Unaangalia maandishi ya redio kuhusu Kilimo
Taarifa za awali: Kilimo Hifadhi
Utangulizi Siku hizi, wakulima wadogo wadogo wanakumbana na changamoto kutokana na mabadiliko ya tabia nchi. Lakini kilimo hifadhi kimeonyesha kuwa wanaweza kupata mafanikio katika ugumu huu. Kilimo hifadhi kinatoa njia rahisi ambayo wakulima wanaweza kuitumia ili kupambana na athari mbaya za mabadiliko ya tabia nchi na kujifunza kulima mashamba amba kwa kuzingatia “uasilia wake”. Hii…
Utangulizi: Ufugaji wa Mbuzi
Kwa nini somo hili ni muhimu kwa wasikilizaji? Kwa sababu wakulima ambao wanataka kuongeza mbuzi wanapaswa kujua: Umri sahihi na uzito kwa ajili ya mbuzi kuanza uzalishaji na msimu bora wa upandishaji. Mbinu bora za uzalishaji. Dalili za magonjwa ya mbuzi na maambukizi. Jinsi ya kutunza mbuzi wajawazito pamoja na watoto kabla na baada ya…
Taarifa za awali: Usindikaji wa muhogo
Utangulizi Mihogo asili yake ni tropiki ya Amerika ya Kusini. Ililetwa katika bonde la Congo katikati mwa miaka ya 1500, na Afrika Mashariki miaka ya 1700. Asilimia 93 ya mihogo inayozalishwa hutumika kama chakula, hii kulifanya zao la muhogo kuwa muhimu kwa ajili ya usalama wa chakula vijijini. Zaidi ya watu milioni 500 kusini mwa…
Nakala juu ya kilimo cha maharage ya soya
Utangulizi Maharage ya Soya asili yake ni bara la Asia ya Mashariki, na yaliletwa bara la Africa mwishoni mwa miaka ya 1800, na kwa Tanzania mwanzoni mwa miaka ya 1900. Kumekuwa na ongezeko la mahitaji ya maharage ya soya katika kuimarisha lishe kwa vyakula vya binadamu. Wasindikaji wadogo na wa kati (wengiwao wakiwa ni wanawake)…
Madeline na Musa: Kilimo cha maharage ya Soya kwa mazao bora na kipato
Sehemu ya kwanza Eneo: Ndani: Nyumbani kwa Bibi Anase. Mchana. Wahusika: Bibi Anase na Madelina Kwa umbali SFX: Tunasikia kelele za mlango ukigongwa. SFX: TUNASIKIA KELELE ZA MLANGO UKIGONGWA NA BIBI ANASE. BIBI ANASE:(KARIBU NA MIC, ANAPAZA SAUTI) Mende! Mende! Wewe, Mendelina! SFX: BIBI ANASE ANAITA HUKU AKIENDELEA KUGONGA MLANGO. BIBI ANASE: Mende! Wewe Mende,…
Taka ndani, Taka nje: Panda vipando salama vya mihogo kuepuka ugonjwa wa Batobato shambani mwako
WAIGIZAJI: SHOMVI: Mkulima wa mihogo anayejulikana vizuri kijijini Bungu. Anasambaza unga bora wa mihogo ni Mume wa Fatuma. FATUMA: Mke wa Shomvi. JUMA: Anaishi katika kijiji cha Bungu. Moja ya shamba lake lipo karibu na shamba la mihogo la Shomvi. Mume wa Latifa. LATIFA: Mke wa Juma. MWINJUMA: Mkulima wa mihogo ambaye amebobea kulima mihogo…
Kidole kimoja hakiui chawa
WASHIRIKI HADIJA: Mwanamke wa miaka 40 na watoto wanne. Mtoto mkubwa ni wakiume mwenye umri wa miaka 15. Ni mwanamke mjane na Mkulima wa mihogo, analima Mihogo hasa hasa kujipatia chakula na kuuza kidogo kinachobaki kwaajili ya kupata kipato kidogo kwa mahitaji mengine ya familia, kipato kikubwa anajipatia kwa kufanya kazi za vibarua kijiji mwake…
Nakala juu ya kilimo cha maharage
Utangulizi Maharage ni zao maarufu zaidi duniani kati ya mazao mengine ya jamii ya mikunde. Maharage yalifika Tanzania miaka mia tatu (300) iliyopita. Nchini Tanzania na sehemu kubwa ya Afrika Mashariki, maharage yanazalishwa kwa ajili ya matumizi ya nyumbani na kwa ajili ya kuuza. Wakulima wa Afrika mashariki wanazalisha zaidi ya nusu ya maharage yanayozalishwa…
Nakala juu ya Rutuba ya udongo
Utangulizi Rutuba ya ugongo imefafanuliawa kama “uwezo wa udongo kusambaza idadi ya kutosha ya virutubisho muhimu na maji yanayohitajika kwa ajili ya ukuaji wa mimea maalum ikiongozwa na vigezo vya kemikali, maumbile, kibaiologia kwenye udongo.” Kilimo ni chanzo kikuu cha chakula na kipato kwa idadi kubwa ya wakazi wa nchi zilizopo kusini mwa jangwa la…
Kudhibiti magonjwa na wadudu wa maharage
MTANGAZAJI: Salaam, wasikilizaji na karibu katika kipindi. Jina langu ni ____. Leo tutazungumzia kuhusu kuthibiti wadudu na magonjwa yanayoshambulia maharage. Hakuna shaka kwamba maharage ni moja ya chakula kikuu Tanzania. Maeneo yanayolimwa maharage na mahindi ni kama asilimia 11 ya ardhi yote inayolimwa. Baadhi ya familia hula maharage kama chakula cha mchana ama cha usiku…