Uvumbuzi wa Neddy: Mfanyakazi wa afya ya wanyama asaidia kijiji kudhibiti ugonjwa wa Kideri

Mifugo na ufugaji nyuki

Ujumbe kwa mtangazaji

Pakua na hariri taarifa hii kwa matumizi yako

Maelezo kwa mtangaaji

Kuku ni aina ya mifugo ambayo ni rahisi sana kuwafuga kwa sababu wanaweza kujilisha kwa uhuru kwa kula vyakula vinavyopatikana kwa urahisi. Kwa maneno mengine, ni wanayama wajilishao kwa uhuru. Pia, kuku huzalisha kwa urahisi. Lakini ni waathirika wa ugonjwa mkubwa ambao hauwezi kutibika: Ugonjwa wa Kideri. Ingawa hauna tiba, kuna chanjo ya ugonjwa huo. Wafugaji hushindwa kuchanja mara kwa mara kwa sababu ya ukosefu wa ujuzi au kwa sababu chanjo ni ghali. Mara nyingi, dawa hii inauzwa katika chupa kubwa ambayo inaweza kutibu kuku mamia kadhaa. Hii ni ghali sana kwa wakulima ambao wana kuku wachache tu. Na ndiyo sababu chanjo ya kuku kwa jamii nzima kupitia wafanyakazi wa jamii wa afya ya mifugo ni wazo kubwa la muhimu.

Katika maeneo mengi, kuna uhaba wa madaktari wa mifugo. Wataalam wasaidizi, pia huitwa wafanyakazi wa jamii wa afya ya mifugo au wajitolea wa mifugo, kusaidia kutoa huduma ambapo hakuna wataalam wa mifugo. Wao ni wajitolea ambao hawapati mshahara wowote, lakini wanapata maisha kwa ktoza ada ndogo ya ajira kwa huduma zao. Wamepata mafunzo ya kutambua na kutibu magonjwa mengi ya mifugo, na kupeleka rufaa ya magonjwa mengine kwa wataalam Zaidi wa mifugo. Wafugaji mara nyingi wanatumia dawa za mifugo na kutoa usafiri kwa wafanyakazi wa jamii wa afya ya mifugo na kutoka shamba lao.

Katika muongozo huu, wafanyakazi wa jamii wa afya ya mifugo huwaambia wanakijiji kuwa chanjo ya ugonjwa wa Kideri inapatikana tu kwa dozi kwa idadi kubwa ya kuku, kama 300 au zaidi. Katika baadhi ya nchi za Afrika, chanjo zilizo na dozi ndogo zinaweza kununuliwa. Pia, katika baadhi ya nchi za Kiafrika kama vile Zambia, Msumbiji na Ghana, chanjo zinapatikana ambazo hazipaswi kuhifadhiwa kwenye jokofu. Fanya utafiti wa hali katika nchi yako.

Muongozo huu ni igizo fupi linaloonyesha haja ya chanjo dhidi ya ugonjwa wa Kideri na faida za kuwa na wafanyakazi wa jamii wa afya ya mifugo katika jamii yako. Njia mbili za kutumia muongozo huu ni kwa kurekebisha tu mchezo wa kuigiza kwa wasikilizaji wako au kuitumia kama msukumo wa kuzalisha mchezo huu wa kuigiza juu ya magonjwa ya mifugo katika eneo lako.

Script

MSIMULIZI:
Katika nchi nyingi za Afrika, ikiwa ni pamoja na Malawi, wakulima wengi wana angalau kuku mmoja. Kuku hawa ni mifugo ya ndani ambayo huachiliwa kula kwa uhuru. Kwa maneno mengine, ni kuku wanaojilisha. Kuongezeka kwa ugonjwa wa Kideri kunaweza kuua kuku wote wa kijiji. Kideri inaweza kuzuiwa na chanjo. Kwa nini wakulima wengi hawanunui dawa ya chanjo kwaajili ya kuku wao? Uwe tayari kujua.

FX:
SAUTI YA KUPIGA CHUMA NA NYUNDO NDOGO.

MKE:
Mume wangu Neddy, kwa nini unatengeneza baiskeli wakati huu wa jioni? Unataka kwenda wapi muda huu?

NEDDY:
Oh! Mke wangu … Sienda mahali popote leo. Mimi ninajitayarisha tayari kwa ajili ya kesho. Unajua majira ya joto yanakaribia ….

MKE:
(Kwa tabasamu) Nilidhani ni ng’ombe mwingine mgonjwa. Kwa kuwa umekuwa mfanyakazi wa jamii wa afya ya mifugo, wewe umekuwa ni mtu wa kutoka toka kila saa …

NEDDY:
Je sasa umefurahi mke wangu?

MKE:
Naam. Kwa nini isiwe hivyo?

NEDDY:
Hivi ni nini hasa maana ya kuwa mfanyakazi wa afya ya mnyama wa jamii. Je, sio kuongeza kipato katika maisha yetu, mke wangu?

MKE:
Najua. Lakini watu wanahitaji kukupa wakati fulani wa kupumzika. Wanakuita wakati wote. Hata katikati ya usiku! Njoo hapa! Mnyama alifanya hivyo, nguruwe ana shida hii …. Hakuna wakati wa kupumzika.

NEDDY:
Kwa hiyo unanijali sana kiasi hicho?

MKE:
Ndio nakujali, mpendwa wangu.

Wote wakicheka.

MKE:
Lakini Neddy, nikasikia unasema kitu kuhusu majira ya joto yanakaribia. Kuna uhusiano gani kati ya majira ya joto kukaribia na wewe kwenda mjini kesho?

NEDDY:
Unajua kuwa majira ya joto ni msimu wa ukavu. Lakini je, unajua pia kwamba wakati wa majira ya joto tunapoteza kuku wale ambao wameongezeka wakati wa mvua kwa ugonjwa wa Kideri?

MKE:
Ndiyo, najua.

NEDDY:
Hivi sasa ni wakati mzuri wa kuchanja kuku zetu – kabla ya Kideri kuja. Ni karibu ni miezi mitatu tangu tulipata chanjo katika kijiji hiki na vijiji vingine vinavyotuzunguka.

MKE:
Sawa. Hivyo unataka kununua dawa ya chanjo kwaajili ya kuku wenu?

NEDDY:
Hapana! Si kwa ajili ya kuku zetu tu, lakini …

MKE:
(Kwa hasira akamdakia) Lakini ni nini? Je! Unataka tena kukabiliana na aibu kama hapo awali? Je! Umesahau jinsi watu walivyosema kuwa unatoa chanjo ya kuku ili upate fedha?

NEDDY:
Nakumbuka vizuri sana mke wangu, lakini unajua …

MKE:
(Akimdakia) Kujua nini? Usijibizane nami zaidi. Kesho ukienda mjini, nunua dawa ya chanjo ya kuku kumi. Ni hayo tu!

NEDDY:
Hapana. Unajua hakuna chupa ndogo kwa ajili ya kuku 10. Duka moja huuza dawa ya chanjo kwa kuku 1000 kwenye MK850 (2615 Tshs) na duka lingine linauza chanjo kwa kuku 300 kwenye MK600 (1845 Tshs). Hivyo …

MKE:
(Kwa kumdakia) Hivyo nunua moja kwa kuku 300, tumia kwa kuku kumi na uitupe inayobaki.

NEDDY:
Tutapoteza pesa. Ina maana kwamba tutaweza kukuza kuku kwa MK60 (185 Tshs) kila mmoja badala ya MK10 (31 Tshs), ambayo ninaweza kutoza wengine na tukapata faida.

MKE:
Kwa hiyo ni kweli kama watu wanavyosema – kwamba unafanya kwa biashara?

NEDDY:
Mke wangu, kumbuka nini kilichotutia moyo kujitolea kujifunza ujuzi wa kutibu mifugo. Je! Sio ili kukomesha matatizo ya afya ya wanyama katika kijiji hiki? Nilidhani ndoto yetu ilikuwa kuokoa kijiji chetu kutokana na magonjwa ya mifugo na matatizo ambayo yanaweza kuzuiwa?

MKE:
Ndiyo, nakumbuka na kwa sababu hiyo mimi nakuruhusu kufanya kama ulivyopanga.

NEDDY:
Huyu sasa ndiye mke wangu anazungumza.

Wakicheka wote kwa pamoja.

Mpito wa mabadiliko. Pandisha Muziki, kisha shusha na kuacha chini chini.

MSIMULIZI:
Neddy anajua vizuri kwamba kununua chupa kubwa ya chanjo kwa kuku wachache tu ni kupoteza pesa. Je! Umewahi kujaribu kuhusisha jirani yako katika chanjo ya kuku zako? Ni ngumu! Je ukijaribu kuhusisha kijiji chote kwa ada ndogo? Je! Umewahi kujaribu kuhusisha jamii nzima ili kuzuia ugonjwa wa Kideri?

PANDISHA MUZIKI NA UACHE UENDELEE CHINI CHINI.

MSIMULIZI:
Neddy anajua kuwa tangu alipoponya kuku kwa miezi mitatu iliyopita hakuwa na habari kuhusu ugonjwa wa Kideri, hata katika vijiji ambavyo havikuchanja kuku zao. Je! Wanakijiji watamruhusu kuchanja kuku zao wakati huu? Watu wameitwa kwenye ofisi ya Mwenyekiti wa kijiji na wanasubiri kusikia kwa nini wameitwa.

FX:
UMATI KATIKA OFISI YA KIJIJI

KIONGOZI WA KIJIJI:
Wananchi. Nyamazeni. Kimya tafadhali. Kimya tafadhali.

MWALE:
(Yeye amelewa na kuimba polepole na kucheza kama anakaribia mahakama akienda mbali na kipaza sauti) Ayo! Ayo! Ayo! Mpe glasi iliyojaa bia!

FX:
WATU WOTE WAKICHEKA

MKE:
(Akinong’ona) Ndugu yangu Mwale wanitia aibu. Muda wote umelewa. Ni kwa kiasi gani mkeo huaibika?

BI KWENDA:
Ndiyo, kaka yako daima hunywa. Lakini kwa upande mwingine, ndugu yako Mwale ni mchapa kazi. Angaliweza kupunguza unywaji wake wa pombe, basi angefanikiwa sana.

MKE:
Uko sawa.

KIONGOZI WA KIJIJI:
Bw. Mwale! Bw. Mwale!

MWALE:
Chifu!

KIONGOZI WA KIJIJI:
Ninasema kimya, tafadhali!

MWALE:
(Kwa upole) Sawa mkuu, sawa. Nitaketi karibu na mkwe wangu Neddy. Lakini kwanza tuambie kwa nini umetuita …. Tunataka kwenda nyumbani. Tuna mambo mengine muhimu ya kufanya … sisi tunakunywa.

Watu wengine wakicheka. Wengine wananong’na kwa kumsaidia na wengine wanampinga Mwale.

KIONGOZI WA KIJIJI:
Mwale! Kimya. Kumbuka utatozwa faini ukikosa adabu katika mahakama yangu.

MWALE:
Samahani, chifu. Samahani, chifu.

KIONGOZI WA KIJIJI:
(Anapumua kwa ishara ya kupumzika kuleta mabadiliko ya somo) Mkutano huu umeitishwa na madkatari wetu wa jamii wanaojitolea kutibu mifugo, ni mwana wetu wenyewe, ni mtu ambaye amewawezesha wengi wetu kuwa na ng’ombe wa maziwa wa kisasa kwa njia ya kienyeji kupandisha mbegu akitumia mikono yake ya ajabu. Hebu tumkaribishe Mheshimiwa Neddy.

WATU:
(Watu wakiimba na kupigia miluzi) Neddy! Neddy!

NEDDY:
(Anaanza kuzungumza wakati watu bado wanapiga kelele) Asante, mkuu, kwa heshima hiyo.

MWALE:
Nenda moja kwa moja kwenye lengo na usitucheleweshe tena.

BI KWENDA:
(Kwa sauti yake yote) Utulivu! Utulivu! Sala! (Ukimya kabisa) Hebu tukasikie ni nini mfanyakazi wetu wa jamii wa afya ya mifugo ametuletea. (Kimya)

NEDDY:
(Akisafisha koo) Kama unavyojua, miezi mitatu imepita tangu tulipochanja kuku zetu, na majira ya hatari yanakaribia wakati ugonjwa wa Kideri unaweza kuambukiza tena kuku zetu.

WOTE:
Ndiyo.

NEDDY:
Ni wakati wa kuchanja kuku zetu tena.

Bw. KWENDA:
Je! Ungependa chanjo hii ifanyike lini?

NEDDY:
Mmm … Leo ni siku ya Jumamosi. Ili kukupa muda wa kukusanya pesa, unadhani tunaweza kufanya lini, Bwana Kwenda?

Bw. KWENDA:
Siku ya Jumanne asubuhi wiki ijayo.

NEDDY:
Je wote mnakubaliana na hilo? Siku ya Jumanne wiki ijayo!

WOTE:
Ndiyo.

NEDDY:
Usiwafungulie kuku wako waende huru siku ya Jumanne hadi watakapopata chanjo.

WOTE:
Ndiyo.

MWALE:
Je ni shilingi ngapi kwa kuku safari hii?

NEDDY:
Kwa sababu watu wengi wana kuku katika kijiji hiki, nimepunguza ada kutoka K10 (31 Tshs) kila mmoja hadi K5 (15 Tshs) ili kuwatumikia ninyi, watu wangu. Hiyo ni punguzo la 50%.

FX:
(Wote wamefurahi na kupaza sauti) Neddy! Neddy!

MWALE:
(Mgomo) Hicho kiasi ni kikubwa sana. Kikubwa sana.

NEDDY:
K5 (15 Tshs) ipo upande wa chini. Je, unatumia kiasi gani katika bia? Malipo ya kawaida katika vijiji vyote vilivyo karibu ni K10 kwa kila kuku.

Bi. KWENDA:
Kwa nini wewe unatoza tofauti? Kwa nini bei ya chini kwa kuku wengi?

NEDDY:
Asante, Bi Kwenda, kwa swali hilo. Kumbuka wakati nilipowaambia kuwa ninanunua dawa ya chanjo kwa fedNEDDYha yangu mwenyewe na kwamba ninawatoza tu malipo ya kurudisha fedha na kazi yangu? Ikiwa kuna kuku wachache tu, basi ninahitaji kuongeza bei kwa kila kuku ili kupata pesa yangu niliyoitumia.

MWALE:
Wewe unadanganya. Je, huwezi kutunza dawa iliyobaki kuchanja kijiji kingine? …

NEDDY:
Hapana! Mara baada ya chupa kufunguliwa, ni lazima itumiwe dawa yote aliyomo humo ndani ya saa mbili hadi nne vinginevyo itaharibika na inakuwa haina kazi.

MWALE:
Usije nyumbani kwangu.

NEDDY:
Nimerudia mara kwa mara kwako: Unaweza kununua chupa kubwa ya chanjo kwa kuku 300 ikiwa una pesa nyingi. Kama bwana Mwale – nafikiri anataka kununua mwenyewe.

Bi. KWENDA:
Tumekuelewa. Njoo Jumanne, waache wale ambao hawataki chanjo. Tuna kuku wachache. Kwa nini kutumia fedha nyingi kwa kuku wawili badala ya K10 (31 Tshs) kwa idadi hiyo hiyo?

NEDDY:
Kwa hiyo ni Jumanne, kila mtu.

WOTE:
Ndiyo.

MWALE:
Mkwe wangu Neddy, nimesema kuwa sikutaki uje nyumbani kwangu. Nitakufukuza na mbwa ikiwa utakuja.

KIONGOZI WA KIJIJI:
(Akipiga kelele) Mnaweza kurudi nyumbani. Lakini kumbukeni Jumanne asubuhi. Na K5 (15 Tsjs) kwa kila kuku.

WOTE:
(Wakiwa mbali na kipaza sauti) Ndiyo.

MWALE:
Neddy, Neddy, usije nyumbani kwangu. Ninarudia. Katika nyumba yangu usije.

NEDDY:
Usinisumbue kwa hilo, bwana Mwale. Hebu tujadili kuhusu hilo tunapoenda. (Kwa kiongozi wa kijiji) Asante, mkuu. Nitawaona siku ya Jumanne asubuhi.

KIONGOZI WA KIJIJI:
(Akiwa mbali na kipaza sauti) Usisahau kuku wangu, Neddy. Nitakuwa mbali kwenye semina lakini tafadhali tafadhali uje. Utakuta kila kitu katika utaratibu. Binamu yako na mama yao watawasaidia.

NEDDY:
Usijali, mkuu. Mimi nitafanya huduma hiyo. (Kimya, halafu Mwale) Kwa hiyo wewe, Mwale. Kwa nini ni wewe, mkwe wangu, ambaye ananipa matatizo daima?

MWALE:
Unatutapeli.

NEDDY:
Unafikiri hivyo? Je! Umewahi kuona ugonjwa wa Kideri katika kijiji hiki tangu mradi wa chanjo ulipoanza?

MWALE:
Kamwe wala sijaiona katika vijiji vyote ambako nimekwenda kunywa bia kwa miezi nane iliyopita. Hata katika vijiji ambako hawakuchanja kuku zao.

NEDDY:
Hata wao wakati huu wameniomba niwapelekee chanjo kwa ajili ya kuku zao pia.

MWALE:
(Akicheka) Ha ha! Ha! Mkwe wangu, umeweza kuwadanganya nao pia?

NEDDY:
Mwale, tafadhali nisikilize. Huu ndio wakati muhimu zaidi wa kuchanja kuku zetu, kwa sababu majira ya joto yanakaribia.

MWALE:
Kawadanganye wale ambao hawana matumizi bora ya pesa zao. Si mimi.

NEDDY:
(Kwa hasira na kuhoka) Sawa! Unafikiri kila mtu ni mjinga lakini wewe ni mjanja? Imekubaliwa! Sitakuja nyumbani kwako ili kuchanja kuku zako. Kwaheri.

MWALE:
(Akiwa mbali na kipaza sauti) Huyo ni mkwe wangu. Usije tafadhali, Neddy.

MUZIKI: PANDISHA KISHA WEKA CHINI CHINI.

MSIMULIZI:
Jumanne alikuja. Neddy alichanja kuku kwa kila mtu isipokuwa kwa yule bwana Mwale. Watu wengine katika vijiji vya jirani walimruhusu kuchanja kuku, lakini wengine hawakukubali. Mwezi mmoja uliopita bila fununu yeyote ya ugonjwa wa Kideri. Je! Hii inamaanisha kuwa wale watu ambao hawakuweza kuchanja kuku zao walikuwa sawa?

MUZIKI:
SHUSHA CHINI HUKU UKIPANDISHA FX.

FX:
JOGOO ASUBUHI.

FX:
Kubisha mlango kwa nguvu. Na weka sauti chini chini.

MKE:
(Akimwamsha mumewe) Neddy! Neddy! Amka. Mtu anagonga mlango.

NEDDY:
(Akiamka na kupiga kelele) Ni nani huyu mapema yote hii?

MWALE:
Ni mimi, mkwe wako. Tafadhali fungua. (Sauti ya kuku wagonjwa.)

NEDDY:
Unataka nini na kuku zako?

MKE:
Neddy. Amka tu. Je! Huwezi kusikia ni ndugu yangu? (Kwa Mwale) Subiri, ndugu, anakuja.

Kufungua na kufunga mlango.

NEDDY:
(Kwa hasira) Unafanya nini na kuku zako wagonjwa nyumbani kwangu wakati huu wa asubuhi? Je! Unataka kuambukiza kuku zangu? …

MWALE:
Oh, mkwe – kwa sauti tu umejua kwamba kuku wangu ni wagonjwa?

NEDDY:
Angalia kuhara ya njano njano. Vichwa vimevimba. Huu ni ugonjwa wa Kideri.

MWALE:
Wanakufa. Tafadhali, mkwe wangu, nisaidie. Wape dawa.

NEDDY:
Nini?

MWALE:
Neddy, naomba msamaha, lakini kuku zangu zote ni wagonjwa na wanakufa.

NEDDY:
Samahani pia, mkwe wangu. Lakini siwezi kukusaidia.

MWALE:
(Kwa unyenyekevu) Kwa nini ndugu yangu, kwa nini …?

NEDDY:
Neddy: Je, umesahau jinsi ulivyonidharau mbele ya wanakijiji wote?

MWALE:
(Akipiga magoti chini na kusistiza msamaha) Nisamehe, naomba msamaha, baba. (Maelezo ya Mhariri: Mwale anamwita Neddy “baba” kwa sababu anajaribu kumpa aina zote za heshima kupata kile anachotaka.) Dada, nisaidie. Mwambie mume wako ninaomba msamaha. Je, nipige magoti?

NEDDY:
Hapana! Hapana! Usipige magoti chini. Ni kwamba siwezi tu kukusaidia.

MWALE:
(Karibu kilia) Hapana? Neddy, tafadhali nisaidie. Huu ni uwekezaji wangu pekee nilionao. Nisaidie tafadhali.

NEDDY:
Kwa nini hukufikiri hivi nilipokuwa ninatoa chanjo ya kuku?

MWALE:
Sijui ni nini kilichoniloga.

NEDDY:
(Anaheka kwa huzuni) Kwa kweli, Mheshimiwa Mwale, kama ingelikuwa tu ugonjwa wa Kideri una tiba, ningependa kukusaidia. Lakini hakuna tiba, ni chanjo tu.

MWALE:
Basi nakuomba uwape chanjo tafadhali.

NEDDY:
Umeshachelewa sana- hakuna chanjo ya kuku wagonjwa. Na sina chanjo yoyote hapa kwa sababu sina jokofu la kuiweka.

MWALE:
Wewe ni muongo. Tunajua huna jokofu ndani ya nyumba yako, lakini … Je! Uliwekaje chanjo uliyowapa kuku za watu wengine?

NEDDY:
Je unakumbuka kuwa ninawaandaa watu mapema kabla ya kuleta chanjo?

MWALE:
Ndiyo, kwanini?

NEDDY:
Ili Mimi nifanye chanjo, nawaandaa watu siku moja kabla ya siku ya chanjo. Mimi huwa naazima sanduku la baridi ambalo tunaweka mawe ya barafu kutunzia dawa ya chanjo.

MWALE:
Kwanini dawa hii ya chanjo inatunzwa sehemu ya baridi?

NEDDY:
Ikiwa utaacha dawa ya chanjo kwenye joto inaharibika. Na ndiyo maana baada ya chanjo tunatupa dawa iliyobaki.

MWALE:
Nadhani nimejifunza kwa njia ngumu. Sitirudia tena kosa hili.

NEDDY:
Ni vema kwako wewe kutorudia, mkwe wangu.

MWALE:
Kuanzia leo na kuendelea nitawapa chanjo kuku zangu kwa msimu au sio msimu.

NEDDY:
Ndivyo hivyo mkwe wangu. Fikiria ni kiasi gani cha fedha utahitaji kutumia kununua kuku wengine.

MWALE:
Uko sahihi. Nitalazimika kutumia pesa kununua kuku wengine.

NEDDY:
Sawa. Kwa kuwa unajua uzuri wa chanjo, nipe K750 (2300 Tshs) unayotaka kutumia kwenye kuku moja, na nitakupa vifaranga vitatu vya wiki sita kwa kila K250 (770 Tshs) kutoka Mikolongwe yangu. (Maelezo ya Mhariri: Uzazi huu, unajulikana pia kama Black Australorp, ni nzuri sana kwa nyama na mayai, na ina uwezo mkubwa kupambana na magonjwa kuliko uzao mwingine wa asili. Watangazaji wanaweza kubadilisha uzao wa kuku inayojulikana kuwa na faida zaidi katika eneo lao.)

MWALE:
Watoto wa hao kuku zako mseto wakubwa?

NEDDY:
Ndiyo.

MWALE:
Sina pesa kwa sasa. Nitafanya kazi fulani katika bustani za watu. Nitaacha kunywa bia mpaka nitanunua vifaranga hivi.

NEDDY:
(Akicheka) Ha! Ha! Usiue tena kuku hizi, mkwe wangu.

MWALE:
(Akitoka nje ya kipaza sauti) Mimi najua. Mimi sitawaua tena, mkwe wangu mzuri. Njoo oa dada yangu wa pili kama ishara ya tabia yako nzuri. (Maelezo ya Mhariri: Huu ni utani. Katika Malawi, watu walikuwa wakiwapa binti ya pili kuolewa ikiwa walionyesha tabia nzuri na mafanikio. Kwa siku hizi, watu wanashangaa tu na desturi hiyo ya zamani.)

NEDDY:
(Akicheka) Ha! Ha!

MSIMULIZI:
Ulikuwa unasikiliza maajabu ya Neddy mfanyakazi wa jamii ya afya ya mifugo. Kumbuka kwamba ikiwa una kuku wachache tu, wewe na marafiki zako mnaweza kushiriki gharama za kuponya kuku wako dhidi ya ugonjwa wa Kideri. Jambo lingine kukumbuka ni kwamba chanjo huwekwa daima mahali pa baridi kwenye barafu. Mara baada ya chupa kufunguliwa, huwezi kuitumia tena siku nyingine. Mwishowe, usisahau kwamba ugonjwa wa Kideri hauna tiba. Unaweza tu kuwapa chanjo kuku kabla ya kupata ugonjwa huo.

Kwa niaba ya Warsha ya Hadithi, ambao ni wazalishaji wa mpango huu, mimi ni Gladson Makowa. Hebu tukutane tena wiki ijayo kwa wakati kama huu.

Acknowledgements

Imetolewa na: Gladson Makowa, Warsha ya Hadithi, Blantyre, Malawi, mdau wa Utangazaji wa Kimataifa wa Farm Radio.
Imepitiwa na: Dilip Bhandari, mifugo, Heifer International.

Mpango huu ilifanywa na msaada wa kifedha wa Serikali ya Canada iliyotolewa kupitia Shirika la Maendeleo la Kimataifa la Canada (CIDA)

Tafsiri ya hati hii inafadhiliwa na ELANCO ANIMAL HEALTH