Wanasayansi wanaboresha vichanja vya asili vya mahindi

Shughuli za baada ya mavuno

Ujumbe kwa mtangazaji

Pakua na hariri taarifa hii kwa matumizi yako.

Kusheherekea kufikisha maandalizi ya vyanzo 100 vya taarifa, tunarudia kuandaa moja kati ya mwongozo Namba #1, mwongozo ambao umesambazwa kwa waandishi 34 katika nchi 26 mnamo mwezi wa Tano mwaka 1979. Kipengele kifuatacho ni mwongozo #6 katika kifungu hicho cha kwanza. Tunasambaza kama kilivyo andikwa mwaka huo wa 1979.

Kwa miezi inayokuja, FRI itarejea miongozo ya zamani na kuzichapisha katika tovuti yetu. Tutahakikisha kuwa taarifa ni za wakati na ni taarifa husika, na kuweka katika mfumo mzuri ili ziweze kutumika.

Hivyo … Karinu katika Mwongozo wa awali wa Farm Radio International! Kipengele kifuatacho kimeonyeshwa neon –kwa-neno, kama ilivyo chapishwa na kusambazwa mwaka 1979 na mwanzilisho waFRI, George Atkins.

Script

George Atkins, mkulima kwa miaka mingi, amesafiri duniani kwa Massey-Ferguson, Chuo cha Guelph na Shirika la maendeleo la kimataifa la Kanada, akitafuta namna ya kuwasaidia wakulima kuongeza mavuno yao. Barani Afrika, alikutana na mwanasayansi aliyekuwa akifanya utafiti jinsi ya kubadilisha vichanja vya kienyeji vya mahindi ili mahindi yakauke haraka Zaidi, vizuri, hasahasa katika maeneo yenye unyevu.

Washiriki:

George Atkins

Daktari. W. H. Boshoff, Msimamizi wa mradi, FAO Maghala ya kuhifadhi mazao vijijini Afrika, Taasisi ya kimataifa ya Kilimo cha nchi za Kitropiki, Ibadan, Nigeria, Afrika Magharibi

ATKINS:
Nikisimama shambani nchini Nigeria na Daktari. W.H. Boshoff, tulikuwa tungiangalia vichanja virefu, vyembamba vya pembe nne. Ujenzi wa vichanja ulikuwa mrahisi. Vifaa vya kujengea vichanja vilikuwa vimekatwa msituni kwa mikono. Kichanja kilikuwa kimejengwa na nguzo za miti, vijiti na mianzi vikiwa vimeezekwa na majani ya minazi katika kuta. Kichanja kilikuwa kimejengwa kwa muundo kwamba kimenyanyuka usawa wa mita moja kutoka ardhini (hatua 1).

Tulivyokuwa tukizungumzia vichanja hivi na Daktari, Daktari. Boshoff hodari wa wote, aliniambia.

BOSHOFF:
Hatuku buni vichanja hivi, Vichanja hivi vilikuwa vikitumika kwa miaka mingi.

Ni muundo weney kuruhusu hewa kuingia ndani na kuuwa kukua kwa ukungu ndani ya kichanja.

Kwahiyo tumeanzisha, kama, kutokana na hali ya mazingira yako, eneo lenye unyevu Zaidi ndivyo kichanja kinakuwa chembamba zaidi. Katika maeneo yenye unyevu Zaidi inatakiwa tu kuwa na upanda wa mite mbili au sentimita 60. Katika maeneo yenye unyevu wa chini unaweza kuwa na upana wa sentimita 10 au futi 5.

Hii inaruhusu hewa kupita vyema. Itazuia fangasi kutengeneza, na ukiwa unatumia viuatilifu mazao yatakuwa salama. Itakauka polepole na itafikia kiwango cha chini cha unyevu, nyuzi 15 na kuwa tayari kwa kupukuchua na kuhifadhi katika magunia; — hii ni kwa maeneo yenye unyevu.

Kama hali ya hewa ni nzuri kiasi cha kuweza kushusha hali ya hewa na kuwa na kiwango cha unyevu chini ya asilimia 12%, mtu anaweza kuhifadhi mahindi katika jingo lililojengwa hata kwa matofali. Lakini hii haishauriwi kutumika katika maeneo yenye Joto.

ATKINS:
Ni muhimu kuelekeza vichanja hivi katika muelekeo Fulani, kama kaskazini, kusini, mashariki au magharini?

BOSHOFF:
Kitu cha muhimu. Ndio-Katika maeneo ya nchi ambapo kuna pepo kuu, utaelekeza kichanja upande wenye upepo. Lakini katika nchi za kikweta zenye latitude za kawaida, utakuta hakuna pepo kuu. (Utaona, kwa sasa hakuna upepo kabisa.) Lakini kuna kipupwe kidogo mida ya jioni.

ATKINS:
Pamoja na hayo, vipi kihusu jua─ jua ni kali, kwa mfano, kipindi cha jioni ni kali kuliko muda wa asubuhi mapema? Labda kichanja kinapata jua vizuri kwa kujenge kwa muundo wa Kidaktari.

BOSHOFF:
Ndio, tena hili ni swali zuri sana, kwasababu katika kipindi cha mwezi was aba mpaka mwezi wa tisa. Kuna kuwa na jua kidogo sana muda wa asubuhi kuliko mchana. Hivyo kichanja chako kinakuwa kipana, utaona kuwa inakauka haraka upande wa magharibi kuliko mashariki. Kama ni ya upana wa kawaida kwa unyevu wa kawaida na hali ya kawaida, ita kauka kwa usawa.

Kwa kawaida zitaanza kukauka mbegu chache tu zilizoko juu; chini ya hapo zitakuwa katika layer ya pili na au chini.

Utapata upepo unao kausha wakati wa jioni zitokazo magharibi hapa Nigeria.

ATKINS:
Sawa, sasa niambie kuhusu, kuhusu sakafu katika vichaja hivi.

BOSHOFF:
Sawa, zimetengenezwa na mianzi yenye vitobo vilivyozibwa, Wakati wa kutoa mazao unaweza kutoa vizibo na kuweka vikapu chini na kukinga mbegu kama unavyokinga maji, rahisi kama hivyo.

ATKINS:
Kwa hali hii, kichanja kinakuwa kimejengea kwa mianzi, ninashauri mianzi kwasababu inaacha uwazi kati ya mwanzi na mwanzi na kupelekea hewa kuingia.

BOSHOFF:
Ndio, lakini vifaa vyovyote mkulima anavyoweza kupata katika eneo lake atumie kujenga kichanja. Inahitajika kuwa imara kwasababu inabebe mzigo mkubwa.

ATKINS:
Yote hayo kutoka kwa mtaalamu mmoja aliyebobea kuongelea kuhusu uhifadhi wa mahindi katika nchi zinazoendelea Duniani – Daktari. W.H. Boshoff, Taasisi ya kimataifa ya kilimo za nchi za Kitropiki Ibadan, Nigeria, Afrika Magharibi.

Kuhudumia “Kilimo, Kiwanda cha kawaida,” huyu ni George Atkins.

Acknowledgements

gac-logoMradi umefanyika na msaada wa kifedha kutoka serikali ya Kanada kupitia kitengo cha Mahusiano ya kimataifa, Biashara na Maendeleo (DFATD)

The translation of this resource was made possible with the support of USAID’s New Alliance ICT Extension Challenge Fund, through the International Fund for Agricultural Development in Tanzania. For more information about the Fund, please see: https://www.ifad.org/