Usindikaji wa nafaka kuwa pombe ya kienyeji: shughuli ya uongezaji kipato kwa wanawake

Shughuli za baada ya mavuno

Ujumbe kwa mtangazaji

Save and edit this resource as a Word document.

Muhtasari kwa watangazaji
Tokea kipindi cha hapo awali, kila jamii ilikuwa ikisindika mazao yanayotokana na vyakula vya asili ili kuyaweka katika hali ya usalama kwa matumizi ya familia kula na kunywa. Mazao mengine yaliyosindikwa yalikuwa ni kwa ajili ya kuuza.

Hivyo ndivyo ilivyo kwa nafaka huko Burkina Faso, Nchi iliyo katikati ya Afrika magharibi. Nchini Burkina Faso, Nafaka hasa ulezi mwekundu na mweupe, husindikwa kuwa dolo, au pombe ya kienyeji. Dolo huwa na kileo inaposindikwa na huwa haina kileo inapokuwa haijasindikwa.

Ieleweke kwamba huko Burkina Faso na baadhi ya nchi zingine zinazotumia lugha ya kifaransa huko Afrika magharibi, pombe hii ya kienyeji inasemekana kutengenezwa kwa kutumia “mtama” japokuwa kiuhalisia hutengenezwa kwa ulezi mwekundu au mweupe. Katika matini hii itakuwa ikiitwa “pombe ya ulezi” au Dolo.

Mara nyingi pombe hii ya kienyeji huandaliwa maalumu kwa ajili ya matukio maalumu kama vile sherehe za kijadi, mazishi na sherehe za siku ya uhuru, lakini leo hii ni kinywaji maarufu cha kibiashara ambacho ni salama kwa kunywa na ina kiasi kidogo cha kileo, pia huweza kupatikana katika masoko yote ya mijini na vijijini kote nchini. Utengenezaji wa pombe ya ulezi ni shughuli ya kuongeza kipato inayowaweka wanawake wengi katika hali ya kujishughulisha “katika nchi ya watu waaminifu” Hii ndio maana ya Burkina Faso katika lugha ya Kiswahili.

Mswada huu umejikita katika mahojiano halisi. Unaweza kuutumia kama hamasa ya kuandika mswada wenye mada sawa na huu katika eneo lako, au unaweza kuchagua kutengeneza mswada huu kituoni pako kwa kutumia waigizaji wa sauti kumuwakilisha mzungumzaji mkuu. Kama ndivyo tafadhali hakikisha unawaambia wasikilizaji wako mwanzoni kabisa mwa kipindi kuwa sauti zitakazosikika ni za waigizaji na sio za watu halisi waliohusika katika mahojiano.

Script

MTANGAZAJI:
Bernadette Zongo ni mwanamke mwenye umri wa miaka hamsini. Ameolewa na mwalimu, wana mabinti wawili na kijana mmoja. Mke wa zongo anaishi Ziniaré, mji ullilopo kilomita thelathini na tano kutoka mji mkuu wa Burkina Faso, Ouagadougou.
Mke wa Zongo hakutegemea kila kitu kutoka kwa mumewe. Alitaka kufanya shughuli yoyote ambayo ingeweza kumuingizia kipato. Hivyo mara tu baada ya kuolewa, aliamua kuanza kutengeneza pombe ya ulezi, kinywaji cha kienyeji kinachopendwa na wakazi wa vijijini na mjini. Mke wa zongo ni mwenyekiti wa kikundi cha wanawake wanaotengeneza pombe ya ulezi katika jamii yake. Mwandishi wetu, Adama Zongo, alimhoji ili kuelewa jinsi pombe hiyo inavyotengenezwa. Alianza kwa kutuelezea hatua zinazopitiwa katika utengenezaji wa pombe ya ulezi.
BERNADETTE ZONGO:
(Kwa sauti ya haya) Utengenezaji wa dolo (Maelezo ya mhariri: jina maarufu la pombe ya ulezi nchini Burkina Faso) huhusisha hatua mbalimbali. Hatua ya kwanza ni kupata kimea cha ulezi. Ninapopata kimea cha ulezi, ninakisaga, kisha naongeza maji kwenye kimea cha ulezi kilichosagwa na kusubiri mpaka zile punje za nafaka zituame chini ya chombo. Hatua inayofuata, natengeneza maji ya kunata kwa kuloweka mashina ya mbamia, mboga za majani zenye majimaji kama gundi. Ninachanganya maji haya ya kunata na maji ya kawaida. Kisha nasubiri mpaka kimea cha ulezi kituame chini ya chombo tena.
ADAMA ZONGO:
Hatua inayofuata unafanyaje, Bibi Zongo, mara tu kimea cha ulezi kinapotuama chini ya chombo?
BERNADETTE ZONGO:
Ninautoa ulezi majini na kuuchemsha kwenye moto kwa muda wa saa moja na nusu. Kisha ninaumimina tena kwenye maji yale yale. Maji hayo yanakaa kwa masaa ishirini na nne mpaka yanapokuwa na hali ya uasidi. Kisha ninayafanya yatuame kwa mara ya pili ili kutenganisha makapi na maji ya uasidi.
ADAMA ZONGO:
Unaweza kufafanua “makapi” ni nini?
BERNADETTE ZONGO:
Makapi ni masalia magumu yanayobaki baada ya kutengeneza dolo. Kisha ninarudisha kile kimiminika cha uasidi kwenye moto kwa muda wa masaa mawili. Alafu ninachemsha kwa kutumia mitungi ya udongo wa mfinyanzi iliyochomwa. Ninatumia mitungi; mitano kwa kila pombe inayotengenezwa kutokana na makapi na maji yenye uasidi. Kila mtungi huchukua kiasi cha lita thelathini. Baada ya kuchemsha, ninaacha maji yatuame kwa mara ya mwisho, kisha ninaacha kimiminika kipoe. Halafu ninaongeza hamira. Dolo inakuwa tayari kwa kunywa baada ya siku ya pili ya kuchemshwa.
ADAMA ZONGO:
Sawa, sasa ngoja nieleze kwa muhtasari mchakato mzima kuanzia mwanzo na kuendelea kwa manufaa ya wasikilzaji wetu. Kwanza, unasaga kimea cha ulezi, weka maji kwenye ulezi, na subiri mpaka maji yatulie vizuri.
BERNADETTE ZONGO:
Sawa.

ADAMA ZONGO:
Kisha unaloweka mashina ya mbamia kwenye maji na kuongeza maji ya kunata kwenye maji ya ulezi, alafu subiri ulezi utuame kwa mara nyingine.
BERNADETTE ZONGO:
Sawa kabisa.

ADAMA ZONGO:
Kisha unautoa ulezi majini na kuupika kwa muda wa saa moja na nusu, halafu mimina ulezi kwenye maji yaleyale ulimotoa ulezi.
BERNADETTE ZONGO:
Hapo sawa.

ADAMA ZONGO:
Kisha utayaacha maji yatulie kwa muda wa masaaa 24 mpaka yawe na hali ya uasidi, halafu unayafanya maji yatuame kwa mara ya pili ili kutenganishja makapi na maji.
BERNADETTE ZONGO:
Hapo sawa kabisa. Halafu hatua ya mwisho ni kuchemsha maji hayo kwa muda wa masaa mawili. Baada ya maji kupoa, weka hamira. Kisha subiri kwa masaaa 24 na dolo inakuwa tayari kwa kunywa.
ADAMA ZONGO:
Mchakato huo unahusisha hatua mbalimbali. Kama wasikilizaji wetu wowote wanahitaji taarifa kuhusu mchakato huu, wanaweza kupiga simu.
SFX
Kwenye kituo chetu na tutawaelezea hatua zote.
BERNADETTE ZONGO:
Vizuri sana.

MTANGAZAJI:
Tutarudi mara tu baada ya pumziko fupi kuwaelezea zaidi jinsi Bibi Zongo alivyoboresha maisha yake kutokana na kutengeneza dolo.
SFX
Pumziko fupi la muziki
ADAMA ZONGO:
Utengenezaji wa dolo hutokana na mazao yanayoliwa na binadamu na wanyama. Bibi Zongo anaelewa jinsi ya kupata faida kutokana na mazao hayo.
BERNADETTE ZONGO:
(Tabasamu) Hiyo ni sawa! Mabaki yanayotokana na usindikaji wa kimea cha ulezi kuwa pombe ni makapi na hamira. Ndio, pia hamira hutumika kama mali ghafi katika utengenezaji wa dolo. Lakini kiasi kikubwa cha hamira huzalishwa wakati wa usindikaji wa pombe. Makapi hutumika kama chakula cha ng’ombe na nguruwe, pia hutumika kama chambo kwa ajili ya kulowea samaki. Hamira huongeza ladha ya chakula, na inatumika kuungia nyama ya kuku. Kwa kuuza hivyo vyote vinavyotokana na usindikaji wa pombe, Huwa napata faranga 500 (kama dola 1 ya kimarekani) kwa kila kilo ya hamira, na faranga 2500 (kama dola 5 za kimarekani) kwa kila mkokoteni uliojaa makapi.
ADAMA ZONGO:
Lakini Bibi Zongo hujipatia fedha kiasi kikubwa zaidi ya hicho. Fedha alizopata kutokana na kuuza dolo, alinunua kiwanja cha nyumba ili kuboresha maisha. Kwa kukikodisha kiwanja hicho alijipatia fedha mwishoni mwa kila mwezi. Pia anajishughulisha na ufugaji. Bibi Zongo huwatunza ndama wachache alionunua kutokana na fedha alizopata kwa kuuza pombe ya ulezi. Lakini haitoshi kwa Bibi Zongo kutengeneza dolo na kuiuza. Pia huisambaza katika jiji la Ziniaré.
BERNADETTE ZONGO:
(Kwa kujiamini) Ninauza pombe kwa wafanyabiashara wanawake. Wananunua chupa moja au mbili na kuziuza kwa wateja. Hivyo nao pia wanajipatia kipato kiasi kutokana na mauzo yao. Hivyo basi kila mtu anajipatia faida, hata kama ni kidogo.
ADAMA ZONGO:
Utengenezaji wa dolo ni shughuli ngumu inayohitaji sifa maalum. Bibi Zongo alituambia kwa kifupi kuhusu hilo.
BERNADETTE ZONGO:
Ili kuwa mtengenezaji wa dolo, lazima uwe mwenye afya njema na kuwa na nguvu za kimwili. Ninasema hivyo kwa sababu kazi hiyo haiwezi kumalizika kwa siku moja au nusu siku. Kama tayari unacho kimea cha ulezi, Itakuchukua siku mbili kufanya kazi ngumu. Pia lazima uwe imara kuhakikisha mitungi iko tupu, kuchotea pombe kutoka kwenye ndoo zilizojaa kutoka kwenye chombo kimoja hadi kingine, kubeba mizigo ya kuni kupeleka mahali pa kupikia, na kazi nyinginezo.
ADAMA ZONGO:
Bibi Zongo hutumia kuni kutengeneza dolo, Hutengeneza pombe kila wakati, Bibi Zongo huweka mitungi yenye ujazo wa lita 30 kwenye mafiga ya moto kila mtungi. Tafakari! Ninaamini kuwa Bibi Zongo anataka kuongea…
BERNADETTE ZONGO:
(Bila subira) Unaweza kufikiri ninashiriki katika ukataji wa misitu. Ninatambua kuwa ninatumia kiasi kikubwa cha kuni kutengeneza dolo. Kuni ni chanzo chetu cha nishati. Licha ya kwamba kuni zimezidi kuadimika katika mkoa wetu. Ndio maana nimechagua kutumia mafiga yenye ubora yanayotumia kuni chache na kuhifadhi moto kwa muda mrefu. Mafiga ni kama kifaa cha kupikia ambapo chungu hukaa juu yake. Kuni huingizwa kupitia uwazi uliopo upande mmoja wa mafiga. Hii husaidia mafiga kuwaka kwa ufanisi: hutumia kuni chache, ninaendelea kutumia kuni huku nikisubiri kusimika mtambo wa baiodaijesta. Huu utakuwa wa gharama ya chini na hautatatumia kuni.
ADAMA ZONGO:
Biodijesta ni chombo ambacho kinyesi cha wanyama hubadilishwa na kuzalisha gesi ya methane. Gesi hii inaweza kutumika kupikia, kuangazia na shughuli zingine. Biodigesta ni mtambo wa gharama nafuu na rahisi kuunganisha vifaa vyake. Pia hulinda afya ya Bibi Zongo kwa kumkinga asifikiwe na harufu kali ya moshi wa moto.
MTANGAZAJI:
Wasikilizaji, kipindi cha leo kimekwisha. Kimemleta kwenu mwanamke aliyekuwa akichangia maendeleo ya kiuchumi ya jamii yake kwa kutengeneza dolo. Kwa herini na tutaonana katika kipindi kingine. Kama una swali lolote juu utengenezaji wa dolo, Tafadhali wasiliana nasi kituoni.

Acknowledgements

Imechangiwa na: Adama Gondougo Zongo, mwandishi wa habari wa Jade Productions, Burkina Faso
Imehaririwa na: Barrie Axtell, mshauri wa kujitegemea, kimehaririwa kwa mara ya kwanza na ITDG / Practical Action.
Shukrani kwa: Alfred Kagambèga, meneja wa Vipindi vya Redio Kakoaadb Yam Vénègré
Ziniaré.

Information sources

Mahojiano na Bibi Bernadette Zongo mzaliwa waTapsoba, mtengenezaji wa dolo Ziniaré, Burkina Faso, Desemba 17, 2011

gac-logoMradi umefanywa kwa msaada wa Serikali ya Kanada kupitia Shirika la Maendeleo ya Kimataifa la Kanada (CIDA)