Kupanda Viazi kunaongeza kipato kwa wakulima wa Kabale, nchini Uganda

Uzalishaji wa mazao

Ujumbe kwa mtangazaji

Pakua na hariri taarifa hii kwa matumizi yako.

Mazao yakipekee ni mazao ambayo ni mazao yanyopatikana kwa uchache lakini pia yana uzwa tu katika masoko maalumu. Mazao haya ya pekee ni mazao ambayo yanawez kuipatia familia ya mkulima kipato pamoja na usalama wa chakula. Viazi ni moja kati ya mazao ya kipekee katika meneo yenye baridi barani Afrika.

Viazi ni zao kuu la kibiashara na zao saidizi katika ukanda wa juu magharibi nchini Uganda na maeneo mengine ya miinuko uanda wa kati, mashariki na kusini mwa Afrika. Lakini zao la viazi linashambuliwa sana na wadudu na magonjwa, hivyo wakulima wanapaswa kutumia mbinu ili waweze kuendelea.

Nchini Uganda, kabla ya mwaka 1995, uzalishaji wa zao la viazi haukuwa wa kueleweka, kulikuwa hakuna mbinu fasha kwa uzalishaji wa na uzalishaji wa viazi kama chakula. Kuboresha uzalishaji wa viazi na kuongeza masoko ya zao la viazi, nchi ya Uganda na mashirika ya kimataifa yanafanya kazi kwa pamoja kuhakikisha wakulima wana tumia mbinu za kisasa kufanya uzalishaji, ikiwemo kuhakikisha mbegu bora za viazi zinapatika na kwa bei rahisi. Mradi wa mashamba darasa ujulikanao kama (FFS) uliofadhiliwa na mashirika ya kimataifa na kushirikisha mtandao wa utafiti wa zao la viazi liitwalo PRAPACE ulikuwa ukiwafundisha wakulima jinsi ya kulima viazi ili kupata faida. Wakulima walipatiwa mafunzo jinsi ya kukabiliana na magonjwa na wadudu, matumizi ya mbolea, na kulima kilimo biashara. Mfunzo na kuongezeka kwa mavuno kulipelekea kuongezeka kwa kipato, kutokana na jitihada za shirika kutafuta masoko ya mazao. Kwa matokeo haya sasa kuna kikundi cha’ wakulima, Umoja wa wakulima Nyabyumba (NUF), kikundi hiki kinazalisha viazi bora vinavyoliwa kwa kukaangwa kama chipsi. Wakulima wameongeza uzalishaji wa viazi kwa eneo na muda. Mwongozo huu unaangalia kazi zinazofanywa na kikundi cha umoja wa wakulima Nyabyumba, shirika lililoanza kwa kujiunga kwa vikundi saba vya wakulima, vikundi hivi vilianza katika vikundi vya mashamba darasa.

Mwongozo huu unaonyesha samani na umuhimu wa umoja wa wakulima. Kama mwandishi wa habari, unaweza kuwasaidia wakulima kwa kujua vikundi vya wakulima katika eneo lako kuwapa taarifa jinsi vikundi vinavyoundwa na kukuzwa, na kwa kurusha simulizi zenye kuonyesha mafanikio yatokanayo na wakulima kufanya kazi katika vikundi

Script

Musiki kiashiria kwa sekunde moja, kasha shusha sauti ya muziki polepole.
Jingo za kipindi (jogoo anawika).

MTANGAZAJI:
Kwa mara nyingine ni muda wa “Sauti ya Mkulima.” Kama umekaa baa unasubiria kugongwa kinywaji na rafiki yako, basi hauko mahali sahihi! Kama uko tayari kumeza haraka haraka gulp… gooooo na kurudi kazini!! Leo, tutaongea na mkulima wa viazi atakaye tuelezea jinsi yeye alivyopata mafanikio. Labda unaweza kujifunza kupitia mkulima huyu na ukawa na mafanikio pia! Tutaenda kuangalia ni wapi unaweza kupanda viazi vyako, na umuhimu wa kulimia mazao yako na kupanda mbegu safi na salama za viazi. (Kwa wageni wake). Karibu katika kipindi chetu, Bw. Unaweza kujitambulisha, waambie wasikilizaji wewe ni nani, unatoka wapi, na umekuaje mkulima mwenye mafanikio.

BW. BYARUGABA:
Habari za asubuhi wasikilizaji, nina mafua kidogo asubuhi hii lakini nitajitahidi kuzungumza. (akakohoa kidogo kusafisha koo yake). Jina langu ni Byarugaba, ni katekisti wa kanisa na pia ni mkulima mwenye mafanikio mwanachama wa kikundi cha Nyabyumba cha Umoja wa wakulima.

Mwanangu (akimwambia mtangazaji), kilimo sio kipande cha keki. Unahitaji kujitolea kama unahitaji kuendelea. Sikuenda shule kujifunza kingereza kama maprofesa, lakini, nina ona fahari kwani ninaweza kukaa chini na maprofesa nikawambia jambo na wakanisikiliza. Miaka ya nyuma mnamo 1999 nilikuwa masikini kama panya. Nilitegemea kabustani kadogo nilichokuwa nikilima hapo nyumbani. Hii haikutosha kulisha familia yangu achilia kupata mavuno ya ziada kuuza na kujipatia kipato ili niweze kupata ada ya watoto wa shule. Lakini sasa hivi hii imebaki kuwa historia tu.

MTANGAZAJI:
“Kumbukumbu iliyopita muda Mrefu!” Tafadahli tuelezee umepataje mafanikio na nani alikupa msaada, ulitumia vitu gani? na je, ulizipata wapi na mengineyo.

BW. BYARUGABA:
Mwaka 1999 utabakia katika kumbukumbu zangu. Nilikuwa nina ploti mbili tu za shamba ambazo zilikuwa zinalimika kwasababu zilikuwa bondeni. Niliona kuwa ploti hizi ndio matumaini pekee kwa familia yangu. Ploti nyinginezo zilikuwa vipande vya shamba milimani zisizo limika, na sikuzitilia maanani kwasababu nilijua hazina manufaa.

Nilialikwa katika kikao cha kijiji kilicho andaliwa na mashirika mawili yaitwayo, Shirika la taifa la Utafiti lijulikanalo kama NARO na Africare. Walitaka kufanyakazi na wakulima wazawa. Kushiriki katika kikao hiki mkulima alipaswa awe na shamba mlimani. Nilicheka na niliona kuwa hakuna chochote cha maana tutakachopata kutoka katika Bwadi huu. Lakini nilikuwa niko tayari kutoa shamba langu kwani tayari nililiona kuwa halina maana, na nilitaka kuona miujiza ambayo mashirika haya yangefanya.

MTANGAZAJI:
Kwanini shirika lilitaka mkulima mwenye shamba mlimani?

BW. BYARUGABA:
Walisema shamba la juu mlimani ndi shamba zuri kwasababu liko mbali na wadudu – kulinganisha na ardhi ya bondeni. Nilipanda viazi mabondeni kipindi cha nyuma, lakini sikuzote viazi vilishambuliwa na magonjwa kama backteria mkunjo na madoa doa mwishoni. Mtu anaweza kupanda gunia moja ya viazi na akavuna kiasi kidogo, kwasababu nusu ya mazao yataoza tu.

Tuliambiwa na shirika la NARO na Africare kuwa viazi vinaoza kwasababu ya ugonjwa wa backteria mkunjo ambayo imekuwa katika udongo kwa miaka mingi. Mbegu dhaifu na zenye magonjwa yalikuwa ni matatizo mengine pia. Hatukuamini hiki mpaka tulipo hakikisha kwa mavuno yetu ya mwanzo.

MTANGAZAJI:
Asante, Bw. Byarugaba, kwa taarifa hii. Baada ya mapumziko mafupi tutarudi na mgeni wetu ataendelea kutuambia Zaidi.

Muziki

MTANGAZAJI:
Tumerudi, unaweza kutuelezea zaidi ilikuwaje mlipo anza kufanya kilimo cha viazi kwa mara ya kwanza na shirika la NARO na Africare?

BW. BYARUGABA:
Mashirika mawili haya yaliahidi kutupatia mbegu safi na salama hivyo tukaanza kuandaa shamba na vitalu vya kupandia mbegu katika mashamba ya milimani. Baada ya kumaliza maandalizi tulipatiwa mbegu salama za viazi. Tulipanda mbegu hizi na mbolea za madidni, na kwa nafasi ya sentimita 70 kutoka msatri na msatri na umbali wa sentimita 30. Tuliambiwa kunyunyuza dawa kwenye mbegu hizi za viazi kuepuka magonjwa kama bakteria baka, ili mmea uwe na majani ya kutosha kuwezesha kutengeneza chakula cha kutosha katika mizizi. Pia tulihakikisha mmea unapata jua la kutosha kwa kuondoa magugu isinyanganyane chakula na mme na kukinga jua, na kipindi cha ukuaji tukaendelea kukabiliana na wadudu. Baada ya siku 90, tulivuna viazi vingi. Huu ulikuwa ni mwanzo wa barabara ya mafanikio, mwanangu.

MTANGAZAJI:
Unafikiri watu wengine wanaweza kupata maendeleo kama wewe?

BW. BYARUGABA:
Waache wajaribu, na siku moja nitawasikia redioni wakisimiliz simulizi lao pia!

MTANGAZAJI:
Asante, Bw. Byarugaba, kwa kushiriki katika “Sauti ya Wakulima” Kachwekano FM 103.7. Tutapata mapumziko mafupi na tutakaporudi tutakwambia jinsi mradi unavyoweza kukunufaisha wewe or kikundi chenu?

BW. BYARUGABA:
Ndio, kwa furaha.

Jingo ya kipindi (jogoo anawika), ikifuatiwa na muziki wa kilimo

MTANGAZAJI:
Akama tulivyo kuahidi kabla ya mapumziko, Bw. Byarugaba atatuelezea sasa juu ya kikundi chake. Bw. Byarugaba?

BW. BYARUGABA:
Kikundi chetu cha Umoja wa wakulima Nyabyumba kimenufaika sana kwa kushiriki katika utafiti wa kisayansi. Sasa tunaweza kuzalisha aina tofauti za viazi – kwa kula ua kwa kuuza. Kwa pamoja tumeanzisha kituo ambacho wakulima wanaweza kukusanya viazi vyao na kuuza kwa pamoja. Lakini hatuja simama hapo! Nguvu yetu ya kufanya mapatano na madalali na masoko imekuwa kubwa, na sasa tunaweza kujua ni muda gani mzuri wa kulima, kuuza, na kuchukua masoko.

MTANGAZAJI:
Hii ni nzuri, safi sana. Na ninaelewa kuwa umeanzisha shule ya kilimo, sahihi?

BW. BYARUGABA:
Ndio. Tumetunukiwa na NARO na Africare kuwa sisi ni moja kati ya shamba darasa bora. Kwa matokeo haya tumweweza kunzisha huduma tunayoiita shamba shule. Kama kikundi tumeweza kununu gari ambalo tunatumia kupeleka viazi vyetu sokoni. Habari njea, Kituo cha utafiti wa viazi cha kanda hapa Uganda kijulikanacho kama PRAPACE imetusaidia sisi kupata mkataba na mgahawa mjini Kampala, kuwapelekea viazi kwaajili ya kutengeneza chipsi. Na bei wanayonunulia ni nzuri! Nini kingine nikwambie, mwanangu? Sasa tunaweza kulipa ada za watoto wetu na kuboresha lishe zetu kwasababu tuna pesa, na “kuzungumza kama mwanaume yeyote.” (Ed. Nukuu: msemo huu unatumika kuelezea mtu mwenye hela.)

MTANGAZAJI:
Asante, Bw. Byarugaba. Natumaini wasikilizaji wetu wataona vitendo vyako na mafanikio yako kama chachu ya maendeleo na wao watafanya kama wewe! Kama nitaweza kurudi dondoo muhimu ulizo toa hap awali juu ya upandaji wa viazi, ulisema, Mkulima akumbuke kutumia mbegu bora na mbegu bora, na kukabiliana na wadudu na magonjwa. Ni muhimu pia kupambana na magugu ili kuepuka kunyonya chakula cha mmea na kupelekea kutengeneza makazi ya wadudu. Wakulima watafuta ushauri kwa mtaalamu wa kilimo ambao wanaujuzi wa kuzalisha viazi. Ni vyema pia kupanga katika vikundi na kuudhuria vikao vya vijijini. Na pia unatakiwa kufanya kazi kwa bidii!

BW. BYARUGABA:
Ndio, Hivyo ni sahihi.

MTANGAZAJI:
Nina kushukuru kwa ujumbe uliousambaza kwa wasikilizaji wetu leo wa kipindi cha “Sauti ya Wakulima.”

BW. BYARUGABA:
Asante kwa kunialika. Nina tumaini wakulima huko wako na majembe yao tayari kabisa kwenda kukifanya kile nilicho waambia! Wajarinu na kujionea. Tuna usemi kuwa “jarinu na amini.” Waache wajaribu, na wabarikiwe wale waaminio bila kuona. Asante na Mungu akubariki “Sauti ya Wakulima.”

MTANGAZAJI:
Wapenzi wasikilizaji asante kwa kuwa sehemu ya kipindi na ninatumaini mtafungulia redio zenu katika kipindi kijacho.

Zima muziki kwa sekunde tano, kasha punguza sauti.

Shukrani

Imechangiwa na: Tumwebaze Baryamujura Adrian, Kachwekano Community Multi-Media Center, Kabale, Uganda, na taarifa kutoka Bw. Byarugaba (mwenyekiti wa umoja wa wakulima yabyumba), Rogers Kakuhenzire (daktari wa magonjwa ya mmea, NARO), Tibanyendera Deo (mtafiti msaidizi /mwezishaji, Shamba Darasa, NARO), na Africare.
Imehaririwa na: Daktari. Berga Lemaga, mwandamizi PRAPACE, na Dkt. William Wagoire, mkuu wa mradi wa viazi shirika la NARO Uganda. Shukrani ziwaendee CIAT pamoja na, walio wasaidia kuwaunganisha kikundi cha wakulima na soko, NANDOS masoko endelevu.

Acknowledgements

gac-logoMradi umefanyika kwa msaada wa kifedha kutoka serikali ya Kanada kupitia kitengo cha mahusiano cha kimataifa (CIDA)

The translation of this resource was made possible with the support of USAID’s New Alliance ICT Extension Challenge Fund, through the International Fund for Agricultural Development in Tanzania. For more information about the Fund, please see: https://www.ifad.org/