Utangulizi katika kuthibiti magonjwa ya mifugo: Ugonjwa wa mfumo wa hewa na ugonjwa wa kuhara damu

Mifugo na ufugaji nyuki

Backgrounder

Pakua na hariri taarifa hii kwa matumizi yako

Utangulizi:

 
Je ni kwanini somo hili ni muhimu kwa wasikilizaji?

  • Ili wakulima wajue jinsi ya kujihami na ugonjwa wa kuhara damu na ugonjwa wa mfumo wa hewa.
  • Ili wakulima weweze kugundua dalili za ugonjwa wa kuhara damu na ugonjwa wa mfumo wa hewa kwenye mifugo yao na kugundua mifugo iliyoathirika na magonjwa hayo.
  • Ili wakulima waweze kuzingatia usafi wa mabanda ya mifugo yao.
  • Ili wakulima waweze kujua jinsi ugonjwa wa kuhara damu na ugonjwa wa mfumo wa hewa unavyoenea.

Mambo ya msingi

  • Ugonjwa wa kuhara damu na ugonjwa wa mfumo ni magonjwa yanaathiri kuku, ng’ombe, kondoo na mbuzi, lakini hauwezi kusambazwa kati ya mifugo tofauti.
  • Kwenye kuku, ugonjwa wa kuhara damu ni zaidi ya kwenye ndege kuanzia wiki ya 3-4, lakini hushambulia kuanzia siku ya saba na kuendelea.
  • Ugonjwa wa kuhara damu and ugonjwa wa mfumo wa hewa huenea kwa kupitia malisho, maji, kinyesi, na maziwa ambayo yana viambukizi.
  • Wakulima wanapaswa kuweka chakula/malisho na maji kwenye vyombo juu ya kabisa ili kudhibiti maambukizi kutoka kwenye kinyesi cha mifugo.
  • Wakulima wanapaswa kuweka mabanda ya mifugo katika hali kali na ya usafi kwani unyevunyevu na mazingira machafu hupendwa na viambukizi vya ugonjwa wa kuhara damu and ugonjwa wa mfumo wa hewa.
  • Mifugo inaathiriwa na ugonjwa wa mfumo wa hewa na ugonjwa wa kuhara damu na kuku hushambuiwa na ugonjwa wa avian wa kuhara damu.
  • Kuku hushambuliwa na aina mbili za ugonjwa wa kuhara damu. Kuna ugonjwa unaoshambulia utumbo mdogo na mwingine hushambulia utumbo mpana.

Je, kuna changamoto gani katika kuthibiti magonjwa haya?

  • Wakulima hushindwa kugundua maganjwa haya mapema, kwa wakati ambao huweza kutibika, kama inavyoshauriwa na mtaalamu wa mifugo.
  • Wanyama walioathirika hawaonyeshi dalili hivyo huafnya wakulima kutogundua kua mifugo yao inahitaji matibabu.
  • Wakulima kushindwa kuhakikisha mazingira ya usafi kwenye sehemu wanazotunizia mifugo yao.
  • Mifugo inayokula malisho yenye viambukizi vya ugonjwa wa kuhara damu na ugonjwa wa mfumo wa hewa.
  • Wakulima kujaza mifugo huchangia kueneza viambukizi vya ugonjwa wa kuhara damu na ugonjwa wa mfumo wa hewa.
  • Upungufu wa chanjo za ugonjwa wa kuhara damu na ugonjwa wa mfumo wa hewa.

Kwa taarifa zaidi, soma jarida namba 1 – 17.

Taarifa muhimu za kudhibiti ugonjwa wa kuhara damu na ugonjwa wa mfumo wa hewa:

 
Ugonjwa wa kuhara damu:
Ugonjwa huu husababishwa na vimelea na huathiri kuku, ng’ombe, mbuzi na kondoo. Mifugo itakayo kwenye spishi moja huweza kuambukizana ugonjwa huu.

Kuku

Kwenye kuku, kuhara kwa damu huenea moja kwa moja kupita chakula na maji yenye viambukizi na kinyesi na pia huenezwa kupitia kwa panya, vumbi, nzi au vyombo vyenye viambukizi, ndege pori, viatu vilivyo na viambukizi pamoha na nguo.

Aina mbalimbali za viambukizi vya ugonjwa wa kuhara damu huathiri kuku kwa namna tofauti tofauti.

  • Kwenye kuku, aina moja wapo ya viambukizi vya ugonjwa wa kuhara damu hushambulia utumbo mwembamba, sehemu za utumbo mpana ambao hukutana na utumbo mwembamba na kwenye figo.
  • Ndege waliopona na ugonjwa wa kuhara damu huweza kuambukiza viambukizo hivyo kwa ndege wengine kwa miezi sita toka kupona.
  • Ndege wenye umri mkubwa huweza kubeba viambukizi vya ugonjwa wa kuhara damu na kuambukiza ndege wengine, japo hawaonyeshi dalili za kua na ugonjwa huo. Hivyo, inapaswa ndege hao kutenganishwa na ndege ambao hawajaathirika.
  • Bata mzinga na kuku hawawezi kuambukizana. Kwahiyo, hata kama watapata viambukizi vya ugonjwa wa kuhara damu kutoka kwenye kinyesi hawawezi kuugua.

Dalili za ugonjwa wa kuhara damu unaosababishwa na kuathirika kwa utumbo mpana

Ugonjwa wa kuhara damu unashanbulia vifaranga wa wiki 3-12 kupitia sehemu ya utumbo mpana, japokuwa kuku huweza kuathiriwa pia. Ugonjwa wa kuhara damu unaosababishwa na kuathirika kwa utumbo mpana huweza kutokea na kuua kuku bila kuonyesha dalili zozote.

  • Vifaranga vilivyo na ugonjwa wa kuhara damu unaosababishwa na kuathirika kwa utumbo mpana huharisha na kua wanyonge na hufa kwa idadi kubwa.
  • Vifaranga huwa na manyoya yaliyovurugika na hupenda kujificha kwenye sehemu yenye joto.
  • Vifaranga vilivyoathirika na ugonjwa huu huyumba wakati wanatembea na hukaa kwa utulivu huku wakifumba macho na mabawa.
  • Damu huganda kwenye matundu yaliyoko kwenye ngozi.
  • Kuta za utumbo mpana wa kuku walioshambuliwa na ugonjwa huo hua zimegandia damu.

Dalili za ugonjwa wa kuhara damu unaosababishwa na kuathirika kwa utumbo mwembamba

Ugonjwa wa kuhara damu unaosababishwa na kuathirika kwa utumbo wote hushambulia kuku wa miezi 6-8 kwa kuathiri sehemu ya juu, ya kati na ya chini ya utumbo mwembamba. Japo kuku wengine hupona ugonjwa huu, hubaki dhaifu.

  • Kuku walioathirika na ugonjwa huu hawali vizuri na huwa wadhaifu.
  • Rangi ya upanga wa kichwani na ndevu hufifia na miguu hudhoofika.
  • Hukosa hamu ya kula na hupungua uzito.
  • Kuku walioathirika hutembea taratibu.
  • Manyoya huvurugika.

Jinsi ya kujikinga na ugonjwa wa kuhara damu unaosababishwa na kuathirika kwa utumbo mpana na mwembamba

  • Hakikisha mazingira unayofugia kuku ni masafi.
  • Hakikisha unakofugia kuku/mabanda ya kuku hayana unyevu au maji yaliyotuama has maji yenye chakula au kinyesi.
  • Hakikisha vyombo unavyotumia kulishia kuku ni visafi.
  • Hakikisha huweki kuku wengi sana kwenye banda moja.
  • Tumia dawa haraka punde unapogundua vifaranga wako wana dalili ndani ya wiki 3-10 kama kuwa wadhaifu na damu kuganda kwenye matundu ya ngoz au kinyesi cheusi.
  • Kugundua mapema humsaidia mfugaji kutenganisha kuku walioathirika na wale ambao hawajaathirika ili kuzuia kuenea kwa ugonjwa huo.
  • Hakikisah chakula na maji ya kuku wako hayana kinyesi.
  • Osha vyombo vya chakula na maji kwa kutumia maji yaliyochemshwa kuua viambukizi.
  • Hakikisha hauchanganyi kuku wa muda mrefu na vifaranga. Wafugaji wanapaswa kuhakikisha anafuatilia mienendo ya kuku wake.
  • Mfugaji anapaswa kuhakikisha sehemu wanayolalia kuku ni kavu kwani unyevu husababisha viambukizi vya ugonjwa huo kumea.
  • Kuku walioshambuliwa na ugonjwa huo hupaswa kutengwa na kuuwawa au kuchomwa moto.
  • Weka sakafu yenye waya meshi kupunguza maambukizi ya magonjwa hayo kupitia kinyesi.
  • Hakikisha unatoa mabaki/mbolea yote kwa kuchoma au kutumia kwenye mboji mbali na mabanda au sehemu unayofugia kuku wako. Hii itasaidia kupunguza maambukizi ya magonjwa hayo.
  • Baadhi ya madawa ya kutibu magonjwa hayo ni Intracox, Prococ na Sulphaepron.
  • Impextraco ni kampuni ya kimataifa inayotengeneza madawa mbalimbali kwaajili ya kuzuia na kutubu magonjwa hayo kama Saligran, Madimpex, Monsingran, Lerbek, Robimpex, Dufacox, na MNGrow.
  • Dawa ya mifugo inayoitwa Dufacox hupatikana kama kinga ya ugonjwa wa kuhara damu.
  • Kunyunyiza dawa sehemu za kutagia mayai siku ambayo kuku huanza kutaga husaidia kukinga maambukizi ya ugonjwa wa kuhara damu.

Matibabu

  • Ugonjwa wa kuhara damu kwa kuku unaweza kutibiwa kwa kutumia Elanco’s ESB 3, dawa ambayo huwekwa kwenye maji ya kunywa ya kuku. Changanya dawa hio kwenye maji ya kunywa ya kuku kama ilivyoelekezwa kwenye lebo.
  • Pia dawa kama Pluricoccin, Intracox, na Sulphaepron huweza kutumika kutibu ugonjwa wa kuhara damu.

Kwa taarifa, soma jarida 4, 5, 8, 10, 12, 16, na 17.

Mifugo

Ugonjwa wa kuhara damu unaharibu ukuta wa utumbo mpana na mwembamba. Ndama wa miezi 3-9 wana hatari ya kupata ugonjwa huo na huonyesha dalili tofauti tofauti. Hakuna chanjo ya ugonjwa wa kuhara damu lakini mifugo huweza kujenga kinga dhidi ya ugonjwa huo. Viambukizi vya ugonjwa wa kuhara damu huweza kuishi kwa zaidi ya mwaka mmoja kwenye malisho au majani.

Usambaaji

  • Viambukizi vya ugonjwa wa kuhara damu hutoka na kinyesi na kukaa kwenye mbolea. Viambukizi hivyo hupata ndama pale wanapokula au kwenye malisho au wanapokunywa maji.

Dalili

  • Ndama wenye kinga hafifu walioshambuliwa na ugonjwa huo huharisha na kukosa maji mwilini, hukosa hamu ya kula na hukonda na pia kinyesi chake huwa majimaji na chenye damu.
  • Ndama hukosa hamu ya kula na hukonda na mwishowe huweza kufa.

Kinga

  • Hakikisha kua maji ya kunywa na chakula hakina kinyesi.
  • Hakikisha sakafu na sehemu za kulalia ni kavu.
  • Hakikisha vyombo vya kunywea maji vimenyanyuliwa juu ya ardhi au sakafu.
  • Usipendelee kulisha mifugo yako kwa majani yaliyoko pembezoni mwa mifereji au mabwawa.
  • Tenga mifugo iliyoshambuliwa na ugonjwa wa kuhara damu isichanganyike na mifugo mingine kasha itibu.
  • Epuka kufuga mifugo mingi sana kwenye eneo dogo. Mizizi ya mimea iliyoko kwenye eneo la malisho huweza kuhifadhi viambikizi vya ugonjwa wa kuhara damu.
  • Fuga mifugo yako kwenye eneo la malisho lisilo tuamisha maji.
  • Madawa ya mifugo kama Decoquinate, Diclazuril, na Toltrazuril huweza kutumika kwenye mifugo kama kuna mashaka ya kua na mlipuko wa ugonjwa wa kuhara damu au pale kunapokua na historia ya mlipuko wa ugonjwa huo kwenye eneo hilo.

Matibabu

  • Sulfonamides imekua ikitumika kutibu ugonjwa wa kuhara damu lakini imekua hiangamizi ugonjwa huo kabisa. Hata hivyo, ni nzuri kwa kuzuia maambukizi.
  • Amprolium pia ni dawa inayoweza kutumika kutibu ugonjwa wa kuhara damu.

Kwa taarifa zaidi, soma jarida namba 4, 7 na 9.

Kondoo na mbuzi

Mifugo kama kondoo na mbuzi huweza kushambuliwa na ugonjwa wa kuhara damu unaosababishwa na kuathirika kwa utumbo mpana na mwembamba. Ugonjwa huo mara nyingi hushambulia kondoo na mbuzi wadogo wa miezi 4-6. Ugonjwa huo huharibu celi za kwenye utumbo na kusababisha virutubisho vya chakula kutoingia mwilini na hupelekea mfugo kuwa na upungufu wa damu.

Usambaaji

  • Kufuga idadi kubwa ya kondoo na mbuzi kwenye eneo dogo kunakuwa na uwezekano mkubwa wa kuenea kwa ugonjwa huo.
  • Hali ya hewa ikiwa mbaya, mabadiliko ya malisho na kusafiri kutoka eneo moja kwenda lingine huchangia katika kueneza ugonjwa wa kuhara damu kwa kondoo na mbuzi.
  • Viambukizi vya ugonjwa wa kuhara damu unaweza kuenezwa kupitia kinyesi.
  • Ugonjwa wa kuhara damu huweza kuenezwa kupitia matandiko machafu na mazingira machafu na pia kupitia chakula na maji.

Dalili

  • Kondoo na mbuzi wadogo walioshambuliwa na ugonjwa huharisha damu.
  • Kondoo na mbuzi walioshambuliwa na ugonjwa wa kuhara damu huonekana wadhaifu.
  • Kondoo na mbuzi wakubwa kwa wadogo huacha kuongezeka uzito.

Kinga

  • Fuga kondoo na mbuzi wadogo kwenye eneo kavu na safi kuzuia kuenea kwa ugonjwa huo.
  • Wape kondoo na mbuzi chakula chenye virutubisho vyote.
  • Chemsha maji vizuri na uweke ammonia ili kuthibiti ugonjwa huo.
  • Fuga kondoo na mbuzi kwenye eneo tofauti tofauti kulingana na umri wao.
  • Nyanyua juu vifaa vya kuwekea chakula na maji kuthibiti kuingiliwa na viambukizi vya ugonjwa huo.
  • Badilisha badilisha malisho kuzuia maambukizi ya ugonjwa huo.
  • Zuia kinyesi kisikae kwenye sehemu wanayolalia kondoo na mbuzi wako.

Matibabu

  • Anza kutibu mifugo yako yote punde unapoona dalili za ugonjwa wa kuhara damu.
  • Wafugaji huweza kutibu ugonjwa wa kuhara damu kwenye kondoo kwa kutumia antibiotiki iitwayo Monensin, na Lasalocid ya kuzuia bakteria, na dawa iitwayo Decoquinate.

Kwa taarifa zaidi, soma jarida namba 4, 7, 11, na 15.

Ugonjwa wa mfumo wa hewa

Ugonjwa wa mfumo wa hewa unasababishwa na bacteria wanaoshambulia mfumo wa hewa wa kuku na mifugo. Kwenye kuku, ugonjwa huo huitwa ugonjwa wa mfumo wa hewa unaoshambulia ndege na kwenye mifugo ugonjwa huo huitwa ugonjwa wa mfumo wa hewa unashambulia mifugo.

Kuku

Kwenye kuku, ugonjwa unaoshambulia mfumo wa hewa unaenezwa kwa kukaribiana na wanyama walioathirika, matongotongo au majimaji yanayotoka kwenye macho, kwa njia ya hewa na kwenye kiloaka*. Huweza pia kuenezwa kwa upepo. Ndege huweza kupata ugonjwa huo kwa kua au kupita karibu na kuku waliathirika au sehemu wanazo lala kwenye kimvuli. Pia huweza kuenezwa kwa kupitia mayai yaliyovunjika au kuathirika.

Dalili

  • Kuku au ndege walioshambuliwa na ugonjwa wa mfumo wa hewa hukohoa, hupiga chafya, huwa na mafua na hupumua kwa shida.
  • Kuku walioathirika na ugonjwa wa mfumo wa hewa hudhoofika, hukua kwa shida na huvimba kwenye viungo vya miguu.
  • Macho hutoa maji maji.
  • Sehemu ya pua huvimba.
  • Kuku na ndege walioathirika na ugonjwa wa mfumo wa hewa huwa na rangi iliyofifia na hupunguza kutaga mayai.
  • Uso hukosa ung’aavu na manyoya husimama au huchanganyikana.
  • Kuku au ndege waliathirika na ugonjwa wa mfumo wa hewa huharisha kinyesi chenye rangi ya kijani.

Kinga

  • Wafugaji hupaswa kuanza kwa upya kufuga bata mizinga na kuku kwa kuanza na vifaranga au mayai ambayo hayajaathirika na ugonjwa huo.
  • Wafugaji hupaswa kufuatilia maendeleo ya mifugo yao mara kwa mara ili kugundua dalili zozote za ugonjwa huo.
  • Mabanda ya kuku yasafishwe mara kwa mara na mazingira yawe safi wakati wote.
  • Vyombo vya kuhifadhia au kubebea chakula hupaswa kuwa safi wakati wote.
  • Kuku huweza kupatiwa chanjo dhidi ya ugonjwa wa mfumo wa hewa japo uhakika wa ufanisi wa chanjo hio haujathibitika.
  • Kuchinja kuku walioathirika kunazuia kusambaa kwa ugonjwa huko kwa kuku wengine.
  • Kuku walioathirika huweka kuacha majimaji kwenye vyombo vya chakula na kuku ambao hawajaathirika huweza kugusa majimaji hayo na vichwa vyao na kasha kuambukizwa.

Matibabu

  • Antibiotiki huweza kutibu kuku wanaonyesha dalili za ugonjwa wa mfumo wa hewa, japo haziwezi kuangamiza ugonjwa huo kabisa.
  • Antibiotiki aina ya Aivlosin na Elanco’s Tylan Soluble inethibitika kua inaweza kutibu ugonjwa wa mfumo wa hewa.

Kwa taarifa zaidi, soma jarida namba 1 na 6.

Mifugo

Ugonjwa wa mfumo wa hewa unaoshambulia mifugo husababishwa na bacteria na ni vigumu kuutibu. Hushambulia mfumo wa hewa ambapo husababisha masikio kuathirika hasa kwa ndama, wakati ugonjwa wa mgongo, ugonjwa wa kuvimba matiti na numonia, na pia mimba huweza kutoka na macho ya ng’ombe huathirika. Ndama huweza kuathirika hata wakiwa na wiki.

Uenezwaji

  • Ugonjwa wa mfumo wa hewa huenezwa kupitia hewa.
  • Kwenye ndama, ugonjwa huo huenezwa kupitia maziwa ya ng’ombe aliyeathirika.
  • Ngo’mbe wanaoishi kwa kukaribana na kwenye zizi lililofungwa huweza kuambukizana.
  • Ugonjwa wa mfumo wa hewa wa mifugo huweza kuenezwa na mikono ya wakamuaji na vyombo vya kukamulia maziwa. Huenezwa pia na maziwa yaliyona viambukizi na majimaji yatokayo machoni, kwenye pua, kwenye uke na kwenye sehemu ya nyuma.

Dalili

  • Ng’ombe walio na ugonjwa wa mfumo wa hewa hutoa maziwa kidogo japokuwa huweza kuonekana wenye afya nzuri.
  • Maziwa ya ng’ombe walioshambuliwa na ugonjwa wa mfumo wa hewa huwa na maji maji yenye madini ya protini nyingi.
  • Ng’ombe pamoja na ndama walioathirika na ugonjwa wa mfumo wa hewa huwa na homa ya mgongo, na jointi zilizovimba kwenye miguu.
  • Ndama hupindisha vichwa vyao, masikio yao huanguka na hutoa usaha wa njano.
  • Ndama hushindwa kupumua vizuri na masikio huathirika.
  • Ndama na ng’ombe, huweza kupata nimonia, kikohozi na homa.
  • Kwa mfugo wenye umri mkubwa, ugonjwa wa mfumo wa hewa huweza kusababisha matiti kuvimba, macho kuathirika na mimba kutoka.
  • Ugonjwa wa mfumo wa hewa hufanya miguu kuvimba na mapafu kwa ndama, na pia huathiri mfumo wa uzazi kwa ng’pmbe na ndama.
  • Ndama walioshambuliwa na ugonjwa huu hutoa machozi.

Kinga

  • Tenganisha ng’ombe walioshambuliwa na ugonjwa huo na wale wasio shambuliwa na ugonjwa ili kuepusha maambukizi.
  • Kamua ng’ombe walio na ugonjwa wa mfumo wa hewa kwa kutumia vyombo tofauti.
  • Ndama walioshambuliwa na ugonjwa wa mfumo wa hewa wapewe maziwa ya ng’ombe amabo hawajaathirika na ugonjwa huo kuthibiti maambukizi.
  • Wataalamu hushauri kuchinjwa kwa ng’ombe walioshambuliwa na ugonjwa wa mfumo wa hewa has wale wanaovimba matiti kwani ni vigumu kutibika.
  • Tibu mifugo yako punde unapoona dalili za ugonjwa wa mfumo wa hewa. Ndama wanaotibiwa mapema hupona ila inabidi watibiwa ndani ya siku 10 mpaka 14.
  • Kuna chanjo dhidi ya ugonjwa wa mfumo wa hewa. Ng’ombe wenye historia ya kushambuliwa na ugonjwa huo hupaswa kupewa chanjo kabla ya dalili kuonekana.
  • Chanjo kama Pulmo-Guard, MpB, Mycomune, Mycoplasma Bovis bacterin, na Myco-Bac huweza kuzuia ugojwa wa mfumo wa hewa.

Kwa taarifa zaidi, soma jarida nmaba 2, 3, 13, na 14.

Maana ya maneno

 
Anaemia: Ni hali ambayo namba ya chembe chembe nyekundu za damu hupunguza uwezo wake wa kuhifadhi oxijeni. Anaemia inapozidi, husababisha kizunguzungu, na kudhoofika.

Cecal: Ni sehemu ile ambayo utumbo mpana huanza.

Cloaca: Sehemu ya kuku ambayo kusagwa kwa chakula, kizazi na mfumo wa mkojo hukutana.

Je ntapata wapi taarifa zaidi kuhusu mada hii?

 
Dondoo rejea

  1. The Centre for Food Security & Public Health-Iowa State University, 2018. Avian Mycoplasmosis (Mycoplasma gallisepticum). http://www.cfsph.iastate.edu/Factsheets/pdfs/avian_mycoplasmosis_mycoplasma_gallisepticum.pdf (510 KB)
  2. Pfützner, H., and Sachse, K., 1996. Mycoplasma bovis as an agent of mastitis, pneumonia, arthritis and genital disorders in cattle. Scientific and Technical Review of the Office International des Epizooties, 1996, 15 (4), 1477-1494. https://www.oie.int/doc/ged/D9106.PDF (1.16 MB).
  3. DairyNZ, undated. Mycoplasma bovis – what to look out for. https://www.dairynz.co.nz/media/5788128/mycoplasma-bovis-what-to-look-out-for-a3-poster.pdf (631 KB).
  4. Vorster, J.H., and Mapham, P.H., undated, Coccidiosis. http://www.cpdsolutions.co.za/Publications/article_uploads/COCCIDIOSIS.pdf (180 KB).
  5. Pitesky, M., undated. Coccidiosis in Chickens. https://ucanr.edu/sites/poultry/files/201392.pdf (54.3 KB).
  6. Bronson Animal Disease Diagnostic Laboratory, 2013. Mycoplasma gallisepticum and Mycoplasma synoviae in domestic poultry. https://www.freshfromflorida.com/content/download/77376/2221714/Mycoplasma-Brochure.pdf (2.74 MB).
  7. Animal Health Ireland, 2015. Bovine Coccidiosis – The Facts. Parasite Control Leaflet Series, Vol 1, Ver 1, October 2015. https://www.slaneyfarmers.com/documents/Bovine_Coccidiosis_the_facts_(002).pdf (805 KB)
  8. Graham, R., and Brandly, C.A., 1938. Coccidiosis of Poultry. University of Illinois, College of Agricultural Experiment Station and Extension Service in Agriculture and Home Economics, Circular 485. https://www.ideals.illinois.edu/bitstream/handle/2142/33299/1093041.pdf?sequence=2 (2.11 MB).
  9. Kennedy, M.J., 2007. Coccidiosis in Cattle. https://open.alberta.ca/dataset/f3d661cd-cde2-456a-9872-2073e2796cf8/resource/92083fd8-04cb-4622-9a26-cef1841bbcfe/download/2007-663-16.pdf (147 KB)
  10. Ontario Ministry of Food and Rural Affairs, undated. Managing Coccidiosis in my Poultry Flock. https://atrium.lib.uoguelph.ca/xmlui/bitstream/handle/10214/11932/ManagingCoccidiosisInMyPoultryFlock.pdf?sequence=3&isAllowed=y (3.16 MB).
  11. Khodakaram‐Tafti, A., and Hashemnia, M., 2017. An overview of intestinal coccidiosis in sheep and goats. https://www.revmedvet.com/2017/RMV168_9_20.pdf (2.49 MB).
  12. de Gussem, M., 2007. Coccidiosis in poultry: review on diagnosis, control, prevention and interaction with overall gut health. 16th European Symposium on Poultry Nutrition, Strasbourg, France, 26-30 August 2007. https://www.cabi.org/isc/fulltextpdf/2009/20093257328.pdf (201 KB).
  13. Carty, Catherine, 2017. Mycoplasma Bovis. Veterinary Ireland Journal, Volume 7, Number 6, pp. 308-311. http://www.veterinaryirelandjournal.com/images/pdf/large/la_jun_2017.pdf (570 KB).
  14. Wisconsin Veterinary Diagnostic Laboratory, University of Wisconsin-Madison, 2016. Mycoplasma species. https://www.wvdl.wisc.edu/wp-content/uploads/2016/07/Mycoplasma-species-15-08-05.pdf (97.3 KB).
  15. University of Guelph, 2012. Control of Coccidiosis in Lambs and Kids. In Handbook for the Control of Internal Parasites of Sheep and Goats, pp 55-58. https://www.uoguelph.ca/~pmenzies/PDF/Handbook/Handbook_Coccidia_2012.pdf (246 KB).
  16. Novartis Animal Health, undated. Esb3. http://avipharm.co.za/wp-content/uploads/2011/04/ESB3.pdf (159 KB).
  17. Hafez, H.M., 2008. Poultry coccidiosis: prevention and control approaches. Archiv fur Geflugelkunde, 72 (1). S. 2–7, 2008. https://www.european-poultry-science.com/artikel.dll/m07-63mk_NTU4NjM1.PDF (256 KB)

Acknowledgements

Taarifa hizi zimechangiwa na: James Karuga, Agricultural journalist, Kenya
Taarifa hizi zimehakikiwa na: Sylviah Achieng, Elanco.

Tafsiri ya hati hii inafadhiliwa na ELANCO ANIMAL HEALTH