Kidole kimoja hakiui chawa

Uzalishaji wa mazao

Ujumbe kwa mtangazaji

Ugonjwa wa Batobato (CMD) ni moja kati ya magonjwa muhimu sana ya mihogo nchini Tanzania. Batobato (CMD) inapelekea kupungua kwa ukubwa wa jani la muhogo na kuharibu umbile la jani la muhogo (majani ya mihogo hujikunja kunja). Mmea wa muhogo ulio shambuliwa na batobato unabadilika rangi na kuwa na michirizi ya njano na kijani. Mmea wa muhogo ulioshambuliwa na ugonjwa wa batobato unazalisha mihogo kidogo na hafifu sana sana kama mmea ulishambuliwa mapemwa mwanzoni mwa msimu.

Ugonjwa huu unasababishwa na Virusi na unaambukizwa kutoka mmea ulioathirika kwenda mmea wenye afya na mdudu aitwaye Nzi mweupe. Pia unasambazwa sana kwa kuotesha pandikizi za mihogo kutoka kwenye mmea ulioathirika. Hakuna dawa ya kuuwa ugonjwa huu.

Jinsi ya kukabiliana na Batobato CMD:

  • Panda vipando visivyo na daliliza maambukizi.
  • Chagua vipando kutoka katika shamba lisilo na maabukizi ya magonjwa.
  • Ng’oa na teketeza kwa kuzika mihogo yenye dalili za ugonjwa wa Batobato CMD pindi tu unapoona dalili.
  • Panda mbegu zenye ukinzani na magonjwa. Tanzania, mbegu kinzani ni pamoja na Chereko, Mkuranga 1, Kiroba, Kipusa na Kizimbani.
  • Fanya kilimo mzunguko kuepuka mazalia ya ugonjwa.

Igizo hili litamuangalia mkulima Hadija ambaye mihogo yake imeathirika na Batobato mwaka uliopita. Muhogo ikiwa kama chakula kikuu, hakuwa na chakula cha kutosha kulisha familia yake. Kwa msimu uliofuatia aliamua kulima mbali na mashamba ya jirani zake kuzuia kusambaa kwa ugonjwa wa batobato. Mtu mmoja aitwaye Semvua alipoamua kuanzisha shamba jirani yake, balaa likarudi tena. Ni katika ugomvi huu ndipo Semvua alijua kuwa kuna engi ya kukingana nayo ukiachilia ugonjwa wa Batobato.

Unaweza kutumia igizo hili katika vipindi vyako vya kila siku.

Unaweza pia kutumia Muongozo huu kama chanzo cha utafiti au kama kishawishi kitakachokupa msukumo kuandaa kipindi chako juu ya magonjwa ya mihogo au mada zinazofanana na hizi nchini kwako.

Ongea na wakulima na wataalamu wenye uzoefu na upandaji wa zao la muhogo au watu wenye uzoefu na zao la mihogo.

Utahitaji kuwauliza wakulima:

  • Unaufahamu ungonjwa wa Batobato?
  • Unafahamu namna ugonjwa unavoenezwa?
  • Unafahamu namna unazoweza kutumia kuzuia ungonjwa usienee shambani kwako?

Na wataalamu unaweza kuwaulizas:

  • Wakulima wanaweza kupata wapi mbegu/mapando ya mihogo salama ambayo hayaja shambuliwa na magonjwa?
  • Muda uliokadiriwa kurusha muongozo ni dakika 20 ikiwemo utangulizi na muziki wa kumalizia.

Muda uliokadiriwa kurusha muongozo ni dakika 20 ikiwemo utangulizi na muziki wa kumalizia.

Script

WASHIRIKI

HADIJA:
Mwanamke wa miaka 40 na watoto wanne. Mtoto mkubwa ni wakiume mwenye umri wa miaka 15. Ni mwanamke mjane na Mkulima wa mihogo, analima Mihogo hasa hasa kujipatia chakula na kuuza kidogo kinachobaki kwaajili ya kupata kipato kidogo kwa mahitaji mengine ya familia, kipato kikubwa anajipatia kwa kufanya kazi za vibarua kijiji mwake na vijiji vya ng’ambo.
REHEMA:
Mtoto wa kiume wa Hadija mwenye miaka 15 ambae yupo shule ya sekondari umbali wa kutembea kutoka nyumbani. Yeye na wadogo zake humsaidia Mama yao katika shughuli za shamba wanapotoka shule.
MTULIA:
Mwanaume wa miaka 45 mkulima ambae anaonekana kufahamu vizuri changamoto za kilimo kijijini. Ni mwema na rahisi kujumuika naye, yu tayari kutaarifu wengine juu ya alichonacho kwenye bustani yake na kufundisha wengine juu ya uelewa wake wa changamoto za kilimo. Ameoa.
SEMVUA:
Mwanaume wa mika 42 kutoka kijiji hicho hicho. Ameoa.

SEHEMU YA KWANZA

FX:
MANDHALI YA MCHANA KIJIJINI.
NDEGE WANAIMBA, SAUTI ZA MBUZI NA MBWA ANABWEKA TOKA MBALI.
CHIMWENE AMEKUJA TU KUTOKA SHULENI. ANACHUKUA CHAKULA CHAKE TOKA JIKONI AMBAPO MAMA YAKE ALIMUACHIA.
REHEMA:
(ANAKARIBIA) Mama hiki chakula cha mihogo ni kichungu. Unategemea mimi nitakulaje?
HADIJA:
Samahani/pole mwanangu, ila hicho ndicho kila mtu amekula humu ndani leo.
REHEMA:
Kwanini hujaandaa chakula kitamu cha mihogo tunachokula kila siku?
HADIJA:
Ina maana hujui tumevuna mihogo mitamu ya mwisho jana?
REHEMA:
Mama, unamaanisha?
HADIJA:
Usifanye hujui tulikua na mazao machache ya kuvuna mwaka huu. Je ni habari kwako ya kuwa tuling’oa mihogo mingi sababu ya ugonjwa wa batobato kwenye mihogo?
REHEMA:
Najua hilo, ila mama sikujua kama tutaishiwa mapema.
HADIJA:
Vizuri, tumeishiwa. Kama akiba ya mwisho nilijaribu kumwaga maji ya kupikia ili isiwe mikali, na hivyo ndiyo tumepata. Vyovyote vile, sio mikali kama unavyosema, Rehema.
REHEMA:
Lakini mama, leo darasani tumejifunza kuwa hii mihogo mikali hatutakiwi kuila sababu ni sumu.
HADIJA:
(AMEKASIRIKA) Rehema, huna njaa, si ndio eeh?
REHEMA:
Hakika, nina njaa mama.
HADIJA:
Basi usifanye kama mtoto mdogo. Nenda kale chakula chako.
REHEMA:
(KWA HUZUNI) Sili hii sumu.
HADIJA:
Ni wazi hauna njaa.
REHEMA:
Naenda kwa mjomba Magombela. Yeye bado ana mihogo mitamu kwenye bustani yake. Ataweza kutupa vipando vichache.
HADIJA:
Hapana hapa hapanaa … Sitakuruhusu uende kuomba kwa ndugu zangu. Naweza kuwa mjane, lakini nimeweza kujitunza mimi mwenyewe na watoto wangu tangu baba yenu afariki miaka sita iliyopita.
MTULIA:
(ANAKARIBIA) Hadija, napita nikielekea nyumbani kutoka shamba, nikaona nijue mnaendeleaje wewe na familia.
HADIJA:
Asante, Bwana Mtulia. Sisi wazima kabisa. Mnaendeleaje wewe na familia?
MTULIA:
Mungu ametujaalia na afya njema.
REHEMA:
Mama hasemi ukweli…
HADIJA:
Shiiiiii, Rehema, nyamaza!
MTULIA:
Hapana, mwache aongee, Hadija. Miaka 15, Rehema ni mkubwa kuweza kuongea mawazo yake. Ni kitu gani, Rehema?
REHEMA:
Tunaweza kuwa wazima kiafya, Bwana Mtulia, lakini hii nyumba haina chakula. Nimerudi kutoka shule nikakuta hii mihogo michungu ndio chakula na napata shida hata kumeza.
MTULIA:
Usipate shida. Nenda ukachukue mihogo mitamu kwenye bustani yangu karibu na msitu.
REHEMA:
(AKIACHA MIC) Asante, Bwana Matulia. Naenda sasahivi.
MTULIA:
(AKITA) Unaweza chukua yakutosha siku mbili.
HADIJA:
Sijui nikushuru vipi kwa hili, Bwana Mtulia. Mungu akubariki.
MTULIA:
Usijali si kitu, Hadija. Sasa ni lazima nianze kwenda.
HADIJA:
Salamu zangu kwa mkeo.
MTULIA:
Zimefika.

SEHEMU YA PILI

FX:
MAZINGIRA YA SHAMBA NA SAUTI ZA MSITUNI. HADIJA ANACHIMBA KUTENGENEZA MIFEREJI KWENYE SHAMBA LAO JIPYA LA MIHOGO.
SEMVUA:
(ANAKARIBIA) Habari za asubuhi, Hadija.
HADIJA:
Habari za asubuhi, Bwana Semvua. Nyumbani wazima, wewe, mkeo na watoto?
SEMVUA:
Sisi wote ni wazima. Vipi wewe na nyumbani kwako?
HADIJA:
Wote ni wazima wa afya.
SEMVUA:
Naona unaandaa shamba peke yako. Kwanini? Mara zote huwa na watoto wako.
HADIJA:
Wata ungana nami waki toka shule.
SEMVUA:
Naona. Na wakati huu umeamua kupanda mihogo mahali palipo jitenga. Kwanini?
HADIJA:
Nilipoteza mihogo mingi sana mwaka jana sababu ya ugonjwa wa batobato. Jirani yangu ambae shamba lake lilikua karibu na langu hakutoa mihogo iliyoshambuliwa na ugonjwa. Niling’oa mihogo ya shambani kwangu iliyoshambuliwa na ugonjwa na kuichoma, ila mingine iliambukizwa kutoka kwenye shamba la jirani yangu.
SEMVUA:
Kwa hiyo ulihisi wakati huu unapaswa kupanda mihogo yako mbali na Bustani zote ili kuepuka maambukizi enezi ya wa magonjwa shambani
HADIJA:
Bila shaka, Ndiyo.
SEMVUA:
Naam, Huwezi kuwepo hapa pekee yako, Kwa sababu nitakuwa Jirani yako.
HADIJA:
(NIMESHANGAA NA KUSHTUKA) Nini? Haujatilia maanani!!
SEMVUA:
Oh ndiyo, Nitafungua shamba langu jipya la Mihogo katika upande wa pili wa msitu. Shamba hili lilitumika na Marehemu Bibi yangu miaka mitano iliyopita, na hapa ndipo nitakapopanda mihogo yangu mwaka huu.
HADIJA:
Huwezi kuanzisha Shamba lako pale!
SEMVUA:
Umesemaje?
HADIJA:
Umenisikia vizuri, Nimesema “HAUTA PANDA MIHOGO YAKO KATIKA SHAMBA LILE”!
SEMVUA:
Unamaanisha?
HADIJA:
Namanisha nilichokisema. Mimi ndiye wa kwanza kuja katika eneo hilo mbali na mtu yeyote ili kuweza kuepuka kuwa karibu na mashamba mengine ya mihogo. Kwa hali hiyo, sitakuwa muathiriwa wa ugonjwa wa batobato … lakini bado unanifata? Sitakuwa nayo!
SEMVUA:
Lakini hauna uwezo ya kunizuia mimi. Haijalishi kama umekuja hapa wa kwanza au la, hilo si jambo muhimu, kipande cha ardhi ninachotaka kupanda mihogo yangu si mali yako.
HADIJA:
Sina uwezo wa kukuzuia wewe? Kwanini? Kwa sababu mimi ni Mwanamke? Au kwa sababu mimi ni mjane? (AKANZA KULIA) Kwa sababu mume wangu amekufa? Unataka mimi na watoto wangu tufe kwa njaa. (AKAANZA KULIA KWA SAUTI NA KUONGELEA HABARI ZA MAREHEMU MUME WAKE) Mmmmmm, Manoza, kwa nini ulituacha weneyewe ili tuteseke hivi? Mmmmm…
SEMVUA:
Hadija, unalia kwa sababu nimesema ninahitaji kulima shamba la mihogo karibu na shamba lako? Je hiyo ni sababu tosha ya kuanza kumuita marehemu kaburini? Aaa … ebu acha fikira hizi!
HADIJA:
HADIJA AKAONGEZA KULIA KWA SAUTI.
MTULIA:
(AKIWA ANAKUJA KWA KUKIMBIA BAADA YA KUSIKIA KILIO CHA AYAYA AKIWA ANAPITA NJIANI AKIELEKEA KATIKA SHAMBA LAKE LA MIWA) Nini kinachoendelea hapa? Nilikuwa nikielekea katika shamba langu la miwa nikasikia Analia. Semvua, Kwanini analia?
SEMVUA:
Muulize.
HADIJA:
(AKIENDELEA KULIA) Manoza, Manoza! Kwa nini umetuacha tunahangaika hivi? Manoza, Manoza, njoo uone jinsi gani mke wako na watoto tunavyongaika!
MTULIA:
Hadija, Tafadhali unaweza ukatueleza nini kilichotokea?
HADIJA:
(AKAACHA KULIA NA KUVUTA HISIA WAKATI AKIONGEA) Ahh, Mtulia, unajua mwaka jana mihogo yangu yote iliangamizwa na ugonjwa wa batobato ikaoza, na mpaka sasa sina kitu cha kuwalisha wanangu. Njia pekee ya kuweza kujizuia na ugonjwa huu usisambae tena msimu huu, ni kuamua kulima shamba jingine la mihogo mbali nna shamba la mtu yoyote yule. Lakini Semvua akaamua kunifuata mimi na kulima shamba lake la mihogo karibu na shamba langu.
MTULIA:
Hiyo ndo sababu ya wewe kulia? Nimetoka kule nikikimbia nikajua Semvua amekupiga au kuna kitu.
SEMVUA:
Hata sikuweza kuamini wakati alipoanza kulia.
MTULIA:
Kweli, Hakuna madhara yoyote kwa Semvua anapolima shamba lake la mihogo karibu na shamba lako. Unajua namna ambavyo ugonjwa wa batobato unavyoambukizwa?
HADIJA:
Ndiyo. Ikiwa shamba la mtu la mihogo lipo karibu na shamba lingine la Mihogo, ugonjwa unaweza ukatoka katika shamba lingine na kuingia katika shamba lako.
MTULIA:
Hiyo inaweza ikatokeaje?
HADIJA:
Sijui. Ninavyojua mimi ni kwamba ugonjwa unatoka katika shamba lililopo karibu na shamba lako.
MTULIA:
Semvua, Ni kwa vipi virusi huambukizwa kutoka shamba moja la mihogo na kufika katika shamba lingine?
SEMVUA:
Kuna baadhi ya wadudu wadogo weupe ambao hunyonya majani ya mihogo, hao ndiyo hubeba ugonjwa kutoka kwenye shamba moja hadi jingine.
MTULIA:
Uko sawa. Ulijifunza wapi hicho?
SEMVUA:
Kutoka katika vipindi vya kilimo kwenye radio.
MTULIA:
Hadija, ulisema shamba lako la mihogo lilishambuliwa na ugonjwa wa Batobato msimu uliopita. Ulijuaje ni ugonjwa wa Batobato ndio ulioshambulia shamba lako?
HADIJA:
Majani ya mihogo yangu yalibadilika umbo na namna fulani yalikuwa yamejikunja. Kulikuwa na madoa ya kijani hapa na pale.
MTULIA:
Na ulifanya nini ulipoona mihogo yako imeathirika?
HADIJA:
Niling’oa mimea yote na nilifanya walichokisema kwenye redio.
MTULIA:
Walisema nini kwenye redio?
HADIJA:
Kwamba tuchimbe shimo mbali na shamba na kufukia mimea iliyoathirika.
SEMVUAA:
Nimesikia pia tunaweza kuchoma mimea iliyoathirika.
MTULIA:
Yote hayo ni sahihi. Sasa, Hadija, kama ni nzi wadogo weupe ndio wanao sambaza huu ugonjwa, nini kitawazuia kutua katika shamba lako hapa, kwa chochote kinacho waleta?
HADIJA:
Nadhani hakuna.
MTULIA:
Ninakubali kuwa kulima katika maeneo mbalimbali kunasaidia kuepuka maambukizi, ila umbali peke yake haisaidii wote mnatakiwa kuwa makini. Unapaswa kuhakikisha unapata vipando vya mihogo kutoka katika vyanzo vinavyoaminika—na lazima viwe na uwezo wa kustahimili magonjwa.

Unapopanda mihogo hakikisha unapanda vipando ambavyo havijashambuliwa na magonjwa ya virusi. Na kagua shamba lako la mihogo kila baada ya wiki mbili au kila wiki ikiwezekana. Hii itakusaidia uweze kugundua kama majani ya mihogo yako yameanza kujikunja. Pindi tu unapoona mmea wenye majani yaliyojikunja yenye madoa ya njano na kijani, ng’oa na itoe shambani, na zika au choma. Na panda vipando vyenye ustahimilivu wa magonjwa ili kukinga mihogo yako kushambuliwa.

HADIJA:
Lakini hizi mbegu zenye ustahimili wa magonjwa zinatoa mihogo michungu ambayo huwezi kuila ikiwa mibichi
MTULIA:
Najua, unaweza ukaisaga katika unga wa muhogo na kutumia mwaka mzima, itaokoa janga la njaa kwa mwaka mzima.
SEMVUA:
Unaona, sio tu kuwa na mashamba karibu karibu tunaweza tukawa na mashamba karibu na wote tukayahudumia vizuri tukaweza kutunza mihogo yetu na tukapata mazao mazuri.
HADIJA:
Mmm, unatafuta tu sababu za kuanzisha shamba la mihogo karibu na shamba langu la mihogo.
MTULIA:
Wala hata sio kweli, Hadija. Unaona kuna namna nyingi za kuzuia Ugonjwa wa batobato. Kama wakulima tuepuke kuoanda mazao kama nyanya pembeni mwa shamba la mihogo.
HADIJA:
Kwanini?
MTULIA:
Kwasababu mazao kama Nyanya yanaweza kuwa ni vyanzo vya wadudu kama nzi weupe ambao wanasambaza magonjwa. Badala yake tunaweza kulima mazao kama mahindi na Soya ambazo hazivutii wadudu.
HADIJA:
Hili sikulijua.
MTULIA:
Nimejifunza pia katika kipindi cha redio kwamba ukiepuka kupanda mihogo pembeni mwa shamba lililoathiriwa na Babatobato unaweza kuepuka mashambulizi ya ugonjwa huu.
SEMVUA:
Hii ni sawa, Bwana Semvua. Cha muhimu kwa wakulima wa Muhogo sisi—na nina maanisha jamii nzima—lazima tushirikiane katika kufuata hatua hizi za kuzuia ugonjwa huu. Mtu mmoja kati yetu asipofuata mbinu hizi itasababisha uharibifu kwa wakulima wote katika jamii.
HADIJA:
Bwana Mtulia, ijapokuwa wewe ni mkulima wa mihogo kama sisi hapa lakini unaonekana kujua mengi zaidi—kama vile wewe ni mshauri wa kilimo.
SEMVUA:
(AKACHEKA) Hadija, kuna usemi unasema uking’atwa mara moja, aibu mara mbili. Mihogo yangu ilishambuliwa vikali na ugonjwa wa Batobato miaka miwili iliyopita ikawa fundisho kwangu jinsi ya kukabiliana na ugonjwa huu.
MTULIA:
Moja kati ya changamoto ninayokutana nayo ni kupata mbegu za mihogo ambazo hazijaathirika na virusi. Labda ujuzi wako unaweza ukatumika hapa Bwana Mtulia.
SEMVUA:
Unaweza kupata ushauri jinsi ya kupata mbegu salama za mihogo ambazo hazija athirika na magonjwa katika vituo vya utafiti vifuatavyo hapa nchini Tanzania: Kwa ukanda wa kati ni kituo cha utafiti Hombolo kilichopo mkoani Dodoma. Kwa kanda ya kusini, ni kituo cha utafiti Naliendele kilichopo mkoa wa Mtwara. Kwa kanda ya Mashariki kuna vituo kama Kibaha na Chambezi wilaya ya Bagamoyo. Kwa kanda ya ziwa kuna tasisi za Ukiriguru mkoa wa Mwanza na kituo cha utafiti cha Maruku kilichopo Bukoba.
HADIJA:
Je kama vituo hivi vya utafiti viko mbali na hapa, Bwana Mtulia? Mkulima mdogo kama mimi ninawezaje kupata taarifa zitakazo niwezesha kupata pandikizi salama za mihogo?
SEMVUA:
Unaleta mjadala mwingine mzuri Hadija, Njia nyingine ambayo tunaweza kupata taarifa za mbegu salama za Muhogo ni kutoka kwa wataalamu wa Kilimo wa Wilaya. Wanaweza wakatuunganiha na wasambazaji wanao sambaza mbegu salama za mihogo. Nadhani kuna jumuia kama hizi vijiji viwili tu kutokea hapa nilipo.
HADIJA:
(AKACHEKA) Bwana Semvua Samahani kwa kicheko kikubwa. Ijapo Kuwa hii ni baraka iliyojificha. Tungejifunzaje kuhusu magonjwa haya ya mihogo kama sio tumekutana? Wanasema maarifa ni nguvu. Kwa mara nyingine tena Samahani.
SEMVUA:
(ANACHEKA) Usijali kabisa, Hadija. Wote tunapaswa kumshukuru Bwana Mtulia kwa kutukomboa.
MTULIA:
ISHARA YA SHUKRANI
HADIJA:
Utakubali mkono wangu kama ishara ya mapatano,
Semvua?
SEMVUA:
Ndio, kutoka moyoni mwangu!

Acknowledgements

Imechangiwa na: Marvin Hanke, Washauri wa Maendeleo ya Redio, Blantyre, Malawi.
Imepokelewa na: Andrew Mtonga, Kitengo cha Kilimo na Utafiti, Kituo cha utafiti cha Chitedze, Malawi.

Information sources

Mahojiano na wakulima wa mihogo kutoka kijiji cha Mulangala Wilaya ya Mulanje, Kitengo cha Maendeleo ya kilimo Blantyre, Malawi.

Mwongozo huu umeandaliwa na msaada wa shirika la CABI Plantwise kupitia Farm Radio Trust.
cabifr-trust