Utangulizi: Uhifadhi wa mazingira kwa njia za asili

Mazingira na Mabadiliko ya Tabianchi

Backgrounder

Maana ya uhifadhi wa mazingira kwa njia za asili

Kulingana na shirika la kimataifa la uhifadhi wa mazingira (IUCN), uhifadhi wa mazingira kwa njia za asili unaweza kufafanuliwa kama “hatua za kulinda, kudhibiti kwa uendelevu na kurejesha mifumo ya asili na iliyorekebishwa kwa njia zinazoshughulikia changamoto za kijamii kwa njia ipasayo, ili kutoa faida za ustawi wa binadamu na bioanuwai,”

Uhifadhi wa mazingira kwa njia za asili unalenga changamoto kuu kama vile mabadiliko ya tabianchi *, hatari ya maafa, usalama wa chakula na maji, bioanuwai * upotevu, na afya ya binadamu.

Sehemu zifuatazo hapa chini zinajadili changamoto hizi, na kuonyesha jinsi uhifadhi wa mazingira kwa njia za asili unavyoweza kuzishughulikia.

 

Uhifadhi wa mazingira kwa kwa njia za asili kwa ajili ya mabadiliko ya tabianchi

 

  • Uhifadhi wa mazingira kwa njia ya asili kwa njia ya kukabiliana na mfumo ikolojia inaweza kuchangia pakubwa katika mapambano dhidi ya mabadiliko ya tabianchi kwa kuzuia uharibifu na upotevu wa mifumo ikolojia asilia.
  • Mifumo ya asili na iliyorekebishwa inaweza kukabiliana vyema na mabadiliko ya tabianchi kwa kufanya kazi kama “njia ya asili ya kumbukuza kaboni,” kufyonza na kuondoa * utoaji wa * kaboni dioksidi (CO2). Njia za asili zenye uwezo wa kupunguza kaboni ni pamoja na bahari, udongo, na misitu, wakati mifumo iliyorekebishwa inayoweza kuchukua kaboni ni pamoja na mashamba ya kilimo yanayosimamiwa na kutumia njia bora za kilimo kama vile mzunguko wa mazao, marekebisho ya mboji na kiwango cha kidogo cha kulima.
  • Kuhifadhi, kurejesha na usimamizi endelevu wa misitu, ardhi oevu na bahari kuna umuhimu katika utendaji kazi mzuri wa mzunguko wa kaboni * na udhibiti wa mabadiliko ya tabianchi. Kwa mfano, misitu inaweza kusimamiwa kwa njia endelevu kwa kutumia mikakati mbalimbali, ikiwa ni pamoja na kuanzisha maeneo ya hifadhi na kutekeleza programu za upandaji miti.
  • Marekebisho kulingana na mfumo wa ikolojia na upunguzaji wa hatari ya maafa kulingana na mfumo wa ikolojia (tazama sehemu inayofuata hapa chini) huruhusu mifumo ikolojia kusaidia jamii zilizo hatarini, haswa zile ambazo zinategemea sana maliasili, kuendana na mabadiliko na tabianchi * na kustahimili athari mbaya za mabadiliko ya hali ya tabiannchi, ikijumuisha matukio ya hali ya hewa na majanga yanayohusiana na hali ya hewa.

 

Uhifadhi wa kwa njia za asili kwa ajili ya kupunguza hatari za maafa

 

  • Maafa makubwa ya asili katika muongo mmoja uliopita yameonyesha jukumu ambalo mazingira ya asili yanaweza kuchukua katika kupunguza hatari kutoka kwenye majanga ya asili kama vile vimbunga na tsunami*, na ikaonyesha kuwa kutumia faida za mfumo asilia wa ikolojia ni njia ya gharama nafuu ya kupunguza hatari zinazotokana na majanga. Kwa mfano, mikoko, na maeneo oevu ya pwani hupunguza hatari inayoletwa na tsunami na vyanzo vingine vya mafuriko katika pwani.
  • Mifumo ya ikolojia kama vile maeneo oevu, misitu, na mifumo ya pwani (kwa mfano, mikoko) inaweza kupunguza kukabiliwa na hatari za asili kama vile mafuriko kwa kutumika kama vizuizi vya ulinzi au bafa. Zinalinda miundombinu na mali na kusaidia urejeshaji wa haraka wa shughuli za kujipatia riziki.

 

Uhifadhi wa mazingira kwa njia za asili kwa ajili ya usalama wa chakula

 

  • Usalama wa chakula unaweza kufafanuliwa kuwa ni “upatikanaji wa chakula kinachoweza kupatikana, kikiwa salama, kinachofaa mahali ulipo, na kinachotegemeka kwa wakati na katika anga nyingi.”
  • Suluhu ya uhaba wa chakula lazima zishughulikie mahitaji mengi, kwa mfano, kurekebisha mifumo ya chakula kulingana na mabadiliko ya mazingira, kushughulikia masuala ya msingi ambayo yanaimarisha usalama wa chakula (kama vile umaskini na ubaguzi wa kijinsia), na kuhakikisha kwamba mitazamo ya mabadiliko ya hali ya tabianchi inazingatiwa katika mipango yote ya maendeleo.
  • Uhifadhi wa mazingira kwa njia za asili unaweza kushughulikia uhaba wa chakula kwa njia nyingi. Njia hizi ni pamoja na kulinda rasilimali za kijenetiki (wanyama na mimea), kudhibiti spishi za pori (hasa samaki), na kutoa maji ya umwagiliaji.
  • Kuzingatia kurejesha, kuhifadhi na kudhibiti mifumo ikolojia ili kutoa huduma za mfumo ikolojia kunaweza kusaidia kuleta usalama wa chakula wakati wa majanga ya asili, mabadiliko ya hali ya tabianchi na ukosefu wa utulivu wa kisiasa. Mifumo ya ikolojia yenye afya kama vile misitu, matuta ya mchanga, miamba na ardhioevu, hufanya kazi muhimu zinazopunguza hatari ya maafa na kuchukua jukumu muhimu katika kujenga ustahimilivu wa jamii.

 

Uhifadhi wa mazingira kwa njia za asili kwa kwa ajili ya usalama wa maji

 

  • Takriban watu bilioni nne, au asilimia 60 ya idadi ya watu ulimwenguni, wanaishi katika maeneo yenye matatizo ya kudumu ya upatikanaji wa maji. Katika maeneo haya, utumiaji wa maji yaliyo juu na chini ya ardhi ni sawa au huzidi kiwango cha maji kinachopatikana, kumaanisha kuwa hakuna maji ya ziada yanayopatikana ili kukidhi mahitaji ya siku zijazo.
  • Changamoto katika rasilimali maji inazidishwa pia na uchafuzi wa maji. Sehemu kubwa (80-90%) ya maji machafu katika nchi zinazoendelea huelekezwa moja kwa moja kwenye maji yaliyopo juu ya ardhi, na kusababisha hatari kubwa kwa afya ya binadamu.
  • Migogoro inayohusiana na maji inaweza kutatuliwa na njia za uhifadhi wa mazingira kwa njia za asili kwa kutumia “miundombinu asilia” kama vile misitu, ardhioevu na maeneo tambarare ya mafuriko. Kwa mfano, mikoko ya pwani hupunguza hatari ya mafuriko kutokana na mabadiliko ya mawimbi na majanga kama vile tsunami. Pia huongeza ubora wa maji na huduma za mfumo wa ikolojia * kwa kupunguza mmomonyoko wa ufuo wa bahari, ambao huongeza uvuvi na kupunguza uchafuzi wa maji. Lakini asili pekee haiwezi kuhakikisha usalama wa maji katika kila hali. Miundombinu iliyojengwa na asilia inahitajika ili kusimamia vyema rasilimali za maji.
  • Huduma za mfumo wa ikolojia zinazohusiana na maji ni muhimu kwa ustawi wa binadamu, kwa usalama wa chakula na nishati, kwa viwanda, na kwa uchumi, na kufanya asili kuwa msingi wa ujenzi wa usalama wa maji.

 

Uhifadhi wa mazingira kwa njia za asili kwa ajili ya Afya ya binadamu

 

  • Ubora wa mazingira asilia, na hasa zaidi mfumo ikolojia, hali ya hewa, na bayoanuwai, huathiri sana afya ya binadamu, ustawi na utengamano wa jamii.
  • Kwa mfano, misitu yenye afya na miamba ya matumbawe ni chanzo cha bidhaa za dawa na dawa nyinginezo zinazochangia pakubwa afya na ustawi wa binadamu.

 

Mbinu zinazohusiana na mfumo ikolojia ndani ya njia za uhifadhi wa mazingira kwa njia ya asili

 

Njia za asili za uhifadhi wa mazingira hujumuisha mbinu mbalimbali zinazohusiana na mfumo ikolojia, ambazo zote hushughulikia changamoto mahususi za jamii. Mbinu zilizoorodheshwa hapa chini, ambazo nyingi zilikuwepo kabla ya ujio wa dhana ya uhifadhi wa mazingira kwa njia za asili, ni njia za vitendo za kutekeleza njia za asili za kuhifadhi mazingira.

 

Marekebisho kulingana na mfumo wa ikolojia

 

  • Marekebisho kulingana na mfumo ikolojia yanaweza kufafanuliwa kuwa ni “usimamizi endelevu, uhifadhi na urejeshaji wa mifumo ikolojia, kama sehemu ya mkakati wa jumla wa urekebishaji unaozingatia manufaa mengi ya kijamii, kiuchumi na kiutamaduni kwa jamii.”
  • Marekebisho kulingana na mfumo wa ikolojia yaliundwa kama mfumo wa kushughulikia jinsi huduma za mfumo ikolojia zinaweza kupunguza athari za mabadiliko ya hali ya tabianchi kwa watu, bioanuwai na mifumo ikolojia.
  • Marekebisho kulingana na mfumo ikolojia yanaweza kutumika katika viwango mbalimbali, lakini kwa ujumla hutoa manufaa katika eneo husika. Miradi yenye kuzingatia ikolojia kwa kawaida hujumuisha ushirikishwaji thabiti wa jamii ili kuongeza ufahamu kuhusu kusimamia maliasili na kuongeza usaidizi kutoka kwa watu wa eneo husika kwa shughuli zinazorejesha na kudhibiti mifumo ikolojia kwa njia endelevu.

Mifano ya urekebishaji kulingana na mfumo ikolojia ni pamoja na:

  • Kulinda na kurejesha ardhi oevu kama vile vijito na maziwa ambayo hufanya kama sponji, kupeleka maji chini ya ardhi na kuweka upya maji ya ardhini, kuyahifadhi kwa nyakati za ukame.
  • Kupanda miti kama vile mitarakwa ya Mediterania kama njia za asili za kuzuia moto. Spishi hizi hustahimili moto wa mwituni kwa sababu majani yao huhifadhi kiwango cha juu cha maji hata kwenye joto kali, na huunda mazingira yenye unyevunyevu chini ya shina.
  • Kurejesha mikoko na miamba ya matumbawe, ambayo husababisha mawimbi ya bahari kutawanyika kabla ya kugonga ufuo, na hivyo kupunguza urefu na nguvu zake. Hii inapunguza uwezekano wa mawimbi kufika ardhini nnchi kavu na hatari ya mazao kuharibiwa na chumvi.

 

Urejeshaji wa mazingira ya misitu

 

  • Urejeshaji wa mazingira ya misitu ni mchakato unaoendelea wa kurejesha utendaji kazi wa ikolojia na kuimarisha ustawi wa binadamu katika mandhari yote ya misitu iliyoharibiwa. Urejeshaji wa mazingira ya misitu haiishii tu katika upandaji miti, bali hurejesha mandhari nzima ili kukidhi mahitaji ya sasa na ya baadaye na kutoa manufaa mengi na matumizi ya ardhi kwa kipindi cha muda fulani.
  • Urejeshaji wa mazingira ya misitu haulengi katika kurejesha mandhari katika hali iliyokuwapo awali. Badala yake, inalenga katika kuboresha huduma za mfumo ikolojia, kwa mfano, kuimarisha uhusiano kati ya maeneo yaliyohifadhiwa, kulinda rasilimali za maji na udongo, na kuimarisha maadili ya kitamaduni.

 

Miundombinu ya kijani

 

  • Mifumo ya ikolojia hufanya kazi kadhaa sawa na miundombinu mingine ya kawaida kijivu * kama vile kukusanya, kusafisha, kuhifadhi na kusambaza maji. Kwa mfano, “miundombinu ya kijani kibichi” kama vile misitu ya miinuko, chemichemi, maziwa, na maeneo oevu huhifadhi maji; maeneo oevu huchuja maji; mito hutoa usafiri; maeneo ya mafuriko na ardhi oevu hupunguza vilele vya mafuriko katika miji iliyo maeneo ya chini ya mito; na mikoko, miamba ya matumbawe, na visiwa vizuizi hulinda pwani dhidi ya dhoruba na mafuriko.

 

Kupunguza hatari ya maafa kulingana na mfumo wa ikolojia

 

  • Kupunguza hatari ya Maafa kwa msingi wa Mfumo wa ikolojia ni mbinu inayotumia uwezo wa mifumo ikolojia kudhibiti michakato (kama vile hali ya hewa, ubora wa hewa na uhifadhi wa kaboni) ili kupunguza, kuzuia au kuepusha majanga.
  • Mbinu za kupunguza hatari ya maafa kulingana na mfumo wa ikolojia zinalenga hasa kupunguza athari za matukio ya hatari kwa kuimarisha uwezo wa watu wa kudhibiti na kurudi katika hali ya kawaida kutokana na athari za majanga.
  • Kupunguza hatari ya maafa inahusishwa kwa karibu na mbinu zinazotegemea mfumo-ikolojia wa kurekebisha na kukabiliana na hali hiyo, lakini ni mahususi zaidi, ikilenga matukio fulani ya hatari (k.m., tsunami, matetemeko ya ardhi, mafuriko na vimbunga), na mara nyingi hufanya kazi ndani ya muda na maeneo mahususi.
  • Mbinu za kupunguza hatari ya maafa kulingana na mfumo wa ikolojia inaweza kutekelezwa katika viwango vyote. Mifano ni pamoja na kurejesha maeneo yenye tindiga ili kulinda maeneo ya karibu kutokana na mafuriko kutokana na vimbunga, na kupanda miti au aina nyingine za mimea kwenye ardhi ambayo inaweza kuathiriwa na maporomoko ya ardhi, ambayo huongeza uwezo wa kuunganisha udongo na kupunguza mmomonyoko wa udongo kutokana na kutiririka kwa maji.

 

Vigezo vya uhifadhi wa mazingira kwa njia za asili

 

Vigezo vinane vya uhifadhi wa mazingira kwa njia za asili vilivyoorodheshwa hapa chini vinashughulikia mambo mbalimbali ambayo yameundwa ili kuongoza utendaji na utekelezaji wa uhifadhi wa mazingira kwa njia za asili, na kutoa hatua rahisi kufuata za jinsi ya kutekeleza vyema njia za uhifadhi zinazotokana na Mazingira. Ikumbukwe kwamba kila kigezo kinajumuisha viashiria vitatu hadi vitano vya kupima nguvu na ufanisi wa ufumbuzi.

Vigezo na viashirio hufanya kazi kama zana rahisi lakini thabiti inayowawezesha watendaji kutafsiri dhana ya uhifadhi wa mazingira kwa njia za asili katika shughuli zinazolengwa, kuimarisha mbinu bora, kushughulikia mapungufu katika utekelezaji, na kuwezesha njia hizo kupatana na kanuni za uhifadhi wa mazingira kwa njia za asili zinazokubalika kimataifa.

Watumiaji wanaweza kukokotoa jinsi njia yao ya uhifadhi inavyolingana na vigezo nane na kukadiria iwapo ulinganifu ni thabiti, ni wakutosha, dhaifu au hautoshi.

 

Kigezo cha 1: Njia za asili za uhifadhi wa mazingira zinashughulikia kwa ufanisi changamoto za kijamii

 

Njia za asili za uhifadhi wa mazingira zinapaswa kuundwa ili kushughulikia kwa kina na kwa ufanisi changamoto mahususi za kijamii.

Hizi zinaweza kujumuisha:

  • kuzoea na kukabiliana na * mabadiliko ya tabianchi,
  • kupunguza hatari za maafa, na
  • kushughulikia masuala kama vile uharibifu wa mfumo ikolojia, upotevu wa viumbe hai, afya ya binadamu, maendeleo ya kijamii na kiuchumi, usalama wa chakula na usalama wa maji.

Changamoto moja au zaidi za jamii inaweza kuwa mahali pa kuanza kutekeleza njia za asili za uhifadhi wa mazingira, lakini kipaumbele cha utekelezaji wa njia hizi ni kutoa aina nyingi za manufaa na kushughulikia changamoto kadhaa.

 

Kigezo cha 2: Muundo wa njia za asili za uhifadhi wa mazingira unafanywa kulingana na ukubwa wa eneo

 

Njia za asili zauhifadhi wa mazingira hutilia maanani ukubwa wa kijiografia na nyanja za kiuchumi, ikolojia, na masuala ya kijamii yanayohusiana na ardhi au mandhari ya bahari, kuelewa kuwa eneo lengwa la uhifadhi kwa njia za asili ni sehemu ya mifumo mikubwa ya kiikolojia, kiuchumi na kijamii. Ingawa njia za uhifadhi zinazofanywa na mtu binafsi zinaweza kulenga maeneo mahususi ya eneo fulani, nguvu, utekelezaji wake, na mwitikio wa njia hiyo ya uhifadhi unapaswa kuzingatia mifumo hii mipana.

 

Kigezo cha 3: Njia za asili za uhifadhi wa mazingira husababisha faida kamili kwa bioanuwai na uadilifu wa mfumo ikolojia

 

Upungufu wa sasa wa bayoanuwai sio tu unatishia spishi adimu zinazotoweka, lakini pia huharibu kwa kiasi kikubwa mifumo mingi ya ikolojia, kudhoofisha afya ya sayari na ustawi mpana wa binadamu. Njia za asili za uhifadhi wa mazingira zinapaswa kuboresha uanuwai wa kibayolojia na uadilifu wa ikolojia.

 

Kigezo cha 4: Njia za asili za uhifadhi wa mazingira zinaweza kutumika kiuchumi

 

Siri ya mafanikio ya njia yoyote ya asili za uhifadhi wa mazingira ni pamoja na kurudisha faida ya uwekezaji, ufanisi wa njia yenyewe, na usawa katika usambazaji wa faida na gharama. Kigezo hiki kinaangazia haja ya kuhakikisha kwamba uimara wa kiuchumi na uendelevu unazingatiwa katika hatua ya usanifu na wakati wote wa ufuatiliaji na utekelezaji. Vinginevyo, utekelezaji hauwezi kudumu katika kipindi cha maisha ya mradi.

 

Kigezo cha 5: Njia za asili za uhifadhi wa mazingira ni jumuishi, wazi na huwezesha usimamizi

 

Kigezo hiki kinahitaji kwamba njia za asili za uhifadhi wa mazingira zitambue, zihusishe, na zijibu maswala ya wadau mbalimbali, hasa washika dau *. Mipango ya utawala bora ni pamoja na kufuata sheria na kanuni, na ushirikishwaji imara na uwezeshaji wa jumuiya za mitaa. Haipunguzi tu hatari ya uendelevu wa njia za asili za uhifadhi wa mazingira, lakini pia kuboresha kukubalika katika jamii zilizoathiriwa. Njia za asili za uhifadhi wa mazingira zinapaswa kutambua na kuheshimu tamaduni zilizokuwepo hapo awali na matumizi ya ardhi wakati wowote inapowezekana, katika kipindi chote na zaidi ya mzunguko wa maisha wa shughuli zilizopangwa.

 

Kigezo cha 6: Njia za asili za uhifadhi wa mazingira zinasawazisha usawa kati ya mafanikio ya lengo/malengo yake ya msingi na kuendelea kutoa faida nyingi

 

Katika kusimamia ardhi na maliasili, mabadilishano ya kibiashara hayaepukiki. Mifumo ya ikolojia hutoa utajiri wa faida tofauti, na sio kila mtu anayethamini kila moja yao kwa njia sawa. Njia za asili za uhifadhi wa mazingira lazima zitambue mabadiliko haya na kufuata mchakato wa haki, uwazi na jumuishi ili kusawazisha na kudhibiti kwa muda na nafasi ya kijiografia.

 

Kigezo cha 7: Njia za asili za uhifadhi wa mazingira hudhibitiwa kulingana na ushahidi

 

Mifumo ikolojia inaweza kujibu kwa njia zinazohitajika kwa njia za asili za uhifadhi wa mazingira. Hata hivyo, shughuli za uhifadhi wa mazingira kwa njia za asili pia zinaweza kuunda matokeo yasiyotarajiwa, yasiyotegemewa na yasiyofaa. Kwa hivyo, mchakato wa utekelezaji unahitaji kuwezesha usimamizi unaofaa * kama jibu la kutokuwa na uhakika.

 

Kigezo cha 8: Njia za asili za uhifadhi wa mazingira ni endelevu na zimejumuishwa ndani ya muktadha unaofaa wa mamlaka

 

Njia za asili za uhifadhi wa mazingira zimeundwa na kusimamiwa kwa kuzingatia uendelevu wa muda mrefu. Pia huzingatia, kufanya kazi, na kuoanisha mifumo ya sera za kisekta, kitaifa na nyinginezo. Mikakati ya kujumuisha njia za asili za uhifadhi wa mazingira inawafikia watu binafsi (k.m., umma kwa ujumla na wasomi), taasisi (k.m., serikali, biashara, na mashirika yasiyo ya kiserikali), na mitandao ya kimataifa (k.m., inayohusiana na Malengo ya Maendeleo Endelevu, na Mkataba wa Paris).

 

Ufafanuzi

 

Bioanuwai (Biodiversity): Anuwai na utofauti wa viumbe hai duniani, unaojumuisha viwango vitatu: uanuwai wa viumbe, uanuwai ndani ya spishi, na utofauti wa mifumo ikolojia.

Ekolojia (Ecosystem): Seti ya viumbe hai wanaoishi ndani ya mazingira maalum na kuhusiana na kwa mazingira haya.

Gesi chafu (Greenhouse gas): Dunia hupokea nishati kutoka kwenye jua katika umbo la miale ya jua (mwanga) na kutoa baadhi ya nishati hii kwenye angahewa kama miale ya joto. Gesi za angahewa kama vile kaboni dioksidi, methane, na nyinginezo hunasa nishati inayotoka angani, na hivyo kuinua halijoto ya angahewa.

Hatari (Hazard): Uwezo wa tukio la asili au shughuli za binadamu kusababisha upotezaji wa maisha, majeraha, au athari zingine za kiafya, pamoja na uharibifu na hasara ya mali, miundombinu, maisha, mifumo ikolojia na rasilimali za mazingira.

Hatari au majanga yanayohusiana na hali ya hewa (Climate-related risks or hazards): Athari zinazoweza kutokea kwa binadamu au ikolojia kutokana na mabadiliko ya tabianchi. Hatari ni matokeo ya mwingiliano wa majanga, mazingira hatarishi na kuwa kwenye mazingira hayo.

Huduma za mfumo ikolojia (Ecosystem services): Manufaa ambayo watu hupata kutoka kwa mifumo ikolojia. Huduma za mfumo wa ikolojia zimegawanywa katika makundi manne: huduma za utoaji (chakula, malighafi, maji safi, madawa); kudhibiti huduma (kudhibiti hali ya hewa na ubora wa hewa, kudhibiti uhifadhi wa kaboni); huduma za usaidizi (sio zenye manufaa moja kwa moja kwa binadamu lakini ni muhimu kwa utendaji kazi wa mfumo ikolojia na hivyo kuwajibika kwa njia isiyo ya moja kwa moja kwa huduma zingine zote, ikijumuisha uundaji wa udongo na ukuaji wa mimea); na huduma za kitamaduni (burudani, utalii, maeneo matakatifu).

Kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi (Climate change adaptation): Matendo yanayofanya watu, mifumo ikolojia na miundombinu kutokuwa hatarini zaidi kwa athari za mabadiliko ya tabianchi.

Kuwa hatarini kwa mabadiliko ya tabianchi (Climate vulnerability): Inajumuisha vipengele mbalimbali, ikiwa ni pamoja na unyeti au urahisi wa madhara yanayosababishwa na mabadiliko ya hali ya tabianchi, na ukosefu wa uwezo wa kukabiliana na kuendana na madhara hayo.

Mabadiliko ya hali ya tabianchi (Climate change): Mabadiliko ya hali ya hewa ya wastani—kama vile joto na mvua—katika eneo kwa muda mrefu.

Miundombinu ya kijivu (Green infrastructure): Miundombinu iliyobuniwa na binadamu kwa rasilimali za maji. Inajumuisha mitambo ya kutibu maji na maji machafu, mabomba, mabwawa, kuta za bahari na hifadhi.

Mzunguko wa kaboni (carbon cycle): Mchakato ambapo kaboni huhamishwa kati ya bahari, anga, udongo, na viumbe hai.

Njia za kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi (Climate change mitigation): Hatua zinazopunguza utoaji wa gesi chafuzi kwenye angahewa.

Uhusiano kati ya mabadiliko ya hali ya hewa na bayoanuwai (Links between climate change and biodiversity): Mabadiliko ya tabianchi yamesababisha uharibifu mkubwa, na hasara zinazozidi kutoweza kutenguliwa, kwa ardhi, maji safi, pwani na mifumo ikolojia ya bahari. Hii mara nyingi hujulikana kama shida mbili za hali ya hewa na bayoanuwai.

Usimamizi wa uwezo wa kukabiliana (Adaptive Management): Mbinu iliyopangwa ya kufanya maamuzi ambayo inasisitiza uwajibikaji na uwazi. Usimamizi wa uwezo wa kukabiliana ni muhimu hasa kunapokuwa na kutokuwa na uhakika kuhusu mkakati unaofaa zaidi wa kusimamia maliasili.

Utengaji wa kaboni (carbon sequestration): Uhifadhi wa muda mrefu wa kaboni katika mimea, udongo, miundo ya kijiolojia, na bahari. Uondoaji wa kaboni unaweza kutokea kwa njia ya asili na kama matokeo ya shughuli za kibinadamu. Ni njia mojawapo ya kupunguza kiasi cha kaboni dioksidi katika angahewa kwa lengo la kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi duniani.

Uwezo wa Kukabiliana (Adaptive capacity): Katika muktadha wa tathmini ya hatari ya hali ya hewa, hii inarejelea uwezo wa jamii kujiandaa na kukabiliana na athari za sasa na zijazo za mabadiliko ya tabianchi.

Wamiliki wa haki (Right holders): Watu binafsi au vikundi vinavyopata manufaa kwa kutumia rasilimali, wanajali kuhusu suala fulani, na/au wana haki za kisheria au kihalisi za kusimamia au kufanya maamuzi kuhusu jambo fulani.

 

Ninaweza kupata wapi taarifa zaidi juu ya mada hii?

 

  1. Africa Center for Strategic Studies, 2022. African Biodiversity Loss Raises Risk to Human Security. https://africacenter.org/spotlight/african-biodiversity-loss-risk-human-security/#:~:text=Africa’s%20rich%20biodiversity%20is%20under,are%20at%20risk%20of%20extinction
  2. Akana, D., 2019. Webinar: Communicating the impacts of climate change on Food and Agriculture. Earth Journalism Network. https://earthjournalism.net/resources/webinar-communicating-the-impacts-of-climate-change-on-food-and-agriculture
  3. Angula, M. N. et al, 2021. Strengthening Gender Responsiveness of the Green Climate Fund Ecosystem-Based Adaptation Programme in Namibia. Sustainability, 13 (18). https://doi.org/10.3390/su131810162
  4. Cohen-Shacham, E., et al, (eds.), 2016. Nature-based Solutions to address global societal challenges. Gland, Switzerland: IUCN. xiii + 97pp. https://portals.iucn.org/library/sites/library/files/documents/2016-036.pdf
  5. Conservation of Biological Diversity 5, 2020. Global Biodiversity Outlook. https://www.cbd.int/gbo/gbo5/publication/gbo-5-en.pdf Summary for Policymakers: https://www.cbd.int/gbo/gbo5/publication/gbo-5-en.pdf
  6. Convention on Biological Diversity (CBD), 2010. X/33 Biodiversity and climate change, Decision Adopted by the Conference of the Parties to the Convention on Biological Diversity at its Tenth Meeting; UNEP/CBD/COP/DEC/x/33; 29 October 2010. Nagoya, Japan: Secretariat of Convention on Biological Diversity. https://www.cbd.int/decision/cop/?id=12299
  7. Earth Journalism Network, 2016. Climate change and agriculture. Earth Journalism Network. https://earthjournalism.net/resources/climate-change-and-agriculture
  8. Earth Journalism Network, 2016. Intergovernmental Panel on climate change. Earth Journalism Network. https://earthjournalism.net/resources/intergovernmental-panel-on-climate-change
  9. Earth Journalism Network, 2016. Introduction to climate change. Earth Journalism Network. https://earthjournalism.net/resources/introduction-to-climate-change
  10. European Commission, 2015. Biodiversity and climate change. Biodiversity and Climate Change – Environment – European Commission. https://ec.europa.eu/environment/nature/climatechange/index_en.htm#:~:text=Healthy%20ecosystems%20must%20lie%20at,are%20major%20stores%20of%20carbon
  11. Global Affairs Canada, 2023. Government of Canada. GAC. https://www.international.gc.ca/world-monde/funding-financement/partnering-climate-partenariats-climat.aspx?lang=eng
  12. IUCN, 2020. Global Standard for Nature-based Solutions. A user-friendly framework for the verification, design and scaling up of NbS. First edition. Gland, Switzerland: IUCN. Downloadable at https://portals.iucn.org/library/node/49070
  13. IUCN, 2020. Guidance for using the IUCN Global Standard for Nature-based Solutions. A user-friendly framework for the verification, design and scaling up of Nature-based Solutions. First edition. Gland, Switzerland: IUCN. Downloadable at https://portals.iucn.org/library/node/49071
  14. IUCN, undated. Nature-based Solutions. https://www.iucn.org/our-work/nature-based-solutions
  15. Nature Based Conservancy, 2021. Three things to know about nature-based solutions for Agriculture. The Nature Conservancy. https://www.nature.org/en-us/what-we-do/our-insights/perspectives/three-things-nature-based-solutions-agriculture/
  16. Nature Based Solutions Initiative, 2022. Nature-based solutions to climate change. https://nbsguidelines.info/
  17. Pausata, F. S., R. et al, 2020. The Greening of the Sahara: Past Changes and Future Implications. One Earth, Vol. 2(3), p 235-250. https://www.sciencedirect.com/science/article/pii/S2590332220301007
  18. Renaud, F. G., Sudmeier-Rieux, K., and Estrella, M., 2013. The role of ecosystems in disaster risk reduction. United Nations University Press. Downloadable at https://www.unep.org/resources/publication/role-ecosystems-disaster-risk-reduction
  19. Secretariat of the Convention on Biological Diversity, 2008. Biodiversity and Agriculture: Safeguarding Biodiversity and Securing Food for the World. Montreal, 56 pages. https://www.fao.org/fileadmin/templates/soilbiodiversity/Downloadable_files/P020080603430792943555.pdf
  20. Shanahan, M., 2016. Seven things every journalist should know about climate change. Earth Journalism Network. https://earthjournalism.net/resources/seven-things-every-journalist-should-know-about-climate-change
  21. UNESCO, 2013. Climate change in Africa: a guidebook for journalists, 91 pages. Downloadable at https://www.iied.org/g03710
  22. United Nations Environment Programme, 2022. Nature-based Solutions: Opportunities and Challenges for Scaling Up. Nairobi. Downloadable at https://wedocs.unep.org/handle/20.500.11822/40783;jsessionid=15415E686538DB702C504997FC8905D2
  23. Vignola R et al, 2015. Ecosystem-based adaptation for smallholder farmers: Definitions, opportunities and constraints. Agriculture, Ecosystems, & Environment, Vol. 211, p. 126-132. https://www.sciencedirect.com/science/article/pii/S0167880915002157
  24. World Meteorology Organization, 2022. State of the Climate in Africa 2021. https://library.wmo.int/doc_num.php?explnum_id=10421

Acknowledgements

Lora Onion, mtaalamu wa mazingira wa kujitolea, Farm Radio International

Imehaririwa na: Sareme Gebre, mtaalamu wa masuala ya Uhifadhi wa Mazingira kwa njia za asili kutoka Farm Radio International.