Wakulima Wanaotumia Njia bora za Kupumzisha Mashamba Lazima Waongeze Fosforasi katika Udongo

AfyaMazingira na Mabadiliko ya TabianchiMiti na kilimo msetoUzalishaji wa mazao

Ujumbe kwa mtangazaji

Pakua na hariri taarifa hii kwa matumizi yako

Ukosefu wa upatikanaji wa fosforasi kwa ajili ya mazao ni shida kubwa kwa wakulima wengi kusini mwa Jangwa la Sahara. Utekelezaji wa kilimo mseto (agroforestry) kama vile matumizi ya njia bora za kupumzisha ardhi inaweza kusaidia wakulima kuongeza virutubisho (hasa nitrojeni) na kuboresha muundo wa udongo. Kwa bahati mbaya, njia bora zilizoboreshwa za kupumzisha ardhi pekee haziwezi kuboresha kiwango cha fosforasi katika udongo. Chanzo cha kemikali au madini ya mbolea lazima iongezwe kwenye udongo ili kuondokana na viwango vya chini vya fosforasi ambayo husababisha ukuaji duni na kupunguza kiwango cha mazao.

Simulizi ifuatayo inapitia baadhi ya faida za njia bora za kupumzisha shamba na kuhimiza wakulima kuzingatia hitaji la kuongeza fosforasi kwenye udongo mashambani mwao kabla ya kuanza tena kutumia ardhi kwa kilimo.

Script

Wahusika

Katika kipindi hiki, wenyeji ni Onyango na Rose. Tafadhali tumia majina ambayo wasikilizaji wako watayahusisha na kuyatambua. Rose ana uelewa sana kuhusiana na mada ya kilimo na kilimo mseto (agroforestry). Onyango pia ana hamu sana na anauliza maswali mengi mazuri, lakini wakati mwingine anaonekana kukosa uvumilivu/subira. Wahusika hawa wawili wanatumia njia ya kufurahisha kupeana majibu.

Utangulizi wa kipindi

MZIKI WA KUFUNGUA KIPINDI. PUNGUZA MZIKI POLEPOLE.

Onyango:
Habari na karibuni kwenye kipindi. Leo tunataka kuongelea kuhusu njia bora za kupumzisha shamba na umuhimu wa kuongeza fosforasi ili kuongeza rutuba ya udongo wakati wa kutumia njia bora za kupumzisha shamba. Kwa kuanza, Rose unaweza kuelezea nini maana ya njia bora za kupumzisha shamba kwa wasikilizaji wetu?

Rose:
Hakika, Onyango! Kwanza kabisa ngoja tuwakumbushe watu tofauti kati ya njia za kawaida za kupumzisha shamba na njia bora za kupumzisha shamba. Njia ya kawaida ya kupumzisha shamba ni shamba tu ambalo limepumzishwa – ardhi ambayo hailimwi kwa wakati huu. Mkulima hajapanda mahindi au mtama lakini ameacha ardhi kuendelea na uoto wa asili. Mara nyingi hii inafanywa ili kuruhusu ardhi kurudisha rutuba yake.

Onyango:
Ndio, kweli. Njia iliyoboreshwa ya kupumzisha shamba ni nini?

Rose:
Usijali, Ninaelezea hilo pia! Njia iliyoboreshwa ya kupumzisha shamba, ni ardhi iliyopumzishwa pia, lakini mkulima amepanda mazao maalumu kwa ajili ya kuboresha rutuba ya udongo.

Onyango:
Njia bora za kupumzisha mashamba zimekuwa zikikuzwa sana katika jamii yetu. Endelea kubaki hewani kusikia zaidi juu ya jinsi wakulima wanaweza kufaidika kwa kutumia njia bora za kupumzisha mashamba.

MZIKI (Sekunde 5).

Onyango:
Karibuni tena kwenye kipindi. Tumekuwa tukiongea kuhusu njia bora za kupumzisha mashamba – njia ambayo unaweza kutumia kuboresha rutuba ya udongo kwenye shamba lako. Tumesema kwamba mkulima hupanda mazao maalumu kusaidia kuboresha rutuba ya udongo.

Rose:
Ndio. Wakulima wanaweza kupanda vichaka katika ardhi yao. Tunashauri upandaji wa vichaka kama vile Sesbania au Crotolaria. Kupanda vichaka katika shamba lililopumnzishwa inaboresha udongo, inazuia mmomonyoko wa udongo na hupunguza ukuaji wa magugu. Wakulipa pia wanapenda njia bora za kupumzisha mashamba kwasababu wanaweza wakatumia vichaka kupata kuni na lishe ya mifugo.

Onyango:
Uelewa wangu ni kwamba njia bora za kupumzisha shamba zina faida pia kwasababu zinaongeza virutubisho muhimu kwenye udongo. Kwa mfano, njia bora za kupumzisha mashamba, zinaweza kuongeza kiwango cha nitrojeni kwenye udongo.

Rose:
Hii ni kweli! Nitrojeni inaweza kuongezwa na aina maalumu ya mimea. Moja ya mimea hii ni Tephrosia. nitrojeni inaongezwa kwenye udongo pale ambapo majani, maganda na mizizi ya mmea inaoza.

Onyango:
Kwahiyo njia bora za kupumzisha mashamba zinaweza kusaidia kwa kuongeza nitrojeni kwenye udongo. Vipi kuhusu kirutubisho kingine cha muhimu – fosforasi?

Rose:
Swali lingine zuri! Onyango anauliza kama njia bora za kupumzisha mashamba zinaweza kuwasaidia wakulima kwa kuongeza fosforasi kama kirutubisho kwenye udongo. Jibu ni kwamba, fosforasi haitaongezwa kwenye udongo kama utatumia njia bora za kupumzisha ardhi. Kwa uhalisia, vichaka huondoa fosforasi kwenye udongo kadri vinavyokuwa.

Onyango:
Inaonekana kama njia bora za kupumzisha shamba peke yake haziwezi kutatua tatizo la kiwango kidogo cha fosforasi kwenye udongo?

Rose:
Uko sawa. Kwa kweli, wakati vichaka kama vile Sesbania au Crotalaria vinapokatwa na kuvunwa, fosforasi (Iliyohifadhiwa katika mimea hii) huondolewa kutoka ardhini. Ndio maana ni muhimu kwa wakulima wanaotumia njia bora za kupumzisha ardhi kuongeza fosforasi ya ziada kwenye udongo kabla ya kupanda mazao yao.

Onyango:
Unasema wakulima lazima wanunue mbolea ili kuongeza kirutubishi hiki kabla ya kupanda mazao yao?

Rose:
Ndio. Kuongeza mbolea ndiyo njia bora ya kuongeza fosforasi kwenye udongo.

Onyango:
Lakini ni hakika kwamba kuongeza mboji au kulima mazao kwa kutumia samadi itakuwa rahisi kwa wakulima kuliko kununua mbolea ya kemikali!

Rose:
Ndio, hii ni kweli! Tatizo ni kwamba, mazao mengi yana uhitaji wa fosforasi zaidi – yanahitaji zaidi ya kile mbolea au mboji zinaweza kusambaza kwenye udongo.

Onyango:
Kwa hivyo, suluhisho ni nini?

Rose:
Mkulima lazima aongeze mbolea ya fosfati. Kuongeza mbolea itahakikisha kwamba fosforasi ya kutosha inapatikana kwa ajili ya mazao.

Onyango:
Kwahiyo wakulima wanaweza kutumia mbolea ya fosfati kama DAP, SSP na TSP, au mbolea ya fosfati ya miamba kabla ya kupanda mazao yao.

Rose:
Haswa.

Onyango:
Kama tulivyojadili, njia bora za kupumzisha mashamba zina faida nyingi kwa wakulima. Vichaka vinaweza kuboresha udongo na kutoa mali ghafi za ziada kama kuni na lishe kwa mifugo.

Rose:
Njia bora ya kupumzisha shamba, inaongeza pia kiwango cha nitrojeni kwenye udongo, ambayo itafaidisha mazao yajayo yatakayopandwa kwenye shamba hilo. Lakini wakulima kumbukeni, kama unatumia njia bora za kupumzisha mashamba, ni muhimu kuchukua tahadhari ili kubadilisha fosforasi kwenye udongo baada ya kukata vichaka na kabla ya kupanda mazao yako. Kwa uchache sana unaweza kuongeza mboji au mbolea ili kuongezea fosforasi ambayo hutolewa wakati vichaka vimekatwa.

Onyango:
Lakini, kama tulivyosema, ili kuhakikisha kuwa pana fosforasi ya kutosha kwenye udongo, inaweza kuwa muhimu kutumia mbolea ya fosfati.

ONGEZA MZIKI POLEPOLE NA SHIKILIA.

Rose:
Njia bora za kupumzisha mashamba zinaweza kuboresha udongo, kupunguza mmomonyoko na kupunguza ukuaji wa magugu. Kama utatumia njia bora za kupumzisha mashamba, kumbuka kwamba utahitajika kuongezea fosforasi kwenye udongo, baada ya kukata vichaka na kabla ya kupanda mazao yako.

PUNGUZA MZIKI POLEPOLE

Vidokezo

Maandishi haya yametaja matumizi ya mbolea ya mwamba ya fosfati kwa ajili ya kuboresha mifumo ya njia za kupumzisha mashamba. Kwa taarifa zaidi kuhusu fosfati ya mwamba kwa kilimo endelevu Africa, tafadhali angalia tovuti ya “Miamba kwa Mimea – Rocks for Crops” kupitia: http://rocksforcrops.lrs.uoguelph.ca/
Majina kamili ya mbolea ya fosfati yaliyotajwa katika maandishi haya ni kama ifuatavyo:
DAP – di-ammonium phosphate
TSP – triple superphosphate
SSP – single superphosphate

Acknowledgements

Shukrani

Imechangiwa na: Heidi Braun, Chuo kikuu cha Guelph, Ontario, Canada.

Imehakikiwa na: Professor Helen Hambly Odame, Masomo ya ugavi vijijini, Chuo kikuu cha Guelph, Canada

Information sources

Chanzo cha Habari

Amadalo, B. et. al. (2003). Improved fallows for western Kenya: an extension guideline. Nairobi, Kenya, World Agroforestry Centre.

Sanchez, P.A., and C.A. Palm. “Nutrient cycling and agroforestry in Africa.”Toleo la Kiswahili la jarida hili limeandaliwa kwa ufadhili wa Justdiggit kupitia mradi wake wa Kisiki Hai (Farmer Managed Natural Regeneration – FMNR) ulioko mjini Dodoma.