Utunzaji wa ndama na mama yake

Mifugo na ufugaji nyuki

Ujumbe kwa mtangazaji

Afya ya wanyama wanaofugwa ndani ni muhimu sana kwa wafugaji. Wanyama hawatoi chakula tu, pia hutusaidia kulima na kusafirisha bidhaa zetu za kilimo.  Mbolea yao ya samadi ni chanzo muhimu cha mbolea na nishati. Wakati wanyama wanapougua au kufa, mapato ya familia na afya yote yanayumba.

Wanyama wote wana mahitaji ya muhimu, kama chakula na maji na nyumba nzuri.  Lakini wanyama pia wana haja ya kutendewa vyema. Hii inajumuisha kuishi katika mazingira mazuri, kuwa na wanyama wengine, na kuepuka hali zinazosababisha matatizo.

Wakati wanyama wanapopata huduma nzuri, hii ina faida kubwa kwa mmiliki. Mifugo ya ndani iliyotunzwa vizuri hutoa maziwa zaidi, kuwa wakubwa, na kuwa na watoto wenye afya. Kiwango cha ubora wa nyama yao ni bora zaidi.

Magonjwa ya wanyama ni tatizo kubwa la kimataifa. Kwa wakulima maskini, athari za ugonjwa juu ya maisha ya mifugo na maisha kwa ujumla ni mbaya sana. Kuongezeka kwa magonjwa kunaweza kumaanisha tofauti kati ya kuwa na chakula cha kutosha na njaa, kati ya kuwa na mapato salama na kuuza bidhaa muhimu za kaya.

Mifugo nayokutana na mkandamizo wa maisha kama vile nafasi zilizojaa, joto kali, ukosefu wa uingizaji hewa nzuri, makazi duni, na chakula dhaifu na maji yasiyo na afya, huathiriwa na magonjwa na vimelea. Badala ya kumtegemea mtaalam wa mifugo wakati wanyama wanapokuwa wagonjwa, wakulima wanaweza kuzuia
magonjwa na matatizo ya tabia kwa kuwapa wanyama wao huduma nzuri, na kufanya mazingira ya mifugo yao kuwa salama, kiafya kadiri iwezekanavyo.  Wanyama pia wanahitaji fadhili, upendo, na uhuru wa kuelezea tabia za asili za kijamii.

Muongozo huu unafafanua jinsi wakulima wanavyoweza kutoa huduma nzuri kwa ndama wachanga waliozaliwa na mama zao. Huduma nzuri huleta matokemazuri katika ukuaji mzuri na afya njema. Ni nzuri kwa wanyamana ni nzuri kwa mfugaji.

Inakadiriwa muda wa muongozo huu ni: dakika 10-15, ikiwa ni pamoja na muziki wa kufungua na kufunga.

 

Script

PEACOCK:
Leo, nina vidokezo kwa mtu yeyote ambaye ana ng’ombe mmoja au zaidi na anataka kuzalisha ndama wenye nguvu na afya ambao hawawezi kupata magonjwa kwa urahisi.

Kwa kuanza, kuwa na ndama aliyezaliwa na afya, mama wa ndama lazima awe na afya wakati ndama anakua ndani yake. Ili awe na afya, lazima awe na malisho mengi na maji safi, hasa katika miezi miwili au mitatu kabla ya ndama kuzaliwa. Na ni lazima aendelee kupata chakula kizuri na maji safi baadaye. Ikiwa ng’ombe wako ana afya na analishwa vizuri, atazaa ndama wenye afya na atatoa maziwa mengi.

Kitu kingine: ni bora zaidi, wakati unapofika wa ndama kuzaliwa, ikiwa ng’ombe wako anajua na anahisi kuwa wewe ni rafiki yake. Ikiwa yeye ni mdogo na atakuwa na ndama wake wa kwanza, miezi michache kabla ya kuzaliwa kwa ndama ni wakati mzuri wa kumjua, na hata muhimu zaidi, ili ajue na kujisikia vizuri unapokuwa karibu naye. Wakati huu, uonyeshe huruma kwake, mbembeleze, zungumza naye, mshikeshike, msafishe, mpe chumvi wakati wowote unapokuwa karibu naye. Kisha wakati ndama atakapokuja, ng’ombe atatoa ushirikiano unapokuwa pamoja naye ili kumsaidia ikiwa ni lazima.

Sasa, siku chache kabla ya kuzaliwa kwa ndama, tayarisha mahali safi, kavu, pamoja na kuweka paa ikiwa inawezekana, ambapo mama anaweza kukaa wakati ndama atakapozaliwa. Hii inaweza kuwa mahali ambako ndama anaweza kulala na kukingwa na kuokolewa na jua na mvua, angalau kwa wiki chache za kwanza za maisha yake. Hakikisha unaiweka safi, na kavu. Ikiwa hutafanya hivyo -kama ardhi inakuwa na maji na matope, na nzi na kinyesi kipo mahali pote, ndama wako anaweza kupata magonjwa kwa urahisi sana, na anaweza hata kufa. Kwa hiyo, hakikisha mahali pako tayari na majani safi au vitu nyingine kama kitanda safi, kama vile majani makavu-kwa ndama kabla ya kuzaliwa.

Ikiwa ng’ombe wako ni ng’ombe wa maziwa ambaye atalishwa chakula kinachowezesha maziwa kutoka baada ya kuzaa, unapaswa kuanza hatua kwa hatua kumlisha chakula hicho cha maziwa mwezi mmoja kabla ya kuzaa ili tumbo lake lianze kuzoea chakula hicho, na kumsaidia mama kutoa maziwa zaidi baada ya kuzaa. Anza na nusu kilo mwezi mmoja kabla ya kuzaa, na baada ya wiki moja, ongeza kilo moja kwa siku. Kwa kila wiki inayofuata, endelea kumuongezea nusu kilo nyingine kwa siku (kilo 1 ½ kg / siku kwa wiki mbili kabla ya kuzaa, kilo mbili kwa siku kwa wiki moja kabla ya kuzaa), ili mama atakapokuwa tayari amezaa, atakuwa tayari anatumia kilo 2 ½ kwa siku ya chakula cha kuongeza maziwa ndipo utaongeza kama uzalishaji wake wa maziwa unavyoongezeka.

Ikiwa unataka kujua chakula cha kumpa, hapa kuna kanuni: 1) Ondoa lita 5 kutoka kwenye lita za maziwa ng’ombe anaozalisha, na kisha ugawanye 2) Hii itakupa kilo za posho za mgawo wa chakula cha maziwa cha kumlisha ng’ombe kila siku.

Kwa mfano, ikiwa ng’ombe hutoa lita 10 za maziwa basi:

(Kilo 10 – kilo 5) ÷ 2 = kilo 2.5 ya posho ya chakula cha kuongeza ili atoe maziwa.

Wakati unapofika wa ndama kuzaliwa, Simamia kusiwepo na kelele au fujo yoyote karibu na ng’ombe wako. Waweke watoto mbali ili ng’ombe asisumbuliwe. Ni vizuri kuwepo hapo. Hii itasaidia ikiwa kitu kitaenda vibaya, unaweza kuomba msaada haraka. Kwa kawaida, ndama atazaliwa kawaida bila msaada wowote, na ni bora kutofanya kitu isipokuwa kama unapaswa kufanya hivyo. Tazama tu kama kila kitu kipo sawa. Mara baada ya mikazo kwa ng’ombe kuanza, tazamia kumuona ndama ndani ya saa nne, (au masaa nane kwa mama anayezaa kwa mara ya kwanza). Kama hii haitokei, au unamuona ndama lakini hatoki nje zaidi kutoka kwa mama kwa nusu saa, omba msaada au toa msaada kama unaweza.

Sababu nyingine nzuri ya kuwepo hapo ni ili uweze kumsaidia ndama baada ya kuzaliwa. Wakati mwingine pua ya ndama mchanga hufunikwa na kioevu cha majimaji mazito, yanayoitwa ute. Ikiwa pua imefungwa kwa njia hii, hawezi kupumua, na anaweza kufa. Kwa hiyo, mara tu baada ya kuzaliwa, fanya haraka safisha ute wote kutoka ndani ya pua zake na kuzunguka kinywa chake. Unaweza kufanya hivyo kwa kidole gumba na vidole vyako. Njia nyingine ni kushinikiza mrija katika pua ya ndama pole pole. Hii itamfanya ndama kupiga chafya-hiyo ndiyo njia nzuri ya kufuta ute. Ikiwa bado ndama hapumui baada ya hilo, mpige ndama kwa nguvu upande wake kwa mkono wako, karibu tu na mguu wa mbele, au kwa nguvu nyingi sugua kifua chake. Hiyo itasaidia. Kumwaga maji baridi ndani ya sikio pia kunaweza kusababisha ng’ombe kuitingisha kichwa chake, ambacho kinaweza kufuta ute huo.

Ndama mchanga aliyezaliwa anapaswa kunyonya maziwa ya mama yake mara baada ya kuzaliwa-ndani ya saa moja au mapema iwezekanavyo.

Pengine umeona sasa kwamba ng’ombe wa maziwa huzalisha kwa siku chache za kwanza baada ya kuzaliwa kwa ndama yake ni tofauti na maziwa anayozalisha wakati mwingine. Ni mazito na ya rangi ya njano zaidi. Hiyo ni kwa sababu ina protini zaidi na vitu vingine vilivyo ndani yake kuliko maziwa ya ng’ombe ya kawaida. Pia ina kitu maalum ndani yake kinachoitwa kingamwili ambacho hulinda ndama wadogo kutokana na kuhara na matatizo mengine. Maziwa maalum husaidia ndama kukua akiwa na nguvu na afya nzuri tangu mwanzo wa maisha yake. Ikiwa ndama yako hatakunywa maziwa haya maalum, anaweza kupata magonjwa kwa urahisi sana na anaweza kufa.

Hakikisha, basi, kwamba ndama wako hunywa maziwa haya maalum baada ya kuzaliwa. Ikiwa hajaanza kunywa ndani ya saa moja au mbili, msogeze kwa mama yake na sogeza pua yake karibu na kiwele cha mama, na upake maziwa kidogo ndani ya kinywa chake ikiwa ni lazima. Hakikisha kiwele ni safi ili chakula cha kwanza cha maziwa yasiwe na uchafu. Ikiwa unaweza kukamua maziwa kutoka kwa ng’ombe na kumnywesha ndama, hiyo ni bora kwa sababu utajua ni kiasi gani ndama atapata. Ni bora kwa ndama kunywa angalau lita nne za maziwa ya kwanza ya mama ndani ya saa sita hadi kumi na mbili baada ya kuzaliwa ili kumpa kinga bora dhidi ya magonjwa.

Ni muhimu kuzuia maambukizi ya vidonda vinavyovimbisha kitovu, ambayo inahusisha kuiogesha au kunyunyizia dawa baada ya kuzaliwa-na kisha kila siku hadi kitovu kikauke, ambacho kinapaswa kuchukua takriban wiki moja. Suluhisho la 7-10% la iodini hufanya vizuri zaidi. Uliza mtaalam wa dawa aliye karibu. Ndama wanaweza kufa kutokana na maambukizi ya kuvimba kwa kitovu, hivyo muite mtaalam wa mifugo mara unapogundua kuna uvimbe.

Hakikisha, pia, kuwa ng’ombe mama huendelea kupata chakula na maji mengi iliaweze kutoa maziwa ya kutosha kwa ndama wake ili kumpa uimara na afya. Angalau lita nne kwa siku zinahitajika kwa afya nzuri na ukuaji mzuri. Pia, hakikisha mama anapata maji ya kutosha wakati wote, hasa wakati wa msimu wa ukame.

Na, hatimaye, hakikisha ndama wako ana mahali penye ukavu, mahali pasafi pa kupumzika, usafi wa hali ya juu, majani makavu ya kulalia. Safisha kinyesi kuondoa matandazo yaliyo mabichi kila siku. Kwa njia hii, hatapata maji na uchafu kutoka kwenye matope na kinyesi. Na uangalie kwa makini-angalia mara moja au mara mbili kwa siku. Ikiwa anaonekana kuwa ni mgonjwa, fanya kile unachoweza ili kumsaidia kupata afya nzuri mara moja. Piga simu kwa mtaalamu wa mifugo au msaidizi wa afya ya mifugo haraka iwezekanavyo, na mtenge mnyama huyo mgonjwa mbali na wengine ili kuzuia kuenea kwa magonjwa.

Ndama wako ni mnyama mzuri sana wa thamani. Ikiwa utamuangalia vizuri, atakuja kuwa imara na mwenye afya na atakuhudumia vizuri zaidi.

Acknowledgements

Shukrani

Muongozo huu uligawanywa awali mwaka wa 1985 kama Kifurushi cha 10, muongozo wa 2. Ilibadilishwa na kurekebishwa upya na John VanLeeuwen, Profesa wa magonjwa yanayosababishwa na Usimamizi wa Afya ya Wanyama wanaocheua Mwenyekiti-Daktari wa Wanyama bila Mipaka-Kanada, Idara ya usimamizi wa Afya, Mifugo ya Mifugo ya Atlanticki Chuo Kikuu cha Kisiwa cha Mfalme Edward, Charlottown, PEI, Kanada.

Tafsiri ya hati hii inafadhiliwa na ELANCO ANIMAL HEALTH