Mboga za majani za asili za kiafrika kutumiwa tena mezani.

Uzalishaji wa mazao

Ujumbe kwa mtangazaji

Pakua na hariri taarifa hii kwa matumizi yako

Muhtasari kwa mtangazaji

Kuna aina zaidi ya 300 za mboga za majani za asili za kiafrika ambazo zimekuwa zikilimwa Afrika mashariki kwa miaka mingi. Mboga hizi zinafahamika kwa virutubisho vyake pia kama dawa.

Mboga za majani za asili za kiafrika ilikuwa utamaduni na sehemu kubwa ya chakula cha watu hadi mboga za majani za kisasa kama kabeji na karoti zilipoingizwa. Miaka michache iliyopita, hata hivyo mboga za majani za asili zimeanza kurudia umaarufu wake taratibu. Kwa sasa mboga za majani zilizopuuziwa zinalimwa na wakulima wadogowadogo, na kuuzwa katika masoko madogo na masoko makubwa, huliwa na watu wa mijini na vijijini.

Mswada huu umegusia uzoefu wa watu ambao wamekuwa wakifanikiwa kuzalisha na kuuza mboga za majani za asili nchini Kenya. Inaonesha jinsi wakulima wanavyoweza kuzalisha mboga za majani za asili ili kujiongezea kipato na uhakika wa chakula.

Mswada huu unatokana na mahojianao halisi. Utautumia kama hamasa ya kufanya utafiti na kuandika mswada juu ya mada hiyohiyo katika eneo lako. Au unaweza kuandaa mswada huu katika kituo chako, kwa kutumi waigizaji kuwakilisha wahojiwa. Kama utafanya hivyo, hakikisha unawaambia wasikilizaji wako mwanzoni mwa kipindi, kwamba sauti sio za wahojiwa bali ni za waigizaji.

Script

SFX
Melodi inapanda kisha inashuka
MTANGAZAJI:
Jaribu kukisia. Zina virutubisho, Zinakua vizuri katika mazingira yenye ukame, zinaweza kuwa chanzo cha kipato, na zinatunza mazingira … kama ukisema mboga za majani za asili za kiafrika, uko sahihi na ndicho tunaenda kujifunza leo.
SFX
Sauti ya melodi inapanda na kushuka
MTANGAZAJI:
Habari na karibuni katika Farmer to Farmer. Jina langu ni Winnie Onyimbo. Katika eneo la Afrika Mashariki, mboga za majani za asili za kiafrika kama vile mchicha, mgagani, kale ya kiethiopia au ya kiafrika na zingine vimerudi kutumiwa mezani. Sio muda mrefu sana, mboga hizi zilikuwa zikidhaniwa kutokuwa na mvuto na zilizopitwa na wakati. Wakazi wengi wa mijini hawakujua namna ya kuzipika vizuri. Lakini yote hayo yameishabadilika.
Leo tutaendelea kufuatilia kwa mtiririko thamani ya mboga za majani za kiafrika. Katika safari yetu, tutajifunza umuhimu wake katika chakula na namna zinavyoweza kuimarisha suala zima la uhakika wa chakula barani Afika. Hatuta watembelea wazalishaji wa mboga hizo tu bali na wale wanaopenda kuzitumia. Kwanza kabisa tutawatembelea wauzaji wa mbegu halafu wakulima wanaolima mboga za majani za asili za kiafrika, Kisha wanasayansi mahususi wa mboga za majani za asili na mwisho tutawaona wawakilishi wa soko kuu. Lakini safari yetu itaanza na kuishia jikoni.
SFX
Sauti ya kupika. Inafifia na kuendelea na majadilino.
MTANGAZAJI:
Nimesimama jikoni mwa Anne. Anne hupika na kula mboga za majani za kiafrika. Ninamtazama akiandaa chakula cha mboga za majani za asili ambazo kwa sasa zinafahamika sana Afrika Mashariki. (Pumziko fupi) Kwa hiyo tunapika nini leo?
ANNE:
Leo tunapika mchicha na mgagani.
MTANGAZAJI:
Kwanini unapendelea mboga za majani za asili za kiafrika?
ANNE:
Ni tamu, zinajenga afya vizuri kuliko kale na kabeji. Na hutumia muda mfupi katika upikaji wake.
MTANGAZAJI:
Zinanukia vizuri. Zitachukua muda gani kuiva?
ANNE:
Si zaidi ya dakika 10.
MTANGAZAJI:
Sawa, Huo ni muda wa kukadiria nitakaohitaji kusimulia katika safari yangu ya utafiti kuhusu mboga za majani za asili za kiafrika huko Kenya. Kituo changu cha kwanza kilikuwa Wangige, mji mdogo uliopo pembeni ya jiji la Nairobi, mji mkuu wa Kenya, nilipoonana na Kangara, muuzaji wa mbegu.
SFX
Sauti ya kufifia ya kupika
SFX
Sauti ya gari likiwashwa, kisha inafifia
MTANGAZAJI:
Mbegu ndizo chanzo cha mlolongo wa ukuaji wa mboga za majani za asili za kiafrika. Kangara huuza mbegu zenye ubora za mboga za majani za asili za kiafrika tu.
KANGARA:
Huwa nachukua mbegu zangu kutoka Nakuru. Kwa sasa uhitaji wa mbegu hizi ni mkubwa sana. Watu wengi hupendelea hizi mboga za majani, hata katika majiji makubwa.
MTANGAZAJI:
Ingawa hapo awali waandaaji wa mbegu walishuku kujishughulisha na mboga za majani za asili za kiafrika, umaarufu wake katika Maduka makubwa na masoko madogo imepelekea kuwepo kwa soko kubwa la mbegu za mboga za majani za kiafrika.
KANGARA:
Huwa nawauzia wakulima na wauzaji wengine wa mbegu wanaohitaji mchicha, mgagani, kale za Kiafrika, mnavu, huwa nazisambaza mbegu hizo mijini na vijijini. Nimekuwa nikifanya hivi kwa muda wa miaka 30 na kutokana na shughuli hii nimewasomesha watoto wangu hadi ngazi ya chuo.
SFX
Sauti ya kufifia ya kupika inapanda kisha inashuka
MTANGAZAJI:
Huyo alikuwa Kangara, muuzaji wa mbegu za mboga za majani za asili. (Pumziko) Kutoka katikati mwa Kenya, safari yangu ya kutafiti mboga za majani za kiafrika ilinichukua mpaka Kiserian, eneo la makazi la Kenya katika mkoa wa Rift Valley, nilipoonana na Stephen Kimondo, mkulima anayelima mboga za majani za kiafrika pekee.
SFX
Sauti ya gari likiwashwa, kisha inafifia katika sauti za shamba. Inazidi kuishia na kuanza majadiliano.
MTANGAZAJI:
Kwa sababu mbegu za Stephen Kimondo zina ubora mzuri na hutumia mbolea ya samadi, mboga zake za majani hukua vizuri na huwa na soko kubwa (pumziko) kwanini watu wanapendelea mboga za majani za kiafrika ?
KIMONDO:
Watu wanaachana na vyakula vinavyosindikwa na kemikali na kurudia misingi yao ya awali, na kurudia misingi ya awali inamaanisha kutumia mboga za majani za asili. Hivyo ninawapatia watu kile wanachohitaji.
MTANGAZAJI:
Ulianza lini kilimo cha hizi mboga za majani?
KIMONDO:
Nimekuwa nikijishughulisha na hiki kilimo tangu mwaka 2000, na ninaipenda shughuli ninayoifanya.
MTANGAZAJI:
Huwa unawauzia akina nani?
KIMONDO:
Tulianza na Maduka makubwa. Kisha tuliona kuwa baadhi ya watu hawaendi kwenye Maduka makubwa. Hivyo tukajiuliza, kwanini tusiwauzie katika masoko madogo? Kwa hiyo asubuhi huwa tunazipakia kwenye pickups zetu na kuzipeleka kwenye soko la wazi.
MTANGAZAJI:
Umeona mabadiliko gani tangu umeanza kuwauzia watu wanaonunua mboga za majani kwenye masoko ya kawaida?
KIMONDO:
Ungeweza kushangaa; hatuwezi kukidhi hitaji la soko. Soko lake ni kubwa sana. Wamasai walio wengi walikuwa hawali mboga za majani, lakini kwa sasa wanakula!
MTANGAZAJI:
Unatumia mbolea ya aina gani?
KIMONDO:
Mbolea ya kawaida inayotakana na ng’ombe. Hapa tumezungukwa na wamasai pamoja na mifugo yao. Mbolea zetu ni za asili; huwa hatutumii mbolea za viwandani.
MTANGAZAJI:
Vipi kuhusu maji? Naona kuna mabomba yamepita katikati ya shamba lenu la mboga. Mnapata wapi maji?
KIMONDO:
Ni kweli – tunatumia njia ya umwagiliaji wa matone. Tunachimba kisima, na kuweka mashine ya kumwagilia kwenye chanzo cha maji cha kisima. Inahifadhi kiasi kikubwa cha maji. Ni vigumu kushughulika na sehemu ya juu ya kifaa cha kumwagilia.
MTANGAZAJI:
Huwa unamwagilia mara ngapi?
KIMONDO:
Huwa tunamwagilia wakati wa usiku kwa sababu wakati wa mchana huwa kuna jua kali.
MTANGAZAJI:
Ninaona una aina mbalimbali za mboga za majani. Zote hukua kipindi cha masika na kiangazi au huwa mnalima mboga hizo kufuatana na majira?
KIMONDO:
Huwa hatubadilishi mazao tunayolima kufuatana na majira. Huwa tunalima mboga za majani za asili tu, na aina nyingi ya mboga hizo hukua vizuri kadri utakavyokuwa ukilima shamaba lako na kumwagilia hizo mboga za majani.
MTANGAZAJI:
Ninajua unazilima, lakini wewe mwenyewe huwa unakula hizi mboga za majani?
KIMONDO:
Utaweza kushangaa. Huwa nakula kilo ya mboga mbichi kwa kipindi ninachokuwa nimetembelea shamba langu. Nionapo tu jani zuri, huwa naliweka kinywani mwangu. Hata familia yangu inazipenda. Wanaelewa kuwa mboga hizo zina virutubisho na ni dawa. Unajua inatakiwa sisi ndio tuwe mfano.
MTANGAZAJI:
Ulisema umekuwa ukilima mboga hizi za majani za asili tangu mwaka 2000. Kilimo hiki kimewezaje kubadilisha maisha yako?
KIMONDO:
Ninapenda kilimo. Kama ninapata shilingi moja au mbili, kwanini nisiendelee nacho? Jambo la muhimu ni kuwa huwezi kukidhi umati kwa mboga za majani za kiafrika. Kama ningekuwa na heka 100, bado ningeendelea kufanya shughuli hii na pengine kupata fedha nyingi. Lakini kwa kidogo nilichonacho, namshukuru Mungu.
MTANGAZAJI:
Ninaona kwamba kwako hii ni zaidi ya kulima. Unaona kulima hizi mboga za majani kama njia ya kuwasaidia watu.
KIMONDO:
Ni kweli, mara tu, duka kubwa la uchumi nchini Kenya lilipowakusanya pamoja wakulima 87 kutoka nchini kote, na siku hiyo nzima tulijifunza kuhusu kilimo cha mboga za majani za asili. Walio wengi miongoni mwao kwa sasa wanalima hizi mboga za majani za asili katika nchi nzima. Pia nilijaribu kushirikisha watu kanisani vile ninavyopenda mboga za asili, na watu waliposikia kuhusu mboga za majani walifurahia na kuagiza. Nimeona mabadiliko mengi.
MTANGAZAJI:
Kimondo hauzi mboga za majani za kawaida za Kiafrika tu, Pia alianzisha mboga ambazo baadhi yetu tungeziita magugu – na zinauzika!
KIMONDO:
Tuna mboga kama kishona nguo. Watu wengi hawajui kuwa kishona nguo ni mboga nzuri zaidi kuliko mboga za majani za asili za kawaida, ni vigumu kuwaelezea watu ni nini hasa kama usipowapikia na kuionja. Huwa wananiona nikizila na ninawaonesha jinsi ya kuzipika. Watu wengi wana mboga za majani za asili ikiwa ni pamoja na kishona nguo. Katika bustani ya mbogamboga huwa tunawaeleza watu namna ya kulima mboga za majani na jinsi ya kuzipika kwa sababu tunataka wanufaike na vile walivyonavyo katika bustani zao. Tunawahamasisha watu waende zaidi ya kile walichozoea. Ndio maana kwa sasa tunauza kishona nguo kwa wingi na majani.
MTANGAZAJI:
Huyo alikuwa Kimondo mwenye shauku kubwa, mkulima wa mboga za majani za kiafrika kutoka mkoa wa Rift Valley nchini Kenya. (Kicheko) Sina hakika kama ningekula kishona nguo, ingawa Mmmm …mboga za majani zinaanza kunukia vizuri sana (pumziko). Lakini nikirudi katika safari yangu. Kituo changu kilichofuatia kilikuwa Bioversity International katika jiji la Nairobi ili kuelewa zaidi juu ya kishona nguo na mboga zingine za majani za asili za kiafrika.
Nina dakika chache kabla chakula changu hakijawa tayari. Ninadhani ninaweza kuvifikia vituo viwili kabla sijafurahia mboga zangu za majani za asili.
SFX
Sauti ya gari likiwashwa, kisha inafifia
MTANGAZAJI:
Katika kituo cha Bioversity International, nilionana na Patrick Maundu, mwanasayansi mtafiti wa vyakula vya kiafrika. Kwa mujibu wa bwana Maundu, hizi mboga za majani zina protini, madini ya chuma, Vitamini A, madini ya joto, zinki na saliniamu kiasi cha mpaka mara saba ya kiasi kinachopatikana kwenye kabeji.
MTANGAZAJI:
Kwa hiyo ni nini kilichochochea kuwepo kwa faida kwenye hizi mboga za majani za kiafrika zilizotelekezwa?
MAUNDU:
Ni matokeo ya sababu fulani fulani, Mojawapo ni kwa sababu sasa hivi watu wengi wana uelewa juu ya afya zao na wanajitahidi kadri iwezekenavyo kula kiafya. Ukilinganisha na kabeji na kale, mboga za majani za asili zina virutubisho sana, sababu ya pili ni kuwa watu wanataka kubadilisha mwelekeo na kula vitu vingine. Uchumi wa Afrika unakua kila mwaka na watu wana fedha kidogo kwa ajili ya matumizi ya vitu vingine. Ndio maana hawatumii vyakula vya ladha nyingine. Sababu nyingine ni kwamba watu wamekuwa wakifahamu zaidi na zaidi juu ya utamaduni wao, watu wanataka kurudia misingi yao, na chakula ni sehemu kubwa ya desturi zetu. Ninafikiri sababu zote hizo ndio zimechangia kile tunachokiona sasa. Labda ningetaja kitu kingine ambacho tungekipuuzia, na hicho ni VVU na UKIMWI. Kwanini? Kwa sababui waathirika wa VVU wanahitaji kula kiafya. Madaktari wengi wamependekeza kuwa watu wengi wangebadilisha mwelekeo na kuanza kutumia mboga za majani. Mboga zetu za majani za asili zina virutubisho vingi, hivyo kwanini usizipatie nafasi kama unataka kuishi kwa afya nzuri?
MTANGAZAJI:
Unaweza kutaja mboga za majani chache na virutubisho zilizonavyo?
MAUNDU:
Mboga za majani tofauti tofauti zina virutubisho vya aina tofauti tofauti. Kuna aina nyingi za mchicha, lakini kwa ujumla mchicha una kiasi kikubwa cha vitamini A na madini ya chuma. Mnavu wa kiafrika una kiasi kikubwa cha madini ya kalisiamu. Mboga nyingine ya majani ambayo wasikilizaji wetu wanaweza kuifahamu ni mlonge. Aina inayofahamika zaidi inajulikana kama mlonge wa oleifera. Mara nyingi hukaushwa na kusagwa kuwa unga na hupatikana katika Maduka makubwa. Mlonge hujulikana kama mboga za majani za miujiza kwa sababu zina kiasi kikubwa cha kila virutubisho unavyoweza kuvifahamu, pamoja na madini adimu yanayohitajika mwilini. Kila aina ya mboga za majani zina faida zake na ndio maana ni wazo zuri kula aina tofauti tofauti ya mboga za majani kadri iwezekanavyo, hivyo tunaweza kunufaika kutokana na aina nyingi ya virutubisho vya mboga za majani.
MTANGAZAJI:
Licha ya virutubisho vya hizi mboga za majani, pia ni dawa. Labda unaweza kutaja aina chache ya mboga ambazo unadhani ni dawa.
MAUNDU:
Aina nyingi ya hizi mboga za majani hutibu tumbo. Mojawapo ni mlenda. Unapokuwa na anaemia, kuna mgagani unaotibu huo ugonjwa. Watu wanapougua ugonjwa wa kuvimba tezi, utawaona wakitumia mnavu wa kiafrika kwa sababu baadhi ya watu huamini kuwa ni nzuri katika kupambana dhidi ya bakteria. Pia ni nzuri kwa kutibu koo.
MTANGAZAJI:
Kuna umuhimu gani wa chakula cha mboga za majani za kiafrika katika suala zima la uhakika wa chakula Afrika.
MAUNDU:
Barani Afrika, watu wengi walikuwa hawali mboga za majani zilizolimwa kwenye vitalu. Badala yake walienda kwenye Maduka makubwa kununua mboga ambazo hawakuweza kulima. Walitumia fedha nyingi kununua vyakula vyenye virutubisho kiasi kidogo. Na kwa sababu vina virutubisho kidogo, hii ilihatarisha usalama wa chakula majumbani.
Faida moja kubwa ya mboga za majani za kiafrika ni kuwa, kwa sababu kila jamii ina orodha yake ya mboga za majani zinazolimwa na watu katika maeneo yao, mboga za majani hizo zilihimili hali ya hewa ya eneo hilo. Kwa hiyo kushindwa kunyesha kwa mvua mara kwa mara kuliathiri kwa kiasi kidogo mboga za majani. Na wenyeji wanaelewa namna ya kuzipika mboga hizo. Ni sehemu ya utamaduni wao. Katika suala la usalama wa chakula, kulima mboga za majani kunasaidia uhakika wa chakula kwa mwaka mzima, Pia mazao ya ziada ya kuuza kwenye soko la ndani.
MTANGAZAJI:
Hebu tuzungumzie mboga za majani ambazo huwa haziliwi na watu mara nyingi na kudhani kuwa ni magugu. Unaweza kutaja chache?
MAUNDU:
Ninaweza kutaja chache ambazo huwa hazilimwi lakini huchumwa porini: mifano miwili mizuri ni kishona nguo na gallant soldier, ambazo hupatikana sana mashambani mwetu.Wakati mwingine wakulima huzichuma mashambani mwao na kuzichanganya na mboga zingine kwa sababu mbalimbali, pengine kuleta ladha au kubadilisha mlo – na hiyo ni sehemu ya mapishi ya kiafrika.
MTANGAZAJI:
Sawa, hebu tuongelee juu ya kuzilima. Wakulima wengi nilioonana nao walikuwa wakizungumzia mbegu tu.
MAUNDU:
Utaratibu unaofahamika ni kuwa kama mboga za majani zikikuwa hadi kimo cha futi tano, hakuna haja ya kuiachia mimea nafasi ya karibu karibu. Lakini mboga zikikua mpaka kufikia urefu wa futi moja, unahitajika kuiwekea mimea nafasi ya kukaribiana. Kwa mfano, mnavu wa kiafrika hukua vizuri kama ikiachiana nafasi ya umbali wa futi moja na kupangwa katika mistari. Kwa upande wa crotalaria, ambao ni mmea unaopatikana sana magharibi mwa Kenya na kaskazini mwa Uganda, zinafaa kwa upandaji wa kutupia mbegu, kwa sababu hata kama zikikusanyika pamoja, haiathiri mavuno.
MTANGAZAJI:
Umesema kuwa mboga hizi ni nzuri kwa suala zima la usalama wa chakula kwa sababu zinastahimili ukame. Vipi kuhusu maji na mbolea – vinahitaji kiasi kikubwa?
MAUNDU:
Inategemeana na aina ya mboga. Kwa mfano baadhi ya aina za mchicha zinahitaji naitrojeni kiasi kikubwa Pia mnavu wa kiafrika unahitaji kiasi kikubwa cha naitrojeni. Ndio maana hukua zenyewe kwa asili jirani na zizi la mifugo ambapo kuna mbolea nyingi. Lakini baadhi ya mboga za majani za kiafrika hukua vizuri katika udongo usio na rutuba, baadhi zinahitaji mbolea nyingi, na baadhi hazihitaji mbolea nyingi, baadhi huhitaji maji mengi kama mnavu. Ndio maana unahitajika kufanya mabadiliko kwa kulima mboga nyingi za aina mbalimbali katika shamba lako kadri inavyowezekana.
MTANGAZAJI:
Ungewashauri nini wakulima wadogowadogo au mtu yeyote katika jiji ambaye angependa kulima hizi mboga za majani?
MAUNDU:
Kwanza kabisa unahitaji kuwa na mbegu. Lakini siku hizi ni rahisi sana kupata mbegu, unaweza kupata kutoka kwenye maduka ya usambazaji wa mbegu za kilimo au kwenye taasisi zinazofanya utafiti juu ya mboga za majani za kiafrika. Watafiti watafurahi sana kukupatia mbegu za kupanda. Pia unaweza kuweka udongo na mbolea kwenye magunia na kuotesha aina zote za mboga za majani ilimradi tu unazimwagilia. Hivyo nafasi sio kikwazo, hata kama upo kwenye ardhi tambarare.
MTANGAZAJI:
Sawa, hebu tuongelee juu ya upikaji wake. Ni njia ipi nzuri zaidi inayofaa kuzipika?
MAUNDU:
Mboga nyingi zinahitaji kupikwa kwa dakika kumi tu au chini ya hapo. Kama ukizipika zaidi ya huo muda, utakuwa unapoteza vitamini nyingi ambazo huyeyushwa kwa joto na kupotea, ikiwemo vitamini C na A. Kwa hiyo njia nzuri ya kuzipika ni kutumia muda mfupi kadri iwezekanavyo bila kupoteza ladha yake.
MTANGAZAJI:
Huyo alikuwa Patrick Maundu, mtafiti wa kisayansi wa vyakula vya kiafrika kutoka Bioversity International Nairobi.
SFX
Sauti ya gari likiwashwa, kisha inafifia
MTANGAZAJI:
Bado nina muda kwa ajili ya kituo kimoja zaidi kabla sijala chakula changu. Katika kituo, nililipitia moja ya maduka makubwa Nairobi kuangalia mboga zao za majani na kuona kama soko la mboga za majani za kiafrika linafanya vizuri.
SFX
Sauti za dukani kisha zinafifia
MTANGAZAJI:
Nipo katika duka kubwa la Uchumi Nairobi, kwenye sehemu ya vyakula vibichi. Mchana umeenda sana na wateja wengi wamejipanga ili kununua mboga za majani. Ninaweza kuona mboga mbichi za mchicha, safi na zilizofungwa vizuri, mgagani, Kale ya kiafrika, mnavu wa kiafrika, malenge/majani ya maboga na majani ya kunde. Mboga za majani hizi zilikuwa haziwekwi katika Maduka makubwa miaka michache iliyopita. Edward Azere ni kiongozi wa wafanyakazi wa duka kubwa la uchumi katika mtaa wa Kainage jijini Nairobi.
MTANGAZAJI:
Kwanini huwa mnaweka mboga za majani za asili ?
EDWARD AZERE:
Wakenya wanapenda sana mboga za majani za asili. Ni nzuri kwa afya zao. Wanapendelea mboga za majani za asili hasa mchicha, mgagani, mnavu wa kiafrika na majani ya kunde, ambazo zina virutubisho sana, pia huweza kuwa dawa za kienyeji.
MTANGAZAJI:
Mnauzaje hizi mboga za majani za asili?
EDWARD AZERE:
Huwa tunauza takribani nchi nzima, mboga za majani za asili zinaongoza kwa kuuzwa katika soko la vyakula vibichi. Hufikia hadi asilimia 80 ya mauzo katika vyakula vibichi tunavyozalisha. Wakati mwingine hitaji huwa kubwa kuliko upatikanaji.
MTANGAZAJI:
Huwa mnazitoa wapi hizi mboga za majani?
EDWARD AZERE:
Wasambazaji wetu huwa wanazipata kutoka kwa wakulima, na kutuletea asubuhi na mapema. Huwa wanatokea mbali magharibi mwa Kenya na mkoani Rift Valley, kwa sababu hapa Uchumi tunaamini katika vyakula vibichi. Hatuchukui mboga zetu za majani kutoka Nairobi kwa sababu hatuna mashamba Nairobi, lakini pia wanaweza kuwa wanatumia kemikali za hatari.
MTANGAZAJI:
Nilikuwa naongea na Edward Azere, meneja wa tawi la duka kubwa la uchumi Nairobi. Hicho kilikuwa kituo changu cha mwisho katika safari yangu. Hebu tuone kama mboga za majani za kiafrika ziko tayari kwa kula. Niko tayari kwa kula mboga za mchicha na mgagani.
SFX
Sauti za kutembea kwa miguu
MTANGAZAJI:
Nimefika hapa. Habari…
ANNE:
Umefika katika wakati mwafaka.
MTANGAZAJI:
Harufu nzuri ya mboga za majani za kiafrika. Siwezi kusubiri kuonja. Hmmm … tamu sana!
Na huo ndio mwisho wa safari yangu kutafiti mlolongo mzima wa mboga za majani za kiafrika nchini Kenya. Asante sana kwa kuwa pamoja nami katika safari yangu yote. Tumejfunza kwanini mboga za majani za kiafrika zimerudi kutumiwa katika chakula, umuhimu wake katika lishe, na namna inavyoweza kusaidia katika suala zima la usalama wa chakula barani afrika.
Tumesikia kutoka kwa Kangara, ambaye ni muuzaji wa mbegu za mboga za majani za asili, na Kimondo ambaye ni mkulima wa mboga za majani za kiafrika. Pia tumesikia kutoka kwa Edward Azere, mwakilishi wa soko kuu, na Patrick Maundu, mwanasayansi wa Bioversity International. Mpaka wiki ijayo, mimi ni mtangazaji wako wa Farmer to Farmer, Winnie Onyimbo.

Acknowledgements

Kimechangiwa na: Winnie Onyimbo, Radio Transworld, Nairobi, Kenya
Kupitiwa upya na: Patrick Maundu, Bioversity International

Information sources

Mahojiano na:
Gidreff kangara, muuzaji wa mbegu wa Wangige, Central province nchini Kenya, Julai 31, 2012
Stephen Kimondo, mkulima wa Kiserian, mkoa wa Rift Valley nchini Kenya, Agosti 3, 2012
Patrick Maundu, Mtafiti wa kisayansi wa Bioversity International, Agosti 18, 2012
Edward Azere, Meneja wa Tawi la duka kubwa la Uchumi Nairobi, Septemba 17, 2012

Kwa habari zaidi na maelekezo ya kutumia mboga za asili:
International Plant Genetic Resource Institute (IPGRI), 2006. Back by popular demand: The benefits of traditional vegetables. http://www.bioversityinternational.org/fileadmin/bioversity/publications/pdfs/1090_Back_by_popular_demand.The_benefits_of_traditional_vegetables.pdf?cache=1342739098

AVRDC (The World Vegetable Centre), hakuna tarehe. African Traditional Vegetables: Recipes for Good Health. http://libnts.avrdc.org.tw/web_docs/recipes/African%20Traditional%20Recipes_final_English.pdf

Slow Food, hakuna tarehe. Cooking with Traditional Leafy Vegetables: Indigenous Plants in Tanzania’s Kitchen. Imepakuliwa katika: http://www.slowfoodfoundation.com/pagine/eng/pubblicazioni/pubblicazioni.lasso?-id_pg=27

Majina ya kawaida ya mboga za majani za asili za kiafrika: Orodha ifuatayo inatoa majina ya kawaida katika lugha mbalimbali kwa baadhi ya mboga za majani zilizotajwa katika kisa. Orodha hii haimaanishi kuwa ni kamilifu. Katika hali nyingi, lugha inatajwa kwanza (katika italiki) na kisha jina la kawaida. Katika baadhi ya sehemu, jina la nchi ndilo limetajwa (katika italiki), si lugha mahususi. Katika hali nyingi, lafudhi haikuhusishwa. Orodha hii imetokana na vyanzo vya internet ambavyo usahihi wake haujathibitishwa.

Mnavu: (Solanum villosum) Adja: gboyame; Kichagga: kimachame; Cotafon; gboyame; kifaransa: morelle jaune, morelle poilue ou velue; Holly: ossun; Kikamba: kitulu; Kipsigis: isoiyot; Kisii: rinagu; Kimasai: nyafu; Kizigua: mnavu; Luhya: namaska, lisutsa; Kijaluo: osuga; Kimasai: ormomoi; Luganda: nsugga; Kiswahili: mnavu; Taita: ndunda.

Mchicha: (aina za Amaranthus) Adja: tete; Kiafrika: hanekam, kalkoenslurp, misbredie, varkbossie; Aizo: fotete, gboholou; Anii: alefo, guiweguifonon, ifofonon; Bariba: afonnou; Kibemba: lengalenga; Boko: efo, gasia; Chichewa: bonongwe; Congo: bitekuteku (Amaranthus viridis, mkoa wa Kinshasa); Cotafon: fotete, tete; Dendi: abahoham; Fon: fotete; Kifaransa: calalou, callalou; Fulani: boroboro; Ghana: madze, efan, muotsu, swie; Giriama: logatsi; Gourmantche: aiinkpinnan; Hausa: alayyafu; Holly: thokoagbodjouba, tete ognibo, tetedudu, tetefounfoun, tetefufu; Idatcha: fotete; Ife: adjogodo; Kamba: woa; Kikuyu: terere; Kipsigis: kelichot; Kisii: embog; Kotokoli: alefo, karatchitou; Lozi: libowa; Luhya: libokoi; Luo: ododo; Maasai: nanyi; Mahi: fotete, tete; Nigeria: efo, tete, inene; Northern Soto: thepe; Nyanja: bonongwe; Oueme: soman; Otammari: adefo; Sierra Leone: grins (Creole), hondi (Mende); Kiswahili: mchicha; Tchabe: efo docteur, olowon’djedja; Temne: ka-bonthin; Tonga: bonko; Tsonga (Shangaan): cheke; Tswana: imbuya, thepe; Venda: vowa; Wana: yonbita, yonbtena, yonman; Xhosa: umfino, umtyuthu, unomdlomboyi; Zulu: imbuya, isheke.

Kishona nguo: (Bidens pilosa) ki-Adja: djankoui; Anii: boboyo; ki-Bondei: twanguo; Kichagga: imbara; kifaransa: coréope odorante; Gogo: mhangalale; ki-Haya: obukuruna; ki-Hehe: livanivani; Kamba: musee; Kikuyu: mucege; Luo: onyiego; ki-Luhya: orogohe; k-Maasai: oloreperep; ki-Matengo: injule; Mbwembwe Meru: ishashando; ki-Ndebele: ucucuza; ki-Ngoni: kisosoki, manyonyoli; Northern Soto: monyane; ki-Nyamwezi: lekalamata; Nyaturu: mpangwe; Sambaa: kitojo; ki-Shona: nhungunira; Kiswahili: kishona nguo; Tsonga (Shangaan): muxidji; ki-Zulu: uqadolo.

Kunde: (Vigna unguiculata) Acholi: boo, ngor, enkoole; Adja: ayiman; Aizo: ayiman, yiviman; Alur na Jonam: amuli, obo; Amharic: adenguare; Anii: atchakobo, guisei; Arabic: lubia hilo; Bariba: suiwurusu; Boko: blaa; Bugisu: likote; Chichewa: khobwe; Cotafon: ayiman; Ethiopia: nori; Fon: ayiman; Kifaransa: niébé; Giriama: tsafe; Gourmantche: titukpindi, toutoufari; Holly: ewa, eweewa; Idatcha: ewa; Kakwa: nyele, laputu; Kambe: nthooko; Kikuyu: thoroko; Kisii: egesare, kunde; Kiswahili: kunde; Kokokoli: sonanfade; Langi: eggobe, ekiyindiru, mpindi; Luganda: kiyindiru, bojo; Luhya: likhuve; Luo: a lot-bo; Maasai: soroko; Mahi: ayiku, ayiman; <>Ndebele: ndlubu, indumba; Nigeria: agwa, akidiani; Northern Sotho: dinawa, monawa; Nyiha: kunde; Otammari: titu’nti, tituti; Oueme: ayiman; Oshiwambo: omakunde, olunya (white with black eye), omandume or ongoli (mixed black, brown, purple); Runyankore: omugobe; Rutooro: omugobe; Runyoro: omugobe; Sesotho: linaoa; Setswana: dinawa, nyeru, dinawa, morogo wa dinawa; Shona: nyemba; Siswati: tinhlumayi; Tchabe: ewa; Teso: eboo, imere; Tonga: ilanda, nyabo; Tsonga (Shangaan): msoni; Tumbuka: nkunde; Uganda: amuli, boo-ngor, omugobe, boo (in Acholi and Luo); Wama: yangutu, yonguitu.

Crotalaria: (aina za Crotalaria) Kifaransa: crotalaria, crotalaire, chanvre de Bengale, sunn; Gourmantche: kumalikoungu; Kikamba: kamusuusuu; Kipsigis: kipkururiet; Luhya: emiro, mitoo; Luo: mito, mitoo; Kimasai: oleechei; Pokot: karma; Wama: kuanonman.

Kale ya Kiethiopia au Kiafrika: (Brassica carinata) Kifaransa: chou frisé africain; Luhya: kanzira; Kijaluo: kadhira.

Gallant soldier: (Galinsoga parviflora) Francais: Galinsoga à petites fleurs.

Mnavu: (Solanum scabrum) Adje: lanman; Bariba: kopwonka; Francais: morelle scabre; Kamba: kitulu; Kikuyu: managu; Kipsigis: isoiyot; Luhya: namaska; Luo: osuga; Luganda: nsugga; Maasai: ormomoi; Kiswahili: mnavu; Taita: ndunda; Wama: kotorokou.

Mlende: (Corchorus olitorius) Adja: demi; Aizo: azatalouga, nenouwi, ninhouin, ninjouinaman; Anii: ayoyo, banan, bawounna, gbannan; Arabic: molkhia; Bariba: yoyokun; Bembe: lusakasak; Boko: viohounda, viola, yoyogunan; Cotafon: ademe, demin, deminve; Dendi: ayoyo; Fon: ninnouwi; Giriama: vombo; Francais: corète, corète potagère, corette, corette potagère, craincrain, jute potager, krinkrin, mauve des Juifs, épinard égyptien, gombo de brousse; Gourmantche: minapuopuoma, oyo, tibagnalifare; Hausa: láálò, malafia, tùrgúnùùwáá; Holly: eyo, obeodundun, obeyofunfun, obeyoloyo; Idatcha: yoyo; Ife: ayoyo; Kisii: omotere; Kotokoli: ayoyo; Luhya: omurere; Luo: apoth; Mahi: nennuwi, ninnou; Ndebele: idelele; Northern Soto: thelele; Nyanga: tindingoma; Otammari: tifaanti; Oueme: nenoun; Shona: nyenje, gusha; Sierra Leone: crain crain; Songhai: fakohoy; South African languages: telele, delele and gushe; Sudanese Arabic: khudra; Swahili: mlende; Tchabe: ooyo; Tonga: delele, cikombo bbuyu; Tsonga (Shangaan): guxe; Wama: sekefeman, yoyora, yroyrogou.

Mlonge: (Moringa oleifera) Adia: kpashima; Adje: drele; Aizo: celiman, yovokpatin; Bariba: yuru ara, yorwata yoroguma, goratonou, waguiri; Boko: worousolola, woso; Cotafon: kpatovi, kpatovigbe; Dendi: windi boundou; Kingereza: moringa, horseradish tree, drumstick tree, sujuna, ben tree, ben oil tree; Fon: kpatima, yovokpatin, kpano, yovotin, kpanuman, kpanuyedede; Kifaransa: ben ailé, ben oléifère, benzolive, arbre radis du cheval; Giriama: muzungi; Gourmantche: bouloubouli, ganbaaga; Gun: èkwè kpatin, kpajima; Hausa: jagalandi, bàgààrúúwár ÞMásàr, barambo, karaukin zaila, mákkà, ríímín násárà, sàmààrín dángáá, shùùkà hálíí, taɓa ni ka saamuu, zóógálé; Idatcha: langalanga, langali; Ife: ayinyere; Mahi: kpalouman, yovokpatin; Mina: yovo vigbe, yovo kpati; Oueme: yovokpatin; Saxwe: kotba; Swahili: mzunze, mlonge, mjungu moto, mboga chungu, shingo; Tchabe: agunmonliye, lagalaga; Yoruba and Nago: ewè igbale, ewè ile, ewè oyibo, agun oyibo, ayun manyieninu, ayèrè oyibo; Wama: masamanbu, yorikungufa.

Malenge: (Cucurbita moschata) Francais: feuilles de citrouille; Holly: aguidi; Kisii: omuongo; Luhya: lisebebe; Luo: budho; Northern Soto: mophotse; Swahili: malenge; Tsonga (Shangaan): tinwembe; Zulu: intanga.

Mgagani: (Cleome gynandra): Adja: sabo; Bariba: garsia; Bembe: lubanga; Cotafon: kaya; Dendi: foulbe; Fon: akaya; Giriama: mwangani; Francais: plante-araignée, phalangère; Holly: djen’dje, effooko; Idatcha: efo; Ife: akaya, efun; Kalenjin: saget; Kamba: mwianzo; Kikuyu: thagiti; Kipsigis: isakyat; Lozi: sishungwa; Luganda: jjobyu; Luhya: tsisaka; Luo: alot-dek; Lusoga: yobyu; Maasai: lemba-e-nabo; Mahi: akaya: Marakwet: sachan, suroyo; Meru: munyugunyugu; Ndebele: elude; Nyanza: suntha; Okiek: isakiat; Pokot: suriyo, suriya, karelmet; Rendille: bekeila-ki-dakhan; Sabaot: sakiantet; Samburu: sabai, lasaitet; Sanya: mwangani; Setswana: lothue; Shona: nyeve, runi; Somali: jeu-gurreh; Swahili: mwangani, mgagani; Tonga: shungwa; Tsonga (Shangaan): bangala, xibangala; Wama: garsia.

Stinging nettle: (Urtica massaica) Francais: grande ortie, ortie élevée; Kikuyu: thabai.

gac-logoMradi umefanywa kwa msaada wa Serikali ya Kanada kupitia Shirika la Maendeleo ya Kimataifa la Kanada (CIDA)