Habari za msingi kuhusu ugonjwa wa virusi vya corona (COVID-19)

Backgrounder


Pakua habari hii : Habari za msingi


Pakua habari hii : Hatua za tahadhari

1. Jinsi virusi vinavyoenea kutoka kwa mtu hadi mtu

Watu hupata ugonjwa wa virusi vya corona (COVID-19) kutoka kwa wengine ambao wana virusi hivyo. Ugonjwa huenezwa kupitia matone madogo yanayotengenezwa wakati watu walioambukizwa wanakohoa, wanapiga chafya, au wanapumua.
Matone haya yanaweza kuvutwa na watu walio karibu wakati wa kupumua au yanaweza kutua juu ya sura ya vitu vilivyo karibu. Wakati watu wanapumua na kuvuta pumzi yenye matone au kugusa nyuso za vitu vilivyo na matone haya, kisha kugusa macho yao, pua, au mdomo, wanaweza kuambukizwa. Hii ndio sababu ni muhimu kukaa umbali wa zaidi ya mita 1 kutoka kwa mtu mgonjwa. Nchi nyingi zimetunga sera za kukaa mbali kati ya mtu na mtu ambazo zinasema kwamba, kwa ulinzi kamili dhidi ya kuenea kwa virusi vya ugonjwa wa corona (COVID-19), watu wanapaswa kukaa angalau umbali wa mita 1 kutoka kwa watu wengine wote isipokuwa familia zao.

2. Dalili za maambukizi

Dalili za kawaida za ugonjwa wa virusi vya corona (COVID-19) ni homa, uchovu, na kikohozi kavu. Kwa kawaida, dalili huanza pole pole. Baadhi ya watu wengine walioambukizwa hawaonyeshi dalili na hawajisikii kuumwa. Watu wengi (karibu 80%) hupona bila matibabu maalum. Karibu mtu 1 kati ya watu 6 huwa mgonjwa sana. Wazee na watu wenye matatizo ya kiafya kama vile matatizo ya moyo, ugonjwa wa kisukari na shinikizo la damu wana uwezekano mkubwa wa kuwa wagonjwa sana. Watu wenye homa, kikohozi, na shida ya kupumua wanapaswa kutafuta matibabu.

3. Hatua za tahadhari

Osha mikono yako mara kwa mara. Osha mikono yako kila mara na mara zote kwa angalau sekunde 20 kwa maji na sabuni au kitakatisha mikono kilicho na pombe. Kwa nini? Kuosha mikono yako kwa maji na sabuni au kutumia kitakatisha mikono kilicho na pombe huua virusi kwenye mikono yako.

Dumisha umbali wa kijamii/Kimwili. Kaa umbali wa angalau mita 1 kati yako wewe mwenyewe na mtu yeyote anayekohoa au kupiga chafya. Kwa nini? Wakati mtu akikohoa au kupiga chafya, hutoa matone madogo kutoka katika pua au mdomo ambayo yanaweza kuwa na virusi. Ikiwa upo karibu sana, unaweza kuvuta matone hayo wakati wa kupumua. Nchi nyingi zimetunga sera za kukaa mbali kati ya mtu na mtu ambazo zinasema kwamba, kwa ulinzi kamili dhidi ya kuenea kwa virusi vya ugonjwa wa corona (COVID-19), watu wanapaswa kukaa angalau umbali wa mita 1 kutoka kwa watu wengine wote isipokuwa familia zao.

Epuka kugusa macho yako, pua na mdomo. Kwanini? Mikono inagusa vitu vingi na inaweza kubeba virusi. Mara baada ya kuvichukua, mikono yako inaweza kuvisafirisha virusi kwenda kwenye macho yako, pua, au mdomo. Kutoka hapo, vinaweza kuingia mwilini mwako na kukufanya mgonjwa.

Fanya upumuaji wenye kuzingatia usafi. Wakati wa kukohoa au kupiga chafya, funika mdomo wako na pua kwa kutumia kiwiko chako cha mkono kilichokunjwa au tishu. Tupa tishu zilizotumika mara moja. Kwa nini? Matone husambaza virusi. Kwa kufuata na kuzingatia usafi mzuri wakati wa kupumua, unaweza kuwalinda watu wanaokuzunguka kutokupata maambukizi ya ugonjwa wa virusi vya corona (COVID-19) na virusi vingine kama homa na mafua.

Kama una homa, kikohozi, na shida ya kupumua, tafuta huduma ya matibabu mapema. Kaa nyumbani ikiwa unajisikia vibaya. Tafuta matibabu na upigie simu mapema. Fuata maelekezo ya mamlaka ya afya katika eneo lako. Kwa nini? Mamlaka za kitaifa na za ndani zina habari mpya na za kuaminika juu ya hali katika eneo lako. Kupigia simu mapema kunaruhusu mtoaji wako wa huduma ya afya akuelekeze haraka katika kituo cha afya kinachofaa. Hii itakulinda na itasaidia kuzuia kuenea kwa ugonjwa wa virusi vya corona (COVID-19).

Fanya salamu salama. Ili kuepuka ugonjwa wa vurusi vya corona (COVID-19), ni salama kabisa kuepuka kugusana wakati wa kusalimiana. Salamu salama ni pamoja na kupunga mkono, kutikisa kichwa, au kuinamisha kichwa.

 

Vidokezo vya watangazaji kubaki salama wakati unaendelea kufanya kazi


Pakua habari hii : Kubaki salama wakati unaendelea kufanya kazi

Fanya kazi kwa kukaa mbali. Kila inapowezekana, fanya mahojiano na mikutano na watu kwa njia ya WhatsApp au kwa simu.

Kama ni lazima kufanya mahojiani ya uso kwa uso, heshimu suala la umbali. Funga kijiti kirefu cha selfie kwenye kipaza sauti chako. Pia, simama upande unapofanya mahojiano badala ya uso kwa uso. Ikiwa haiwezekani kufuata suala la kukaa umbali kati yako na unayemuhoji, fikiria kufuta mahojiano.

Jitakase/Jisafishe wewe mwenyewe na vifaa vyako. Jitakase mikono yako kabla ya kuingia studio au kutumia vifaa kama kipaza sauti, meza, dawati, kompyuta na viti na usafishe mikono yako baada ya kumaliza. Safisha vifaa vya sauti kila baada ya kipindi. Safisha kwa maji na sabuni au tumia kitakatishi chenye pombe kufuta. Usisahau kusafisha simu yako ni muhimu!

Linda afya yako ya akili. Hata waandishi wa habari wenye uzoefu zaidi wanaweza kupata shida ya kisaikolojia wakati wanaripoti juu ya ugonjwa wa virusi vya corona (COVID-19). Uongozi wa kituo unapaswa kuwaangalia mara kwa mara wafanyakazi ili kuona jinsi wanavyokabiliana na kutoa mwongozo au msaada. Chukua mapumziko ya mara kwa mara na uzingatie kiwango chako cha nguvu uliyonayo na uchovu, ukikumbuka kuwa watu waliochoka wana uwezekano mkubwa wa kufanya makosa katika kuzingatia usafi wao.

Usiache vifaa vinazagaa wakati ukiwa kwenye shughuli. Pia, tumia kasha gumu kuhifadhi vifaa. Ni rahisi kufuta na kusafisha kasha iliyo ngumu. Weka kila kitu katika kasha wakati ambapo hauvitumii, na funga kasha hilo.

Unapokuwa kwenye uwajibikaji, vaa vifaa vya kujikinga. Hii ni pamoja na glavu zinazoweza kutupwa baada ya kutumika, barakoa, aproni za kujikinga, ovaroli na suti ya mwili, na vifunika viatu vinavyoweza kutupwa baada ya kutumika. Hatari ya kupata maambukizi ni kubwa, kwa hivyo chukua hatua hizi kwa uzito. Ikiwa una shaka, tafuta mwongozo wa kitaalam na mafunzo kabla ya kwenda kufanya kazi.

Zingatia kukaa mbali na watu wagonjwa. Ingawa hospitali na vituo vya afya vinaweza kuwa “mahali palipo na habari kubwa,” fikiria kutotembelea maeneo haya ili kutunza afya yako na usalama wako. Unaweza kuchagua habari zingine zinazohusiana na ugonjwa virusi vya corona (COVID-19). Hii inaweza kumaanisha kuepuka vituo vya afya, vituo vya upimaji, mochwari, kambi za wakimbizi, maeneo ya kutenga watu, maeneo yenye watu wengi au mikusanyiko mijini, au nyumba za wagonjwa.

Jihadhari sana wakati wa kuonana na wazee na wale walio katika hali ya matibabu. Makundi haya ya watu yamo kwenye hatari kubwa ya kuadhirika na ugonjwa wa virusi vya corona (COVID-19), kwa hivyo unaweza kuchagua kufanya mahojiano kwa njia ya simu au WhatsApp. Ikiwa wewe mwenyewe unaangukia katika moja ya makundi haya mwenyewe, unaweza kuamua kukaa nyumbani kwani ni salama zaidi.

Panga mipango na wenzako na familia yako. Jadili mipango ya timu yako ya usimamizi ikiwa wanahitaji kukusaidia au kutoa msaada ikiwa utaugua wakati wa uwajibikaji. Kumbuka kuwa unaweza kuhitaji kujitenga na / au kuwekwa kwenye eneo la karantini/ukanda uliofungwa kwa kipindi kirefu cha muda.

 

Ukweli juu ya hadithi za uwongo, habari potofu na habari za kughushi zinazohusiana na COVID-19


Pakua habari hii : Ukweli juu ya hadithi za uwongo

Hadi leo, hakuna dawa maalum ambazo zimetambuliwa ambazo zinazuia au kutibu ugonjwa wa virusi vya corona (COVID-19).
Watu walioambukizwa wanapaswa kupata utunzaji sahihi wa kupunguza na kutibu dalili. Watu wanaougua au kuumwa sana wanapaswa kupatiwa huduma inayofaa. Matibabu fulani maalum yanachunguzwa, na yatapimwa kupitia majaribio ya kliniki.

Chloroquine sio tiba ya ugonjwa wa virusi vya corona (COVID-19).
Chloroquine inatumika kutibu ugonjwa wa malaria, na inafanyiwa majaribio kama tiba ya ugonjwa wa virusi vya corona (COVID-19). Lakini sio tiba, na majaribio yanaendelea. Kuwa mwangalifu: ingawa chloroquine kwa ujumla ni dawa salama, kumekuwa na baadhi ya kesi zilizoripotiwa za athari hasi za chloroquine.

Kuna uvumi wa uwongo kwamba “Damu ya Kiafrika na ngozi nyeusi inapingana na COVID-19.”
Hakuna ushahidi wa kisayansi kuunga mkono hoja hii. Na Waafrika wengi ni kati ya wale walioambukizwa COVID-19.

Hauwezi kupata ugonjwa wa virusi vya corona (COVID-19) kwa kugusana na wanyama.
Kuna uvumi unaozunguka kwamba kuku na mifugo mingine inaweza kuambukiza binadamu ugonjwa wa virusi vya corona (COVID-19). Uvumi huu ni wa uwongo. Hakuna ushahidi wa kupendekeza kwamba mnyama wa aina yoyote anaweza kuambukiza binadamu ugonjwa wa virusi vya corona (COVID-19). Maambukizi ya binadamu husababishwa na muingiliano kati ya mtu na mtu au kugusana nyuso za vitu vyenye matone yenye virusi.

Kunywa pombe HAKUKUKINGI dhidi ya ugonjwa wa virusi vya corona (COVID-19) na inaweza kuwa hatari.
Kunywa pombe SIO KINGA dhidi ya COVID-19 na inaweza kuwa hatari. Pombe pekee ambayo Shirika la Afya Duniani linapendekeza kutumia kukabiliana na COVID-19 ni vitakatisha mikono vyenye pombe/kilevi. Kwa kweli, kunywa pombe mara kwa mara au kupita kiasi kunaweza kuongeza hatari kwako kwa kupata shida za kiafya kama saratani na uharibifu wa ini.

Chanjo inaweza kuwa tayari katika miezi michache.
Huu ni uwongo. Haiwezekani kwamba kutakuwa na chanjo kwa angalau mwaka

Chanjo dhidi ya pneumonia haiwezi kukulinda dhidi ya ugonjwa wa virusi vya corona (COVID-19).
Virusi vya COVID-19 ni vipya kabisa na tofauti kiasi kwamba vinahitaji chanjo yake vyenyewe. Kwa sasa watafiti wanajaribu kutengeneza chanjo.

Dawa za kuua bakteria HAZINA ufanisi katika kuzuia na kutibu ugonjwa wa virusi vya corona (COVID-19).
Dawa za kuua bakteria hazifanyi kazi dhidi ya virusi, ni kwa bakteria tu. COVID-19 ni virusi na dawa za kuua bakteria hazipaswi kutumiwa kuzuia au kutibu ugonjwa wa virusi vya corona (COVID-19). Walakini, ikiwa umelazwa hospitalini kwasababu ya COVID-19, unaweza kupokea dawa za kuua bakteria kwa ajili ya kutibu maambukizo mengine

Kuna uvumi wa uwongo kwamba vitu vingine vinaweza kuponya au kuzuia maambukizi ya ugonjwa wa virusi vya corona (COVID-19).
Hii ni pamoja na kunywa mchanganyiko wa limao na baking soda, kuvuta mvuke kutoka katika maganda ya machungwa au malimao yaliyochemshwa, kula vyakula vyenye alkali, na kusukutua maji ya chumvi au maji ya ndimu. Kulingana na Shirika la Afya Ulimwenguni, njia ya kuzuia kutokuambukizwa ugonjwa wa virusi vya corona (COVID – 19) na kuzuia virusi kusambaa, ni kuosha mikono yako mara kwa mara, kudumisha angalau umbali wa mita moja kati yako na mtu anayepiga chafya au kukohoa, epuka kugusa uso wako, na funika mdomo wako na pua na kiwiko chako cha mkono au tishu wakati unapokohoa au kupiga chafya

Kuota jua au kukaa kwenya joto zaidi ya nyuzi joto 25 HAKUZUII ugonjwa wa wa virusi vya corona (COVID-19).
Unaweza kupata ugonjwa wa virusi vya corona (COVID-19) bila kujali hali ya jua au joto ilivyo. Nchi zilizo na hali ya hewa ya joto zimeripoti visa vingi vya maambukizi ya ugonjwa wa virusi vya corona (COVID-19). Ili kujikinga, hakikisha unasafisha mikono yako mara kwa mara na epuka kugusa macho yako, mdomo na pua.

Kuna uvumi wa uwongo kwamba “kufanya ngono mara kwa mara huua virusi vya ugonjwa wa corona (COVID-19).”
Kama aina zingine za migusano, ufanyaji ngono unaweza kusababisha hatari ya kuambukizwa.

Kuoga maji ya moto au kutumia kikausha mikono cha joto HAITAKUKINGA wewe kupata maambukizi ya ugonjwa wa wa virusi vya corona (COVID-19).
Kulingana na shirika la Afya Ulimwenguni, tiba zingine zinaweza kusaidia kupunguza dalili za ugonjwa wa virusi vya corona (COVID-19), lakini hakuna ushahidi kwamba dawa yoyote iliyopo sasa au shughuli yoyote inaweza kuzuia au kuponya ugonjwa huo.

Kula vitunguu swaumu HAKUWEZI kusaidia kuzuia maambukizi ya ugonjwa wa virusi vya corona (COVID-19).
Vitunguu swaumu ni chakula cha afya ambacho kinaweza kuwa na viua bakteria. Walakini, hakuna ushahidi kwamba kula vitunguu swaumu kunaweza kuwalinda watu dhidi ya ugonjwa wa virusi vya corona (COVID-19).

Ugonjwa wa virusi vya corona (COVID-19) hauwezi kuambukizwa kupitia kuumwa kwa Mbu.
Hakuna ushahidi kwamba COVID-19 inaweza kuambukizwa na mbu. COVID-19 huenea kupitia matone yanayotokana wakati mtu aliyeambukizwa anakohoa au kupiga chafya, au kupitia matone ya mate au kutoka kwenye pua.

Mawasiliano ya simu kiwango cha 5G HAYASAMBAZI ugonjwa wa virusi vya corona (COVID-19).
Virusi haviwezi kusafiri kwenye mawimbi ya redio au mitandao ya simu. COVID-19 inaenea katika nchi nyingi ambazo hazina mitandao ya simu ya mawimbi yenye kiwango cha 5G.

Kuwa na uwezo wa kushikilia pumzi yako kwa sekunde 10 au zaidi bila kukohoa au kujihisi vibaya HAINA maana huwezi kuwa na ugonjwa wa virusi vya corona (COVID-19).
Shirika la Afya Ulimwenguni linawashauri watu ambao wanafikiria wanaweza kuwa na ugonjwa wa virusi vya corona (COVID-19) kukaa nyumbani na kutafuta matibabu kwa kupiga simu mamlaka zao za kiafya. Njia bora ya kudhibitisha ikiwa unavyo virusi vya COVID-19 ni vipimo vya maabara. Hauwezi kujipima kwa zoezi hili la kupumua, ambalo linaweza kuwa hatari.

 

Baadhi ya ukweli muhimu kuhusu ugonjwa wa virusi vya corona (COVID-19)


Pakua habari hii : Baadhi ya ukweli muhimu

UNAWEZA kupona ugonjwa wa virusi vya corona (COVID-19).
Kupata ugonjwa wa virusi vya corona (COVID-19) haimaanishi utakuwa nao kwa maisha yote. Watu wengi ambao wanapata COVID-19 hupona na virusi kutoka katika miili yao. Ikiwa utapata ugonjwa, hakikisha unatibu dalili zako. Ikiwa una kikohozi, homa, na shida ya kupumua, tafuta huduma ya matibabu mapema – lakini piga simu kituo chako cha afya kwanza. Wagonjwa wengi hupona baada ya uangalizi.

Ugonjwa wa virusi vya corona (COVID-19) hauathiri tu watu wazee –unaathiri watu wa rika zote.
Watu wazee na watu wenye uhitaji wa matibabu kama vile wagonjwa wa moyo, pumu, ugonjwa wa kisukari, na shinikizo la damu huonekana kuwa katika hatari kubwa ya kuathiriwa sana na ugonjwa wa virusi vya corona (COVID-19). Shirika la Afya Ulimwenguni linashauri watu wa rika zote kujikinga na virusi, kwa mfano, kuzingatia usafi mzuri wa mikono na usafi katika kupumua.

Unahitaji kukaa na mtu mwenye maambukizi kwa dakika 10 ili kupata maambukizi ya ugonjwa wa virusi vya corona (COVID-19). Hii ni UONGO. Inawezekana kuambukizwa kwa muda mfupi au kupata virusi kutoka kwa nyuso za vitu vilivyo dondokewa na virusi.

Wakati maji safi hayapatikani, maji chafu kidogo yanafaa dhidi ya ugonjwa wa virusi vya corona (COVID-19) kama utatumia sabuni wakati wa kuosha mikono yako.