Wakulima nchini Kenya wahamia kilimo cha Maharage kutoka kilimo cha Ngano: Aina Mpya ya maharage inamavuno mazuri

Uzalishaji wa mazao

Ujumbe kwa mtangazaji

Nukuu kwa Waandishi

Maharage (Phaseolus vulgaris L.) ni zao muhimu la jamii ya mikunde duniani. Mbegu hii ilikuja Afrika ya mashariki kutoka nchi za kati na kusini mwa bara la Amerika miaka 300 iliyopita. Sehemu kubwa barani Afrika ya mashariki, maharage yanalimwa kama zao la biashara pamoja na zao la chakula. Africa mashariki inazalisha Zaidi ya asilimia hamsini ya maharage barani Afrika. Watu wote wa mjini na wakazi wa vijijini wanakula maharage kama chakula chao cha kila siku.

Maharage ni chakula kikuu nchini Kenya, na sasa kimekuwa chakula kikuu kwa wakulima vijijini pia. Kutokana na mabadiliko ya hali ya hewa, Wakulima wa Kenya wanabadilisha mazao na kuanza kulima mazao yenye ustahimili wa ukame kama maharage. Mbegu mpya sokoni inawateja wengi hivyo wakulima wananufaika kwa kupata faida kidogo kulinganisha na mbegu za zamani.

Kupanda na kula maharage kuna manufaa mengi ikiwemo:

Lishe na Usalama wa chakula: Maharage yana vyanzo vikubwa vya protini, na zina vitamini. Majani machanga na mbegu za maharage yote yanaliwa.

Mifugo: Mabaki ya mazao ni vyanzo vikuu vya malisho ya mifugo.

Maisha: Tayari kuna masoko ya zao la maharage nchini Kenya na nchi za jirani.

Faida za Udongo: Maharage ni zao zuri kwani linatunza pia udongo kwa uwezo wake wa kubadilisha hewa ya Naitrojeni na kuwa mbolea za naitreti. Ukiacha mizizi ya maharage baada ya kuvuna inachangia kilo 20-60 za ziada za naitrojeni katika udongo, ambayo itatumika kurutubisha mpando ujao. Hii ni sawa na ¾-2 mfuko wa mbolea ya Urea. Kama zao funika, maharage yanasaidia kuzuia mmomonyoko wa udongo.

Mavuno: Kwa mbinu sahihi za kilimo—ikiwemo maandalizi bora ya udongo, mbolea inapohitajika, na kupanda mbegu bora kilo 30-40—maharage yanaweza kutoa kilo 800 kg/ekari.

Mwongozo huu umeandaliwa kutokana na mahojiano halisi. Unaweza kutumia mwongozo huu kama chanzo cha habari na kufanya utafiti wako na kuandaa mwongozo kama huu. Au unaweza kutumia mwongozo huu katika kituo chako cha habari, kwa kutumia waigizaji wakisoma mwongozo. Kama hivyo, kumbuka kuwataarifu wasikilizaji wako wa kipindi kwanzia mwanzo wa kipindi kuwa sauti watakazozisikia sio sauti za watu halisi bali ni sauti za waigizaji.

Unaweza ukarusha kipindi hiki kama kilivyo na kukawa na kipengele cha majadiliano (kwa kupokea simu-na kutuma SMS) juu ya uzalishaji wa zao la maharage katika maeneo yao.

Je wakulima wanalima mbegu za kisasa au mbegu za kienyeji za maharage?

Wanaona utofauti gani?

Wanakumbana na changamoto zozote katika kulima maharage?

Wakulima wanaweza kupata wapi msaada ili kuweza ili kuweza kupata mavuno bora ya maharage?

Mwongozo huu unakadidiriwa kuruka kwa muda wa dakika 20

 

 

Script

 

SAUTI KIASHIRIA IKIPIGWA KWA SUTI YA CHINI

MTANGAZAJI:
Habari Karibu katika Kipindi cha kutoka kwa mkulima kwa mkulima. Katika kipindi chetu leo, tunaongelea juu ya zao kuu barani Afrika—maharage. Tunakuwa tukisikia sauti ya Dkt. Davis Karanja, mratibu wa mradi wa mazo ya jamii ya mikunde kutoka serikali ya Kenya kitengo cha Kilimo na Mifugo. Baadaye pia tutamsikia mkulima kutoka Kenya maeneo ya Bonde la Ufa, mkulima huyu alikuwa akilima ngano na sasa amehamia kilimo cha maharage.

SAUTI KIASHIRIA KWA SAUTI YA JUU

MTANGAZAJI:
Dkt. Karanja, zao la maharage lina umaarufu gani nchini Kenya kwa sasa ukilinganisha na hapo awali?

DAVIS KARANJA:
Zao la maharage limekuwa zao lenye virutubisho la lenye kusaidia ulinzi wa chakula, na zao lenye kuwapatia wakulima kipato. Bei ya zao la Maharage limekuwa zuri, dola 50 kwa kilo 90. Hii imefanya wakulima kuvutiwa na zao hili. Wakati huo huo, kutokana na mabadiliko ya tabia ya nchi wakulima wameripotiwa kupunguza uzalishaji wa mazao kwa Ekari.

MTANGAZAJI:
Kuna faida gani za kupanda maharage badala ya kupanda mazao mengine kwa wakulima nchini Kenya?

DAVIS KARANJA:
Maharage yanaliwa na yanapendwa na wakulima. Bei nzuri masokoni inafanya zao hili kuwa kipenzi cha wakulima. Kwa baathii ya maeneo ambayo magonjwa yanashambulia mazao kama mahindi wakulima wanashauriwa kulima mazao kama maharage. Maharage yanasoko zuri, soko la ndani na soko la nje. Kenya ina agiza kama asilimia 60 ya maharage.

MTANGAZAJI:
Kwa uzoefu wako na wakulima, nani anaye lima maharage mengi kuliko mwenzie, ni mwanamke au mwanaume?

DAVIS KARANJA:
Kwa utamaduni zao la maharage linachukuliwa kama zao la wanawake na tunakitahidi tuwezavyo kuhakikisha wanawake wananufaika na mazao haya kwa kupata mavuno mazuri na masiko mazuri ya mazao yao. Changamoto tulio nayo sasa ni kuwa maharage yanalimwa kama zao la biashara. Aina nyingi za mbegu za maharage zinazalishawa kwaajili ya kusafirishwa, na pesa zinapopatikana wanaume wanataka kuwa watawala na kufanya maamuzi ya kifedha. Hivyo changamoto ya kuifanya familia kuchukulia uzalishaji wa zao hili kuwa ni kazi ya familia na hivyo pia mwanamke anasauti.

MTANGAZAJI:
Kama mtafiti, umewasidia vipi wakulima kukabiliana na changamoto hizi?

DAVIS KARANJA:
Tumekuwa tukishirikiana na taasisi za kiserikali kufanya mafunzo ambaoyo yana himiza umoja katika familia, tunawahimiza wanaume kuona uzalishaji wa zao la maharage kuwa ni zao la kibiashara na wote mama na baba wanaweza kuwa na maamuzi.

MTANGAZAJI:
Wakulima wanakumbana na changamoto zipi katika kuzalisha maharage?

DAVIS KARANJA:
Changamoto kubwa imekuwa katika mabadiliko ya hali ya nchi na upungufu wa kiwango cha mvua. Maharage pia yanahitaji palizi la mapema ukosefu wa vibaru ni tatizo pia, hasahasa kwa wakulima wadogowadogo. Kubangua pia ni tatizo kwani mara nyingi hufanyika kwa njia ya mikono, ambapo ni changamoto kwa wakulima wanao taka kupanda maeneo makubwa. Baathi ya aina za maharage zenye uhitaji mkubwa sokoni zinashambuliwa sana na wadudu wakati ikiwa shambani na ikiwa imehifadhiwa ghalani hivyo shughuliza ungalizi na kutunza ni muhimu.

MTANGAZAJI:
Mkulima anaweza kukabiliana vipi na changamoto hizi?

DAVIS KARANJA:
Kuna aina nyingi mpya za maharage sokoni kuliko mbegu za asili, mbegu hizi mpya zina mazao mengi na zina vumilia ukame. Zinaweza kusindikwa mfano kuuzwa kwenye makopo na pia zinakomaa mapema. Pia tunawahimiza wakulima kupanda maharage kwa njia ya kisasa.

MTANGAZAJI:
Mbinu hizi mpya ni zipi?

DAVIS KARANJA:
Njia moja wapo ni kuboresha udongo kwa kutumia mbolea katika kipindi cha kuota na kutoa maua. Kwa baathi ya mbegu wakulima wanaweza kutumia mbolea baada tu ya maharage kuota. Hii inasaidia kuongeza mavuno. Wakulima pia wanaweza kushirikiana kuchagua mbegu.

MTANGAZAJI:
Kushirikiana kuchagua mbegu kunafanyikaje?

DAVIS KARANJA:
Inahussha kuwashirikisha wakulima kuchagua mbegu. Njia inayotumika Zaidi ni njia ya Ribon ambapo wakulima wanachagua mbegu zao bora kuliko zote na zile ambazo wanafikiria ni mbaya kuliko zote na kufanya majaribio kwa kuzizalisha. Kila mkulima anatumia ribbon kupiga kura na kuchagua mbegu, yunatumia rangi tofauti kwa wanawake na wanaume ili kujua machaguo ya wanawake na wanaumme.

MTANGAZAJI:
Unaweza ukaniambia simulizi lolote la mafanikio la kuzalisha maharage?

DAVIS KARANJA:
Mbegu aina ya KAT B1 ni maharage ya njano ambayo yanapata umaarufu sana na inakubalika na wakulima wengi na walaji nchini Kenya na nchi za Afrika Mashariki. Maharage yana komaa mapema hivyo huepuka ukame. Inapopikwa ni tamu na inaogezeka ukubwa mara tatu, haisababishi gesi na inatengeneza supu nzuri. Bei yake siku zote iko juu kulinganisha na maharage mengine Inatumika kutengeneza bithaa ambazo hauhitaji friji kuzitunza na kusafirisha. Wafanyabiashara wanasafirisha takribani kilo milioni 20.

SAUTI KIASHIRIA IKIPINGWA KWA SAUTI YA CHINI

MTANGAZAJI:
Unasikiliza kipindi cha kutoka kwa mkulima kwa mkulima na tunajifunza kuhusu kilimo cha maharage nchini Kenya. Tumemsikia Dkt. Davis Karanja, mratibu wa mradi wa mazao kijani ya jamii ya mikunde katika taasisi ya utafiti ya kilimo na ufugaji, tunamsikia mkulima anayepanda maharage shambani kwake lakini kwa sasa tusikie muziki.

MUZIKI SAUTI YA JUU

MTANGAZAJI:
Loise Chelagat ni mkulima anayelima Bomet nchini Kenya katika bonde la ufa. Amekuwa akilima mahindi na ngani kwa kipindi kirefu sasa shambani kwake, lakini hivi karibuni amehamia kuzalisha zao la maharage. Nimeonana naye nilipo tembelea Nairobi, na nilimuuliza kwanini analima Maharage.

LOISE CHELAGAT:
Wakwe zangu wamekuwa wakizalisha ngano kwa miaka mingi sana, tumeamua sasa kujaribu kulima maharage kwasababu kwa nyakati hizi amabzo kuna mabadiliko ya tabia ya nchi mahindi na ngano hazifanyi vizuri.

MTANGAZAJI:
Umeona mabadiliko gani?

LOISE CHELAGAT:
Mvua hazinyeshi kama zinavyonyesha miaka ya nyuma, na ikinyesha hainyeshi kwa muda mrefu. Mazao yetu yamekuwa yakifanya vibaya, na hatupati masoko. Magonjwa ya mazao ya ngano yanaongezeka na madawa yanongezeka gharama. Nina watoto wanne wanaohitaji ada za shule na mahitaji mengine hivyo nilazima nitafute njia mbadala.

MTANGAZAJI:
Umeanzaje kupanda maharage?

LOISE CHELAGAT:
Shirika la umoja wa wakulima lilitupatia mafunzo, na lilitu himiza kujaribu kuzalisha maharage kipindi cha mvua. Mume wangu na mimi tulijaribu kupanda. Hii ilikuwa miaka 7 iloyopita na hatuku rudi nyuma tena. Tulipanda maharage na tulivuna baada ya wiki 6 hadi 7—na soko lilikuwa kubwaa! Maharage yanahitajika masoko ya ndani na kwa wale wanaotaka kusafirisha.

MTANGAZAJI:
Umekabiliana vipi na changamoto za kulima maharage mpaka kuvuna?

LOISE CHELAGAT:
Ninaandaa shamba langu kwa kupanda mapema ili mazao yangu yaepuke kukabiliwa na magugu. Kitu kizuri juu ya mbegu hii ya maharage ya KAT B1 ni kwamba haihitaji maji mengi—itaota hata kama kipindi cha mvua ni kifupi.

Nina chukua mbegu zilizo halalishwa nan a vituo vya kilimo. Baada ya kupanda ninatumia mbolea ya samadi na wakati wa mmea kutoa maua tena natumia mbolea. Hii inazuia magonjwa ya maharage na wadudu. Pia tumeshauriwa kutumia kichanjio chenye bakteria kijulikanacho kama rhizobial, ambayo tunakinunua kutoka kwa maafisa ugani.

MTANGAZAJI:
Chanjo ya rhizobial inasaidi vipi?

LOISE CHELAGAT:
Tulikuwa tunapata mavuno machache lakini tumegundua kuwa unaweza kupata mavuno mengi ukitumia chanjo hii ya rhizobial ambayo unachanganya na mbegu. Inaongeza kiasi cha Naitrojeni katika udongo, na naitrojeni ni muhimu maharage yanapoanza kuota. Palizi pia ni muhimu. Kulinganisha na mazao mengine tunayolima, Nimeona kuwa zao la maharage unapaswa kufanya palizi, hasa hasa muda kati ya kuota kwa mbegu na kutoa maua.

MTANGAZAJI:
Una hakikishaje kuwa palizi, uvunaji, na kubangua kunafanyika kwa muda muafaka hasa unapokuwa na shamba kubwa?

LOISE CHELAGAT:
Ni ngumu na nimeona kuwa siwezi kukamilisha hili mwenyewe. Katika maeneo mengi wanawake san asana ndio wanalima maharage, hivyo tunasaidiana. Katika kupanda, kupalilia, kuvuna, na kunagua, tuna saidiana kwa zamu leo shamba hili kesho shamba lile. Kama watoto wetu hawako likizo pia wanasaidia. Kwa utaratibu huu tunaweza kukodisha mashamba Zaidi kipindi cha shughuli nyingi. Kwasababu tuko wengi tunao kodisha mashamba katika eneo moja inasaidia katika ulinzi na kuweka. Kazi hizi tunafanya kwa umoja, na nafikiri ni rahisi kwa wanawake kukubali kufanya kazi katika kikundi.

MTANGAZAJI:
Je vipi kuhusu uhifadhi na wadudu—unapambana nao vipi?

LOISE CHELAGAT:
Ninavuna maharage yangu vibebea vinapokuwa vya njao na vimekauka, na zinapasuka ukizitingisha. Ni vyema kuvuna wakati wa jua kali kabla mvua hazijaanza. Ghala langu lilikuwa limejengwa na mabati. Ghala lako likiwa limejengwa na nguzo za mbao na manyasi basi panya na dumuzi watakuwa wakishambulia sana.

Ghala limenyanyuliwa juu ya ardhi na linanafasi ya kuingiza hewa kutoa unyevu na kusaidi mazao kukauka. Nina osha ghala vyema kabla ya kuhifadhi kwasababu wadudu wanaweza kujificha ndani ya nyufa. Kwa namna hii ninaweza kuweka maharage yangu hata kwa mwaka mmoja bila kubunguliwa na wadudu.

Kuna maghala ya Silo yaliyoletwa hivi karibuni kijijni hapa yana saidia sana kupunguza vamizi la dumuzi na panya Dkt.

Msimu ujao nitajaribu.

MTANGAZAJI:
Na bado unalima ngano?

LOISE CHELAGAT:
Ndio, lakini sio kama ndio zao pekee, na sio katika eneo kubwa. Tuna ekari 12 za shamba. Ekari nne tumepanda ngano na Ekari nyingine 8 tumepanda maharage, mahindi, mbogamboga, na mtama. Tunapanda maharage eneo la ekari 3 inatuwezesha kulipa gharama za kila siku na kupata faida baadaye.

MTANGAZAJI:
Unapanda kiasi gani cha maharage kuhakikisha mavuno ya kutosha.

LOISE CHELAGAT:
Tukipanda kilo 1 ya mbegu za maharage tunavuna, tunavuna kama kilo 30 za maharage ndani ya wiki sita. Na kwakuwa tunalima mbegu bora wadudu na magonjwa hazishambulii, Maharage yanastawi vizuri sana kwangu. Watu wanakuja kununua kwangu na kusafirisha nje na pia ninauza maharage yangu soko la ndani.

MTANGAZAJI:
Hela unayopata unafanyia nini?

LOISE CHELAGAT:
Mume wangu anafanya kazi serikalini, lakini hela anayoipata haitoshi kutunza familia. Hivyo ninamsaidi kulipa bili za nyumbani. Ni maharage haya ndio ninauza na kulipa ada za watoto wa shule, kununua sare za shule na mahitaji yao mengine.

MTANGAZAJI:
Kwahiyo wewe na mume wako hamgombani mnapo uza mahaerage?

LOISE CHELAGAT:
(AKICHEKA) Hapana, ananiheshimu hivyo hela zitokanazo na mauzo ya maharage zinatumika kwa matumizi ya nyumbani. Bado tunalima ngano kwasababu tuna ardhi ya kutosha na familia yake bado inaamini kuwa lazima tuzalishe ngano, yeye ndiye anasimamia shamba la ngano.

MTANGAZAJI:
Unalima maharage ya zamani?

LOISE CHELAGAT:
Ndio, kwasababu nina wateja wanao penda maharage ya zamani, hasahsa watu wa rika la zamani. Mbegu mpya inachukua siku 30 kutoa maua, kasha siku zingine 35 kabla ya kuvuna. Mbegu ya zamani inachukua siku 90 kuweka maua na siku nyingine 30.

MTANGAZAJI:
Unapika maharage nyumbani kwako?

LOISE CHELAGAT:
Oh ndiyo! (AKICHEKA) Mwanangu wa mwisho wa kiume anapenda kula maharage katika kila milo yake yote. Nina pika maharage ya zamani na maharage mapya lakini wanangu wanapendelea maharage mapya kwasababau hayana gesi na pia yanaiva mapema nichemsha tu kwenye jiko la mkaa sina haja ya kutafuta kuni nyingi.

Acknowledgements

Imechangiwa na: Winnie Onyimbo, Trans World Radio Kenya
Imehaririwa na: Bw. Paul Aseete, Taasisi ya taifa ya utafiti wa mazao (NaCRRI), Shirika la Taifa la utafiti (NARO).

Kazi hii imefanyika na msaa wa kifedha kutoka kituo cha kimataifa cha urafiti, Ottawa, Canada, www.iDktc.ca, na serikali ya Canada, kupitia kitengo cha mahusiano ya kimataifa Canada, www.international.gc.ca

The translation of this script was made possible with the support of USAID’s New Alliance ICT Extension Challenge Fund, through the International Fund for Agricultural Development in Tanzania. For more information about the Fund, please see: https://www.ifad.org

Information sources

Mahojiano na:
Loise Chelagat, mkulima wa maharage Bomet Nchini, Kenya.
Dk. Davis Karanja, mratibu wa mradi wa mazao ya jamii ya mikunde Kenya Shirika la Kilimo na Ufugaji
Mahojiano yalifanyika Mwezi wa 721 na Mwezi wa Nane 26, 2016