hutoboa na kuingia kwa shina la mwembe unaoanza kuota, hii inasababisha mti kunyauka na kukauka. Mayai ya dumuzi ni rangi ya maziwa na yanatagwa kwa shina na miti midogo inayoanza kuota. Dumuzi walio komaa ni rangi ya kijivu-nyeusi.
Jinsi ya kuthibiti dumuzi
- Chaza sehemu zilizovamiwa na uchome au uzike mbali na bustani.
- Nyunyiza mchanganyiko wa pilipili, kitunguu saumu, na tangawizi.
- Tumia mwarubaini ili kuangamiza dumuzi. Changanya gramu 50 ya unga wa mwarubaini na lita moja ya maji, wacha zikae kwa masaa sita, ongeza sabuni na ukoroge. Unapopaka mchanganyiko huu kwa mwembe, hakikisha unatingisha kila mara na kukoroga.
Kwa habari zaidi, tafadhali angalia hati 6, 7, 9, 11, 13, na 15.
Ufafanuzi
Kijani Kibichi: Hatua ya ukuaji ambapo maembe yanaanza kugeuka manjano au nyekundu.
Kukoma kwa maembe kwa undani: Hatua ya ukuaji ambapo mmea umekuwa na kukomaa, mara nyingi hulinganishwa na tunda kuiva. Kukoma kwa maembe huonekana kwa dalili kama kugeuka kwa rangi, kuanguka kwa matunda na matunda kuwa laini.
Ninaweza kupata wapi habari zaidi zingine kwenye mada hii?
Hati
- Bissdorf, J., 2005. Field Guide to Non-chemical Pest Management in Mango Production. Pesticide Action Network (PAN) Germany. http://www.oisat.org/downloads/field_guide_mango.pdf (712 KB).
- De La Cruz Medina, J., and García, H. S., 2002. Mango: Post Harvest Operations. Food and Agriculture Organization of the United Nations. http://www.fao.org/fileadmin/user_upload/inpho/docs/Post_Harvest_Compendium_-_Mango.pdf (1.86 MB).
- Feed the Future, 2018. Mango Bagging: Farmers Stay Happy, Fruit Flies Stay Away. https://ipmil.cired.vt.edu/wp-content/uploads/2018/06/Mango-Bagging.pdf (1.1 MB).
- Food and Agriculture Organization, 2015. Fruit fly control for mango farmers in Ghana. http://www.fao.org/3/CA2808EN/ca2808en.pdf (1.71 MB).
- Griesbach, J., 2003. Mango Growing in Kenya. World Agroforestry Centre. http://www.worldagroforestry.org/Units/Library/Books/PDFs/97_Mango_growing_in_kenya.pdf (2.67 MB).
- Jomo Kenyatta University of Agriculture and Technology Enterprises Limited, undated. Mango Cultivation in Kenya. http://jkuates.co.ke/MANGO_CULTIVATION_IN_KENYA.pdf (770 KB).
- Korlapati, S. et al, 2014. AESA based IPM: Mango. Department of Agriculture and Cooperation, Ministry of Agriculture. https://farmer.gov.in/imagedefault/ipm/mango.pdf (3.37 MB).
- Ngethe, E. et al, undated. Mango Planting Manual. World Agroforestry Centre and International Fund for Agricultural Development. https://www.worldagroforestry.org/sites/default/files/users/admin/mango-planting-manual.pdf (6.01 MB).
- Pest Control Products Board (Kenya), 2018. Registered pest Control Products for Use in Kenya. http://pcpb.go.ke/listofregproducts/List%20of%20Registered%20Products%20%20Version%201_2018.pdf
- Plantwise, 2014. Pest Management Decision List: Green and Yellow Guide. Fruit flies on mangoes. https://www.plantwise.org/FullTextPDF/2015/20157800650.pdf (217 KB).
- Pole, F. et al, 2014. Mango seed weevil (Sternochetus mangiferae). KARI E-Mimea Plant Clinic. KARI/Mimea Factsheet No.14/2014. http://www.kalro.org/emimi/sites/default/files/Mango%20seed%20weevil_Sternochetus%20mangiferae.pdf (88.5 KB).
- Pole, F., et al, 2014. Mango Fruit fly Ceratitis cosyra (Walker). KARI E-Mimea Plant Clinic. KARI/Mimea Factsheet No.13/2014. http://www.kalro.org/emimi/sites/default/files/Mango%20Fruit%20fly%20Ceratitis%20cosyra.pdf (272 KB).
- Prabhuraj, A., undated. Integrated Pest Management in Mango. https://nptel.ac.in/courses/126104003/LectureNotes/Week-8_MANGO_IPM%20lect%203.pdf (2 MB).
- Prakash, O., 2012. IPM Schedule for Mango Pests. National Horticulture Mission, Ministry of Agriculture, Extension Bulletin No. 1. https://midh.gov.in/technology/IPM-Mango-Revised-Sept2011.pdf (5.03 MB).
- Queensland Government, 1999. Mango Information Kit. http://era.daf.qld.gov.au/id/eprint/1647/4/3gro-mango.pdf (2.48 MB).
- UC Davis – Western Institute for Food Safety & Security, undated. Mangos. https://www.wifss.ucdavis.edu/wp-content/uploads/2016/10/Mangos_PDF.pdf (5.03 MB).
Acknowledgements
Kimechangiwa na: James Karuga, Mwanahabari wa Kilimo, Kenya
Kimedhibitishwa na: Charles Murage, Mshauri wa mwashwa ya kilimo biashara, Shirika laTechnoserve
Makala haya yametayarishwa kwa hisani ya The Rockefeller Foundation kupitia mikakati yao ya Yieldwise