Taka ndani, Taka nje: Panda vipando salama vya mihogo kuepuka ugonjwa wa Batobato shambani mwako

Kilimo

Ujumbe kwa mtangazaji

Mihogo ni chakula cha tatu cha ukubwa nchini Tanzania mahindi na mchele zikiongoza, hasa hasa maeneo ya kaskazini mwa nchi. Muhogo unakuwa zao muhimu la kibiashara na uzalishaji umeongezeka mara tatu kwa miaka kumi iliyopita.

Pamoja na kuuza mihogo mibichi katika masoko ya ndani, wakulima wanaweza kuuza kwa waokaji wadogowadogo na wazalishaji. Kuna uwezekano wa soko kubwa la unga wenye ubora wa mihogo na kwa wazalishaji wa Biskuti na unga wa kwenye vifungashio.

Igizo hili linaonyesha jinsi gani ugonjwa wa hatari uitwao Batobato unaweza kusababisha asilimia 100 hasara kama ikisambaa na kuelezea jinsi inavyoweza kuzuilika.

Igizo hili limeangalia sana taarifa zilizotokana na mahojiano ya Wakulima na Wataalamu kutok nchini Malawi, na kubadilishwa kutumika Tanzania. Unaweza kuchagua kutumia maigizo haya kama sehemu ya kila siku ya vipindi vyako vya redio, tumia sauti ya muigizaji kumuwakilisha mzungumzaji. Kama ndivyo tafadhali kumbuka kuwajulisha wasikilizaji wako kuwa sauti watakazo sikia ni za waigizaji na sio sauti za wakulima na wataalamu waliofanyiwa mahojiano.

Au unaweza kutumia Maigizo haya kama chanzi cha habari au ushawishi katika kuandaa kipindi kinachoelezea jinsi ya kukinga ugonjwa wa Batobato katika eneo lako.

Nukuu vipengele muhimu vifuatavyo:

  • Kupanda vizuri, vipando vyenye afya ni hatua ya kwanza kuzuia ugonjwa wa muhogo wa Batotobato na kupata mavuno mazuri.
  • Njia nyinginezo ya pili ya kuzuia magonjwa ni kupanda mbegu za muhogo zenye usatahimili wa magonjwa na kukagua shamba lako la muhogo kuona dlili za awali za magonjwa.
  • Ugonjwa wa Batobato unaambukizwa na Nzi mweupe anaye toa virusi kutoka kwnye mmea ulioathririka na kuhamishia kwenye mmea salama.
  • Nzi weupe ni vigumu kuwakabili njia salama ya kupambana na ugonjwa ni kung’oa mmea ulioathirika na kuuzika mbali na shamba.
  • Hakuna mbinu zilizopo za kupambana na ugonjwa wa Batobato. Neem wanaweza wakafukuza nzi weupe na kuepusha mashambulizi lakini njia hii haijafanyiwa majaribio ya kisayansi.
  • Ugonjwa wa Batobato unaweza kuwa wa hatari sana kwa Mihogo na kipato cha mkulima lakini hauna madhara yeyote kwa Binadamu.

Muda uliokadiriwa kwa Muongozo huu ni Dakika 20 Pamoja na utangulizi na Muziki wa Hitimisho.

Script

WAIGIZAJI:
SHOMVI: Mkulima wa mihogo anayejulikana vizuri kijijini Bungu. Anasambaza unga bora wa mihogo ni Mume wa Fatuma.
FATUMA: Mke wa Shomvi.
JUMA: Anaishi katika kijiji cha Bungu. Moja ya shamba lake lipo karibu na shamba la mihogo la Shomvi. Mume wa Latifa.
LATIFA: Mke wa Juma.
MWINJUMA: Mkulima wa mihogo ambaye amebobea kulima mihogo mitamu na kuuza kwa wafanya biashara. Hivi karibuni alijiunga na Shomvi kusambaza unga wa mihogo wenye ubora wa hali ya juu.

SFX:
SAUTI ZA KULIMA NA NDEGE
SHOMVI:
Mke wangu, Fatuma … (MSHANGAO WA KUMFURAHISHA) Shaa! … Aina hii ya mihogo inatoa mazao sawa sawa na ile mihogo michungu iitwayo Kalolo.
FATUMA:
Kweli, Mume wangu, Shomvi. Ina mazao mengi. Ni kiroba, ni aina tamu.
SHOMVI:
Angalia huu mzizi—Mkubwa kama Mkono wangu.
FATUMA:
Na huu hapa mkubwa kama mguu wako.
SHOMVI:
(KICHEKO) Ha! Ha! Ha! Kwa nini usilinganishe na mguu wako?
FATUMA:
Vizuri, Ulilinganisha ya kwanza na mkono wako, hivyo nimeendeleza mlinganisho.
SHOMVI:
Sawa. Naamini imekuwa mikubwa kwa sababu tumiepanda na mvua ya kwanza na tumeivuna ikiwa imekomaa kabisa.
MWINJUMA:
Habari, Shomvi.
SHOMVI:
Salama, Mwajuma, Karibu.
MWINJUMA:
Ahhhh … Hii haina ya mihogo mitamu ambayo nafikiri Skuwa ni Kiroba mazao yake yanakaribiana na Kalolo, ile mihogo michungu.
FATUMA:
Hiyo ndiyo tulikuwa tukiisifia kabla wewe kuja. Tulikuwa tunasema kwamba tunapaswa kuipanda aina hii tena kama tukiamua kupanda mihogo mitamu.
MWAJUMA:
Ndiyo, inamazao mengi. Ila tatizo la mihogo hii mitamu haistahimili ugonjwa wa Batobato. Ninatamani hawa wazalishaji wa mbengu hizi za mihogo wangezalisha mbegu ya mihogo mitamu ambayo ni kinzani na yenye ustahimili wa ugonjwa wa Batobato na mazao yake yakawa mengi kama kalolo.
SHOMVI:
Kweli, na sisi wauzaji wa unga bora, tunaipenda kwasababu haizalishi mizizi mingi.
MWINJUMA:
(VICHEKO) Vizuri Aina hii ya mihogo mitamu ni kwa ajili ya wakulima ambao hawana hofu ya kujaribu uzoefu wa vitu vipya.
FATUMA:
Unamaanisha nini?
MWINJUMA:
Unajua ninatengeneza pesa nyingi kutoka kwenye Mihogo mitamu. Kwa hiyo wakati nzi weupe huja, ninahakikisha nawadhibiti kabla hawajaleta ugonjwa kwenye shamba langu, pale inapotokea.
SHOMVI:
Ni kwa namna gani unawadhibiti nzi weupe? Nilijua kuwa hakuna dawa inayoweza kuwa tokomeza.
MWINJUMA:
Niladhari nimekwambia…….aah…. inamaana hujui?
FATUMA:
Hujui nini?
MWINJUMA:
Sawa, Wanasayansi wanasema hakuna dawa ambayo inaweza kuzuia nzi weupe wasieneze ugonjwa wa Batobato isipokuwa sisi wakulima hutumia neem kuuwa na kuwafukuza inzi weupe mbali na Mashamba yetu.
SHOMVI:
Mimi pia natumia Neem. (UTANI) Badala ya kujaribu kutumia njia isiyowezekana ya kutumia Bunduki, nilitumia Neem.
FATUMA:
(VICHEKO) Shomvi, usiniue na matani yako. Unawezaje kuua nzi kwa bunduki?
SHOMVI:
(UTANI UKIENDELEA) Kama ni vigumu kuua kitu, njia gani mbadala utaitumia kukiua?
Lakini afisa kilimo aliniambia kwamba Neem haijajaribiwa kitaalamu na kuthibitishwa kama dawa ya kukinga mihogo thidi ya Batobato hivyo hawashauri tuitumie. Na pia alisema inamanufaa kuitumia tu katika eneo hili endapo utaona nzi watano au zaidi katika mmea wa Muhogo vinginevyo nzi weupe hawana mazara makubwa kiasi cha kuingia gharama kukabiliana nao.
MWINJUMA:
Ninajua, lakini imekuwa ikinisaidia.

Hata hivyo ninaona nzi weupe wameshambulia majani ya muhogo huu, na kwa bahati mbaya ninaona dalili za ugonjwa wa Batobato katika mazao haya.

SHOMVI:
Kweli wewe ni Mkulima wa mihogo. Kumbe umegundua kuwa imeathirika hata kwa kiasi hiki kidogo?
MWINJUMA:
Oh ndiyo. nilikwambia, adui wangu mkubwa ni nzi weupe. Ni muhimu sana kukagua shamba lako mara kwa mara ili uweze kugundua dalili za ugonjwa wa Batobato mapema.
FATUMA:
Upo sawa. Nzi weupe walikuja baada ya Mihogo kukomaa. Kama wangekuja mapema tungepoteza mazao yote.
SHOMVI:
Ni kweli, ingekuwa majanga. Batobato siyo ugonjwa wa kupuuzia una hatari. Unaweza ukapoteza mazao yako yote.
MWINJUMA:
Ninahitaji kujua, Utafanyia nini hii mimea iliyoathirika? Je, utakata vipandikizi kwenye mimea hiyo?
SHOMVI:
Kwa nini unauliza swali la kijinga hivi? Bila shaka hapana!

Hata hivyo kwa kuwa tuna soko zuri la unga mihogo wenye ubora wa hali ya juu. Tunaweza tukalima Kalolo, ile aina ya mihogo michungu na tena ni kinzani na ugonjwa wa Batobato.

MWINJUMA:
Nilitaka kuhakikisha kuwa utalinda kiwanda chetu cha uzalishaji wa mihogo kwa kutopanda mihogo iliyo athirika.
FATUMA:
Mimea hii iliyoathirika itakuwa kuni zangu mwaka huu. Tutazipanga hapa na kuikausha na kuitumia kama kuni nyumbani kwangu.
MWINJUMA:
Kwa nini usiikaushe nyumbani kwako?
SHOMVI:
Tutaipeleka nyumbani leo baadae…….Kwa sasa nitazipanga karibu na jirani yetu Juma na kuzipeleka nyumbani ili zikauke pindi nitakapotoka sokoni.
JUMA:
(AKIKARIBIA) Bwana Shomvi, hii mihogo iliyojaza Kirikuu zako mbili ni Michungu au Mitanu?
SHOMVI:
Juma, Hii ni mihogo mitamu. Haujui mizizi ya mihogo yangu michungu ilivyo?
LATIFA:
Shomvi, Ninajua nimikubwa (AKISHUSHA SAUTI YAKE). Juma, Mume wangu.
JUMA:
(KWA UKIMYA) Ndiye, Latifa.
LATIFA:
Tunahitaji kufanya kitu. (KWA SAUTI) Kirikuu mbili kwenye shamba dogo hivyo? Utakuwa tajiri.
FATUMA:
Ndiyo, itaniletea pesa nyingi, hata Hatukutumia mbolea ya aina yeyote na tela moja la ng’ombe litatupatia zaidi ya shiling 700,000 taslim.
SHOMVI:
(AKIONDOKA) Hapana … Usilichukulie swala la Fatuma kwa uzito. Hatukutengeneza pesa nyingi.
MWINJUMA:
Latifa na Juma, mnapaswa kuchulia swala la Fatuma kwa uzito. Unaweza ukatengeneza pesa nzuri ukilima mihogo mitamu.
SHOMVI:
Sawa, utahitaji kuchagua unamuamini nani. Tunaondoka sasa; tunahitaji kufika sokoni kabla jua halija zama ili tuweze kukutana na mnunuzi.
JUMA:
(KWA SAUTI) Safari njema, Jirani. Mafanikio mema. (KWA SAUTI NYORORO) Latifa, uko sawa, ebu tufanye kitu. Tupande mihogo kwenye shamba pembeni mwa shamba la Fatuma.
LATIFA:
Kweli, tunaweza kutumia hiyo miche. Ikiwa imepangwa kama hivyo, ninajua inakauka. Tunaweza tukaibeba tukaipeleka kwenye shamba letu na kuipanda.
JUMA:
Oh sawa! Nakumbuka kwa mara ya Mwisho walitupatia baadhi ya miche tuitumie kama kuni.
KIPENGELE KINABADILIKA
FX:
HODI! HODI! MBWA ANABWEKA.
SHOMVI:
(ANAFUKUZA MBWA) Juma, uko hapa?
LATIFA:
(MBWA ANAACHA KUBWEKA) Fatuma, subiri! Juma alikuwa anaoga, lakini kwa sasa anavaa na anakuja.
JUMA:
(ANAKARIBIA) Kaka Fatuma, unahitaji twende mjini tukanunue gari kwa pesa ulizozipata?
SHOMVI:
Juma! Acha hizo! Kwanini mara nyingi unarukia kwenye hitimisho?

Tuache hayo, miche yangu ya mihogo iko wapi?

JUMA:
Wewe Jamaa, Ulipo ondoka asubuhi hukuomba familia yetu ikuangalizie hiyo Mihogo?
LATIFA:
Ahaa! Kwa hiyo umekasirika, Shomvi, kwa sababu tulichukua kuni mlizoacha karibu na shamba lenu?
SHOMVI:
Sina hasira kwa sababu mmeiba miche yangu ya mihogo, ila kwa sababu mmepanda miche yenye magonjwa kwenye shamba lilolopo karibu na langu.
JUMA:
Kuiba? Niliiba mihogo yako?
SHOMVI:
Nani aliyekupa mamlaka ya kuchukua miche yangu?
LATIFA:
Mara nyingi unatupatia kuni, kipindi hiki tulichagua tupande gawio letu.
SHOMVI:
Gawio gani unalo lizungumzia? Nulisema mchukue?
LATIFA:
Hapana, tuliamua tuwe matajiri kama wewe, hivyo tukazipanda.
SHOMVI:
Ninawa amuru mkaing’oe hiyo miche ya mihogo, itasambaza ugonjwa wa Batobato katika eneo hili.
JUMA:
Hapana, Hatutaweza kuing’oa, tunaweza tukakulipa kwa madi kuwa tumekuibia miche yako. Ni shilingi ngapi unahitaji tukulipe?
LATIFA:
Ndiyo, Tunaweza kukulipa.
SHOMVI:
Sihitaji pesa zenu, ila.
JUMA:
(AKADAKIA) … Lakini nini? Unahitaji sisi tubaki kuwa maskini, unafurahi kutuona sisi tukiendelea zaidi yako …?
SHOMVI:
(AKADAKIA) … Mihogo hiyo ilikuwa migonjwa.
LATIFA:
Kama ilikuwa migonjwa, kwa nini unataka sisi tuing’oe? Kwani tuliipanda kwenye shamba lako?
JUMA:
Hataki na sisi tupate pesa kama.
SHOMVI:
Hapana, sio hivyo sio kwamba sitaki utajirike. Sitaki tu usambaze magonjwa. Sijakupa kipindi kile.
LATIFA:
Ulitupatia vipando. Lakini kwanini unahofia wadudu waliopo katika shamba letu?
SHOMVI:
Ni kwasababu ugonjwa ni hatari sana, na inaweza kusambaa katika eneo zima kama isipoangaliwa. Hatutapata faida yeyote kama ugonjwa utasambaa.
LATIFA:
Hmmm … Mazao yako yamestawi vizuri kuliko mazao ya wakulima waliyopewa vipando na NGO katika kijiji nilichotembelea, na wakulima walipanda vipando hivyo.
SHOMVI:
Ndio, Ninajua kuwa baathi ya NGO hawajui kwamba wanasambaza vipando vyenye magonjwa…. Lakini haimaanishi kuwa hao wakulima walinufaika na vipando hivyo.

Hivyo, ng’oa hizi kabla eneo zima halija athirika na magonjwa.

JUMA:
Nimekusikia lakini sita ngo’a mpaka nitakapo ona huu ugonjwa unahatari kiasi gani.
LATIFA:
Hatuta Ng’oa. Hatuta ng’oa kwasababu tu eti mtu mwenye wivu anatulazimisha kung’oa.
SHOMVI:
Ninakuonya huu ugonjwa ni hatari na unaweza ukaangamiza kilimo cha mihogo katika eneo hili lote.
JUMA:
Tuko tayari kukabiliana nao.
SHOMVI:
Nimejaribu kila kitu lakini hautilii maanani ushauri wangu.

Sawa, nitakupa mbegu salama za kupanda katika bustani yako, sitakutoza pesa nyingi.

JUMA:
Asante kwa hili. Nitaninua na kuzipanda kisha nitalinganisha na mihogo ambayo nimeshaipanda —vipando ninavyovijua vinatoa mavuno mengi. Lakini sitazingoa hizo.
SHOMVI:
Unaniacha na chaguo moja—kukushataki kwa kiongozi wa kijiji kuwa umeiba vipando vyangu vya mihogo.

Ila kama umezing’oa hivi karibuni, unaweza kuzitumia kama kuni.

JUMA:
Umesema nini!
SHOMVI:
Nina kushitaki kwa Chifu kuwa umeiba vipando vyangu!
JUMA:
Hapana, tafadhali usinishataki! Hii isifike mbali kiasii hiki, Tukubaliane.
SHOMVI:
Tukubaliane kwa lipi? … Nimejaribu kuelewana na wewe, na sasa ninaenda kwa Chifu.
LATIFA:
Hapana, subiri! … Kama tuking’oa utaturuhusu tubaki nazo?
SHOMVI:
Utabakinazo kama kuni.
JUMA:
Utanipa pandikizi salama kama ulivyoahidi?
SHOMVI:
Kama utakubali kung’oa hizi zilizo haribika, Ndio nitakupatia.
JUMA NA LATIFA:
Sawa, Tutazing’oa.
SHOMVI:
Asante. Nitafanya kama tulivyo kubaliana.
LATIFA:
Utatushtaki kwa Chifu?
SHOMVI:
Hapana, tuko sawa!
LATIFA:
Asante Bw. Shomvi. (KWA UPOLE) Mume wangu tung’oe hii mihogo na tupande kwenye shamba langu kule kijijini.
JUMA:
(KWA UPOLE) Oh Ya, vizuri sana; Sijawahi kufikiria hilo. (SAUTI YA KAWAIDA) Shomvi, chukulia hili limeshafanyika. Lakini tunaweza kupanda vipando hivi salama ulivyotupatia karinu na shamba lako sio?
SHOMVI:
Hakuna shida. Ninataka tu kuwalinda wazalishaji wa mihogo katika eneo letu.
LATIFA:
Asante.

NYIMBO YA KUBADILISHA KIPENGELE

FX:
PIGA NYIMBO KWA SAUTI YA CHINI IKIINGILIANA NA SAUTI ZA NDEGE NA ISHIKILIE CHINI
JUMA:
Latifa, Shomvi alikuwa sahihi. Hivi vipando vya mihogo tunavyochukua kwa Shomvi zinamagonjwa, ebu ziangalie!
LATIFA:
Mmea umedumaa kama mtoto aliyekosa lishe…. Majani yamejikunja, yamejisokota na umbo baya kama Kondoo wa India (VICHEKO) … na zina madoa ya unjano na kijani.
JUMA:
Uko sahihi.
LATIFA:
Kinachonishangaza mimi ni kwamba shambani tumepanda vipando kutoka kwa Shomvi, mihogo ni mikubwa, na kunamipasuko kwenye matuta kuonyesha kuwa mizizi inakuwa lakini sio hapa. Kwanini?
JUMA:
Ndio, uko sahihi mke wangu. Tung’oe baathi ya mihogo tuonene kunanini chini.
LATIFA:
Sawa …
FX:
SAUTI YA KUCHIMBA
JUMA:
Hey, Nimekufa! Angalia mizizi! Hakuna mihogo kabisa ni mizizi midogo tu.
LATIFA:
Siamini kabisa. Tung’oe nyingine.
FX:
SAUTI YA KUCHIMBA
JUMA:
Bora tung’oe hii mihogo na kutumia miti kama kuni, tumepoteza nguvu zetu kupanda hapa.
LATIFA:
Ulitilie mkazo tupande vipando hivi.
JUMA:
Tulitaka kulinganisha kumbuka.
LATIFA:
Shomvi alikuwa sahihi kutuonya. Huu ni upotezaji wa nguvu. Siwezi hata kumuangalia usoni. Nahisi kama dunia ifunguke na kunimeza.
JUMA:
Ninajihisi sina nguvu. Ngoja nikae chini. Huwwu (SAUTI YA UCHOVU).
LATIFA:
Kwanini unajihisi umechoka? Hii sio dalili kwamba msukumo wako wa damu umeongezeaka?
JUMA:
Labda. Labda ninajutia na kufikirika juu ya muda niliopotea kwa kitu nilichoshauriwa … Lakini kama Shomvi amesisitiza kuwa tung’oe mmea sio kwamba ni kwasababu ugonjwa unaambukiza mwanadamu? Alesema kuwa ni ugonjwa wa virusi.
LATIFA:
Nilifikiri kuwa ni virusi kwa mimea. Inaweza kuwaathiri wanadamu? Embu tumuulize tena kabla hatujaendelea kulima zaidi.

MABADILIKO YA KIPENGEE

FX:
SAUTI ZA NDEGE
SHOMVI:
(KWA MSHANGAO) Shaa, Juma … Hili ndilo shamba ulilopanda mihogo ile ambayo nilikuwa najarinu kukushauri usipande?
JUMA:
Ndio, Shomvi, Hili ndilo shamba lenyewe. Tunashukuru kwa kuja kushuhudia bahati yetu mbaya.
SHOMVI:
Ni bahati mbaya au ni maamuzi mabaya?
LATIFA:
Kwanzia tutilie mkazo kupanda vipando vilivyo athirika, ni maamuzi yetu mabovu.
SHOMVI:
Ulichokifanya hakina utofauti na watu wengine wanavyofanya, wanavyogoma kuhama katika maeneo yenye mafuriko, hii ni kukaribisha kifo.
JUMA:
Kwahyo ni kweli kwamba virusi vya Batobato vinaweza kumuathiri mtu?
SHOMVI:
Hapana, simaanishi hivyo. Ni ugonjwa wa mmea, sio ugonjwa wa mwanadamu, haiwezi kukuthuru wewe. Nimemaanisha umealika hasara kwako.
LATIFA:
Sawa. Ya, uko sahihi. Lakini tunaweza kula mihogo midogo tutakayoipata hapa shambani, si sawa?
SHOMVI:
Ndio, unaweza kula. Angalia, kitu kibaya ni kwamba umesambaza magonjwa katika eneo.
JUMA:
Tunasikitika. Lakini tunaweza kufanya nini?
SHOMVI:
Ngoa Mihogo yote na uzike. Hakuna muda wa kuweza kuzikausha sasa, mvua zitaanza muda si mrefu.

Angalia, hawa wadudu wadogo ndio Nzi weupe. Ndio wenye kusambaza virusi vinavyosababisha Batobato wanapofyonza mmea ulioathirika na kuhamia kwenye mmea ulio salama.

JUMA:
Sawa—kwahiyo hivyo ndivyo ugonjwa wa Batobato sambazwa?
SHOMVI:
Ndio. Tuana taka kuhakikisha kuwa nzi weupe hawapati nafasi yeyote ya kula hii miti iliyoathirika. Ngo’a na teketeza mihogo.
LATIFA:
Tung’oe mihogo yote tutumie miti kama kuni.
SHOMVI:
Nina sikitika sio. Kama unataka kutumia kama kuni toa majani yote na fukia hapa. Kisha unaweza kutumia mti kama kuni. Uzalishaji wa mihogo uko hatarini, wewe huwezi kuona hili?
JUMA:
Tunakuelewa. Tumetengeneza hela nyingi kwa kuanda mbegu salama ulizotupatia kwahiyo hatutatumia hata hii miti kama kuni tumeshapata hasara ya kutosha.

Asante, Shomvi, kwa ushauri wako. Tutafukia hii mimea yote.

LATIFA:
Ndio, mume wangu, Juma. Tung’oe mihogo yote mara moja.
SHOMVI:
Ndio, Ngo’a yote na zika majani. Umesha sababisha hasara kubwa hapa. Nitaanza kupulizia Neem shambani kwangu mara moja.
LATIFA:
Kwanini?
SHOMVI:
Kuwafukuza nzi weupe kama wakija shambani kwangu na kuambukiza mazao.
JUMA:
Tuta pulizia Neem katika shamba letu jinpya—lile shamba lililopo jirani na shamba lako.
SHOMVI:
Ndio, ni vyema ukafanya hivyo. Kwahiyo, Juma na familia yako, kumbuka kuwa kupanda vipando salama ni hatua ya kwanza kuepuka ugonjwa wa Batobato. Lakini sio kila mmea ni salama; nyingine inaweza kubeba magonjwa ambayo yanaweza kujitokeza kwa msimu wa pili baada ya kupndwa..
LATIFA:
Ndio. Tumejifunza kupitia njia ngumu na hatutapanda tena vipando vilivyo athirika. Angalia hii mimea mifupi isiyo na chochote, haina hata mizizi!
SHOMVI:
Mazao salama yanatoa mavuno bora. Kumbuka kwamba Ugonjwa wa Mihogo wa Batobato unaambukizwa na nzi weupe wanaosambaza virusi kutoa katika mmea ulioathirika na kusambaza katika mmea salama. Kwa hivyo hakikisha unang’oa mmea ulioathirika na zika eneo mbali na shamba lako.
LATIFA:
NDIO. Bwana.
SHOMVI:
(VICHEKO) Sasa unaniita “Bwana.”

Sawa, nakumbuka unaweza kutumia majani ya Neem au Unga wa Neem, kukinga Nzi weupe katika shamba lako na kuwazuia wasiambukize magonjwa katika mihogo iliyo salama. Ijapokuwa mbinu hii haijahakikishwa na kuthibitishwa kitaalamu bali sisi wakulima tunaijaribu hivyo hivyo. Kama unaahidi kufanya yote haya, Juma na Latifa, mnaweza kujiunga na Chama chetu kinachouza unga wa mihogo wa kiwango cha juu.

JUMA:
Asante, Shomvi. Tunafikiria unapaswa kuwa mkulima wa kuigwa katika eneo hili. Huna wivu na unataka kila mkulima anufaike na zao la Mihogo. Na tunakubali kujiunga na Chama chako. Asante.
SHOMVI:
Karibuni, niko kwaajili yenu.
FX:
SAUTI CHA KIASHIRIA
MTANGAZAJI:
Wapendwa wasikilizaji, mmesikia kilichowatokea marafiki zetu Juma na Fatuma walipo puuzia ushauri wa Rafiki yao. Lakini kama hawakumuamini Shomvi kwanini Familia ya Juma ilimuuliza Mtaalamu wa Kilimo kuhusu ugonjwa kabla ya Kupanda?

Hapana, iliwalazimu kujifunza somo lao kwa njia ngumu, usifanya makosa waliyoyafanya.

Acknowledgements

Imechangiwa na: Gladson Makowa, Story Workshop Educational Trust, Blantyre, Malawi.

Imehakikiwa na: Bw. Stellia Victoria Mangochi, Waziri wa Kilimo, Umwagiliaji na Maendeleo ya maji, Wilaya ya Nkhotakota ofisi za Kilimo, Nkhotakota, Malawi

Information sources

Profesa Vincent Saka, Daktari wa Magonjwa ya Mimea, Kitengo cha sayansi ya Mazao, Chuo kikuu cha Lilongwe cha kilimo na Maliasili (LUANAR), Tarehe 23,Mwezi wa kumi na moja 2016
Stella Mangochi, Mtaalamu wa Mazao, Wilaya ya Nkhotakota ofisi za Kilimo, Tarehe 23,mwezi wa kumi na moja 2016
Andrew Nganga, Mtaalamu wa utafiti, Shirika la Kimataifa la Kilimo kwa nchi za Kitropiki Tarehe 25, Mwezi wa kumi na moja 2016,  Tarehe 21, Mwezi wa kumi na mbili 2016.

 

Muongozo huu uliandaliwa na msaada wa CABI Plantwise kupitia Farm Radio Trust.

cabifr-trust