English, Français

Script 104.15

Script

Pakua na hariri taarifa hii kwa matumizi yako

Utangulizi:

 
Mahindi ni zao la muhimu sana nchi za kusini mwa Bara la Afrika, na inaweza kuzalishwa na wakulima katika maeneo mbali mbali bila kumwagiliwa. Kwa kuongeza ni chanzo kikubwa cha chakula kwa mwanadamu, ni zao moja wapo kuu na linalohitajika Zaidi kama chanzo cha chakula cha wanyama. Yote mbegu na sehemu zinginezo za mmea zinaweza kuwa chakula cha wanyama. Mahindi kwa mara ya kwanza ilianza kulimwa kama zao la chakula mika 10,000 iliyopita nchini Mexico. Leo hii wakulima wanazalisha mahindi Zaidi kuliko zao lingine Duniani na mahitaji ya zao la mahindi Duniani inategemewa kuongezeka Zaidi kufikia mwaka 2050.

Mambo muhimu:

 • Mahindi yanakiwango kikubwa cha mavuno, na inastawi katika nchi nyingi za kitropiki.
 • Asilimia 10 ya mbegu ya mahindi inakirutubsho cha protini na asilimia 70 ni wanga na pia inavirutubisho vya vitamin A, E, na riboflavin. Ingawa mahindi lazima kiliwe na vyanzo vingine vyenye chanzo kikubwa cha protini kuhakikisha upatikanaji wa kutosha wa kirutubisho cha protini.
 • Mahindi yanaweza kuwa chanzo kizuri cha chakula kwa wanyama na wanadamu. Sehemu ya mmea inayobaki baada ya kuvunwa inaweza kulishiwa mifugo au kuachwa juu ya shamba na kuoza na kuwa mbolea pamoja na kutunza unyevu wa ardhi.

Kuna changamoto gani kubwa za kulima zao la mahindi?

 • Kupanda aina sahihi ya mbegu katika muda sahihi.
 • Kuzuia ukame au magonjwa.
 • Kukosa mbegu bora za kupanda, mbolea, ushauri, vifaa vya kulimia, au vibarua katika maeneo mbalimbali.
 • Kutunza udongo.
 • Kulima zao la mahindi na mazao mengine.

Matokeo ya Mabadiliko ya hali ya hewa na uzalishaji wa mazao

 • Kupungua kwa mvua na kuongezaka kwa joto katika maeneo mengi kutapelekea kupungua kwa mazao. Kwa baathi ya maeneo mabadiliko ya hali ya nchi yatapelekea kuongezeka kwa uzalishaji wa mahindi, hii ni katika maeneo ya kati.
 • Mabadiliko ya hali ya nchi yanapelekea kuwepo na hali za—ukame mkali, mafurikof—ambayo yanaweza kuharinu mazao ya mahindi shambani.
 • Mabadiliko ya hali ya nchi pia yatapelekea mabadiliko ya namna ambavyo magonjwa yanasambazwa.

Mambo muhimu juu ya uzalishaji wa mahindi

 

1. Ardhi inayofaa na maandalizi ya shamba:
Mahindi yanaweza kupandwa katika maeneo ya kanda juu na kanda za chini, maeneo tambarare na yenye mteremko. Undongo wenye kina kizuri unahitajika katika ukuaji wa mahindi, pamoja na hali sahihi ya unyevu na njia za umwagiliaji. Mafuriko yanaweza kutokea kama hakuna mifumo ya kuingiza na kutoa maji shambani. Kuepuka upotevu wa mazao unaweza kusawazisha shamba, epuka kulima katika maeneo ya mabonde, tengeneza miferegi ya maji au panda katika matuta marefu.

Lini?

 • Uandaaji wa shamba unatakiwa kufanyika muda mfupi kabla ya kupanda mahindi, ili kupunguza nafasi ya magugu kuota.

Inawezekana kulima bila kukwatua shamba

 • Kulima bila kukwatua kunapunguza kusumbua ardhi, na mabaki ya mazao yakiwa yameozea juu ya shamba au yamechanganyika na udongo wa juu. Hii inawezesha udongo juweza kufyonza na kuhifadhi maji ya mvua kwa muda mrefu na kuwa na unyevu muda wote, na pia inaboresha rutuba ya udongo wakati huo ikiwa na haihitaji vibarua wengi wa kulima shamba.
 • Unapofanya kilimo cha kuto kwatua shamba baathi ya wakulima wanakumbana na changamoto ya kuota kwa magugu, au kutamani kutumia mabaki ya mavuno yaliyopita kama chakula cha mmea. Unaweza kujaribu kutolima katika eneo dogo la shamba kwanza kama majaribio kama asilimia (10 ya shamba), na tafuta maarifa kutoka kwa mkulima aliyeendelea au mtaalamu wa kilimo.

Taarifa zaidi: Conservation Agriculture: A Sustainable System

2. Hali ya nzhi

 • Mahindi yanapendelea hali ya joto, lakini yanaweza kuota katika joto kati ya nyuzi 5 na 45. Hali ya baridi sana na joto kali sana juu ya nyuzi joto (32) itasababisha mavuno kudumaa.
 • Mahindi yanaweza kulimwa katika hali tofauti tofauti za joto na ukanda mbalimbali. Kulingana na aina ya mbegu na mazingira, muda wa kupanda unaweza kuwa siku 70 mpaka siku 210.
 • Mahindi yanaweza kuota katika kiwango cha mvua cha mililita 300, lakini kiwango kizuri ni mililita 500 mpaka 700. Mahindi yanaweza kuvumilia kiwango cha mvua mpaka mililita 1200 endapoa shamba lime andaliwa vyema na inamifumo mizuri ya maji.

Kwa kutumia mbegu zinazostahimili joto na kuacha mabaki ya mimea juu ya shamba kunaongeza ubora wa udongo na kuupa uwezo wa kuvumilia ukame.

3. Mbegu
Kuna aina mbili za mbegu sokoni: zilizochavushwa zenyewe kwa zenyewe (OPVs) na mbegu zulizochanganywa aina:

 • Mbegu zilizochavushwa za aina moja OPVs zinaweza kulimwa hata kwa misimu mitatu, lakini OPVs inamazao kidogo kulinganisha na zilezilizochavushawa kwa kuchanganywa za aina mbalimbali.
 • Mbegu zilizochavushwa za mchanganyiko mara nyingi baada ya kupandwa kwa msimu mmoja zinatoa mavuno hafifu. Ni muhimu kununua mbegu kila baada ya msimu.

Inapowezekana tumia mbegu zilizo thibitishwa, ambazo zimekaguliwa wadudu na magonjwa katika hatua zote za uzalishaji.

4. Rutuba ya Udongo
Udongo ni rasilimali muhimu ambayo lazima itunzwe. Rutuba ya udongo inaweza kuongeza uzalishaji, lakini udongo usipo tunzwa vizuri, mavuno yatapungua baada ya muda na udongo utaweza kuharibika kabisa.

 • Kama udongo unamchanga, ongeza rutuba au mbolea ya Naitrojeni (urea). Kuliko kusambaza mbolea au kusambaza samadi, n vyema Zaidi ukaweka kidogo kidogo katika mashina. Weka kiasi kidogo cha mbolea pembeni mwa shimo la mahindi, au weka umbali wa sentimita 5 za mbolea za chumvi.
 • Matumizi ya shamba mara kwa mara yanaweza kupunguza rutuba. Kilimo mzunguko au kuacha shamba lipumzike kwa muda inaweza kusaidia kurudisha rutuba ya udongo iliyopotea.
 • Mahindi yanaota vyema katika kiwango cha pH 5.5 hadi 7.8. Kama udongo unaasidi nyingi, ni vyema kuweka magadi kabla ya kupanda mahindi.

Taarifa zaidi:
Tataizo la Kuharibika kwa udongo na ardhi
Video juu ya rutuba ya udongo barani Afrika

Kuangalia upungufu wa virutubisho
Virutubisho vitatu vinavyohitajika kwa kukuza zao la mahindi ni: Naitrojeni, phosphorasi, na Potasiamu, lakini pia virutubisho vinginevyo vinahitajika.

 • Mmea wenye rangi ya kufubaa na majanimadogo na ukuaji mdogo inaonyesha upungufu wa Naitrojeni, au mara nyngine upungufu wa salfa.
 • Rangi ya uthurungi-nyekundu katika majani na shina inaashiria ukosefu wa fosforasi.
 • Unjano katika kingo za majani kunaweza kunaashiria ukosefu wa Potasiamu.
 • Michirizi ya kupauka juu ya majani inaonyesha upungufu wa madini ya chuma au kopa; mizunguko yenye rangi nyeupe kwenye majani machanga yanaashiria upungufu wa madini ya zinki; na mistari ya njano chini ya majani inamaanisha kunaupungufu wa magnisiamu.

Kwa taarida zaidi: Mwongozo shambani: Kubaini matatizo ya uzalishaji wa mahindi katika nchi za kitropiki

5. Mbinu za upandaji

 • Wakulima wanapaswa kupanda mara tu baada ya mvua za kwanza za msimu kuanza. Mbegu zipandwe kwa kina cha sentimita 5-10, lakini udongo mzito unahitaji kupiga shimo fupi.
 • Kama shamba halijalimwa, zana na vifaa spesho vitahitajika katika kupanda mbegu. Wakulima wanaweza kutumia jembe au vijiti veynye ncha kali kuchimba shimo ya kuweka mbegu, na mbolea ikiwa inawekwa katika shimo jingine la karibu na mbegu. Ripa (ona vyanzo ya taarifa juu ya zana za mikono na wanyama hapo chini) inaweza kuvutwa na wanyama na kutengeneza mitaro mifupi kwaajili ya kuweka mbegu na mbolea . Zana zingine za moja kwa moja ambazo unaweza kutumia katika kupandia mbegu zinaweza kutumika.
 • Baada ya mmea kuonekana, unaweza kurudishia mbegu katika maeneo ambayo mbegu hazijaota.

Kwa taarifa zaidi:
Agriculture Republic of South Africa Factsheet on Maize Production
Manual and Animal Traction Seeding Systems in Conservation Agriculture

Kilimo mseto
Mahindi yanaweza kupandwa pamoja na mazao mengine kama kunde, karanga, maharage, na mbaazi katika eneo moja lashamba na katika msimu mmoja. Hii inasaidia zao moja kuzalishwa na inasaidia kukabiliana na wadudu na kuboresha Udongo. Chagua mazao yenye urefu tofauti, na mzunguko tofauti na maeneo ya ukuaji tofauti.

Kwa taarifa zaidi: Kilimo mseto cha nafaka na jamii ya mikunde kwa njia ya kilimo hifadhi

Kilimo mzunguko
Kuepuka kupanda zao moja mwaka mzima inawezekana kuokoa udongo usiharibike, Kuongeza mavuno na kuhakikisha kilomo kwa kila msimu.

Taarifa zaidi: Umuhimu wa kilimo mzunguko

6. Magugu

 • Kuepuka usumbufu wa magugu, ni muhimu kupalilia maguhu mwaka mzima, hata kipindi ambacho mimea haioti. Haribu magugu yakiwa madogo kwa mikono (chini ya kimo cha sentimita 10) inaweza kuwa njia nzuri sana lakini inachukua muda mrefu.
 • Kukwatua shamba kunasaidia kupunguza magugu, lakini pia unaweza kuzika mbegu za magugu na zinaweza kuota msimu ujao.
 • Kufunika ardhi na kubadilisha mazao kunaweza kusaidia , pamoja na kuacha mabaki ya mmea shambani, lakini itafanya shuguli za palizi kuwa ngumu.
 • Ua gugu linaweza kutumika kuuwa magugu, lakini itumike tu na mtu ambaye najua jinsi ya kutumia bila kuwaathiri wanadamu, wanyama au, kuuwa mazao yenye manufaa.

Taarifa zaidi: Kukabiliana na magugu, wakulima wadogo wadogo wanaofanya kilimo hifadhi

7. Kukabiliana na Magonjwa na Wadudu

 • Mbegu zenye ukinzani na wadudu na magonjwa pamoja na mbinu sahihi za kilimo zinaweza kutumika kukabilina na wadudu.
 • Ukaguzi wa mara kwa mara vijijini ni msingi mzuri wa kukabiliana na wadudu na magonjwa.
 • Udongo wenye afya na mazao ni kinga nzuri dhidi ya wadudu na magonjwa.
 • Kilomo mseto na kilimo mzunguko inaweza kupunguza magonjwa na wadudu.

Kwa taarifa zaidi:
Magonjwa ya mahindi: Mwongozo wa namna ya kukagua shamba
Wadudu waharibifu wa mahindi: Mwongozo wa namna ya kukagua mashamba

8. Uvinaji

 • Mahindi yanaweza kuvunwa yanapokuwa yakijani kwaajili ya kupikwa , au baada ya mahindi kukauka.
 • Baada ya kuvuna mbegu za mahindi zinaweza kukaushwa kwenye jua ili zikae kwa muda mrefu na inaweza kuhifadhiwa vizuri, na inawea kupata bei nzuri sokoni.
 • Kujua kuwa mahndi yamekauka vizuri, weka chumvi na mahindi kwenye chombo cha kioo na tikisha kwa muda,.Kama chumvi ikinata kwenye kuta za chupa baada ya dakika kadhaa, basi mahndi hayajakauka vizuri.

Wapi ninaweza kupata vyanzo mbalimbali vyenye taarifa za ziada kama hizi?

 1. IIRR na ACT, 2005. Kilimo hifadhi: Mwongozo kwa wakulima na maafisa ugani Afrika. Shirika la kimataifa la uboreshaji wa mbinu za ukuaji vijijini, Nairobi; Afrika Ukwatuaji katika kilimo hifadhi, Harare. http://www.fao.org/ag/ca/AfricaTrainingManual.html
 2. Tovuti ya taarifa zinazopatikana, ni tovuti yenye video a maelezo juu ya mada mbali mbali za kilimo, iikiwemo uzalishaji wa mahindi: http://www.accessagriculture.org/category/53/Maize
 3. Lafitte, H. R., 1993. Utambuzi wa matatizo katika uzalishaji wa mahindi katika nchi za kitropiki: Mwongozo wa shughuli za shambani. Mexico, D.F.: CIMMYT. Kutambua matatizo katika uzalishaji wa mahindi katika nchi za kitropiki: Mwongozo wa shughuli za shambani
 4. TECA: Mbinu na Teknolojia kwa wakulima wadogowadogo http://teca.fao.org/
 5. CIMMYT Dondoo za kilimo hifadhi

Acknowledgements

Imechangiwa na: Sam Storr, Mtaalamu wa mawasiliano, CIMMYT (Centro Internacional de Mejoramiento de Maíz y Trigo).
Imehaririwa na: Tsedeke Abate, Kiongozi wa mradi, STMA (Mbegu za mahindi zenye ustahimili Afrika), CIMMYT; Walter Mupangwa, Mtaalamu wa Mifumo ya umwagiliaji ya kilimo, Sustainable Intensification Program (SIP), CIMMYT.

 
gac-logoMradi umefadhiliwa na serikali ya Kanada kupitia kitengo cha mambo ya mahusiano ya nje Kanada (GAC)

This work was translated with the support of AGRA, the Alliance for a Green Revolution in Africa, as part of the project, “Integrated project to increase income and improve food security and livelihood among smallholder farmers in the Western Tanzania/ Kigoma region.” The views expressed in this resource do not necessarily reflect those of AGRA or any other organization.