Ujumbe kwa mtangazaji
Save and edit this resource as a Word document
Maelekezo kwa Watangazaji
Karatu ni mojawapo ya wilaya tano katika mkoa wa Arusha, kaskazini mwa Tanzania na iko takriban kilomita 150 magharibi mwa mji wa Arusha. Kilimo ndio tegemeo kuu la maisha ya kaya katika eneo hilo, zinazolima mazao ya chakula kama mahindi, njegere, kunde, mihogo, viazi, viazi vitamu, maharagwe meusi, maharagwe na maboga. Udongo wa mfinyanzi wa Karatu ulikuwa na rutuba hapo zamani, lakini katika miaka ya hivi karibuni umeharibika. Kwasababu eneo la Karatu ni lenye vilima, mvua inaponyesha, mtiririko wa maji hubeba udongo wa juu wenye rutuba na kuacha makorongo kwenye mashamba. Aina ya kilimo kama vile kulima mazao mara kwa mara bila kuweka mbolea ili kufanya udongo kuwa na rutuba, na kilimo mseto pia kimechangia uharibifu wa udongo huko Karatu.
Muswada huu unaonyesha jinsi mmomonyoko wa udongo na uharibifu ulivyoathiri rutuba ya udongo na mavuno ya mazao kwa kaya za wakulima wadogo huko Karatu. Mtaalamu wa masuala yanayohusiana na rutuba ya udongo na urejesho wa ardhi katika hali yake ya awali anaelezea sababu za mmomonyoko wa udongo na uharibifu katika eneo hilo. Pia atazungumzia mafunzo ya kilimo wanayotoa kwa wakulima wadogo ili kuwasaidia kukabiliana na mmomonyoko wa udongo na kurutubisha udongo wao unaotoa mazao kidogo. Mtaalamu huyo pia atazungumzia mbinu nyingine za kilimo ambazo zinaweza kuwasaidia wafugaji wadogo wa huko kujiongezea kipato ikiwamo ufugaji wa kuku.
Ili kutoa mwongozo sawa wa mpango wa kuelimisha wakulima wadogo kuhusu jinsi ya kushughulikia mmomonyoko wa udongo na uharibifu, hoji mtaalam wa urutubishaji wa ardhi na wakulima wadogo walioathiriwa na matatizo haya. Mtaalamu anaweza kutoa maarifa ya kiufundi yanayohitajika na wakulima wanaweza kushiriki maoni yao kabla na baada ya kutumia mbinu ambazo mtaalam anapendekeza.
Kama ukichagua mwongozo huu wa redio kama sehemu ya programu yako ya kilimo, unaweza kutumia waigizaji wa sauti kuwakilisha watu waliohojiwa. Ukifanya hivyo, tafadhali wajulishe hadhira ya redio mwanzoni mwa kipindi kwamba hizo ni sauti za waigizaji na sio wahojiwa halisi.
Hapa kuna baadhi ya maswali unayoweza kumuuliza mtaalamu na wakulima wadogo:
Wataalamu
- Ni zipi sababu za kiasili na kibinadamu zinazosababisha mmomonyoko na uharibifu wa udongo katika mkoa huu?
- Ni mbinu gani za kurutubisha ardhi umezianzisha kwa wakulima ili kuwasaidia?
- Mbinu hizi za kurutubisha ardhi zimekuwa na athari gani katika uzalishaji wa mazao?
Wakulima
- Ni mazao gani wakulima wadogo wanalima katika wilaya hii?
- Ni kwa namna gani mmomonyoko na uharibifu wa udongo umeathiri uzalishaji wako wa mazao pamoja na kipato?
- Baada ya kuanza kutumia njia za kilimo zilizoboreshwa pamoja na urutubishaji wa ardhi, je uzalishaji wako wa mazao na kipato chako kimebadilika?
Muda wa mwongozo huu, ikijumuisha utangulizi na baada ya mahojiaono. Dakika 20.
Script
Ili kusaidia katika majadiliano na kujibu maswali, tuko pamoja na Eliud Letungaa, mtaalam wa urejeshaji rutuba ya ardhi anayehusika katika mradi wa kilimo chenye tija katika wilaya ya Karatu unaoendeshwa na MVIWA Arusha, ambalo ni shirika la wakulima.
Tafadhali tupe muktadha mfupi wa jinsi mmomonyoko na uharibifu wa udongo ulivyoathiri kilimo cha wakulima wadogo wilayani Karatu.
Ni muhimu kutambua kwamba maji yanayotiririka yanaweza kuwa na manufaa kwa kuboresha uoto wa mimea ikiwa yatasimamiwa vyema. Kwa mfano, kuunda mtaro au matuta au miundo mingine itakayoshikilia au kuvuna kunaweza kuwezesha ukuaji wa miti na kupunguza hitaji la kumwagilia mara kwa mara. Hayo ni baadhi ya mambo yaliyotufanya tuutambulishe mradi hapa.
Ikiwa wakulima wanaweza kulima mazao mengi na kufuga mifugo, wataunda mfumo ikolojia ambapo mabaki ya mazao yanatumika kama malisho ya mifugo na samadi ya mifugo kutumika kama chanzo cha virutubisho vya mazao.
Pia tulipendekeza kwamba wakulima wapande miti ya kiasili kama miti ya acacia, hasa Acacia nilotica ambayo hufanya kazi kama kizuizi cha upepo na kuzuia mmomonyoko wa udongo. Acacia nilotica pia ina maganda ambayo wafugaji wanaweza kulisha mbuzi wao na kwa ujumla ni miti mizuri kwa mazingira. Kwa mfano, hutengeneza nitrojeni kwenye udongo, na hulinda ardhi ya mimea dhidi ya moto na upepo, na pia kutoa mizizi ambayo husaidia kushikilia udongo.
Tunawahimiza wakulima pia kupanda miti ya kigeni kama Grevillea na Acrocarpus fraxinifolius ambayo inakua haraka, miti yenye matumizi mengi ambayo inaweza kuvunwa kwa ajili ya mbao au kuni. Acrocarpus fraxinifolius hupandwa vyema katika mipaka ya shamba ambapo hufanya kama kizuizi cha upepo. Grevillea robusta ni mojawapo ya miti bora ya kilimo mseto. Inaweza kupandwa kwenye mipaka ya shamba kwa kuweka mipaka au kama kizuizi cha upepo. Huongezewa na nyasi aina ya tembo ambayo hutia nanga kwenye udongo, pia huimarisha matuta au kontua na kuboresha udongo pale majani yake yanapoanguka na kuongeza mbolea kwenye udongo.
Kilimo cha migomba kimeunganishwa na mazao mengine yenye kufunga kama vile aina ya mikunde. Mikunde hii ni mizuri katika kuongeza nitrojeni kwenye udongo na kukabiliana na mmomonyoko wa udongo. Pia, tunasisitiza kilimo mseto na mbinu za kilimo-ikolojia kwa sababu mbinu hizi hujenga ustahimilivu wa udongo kwa aina tofauti za mmomonyoko.
Vitu hivi vyote vimeongeza mavuno ya mazao. Pia tumeanzisha na kuimarisha ufugaji wa kuku kama chanzo cha mapato na uhakika wa lishe kwa jamii. Hii husaidia wafugaji kuzalisha mayai na kuku kwa ajili ya kuuza na kupata samadi inayohitajika sana kwa mashamba yao yaliyoharibiwa na mmomonyoko wa udongo.
Na nimeona matokeo! Mwaka jana, shamba langu halikuharibiwa na maji yanayotiririka kutokana na mvua—na sio mimi pekee bali wakulima wenzangu ambao walifuata njia kama hizo. Wakulima wengine wanakuja kutuomba ushauri juu ya kutekeleza vitendo kama hivyo ili kuzuia mmomonyoko wa udongo kwenye mashamba yao. Natarajia kwamba robo ekari iliyoharibiwa itarekebishika na nitaweza kulima tena mwaka ujao.
Kwa kuwa ni mimea ya kunde, mimea hii pia hufanya mashamba yetu kuwa na rutuba kwa kuweka nitrojeni kwenye udongo. Pia haziingiliani na mbaazi na mazao mengine ninayopanda. Na wakati miti hiyo ya mikunde inapoangusha majani yake, tunaiacha chini na huongeza mbolea na kuimarisha udongo na kuufanya kuwa na rutuba.
Mafunzo kutoka MVIWA Arusha pia yalitusaidia kujifunza umuhimu wa matandazo kwa ajili ya rutuba ya udongo na kuhifadhi unyevu. Baada ya kuvuna, tulikuwa tunaweka kwa wingi mabaki ya mahindi makavu na zao la njegere na kulisha pia mifugo yetu. Lakini sasa baada ya kuvuna, tunatandaza mabaki ya mazao yaliyokauka juu ya ardhi kama matandazo ili kufunika udongo na kuujaza na viumbe hai ili kurutubisha. Lakini ikiwa ni lazima kutumia mabaki ya mazao kama lishe ya mifugo, tunahakikisha kwamba tunarudisha mbolea ya mifugo shambani.
Gitu, unawashauri nini wakulima wa hapa Karatu wanaokabiliana na mmomonyoko wa udongo na uharibifu wa ardhi kutokana na ulichojifunza kutoka kwa MVIWA Arusha?
Mmomonyoko wa udongo pia unaweza kupunguzwa kwa kupanda miti au kufunika makorongo kwa mimea. Mimea hiyo husaidia kunasa udongo unaobebwa na mkondo wa maji, na hatimaye mifereji kujaa na ardhi kuwa sawa. Ingawa shamba langu liko kwenye mteremko na siku za nyuma nimepata mafuriko mengi, sasa ninalilima kwa njia ambayo hupunguza kasi ya mtiririko wa maji na kueneza maji juu ya shamba ili kusiwe na makorongo na kuna uharibifu mdogo.
Pia tunawahimiza wakulima kutunza udongo kwenye ardhi yao kwa kueneza mabaki ya mazao yaliyovunwa ili kutengeneza matandazo badala ya kuwalisha mifugo. Hiyo hulinda udongo kutokana na jua kali. Na wakati wa kulima unapofika, matandazo huwa mbolea kwenye udongo na kufanya udongo kuwa na rutuba. Mazao ya kufunika ardhi pia husaidia kupunguza kasi ya mtiririko wa maji na kupunguza uharibifu wa ardhi.
Ndani ya Karatu, tunapanda Mucuna pruriens na mimea jamii ya mikunde pamoja na Grevillea robusta na Acacia nilotica ili kusaidia kunasa udongo, kujaza makorongo, na kupunguza mtiririko wa maji. Mucuna ni upupu kwa Kiswahili na lablab ni fiwi au ngwara, wakati Grevillea ni mgrivea na Acacia nilotica ni mgunga. Mazao mawili haya aina ya mikunde hukandamiza magugu na nyasi, zinazojulikana sana kama sangari kwa Kiswahili. Pia, mafunzo zaidi yanahitajika kwa wakulima ambao wana shaka kuwa miti ya mikunde kama sesbania inaweza kuboresha rutuba ya udongo kwenye mashamba yao.
Na ikiwa baadaye utaongezea mbolea ya chumvi chumvi au mbolea ya NPK wakati mahindi yana majani sita au yamefikia kiwango cha goti, hiyo inasaidia kuzuia magugu na kuongeza uwezekano wa kupata mavuno mengi. Kwa kufuata maelekezo haya, unaweza kupata mavuno ya gunia 28 hadi 30 za mahindi kwa ekari moja. Katika ekari zetu tano miaka 15 iliyopita, tulivuna magunia 50 ya mahindi. Leo kwenye hizo ekari tano baada ya mafunzo tunapata magunia 100 au zaidi ya mahindi kwa kupanda kwa njia sahihi. Kwa maharagwe tunapata gunia nane hadi 10 kwa ekari moja, kulingana na aina. Soya ya njano tulikuwa tunapata magunia matatu, lakini leo tunavuna magunia matano kwa ekari moja. Hivyo mafunzo hayo yote ya MVIWA-Arusha yametusaidia kutatua matatizo ya mifereji kwenye mashamba na kuboresha rutuba ya udongo. Na tumeona mabadiliko mazuri.
Ikiwa hautadhibitiwa, mtiririko wa maji unaweza kutengeneza mifereji ambayo hufanya kilimo kuwa na changamoto.
Lakini makorongo yanaweza kufukiwa kwa kupanda miti ya mikunde au mazao ya kufunika au mimea mingine ambayo hupunguza kasi ya mtiririko wa maji na kunasa udongo.
Ukosefu wa rutuba ya udongo unaweza kushughulikiwa kwa kupanda miti ya mikunde au mazao ya kufunika.
Mabaki ya mazao yaliyovunwa yaachwe shambani kama matandazo ili kufunika udongo na kuufanya kuwa na rutuba na pia kupunguza mmomonyoko.
Hakikisha kuwa udongo kwenye vilima una kitu kilichoufunika cha kudumu.
Acknowledgements
Shukrani
Imechangiwa na: James Karuga, Mwandishi wa masuala ya Kilimo, Kenya
Imehaririwa na: Eliud M. A. Letungaa. Afisa Kilimo na Mifugo, Mtandao wa Vikundi vya Wakulima na wafugaji Mkoa wa Arusha (MVIWAARUSHA).