Ujumbe kwa mtangazaji
Save and edit this resource as a Word document.
Maelezo kwa mtangaaji
Kufuga ng’ombe ni shughuli kuu kwa wafugaji katika vijiji na katika idara ya Noun katika eneo la magharibi la nchi ya Kameruni. Lakini ufugaji wa ng’ombe una matatizo kadhaa. Katika mwezi wa nane wa muda mrefu wa msimu wa ukame, nyasi nzuri huwa haba sana. Wanyama wanalazimishwa kusafiri umbali mrefu kupata malisho. Majani machache ya nyasi yanayopatikana tayari yameshaliwa na wanyama wengine, ambao wameacha vinyesi vyao na mkojo kwa ajili ya ukuaji wa chakula kingine baadaye. Nyasi kidogo iliyobaki mara nyingi huchanganyika na mabuu kutoka vimelea vya ndani ambavyo vinaweza kupita kwenye mifugo inayokuja kujilisha msimu ujao. (Vimelea huitwa mabuu wakati wa ukuaji, hii ni katika hatua ya funza kuelekea kukomaa.)
Katika mapambano yake dhidi ya umasikini, serikali inafanya jitihada za kusaidia wakazi wake. Idara za Serikali katika Noun zinaandaa kampeni ya chanjo angalau mara nne kwa mwaka. Kampeni hizi hupunguza uwezekano wa maambuzi ya magonjwa kwa mifugo. Mara baada ya kuambukizwa, athari huwa ni mbaya na ni tatizo kubwa sana. Wakati mwingine wakulima wanaweza kupoteza theluthi ya mifugo yao.
Muongozo huu unategemea mazungumzo kati ya wahusika watatu wakuu: mwenyeji wa redio, mfugaji wa ng’ombe na mtaalam wa mifugo. Unaweza kuurekebisha muongozo huu ili kukidhi mahitaji yako. Unaweza pia kuwaweka wahusika wapya kuoanisha na hao walio
katika jumii yako.
Muongozo huu unategemea mahojiano halisi. Unaweza kutumia muongozo huu kama msukumo wa utafiti na kuandika muongozo wako kwenye mada sawa katika eneo lako. Au unaweza kuchagua kuzalisha muongozo huu kwenye kituo chako, kwa kutumia watendaji wa sauti kuwakilisha wasemaji. Ikiwa ndivyo, tafadhali hakikisha unawaambia wasikilizaji wako mwanzoni mwa kipindi kwamba sauti ni ya washiriki, sio watu wa awali waliohusika katika mahojiano.
Script
MWENYEJI:
Ndugu, marafiki wapenzi na wasikilizaji! Tupo katikati ya mbuga ya nyika mbele na kando kidogo ya sehemu ambako ng’ombe maksai wanapewa chanjo. Kijiji cha Didango kipo kilomita ishirini kutoka mji wa Foumban. Foumban ipo katika Idara ya Noun, katika Wilaya ya Magharibi ya Kameruni. Wanyama wa kufugwa ni chanzo kikuu cha maisha kwa asilimia 90% ya watu huko Didango. Wafugaji katika jamii hii zaidi hufuga ng’ombe maksai. Ndiyo maana ni muhimu sana kuangalia kuhusu minyoo kama chanzo cha magonjwa ya kuambukiza.
Hapa Didango, ng’ombe za mfugaji Baba Abdou wamekusanyika katika eneo ambalo Daktari wa mifugo Issofa Mkpoumie anafanya kazi. Kila wakati mtaalam wa mifugo anapochanja mifugo ama kutoa tiba nyingine kwa ng’ombe, mfugaji anachofanya ni kutambua wanyama ambao tayari wamechanjwa.
Wasikilizaji wapenzi, kujadili suala hili zaidi, mfugaji na mtaalam wa mifugo wameungana nasi. Unasikiliza toleo maalum la kipindi chetu, ambayo inaitwa “Nfuse ne pata’a,” yenye maana ya “utajiri wa ardhi na mifugo.” Tunatarajia kwamba wasikilizaji wetu watafaidika na ushauri wa mtaalam wa mifugo Issofa Mkpoumie na uzoefu wa wafugaji wenzao, Baba Abdou. Bila shaka, ushauri bora kwa wafugaji unaweza tu kutoka kwa wafugaji wenyewe.
Halo Baba Abdou. Halo Issofa Mkpoumie. Kwa hiyo, Bwana Abdou, unaweza kutuambia nini juu ya minyoo?
BABA ABDOU:
Minyoo hawa ni wadudu ambao hawaonekani kwa macho. Lakini tunaweza kuona athari zao katika mifugo kwa kupoteza hamu ya kula, kupoteza uzito, na tabia isiyo ya kawaida. Mfano wa tabia isiyo ya kawaida ni wanyama kukataa kusafiri umbali mrefu kwa sababu wamekuwa dhaifu. Ili kutibu dalili hizi, tunawapa mchanganyiko wa mitishamba na mimea mingine. Lakini matokeo wakati mwingine sio mazuri. Wakati mwingine hatutumii kipimo sahihi au matibabu ya asili hayana mafanikio sana dhidi ya minyoo. Ndiyo sababu wakati mwingine tunatumia bidhaa za kisasa kama vile Vermifuge 2000 na Ivermectin inayotumika kuwaua.
MWENYEJI:
Bwana Daktari wa mifugo, unaweza kutuambia nini juu ya minyoo?
ISSOFA MKPOUMIE:
Ng’ombe hula bila kujali viumbe vidogo vidogo wanavyomeza na vimelea vilivyokomaa vinavyowaambukiza magonjwa. Hatua ya ukuaji wa vimelea hivi kabla ya kukomaa huitwa mabuu. Madhara yao yanakuwepo pale vyakula vya mifugo vinapokuwa vimeambukizwa na vinyesi vya wanyama waliokuwa tayari na magonjwa. Hiyo ndivyo vile vidudu vinavyoletwa katika miili ya wanyama wetu. Wanyama wetu pia hukutana na minyoo kwa kunywa maji ya mito ambayo imenajisiwa na vinyesi ya ng’ombe iliyoathirika na vimelea.
MWENYEJI:
Wafugaji wanatibuje minyoo?
BABA ABDOU:
Wanajaribu kuzuia maambukizi ya minyoo kwa kufuata sheria za usafi zilizoshauriwa na kuelekezwa na wataalam wa mifugo. Kwa mfano, wafugaji wanapaswa kuwatoa mifugo nje wakati wa maawio yaani baada ya jua linapochomoza, wakati jua limekausha umande wa asubuhi kutoka kwenye nyasi. Hii inapunguza idadi ya mabuu ambayo hujishika katika nyasi. Tunapoona kwamba wanyama wameambukizwa, tunawapa kidonge kinachoitwa Levacip Bolus.
MWENYEJI:
Je, unawapaje wanyama kidonge?
BABA ABDOU:
Usiku, wakati ng’ombe wapo ndani ya zizi au nyumba yao, tunamkamata kila mnyama na kumpa kidonge kikubwa, kinachoitwa bolus, kupitia kinywa na bomba ndogo ya bolus. Ni kazi ngumu wakati kundi ni kubwa.
MWENYEJI:
Je, minyoo hao wanaweza kuambukiza wanadamu?
ISSOFA MKPOUMIE:
Kusema kweli, sijui ni magonjwa gani ambayo yanaweza kusababisha katika mwili wa binadamu. Hata hivyo, tunashauri kwamba nyama ipikwe vizuri iive kabisa ili kuepuka hatari zote.
BABA ABDOU:
Mbali na hatari za maambukizi kupitia nyama isiyopikwa vizuri, watu wanapaswa pia kuepuka kushika mkojo wa mifugo na kinyesi ili kuepuka viumbe vingine vinavyoishi katika mfumo wa utumbo wa ng’ombe.
MWENYEJI:
Je! Una ushauri wowote kwa wafugaji wenzako?
BABA ABDOU:
Kaa chonjo muda wote. Waangalie wanyama wako kila siku kwa hali yoyote isiyo ya kawaida, kama wakikataa kwenda umbali mrefu. Ikiwa unapata chochote ulicho nacho wasiwasi, wasiliana na mtaalam wa mifugo haraka iwezekanavyo. Afya ya mifugo yako inakutegemea sana. Ninawahimiza wafugaji wa ng’ombe wafuate ratiba za chanjo ili kulinda mifugo yao. Tafadhali wasiliana nasi mara tu unapogundua hali isiyo ya kawaida.
MWENYEJI:
Sasa nitauliza maswali kwa Maloum, ambaye ni mkulima wa kwanza na pia tabibu wa kiroho!
MALOUM:
Bwana. Mwanahabari, unauliza maswali mengi sana!
MALOUM:
Sasa, ni wakati wangu kuuliza maswali.
MWENYEJI:
Kwanini usiulize?
MALOUM:
Umesahau kipengele kimoja.
MALOUM:
Kuna imani kwa wafugaji wengine kwamba wanyama wanaweza kulaaniwa. Wafugaji wengi bado wanaamini kwamba kama wanyama wao ni wagonjwa, lazima iwe kwa sababu adui amewapa mabaya juu yao. Mazoea haya ya jadi hayawezi kuwa ya kawaida kama ya zamani, lakini kwa bahati mbaya wanaendelea kuwa na wasiwasi katika ufugaji, ambao mara nyingi huwaambia: “Nina hakika kwamba kuwapoteza wanyama wangu sio tu kuhusiana na magonjwa. Mifugo yangu iliyokua ikiongezeka kwa hakika imeunda wivu. Tafadhali nisaidie kulipiza kisasi.”
MWENYEJI:
Maloum, wewe ni mfugaji. Una ujumbe wowote kwa wafugaji wenzako?
MALOUM:
Wapenzi wafugaji wenzangu: Ujinga ni kweli ndio unaotufanya kushindwa kuwa bora kwa muda sasa. Inachukua nafasi sawa na matako yetu, daima huwa nyuma. Tafadhali, hebu tuache kusema na kuamini kuwa uchawi unaharibu wanyama wetu! Badala yake, ikiwa kuna kitu kibaya kwa wanyama wetu, hebu tuende tukamuone mtaalam wa mifugo.
MWENYEJI:
Bwana Daktari wa Mifugo, unataka kusema nini kuhusiana na hilo?
VETERINARIAN:
Nadhani kila mkulima anapaswa kuchukua majukumu yake kwa uzito. Tuko hapa kukutumikia. Tafadhali, usisubiri mabaya zaidi yatokee, na kisha utafute visingizio.
MWENYEJI:
Hakika, katika maisha, ikiwa kuna kitu kinachopaswa kuepukwa, ni ujinga. Mara nyingine tena, nataka kumshukuru rafiki yangu Maloum kwa kutukumbusha tatizo hili kubwa. Leo, tumejadili kuhusu magonjwa ya ng’ombe kwa ujumla, na kukazia hasa kuhusu wadudu aina ya minyoo. Ikiwa ulifuatana nasi, usisahau kuwashirikisha na wengine yale uliyojifunza. Mpaka tukutane tena juma lijalo, Kwaheri!
Acknowledgements
Shukrani
Imetolewa na: Josue Yaneya, Rais Communautaire du Noun, Foumban, Kameruni, Mdau wa Utangazaji wa shirika la kimataifa la Redio kwa Mkulima.
Imepitiwa na: Terry S. Wollen, Mkurugenzi wa Utetezi wa Mifugo, Shirika la kimataifa la Heifer.
Mpango uliofanywa na msaada wa kifedha wa Serikali ya Kanada kupitia Shirika la Maendeleo la Kimataifa la Kanada (CIDA)
Tafsiri ya hati hii inafadhiliwa na ELANCO ANIMAL HEALTH