Maswali ya Mahojiano Yaliyopendekezwa: COVID-19 sugu, au COVID -19 ya muda mrefu

Afya

Ujumbe kwa mtangazaji

Save and edit this resource as a Word document

Maelezo kwa watangazaji

Maswali haya yameundwa ili kuwasaidia watangazaji kufanya mahojiano na wataalam wa afya ambao wanaweza kuzungumza kuhusu COVID-19 sugu, au COVID-19 ya muda mrefu, au na watu ambao wameathiriwa na COVID-19, au COVID-19 kwa muda mrefu. Maswali haya yameundwa ili kukusaidia kuunda mijadala yenye taarifa kuhusu dalili, visababishi na athari za muda mrefu za COVID-19 au COVID-19 ya muda mrefu. Uliza baadhi au maswali yote ya ufuatiliaji ili kuchunguza dhana hizi kikamilifu na kuwapa hadhira yako taarifa wanayohitaji.

Ikiwa ungependa kutoa maelezo zaidi kuhusu mada hii, panga mfululizo wa mahojiano na mgeni huyo huyo au na wengine wanaoweza kuzungumza kuhusu masuala haya. Na kumbuka kwamba mahojiano mazuri yanatokana na kusikiliza kwa makini na maswali mazuri ya kufuatilia. Tumia maswali haya kama mwongozo wa mjadala wako lakini uwe mnyumbufu vya kutosha kufuata mjadala unapoongoza, na kuongeza au kuondoa maswali ya kufuatilia kama inavyotakiwa katika mahojiano yoyote.

Hadithi muhimu na habari potofu zinaweza kuja wakati wa majadiliano haya. Hakikisha kuwa umeshughulikia na kuyaondoa haya pamoja na mgeni wako, pamoja na simulizi nyinginezo ambazo ni maarufu katika jumuiya yako.

Hatimaye, dhana zinazojitokeza wakati wa mjadala wako zinaweza kuwa za kiufundi au za kisayansi. Kila mara waulize mhojiwa/wahojiwaji waeleze dhana kama hizi kwa maneno ya wazi na rahisi ambayo msikilizaji yeyote anaweza kuelewa. Ikiwa mgeni anatumia neno tata au la kitaalamu, waambie walielezee—hata kama unaelewa, wasikilizaji wako hawawezi kuelewa.

Script

Maswali kwa wataalam wa afya kuhusu COVID-19 sugu, au COVID- 19 ya muda mrefu

1. COVID-19 sugu ni nini au COVID-19 ya muda mrefu ni nini?

a. Maswali ya kufuatilia:

i. Nini husababisha COVID 19 sugu au COVID-19 ya muda mrefu?

ii. Ni zipi dalili za COVID 19 sugu au COVID-19 ya muda mrefu?

iii. Watu wanapaswa kufanya nini ikiwa wanadhani wana COVID 19 sugu au COVID-19 ya muda mrefu?

iv. Je, makundi fulani ya watu yana uwezekano mkubwa wa kupata COVID-19 sugu au COVID-19 ya muda mrefu? Elezea.

2. Je, ni madhara gani ya kiafya ya muda mrefu yanayoweza kutokea kwa mtu anayeugua kutokana na COVID-19?

a. Maswali ya kufuatilia:

i. Je! ni tofauti gani za muda mrefu za athari za kiafya kati ya watu walioathiriwa na COVID-19 na wale walio na COVID-19 sugu, au COVID- 19 kwa muda mrefu?

3. Je, watu wanaweza kupona vipi COVID-19 au COVID-19 sugu au COVID-19 ya muda mrefu?

a. Maswali ya kufuatilia:

i. Je, watu walio na COVID-19 sugu, au COVID-19 ya muda mrefu wanaweza na wanapaswa kupewa chanjo dhidi ya COVID-19?

ii. Je, chanjo ya COVID-19 inazuia COVID-19 sugu, au COVID-19 ya muda mrefu?

iii. Je, watu walio na COVID-19 sugu, au COVID-19 kwa muda mrefu wana kinga dhidi ya COVID-19 baada ya kuambukizwa?

iv. Je, watu walio na COVID-19 sugu, au COVID- 19 kwa muda mrefu wanapaswa kuendelea kuchukua hatua za tahadhari kama vile kuvaa barakoa? Ikiwa ndivyo, kwa nini?

v. Je, watu walio na COVID-19 sugu, au COVID-19 ya muda mrefu wanapaswa kujitenga na wengine?

Maswali kwa watu walio na dalili za baada ya COVID-19 au COVID-19 ya muda mrefu

1. Ni lini ulipima na kukutwa una COVID-19?

a. Maswali ya kufuatilia:

i. Dalili zako zilikuwa ni zipi?

ii. Je, afya yako imebadilika vipi tangu ulipogunduliwa kuwa na COVID-19 hadi sasa?

iii. Je, una dalili zozote zinazoendelea?

1. Ikiwa ndio, zipi?

2. Dalili zako zimeendelea kwa muda gani?

a. Maswali ya kufuatilia:

i. Je! ni lini uligundua kuwa dalili zako zilizidi dalili za kawaida za COVID-19?

ii. Ulifanya nini ulipogundua kuwa ulikuwa unaugua COVID-19 sugu au COVID-19 kwa muda mrefu?

iii. Je, uliwasiliana na daktari wako?

1. Je, kwa sasa unapokea huduma ya matibabu kwa hali hii? Huduma hizi zinajumuisha nini?

2. Je, huduma hii ya matibabu inasaidia kuponya dalili hizo?

iv. Je, COVID-19 sugu, au COVID-19 ya muda mrefu imekuwa na athari gani kwenye maisha yako?

1. Je, umewezaje kudhibiti dalili za COVID-19 sugu, au COVID- 19 ya muda mrefu?

v. Je, unadhani sasa umepona COVID-19?

1. Ikiwa ndio, je, ni muda gani umepita tangu upone?

2. Ikiwa hapana, una wazo lolote lini utahisi kupona? Je, wahudumu wa afya wamekupa makadirio ya lini unaweza kuhisi kupona?

3. Je, umechanjwa dhidi ya COVID-19?

a. Maswali ya kufuatilia:

i. Kama ndiyo, ni nini kilikuhimiza kupata chanjo?

ii. Ikiwa hapana, kwa nini sivyo?

4. Ikiwa umepona ugonjwa wako, ulijihudumia vipi au watu wengine walikuhudumia vipi?

a. Maswali ya kufuatilia:

i. Umeweza kurudisha uwezo wako wa kuhisi ladha au kusikia harufu?

1. Je, ulikabiliana vipi na kupoteza uwezo wa kusikia harufu na/au ladha wakati wa ugonjwa wako?

ii. Ni ushauri gani daktari wako alikupatia?

iii. Je, hatua zako zinazofuata unapopona COVID-19 sugu au COVID-19 ya muda mrefu ni zipi?

Acknowledgements

Contributed by: Aristide Somié-Abalo Kawele, multimedia journalist and blogger, Sotouboua, Togo

This resource was created thanks to funding by the Government of Canada through Global Affairs Canada as part of the Life-saving Public Health and Vaccine Communication at Scale in sub-Saharan Africa (or VACS) project.