BH2: Kutumia majukwaa ya kwenye mtandao kwa utangazaji ukiwa mbali na studio

Script

Save and edit this resource as a Word document

Kwa nini nitumie majukwaa ya kwenye mtandao kunisaidia kutangaza nikiwa mbali na studio?

Wakati mwingine inaweza kuwa ngumu kwa watangazaji wa redio kukutana ana kwa ana na watu wa kuwafanyia mahojiano kwasababu mbalimbali ambazo zinaweza kuwa za kifedha au mipangilio ikijumuisha ukosefu wa muda. Kwa mfano, wakati wa janga la COVID-19, hatari ya kuripoti habari mahali au kukutana uso kwa uso na watu wanaohusika inaweza kuwa kubwa kwa watangazaji na watu wengine. Kwa bahati nzuri, kuna majukwaa kadhaa kwenye mtandao ambayo watangazaji wanaweza kutumia kufanya mahojiano na wakulima au wataalam wa kilimo, au kuitisha mikutano ya hadithi, majadiliano katika jopo wakati wa vipindi vya majadiliano ya moja kwa moja kwa njia ya redio au yaliyorekodiwa awali, kuitisha vikundi vya wasikilizaji katika jamii, na kufanya aina nyingine ya kazi ya utangazaji. BH2 hii itajumuisha majukwaa yanayotumiwa sana, ambayo ni pamoja na:

 • Zoom
 • Skype
 • Mawasiliano na mikutano kwa njia ya Google (Google Chat na Google Meet – Zamani ikijulikana kama Google Hangouts)
 • WhatsApp
 • Telegram

Ninawezaje kutumia majukwaa haya kunisaidia kutangaza nikiwa mbali na studio?

Kila jukwaa lina kazi na huduma tofauti tofauti (kama ilivyoainishwa katika sehemu inayofuata), lakini kwa ujumla zote zinaweza kutumiwa:

 • Kufanya mahojiano kwa njia ya sauti na/au video;
 • kufanya mahojiano ya mtu mmoja au mawasiliano ya kikundi na wafanyakazi wa kituo cha redio; na
 • kutuma mafaili kama vile nyaraka zilizo katika muundo wa Ms word, PDFs, picha na video kupitia kwenye mtandao.

Tafadhali kumbuka kuwa majukwaa haya yote yanahitaji mambo yafuatayo:

 • muunganisho thabiti wa WiFi au data ya mtandao (3G au 4G / LTE)
 • spika na maikrofoni (iliyowekwa kwa ndani, USB iliyochomekwa, au Bluetooth)
 • kamera ya video (aidha iliyowekwa kwenye kifaa chako, Bluetooth, au iliyo na USB iliyochomekwa)

Kabla ya kuanza na majukwaa ya kwenye mtandao, haswa wakati wa janga la COVID-19 linaloendelea, unaweza kutaka kusoma BH2s zetu za kufanya kazi kwa mbali kama mtangazaji wa redio na jinsi watangazaji wanavyoweza kukaa salama wakati wa janga la COVID-19.

Na kwa jinsi gani kutumia majukwaa kwenye mtandao kunanisaidia kuwahudumia wasikilizaji wangu vizuri?

Wanahabari wa redio wana jukumu muhimu la kuhakikisha kuwa wasikilizaji wao wanapata habari ya kuaminika na iliyohakikiwa ambayo wasikilizaji hawawezi kuipata wao wenyewe, au watapata ugumu wa kuipata kwa njia ambayo wanaweza kuelewa kwa urahisi. Wakati mwingine hii inamaanisha kuwa watangazaji lazima wachukue hatua za ziada kuwasiliana na vyanzo vya habari hiyo kwa njia ya simu, barua pepe, ujumbe wa maandishi, au simu kwa njia ya video. Kutumia majukwaa haya ya kwenye mtandao kuwasiliana na wakulima, wataalam wa mada, maafisa wa serikali, na vyanzo vingine au watu ambao huwezi kukutana nao binafsi itahakikisha wasikilizaji wako wanapata maarifa muhimu.

Uingiliano wa majukwaa haya pia hukuruhusu kushirikishana mafaili (kwa mfano, picha, video, maelezo, au hati zingine) na watu wako wa kuwafanyia mahojiano ili waweze kuelewa habari wanayoshiriki nawe, na kupata maoni kwa wakati halisi. Kwa mfano, ikiwa unashiriki kwa njia ya video na afisa wa serikali kuhusu sera mpya ya kilimo, unaweza kupitia rasimu ya sera kwenye skrini yako na uwaulize waeleze kila hoja. Au, ikiwa uko kwenye simu kwa njia ya video na mkulima, unaweza kupitisha ushauri au ufahamu-na labda hata uwaangalie wakitekeleza njia hizo za kilimo kwenye skrini.

Majukwaa ya kwenye mtandao yaliyoelezewa katika namna – ya – kuuongoza Watangazaji pia huwapa wasikilizaji fursa zaidi za kushiriki katika vipindi vya redio kwa kushirikisha maelezo ya sauti, picha, video, au ujumbe wa maandishi. Wanaweza pia kuwapa wanawake nafasi ya kushirikisha maoni na mrejesho wao bila kuhisi kutishwa au kukatishwa tamaa na majadiliano yanayotawaliwa na wanaume.

Ninaanzaje?

 1. Majukwaa haya ya kwenye mtandao yanafanayaje kazi?
 2. Zoom
 3. Skype
 4. Mawasiliano kwa njia ya Google (Google chat) na mikutano kwa njia ya Google (Google Meet)
 5. WhatsApp
 6. Telegram

Maelezo

1. Majukwaa haya ya kwenye mtandao yanafanayaje kazi? (Jifunze zaidi juu ya kila jukwaa hapa chini.)
Ili kutumia majukwaa haya ya kwenye mtandao vizuri na kutambua ni jukwaa lipi ambalo ni bora kwako na hadhira yako, unapaswa kuzingatia mambo yafuatayo:

 • Gharama (Usajili ni bure au kuna malipo ya kulipia)
 • Mahitaji ya mfumo
 • Vifaa vya kusaidia mfumo
 • Vipengele vinavyopatikana
 • Mapungufu
 • Ni nani unajaribu kuwafikia

Ni muhimu kutumia majukwaa haya kama njia mbadala ya kuwafikia wakulima pia (sio tu wataalamu wa mada) ambao inaweza kuwa ngumu kukutana nao ana kwa ana. Unaweza pia kutumia majukwaa haya kushiriki na vikundi vya wasikilizaji katika jamii.

Hapa kuna njia kadhaa za kuwatumikia wasikilizaji wako vizuri kwa kuwasiliana ukiwa mbali, zaidi ya kupiga tu simu:

 • Kufanya mahojiano kwa kutumia sauti /ujumbe wa sauti. Hii inaruhusu wahojiwa kutoa majibu ya kina zaidi na halisi kuliko kwa kuandika ujumbe. Inawaruhusu pia kujielezea kwa lugha yao wenyewe, bila kulazimika kuandika. Unaweza kuhamisha faili za sauti kutoka kwenye simu kwenda kwenye kompyuta, kubadilisha faili kuwa MP3, na kisha kuhariri rekodi ili kucheza mubashara kwenye programu ya redio.
 • Kuunda vikundi vya wasikilizaji na wataalam wa mada kujadili mada fulani. Kwa mfano, unaweza kuunda kikundi cha WhatsApp na wafanyikazi wa afya au kilimo, wataalam wa eneo hilo, na watu wengine muhimu. Ili kuepuka mafuriko ya ujumbe, jaribu kuunda vikundi viwili tofauti: kundi moja la wasikilizaji na moja la ya wataalamu, na kisha ushirikishe habari muhimu zaidi kutoka kwa wataalamu kwenda kwa wasikilizaji-na habari muhimu zaidi kutoka kwa wasikilizaji kwenda kwa wataalamu.
 • Vikundi vya wanawake pekee ni njia nzuri ya kuhamasisha wanawake zaidi kushiriki na kushirikisha maoni yao hewani bila kutishwa au kukatishwa tamaa na idadi kubwa ya wapigaji simu wa kiume. Kwa mfano, unaweza kuunda Telegraph tu ya wanawake au kikundi cha WhatsApp au laini ya simu kwa ajili ya wanawake tu.
 • Kutoa ripoti za soko na hali ya hewa moja kwa moja kwa wasikilizaji. Unaweza kutuma habari kama ujumbe wa sauti au ujumbe ulioandikwa. Wahimize wasikilizaji kuipeleke pia kwa wanajamii wengine.

Kwa habari zaidi juu ya kuwahoji wakulima, soma BH2 yetu juu ya Jinsi ya kuwafanya wakulima wazungumze juu ya vitu muhimu (Kuwezesha sauti ya mkulima).

2. Zoom

Vipengele vya msingi

Zoom ni huduma ya kwenye mtandao ambayo unaweza kuitumia kushirikisha video mtandaoni, sauti, ushirikishaji wa yaliyomo, na kuwasiliana na ambayo unaweza kuitumia kuandaa mikutano, wavuti (mihadhara), majadiliano katika jopo, na zaidi. Ili kutumia Zoom, lazima upakue programu ya bure kwenye simu au kompyuta na ujisajili kwa akaunti ya bure.

Kuna aina nne za programu zinazopatikana kwenye Zoom: aina tatu za programu za kulipiwa na moja bure. Pale ambapo mwenyeji akipanga simu ya Zoom, jukwaa litatoa Kitambulisho cha Mkutano, kiungo cha kujiunga, nambari ya ufikiaji, na nambari ya simu ambayo inaweza kutumika na washiriki hadharani au kwa mwaliko tu (angalia hapa chini). Washiriki ambao hawana programu ya Zoom wanaweza kujiunga na mkutano wa Zoom kupitia kivinjari cha Mtandaoni au kwa kutumia laini ya simu.

Programu ya bure ya Zoom inajumuishavipengele vifuatavyo:

 • Mikutano: Jukwaa ambalo linaruhusu washiriki wote kuona, kuzungumza, kusikia, na kushiriki skrini kwa kila mmoja. Kwa maelezo juu ya kupanga mkutano wa Zoom, bonyeza hapa.
 • Wavuti (Webinars): Jukwaa la kutazama tu ambapo washiriki hawawezi kuonana na mwenyeji hawezi kuona waliohudhuria, lakini anaweza kuwasilisha kwao moja kwa moja. Kwa maelezo juu ya upangaji wa wavuti ya Zoom, bonyeza hapa.
 • Namba za siri (Passcodes): Kwa ajili ya usalama, nambari za siri zinaweza kuwekwa kwa ajili ya mikutano na wavuti, lakini pia unaweza kuandaa mikutano bila kuweka namba ya siri. Wakati mwenyeji anapanga mkutano au wavuti na kutuma mwaliko, mfumo hutengeneza na kushirikisha Kitambulisho cha Mkutano, kiungo cha kujiunga, na nywila na washiriki wote. Kwa habari zaidi juu ya nambari za siri, bonyeza hapa.
 • Kushiriki skrini (Screen sharing): Wakati wa mkutano wa Zoom, wenyeji na washiriki wanaweza kushiriki pamoja skrini yao ya simu au ya kompyuta na wengine. Kwa usaidizi wa jinsi ya kushiriki skrini, bonyeza hapa.
 • Huduma ya mazungumzo (Chat service): Mikutano ya Zoom na wavuti inajumuisha huduma ya mazungumzo ambayo inawezesha washiriki, jopo na wenyeji kuwasiliana kwa kuuliza maswali, kutoa maoni, au kutumiana mafaili. Mwenyeji anaweza kuhifadhi ujumbe/mazungumzo kwa matumizi ya baadaye. Ili kupata maelezo zaidi kuhusu huduma ya mazungumzo ya Zoom, bonyeza hapa.
 • Kurekodi: Mwenyeji anaweza kurekodi na kuhifadhi mikutano na wavuti kwenye Zoom Cloud (uhifadhi wa mtandaoni wa dijiti) au kwenye kompyuta yao au kwenye simu. Kumbuka kuwa programu ya kulipiwa inahitaji kuhifadhi kwenye Zoom Cloud. Ili kujifunza jinsi ya kurekodi mkutano au wavuti, bonyeza hapa.

Sifa za programu ya kulipiwa ya Zoom zinajumuisha:

 • Mikutano ya kikundi isiyo na kikomo
 • Kikomo cha saa 30 kwa mikutano
 • Uwezo wa kuhifadhi katika anga (Cloud storage)
 • Utiririshaji katika mitandao ya kijamii
 • Malipo ya kila mwezi au kila mwaka

Ninawezaje kutumia Zoom kama mtangazaji wa redio?

Unaweza kurekodi simu ya Zoom pale ambapo unamhoji mgeni wa programu yako ya redio na kuhariri rekodi hiyo ili kuicheza mubashara kwenye programu ya redio moja kwa moja. Au unaweza kuitisha simu ya Zoom ambayo hutumika kama mahojiano au majadiliano katika jopo wakati wa kipindi mubashara cha redio. Hakikisha tu kuwa wewe na wageni wako mna muunganisho wa mtandao ulio thabiti.

Jukwaa la Zoom pia linaruhusu watangazaji kushirikisha ujumbe au faili katika huduma ya mazungumzo, pamoja na maandishi, ripoti, maswali ya mahojiano, picha, video, na zaidi. Watangazaji wanaweza kuhifadhi mafaili moja kwa moja kwenye kifaa chao.

Zoom pia inafaa kwa kuitisha mikutano na timu yako ya uzalishaji wa vipindi ya kituo cha redio, pamoja na mikutano ya upangaji wa simulizi, mikutano ya utawala, na mikutano mingine ya kibiashara. Ni mwenyeji tu ndiye anayehitaji kuwa na programu ya Zoom kwenye simu au kompyuta yake na wengine wanaweza kujiunga kwa kutumia kiunga cha kivinjari cha wavuti au kwa laini ya simu.

Kumbuka kuwa, kupata faida ya kazi zote za Zoom na vipengele vilivyo orodheshwa hapo juu, inashauriwa kupakua programu ya bure.

Mapungufu ya kutumia Zoom

Programu ya bure inaruhusu mikutano halisi na hadi washiriki 100 kwa kiwango cha juu cha dakika 40. Wakati kikomo kinafikiwa, mwenyeji anahitaji kuanza mkutano mpya na kiunga kipya cha kujiunga, Kitambulisho cha Mkutano, na nywila. Mikutano ya mtu mmoja mmoja haina kikomo cha wakati.

Programu ya kulipiwa (Ya Kibiashara) huja na huduma zingine, ikijumuisha kuongezeka kwa kikomo cha muda wa mikutano, uwezo wa kupiga kura, kugawanya vyumba vya mkutano, Kurekodi kwa njia ya anga (Cloud recording), uhifadhi wa data kwenye anga (Cloud storage), tafsiri ya wakati mmoja, na huduma nyingine zaidi.

Kwa habari zaidi juu ya bei na aina ya programu za Zoom, bonyeza hapa.

Mahitaji ya mfumo

 • Windows 7 au kubwa zaidi
 • Mac OS X ikiwa na Mac OS 10.9 au kubwa zaidi
 • iOS 8.0 au toleo la baadae
 • Android OS 5.0 au toleo la baadae

Vifaa ambavyo programu hii inaweza kufanya kazi:

 • Desktop PC (Windows, Mac, Chrome OS)
 • Vifaa vya Android
 • iPhone, iPad, iPod Touch
 • Windows ya tablet

Kwa orodha kamili ya mahitaji ya mfumo wa Zoom na mifumo ya uendeshaji inayoungwa mkono, bonyeza hapa.

3. Skype (inamilikiwa na Microsoft)

Vipengele vya msingi

Skype programu ya kufanya simu za sauti na video za bure na kuzungumza na watu popote ulimwenguni. Unachohitaji tu ni muunganisho wa mtandao, kipaza sauti / spika za kichwani/masikioni (au unaweza kutumia tu kipaza sauti na spika zilizotengenezwa kwenye kifaa chako), na akaunti ya bure ya Skype, ambayo unaweza kuisanidi baada ya kupakua Skype kwenye kompyuta yako au simu yako. Unaweza pia kuingia kwenye Skype ukitumia akaunti ya Outlook, Hotmail n , au Microsoft.

Unaweza kutafuta watu kwenye Skype kwa jina, nambari ya simu, au barua pepe, na kuunda orodha ya anwani.

Vipengele vya msingi vya Skype vinajumuisha:

 • Mikutano (angalia sehemu ya Zoom hapo juu)
 • Kushiriki skrini pamoja (angalia sehemu ya Zoom hapo juu)
 • Kushirikishana mafaili, ikijumuisha picha, video, ujumbe wa sauti, PDFs, majedwali, na mafaili mengine.
 • Mkutano kwa njia ya simu na hadi watumiaji wengine wa Skype 20 kwa wakati mmoja
 • Kupiga simu za mezani na simu za mkononi kutoka mahali popote ulimwenguni. Unaweza kutumia Skype kupiga simu kwa simu za mezani au simu za mkononi kwa kiwango fulani cha ada au tozo. Ili kujifunza zaidi kuhusu Skype kwa simu za kimataifa, bonyeza hapa.
 • Kurekodi: Skype pia hukuruhusu kurekodi simu ndani ya programu, na kisha uhifadhi na upakue rekodi hiyo kama faili ya video ya mp4 au faili ya sauti ya mp3. Kumbuka kuwa rekodi zinahifadhiwa ndani ya sehemu ya kutumiana ujumbe hadi siku 30 kabla ya kufutwa otomatiki.

Ninawezaje kutumia Skype kama mtangazaji wa redio?

Skype ni muhimu kwa ajili ya kurekodi mahojiano na watu ambao inaweza kuwa ngumu kuwafikia. Kwa mfano, mtangazaji kutoka kituo cha redio vijijini anaweza kukosa nauli kwa ajili ya usafiri na fedha kwa ajili ya malazi kwenda kufanya mahojiano ya ana kwa ana na mtaalam wa kilimo anayeishi mbali. Kwa kutumia Skype, mtangazaji huyo angeweza kumpigia simu mtaalam kutoka kwenye kituo au kutoka kwenye mgahawa wa mtandao ulio karibu zaidi, kurekodi mahojiano moja kwa moja kwenye programu, na kuhifadhi rekodi hiyo kwa video bora ya mp4 au katika mfumo wa sauti ya mp3 ambayo iko tayari kutangazwa.

Mapungufu ya kutumia Skype

Programu ya bure ya Skype inaruhusu hadi washiriki 20 kwenye simu. Ikiwa unahitaji washiriki zaidi, unahitaji kujiandikisha kwa programu ya kulipiwa. Ili kujifunza zaidi juu ya usajili wa Skype, bonyeza hapa.

Mahitaji ya mfumo:

Windows 10 toleo 1809 au kubwa zaidi
Mac OS X ikiwa na Mac OS 10.10 au kubwa zaidi
iOS 10 au kubwa zaidi
Android OS 4.0.4 au kubwa zaidi
Skype ya Wavuti kwenye Microsoft Edge au Google Chrome. Kumbuka: Skype ya Wavuti haitumiki kwenye simu za mkononi au tablet.

Kwa maelezo zaidi kuhusu mahitaji ya mfumo wa Skype, bonyeza hapa.

Vifaa ambavyo programu hii inaweza kufanya kazi:

 • Simu za Android na tablet
 • Chromebook
 • iPad, iPhone, iPod Touch
 • Mac
 • Windows

Kwa maelezo zaidi juu ya mifumo ya uendeshaji ambayo inaambatana na Skype, bonyeza hapa.

4. Mawasiliano kwa njia ya Google (Google Chat) na mikutano kwa njia ya Google (Google Meet) – (zamani zikijulikana kama Hangouts)

Vipengele vya msingi

Mawasiliano kwa njia ya Google na mikutano kwa njia ya Google (Google Chat na Google Meet) ndizo programu mbili ambazo zilibadilisha Hangouts za Google. Mawasiliano kwa njia ya Google inaweza kutumiwa kwa ujumbe wa moja kwa moja na mazungumzo ya kikundi, wakati Mkutano kwa njia ya Google inaweza kutumika kuitisha na kurekodi mikutano ya video.

Programu hizi ni sehemu ya Google Suite (G suite) ya huduma ambazo zinajumuisha Drive, Gmail, Docs, Sheets, slaidi, Fomu, Kalenda, Google+, Tovuti, Hangouts, na Keep. Zana hizi zinaweza kutumiwa kupitia Mawasiliano au Mikutano katika Google Chrome. Kumbuka kuwa wewe na / au kituo chako cha redio au shirika lazima muwe na akaunti ya G Suite ili utumie huduma hizi.

Mawasiliano kwa njia ya Google (Google Chat) zinaweza kutumika kwa:

 • Ujumbe wa papo hapo
 • Kushirikishana mafaili, ikiwa ni pamoja na picha, video, ujumbe wa sauti, PDF, majedwali, na faili zingine

Mikutano ya Google (Google Meet) zinaweza kutimika kwa:

 • Kuitisha na kurekodi mikutano ya video (angalia sehemu ya Zoom hapo juu)
 • Kushiriki skrini (angalia sehemu ya Zoom hapo juu)
 • Kushirikishana mafaili, ikiwa ni pamoja na picha, video, ujumbe wa sauti, PDF, majedwali, na faili zingine

Ninawezaje kutumia Mawasiliano kwa njia ya Google (Google Chat) na mikutano kwa njia ya Google (Google Meet) kama mtangazaji wa redio?

Kama ilivyo Zoom na Skype, unaweza kurekodi mkutano wa video katika programu ya Mikutano kwa njia ya Google (Google Meet) na kuhariri rekodi hiyo ili kuicheza mubashara kwenye programu ya redio moja kwa moja. Au, unaweza kuendesha mawasiliano wakati kipindi kikiwa mubashara -hakikisha tu wewe na wageni wako wote mna muunganisho thabiti wa mtandao.

Unaweza pia kushirikisha ujumbe au mafaili katika sehemu ya mawasiliano kwenye programu zote mbili, pamoja na maandishi, ripoti, maswali ya mahojiano, picha, video, na zaidi. Watangazaji wanaweza kuhifadhi mafaili moja kwa moja kwenye kifaa chao.

Programu hizi pia ni muhimu kwa kuitisha mikutano na timu yako ya uzalishaji vipindi vya kituo cha redio, pamoja na mikutano ya kupanga simulizi, mikutano ya utawala, na mikutano mingine ya kibiashara. Hakikisha kwamba washiriki wote wana akaunti ya Google ya kutumia huduma hii.

Kumbuka kuwa Mawasiliano kwa njia ya Google (Google Chat) na mikutano kwa njia ya Google (Google Meet) ni bure kutumia na hakuna kikomo cha wakati wa kupiga simu.

Mapungufu yakutumia Mawasiliano na Mikutano kwa njia ya Google (Google Chat and Meet)

Kuanzisha Mawasiliano au mkutano kwa njia ya Google, unahitaji akaunti ya Google, lakini mtu yeyote anaweza kujiunga na simu bila kuwa na akaunti. Inaruhusu hadi watu 150 kuwa kwenye mawasiliano lakini hupunguza simu za video hadi watu 25 kwa kila simu. Ikiwa unataka kuhifadhi rekodi za simu na mazungumzo ya video, unahitaji kununua hifadhi zaidi kupitia Google Drive yako au akaunti ya Google One.

Mahitaji ya mfumo:

Programu hizi zinaambatana na toleo la sasa na matoleo mawili ya awali ya mifumo ifuatayo ya uendeshaji:

 • Mac OS X
 • Windows
 • Chrome

Google Chat na Google Meet pia zinatangamana na vivinjari vifuatavyo vya wavuti:

 • Google Chrome
 • Microsoft Edge
 • Firefox
 • Safari 13 au toleo la baadae
 • Microsoft Internet Explorer 11

Vifaa ambavyo programu hizi zinaweza kufanya kazi:

 • iPhone au iPad
 • Simu za Android phone au tablet

Kwa habari zaidi kuhusu mahitaji ya mfumo wa Google Hangouts na vifaa ambavyo mfumo huu unaweza kufanya kazi, bonyeza hapa.

5. WhatsApp (inamilikiwa na Facebook)

Vipengele vya Muhimu:

 • Maongezi kwa njia ya WhatsApp: Njia rahisi zaidi ya kutumia WhatsApp ni kama jukwaa la kutuma na kupokea ujumbe wa papo hapo. Unaweza kutuma ujumbe wa maandishi kwa watu binafsi au kwa kikundi, ikiwa ni pamoja na maandishi, picha, video, faili za PDF, ujumbe wa sauti, na mafaili mengine na viunganisho.
 • WhatsApp kwa njia ya wavuti: Kutumia WhatsApp kwenye kompyuta yako, pakua na ufungue programu kwenye simu yako, bonyeza Menyu au Mipangilio, na uchague wavuti ya WhatsApp. Kisha, changanua nambari ya QR inayopatikana hapa.
 • Ujumbe wa sauti: Wakati wa maongezi kwa njia ya WhatsApp, unaweza kutuma ujumbe wa sauti kwa kubonyeza na kushikilia ikoni ya maikrofoni iliyoko kulia kwa mwambaa wa maandishi. Hii ni njia nzuri ya kuwasiliana na wasikilizaji bila kuandika ujumbe kwa lugha za hapa. Unaweza kusambaza sauti hizo kwa watu wengine — kwa mfano, ikiwa unashirikisha kidokezo kinachohusu kilimo.
 • Orodha za Matangazo: Kipengele hiki hukuruhusu kuunda na kuhifadhi orodha za anwani na kutuma ujumbe kwa washiriki wote mara moja. Kwa habari zaidi juu ya kutumia orodha za matangazo, bonyeza hapa.

Ninawezaje kutumia WhatsApp kama mtangazaji wa redio?

 • Kufanya mahojiano kwa kutumia ujumbe wa sauti. Hii inaruhusu wanaohojiwa kutoa majibu ya kina zaidi na ya halisi kuliko kwa kuandika ujumbe. Unaweza kuhamisha faili za sauti kutoka kwenye simu kwenda kwenye kompyuta, kubadilisha faili kuwa MP3, na kisha kuhariri rekodi hizo ili kuzicheza kwenye programu mubashara ya redio moja kwa moja.
 • Kuunda vikundi vya wasikilizaji na wataalam wa mada kujadili mada fulani. Kwa mfano, unaweza kuunda kikundi cha WhatsApp na maafisa wa afya, wataalam wa eneo hilo, na watu wengine wa muhimu. Ili kuepuka mafuriko ya ujumbe, jaribu kuunda vikundi viwili tofauti: moja kwa ajili ya wasikilizaji na moja kwa ajili ya wataalamu, na kisha ushirikishe habari muhimu zaidi kutoka kwa wataalamu kwenda kwa wasikilizaji, na habari muhimu zaidi kutoka kwa wasikilizaji kwenda kwa wataalamu.
 • Kutoa ripoti za soko na hali ya hewa moja kwa moja kwa wasikilizaji. Unaweza kutuma habari kama ujumbe wa sauti au ujumbe ulioandikwa. Wahimize wasikilizaji kuisambaza habari hii watu wengine kwenye jamii.
 • Makundi ya FRI ya WhatsApp katika kila nchi ni mahali pazuri pa kuwasiliana na watangazaji wengine wa redio nchini mwako na kubadilishana maoni, vidokezo, na habari zingine muhimu. Kujiunga na ukurasa wa FRI katika nchi, tuma barua pepe na jina lako, jina la kituo chako cha redio / shirika, na nambari yako ya simu kwa radio@farmradio.org.
 • Laini za WhatsApp kwa ajili ya wanawake tu ni njia nzuri ya kuhamasisha wanawake zaidi kushiriki na kushirikisha maoni yao hewani bila kutishwa au kukatishwa tamaa na idadi kubwa ya wapigaji wa simu ambao ni wanaume.
 • Orodha za matangazo ni njia nzuri ya kushirikisha video ndogo ndogo na habari zingine muhimu kutoka kwenye programu ya redio kwa watu wengi wakati huo huo.

Yapi ni mapungufu ya WhatsApp?

WhatsApp inaweza kuamilishwa na nambari moja tu ya simu kwenye kifaa kimoja kwa wakati mmoja. Hakuna chaguo la kuhamisha historia yako ya mazungumzo kati ya majukwaa, lakini unaweza kusafirisha historia yako ya mazungumzo kama kiambatanisho cha barua pepe. Hii ni muhimu ikiwa unataka kuhifadhi ujumbe wa WhatsApp lakini unahitaji kusafisha nafasi ya kumbukumbu kwenye simu yako au kompyuta. Pia, kiwango cha juu cha ukubwa wa faili kwa media zote (picha, video, ujumbe wa sauti) iliyotumwa kupitia WhatsApp ni 16 MB kwa kila faili.

Kwa sasa hakuna njia ya kurekodi simu za sauti au video ndani ya programu. Walakini, unaweza kurekodi mahojiano ya simu kwenye WhatsApp kwa kuweka simu kwenye spika na kuirekodi na kinasa sauti tofauti.

Mahitaji ya mfumo:

 • Android OS 4.0.3 au kubwa zaidi
 • iOS 9 au kubwa zaidi
  KaiOS 2.5.1 au kubwa zaidi

Vifaa ambavyo progarmu hii inaweza kufanya kazi:

 • Vifaa vya Android
 • Vifaa vya iOS
 • JioPhone au JioPhone 2

6. Telegram

Vipengele vya msingi:

Telegram ni huduma nyingine ya mawasiliano ya bure ambayo ni maarufu katika nchi nyingi. Inaruhusu simu kwa njia ya sauti na video na huduma za mazungumzo kwa kuzingatia usalama na kasi. Ujumbe uliotumwa kupitia Telegram umesimbwa sana na pia ni salama sana, ambayo hufanya huduma hii ya mawasiliano iwe salama na ya kuaminika zaidi kwa watumiaji wengine.

Vipengele vya msingi vyaTelegram ni pamoja na:

 • Maongezi, ikiwa ni pamoja na ujumbe wa maandishi au ujumbe wa sauti kwa mpokeaji binafsi au kikundi
 • Kupiga simu kwa njia ya video
 • Simu kwa njia ya sauti
 • Kushirikisha au kutuma mafaili bila kikomo: Telegram haina kikomo kuhusiana na ukubwa wa media na mazungumzo.
 • Uwezo wa simu isiyo na kikomo: Telegram inaweza kuunganisha watu hadi 200,000 kwenye simu ya kikundi.
 • Mazungumzo ya siri: Ujumbe wote katika mazungumzo ya siri hutumia usimbaji fiche kwa mtumaji na kwa mpokeaji, ikimaanisha kuwa wewe na mpokeaji tu ndio mnaweza kusoma ujumbe, na kwamba ujumbe hauwezi kupelekwa kwa mtu mwingine yeyote. Ukiwa na huduma hii, unaweza pia kuagiza ujumbe wako ujiharibu baada ya muda uliowekwa. Ili kujifunza zaidi juu ya mazungumzo ya siri, bonyeza hapa.
 • Isiyo na Usimbaji (Seamless sync) hukuruhusu kufikia ujumbe wako kutoka kwenye vifaa kadhaa mara moja na utume idadi isiyo na kikomo ya mafaili ambayo yanaweza kufikia 2GB kila moja.

Kwa habari zaidi za msingi kuhusu Telegram, bonyeza hapa.

Ninawezaje kutumia Telegram kama mtangazaji wa redio?

Telegram ni programu muhimu kwa watangazaji wa redio ambao wanaweza kuhitaji huduma salama za mawasiliano ikiwa wanashughulikia mada nyeti au wanafanya kazi katika nchi au mkoa wenye uhuru mdogo wa mawasiliano. Walakini, katika nchi zingine, sio programu ambayo watu wengi hutumia kuwasiliana.

Vinginevyo, Telegram ni jukwaa la mawasiliano la kuaminika na salama ambalo linaweza kutumiwa kwa njia sawa na Skype, Zoom, Google Meet, na WhatsApp kufanya mahojiano na watu ambao ni vigumu kuwafikia, na kutuma mafaili na kuyahifadhi na kuhariri rekodi za matangazo ya redio. Kwa kuzingatia huduma zake za ziada za usalama na uwezo wa kutuma mafaili usio na kikomo na uwezo wa kupiga simu, inaweza kuwa chaguo bora kuliko WhatsApp kwa wakati mwingine.

Mahitaji ya mfumo:

 • Android OS 4.0.3 au kubwa zaidi
 • iOS 9 au kubwa zaidi
 • KaiOS 2.5.1 au kubwa zaidi

Vifaa ambavyo programu hii inaweza kufanya kazi:

 • Vifaa vya Android
 • Vifaa vya iOS

Ni wapi kwingine ninaweza kujifunza juu ya kutumia majukwaa ya kwenye mtandao kwa utangazaji wa redio?

Farm Radio International, 2019. Connecting with farmers, journalists and communicators on social media. Barza Wire. https://wire.farmradio.fm/resources/connecting-with-farmers-journalists-and-communicators-on-social-media

Haburchak, Alan. 2020. Remote video interviews: All you need to know. International Journalists Network. https://ijnet.org/en/story/remote-video-interviews-all-you-need-know

Soon, Alan. 2020. Tips for running an online event in the time of COVID-19. Global Investigative Journalists Network. https://gijn.org/2020/05/05/tips-for-running-an-online-event-in-the-time-of-covid-19/

Tellier, Hannah. 2020. How Ouaga FM creates quality content despite the restrictions of COVID-19, Barza Wire. https://wire.farmradio.fm/spotlights/how-ouaga-fm-creates-quality-content-despite-the-restrictions-of-covid-19/

Acknowledgements

Shukrani

Imechangiwa na: Maxine Betteridge-Moes, mwandishi wa habari wa kujitegemea na Mshauri wa zamani wa Rasilimali za Utangazaji wa FRI Ghana.

Rasilimali hii imeandaliwa kwa msaada wa kifedha wa Serikali ya Canada iliyotolewa kupitia Global Affairs Canada.