Backgrounder
Utangulizi
Umewahi kufikiria kuhusu utofauti wa ajabu wa viumbe hai duniani? Kuanzia wadudu wadogo hadi tembo wenye nguvu, utofauti huu unaitwa bayoanuwai. Lakini bioanuwai siyo tu vitu vya kupendeza – ni msingi wa sayari yenye afya na ustawi wetu.
Bioanuwai ni nini?
Bayoanuwai, ambayo ni kifupi cha anuwai ya kibiolojia, ni utofauti wa aina zote za maisha duniani katika ngazi zote, kutoka kwenye jenetiki na spishi hadi mifumo ya mazingira; kuanzia vijidudu vidogo hadi mamalia wakubwa, na kila kitu kilichomo katikati. Inahusisha spishi mbalimbali, utofauti wa kijenetiki ndani ya spishi hizo, na mifumo mbalimbali ya mazingira ambako viumbe hivi vinaishi. Kuelewa bioanuwai ni muhimu kwasababu inatufanya tuthamini utajiri wa maisha yanayotuzunguka na mtandao tata unaounganisha viumbe hai wote.
Bayoanuwai haijumuishi tu spishi adimu, zilizo hatarini, au zilizo hatarini kutoweka bali pia kila kiumbe hai, kuanzia wanadamu hadi mimea, wanyama, vijidudu, fangasi, na wanyama wasio na uti wa mgongo. Kwa maneno rahisi, bayoanuwai inahusu viumbe hai mbalimbali duniani na tofauti zao.
Viwango vya Bayoanuwai
Jenetiki (Utofauti wa Kijenetiki): Hii inahusu aina mbalimbali za jenetiki au DNA zilizopo ndani ya spishi na idadi ya viumbe. Jenetiki ni kama maelekezo yanayoelekeza jinsi kiumbe kitakavyokua, kustawi, na kufanya kazi. Idadi ya jenetiki inatofautiana kati ya viumbe, kutoka takriban 1,000 katika bakteria hadi 10,000 katika baadhi ya fangasi na kufikia takriban 100,000 kwa mamalia wa kawaida. Mfano wa utofauti wa jenetiki ni utofauti katika mbegu za mbwa, au aina mbalimbali za maembe, mchele, n.k.
Spishi (Utofauti wa Spishi): Spishi ni kundi la viumbe hai ambao wapo sawa au wanafanana katika eneo fulani. Viumbe wa spishi moja wana sifa zinazofanana na wanaweza kustawi pamoja na kuzaliana ili kuzaa kizazi kinachoweza kuishi. Kwa mfano, wanadamu wote ni spishi moja. Kwa mfano, ikiwa msitu una utofauti, unaweza kuwa na spishi nyingi tofauti za miti.
Mfumo wa Ikolojia (Utofauti wa Mifumo ya Ikolojia): Ikolojia ni kama jamii au ujirani ambapo mimea, wanyama, na viumbe vidogo wanaishi pamoja na kuingiliana na mazingira yao, kama vile ardhi, maji, na hewa. Katika “ujirani,” huu, kila kiumbe hai kina jukumu na vyote vinategemeana ili kuishi. Kwamfano, katika ikolojia ya msitu, miti hutoa oksijeni na makazi, wanyama hula mimea au wanyama wengine, na viumbe vidogo vinavunja vunja vitu vilivyokufa, kuweka ikolojia katika hali ya usawa na afya.
Ufafanuzi wa baadhi ya misamiati ya bayoanuwai
- Hifadhi ya Bayoanuwai: Ni zoezi la kulinda na kusimamia anuwai ya viumbe ili kuhakikisha afya yake ya muda mrefu na uhai, hivyo, kudumisha usawa wa asili na afya ya sayari yetu.
- Kupotea kwa Bayoanuwai: Kupungua kwa anuwai ya viumbe katika eneo Fulani
- Hali ya uhifadhi: Onyesho la jinsi spishi inavyoweza kuishi. Mfano: enye kuweza kudhuriwa, iliyo hatarini, au iliyokufa.
- Ikolojia: Aina ya biolojia inayoshughulika na uhusiano na mwingiliano kati ya viumbe hai na mazingira yao, ikiwa ni pamoja na viumbe wengine.
- Huduma za mifumo ya ikolojia: Manufaa wanayopata wanadamu kutoka kwenye mifumo ya ikolojia. Mfano: Maji safi, hewa, na uchavushaji wa mazao.
- Spishi zilizo hatarini kutoweka: Aina zilizo katika hatari ya kutoweka kwa sababu ya mabadiliko ya kimazingira kama vile shughuli za binadamu au mabadiliko ya tabianchi. Kwa mfano, Chui wakubwa wenye milia na vifaru.
- Habitat: Makazu ya asili ya spishi zote.
- Spishi vamizi: Mimea au wanyama wanaoingizwa kwenye eneo jipya ambao hudhuru spishi za asili katika eneo hilo.
- Uvuvi kupita kiasi: Kuvua samaki wengi kwa wakati fulani bila kuwaruhusu kuzaliana.
- Kiumbe mdogo: Kiumbe mdogo anayeweza kuonekana kwa macho.
- Kiumbe mdogo sana: Kiumbe mdogo sana ambaye anaweza kuonekana tu kwa kutumia darubini, hasa bakteria.
- Mazoea Endelevu: Kutumia rasilimali kwa njia ambayo haidhuru mazingira. Kama vile kuwa na kanuni za kusimamia uvuvi ili kuzuia uvuvi wa kupita kiasi.
- Ujangili: Uwindaji haramu wa wanyama. Mfano: Kuua tembo kwa ajili ya pembe zao.
- Mtawanyiko wa miji: Upanuzi wa miji mpaka kwenye maeneo ya asili. Mfano: Kujenga vitongoji vipya vinavyoharibu makazi ya wanyamapori.
Taarifa muhimu kuhusu Bayoanuwai
Aina za Ikolojia
Mifumo ikolojia ya nchi kavu: Hizi ni mifumo ikolojia inayotegemea ardhi
Mifumo ya ikolojia ya misitu ni changamano ya spishi nyingi za miti, wanyama, fangasi na bakteria zikiingiliana. Aina mbalimbali za mimea na wanyama wanaopatikana katika misitu, ikiwa ni pamoja na miti, vichaka, mimea ya dawa, na viumbe vidogo. Misitu ya mvua ya kitropiki barani Afrika ina aina nyingi sana. Mifano ni, Msitu wa Mvua wa Kongo (Afrika ya Kati), Msitu wa Atewa (Afrika Magharibi), na Msitu wa Kakamega (Afrika Mashariki).
Mifumo ya ikolojia ya nyasi inatawaliwa na nyasi fupi kuliko misitu. Savanna za Afrika ni aina ya mfumo wa ikolojia wa nyasi. Mfano: Serengeti (Tanzania)
Mifumo ya ikolojia ya jangwa ni kavu sana na mimea michache. Jangwa la Sahara katika Afrika Kaskazini ni mfano. Ardhi kavu na yenye unyevunyevu ina sifa ya upatikanaji mdogo wa maji na ni makazi ya spishi za kipekee na zilizobadilika kukabiliana na mazingira hayo
Mifumo ya ikolojia ya milima iko katika miinuko ya juu na ina mimea na wanyama wa kipekee wanaozoea hali ya baridi na hali ngumu. Mfano ni Milima ya Rwenzori (Uganda) na Milima ya Drakensberg (Afrika Kusini)
Mifumo ikolojia ya majini (maji ya bara, baharini na pwani): Hii ni mifumo ikolojia inayotegemea maji, ikijumuisha maji safi (maziwa, mito, ardhioevu) na baharini (bahari, mito, miamba ya matumbawe).
- Mifumo ya ikolojia ya maji safi kama Ziwa Victoria katika Afrika Mashariki ina samaki, mimea, na viumbe vingine vilivyozoea maji yasiyo na chumvi.
- Mifumo ya ikolojia ya baharini kama vile misitu ya mikoko ya pwani ya Ghana ina aina mbalimbali za viumbe vya baharini.
Mifumo ya ikolojia ya Bandia: Hii ni mifumo ya ikolojia inayotengenezwa na binadamu, kama vile mashamba ya kilimo, bustani, na mabwawa ya samaki.
- Mashamba ya mazao na mashamba ya mimea ni mifumo ya ikolojia ya bandia iliyotengenezwa na binadamu kwa ajili ya uzalishaji wa chakula.
Kwanini bayoanuwai ni muhimu?
Manufaa ya bayoanuwai ya mimea, wanyama, rasilimali za maji, na viumbe vidogo ni makubwa. Manufaa hayo ni pamoja na:
- kiuchumi (chanzo cha mapato ya vijijini na mijini, mapato ya mauzo ya nje),
- kijamii (kama vyanzo vya chakula na usalama wa chakula, dawa kwa ajili ya kudumisha afya na tiba ya magonjwa na maradhi),
- kidini na kitamaduni (njia ya msukumo wa kiroho),
- urembo na burudani,
- kiikolojia (ulinzi wa maeneo ya vyanzo vya maji na vyanzo vya maji, vizuizi vya upepo/dhoruba, urejeshaji wa misitu, utunzaji wa rutuba ya udongo, n.k.),
- na kimazingira (udumishaji wa viwango vya kaboni angani, ufyonzaji wa uchafuzi wa mazingira, nk).
Bila bayoanuwai, hakuna maisha. Kila kiumbe kidogo katika mfumo wa ikolojia kina jukumu muhimu na kina umuhimu kwasababu kadhaa. Bayoanuwai ni muhimu katika nyanja mbalimbali kama ilivyoelezewa kwa kifupi hapa chini:
- Msaada katika kuendeleza maisha: Viumbe vyote au viumbe hai vinavyojumuisha wanadamu katika viwango vyote vya bayoanuwai vimeunganishwa. Bayoanuwai inasaidia huduma muhimu za mfumo ikolojia ambazo ni muhimu kwa maisha yetu, kama vile uzalishaji wa chakula, udhibiti wa hali ya hewa, na kuzungusha virutubisho. Kwa mfano, mifumo mbalimbali ya ikolojia kama misitu na ardhioevu husaidia kuwa na hali ya hewa ya wastani na kutoa maji safi.
- Afya ya udongo: Fangasi na bakteria kwenye udongo huvunja vunja vitu vya kikaboni, na kutengeneza virutubisho muhimu kwa ukuaji wa mimea. Utaratibu huu husaidia kudumisha rutuba ya udongo na kusaidia uzalishaji katika kilimo.
- Rasilimali za dawa: Michanganyiko mingi ya dawa hutokana na mimea na wanyama muhimu kwa kutibu magonjwa na kuboresha afya. Kuhifadhi bayoanuwai hutusaidia kugundua matibabu mapya. Kwa mfano;
- Mmea wa Pink quarantus unatumika kutibu kansa
- Magome ya mti wa Mwiluti – Prunus africana (African Cherry) hutumika kutibu masuala ya tezi dume,
- Nchini Ghana, Mlonge mara nyingi huitwa “mti wa miujiza,” kwa kuwa majani na mbegu zake hutumiwa kwa manufaa mbalimbali ya kiafya.
Burudani na afya ya akili: Bayoanuwai huwasaidia watu katika maeneo ya mijini kuwa wastahimilivu zaidi kwa kupunguza msongo wa mawazo na kuboresha afya ya akili. Maeneo yenye kijani kibichi, kama vile hifadhi na misitu, katika miji hutoa mahali pa kupumnzika na burudani. Wakati fulani, madaktari wanaweza kupendekeza mtu kutumia muda zaidi katika maeneo ya asili kwa wale ambao wanaougua masuala mbalimbali ya afya, ikiwa ni pamoja na huzuni na sonona. Burudani na shughuli za kimwili pia ni muhimu kwa kudumisha afya ya kimwili na ya akili.
Utalii wa Ikolojia: Hii ni moja ya thamani za kiuchumi. Bayoanuwai inasaidia utalii wa mazingira, kwani wageni huvutiwa na maeneo ya asili, kusaidia uchumi wa maeneo hayo na kukuza ufahamu wa mazingira. Utalii wa kiikolojia na matumizi endelevu ya rasilimali za bayoanuwai hutengeneza ajira na kusaidia uchumi wa eneo hilo. Mifano ni pamoja na safari katika hifadhi za wanyamapori barani Afrika,
- Maasai Mara, Kenya: Inajulikana kwa kuwa na wanyamapori wengi, pia Uhamaji Mkubwa wa Nyumbu,
- Hifadhi ya Taifa ya Kruger, Afrika Kusini: Hutoa safari za kitalii kuwaona “Wanyama watano Wakibwa – Big Five” (simba, chui, vifaru, tembo, na nyati).
- Hifadhi ya Taifa ya Kakum, Ghana: Maarufu kwa njia za kutembea ndani ya misitu, ambayo inatoa mwonekano wa kipekee wa mimea na wanyama mbalimbali wa msitu wa mvua.
- Hifadhi ya Kitaifa ya Mole, Ghana: Inajulikana kwa idadi kubwa ya tembo na wanyamapori wengine, hivyo kuvutia watalii kufanya safari.
- Hifadhi ya Misitu ya Cape Three Points, Ghana: Huvutia wageni wanaopenda kutazama ndege na kutalii mazingira ya pwani.
- Msitu usiopenyeka wa Bwindi, Uganda: Mahali pa sokwe wa milimani, unaovutia watalii kwa safari za kwenda kuwaona sokwe.
Uhifadhi wa urithi wa kitamaduni na kiroho na ustawi: Tamaduni nyingi za Kiafrika, ikiwa ni pamoja na makabila mbalimbali ya Ghana, yanaingiliana kwa kina na viumbe hai na desturi za jadi na imani za kiroho. Watu wengi hupata manufaa ya kitamaduni, kiroho, na burudani kutokana na viumbe hai. Wanyama na mimea fulani huwa na umuhimu mtakatifu au wa kiishara ndani ya tamaduni hizi. Kwa mfano, wanyama na mimea fulani huchukuliwa kuwa takatifu au ishara katika makabila mbalimbali ya Ghana. Maeneo ya asili hutoa nafasi kwa ajili ya kufanya masuala ya kiroho na burudani. Kwa mfano, kuna misitu mitakatifu katika nchi nyingi za Afrika. Kuhifadhi bayoanuwai ni muhimu katika kudumisha mila hizi za kitamaduni.
Ubora wa maji na hewa: Bayoanuwai, hasa katika spishi za mimea, husaidia kusafisha hewa kwa kunyonya vichafuzi na kutoa oksijeni. Vile vile, mifumo mbalimbali ya ikolojia huchuja na kunyonya uchafuzi kutoka kwa maji ya mvua, na kuboresha ubora wa maji. Oksijeni iliyotolewa na mimea hii pia huhakikisha uendelevu wa maisha. Kama msemo wa zamani unavyosema, mti wa mwisho unapokufa, mtu wa mwisho hufa.
Udhibiti wa hali ya hewa: Mifumo mbalimbali ya ikolojia husaidia kuleta utulivu wa hali ya hewa kwa kudhibiti halijoto kali na kupunguza mikao ya joto. Misitu na ardhi oevu zinafanya kazi kubwa katika udhibiti huu.
Ubunifu na maarifa: Kusoma aina mbalimbali za viumbe kunaweza kusababisha uvumbuzi mpya wa kisayansi na uvumbuzi wa kiteknolojia na kunufaisha sekta mbalimbali zikiwemo kilimo, dawa na viwanda.
Kuweka mazingira safi: Viozeshaji kama vile fangasi na viumbe wanaokula mizoga husaidia kuvunja vunja taka na viumbe waliokufa na kuweka mazingira kuwa safi na yenye virutubisho. Viumbe wanaokula mizoga ni wasafishaji wa wanyama waliokufa, hutumia mabaki na wanyama waliokufa kama chakula. Kwa kula mizoga hii, huzuia mrundikano wa taka na kuenea kwa magonjwa, huweka mazingira safi. Wanapozunguka, wao pia hutawanya mbegu za mimea na mbegu za vimelea, kusaidia ukuaji wa mimea na kudumisha mfumo wa ikolojia wenye afya.
Lishe na uhakika wa chakula: Bayoanuwai inahakikisha uwepo wa aina mbalimbali za vyakula muhimu kwa lishe na afya ya binadamu. Wanadamu hula mimea na wanyama. Bayoanuwai huhakikisha kuwepo kwa aina mbalimbali za mazao na mifugo, ambayo ni muhimu kwa lishe bora. Aina mbalimbali za spishi huchangia aina mbalimbali za kilimo, kutoa ustahimilivu dhidi ya wadudu na magonjwa. Ikiwa hatutahifadhi mimea na wanyama hawa ili kuhakikisha uendelevu wake, kungekuwa hakuna chakula.
Hatari kwa bayoanuwai
Kuna mambo mengi yanayoathiri bayoanuwai. Tumezipanga katika makundi makuu manne.
Upotevu au uharibifu wa makazi: Misitu hukatwa kwasababu nyingi, na kuharibu makazi ya wanyama. Kwa mfano:
- Ukataji miti bila kupanda miti mipya ni sababu kuu ya uharibifu wa makazi na kupungua kwa maeneo ya msitu.
- Kubadilisha makazi asilia kuwa ardhi ya kilimo. Kitendo hicho ni cha kawaida barani Afrika.
- Upanuzi wa miji na maendeleo ya miundombinu
Ugawanyaji wa Misitu ni aina nyingine ya uharibifu wa makazi asilia. Fikiria msitu mkubwa na wenye afya ukipungua na kugawanywa kuwa sehemu ndogo ndogo, zilizotengwa. Hii hutokea wakati mambo kama barabara, mashamba, au miji yanapokatiza misitu, na kuigawa kuwa vipande vidogo. Hii husababisha matatizo makubwa kwa wanyama. Wanyama wanapoteza sehemu za makazi yao, na kuwa vigumu kupata chakula na makazi. Wanapotoka katika maeneo yao na kuingia maeneo ya binadamu, wanakutana na hatari ya kujeruhiwa au kuuawa.
Matumizi Kupita Kiasi: Uvuvi kupita kiasi na uwindaji kupita kiasi vinaathiri idadi ya samaki na wanyama pori. (Mfano, uwindaji haramu wa tembo barani Afrika). Hii inajumuisha: Uvuvi kupita kiasi katika bahari za dunia.
- Uwindaji haramu wa wanyama walio katika hatari ya kutoweka kama vile tembo, chui wakubwa wenye milia, simba, paa, n.k. hasa barani Afrika.
- Biashara haramu ya wanyamapori na ukataji magogo.
Uchafuzi na Mabadiliko ya tabianchi: utoaji wa gesi chafu, kemikali kutoka viwandani na mashambani zinachafua hewa, maji, na udongo. Hii inajumuisha:
- Uchafuzi wa plastiki katika bahari za dunia: Uchafu wa plastiki unaoelea, husafirisha viumbe vamizi na kemikali zenye sumu kwenye vyanzo vya maji na kuua viumbe vya majini.
- Uchafuzi wa hewa kutokana na shughuli za viwanda na usafiri katika maeneo ya mijini: Uchafu unaotolewa na kusambazwa kwenye angahewa husambaa maeneo mengi na kuharibu jenetiki, viumbe na makazi ya asili ya viumbe.
- Uchafuzi wa maji kutokana na shughuli za kilimo na uchimbaji madini: Kemikali hatari zinazotumiwa katika kilimo na uchimbaji madini huingia kwenye vyanzo vya maji na hii huharibu makazi katika mfumo huo wa ikolojia.
- Kupanda kwa halijoto huvuruga mifumo ya hali ya hewa na kudhuru mifumo ikolojia. Kwa mfano, kuyeyuka kwa barafu ya bahari ya Aktiki na kuathiri spishi za polar ni moja ya athari za mabadiliko ya tabianchi. Kuyeyuka kwa barafu ya bahari ya Aktiki kuna athari kubwa kwa dubu wa polar, ambao hutegemea barafu kwa ajili ya kuwinda na kuzaliana. Barafu inapoyeyuka, dubu wa polar hulazimika kuogelea umbali mrefu kutafuta chakula na makazi, ambayo inaweza kusababisha kuongezeka kwa matumizi ya nishati na kupunguza kuzaliana kwao.
- Kuongezeka mara kwa mara na ukubwa wa majanga ya asili kama vile moto wa misituni na mafuriko kutokana na mabadiliko ya tabianchi. Mabadiliko ya tabianchi yamesababisha kuongezeka kwa moto wa misituni barani Afrika, haswa katika nchi kama Afrika Kusini, Namibia na Botswana. Mioto hii inaweza kuwa na athari kubwa kwa bayoanuwai, kwani inaweza kuharibu makazi na kuvuruga michakato ya mfumo ikolojia.
Spishi Vamizi: Mimea na wanyama walioletwa kutoka maeneo mengine wanaweza kushindana na kuathiri spishi za asili. Mimea na wanyama hawa wanaweza kuzidi spishi asilia, na kuzifanya ziondoke au kupotea. Hii ni kama kumleta mtukutu kwenye sherehe. Mifano:
- Nyoka wa kahawia (Boiga irregularis) akiwadhuru ndege wa Guam, Nyoka wa mti wa kahawia aliletwa kwa bahati mbaya kwenye kisiwa cha Guam, yawezekana kupitia usafirishaji wa shehena baada ya Vita vya Pili vya Dunia. Nyoka wa mti wa kahawia amewahamisha kabisa ndege wa asili wa Guam kutoka katika makazi yao ya asili, na kusababisha kutoweka kwa aina kadhaa za ndege na kukaribia kutoweka kwa wengine wengi.
- Kuenea kwa spishi za mimea vamizi katika mifumo ikolojia ya maji baridi kama vile Chromolaena odorata na Eichhornia crassipes (gugu maji): Mimea hii ya kwenye maji asili yake ni Amerika Kusini lakini imeingizwa Ghana na nchi nyingine za Afrika. Inaweza kutengeneza mikeka mnene ambayo huzuia mtiririko wa maji, kubadilisha makazi kwenye maji, na kuondoa spishi asilia.
Milipuko ya magonjwa: Milipuko ya magonjwa inaweza kupunguza kwa kiasi kikubwa idadi ya spishi fulani. Ugonjwa ukiua idadi kubwa ya mnyama fulani, unaweza kuathiri wanyama wengine wanaowategemea kwa chakula, makazi, au mahitaji mengine, na kusababisha athari mbaya kupitia mfumo wa ikolojia. Mifano ni:
- Kuibuka kwa magonjwa ya kuambukiza kutoka kwa wanyama kwenda kwa binadamu: Magonjwa kama vile VVU na Ebola yaliua binadamu na wanyama wengi.
- Kuenea kwa vimelea vinavyoathiri bayoanuwai: Baadhi ya magonjwa yanalenga wanyama na mimea, na kuathiri sana idadi yao Kwa mfano, fangasi ya amfibia wameenea duniani kote, na kuua aina nyingi za vyura na kuharibu ikolojia.
Jinsi bayoanuwai inaweza kulindwa (na mifano)
Katika ngazi mbalimbali – kimataifa, kikanda na ndani ya nnchi – kunapaswa kuwa na jitihada za pamoja za kulinda bayoanuwai, hasa bayoanuwai nyingi barani Afrika. Hatua kabambe za uhifadhi ni muhimu katika kupunguza upotevu wa wanyamapori, lakini kaya na jamii zinaweza kuchangia pia.
Kutengeneza maeneo ya hifadhi: Kuanzisha maeneo ya hifadhi na hifadhi za taifa. Nchini Ghana kuna hifadhi ya taifa ya Kakum ili kulinda makazi ya viumbe hai. Jamii inaweza pia kulinda misitu katika eneo lao, kwa kutumia kanuni zao za ndani kuhusu nani anaweza kupata na kutumia nyenzo za misitu.
Usimamizi endelevu wa misitu: Usimamizi wa misitu ya jamii ni njia nzuri kwa jamii kuongoza ulinzi wa msitu na kuepuka matumizi yake kupita kiasi kwa kuvuna kuni au rasilimali nyinginezo. Hii inaweza pia kujumuisha kutumia misitu kwa ufugaji wa nyuki, na hivyo kusababisha faida endelevu, zisizo za kukata mbao kutoka eneo la misitu.
Kupambana na ujangili: Imarisha doria za kupambana na ujangili dhidi ya tembo, faru na wanyama wengine. Kwa mfano, nchini Botswana, mipango iliyofanikiwa ya kupambana na ujangili kama vile “Operesheni Pangolin” ilitumia doria za helikopta, mbwa wa kunusa, na programu za ushirikishwaji wa jamii ili kupunguza kwa kiasi kikubwa ujangili wa tembo.
Punguza matumizi ya plastiki: Punguza uchafuzi wa plastiki unaodhuru wanyamapori na mifumo ikolojia. Marufuku ya nchi nzima ya Rwanda kwa matumizi ya mifuko ya plastiki mwaka 2008 imekuwa hadithi ya mafanikio ya ajabu, kupunguza kwa kiasi kikubwa taka za plastiki na athari zake mbaya kwa wanyamapori na mifumo ikolojia.
Saidia kilimo endelevu: Himiza shughuli za kilimo ambazo hupunguza athari za mazingira, kama vile kutumia mbolea za asili ili kuboresha afya ya udongo. Kutegemea kupita kiasi kwa kemikali katika kilimo ni hatari kwa udongo na pia huua fangasi fulani au bakteria fulani au viumbe hai kwenye udongo. Wakulima wengi katika Afrika Magharibi, kama Senegal na Burkina Faso, hutumia mbinu ya zaï, desturi ya jadi ya kuchimba mashimo madogo na kuyajaza viumbe hai vilivyooza, kusaidia kuhifadhi maji na kuboresha rutuba ya udongo kwa kilimo endelevu.
Kurejesha ardhi iliyoharibiwa: Panda miti na kukarabati maeneo yaliyoharibiwa na shughuli za binadamu ili kuunda makazi mapya. Kwa mfano, mpango wa Ukuta Mkuu wa Kijani (Great Green Wall initiative) katika eneo la Sahel barani Afrika ni juhudi kubwa ya kukabiliana na kuenea kwa jangwa na kurejesha ardhi iliyoharibiwa kupitia upandaji miti na mbinu za usimamizi wa ardhi. Ufufuaji asili unaosimamiwa na mkulima ni utaratibu ambao wakulima wanaweza kuufuata katika mashamba yao wenyewe.
Kukuza utalii wa ikolojia: Himiza utalii unaowajibika ambao unanufaisha jamii za wenyeji na juhudi za uhifadhi. Mfano ni safari katika Maasai Mara ya Kenya. Kwa kuongeza, hifadhi zinazoendeshwa na jamii nchini Namibia, kama vile uhifadhi karibu na Pwani ya Skeletoni, huruhusu jamii za wenyeji kufaidika na utalii huku zikilinda wanyamapori na makazi yao.
Elimisha jamii: Kuongeza ufahamu kuhusu viumbe hai na umuhimu wake kupitia programu za elimu shuleni, kwenye jamii na vijiji. Kwa mfano, mpango wa “Mwitu kuhusu asili – Wild about Nature” nchini Kenya hutumia zana za elimu shirikishi na warsha ili kuongeza ufahamu kuhusu uhifadhi wa bayoanuwai miongoni mwa watoto wa shule na jamii.
Saidia maarifa asilia: Jumuisha desturi za jadi za jamii za wenyeji ambazo zimeishi kwa uendelevu wa asili kwa vizazi. Kwa mfano, Wamasai nchini Kenya wana historia ndefu ya kuishi pamoja na wanyamapori. Mazoea yao ya asili ya malisho na ujuzi wa mimea ya dawa huchangia uhusiano endelevu na mazingira yao.
Wekeza katika nishati mbadala: Punguza utegemezi wa nishati ya kutumia mafuta inayochangia mabadiliko ya tabianchi na kudhuru mifumo ikolojia. Kwa mfano, dhamira ya Afrika Kusini katika miradi ya nishati mbadala, kama vile mitambo mikubwa ya nishati ya jua, inasaidia kupunguza utegemezi wake kwa makaa ya mawe na kupunguza athari za mabadiliko ya tabianchi kwa bayoanuwai.
Dhibiti spishi vamizi: Tekeleza hatua za kudhibiti kuenea kwa mimea vamizi ili kulinda spishi asilia. Kwa mfano, nchini Ethiopia, mbinu za kudhibiti kibayolojia kama vile kuanzisha wadudu wanaokula magugu vamizi ya Parthenium zimetumika kudhibiti kuenea kwake na kulinda jamii za mimea asilia.
Safisha uchafuzi wa mazingira: Kushughulikia uchafuzi wa mazingira kutoka kwenye viwanda na kilimo ili kuboresha ubora wa hewa na maji katika mifumo ikolojia ya Afrika. Kwa mfano, “Mradi wa Kusafisha Mto Ebonyi” nchini Nigeria ni mpango unaoongozwa na jamii wa kuondoa taka za plastiki na uchafuzi mwingine kutoka kwenye Mto Ebonyi ili kuboresha ubora wa maji kwa binadamu na wanyamapori.
Kusaidia uvuvi endelevu: Tekeleza kanuni na viwango ili kuzuia uvuvi wa kupita kiasi na kulinda viumbe hai vya baharini. Kwa mfano, juhudi za Senegal kuanzisha Maeneo Yanayolindwa ya Baharini (MPAs) na kutekeleza viwango vya nyavu za kuvulia samaki zinasaidia kuhakikisha uendelevu wa hifadhi ya samaki na kulinda mifumo ikolojia ya baharini. Na nchini Ghana, uvuvi umepigwa marufuku kwa kipindi cha mwaka ili kukuza uzazi na kuzuia uvuvi kupita kiasi.
Hifadhi maji: Himiza mazoea ya kuhifadhi maji katika kilimo na maisha ya kila siku ili kuhifadhi rasilimali hii muhimu kwa mifumo ikolojia.
Kukuza utafiti: Kusaidia utafiti kuhusu bayoanuwai na uhifadhi ili kuunda mikakati madhubuti ya kulinda spishi za kipekee na makazi yake barani Afrika.
Kukuza ushoroba wa wanyamapori: Tengeneza njia salama kwa wanyama kuhama kati ya makazi yaliyogawanyika, kama vile Mbuga ya Kitaifa ya Kruger inayounganisha maeneo ya hifadhi nchini Afrika Kusini.
Kusaidia uhifadhi wa kijamii: Kuwezesha jamii za wenyeji kusimamia maliasili zao kwa uendelevu, na kukuza hisia za umiliki na uwajibikaji. (k.m., programu za Uhifadhi nchini Namibia)
Kutekeleza mazoea ya matumizi endelevu: Punguza nyayo zetu binafsi kwa kuchagua bidhaa rafiki kwa mazingira na kupunguza uchafu, na kutokuunga mkono biashara za kimataifa ambazo huathiri bayoanuwai barani Afrika.
Juhudi za makusudi za kuzalisha upya spishi zilizo hatarini kutoweka: Mifano
- Nchini Kenya, walinzi wenye silaha hufanya doria kwenye mbuga za wanyama ili kulinda faru dhidi ya wawindaji haramu. (The Living Rainforest) (ScienceDaily).
- Huko Vietnam na China, Kakakuona waliookolewa wanarejelewa na kurudishwa porini. Mamlaka za utekelezaji sheria zinaongeza juhudi za kuwashughulikia wafanyabiashara haramu kwa adhabu kali zaidi (The Living Rainforest) (ScienceDaily).
- Maeneo yanayolindwa nchini Urusi na China yameanzishwa ili kulinda makazi yao. Hatua za kukabiliana na ujangili zimeimarishwa (American Museum of Natural History) (ScienceDaily).
- Siku ya Kijani ya Ghana (Ghana Green Day) tarehe 1 Juni kila mwaka ambapo aina ya miti iliyo hatarini na isiyo hatarini hupandwa kote nchini. Pia kufungwa kwa shughuli za bahari na mito kwa muda maalum ili kulinda samaki wakati wa misimu ya kuzaliana