Taarifa za awali: Kilimo Hifadhi

Afya ya udongo

Backgrounder

Utangulizi

Siku hizi, wakulima wadogo wadogo wanakumbana na changamoto kutokana na mabadiliko ya tabia nchi. Lakini kilimo hifadhi kimeonyesha kuwa wanaweza kupata mafanikio katika ugumu huu.
Kilimo hifadhi kinatoa njia rahisi ambayo wakulima wanaweza kuitumia ili kupambana na athari mbaya za mabadiliko ya tabia nchi na kujifunza kulima mashamba amba kwa kuzingatia “uasilia wake”. Hii inaweza kuhusisha kurekebisha au kubadilisha njia asili za kilimo ili kuchukua fursa kwa kadri uwezavyo kwa kuwa wakati mwingine mvua ni ndogo au mvua zisizokuwa na uhakika na vyanzo vingine vya maji kwa ajili ya mazao.

Wakulima wengi wadogo wadogo wanafikiri kilimo hifadhi kinaweza tu kueleweka na kutumiwa na watu wenye elimu. Kinyume na haya, kilimo hifadhi kinafaa kwa wakulima wenye kiwango chochote cha elimu.

Mazoea muhimu katika kilimo hifadhi ni pamoja na kupanda mazao kwa kupishanisha*, kupunguza usumbufu kwenye udongo, n kufunika na mabaki ya mazao na mazao funika kwa mwaka mzima. Kwa wakulima wenye kipato kidogo, kilimo hifadhi kinahusisha matumizi madogo ya fedha na utegemezi mdogo wa mbolea za viwandani kwa kutumia mabaki ya mazao na kupishanisha mazao. Kutotegemea pembejeo za viwandani, hii ndiyo sababu kubwa kilimo hifadhi kinafaa zaidi kwa wakulima wadogo wadogo, hasa kwa wale wanaokabiliwa na uhaba wa kazi.

Dondoo za msingi?

 • Wakulima wengi wadogo wadogo katika nchi za kusini mwa jangwa la Sahara ni maskini na wanatumia mbinu za kilimo ambazo zinaweza kuharibu rutuba ya udongo, na kusababisha mavuno haba.
 • Kuendelea kulima kwa plau ya kuvutwa au majembe ya trekta inajenga ukanda mgumu chini ya ardhi. Hii husasababisha mmomonyoko wa udongo na kuongeza mtiririko wa maji. Ukanda mgumu chini ya ardhi, huzuia mimea kuwa na mfumo imara wa mizizi.
 • Baadhi ya mazao yanaweza kujulikana kama “mimea inayosaidia kurutubisha udongo” na mengine kama “mimea inayohitaji virutubisho vingi kutoka kwenye udongo” hii inategemea kama yanatoa au yanaongeza rutuba kwenye udongo. Kwahiyo mkulima lazima azingatie uchaguzi mzuri wa aina gani ya mazao ya kupanda.
 • Vikwazo vya matumizi ya kilimo cha asili ni pamoja na mitazamo hasi, changamoto za kifedha, sera ngumu, ukosefu wa elimu, na ukosefu wa upatikanaji wa maarifa endelevu.

Athari zinazotarajiwa za mabadiliko ya tabia ya nchi juu ya matumizi ya kilimo hifadhi

Katika nchi za kusini mwa jangwa la Sahara, athari za mabadiliko ya tabia ya nchi mara nyingi huonekana kwa kupungua kwa kiasi cha mvua au mabadiliko ya muundo wa mvua. Mazoea mengi katika kilimo hifadhi yameundwa kuongeza kiwango cha upatikanaji wa maji ya mvua kwenye mazao katika kipindi cha ukuaji. Kupanda kwenye mashimo na kwenye mistari milalo inaruhusu maji ya mvua kujikusanya karibu na mmea na kuwezesha mizizi kupata unyevu unyevu chini ya ardhi. Huu uhuboreshaji wa matumizi ya maji yanayopatikana katika kilimo hifadhi yamaanisha kuwa, kuna uwezekano wa mazao kukuwa wakati mabadiliko ya tabia ya nchi yakiendelea.

Masuala ya kinjisia juu ya kilimo hifadhi

 • Wanawake wengi wanaoishi kusini mwa jangwa la Sahara wanaonewa na mila potofu zinazohusiana na kilimo, ukihusisha na umiliki wa ardhi*, uchaguzi wa mazao na upatikanaji wa masoko.
 • Baadhi ya zana za kilimo zilizopendekezwa na kilimo hifadhi yanaweza kuwa hayafai kutumiwa na wanawake. Kwa mfano jembe la Chaka linauzito wa kilo 4-5 ulimaji wake unahitaji kutumia ng’ombe.
 • Wanawake wengi hawajasoma hivyo wanapata changamoto kutekeleza mazoea ya kilimo hifadhi ambacho kinahitaji vipimo sahihi na muda.

Taarifa potofu kuhusu kilimo hifadhi

 • Baadhi ya wakulima wadogo wadogo wanaamini kuwa kilimo hifadhi kinatumia nguvu kazi kubwa. Mara nyingi hii huwa kweli kwa hatua za awali, lakini nguvu kazi mara nyingi kupunguzwa baadae kwa sababu wakulima huyatumia mashimo hayo hayo au mistari ya milalo hiyohiyo, mwaka hadi mwaka. Mfumo wa kilimo hifadhi ambacho hutumia madawa ya kuulia wadudu kudhibiti magugu hupunguza kazi nyingi, hasa kazi za wanawake.
 • Kuacha mabaki ya mazao * shambani inachukuliwa kama ni uchafu. Lakini ina faida kadhaa, faida hizo ni pamoja na:
  • Kutenda kama matandazo yanayozuia unyevu unyevu kwenye udongo.
  • Mabaki ya mazao kuoza na kuongeza rutuba kwenye udongo.
  • Hukandamiza kuota na ukuaji wa magugu.
 • Wakulima wengi wanaamini juu ya kulima shamba ili kuruhusu maji kuingia kwenye udongo. Kwa ukweli, kuacha udongo umefunikwa na mabaki ya mazao, hii huongeza upenyaji wa maji kuliko ulimaji.
 • Baadhi ya wakulima wanaamini kwamba, kilimo hifadhi hakitoi nafasi ya kupumzika kwa wakulima ndani ya mwaka. Hata hivyo, kama ukipanga vizuri, kilimo hifadhi hugawanya kazi kwa utaratibu katika msimu. Hii inapunza mkulima kufanya kazi zote kwa wakati mmoja kwa hofu ya mvua kuanza kunyeesha.

Maelezo muhimu kuhusu kilimo hifadhi

1. Kudumisha mabaki ya mazao ya kufunika udongo

Baada ya mavuno, ni muhimu sana kudumisha mabaki ya mazao shambani ili kufunika udongo kipindi kisicho cha msimu wa kulima. Mabaki ya mahindi au kutoka mazao mengine kama, maharage ya soya na karanga lazima yasambazwe kwenye shamba zima. Pia wakulima lazima watafute mbinu za kuzua moto pembezoni mwa shamba ili kuzuia uchomaji wa moto kuingia shambani na kuharibu mabaki ya mazao. Kwa njia hii, mabaki yatalinda udongo kuchomwa moja kwa moja na jua.

Kipindi cha masika, mabaki ya mazao yatapunguza madhara ya mvua kubwa. Matokeo yake ni kwamba, bandala ya kupoteza udongo kwa kuondoka na maji, maji ya mvua yatabaki chini ya ardhi, hii kusaidia kuimarisha unyevu unyevu kwenye udongo na kusababisha upatikanaji wa unyevu uvyevu wakati wa ukame. Na yakioza, mabaki haya hujichanganya na udongo hivyo kuboresha rutuba ya udongo.

2. Kilimo cha kupishanisha mazao

Ubadilishaji wa mazao kwenye shamba moja inajulikana kama kilimo cha kupishanisha mazao while upandaji wa zao moja kwenye shamba moja, msimu hadi msimu hii inaitwa kilimo cha zao moja. Kilimo cha zao moja huongeza wadudu na magonjwa shambani. Kilimo cha zao moja ambacho zao “linayohitaji virutubisho vingi kutoka kwenye udongo” hii inaweza kupoza rutuba ya udongo na kupungza mavuno.

Sababu moja kubwa ya kupishanisha mazao ni kwamba “mazao yanayohitaji virutubisho vingi kutoka kwenye udongo” kama mahindi, mtama na ulezi, mazao haya yanahitaji virutubisho vingi kutoka kwenye udongo kuliko mazao mengine. Vile vile, mihongo haiongezi thamani zaidi kwenye udongo mbali na kusaidia kuvunja. Hii ni nzuri kwa kupitisha hewa kwenye udongo. Kupanda mazao haya kwenye shamba moja kila mwaka, hii inaweza kupunguza rutuba ya udongo na kupunguza mavuno.

Mazao mengine huchukuwa kidogo sana kutoka kwenye udongo lakini kuongeza virutubisho. Mazao ya aina hii yanajulikana kama “mazao yanayosaidia kurutubisha udongo” haya ni mazao kama jungu, kunde, mbaazi, lablab na maharage ya soya yapo kwenye kundi hili. Unashauriwa kipishanisha mazao, kati ya “mazao yanayosaidia kurutubisha udongo” na “mazao yanayochukuwa rutuba kwenye udongo”.

3. Mazao funika*

Udongo ni mhimu sana kwenye kilimo. Kwa bahati mbaya, mara nyingi unaharibiwa na jua, upepo, na mvua kubwa. Katika kilimo hifadhi, wakulima wadogo wadogo hupanda chakula fulani au mazao ya biashara na ambayo yanalinda udongo. Haya mazao jalada hulinda udongo kuzolewa na mvua kali, upeo na jua kali. Mazao jalada mazuri ni pamoja na kunde, lablab na mbaazi.

4. Kusumbua ardhi kwa kiwango kidogo*

Kwa kawaida, wakulima wadogo wadogo hulima shamba nzima ili kudumisha usafi kwenye shamba na wakati mwingine kupanda kwa matuta.

Kupunguza kiwango cha kulima, kwa upande mwingine, inahusisha kusumbua udongo sehemu ambapo mbegu hupandwa. Sehemu nyingine ya udongo shambani inabaki. Hii inazuia udongo kuondoka hasa wakati wa mvua kubwa.

Wakulima wanaweza kutekeleza ulimaji wa kiwango cha chini kwa kutumia majembe au zana za ng’ombe kama vile plau. Wakulima wanaotumia majembe kulima mashimo na kuacha nafasi sahihi lazima wahakikishe kwamba wanalima hadi kwenye ukanda mgumu chini ya ardhi. Wakulima wanaotumia plau, hili lina nguvu ya kulima umbo lolote kwa kupasua mistari ya kina cha chini kwenye ardhi.

Kupasua ukanda mgumu chini ya ardhi kwa kutumia jembe la mkono au plau inasaindia maji kuzama ardhini badala ya kutililika. Mazao yanaweza kusambaza mizizi yake hadi kwenye ukanda mgumu chini ya ardhi, na kufuata unyevuunyevu ndani ya udongo, na kuchipua kwa kawaida wakati wa kiangazi.

Kuchimbua ardhi kwa kiwango cha chini cha ulimaji kinaweza huboresha mfumo wa udongo na rutuba ya udongo kwa miaka mingi. Pia inaongeza kiwango cha uvyevuunyevu kwenye ardhi.

5. Kufunga shamba

Wakulima wadogo wadogo mara nyingi huvuna mazao mara tu baada ya kukomaa, na kisha kuchoma mabaki ya mazao. Hii inaacha udongo wazi, ikiwemo na moto mkubwa ambao si lazima usababishwe na binadamu. Kuharibu au kuondoa mabaki ya mazao pia huondoa virutubisho muhimu kwa mazao ya msimu ujao.

Katika kilimo hifadhi, wakulima wanatumia mbinu iitwayo upumzishaji wa shamba kwaajili ya maandalizi ya msimu unaofuata. Baada ya mavuno, wakulima wengi husambaza mabaki ya mazao ili kufunika udongo. Mabaki haya yanaoza kwenye udongo na kuongeza virutumisho. Kuzuia moto na mifungo kuharibu mabaki ya mazao, wakulima wanazuia moto kwa kutoa nyasi zote zinazozunguka shamba na kuzuia mifungo kuvamia shamba kwa kuweka uzio wa miti nyenye miba kulizunguka shamba.

6. Kilimo mseto

Kilimo mseto* Kilimo cha aina hii kina majukumu maalum sana kwenye kilimo kinachozingatia uhifadhi. Huko Zambia na nchi zingine kusini mwa jangwa la Sahara, miti hii na vichaka ni pamoja na Faidherbia albida, Sesbania sesban, Tephrosia vogelii, Gliricidia sepium, mbaazi na miti mingine. Mizizi yake huchimba chini na kuvunja ukanda mgumu chini ya ardhi. Hii huboresha kupitisha hewa kwenye udongo na kuruhusu maji ya mvua kuzama zaidi ndani ya ardhi. Aidha, mazao ya aina hii nyingi ni jamii ya kunde na huuongeza kiwango cha naitrojeni kwenye udongo.

Changamoto za kutumia kilimo kinachozingatia uhifadhi

 • Uhaba wa vifaa vya kuboji ili kuacha udongo ukiwa umefunikwa.
 • Kushindania mabaki ya mazao na mifugo.
 • Kutokuwa na pembejeo sahihi (zana za kilimo hifadhi, mbegu za mazao ya matandazo na madawa ya kuulia wadudu, na mengineyo).
 • Kupata ujumbe tofauti kutoka serikalini na mashirika yasiyo ya kiserikali.
 • Maarifa madogo juu ya kilimo mseto na mazoea mengine ya kutumia kilimo kinachozingatia uhifadhi.
 • Vikwazo vya wanawake vya kutomiliki ardhi, hii inaleta changamoto kwa wanawake kushiriki kwenye kilimo hifadhi, au pamoja na “mazao ya wanawake” katika kupishanisha mazao.

pic1a

Mkulima mdogo huko Chipata, Zambia akitumia plau aina ya Magoye na ng’ombe katika shamba lililolindwa na athali za moto na likiwa na masalio ya mazao yaliyoshikana..
 

 

 

 

 

pic2
Maharage ya soya “ni mazao yanayosaidia kurutubisha udongo” yakiwa tayari kwa kuvunwa. Mizizi ambayo inabaki ardhini ina vinundu yenye madini ya nitrojeni. Hii inasaidia kulisha zao “linalohitaji virutubisho vingi kutoka kwenye udongo” wakati ujao.
 

 

 


pic3

 

Mabaki ya mahindi baada ya kuvuna. Mabaki haya yanazuia athari za moto kwenye maeneo asilia na vizuizi vya moto. Hii inazuia ardhi kuwa ya moto wakati wa ukame na kuoza ili kuboresha rutuba ya udongo*.

 

 

 

 

pic4

 

Mti wa Faidherbia ambao sasa unamiaka saba katika kituo cha shamba darasa Kalunga, huko Chipata, Zambia. Imepandwa kwa umbali wa mita kumi, matawi ya miti hii hufunika shamba zima na majani yake kutengeneza madini ya nitrojeni. Wakati wa msimu wa kilimo, majani hukauka kwahiyo hayatengenezi kivuli kwenye mazao.

 

 

 

 

pic5

 

Kunde kama zao la kulinda udongo. Udongo umefunikwa kabisa na kuzuia madhara ya mvua na upepo. Zao hili pia linaongeza nitrojeni kwenye udongo.

 

 

 

 

 

Ufafanuzi wa maneno muhimu

Kilimo mseto: Kilimo kinachochanganya na uhifadhi wa miti na vichaka muhimu kwenye shamba ili kuboresha kilimo. Mimea aina hii ni pamoja na: Faidherbia albida, Sesbania sesban, Tephrosia vogelii, Grevillia robusta, na Gliricidia sepium.

Mazao ya kufunika udongo: Mazao yanayolimwa kulinda shamba kwa kufunika udongo uliyo wazi. Mazao haya maarufu ni pamoja na kunde, mbaazi, na lablab.

Mabaki ya mazao: Haya ni mabaki ya mazao baadaa ya kuvuna, kwa mfano mabaki ya zao la mahindi, karanga.

Kilimo cha kubadilisha mazao: Huu ni utaratibu wa kupishanisha mazao shambani. Mara nyingi huongeza virutubisho kwenye udongo, kwa mfano, ukipanda karanga baadae unapanda mahindi ambayo yanahitaji virutubisho vingi.

Kufunga shamba: Hili ni shamba ambalo halijalimwa kwa muda mrefu, kwa kuruhusu a rutuba ya udongo kufufuliwa.

“Mazao yanayosaidia kurutubisha udongo”: Haya ni mazao ambayo huongeza virutubishi kama vile naitrojeni kwenye udongo. Mengi ni mazao jamii ya mikunde, ambayo kwenye mizizi yake kuna vinundu ambayo huongeza nitrojeni. Ukivuna kwa kukatia majani juu badala ya kung’oa, vinundu hivyo hubaki kwenye udongo na kuyaimarisha na madini ya nitrojeni.

Ukanda mgumu chini ya ardhi: Hii ni sehemu ngumu kwenye udongo baada ya kulima udongo na kwa plau ya kuvuta na jembe la mkono. Hii inasababisha maji ya mvua kuondoka na mizizi kushindwa kwenda chini zaidi ndani ya udongo.

Shamba bora: Hili ni shamba ambalo linaudongo bora, miti na vichaka mbalimbali ambayo husaidia kupunguza muda wa kupumzisha shamba ili litumike mapema zaidi. Miti hii pia inafaida zikiwemo za kiuchumi na nyinginezo kwa wakati huo, kwa mfano matunda na kuni.

Umiliki wa ardhi: Katika muktadha huu, umiliki wa ardhi unayohusisha sheria na kanuni zinazoongoza upatikanaji na umiliki wa ardhi kwa wakulima wadogo wadogo. Katika baadhi ya nchi za kusini mwa jangwa la Sahara, hii zaidi huwaonea wanawake hasa walioolewa ambao wakati mwingine wanachukuliwa kama wategemezi katika ndoa. Kama si ndoa, wao ni, hata hivyo, kuchukuliwa kama watu wasio na kipaumbele katika jamii zilizotawaliwa na jinsia ya kiume.

Kusumbua ardhi kwa kiwango cha chini: Kupunguza kuchimba sana kwenye ardhi. Hii huhamasisha mkulima kulima tu sehemu ambapo anapanda mbegu. Eneo lingine linabaki katika asili yake na mbali na kudhurika na athari nyinginezo.

Zao moja: Ni kupanda zao moja kwenye shamba kila mwaka. Mara nyingi hupelekea kupungua kwa rutuba ya udongo na ongezeko la magugu na magonjwa.

Hii ni hali ya udongo: Udongo mzuri na laini. Husababisha mizizi kupenya vizuri ndani ya udongo.

“Mazao yanayohitaji virutunisho vingi kutoka kwenye udongo”: Ni mazao ambayo hutegemea virutubisho vilivyopo kwenye udongo au hutumia pembejeo za nje.

Acknowledgements

Imechangiwa na : Picha zote zimepigwa na Filius Chalo Jere, Breeze FM, Chipata, Zambia, isipokuwa picha ya kwanza iliyopigwa na Par Oscarsson, Mpango wa Usimamizi wa Ardhi na Kilimo Hifadhi, Wizara ya Kilimo, Zambia Sida/Orgut.
Imepitiwa na: Neil Rowe Miller, Kilimo hifadhi, Afisa Ufundi, Mennonite Central Committee, na Godfrey Magoma, Conservation Agriculture Technical Specialist, Tanzania, Canadian Food Grains Bank, East Africa Conservation Agriculture Scale up Program.

Information sources

1. Conservation Farming Unit website. conservationagriculture.org/
2. Stephen Kabwe and Cynthia Donovan, 2005. The Magoye Ripper: Preliminary Findings on Adoption, Benefits, and Constraints. fsg.afre.msu.edu/zambia/GartYearbookdraftarticle_ripper.pdf
3. Conservation Farming Unit. Faidherbia albida, undated. conservationagriculture.org/uploads/pdf/CA-AND-FAIDHERBIA-ALBIDA.pdf
4. Conservation Technology Information Center, Purdue University. Crop residue management. www.ctic.purdue.edu/resourcedisplay/298/
5. Wikipedia: Crop rotation: https://en.wikipedia.org/wiki/Crop_rotation
6. Wikipedia: Cover crops: https://en.wikipedia.org/wiki/Cover_crop
7. Food and Agriculture Organization of the United Nations (FAO), 2002. Land tenure and rural development. www.fao.org/docrep/005/y4307e/y4307e05.htm

Picha zote zimechukuliwa na Filius Chalo Jere, Breeze FM, Chipata, Zambia, with the exception of the first, by Par Oscarsson, Land Management and Conservation Farming Programme, Wizara ya Kilimo, Zambia Sida/Orgut.
Waraka huu umeandaliwa kwa msaada wa shirika la Hifadhi ya Nafaka kutoka Canada kama sehemu ya mradi, “Kilimo Hifadhi ili kujenga ustahimilivu, utumiaji wa mbinu za kilimo kukabili mabadilikoya tabia ya Nchi.” Waraka huu umefadhiliwa na Serikali ya Kanada,kupitia shirika lake la Mahusiano ya Kimataifa. www.international.gc.ca

gac-logoMradi unaendeshwa kwa ufadhili wa serikali ya Kanada kupitia idara ya masuala ya kimataifa (GAC)