Ujumbe kwa mtangazaji
Kusheherekea kufikisha maandalizi ya vyanzo 100 vya taarifa, tunarudia kuandaa moja kati ya mwongozo Namba #1, mwongozo ambao umesambazwa kwa waandishi 34 katika nchi 26 mnamo mwezi wa Tano mwaka 1979. Kipengele kifuatacho ni mwongozo #6 katika kifungu hicho cha kwanza. Tunasambaza kama kilivyo andikwa mwaka huo wa 1979.
Kwa miezi inayokuja, FRI itarejea miongozo ya zamani na kuzichapisha katika tovuti yetu. Tutahakikisha kuwa taarifa ni za wakati na ni taarifa husika, na kuweka katika mfumo mzuri ili ziweze kutumika.
Hivyo … Karinu katika Mwongozo wa awali wa Farm Radio International! Kipengele kifuatacho kimeonyeshwa neon –kwa-neno, kama ilivyo chapishwa na kusambazwa mwaka 1979 na mwanzilisho waFRI, George Atkins.
Script
George Atkins, mkulima kwa miaka mingi, amesafiri duniani kwa Massey-Ferguson, Chuo cha Guelph na Shirika la maendeleo la kimataifa la Kanada, akitafuta namna ya kuwasaidia wakulima kuongeza mavuno yao. Barani Afrika, alikutana na mwanasayansi aliyekuwa akifanya utafiti jinsi ya kubadilisha vichanja vya kienyeji vya mahindi ili mahindi yakauke haraka Zaidi, vizuri, hasahasa katika maeneo yenye unyevu.
George Atkins Daktari. W. H. Boshoff, Msimamizi wa mradi, FAO Maghala ya kuhifadhi mazao vijijini Afrika, Taasisi ya kimataifa ya Kilimo cha nchi za Kitropiki, Ibadan, Nigeria, Afrika Magharibi Tulivyokuwa tukizungumzia vichanja hivi na Daktari, Daktari. Boshoff hodari wa wote, aliniambia. Ni muundo weney kuruhusu hewa kuingia ndani na kuuwa kukua kwa ukungu ndani ya kichanja. Kwahiyo tumeanzisha, kama, kutokana na hali ya mazingira yako, eneo lenye unyevu Zaidi ndivyo kichanja kinakuwa chembamba zaidi. Katika maeneo yenye unyevu Zaidi inatakiwa tu kuwa na upanda wa mite mbili au sentimita 60. Katika maeneo yenye unyevu wa chini unaweza kuwa na upana wa sentimita 10 au futi 5. Hii inaruhusu hewa kupita vyema. Itazuia fangasi kutengeneza, na ukiwa unatumia viuatilifu mazao yatakuwa salama. Itakauka polepole na itafikia kiwango cha chini cha unyevu, nyuzi 15 na kuwa tayari kwa kupukuchua na kuhifadhi katika magunia; — hii ni kwa maeneo yenye unyevu. Kama hali ya hewa ni nzuri kiasi cha kuweza kushusha hali ya hewa na kuwa na kiwango cha unyevu chini ya asilimia 12%, mtu anaweza kuhifadhi mahindi katika jingo lililojengwa hata kwa matofali. Lakini hii haishauriwi kutumika katika maeneo yenye Joto. Kwa kawaida zitaanza kukauka mbegu chache tu zilizoko juu; chini ya hapo zitakuwa katika layer ya pili na au chini. Utapata upepo unao kausha wakati wa jioni zitokazo magharibi hapa Nigeria. Kuhudumia “Kilimo, Kiwanda cha kawaida,” huyu ni George Atkins. Mradi umefanyika na msaada wa kifedha kutoka serikali ya Kanada kupitia kitengo cha Mahusiano ya kimataifa, Biashara na Maendeleo (DFATD) The translation of this resource was made possible with the support of USAID’s New Alliance ICT Extension Challenge Fund, through the International Fund for Agricultural Development in Tanzania. For more information about the Fund, please see: https://www.ifad.org/Acknowledgements