Vidokezo vichache kwa ajili ya kufanya majadiliano ya vikundi lengwa na wakulima

Ujumbe kwa mtangazaji

Pakua na hariri taarifa hii kwa matumizi yako.

Maelezo ya mtangazaji.
Kipengele cha 1 katika kifungu hiki kinatoa maelezo ya kufanya majadilino na vikundi lengwa vya wakulima. Pamoja na maswali muhimu. Kipande hiki cha habari kinatoa taarifa na vidokezo juu ya kufanya majadiliano ya vikundi lengwa na wakulima.

Vikundi lengwa ni kundi la watu linaloongozwa na mwezeshaji akiongea kwa uhuru kuhusu maswala maalum. Majadiliano ya vikundi lengwa mara nyingi huwataka watu kujibu maswali muhimu, ingawa maswali yanaweza kuwa yanaweza kuwa magumu au rahisi lakini maalum.

Tunaita aina hii ya mjadilino kundi lengwa kwa sababu yanalenga katika mada maalum ambayo mwezeshaji anataka kuichunguza. Mwezeshaji haulizi maswali tu bali husaidia katika kuongoza majadiliano akirudi kwenye mada kama itatoka nje ya lengo. lililokusudiwa.

Script

Utangulizi: Panga kukutana na wanaume na wanawake kwa muda tofauti kwa sababu maswala ya kilimo yanayohusu wanawake mara nyingi yako tofauti na yanayohusu wanaume. Pia wakati wanawake wako tayari kusikiliza redio mara nyingi ni tofauti na wakati wanaume husikiliza redio.

Kujiandaa
Katika maeneo mengi, kuna taratibu za asili zinazofuatwa ili kuandaa mkutano na watu katika jamii. Kama huna habari na huzijui taratibu hizi, tafadhali wasiliana na watu au mashirika katika eneo lako ambao wanajua nini cha kufanya.

Hakikisha unaenda na mtu kuandika maelezo na kama inawezekana tumia kinasa sauti kurekodi majadiliano. Unapopanga mkutano hakikisha unaomba ruhusa ya kurekodi mkutano na kuandika maelezo. Mwezeshaji wa kikundi lengwa ahakikishe kwamba wajumbe wote wamekubali kutoa ruhusa kurekodi sauti zao. Kama hakuna makubaliano mwezeshaji anatakiwa kufuata sera kwamba hakuna majadiliano yatakayotangazwa kamwe.

Ni muhimu kufika muda uliopangwa. Wakulima mara nyngi wana shughuli nyingi na hawatakiwi kutolewa kwenye shughuli zao kwa muda mrefu kama si muhimu. Bila shaka majadiliano ya kundi lengwa lazima yafanyike katika lugha ya asili, kwa hiyo kujitayarisha kuwa na mkalimani ni muhimu.

Fikiri kwa makini kuhusu jinsi ya kutunga maswali ya kundi lengwa.
Kumbuka kwamba maswali yako yasiwe na jibu moja. Ina maana uulize maswali yako kwa njia ya kuibua taarifa za kina hapo kwa papo badala ya majibu ya hapana na ndiyo.

Epuka maswali yenye kuongoza. Haya ni maswali yanayopendekeza jibu sahihi ni lipi?
Uweke vifungu vyako vya maneno ili kupunguza kitu kinachoitwa mwitikio wa upendeleo/majibu ya upendeleo wa upande mmoja. “Majibu ya upande mmoja/upendeleo” hutokea watu wanapojibu maswali yako kwa kufikiri kwamba wanatakiwa kujibu jinsi unawataka wajibu badala ya kujibu kulingana na imani yao. Kupunguza majibu ya upendeleo, epuka maswali kama “Unasikiliza maonesho yetu? Unapenda nini kutoka katika maonesho? Utaepuka majibu ya upendeleo zaidi kama utaepuka kuuliza maswali ya moja kwa moja kama “Je, watu katika kijiji husikiliza maonesho? “Wanasemaje kuhusu maonesho”? Mbinu hii ya kupunguza majibu ya upendeleo husaidia kupata majibu mengi ya uhakika kwa sababu wanaojibu watakuwa na msukumo mdogo wa kusifia stesheni ya redio.

Utangulizi
Ufuatao ni mfano wa jinsi ya kujitambulisha katika kundi la wakulima. Tafaadhali rekebisha kama inavyotakiwa kwa wasikilizaji wako na wewe mwenyewe.

Asanteni kwa kutoa muda wenu kukutana nanyi leo.

“Jina langu ni___________ na ni mtangazaji katika __________ [andika jina la stesheni ya redio]. Kaaribuni wote [shika mikono, jitambulishe kwa kila mmoja].

Huyu ni mwenzangu [onesha mtu]. Jina lake ni _______. Atakuwa akinianndikia maelezo lakini hatajihusisha katika mazungumzo yetu.

[Hakikisha wahojiwa wote wamekaa kwa starehe, kwa mfano kukaa katika eneo ambalo kila mtu ana nafasi katika kivuli.

Leo nipo hapa kujifunza kuhusu ni maswala gani ya kilimo ni muhimu kwenu. Pia ninataka kujua ni wakati gani muafaka kusikiliza program ya wiki ya redio inayotangaza juu ya kilimo na [Andika/weka jina la redio].

Nimekuja hapa kujifunza kutoka kwenu. Ninataka kuyakusanya maoni yenu. Sitakataa yale mtakayoyasema au kujaribu kuwashauri kufikiri tofauti. Huu si mtihani, Huu ni muda ambao unaweza kusema chochote unachojisikia au kufikiri kuhusu mada ambazo nitajadiliana na ninyi.

Haya ni majadiliano ya kikundi ambayo tutazungumza kuhusu mambo ya pamoja kama vile tulikuwa tukizungumza na rafiki au familia zetu. Tofauti pekee ni kwamba nipo hapa kuongoza mjadala. Sitaki kujisikia nikiongea peke yangu sana. Nimekuja kusikia maoni yenu. Hata hivyo nina orodha ya mada ambazo ninapenda kuzizungumzia. Kwa hiyo wakati mwingine nitachochea majadiliano kuhusiana na mada hizi.

Mjadala huu utarekodiwa. Ninataka kumbukumbu ya mjadala wetu kwa sababu tutatumia mchango wenu kutusaidia kuendeleza orodha ya mambo tutakayo ya shughulikia katika program ya redio katika kilimo Ninaweza pia kutaka kutengeneza program kuhusiana na kundi lengwa. Lakini nitatangaza program hii kwa ruhusa yenu.

Kikundi kitachukua saa moja hadi saa moja na nusu. Ni matumaini yangu mtaona maajadiliano haya ya furaha na ya kupendeza. “Kumbuka: ni nafasi yako kuchangia maoni yako katika mazingira salama.

Je, kila nilichosema sawa? Je, kuna maswali?

Kama mtu akiuliza taarifa hizi ni za nani, sema: “Mjadala wetu wa leo utaisaidia stesheni ya redio yangu kuanzisha progamu ya wiki. Watatusaidia pia kuamua ni muda gani wa kutangaza program.

Maswali
Mara tu baada ya kujitambulisha na kuainisha mchakato (kama hapo juu), ni muda wa kuwaauliza wakulima maswali uliyoandaa. Angalia kama kuna watu ambao hawaongei na uwatie moyo kuchangia kwenye majadiliano.

Kufunga majadiliano
Ni muhimu kusimamia muda unaopatikana??? uliopewa??? Kama watu wana mambo mengi ya kusema na unafikiri unahitaji muda zaidi, utahitaji kuomba ruhusa kutoka kwa kikundi wakae zaidi. Kama hawawezi kukaa zaidi unaweza kuhitimisha.

Baada ya kumaliza kujadili maswali uliyoandaa, shukuru kila mmoja kwa kuchangia.

Vidokezo vitano juu ya kuwezesha majadiliano ya vikundi lengwa
1) Uwe makini: Maswali yawe mafupi, yasiyo na utata na yanayolenga mada Wanaohojiwa wanaweza kuchanganyikiwa kama watasikia swali zaidi ya moja kwa wakati mmoja au kama maswali ni marefu sana kujibiwa na kumalizwa. Kundi linaweza kupoteza mwelekeo wake kwa urahisi. Lakini kama kiongozi ni wazi kikundi kita kuwa kisikivu.

2) Uwe na mpangilio: Weka pamoja maswali yote yanayohusiana na mada ndogo ya maswali ya msingi.

3) Uliza swali moja baada ya lingine: Kwa mfano, Ni hatua gani zimechukuliwa kuweka mazao yako mseto. Kwa mfano; Ni hatua gani umechukua kuwa na mazao yako ya mchanganyiko? Na ni hatua gani zitakazochukuliwa kuboresha kilimo mchanganyiko katika jamii.

4) Kuendea kina:
a. Anzia maswali rahisi sana halafu magumu sana.
b. Anzia maswali yanayoogopesha halafu maswali
c. Epuka maswali yenye utata kwenda kwenye maswali yasiyo na utata.
d. Epuka maswali yanayo wachanganya wanafunzi au ambayo yataleta utata.
e. Epuka maswali ambayo yatamwuliza mtu kuchagua kati ya majibu mawili. Maswali ya aina hii yanaweza kumchanganya mtu kwa urahisi Kwa mfano, epuka maswali kama vile “Ni nini cha muhimu kwako zaidi. Pesa kutokana na kilimo cha mazao, Mahusiano na familia yako au paa zuri juu ya kichwa chako? ”Kwa hali yeyote ile ni sahihi (Kwa sababu haichanganyi sana) kuuliza? Kipi kati ya hizi ni muhimu zaidi kwako? Kama zote zimeorodheshwa kwenye ubao.
f. Epuka maswali yanayoleta majibu ambayo si sahihi ya kufikirika, yenye kutoa
g. mwelekeo au yanayopoteza uelekeo. Kwa mfano, maswali ”Kutokana na wingi wa makosa kuna usalama gani kutembea usiku? Chukulia kwamba makosa mengi yapo; Kwamba mtu ana taarifa kuhusu kiasi cha makosa na kwamba mtu huyo hutembea usiku.

Acknowledgements

Imetengenezwa na: Vijay Cuddeford, Meneja, Mkurugenzi Mhariri, Redio ya kilimo ya Kimataifa, Hati na David Mowbray, Meneja, Mafunzo na viwango redio ya Kilimo ya kimataifa na, Blythe McKay, Meneja, Raslimali kwa ajili ya watangazaji Resources for Broadcasters, Farm Radio International
Imepitiwa na: David Mowbray Meneja, Mafunzo na viwango redio ya Kilimo ya kimataifa.

Information sources

M. Escalada na K. L. Heong. 2009. Mahojiano ya kundi lengwa. Makala hii ya mahojiano ya kundi lengwa iliandikwa kusaidia watafiti wa kilimo katicha Chuo cha kimataifa cha Mpunga Filipin ikifaya mahojiano ya kundi lengwa na wakulima. http://ricehoppers.net/wp-content/uploads/2009/10/focus-group-discussion.pdf
Monina Escalada, 2012. Focus Group Discussion. Hiki ni kipande kingine na kirefu kidogo zaidi juu ya mahojiano ya Kundi lengwa kwa watafiti wa kilimo kutoka katika Chuo cha Kimataifa cha Utafiti wa Kilimo. http://devcompage.com/wp-content/uploads/2010/12/Focus-group-discussion.pdf

gac-logoMradi fanywa na kupewa msada wa kifedha na nchi ya uliotolwa kupitia wakala wa kimataifa wa mendeleo. (CIDA)