Ujumbe kwa mtangazaji
Ukosefu wa usawa wa jinsia unaendelea kuzua matatizo makuu barani Afrika na kwingineko. Wanawake wanapokosa udhibiti wa raslimali kama vile ardhi, wanashindwa kufanya maamuzi ambayo huboresha mapato ya jamii. Bila udhibiti wa mapato ya jamii, kwa mfano kwa kulima mazao ya biashara, wanawake huchangia muda wao na nguvu kazi yao kwa kudumisha aushi tu, na wanaathirika zaidi na umaskini kuliko wanaume. Na pia mila za kitamaduni, ambazo huenda zikawakataza wanawake kushiriki katika harakati kama vile kupanda miti, hupunguza uwezo wao wa kuhifadhi na kutetea uendelevu wa kimazingira.
Haki za ardhi na mali, ndizo hasa zinachukua nafasi muhimu katika karibu kila jukwaa la umma linaloandaliwa na maofisa wa serikali au mashirika ya kiraia, na wanawake wanachukua jukumu la uongozi katika vita dhidi ya ubaguzi. Usawa wa jinsia ni haki ya kibinadamu na iko katika kiini cha kufikia Malengo ya Maendeleo ya Milenia. Unakuwa wa lazima kabla kuangamiza njaa, umaskini na magonjwa. Usawa wa jinsia unamaanisha usawa katika viwango vyote vya elimu na maeneo yote ya kazi, udhibiti sawa wa raslimali, na uwakilishi sawa katika maisha ya umma na kisiasa.
Makala haya yanaangazia uondoaji wa tofauti za kijinsia katika sekta zote za maisha kwa sababu hatuwezi kufurahia maendeleo bila usalama, hatuwezi kufurahia usalama bila maendeleo na hatuwezi kufurahia moja ya hizo bila heshima kwa haki za binadamu. Njia moja ya kutayarisha makala haya kwa hadhira ya eneo lako ni kumhoji mtu mmoja kutoka jamii yako au hata eneo lako aliye mkereketwa wa usawa wa jinsia.
Makala haya yana misingi ya mahojiano halisi. Unaweza kutumia makala haya kama motisha kutafiti na kuandika makala juu ya mada sawia katika eneo lako. Ama unaweza kuchagua kutoa makala haya katika kituo chako ukitumia waigizaji wa sauti kuwakilisha wazungumzaji. Endapo utafanya hivyo, tafadhali hakikisha unaiambia hadhira yako mwanzoni mwa kipindi kuwa sauti hizo ni za waigizaji na wala si wazungumzaji asilia walioshiriki katika mahojiano.
Script
Wimbo wa kutambulisha kwa sekundi kumi halafu uondoe taratibuNiliishi kwa raha na mme wangu kwa takriban miaka kumi na minane ndipo mkasa ukatokea. Mme wangu Daniel Omollo alifariki kutokana na malaria. Ghafla, dunia yote ikaporomoka, na hata raha yangu ya kuwa mpendwa wa wakwe zangu. Kila mmoja aligeuka kuwa adui. Kuanzia ndugu zake mme wangu hadi wazazi wake, wote walidai sehemu ya mali ile.
(Sita) Leo tumejifunza mambo mengi: aina ya haki za wanawake, jinsi mila baguzi zinaweza kuondolewa, na vile wanaharakati katika Wilaya ya Siaya wanavyoinua uelewaji. Tumesikia kuwa hata waliodhulumiwa wanaweza kupata matumaini tena. (Sita) Msikilizaji, hapa ndipo tunafika mwisho wa kipindi chetu cha leo. Leo tumeangazia wanawake na haki ya kumiliki mali kama njia ya kufikia Malengo ya Maendeleo ya Milenia ya kuinua usawa wa jinsia na kuwawezesha wanawake. Tunatumai kwamba umejifunza jambo fulani. Hadi tutakapokutana tena, kwaheri.
Wimbo wa kitambulisho kwa sekunde 10 kisha ufifie na kumalizikaAcknowledgements
Yamechangiwa na: Rachael Adipo, Ugunja Community Resource Centre, Kenya.
Yamehaririwa na: Carole Houlihan, International Development Consultant, Canada
Information sources
Hakuna utaratibu mwafaka kuhusu aina za umiliki wa ardhi kwa wanawake. Hati miliki zilizosajiliwa huenda zikafaa katika miktatha kadhaa huku hati za kitamaduni zikifaa katika mingine. Utoaji wa uhakika wa kisheria na ufikiaji sawia wa ardhi na mali kwa wanawake unahitaji amali siyo kwa serikali tu, mbali pia kwa sekta zote za jamii, ikiwemo sekta ya kibinafsi, mashirika yasiyo ya kiserikali, jamii na utawala wa mitaani, na pia mashirika wenza na vyombo vya jamii ya kimataifa.
Wanawake wanahitaji sauti sawa katika maamuzi yanayoathiri maisha yao – kuanzia ndani ya familia hadi viwango vya juu zaidi vya serikali. Hii ni nguzo muhimu katika uwezeshaji wa wanawake. Kwa muda mrefu, wanaume wametawala ufanyaji wa maamuzi katika ngazi za juu. Hatua za kuzuia na zile za kurekebisha udhoofishaji unaotarajiwa dhidi ya haki za wanawake kuhusu ardhi na mali kwa sababu ya mikondo ya sasa ya sera za kiuchumi lazima zitayarishwe.
Marejeleo
Kofi Annan. Africa’s Green Revolution (A call to action).UN press release, July 6, 2004. http://www.un.org/News/Press/docs/2004/sgsm9405.doc.htm
UN Millennium Development Goals. United Nations Environment Program. United Nations Development Goals.
Phillip Onyango. Land and Property Rights. Ugunja Community Resource Centre, 2005.