Kufanya Utafiti katika kituo/stesheni ya redio jamii Nkhotakota

Ujumbe kwa mtangazaji

Pakua na hariri taarifa hii kwa matumizi yako.

Maelezo kwa Mtangazaji

Makala hii ya matangazo. Ni makala ya maojiano kati ya Philip Chhinkhokwe, mtayarishaji wa matangazo ya redio katika Nkhotakota kituo cha redio nchini Malawi. Katika mahojiano Philip anaelezea jinsi kituo chake kinafanya utafiti wa wasikilizaji, na anatoa mfano wa utafiti uliofanywa katika programu za kilimo cha hifadhi. Sehemu ya pili ya makala hii ni hati kutoka programu ya redio juu ya kilimo cha hifadhi unaolenga utafiti wa wasikilizaji ulioelezwa katika mahojiano.

Soma kupitia kipande hiki na ona kama kuna kufanana kokote jinsi kituo chako kinafanya utafiti wa wasikilizaji na jinsi Nkhotakota inafanya utafiti wa wasikilizaji. Je, kuna mafunzo yeyote unayoweza kujifunza kutokana na utendaji wa Nkhotakota? Angalia jinsi sauti za wakulima zinavyoonekana katika vipengele kwenye programu ya Nkhotakota, na jinsi gani kituo kinatumia vema upatikanaji haba wa raslimali kwa kutegemea uwepo wa programu nyingine bajeti na programu za mashirika mengine.

Kama ilivyoelezwa katika kipengele namba moja, kwa kuunda programu za kilimo kwa ufanisi ambazo zinaendana na mahitaji ya wasikilizaji wako ni lazima ujue wasikilizaji wako ni wa aina gani, na ujue ni taarifa gani ya kilimo ni muhimu kwo. Baadhi ya shughuli za kilimo ambabazo Philipo anazielezea hapa chini ni njia nzuri za kujua wasikilizaji wako na kutafuta mahitaji yao

Script

Utangulizi.

Wakati vituo vya redio vinatangaazia wasikilizaji wake kuhusu nini wanataka kusikia redioni, kuandaa matangazo kwa njia ya stesheni kunaweza kutekeleza ………………….. Msikilizaji anaweza kujihusisha katika uandaaji kwa kukuambia nini wanachotaka kusikia na ni lini wanataka kukisikia na kufanya sauti zao zisikike hewani.

Maelezo ya Mtangazaji yafuatayo yamegawanywa katika sehemu mbili. Sehemu ya kwanza ni mahojiano kati ya Philipo Chinkhokwe, Mtagazji wa kituo cha redio jamii Nkhotakota ya Malawi. Katika mahojiano, Philip anaeleza jinsi kituo chake cha redio kinafanya utafiti kuunda programu za wakulima na wadau kama Wizara ya Kilimo na Mashirika yasiyo yasiyo ya kibiashara. Sehemu ya pili ni transcript ya sehemu ya programu ambayo Philip ameitengeneza ikihusisha utafiti yeye na wenzake walioufanya.

Sehemu ya kwanza: Mahojiano na mtegenezaji/mwandaa matangazo.

Msaili:
Je, Unaweza kutuambia wewe ni Nani na wajibu wako ni nini? Katika kituo cha redio cha jamii ya Nkhotakota?
Philip Chinkhokwe:
Jina langu ni Phillip Chinkhokwe na ni mwandaaji wa matangazo na Afisa wa kompyuta. Kazi zangu nyingi zinahusu Kukusanya taarifa za wasikilizaji, kuandika simulizi zao za mafanikio pamoja na kutafuta maoni kutoka kwa wasikilizaji.
Msaili:
Unafanyaje utafiti papa Nkhotakota katika kituo cha redio ya jamii?
Philip Chinkhokwe:
Nyingi ya Programu zetu kwa mfano programu za kilimo, afya au elimu zinafanywa kwenye wilaya yetu zikishirikiana na shirika letu, Idara ya Kilimo inafanya haja tathmini ya sekta Fulani ya kilimo halafu kubainisha njia bora ambazo wakulima wanapaswa kutumia. Halafu wanatupeleka katika maeneo ambayo wakulima wanalima mazao kwa bidii tutashughulikia katika programu yetu ya redio.

Zaidi ya kozi za programu, kwa mfano mahindi, tunatembelea wakulima mara kwa mara. Tunarekodi sauti zao na kuzitumia kama kumbukumbu katika programu zetu na tunaweka kumbukumbu ya hadithi za mafanikio. Wakulima pia hupata huduma ughani ya moja kwa moja. Wakulima hawa wanaitwa “Wakulima Hai.

Idara za Kilimo zinatuelekeza kwenye maeneo mengine ambapo pia wakulima wanalima mazao haya lakini hawajapata utendaji bora kwa mapana kama ‘Mkulma Hai.’ Wakulima hawa husikiliza kutoka katika programu na kutupa maoni. Mara nyingine tunawatembelea na kurekodi hadithi za mafanikio na kukadiria athari ya programu zetu kwa watu wanaosikiliza kwa muda huo. ‘hawa tunawaita wasikilizaji baridi/wasikilizaji wakimya kimya.

Msaili:
Unafanya nini unapowatembelea wakulima hawa kwa mara ya kwanza?
Philip Chinkhokwe:
Tunawauliza kuhusu uthabiti na udhaifu wao na nafasi na changamoto.
[Muhtasari wa mhariri: Kwa Mwongozo jinsi ya kupatataarifa, angalia kipengee cha kanza katika mfululizo huu]

Halafi tunaunda vikundi vya kusikiliza katika jamii ambazo zinataka Na mahali ambapo watu wanahisi programu inaweza kuwapatia. Mahitaji yao kwa njia ya taarifa.

Tunaanzisha vikundi kwa kusaidiwa. Na wafanyakazi ughani na kiongozi wa kijiji. kiongozi wa kijijii wanaitisha mkutano kijijini na tunahudhuria mkutano tukiambatana na wafanyakazi ughani. vikundi kwa kawaida vina watu karibu.

Tunawaambia kwa muhtasari wasikilizaji kuhusu programu zijazo.

Msaili:
Baada ya kusikiliza vikundi vilivyoanzishwa, nini kinafuata?
Philip Chinkhokwe:
Halafu tunatoa watangazaji wa progrmu kujua utambuzi kuhusu programu zinazofuata.

Licha ya maeneo hai na yasiyo hai kuna wasikilizaji wengine ambao husikia kuhusu programu zetu kwa njia ya promosheni na kupigia stesheni kuelezea nia zao za kujiunga. Wasikilizaji hawa huunda vikundi na kama wasikilizaji hai na wasio hai tunazichukua shughuli zao na maboresho ya kozi ya programu na baada ya mradi kumalizika. Tunataka kujua ni jinsi gani shughuli za kilimo zinaendelea baada ya programu kufikia mwisho wake. Watangazaji wanatoa namba za simu ambazo wasikilizaji wanaweza kupiga kama wameshaunda vikundi na kusikiliza.

Msaili:
Ni nini lengo lako katika kutoa namba hizi za simu?
Philip Chinkhokwe:
Kila eneo la programu kuna namba mahususi ya simu ambayo watu wanaweza kutoa maoni, Kwa mfano tuna namba moja ya simu kwa ajili ya afya, moja kwa Elimu na moja kwa kilimo.
Baadhi ya wasikilizaji huandika barua pia. Tuna masanduku ya barua katikati ya kijiji. Mwanakijiji hukusanya barua mara moja au mbili kwa mwezi na mfanyakazi wetu wa idara ya masoko huzunguka kuzikusanya.
Msaili:
Unaweza kutushirikisha mfano wa programu ya utafiti wa wasikilizaji?
Philip Chinkhokwe:
Nina husika katika programu ya kilimo. Na kama mzalishaaji nina hakikisha kila taarifa ninayoitoa kwa wakulima ni sahihi, zina uwiano na za kuaminika. Moja kati mipango yangu inalenga mabadiliko ya tabia ya nchi ambayo yanawahitaji wakulima kubadilisha baadhi ya shughuli zao za kilimo.

Niliguundua kwamba wakulima hawapati habari thabiti kutoka mashirika mbalimbali ya kiserikali na yasiyo ya kiserikali.

Mara nyingine wakulima hupuuzia ujumbe ambao si thabiti na hawafanyi lolote kuhusu mambo ya kilimo yaliyosisitizwa. Wakati mwingine mkulima hatekelezi wajibu anapopata ujumbe wa kutatanisha. Mkulima hajui amwamini nani, kwa hiyo hawawajibiki kabisa.

Kwa hiyo nilifanya tafiti katika ujumbe hizi ambazo si thabiti, hasa katika kilimo cha hifadhi. Nilikwenda katika eneo ambapo NASFAM -National Smallholder Farmers’Association of Malawi – kinatoa huduma za ughani. Nilikwenda pia mahali ambapo Shirika lisilo la kiserikali – NGO Concern Worldwide linatoa huduma za ughani. Nilitembelea eneo la tatu ambapo ughani unatolewa na Total Land Care, na sehemu ya nne amabapo wafanyakazi ughani wa serikali hutoa huduma.

Katika maeneo yote manne, niliona ni jinsi gani wakulima wanatumia kilimo hifadhi. Nilijikita zaidi katika kilimo cha kutumia mashimo, ambacho ni kuotesha mmea katika shimo na kuweka mabua juu ya udongo kuhifadhi unyevu. Nilitaka kuona kama kuna tofauti jinsi wakulima walikuwa wakilima kilimo cha hifadhi.

Nilitaka pia kujua ni watoaji huduma ughani wapi ambao wanaweza kunipa taarifa ambayo ni za hali ya juu na za kuaminika juu ya kilimo cha hifadhi iliniweze kutoa habari katika redio. Nilimwuliza mkulima mmoja kutoka kila eneo moja kati ya maeneo manne na kuwauliza kuhusu taarifa walizopata kutoka kwa wafanyakazi ughani.

Msaili:
Ulipata nini? Ulijua nini?
Philip Chinkhokwe:
Kwanza nilijua kwamba wakulima wanajua kuhusu uwezo wa kilimo cha kuhifadhi kupunguza madhara ya mabadiliko ya hali ya hewa. Pia nilijua kwamba asasi mbalimbali zinashauri utumiaji mbalimbali wa kuweka mabua na kutumia, Wakulima wanne niliowasaili na wakulima wengine walipendekeza kwamba taarifa za matendo haya zisanifiwe.
Msaili:
Je, kulikuwa na matokeo mengine ya utafiti kutokana na utafiti?
Philip Chinkhokwe:
Nilijua kwamba licha ya ujumbe wa kutatanisha wakulima bado wanafanya. Walitembelea kijiji na kujadiliana wenyewe ni njia gani waichukue kutoka kwenye jumbe wanazosikia kutoka kwa wafanyakazi ughani. Wakati mwingine wanaziunganisha jumbe na kujaribu njia mpya.

Katika matukio mengine, niligundua kwamba wakulima wamelima kwa mashimo lakini wametandaza mabua pia. Kwa sababu wakulima waliambiwa pia kupanda mimea ya vetiver na kuweka alama za matuta, pia waliichukua. Walizifanyia kazi kila ujumbe walizosikia. Hawakutaka kuziachilia mbali shughuli walizotiwa nazo moyo kujaribu kwa hivyo waliamua kuzijaribu zote katika shamba moja.

Msaili:
Je, kulikuwa na matokeo mengine ya utafiti huku ya tegemea?
Philip Chinkhokwe:
Ndiyo, nilikuta kwamba wakulima hufundishana kila kitu kipya wanachojifunza. Kwa upande mwingine ambao si mzuri nilikuta kwamba baada ya wakulima kujifunza njia mpya wanacha ya zamani wakifikiri kwamba mpya ni ya ufanisi zaidi. Kwa mfano, mwanammke alitumia njia ya kutandaza mabua alikuwa amepewa mafunzo haya kwa upeo na alikuwa mkulima aliyeongoza aliyefundisha wenzake jinsi ya kufanya hivyo.

Lakini shirika lingine lilipomfundisha kuhusu kupanda kwa mashimo aliachilia mbali kabisa utandazji wa mabua na kutizama kwenye upandaji wa mashimo.

Kuna wakulima wengine ambao wanapojifunza mazoea Fulani wanakwama kwa hayo kwamba hawataki kujifunza jambo jipya. Tabia yao ni hivi ndivyo nifanyavyo na hivi ndivyo nilivyofundishwa na ni njia bora. Wamekwisha mwamini mtu aliyewafundisha na hawawezi kumwamini mtu mwingine mbaye anakuja na taarifa nyingine kwa urahisi.

Msaili:
Ni jinsi gani matokeo haya ya utafiti yalijiingiza katika programu yako?
Philip Chinkhokwe:
Nia yangu kubwa ni kutoa taarifa iliyosanifiwa kuhusu kilimo cha hifadhi. Badaa ya kumsaili mkulima, nilimsaili mtaalamu nilitaka kuunda ujumbe thabiti ambao ulielezea kanuni za msingi za kilimo cha hifadhi kuhusu upandaji wa mashimo na upandaji wa utandazaji mabua. Kwa hiyo niliziweka pamoja taarifa kutoka kwa wataalamu na wakulima ili kutambua taarifa ambayo imesanifiwa.
Msaili:
Badaye ulifanya nini?
Philip Chinkhokwe:
Niliihariri programu na kuipeleka kwenye timu ya machapisho-ambayo ni pamoja na wafanyakazi ughani, kwa hiyo waliielewa kilichokuwa kinaendelea. Nili hariri tena kuwa tayari kusikilizwa na wasikilizaji.
Msaili:
Kwa kifupi ni programu gani ambayo ulianzisha ambayo inahusu matokeo ya utafiti wako?
Philip Chinkhokwe:
Nilitoa programu ya dakika 30 kuhusu kama kupanda kwa mashimo na kutandaza mabua kunaweza kusaidia kwa ukame na kunaweza kuongeza mavuno. Watu waliosailiwa kwa programu walielezea jinsi ya kuendesha zoezi. Walizungumza kuhusu faida zinazohusiana na kukabiliana na mabadiliko ya hali ya hewa na mahitaji ya mtu kufuata upandaji. Baada ya programu kutangazwa wakulima waliofanya hivyo waliitwakupewa hati. Nilihakiki hati kwa muda wa dakika tano kimatangazo ambapo ilitangazwa kwa wakulima wengine kusikiiza na kuutiwa moyo kutumia njia hii.
Msaili:
Je, kulikuwanna fedha yeyote iliyotolewa kwa ajili ya utafiti wa watazamaji?
Philip Chinkhokwe:
Kulikuwa hakuna hela kwa utafiti wa watazamaji. Tulitumi rasilimali za programu iliyopo katika mambo ya mazingira.
Msaili:
Nkhotakota anafanya nini kuendelea kutafuta maoni kutoka kwawasikilizaji?
Philip Chinkhokwe:
Tuliwauliza watu wanapenda nini na wanachukia nini katika programu zetu. Hii inafanyika katika meza ya utafiti ambapo mfumo wetu wote wa maoni unasimamiwa. Tuna ujumbe za mstari wa mbele na tuna mfumo wa simu za nje na simu za ndani ambao umejitenga na programu ya simu za ndani na simu za nje. Mara tu hizi zitakapofanya kazi itatusaidia kupata maoni kutoka kwa wasikilizaji kupitia ujumbe na sauti. Wakala wa jamii wa barua wamefundishwa jinsi ya kuwachunguza kwa makini wasikilizaji kuhusu upangaji wetu wa programu na wasikilizaji wanahitaji tufanye nini? Pia tuna wafanyakazi ughani, hasa katika sekta ya kilimo na afya ambao hutuletea maoni.

Kituo kina timu ya mpira ambayo imeundwa kwa ajili ya mahusiano ya kijamii. Tunapanga mechi na mechi za kijamii na zinatangazwa na wafanyabiashara wa kijamii wakiidhamini tukio. Hii insaidia wafanyakazi wa kituo kusafiri ndani ya wilaya na kukutana na wasikilizaji. Watu wanapopiga simu tunawauliza wanapiga simu kutoka wapi. Hii inatupa wazo ni umbali gani, kwa mapana gani mradi Tunaorekodi maoni kutoka katika programu ya kila shamba.

Tuna ujumbe wa simu za mbali za bure. Wakulima ambao ni wanachama wanaotumia mtandao wa airtel wanaweza kutuma ujumbe bure kwa mtandao huu. Wakulima ambao walikuwa wakifanya kwa njia hii iliyopendekezwa katika programu maalumu hueleza walichokifanya, walichojifunza na ni jinsi gani wamefaidika, vilevile matatizo ambayo wanayapata. Tunatumia maoni haya kujibu maswali ambayo watu huuliza wanapopiga simu au wanapotuma ujumbe. Kama maswali ni ya kiutaalamu zaidi, kama vile kuzuka kwa ugonjwa, tunamwona mtaalam wa kilimo. Mtaalamu pia ana imarisha baadhi ya jumbe tunazozipata kutoka kwa wakulima.

Shirika lisilo la kiserikali na idara ya kilimo wanapokuwa na shughuli vijijini, tunaalikwa kurekodi na kutoa tarifa juu ya shughuli. Hii pia ni fursa ya kusikia wakulima wanasema nini?

Licha ya hayo, Tunatembelea jamii kwa vikundi vinavyosikiliza redio karibu na Nkhotakota. Tunatumia safari hizi kusikia na kurekodi mawazo ya watu kuhusu programu yetu.

Tuna mahusiano mazuri na wafanyakazi ughani, ambao wako huru kutembelea kituo. Wakulima wanawambia pia wafanyakazi ughani kwamba wanataka mrusha matangazo kutembelea eneo lao, kurekodi uzoefu wao walioupata kwa njia hii. Idara ya kilimo inatoa pikipiki kutupeleka kwenye maeneo ambayo uhitajiwa huduma yetu.

Msaili:
Kama stesheni ya redio Jamii. Una nia ya tayari kuwekeza raslimali katika kufanya utafiti jamii?
Philip Chinkhokwe:
Kusema kweli ni vigumu kwa redio jamii kuwekeza katika raslimali. Zake katika utafiti. Nilifanya utafiti kwa ajili ya programu juu ya kilimo cha hifadhi kwa nia yangu mwenyewe. Nilitumia raslimali zangu mwenyewe wakati hela za kutoka kituoni hazikutosha. Lakini kituo kilinisaidia katika kukusanya maoni, hasa katika meza ya utafiti. Lakini yote kwa yote stesheni za redio jamii haziwekezi katika utafiti wa wasikilizaji kwa sababu hazina fedha.
Msaili:
Je, kama ungalipewa fedha, unafikiri stesheni ingewekeza katika utafitiwa wasikilizaji?
Philip Chinkhokwe:
Ndiyo, Kama stesheni ya redio ya jumuiya, tuna maoni mengi ambayo tunatakiwa kuyaangalia lakini sisi bado wachanga na tuna ukosefu wa raslimali fedha. Tunatangaza programu lakini usafirishaji ni changamoto, Kwa hiyo wasikilizaji walio karibu nasi tu hufaidika na ziara za uso kwa uso. Mashirika mengine yanapokuwa na miradi ambayo inalenga umbali mrefu tunachukua jukumu la kuwafikia jumuiya ya mbali.
Msaili:
Kama kituo cha redio, Je unatafuta taarifa za watu wa Nkhotakota kwa mfano umri na jinsia?
Philip Chinkhokwe:
Kwa ujumla sisi hushauriana na Halmashauri ya wilaya, Idara ya kilimo na ofisi ya afya ya wilaya kuhusu idadi ya watu. Hii taarifa ni muhimu kwa sababu unaweza kutengeneza programu lakini kundi rika ulilo kusudia lisiwepo katika eneo hilo.

Sehemuya pili Part II: Nakala ya maaendeleo ya programu kutoka katokana na utafiti

Kifuatacho ni dondoo za dakika nne kutokana na programu kuhusu kilimo cha kutumia mashimo kilichotangazwa kituo cha redio jamii cha Nkhotakota tarehe 1/8/2012 na kurudiwa tarehe 5/8/ 2012 Dondoo hizi zimetafsiriwa kutoka lugha ya Kichechewa Programu hii inahusu utafiti uliofanywa na Chinkhokwe, ambaye alimsaili mkulima kiongozi aliye jihusisha na upandaji kwa njia ya mashimo. Dondoo zilihusisha dhana ya mabadiliko ya hali ya hewana vilevile kuanzisha kilimo kwa njia ya mashimo kama njia ya kuyakinga mahindi wakati wa kiangazi. Wakulima wanaelezea jinsi ya kulima kilimo cha kutumia mashimona faida za kulima hivyo.

Mtangazaji akitangaza kwa sauti

Mwasilishaji:
Tukiwa kama wakulima siku hizi, tunatakiwa kutambua kwamba hali ya hewa inabadilikana hii inasababisha matatizo mengi kwenye kilimo. Kama hatutafanya lolote kuhusu swala hili kilimo chetu kitaathirika sana. Usisahau kwamba kilimo kinategemea mali asili, kama raslimali hizi zikitumiwa na kumalizwa kabisa, kilimo kitakuwa hatarini pia.

Wakulima wenzangu mnafanya nini kukabiliana na mabadiliko ya tabia ya nchi? hali ya hewa? Mnafanya mambo gani kufuata uifadhi wa mali asili?

Tatizo moja linaloibuka kwa sababu ya mabadiliko ya hali ya tabia ya nchi ni ukame. Si hali ngeni kusikia matukio ya mvua kabla ya mazao kukomaana kuvunwa. Matokeo ya haya ni kuharibu mazao kama mahindi kwa sababu ya uhaba wa maji.

Leo tutajifunza jinsi ya kuweza kukinga mahindi yetu wakati wa kiangazi kwa kulima kilimo cha kupunguza ukame kama cha kulima kwa mashimo. Katika programu tuna msaili na bi Agnes Macheso kutoka kikundi kikuu cha Kijiji cha Nkhongo katika wilaya ya Nkhotakota.

Agnes Macheso:
Kilimo cha mashimo ni aina ya kilimo ambacho tuachimba mashimo na kupanda mahindi humo. Tunapanda punje nne za mahindi ndani yake, moja katika kila kona. Shimo lina urefu wa kina cha sentimeta 25 na upana wa sentimeta 30. [Maelezo ya/Muhtasari wa mhariri. Kwa maelezo zaidi juu ya upandaji WA mahindi Kwa njia ya mashimo, angalia marejeo mwishoni mwa taaifa ya hati ya mtangazaji.]
Philip Chinkhokwe:
Ulijifunza wapi aina hii ya kilimo?
Agnes Macheso:
Aina hii ya kilimo tumejifunza tu mwaka huu. Kime kuwa kikilimwa Zambia kwa mwongozo wa wafanyakazi ughani. Tumeamua kujaribu aina hii ya kilimo Malawi. Kama matokeo ni mazuri, teknolojia itaendeshwa katika maeneo mengine nchini mwaka ujao.
Philip Chinkhokwe:
Nini kilivutia nia yenu kukubaliana aina hii ya kilimo kwa mara ya kwanza baada ya kukisikia kutoka kwa wakulima kutoka nchi kama Zambia?
Agnes Macheso:
Kilichowavutia wakulima wa Malawi, pamoja na mimi kama kiongozi wa kilimo ni kwamba wana sayansi wamesema kwamba aina hii ya kilimo ni yenye kuzalisha sana ikilinganishwa na utumiaji wa mbegu moja kwa kituo kimoja cha upandaji katika matuta. Mvua inaponyesha maji yanaenda moja kwa moja katika mashimo tofauti na matuta ambayo hayahifadhi maji na kusababisha mahindi kunyauka wakati wa kiangazi. Mahindi yaliyopandwa kwenye mashimo hayanyauki hata baada ya mvua kuacha kunyesha. Kwa sababu maji yaliyokusanywa kipindi cha mvua hubaki katika mashimo na kuimarisha mimea.
Philip Chinkhokwe:
Unafikiri hii itasaidiaje kilimo chako?

Aina hii ya kilimo inayojikita kwenye matokeo ya utafiti uliofanywa inaonekana itawanufaisha Wamalawi, na kwamba mwaka ujao wakulima wengi watafuata kilimo cha mashimo. Kulingana na waliofanya utafiti juu ya kilimo cha kuotesha kwa mashimo mahindi huota vizuri kwa sababu ya maji na mvua inaelekezwa kwenye mashimo.

Philip Chinkhokwe:
Baada ya kuchimba mashimo haya na mvua ikanyesha na ukaotesha mbegu za mahindi, unafanya nini tena kuhakikisha mashimo yanavuna mavuno mengi?
Agnes Macheso:
Baada ya masimo kuchimbwa, unaweka mbolea kwenye mashimo ya miche minne. Miezi miwili baada ya kuweka mbolea miche yote ya mahindi itaota katika kasi sawa. Wakati wa kuvuna utakuwa na mavuno mengi.

Acknowledgements

Imechangiwa na Vijay Cuddeford, Meneja Mhariri Redio ya wakulima ya kimatifa ikilenga kwenye mambo yaliyokusanywa na Tendai Banda na Philip Chinkhokwe.
Imepitiwa upya na: Doug Ward, Mwenyekiti na redio ya kimo ya kimataifa

Information sources

Msaili na Philip Chinkhokwe iliyofanywa na Tendai Banda, 17/9/2012.
Dondoo kutokana na programu zilizotangazwa katika Redio ya jamii ya Nkhotakota

Kwa maelezo zaidi juu ya kupanda mahindi katika mashimo: Soma Karen Sanje, 2011. Wakulima wa Malawi wachimba/walima ili kukabiliana na hali ya ukame. Alertnet, June 10, 2011. http://www.trust.org/alertnet/news/malawi-farmers-digging-in-to-combat-drier-conditions/

gac-logoMradi uliofanywa na kupewa msada wa kifedha na nchi ya Kanada uliotolwa kupitia wakala wa kimataifa wa mendeleo. (CIDA)