Ujumbe kwa mtangazaji
Muhtasari kwa mtangazaji
Kati ya mwaka 2007 na 2010, mradi wa utafiti wa African Farm Radio Research Initiative (AFRRI) uliofnywa na Farm Radio International ulifanya kazi na vituo vitano vya redio nchini Uganda ili kuandaa kampeni shirikishi za redio (PRCs). Moja ya malengo ya AFRRI lilikuwa ni kutafuta kujua namna redio inavyoweza kuwasaidi wakulima kutumia mbinu bora na za gharama ya chini zinazoweza kuongeza usalama wao wa chakula.
Sauti ya Teso ni moja ya kituo kilichohusishwa katika AFRRI. Aina ya muhogo iitwayo Akena ilichaguliwa kama njia ilyoboreshwa ya kilimo kwa ajili ya moja ya kampeni shirikishi za redio.
Sauti ya Teso iliandaa vipindi shirikishivya kila wiki juu ya muhogo wa Akena kwa kipindi cha miezi sita, wakifanya kazi pamoja na jamii za vijijini, wafanyakazi wa uenezi na wataalam wa kilimo.
Mradi wa AFRRI ulionesha kwamba kampeni shirikishi ya redio juu ililyopangiliwa na kutafitiwa vizuri juu maboresho ya kilimo yaliyochaguliwa na wakulima huweza kulete manufaa makubwa zaidi, sio tu katika meneo lengwa bali hata katika jamii iliyoko nje ya maeneo ya maingiliano ya moja kwa moja.
Mswada huu unaonesha kwa ufupi kampeni hii shirikishi ya redio. Unawasilisha mahojiano na mwandaaji wa kipindi, pamoja na mahojiano na wakulima wawili na wafanyakazi wa uenezi. Mahijiano haya yalifanywa miaka miwili baadaye baada ya umalizikaji wa kampeni shirikishi ya redio.
Kwa taarifa zaidi juu ya mradi wa AFRRI, tembelea tovuti ya AFRRI ya Farm Radio International kwenye: http://www.farmradio.org/english/partners/afrri/
Lengo kubwa la mswada huu ni kuripoti juu kampeni shirikishi zilizofanikiwa nchini Uganda. Lakini pia huweza kukufanye uanze kufikiri juu faida ya kuwashirikisha wakulima katika vipindi vyako. Unaweza kuwauliza wanajamii juu ya mabo muhimu ya usalama wa chakula kwa wakulima wanawake na wanaume katika eneo la wasikilizaji wako. Wakulima wanapenda kusikia sauti zao hewani na za majirani zao. Unaweza ukawahusisha wakulima katika vipindi wa kupiga simu, kwa kurekodi mahojiano na wakulima katika mashamba yao, sokoni, studioni, au katika majadilioano na wafanyakazi wa uenezi au wafanyakazi wengine wa kilimo kwenye kituo.
Mswada huu unatokana na mahojianao halisi. Utautumia kama hamasa ya kufanya utafiti na kuandika mswada juu ya mada iyohiyo katika eneo lako. Au unaweza kuandaa mswada huu katika kituoa chako, kwa kutumi waigizaji kuwakiliasha wazungumzaji. Kama utafanya hivyo, hakikisha unawaambia wasikilizaji wako mwanzoni mwa kipindi, kwamba sauti sio za wahojiwa bali ni za waigizaji.
Script
Mtangazaji 1:
Habari zenu wasikilizaji wetu wote. Jina langu ni ___.
Mtangazaji 2:
Nami naitwa ____. Leo tutakueleza juu ya kampeni ya redio iliyorushwa hewani miaka michache iliyopita na Sauti ya Teso huko mashariki mwa Uganda. Kampeni ilitambulisha kwa wakulima aina ya muhogo unaostahimili magonjwa inayoitwa Akena. Iliwapatia habari nyingi za kutosha juu ya aina mpya ambapo wakulima wangeweza kufanya uamuzi ju ya kupanda au kucha kupanda.
Mtangazaji 1:
Swadakta. Usiondoke kando ya redio yako ili uweze kusikia jinsi ambavyo mradi huu wa pekee ulivyosaidia sio kulete tu usalama mkubwa wa chakula katika mkoa wa Teso, bali jinsi ulivyowahusisha wakulima kwa ukaribu katika kutangaza, na kuweka sauti za wakulimahewani.
Pumziko la dakika ishirini, sauti ya mtangazaji inasikika
Mtangazaji 2:
Karibu tena. Sasa tutakueleza zaidi juu kampeni hii ya redio iliyofanikiwa. Farm Radio International ni shirika lisilo la kiserikali la Kanada lililotekeleza mradi unaoitwa African Farm Radio Research Initiative, au AFRRI, kuanzia mwaka 2007 hadi 2010. Mradi ulitekelezwa katika nchi tano za Afrika – Uganda, Tanzania, Malawi, Ghana na Mali.
Mtangazaji 1:
Moja ya shughuli za AFRRI iliitwa Kampeni shirikishi ya redio au PRC. PRC ilikuwa ikitangazwa na vituo vya redio mahalia na ilihusisha wakulima mahalia. Kwa kila kampeni ya redio, wakulima waliombwa kuchagua mbinu maalumu ya kilimo ambayo ingeweza kuwasaidia kuongeza usalama wao wa chakula. Wafanyakazi wa uenezi na wataalamu wengine pia walichangia kufanya uchaguzi mbinu. Mbinu iliyochohuliwa ndio ikawa kitovu cha kampeni.
Mtangazaji 2:
Mbinu ilipochaguliwa, wakulima na watu wengine walisaidia kuweka sawa maudhui ya kipindi. Wakulima waliingiliana na vituo vya redio wakati wote wa kampeni. Walitumia simu zao kuongea na watangazaji na waandaaji wa kipindi. Taarifa walizozipata kupitiasimu zao ziliwasaidia kufanya uchaguzi wa ama kufanya au kutofanya maboresho.
Mtangazaji 1:
(Pumziko) Muhogo ni zao kuu la chakula kwa jamii watu wa mkoa wa Teso mashariki mwa Uganda. Lakini haikuwa rahisi kwa miaka ya hivi karibuni kulima muhogo. Hii hapa ni historia fupi.
Mtangazaji 2:
Mnamo mwaka 1990, kulikuwa na mlipuko wa magonjwa. Ugojwa hu uliwaumiza wakulima sana, ukawalazimisha kupunguza eneo la kulima muhogo. Familia nyingi zililazimika kununua muhogo kutoka katika wilaya za karibu.
Mambo yalianza kuwa mazuri mwaka 2005. Wazalishaji mimea walitengeneza aina nyingine ambayo ilikuwa inastahimili virusi vya muhogo. Hizi aina mpya zilianzishwa katika mkoa wa Teso. Kwa bahati mbaya, mwaka uliofuata tumaini hili likapotea. Aina hii mpya iliathirika kwa urahisi na ugonjwa wa mistari ya kahawia katika muhogo. Wakulima walipoteza maelfu ya heka za muhogo.
Mtangazaji 1:
Kwa hiyo, mwaka 2007, wakiwa na historia hii akilini, wakulima, wafanyakazi wa uenezi, serikali za mitaa na serikali kuu, wanasayansi wa kilimo na watoa ushauri, walikutana pamoja kupitia mradi wa AFFRI. Walikuta ili kuchagua mbinu ya kilimo ambayo itahamasishwa katika kampeni shirikishi ya redio ya AFRRI. Baada ya mijadala mingi waliamua kwamba kampeni itaweka kitovu katika aina mpya ya muhogo inayostahimili magojwa iitwayo
Akena. Wakulima na washikadau wengine walikuwa na imani kuwa
Akena ingeleta usalama mkubwa wa chakula katika mkoa wa Teso. Kwa hiyo mwaka 2008, AFFRI na Sauti ya Teso ilizindua kampeni shirikishi ya redio juu ya muhogo wa
Akena.
Pumziko la muziki kwa sekunde 10
Mtangazaji 1:
Sauti ya Teso inatangaza programu ya kila wiki inayoitwa Akoriok Akoroto Emwogo, inayomaanisha “Ongeza uzalishaji wa Muhogo wa Akena.” Kipindi kililenga juu ya kuongeza ukubwa eneo la kupanda Akena katika mkoa wa Teso. Kilikuwa kikitangazwa katika lugha ya Ateso kila jumatano jioni na kilirushwa kuanzia Novemba 2008 hadi Aprili 2009. Davies Alachu alizalisha kipindi na Oktel Jonathan akawa mtangazaji.
Mtangazaji 2:
Kampeni ilitoa taarifa za kutosha juu kuhusu muhogo wa Akena. Ilihusiha taarifa juu ya kulima muhogo wa Akena, taarifa juu ya wadudu na namna ya kutibu magojwa; taarifa juu ya mavuno, uhifadhi na usindikaji; na taarifa juu ya namna ya kutafuta mbegu za kupanda. Kampeni ilitoa fursa nyingi kuuliza maswali.
Host 1:
Matangazo yalikuw na mvuto mkubwa! Kwa mujibu wa wafanyakazi wa uenezi, mashirika yasiyo ya kiserikali, na shirika la kitaifa la Uganda linalotoa ushauri juu ya kilimo; programu iliongeza uhitaji mkubwa wa mbegu za muhogo wa Akena na huduma za ushauri kuhusu Akena. Eneo lililopandwa Akena liliongozeka kutoka ekari 25 hadi ekari 82 katika jamii zilizokuwa zinasikiliza kampeni na waliokuwa wakiingiliana na watangazaji.
Host 2:
Lakini je, mafanikio haya yalidumu? Na wakulima walifurahia kupanda muhogo wa
Akena? Unakaribia kufahamu. Mnamo Julai 2011, zaidi ya miaka miwili zaidi baada ya kukamilika kwa kampeni, Farm Radio International ilizungumza na Davies Alachu, mwandaaji wa kampeni ya Sauti ya Teso juu ya Muhogo wa
Akena. Septemba na Novemba 2011, Davies Alachu aliwahoji wakulima mahalia na mfanyakazi wa uenezi. Tutasiki mahojiano hayo yaliyofanywa na Davies Alachu baada ya pumziko fupi la muziki.
Sekunde thelathini za pumziko la muziki
Mhojaji:
Karibu, Davies Alachu. Swali langu la kwanza ni: Ni eneo kubwa kiasi gani lililopandwa mhogo wa Akena limebadilika tangu mwisho wa kampeni ya redio ya AFRRI mnao Aprili 2009?
Davies Alachu:
Eneo limeongezea; watu wanapanda sana muhogo wa Akena sasa hivi kuliko ilivyokuwa kabla ya kampeni.
Mhojaji:
Je, jamii zilizoingiliana kwa ukaribu zaidi? Au jamii zote hupanda kwa wingi muhogo wa Akena?
Davies Alachu:
Zaidi, tunaona ongezea katika jamii zinazosikiliza sana. Lakini watu ambao hawapo katika eneo mabapo matangazo ya redio huishia, sasa wanahitaji sana mbegu za muhogo na taarifa juu kuhifadhi baada ya mavuno. Wanaona namna ambavyo wakulima wngine walijufunza kutokana na kampeni, na wanahitaji faida hizo pia.
Mhojaji:
Je, wakulima wameridhika na maendeleo ya muhogo wa Akena?
Davies Alachu:
Ndio, watu wanaufurahia. Katika moja ya soko, wakulima baadhi kutoka katika kijiji cha Amootot walileta muhogo wao sokoni, na cha kufurahisha zaidi mihogo waliyoleta ilikuwa safi sana. Kwa kweli walikuwa makini na kipindi na walijua walitakiwa kuiosha na kuikausha katika mazingira yenye ukavu. Kwa sababu ilikuwa safi sana, ilitengeneza unga daraja la kwanza na ulipata bei ya juu kuliko muhogo mwingine.
Mhojaji:
Kumekuwa na badiliko lolote juu ya muhogo unavyouuzwa baada ya kampeni ya redio?
Davies Alachu:
Ndio. Kwanza kabisa, ubora wa muhogo umeongezeka na wakulima wanapata bei kubwa. Na wakulima pia wanajaribu kufanya mauzo ya pamoja, kitu kilchosisitizwa wakayi wa kampen. Kwa mfano, kama mkulima mmoja ana na beseni moja la mhogo, mwingine ana moja na wa tatu ana matatu, wanayaunganisha kwa pamoja na kasha wanamchagua mtu kuyapeleka sokoni. Wanaweka rekodi ya mabeseni aliyochangia kila mtu. Alafu baada ya mauzo wanagawanya pesa kulinagana na kila mtu alivyochangia.
Kuna kiasi fulani cha thamani kilichoongezeka kwa sababu ya masomu toliyowapa kutoka wenye kipindi chetu ju ya kuyaangalia baada ya mavuno – kuosha muhogo, kuukausha, nk.
Mhojaji:
Je, uhusikaji wako katika kampeni shirikishi ya redio umebadilisha mtazamo wako wa kuangalia wajibu wako kama mtangazaji?
Davies Alachu:
Safi, mfumo waliotumia AFRRI na mafunzo waliyotupatia, yalitusaidia kwa kiwango kikubwa kuingiliana na wakulima. Mifumo tofautitofauti ya vipindi, rekodi za mashambani, kuwapigia simu wataalamu, na wakulima kutupigia simu – ilibadilisha hali kiasi kwamba wakulima ndio waliokuwa wamiliki wa kipindi hiki.
Tulipokuwa tunakwenda mashambani, wakulima waliweza kuzungumza nasi kwa uhuru zaidi. Walijisikia kuwa wao ninsehemu ya kipindi na kipindi kilikuwa ni cha kwao. Kwa kweli ilikuwa ni wazi sana – waliweza kuwa na majadiliano wa wafanyakaziwa uenezi, na waliweza kuelza masuala yao. Wafanyakazi wa uenezi walifanya maandamano hadi kwenye mashamba ya wakulima. Kwa mfan, mkulima anaweza kuleta muhogo ukiwa na ugonjwa Fulani, na wafanya kazi wa uenezi waliweza kuwaonesha hatua kuepuka ugonjwa ule wakiwa mlemle shambani.
Mhojaji:
Je, mwingiliano wa aina hiyo kati ya wakulima na wafanyakazi wa uenezi ulikuwepo kabla ya kampeni?
Davies Alachu:
Kulikuwa na mwingiliano mdogo kabla ya kampeni. Yalikuwa ni mawasiliano ya moja kwa moja. Pengine unapotokea mlipuko wa magonjwa ndipo baadhi ya wataalamu wanakuja kituoni na kulipia kipindi alafu wanatoa mhadhara – kuongea kwingi, kuongea, kuongea, kongea. Watu walikuwa wanapiga simu lakini waliweza kujibu maswali machache tu. Na hivyo ndivyo ilivyokuwa. Halikuwa suala la mwendelezo; kilikuwa ni kitu ambacho kngeweza kutkea wakatika wa majanga.
Lakini aina ya maingiliano iliyoanza wakati wa kampeni, ndiyo inayoendelea mpaka sasa hivi, kwa sababu hata sasa hivi tuanaendelea kufanya kipindi. Tunangaza katika jamii tuliyofanya nayo kazi wakati wa kampeni, na tunajaribu kupanua kwenda katika maeneo mengine. Baadhi ya wakulima katika jamii tuliyofanyanayo kazi wameelimika vya kutosha. Kwa hiyo sasa wakulima wanelimishana wao kwa wao.
Mhojaji:
Inasemekana kuwa wakulima wanapenda kusikia sauti zo na sauti za majirani zao redioni, Je, umegundua kuwa hiyo ni kweli?
Davies Alachu:
Ndio, ni kweli tumegundua hivyo. Wakulima katika jamii ambazo tulikuwa hatufanyi nao kazi, walikuwa wanatupigia na kutuuliza lini tutakwenda kuwahoji. Walisema kuwa wao pia walitaka kusikia mambo yao yanazungumzwa rediona na kufafanuliwa na wataalam. Waliabainisha kuwa redio inaweza kuwa jukwaa bora zaidi kwa ajili yao kujifunza lakini pia kwa ajili kuzungumzia changamoto zao.
Mhojaji:
Je, kujihusisha katika kampeni kumebadilisha namana unavyotafitina kuaanda vipindi kwa ajili ya wakulima?
Davies Alachu:
Ndio, kumebadilisha kwa kiwango kikubwa sana. Kabla ya hapo, pengine ulikuwa unaweza kupata shirika lisilo la kiserikali ndio linakuja kituoni. Walikuwa na lengo lao maalum, baadhi ya mambo waliyotaka kuyazungumzia juu ya wakulima, kilimo au pengine walitaka kuzungumzia juu ya shughuli zao. Lakini hili kwa kweli lisingeweza kuwavutia wakulima. Wakulima wanataka kujua namna gani wanaweza kupa mavuno mengi katika migomba yao au muhogo au mazao mengine muhimu ya chakula wanayolima. Kwa mfano, inaweza kuwa ni fursa iliyopotea endapo utazungumzia juu ya matikiti maji, kwa sababu wakulima wachache sana ndio hulima matikiti maji. Hivyo ndivyo tulivyokuwa tukifanya programu za mkulima, ambazo kwa kweli hazikuwa za kitaaluma.
Tulipoanza kampeni ya AFRRI, tuligundua kwamba unatakiwa kwenda kwa wakulima kwanza ili kujua mahitaji yao ni yapi. Alafu unatafuta mtu sahihi ambaye angeweza kuelezea hayo mahitaji. Na wakulima walifurahishwa kweli na mtazamo huo. Mtazamo huo ulitusaidi sit u kubadili vipindi vyetu vya shambani na kilimo bali hata vipindi vyetu vya afya.
Mhojaji:
Kwa mtazamo wako, unadhani kampeni hiyo ilifanikiwa?
Davies Alachu:
Ndio, ilifanikiwa, ingawaje wakulima bado wanamahitaji mengi. Na hiyo ndio sababu tukaamua kuendelea na programu, ingawaje muda mwingine kutembelea mashambani kunakuwa hafifu. Kunapokuwa hakuna usafiri wa kutupeleka mashambani, tunawapigia simu wakulima alafu tunarekodi simu zao. Tunawatafuta wataalam wanakuja hapa katika ofisi zetu.
Lakini ingekuwa vizuri zaidi kutoka na kwenda kuchangamana kwa uhuru na wakulima, na kuwarekodi. Hii kwa kweli ingeweza kutoa ujumbe mzito. Kwa hiyo changamoto kubwa ni kwenda mashambani na kufanya mahojiano.
Mtangazaji 1:
Kifuatacho, ni Davies Alachu akiongea na mkulima aliyekubali kulima mhogo wa Akena kama matokeo ya kampeni ya AFRRI. Endelea kututegea sikio.
Ungeza sauti ya shambani – wanyama, ndege, sauti za watu wakitembea wakitembea shambani. Punguza na achia sauti ya mahojiano.
Davies Alachu:
Habari za asubuhi, Bi. Alaso. Ulijifunza nini kutoka katika programu ya AFRRI juu ya muhogo wa Akena?
Bi. Alaso:
Tulijifunza juu ya aina tofautitofauti za muhogoa kama vile Akena, 2961, na nyingine nyingi. Unajua watu wengine walifaidika kutoka kwetu kwa kuwa waliona sisi ni wajinga. Lakini sasa tuna maarifa yote muhimu. Hii imetusaidi kuweka pesa walizokuwa wakituibia watu waliokuwa wakiuza madawa. Tumejifunza namna ya kutambua magonjwa mengi ya muhogo. Kwa magonjwa mengi, tiba ni kung’oa tu mche uliathirika na kuuchoma moto. Pia programu ya AFRRI imetusaidia kuingiliana na wafanya kazi wa uenezi na katika studio na mashambani.
Davies Alachu:
Kipi kngine ulichojifunza juu ya muhogo wa Akena?
Ms. Alaso:
Tumejifunza jinsi ya kupanda kwa kuacha nafasi kati ya mche na mche, kipindi cha kupanda na kipindi cha kuvuna. Hii yote huchangi mavuno mazuri.
Tulijufunza jinsi ya kusimamia vizuri mhogo wetu baada ya mavuno na kuhakikisha kuwa ni safi. Kwa mfano, hatukuzoea kuosha mhogo baada ya kuvuna. Tungeweza kuuanika mahali popote pale. Lakini tulifundishwa mbinu za kuangalia mhogo baada ya mavuno ili kuongeza thamani ya mhogo. Hivyo, sasa hivi baada ya kuvuna mhogo tunauosha na kuuanika katika sehemu safi. Mwishowe tunapata unga mweupe sana, safi bila mchanga.
Davies Alachu:
Unapoangalia kipindi cha nyuma wakati kampeni ilipoanza, je, eneo lako la kupanda muhogo limeongezeka uilinganisha na kabla ya kampeni?
Bi. Alaso:
Oo, limeongezeka sana, kama unavyoona. Nina uhakika umeona wakati ulipokuwa unakuja hapa kwamba kila mtu hapa kijijini ana hekta za mhogo zisizopungua moja. Ilikuwa imezoeleka kulima chini nusu hekta. Sasa tutalima eneo kubwa zaidi, kwa kuwa tunajua jinsi ya kuongeza thamani kwenye mhogo ili kupata pesa nyingi zaidi ukilinganisha na siku za nyuma tulipokuwa tunauza kwa bei ya chini. Tunapanga pia kutengeneza gari. (Maelezo ya mhariri: Gari ni unga unaotengenezwa kutokana na mizizi ya mhogo.)
Davies Alachu:
Ulikuwa unatumia njia gani kuuza muhogo wako kabla ya kampeni ya redio na sasa unatumia njia gani?
Bi. Alaso:
(Anachekelea) Baadhi ya watu walikuwa wanauza muhogo wao wakati ukiwa bado upo shambani. Wengine walichukua ukiwa mbichi na kupeleka sokoni na kuiuza katika mafungu madogo madogo kwa shilingi 300 hadi 500 za Uganda kwa kila fungu (Maelezo ya mhariri: karibu senti 12 -20 za marekani). Wengine waliukausha na kuuza kwa wafanya biashara wanaousaga na kuuza kama unga wa muhogo.
Pia tulikuwa tunalima muhogo mashamba madogomadogo kwa ajili ya kula nyumbani. Lakini kuanzia redio AFRRI ije, sasa tunalima muhogo kwa kiwango kikubwa na tunauza kama kikundi. Kwa njia hii tuna uwezo wa kupata pesa nyingi zaidi. Inaitwa uuzaji wa pamoja na tunawakwepa watu wa katikati ambao wanatulaghai.
Davies Alachu:
Sasa kampeni imekwisha, je, bado unatumia muhogo wa Akena?
Bi. Alaso:
Ndio tunatumia, na aina nyingine pia kama vile Mygeria – ambayo tunaiita mbegu ya Nigeria. Akena sasa hivi inashambuliwa na ugonjwa wa mistari ya kahawia. Lakini bado tunaupanda kwa sababu tuna machaguo machache.
Davies Alachu:
Mambo gani mengine uliyojifunza kwenye kampeni ya redio ya AFRRI?
Bi. Alaso:
Kwa sababu programu ilikuwa katika lugha ya kienyeji na kwa kuwa wakulima walihusishwa, ilitusaidia kujifunza kutoka kwa wakulima wengine. Hivyo nikagundua kuwa redio ni chombo chenye nguvu sana katika kuelimisha na kuwafundisha wakulima. Na pia nilijifunza kuwa watu wa redio sio watu wa kujivuna. Watangazaji sikuzote walikuwa wanakuja na kukaa pamoja nasi, kurekodi sauti zetu, na kupeleka redioni.
Davies Alachu:
Endapo kampeni ingekuwa inaendelea, je, ungependa kusema nini?
Bi. Alaso:
Tungependa ienee hadi kwenye mazao mengine na kutufundisha jinsi ya kuongeza thamani kwenye mazao mengine, kama tulivyojifunza kwenye muhogo.
Ongeza sauti za shambani, kisha badili sauti za shambani kwenda kwenye muziki, kisha shusha muziki na achia sauti ya mtangazaji
Mtangazaji 1:
Tutarudi baada ya muda mfupi tukiwa na mahojiano na Bw. Opus Joseph, mfanya kazi wa uenezi aliyefanya kazi katika kampeni ya redio ya Akena. Baki nasi.
Muziki kwa sekunde 20 kisha ondoa
Mtangazaji 1:
Hapa tena ni Davies Alachu, akimhoji Bw. Opus Joseph.
Davies Alachu:
Kama ofisa uenezi, una maoni juu ya pengine wakulima wameongeza ulimaji wa muhogo wa Akena tangu uanzishwaji wa kampeni ya redio?
Opus Joseph:
Ndio, kwa sababu kadhaa. Kwanza walipta taarifa juu ya wapi pa kupata mbegu sahihi za kupanda, pamoja na bei na taarifa nyinginezo. Pili vipindi vya redio viliwapatia maarifa juu ya kuongeza thamani, uuzaji wa pamoja, uangalizi baada ya mavuno, kutambua na kudhibiti viini vya magonjwa, na namna ya kutofautisha mbegu nzuri na ile ambayo tayari imethiriwa na magonjwa. Pia iliwasaidia kujua wakati wa kupanda na aina gani ya udongo inayotoa mavuno mazuri.
Hata hivyo kwa bahati mbaya, muhogo wa Akena ulishambuliwa na ugonjwa wa muhogo wa mistari ya kahawia. Baada ya hapo wakulima wengi wakaacha kuulima na wakaanza kulima aina nyingine ya Mygeria au 2961. Vilevile hata 2961 ilishambuliwa na ugonjwa wa mistari ya kahawia.
Davies Alachu:
Wewe kama mfanyakazi wa uenezi, uliona changamoto gani katika kufanya kampeni ya Akena?
Opus Joseph:
Ambapo redio imethibitika kuwa chombo muhimu sana katika kuwaelimisha wakulima, sio familia zote zina redio. Pia muda wa kipindi haukuwa muafaka katika mazingira Fulani. Pia wakati mwingine mtaalam mahususi alikuwa hapatikani kwa ajili ya kuzungumza. Na mwisho muda wa kipindi ulikuwa mfupi sana.
Davies Alachu:
Kama mfanyakazi wa uenezi, ulijifunza nini katika kuhusika kwako kwenye kampeni ya Akena?
Opus Joseph:
Nilijifunza umuhimu wa kutumia vikundi kupeleka taarifa; nilijifunza jinsi ya kutumia vifaa vya ki-TEHAMA kama vile MP3, na nilijifunza namna ya kuandaa vipindi katika studio kwa kuhariri mahojiano, nk.
Davies Alachu:
Ukiangalia nyuma, kampeli ilikuwa yenye mafankio?
Opus Joseph:
Sana, ilifanikiwa sana kwa sababu uuzaji na uongezaji wa thamanivilisisitizwa kwa nguvu sana.
Davies Alachu:
Asante sana kwa muda wako, Bw. Joseph Opus.
Weka muziki kwa sekunde tano, alafu achia sauti ya watangazaji
Mtangazaji 1:
Leo umesikia yote kuhusu kampeni ya redio iliyofanya na Redio Sauti ya Teso na Farm Radio International. Kampeni iliongeza ekari za muhogo wa Akena katika jamii zilizokuwa zikisikiliza na kuchangamana na vipindi – na hata katika jamii zilizokuwa mbali na eneo la usikilizaji.
Mtangazaji 2:
Hiyo ni kweli. Kama ulivyosikia kutoka kwa afisa wa uenezi, wakati fulani baada ya kampeni ya redio kuisha muhogo wa Akena kwa bahati mbaya ulishambuliwa ugonjwa wa mistari ya kahawia. Lakini hii haimaanishi kampeni hiyo haikufanya kazi.
Mtangazaji 1:
Hapana kabisa. Kampeni imeonyesha kuwa mfululizo wa vipindi vya redio uliojikita katika mbinu za kilimo ambo wakulima wamezichagua na ambazo wakulima hushiriki huweza kuongeza utekelezaji wa mbinu hizo. Hii ni habari njema wa waandaaji wa vipi vya redio vya mkulima!
Mtangazaji 2:
Ndio, ni habari njema! Huyu ni ___ nakuaga kwa sasa. Tuna imani umefurahia kipindi chetu.
Mtangazaji 1:
Na huyu ni __. Kwa herini.
Uongeza sauti ya muziki, subiri kwa dakika 15, alafu ondoa.
Acknowledgements
Imechangiwa na: Vijay Cuddeford, Mhariri mtendaji, Farm Radio International
Imepitiwa upya na: Askebir Gebru, Mkuu wa kipindi, Uganda, Farm Radio International
Information sources
Vyanzo vya taarifa
Mahojiano na Davies Alachu, Mwandaaji, Sauti yaTeso, Julai 15, 2011.
Mahojiano na Bi. Alaso, yalifanywa na Davies Alachu Septemba 22, 2011.
Mahojiano na Bw. Opus Joseph, yalifanywa na Davies Alachu Novemba 25, 2011.
Mradi umefanywa kwa msaada wa Serikali ya Kanada kupitia Shirika la Maendeleo ya Kimataifa la Kanada (CIDA)