Muundo wa Redio

Ujumbe kwa mtangazaji

Pakua na hariri taarifa hii kwa matumizi yako.

Muhtasari kwa mhariri
Programu ya redio ya mkulima inatumia miundo mingi. Makala hii ya taarifa inakupa orodha ya miundo muhimu ya kuzingatia kwa programu yako. Inatoa kwa kifupi kwa kila muundo na kutoa mapendekezo ni tarifa gani inayofaa na bora kwa mawasiliano, au ni jinsi gani muundo unawatia moyo wasikilizaji kujihusisha.

Script

Utangulizi
Katika vituo vingi, kwa kawaida (yaani kwa siku au wiki) programu ya mkulima ni magazeti au programu ya muundo wa aina nyingi. Muundo wa magazeti unaruhusu mtoa matangazo uhuru wa kutumia muundo unaofaa zaidi kwa kila kipengele katika programu yote, kwa sababu ya utofauti wake wa sauti na mbinu, muundo wa mbalimbali huvutia kusikiliza.

Lakini ni muundo gani utakaotumia kwa kipengele kipi cha programu yako?

Ni jambo moja kutambua maudhui unayotaka katika programu ya wakulima. Lakini swali kuhusu ni jinsi gani utabadili hayo maudhui kuwa ya redio ni muhimu kama maudhui yenyewe.

Kuna miundo kadhaa ya katika kutoa maudhui katika kuutangaza. Baadhi ni rahisi, yanabana matumizi na yenye kufaa. Baadhi yanafaa lakini ni gharama kuzalisha.

Unaweza, kwa mfano, kutoa maudhui ya progrmu yako yote katika mgawanyo wa wahusika mbalimbali katika mchezo wa kuigiza. Lakini hii itahitaji timu ya kipekee ya waandishi na waigizaji. Mambo ya starehe hayapo katika programu nyingi za wakulima.

Au unaweza kuwa na mwenyeji akasoma maudhui yote. Lakini kwa uhakika itachosha badala ya kuwahusisha wasikilizaji wako. Hawatawasikia watu kama wao wenyewe katika redio. Na hawataichukulia programu yako kama programu yao.

Baadhi ya vipengele katika programu vinahitaji muundo maalum. Kwa mfano, bei za masoko kwa kawaida zisomwe na mwenyeji (au na mwingine mwenye haiba ya kutangaza) kwa kutumia makala ambayo inafuata mtiririko wa kawaida inatangazwa kila siku kwa muda ule ule. Bei za masoko zinahitaji kuwa sahihi kwa hiyo makala inahitajika. Na bei za masoko zinabadilika kwa siku au wiki. Kwa hiyo kuna uhitaji wa kuwa mawasilisho ambayo ni wazi na mafupi. Kwa kawaida karibu wasikiliaji wako wote watakuwa tayari wamekuwa na motisha wa kusikiliza programu ya bei za masoko. Kwa hiyo hutakiwai kutayarisha taarifa za masoko kufanya ya kufurahisha.

Hata hivyo, unaweza kujaribu miundo mbalimbali kwa progrmu nyingine. Kwa mfano, kama kipenngele cha programu ni kuhusu (swala la kina kiefu cha mzizi) unaweza kuchagua kufanya kwa kutumia muundo mmoja kati yaa miundo mingi, Hii ni pamoja na mahojiano, jopo la majadiliano kupiga simu, mtaalamu wa mahojiano, kuchukua mkanda wa mazungumzo, au mchanganyiko wa zaidi ya muundo mmoja. (Swala la kina kirefu cha mzizi ni swala ambalo linasimama kama njia ya uzalishaji bora kwa hiyo si rahisi kutatuliwa.)

Muundo sahihi kwa programu ya magazeti.
Miundo ifuatayo imechaguliwa kwa sababu:

  • Inaweza kuwa na ufanisi ikitumika sahihi.
  • Ni rahisi kuzalisha.
  • Hazihitaji rasilimali nyingi

Miundo ya kawaida zaidi imetajwa kwanza ikiwa na kiasi kilichotumika kidogo cha muundo karibu na mwisho.

Mahojiano: Mahojiano ni uti wa mgongo wa programu nyingi za kilimo. Muundo huu kwa kawaida humwusisha mwenyeji akiuliza mtu Fulani maswali ili kumfanya mtu huyo kutoa taarifa au maoni muhimu, mahojiano yanaweza kufanywa katika studio, shambani, au kwa simu. Yanaweza kuwa ya papo kwa papo au yaliyorekodiwa. Yanaweza kuhusisha maswali magumu (kwa mfano unaposaili kuhusu jambo la ofisi au yanaweza kuwa ya msaada (Kwa mfano unapomtia moyo mkulima ambaye hana uzoefu wa redio kuelezea maoni yake).

Mahojiano ni muundo mkubwa kwa sababu:

  • Unaruhusu wasikilizaji kusikiliza mazungumzo ya mtu mwingine. (Sisi sote ni wadadisi).
  • Kwenda na kurudi nyuma wakati wa mahojiano kunaondoa mazungumzo ya muda mrefu.
  • Inamwezesha mwenyeji njia ya kuweka majadiliano katika mada.

Mahojiano ya studio ni rahisi kutayarisha na ni mazuri kupatikana:

  • Ukweli kutoka kwa wataalamu ikiwa ni pamoja na matukio na pengine hisia. Kumsaili mtu kunaweza kuwa bila vichocheo. Hata hiyo ni ni muhimu kumwusisha mtaalamu kwenye misingi binafsi. Yachukue matukio, yafunue mahusiano ya mtaalamu na mada na kuweka taarifa sahihi katika kiwango kinachoweza kusimamiwa. Kama mahojiano yanaegemea sana kwenye uhakika hadhira haiwezi kushiriki kama matone/kama watu wasiojua katika azungumzo kama ambavyo hakuna muunganiko wa hisia zozote na mgeni au mwenyeji.
  • Mahojiano binafsi na mtu Fulani ambaye anaonyesha kuhusu wao wenyewe au kuhadithia hadithi nzuri. Hii kwa ujumla inahusisha hadhira kiurahisi na mafanikio zaidi, kwa sababu kuna hisia zenye mguso, maadili na hisia tunazoshirikiana kama binadamu.

Mtangazaji aandae mahojiano kwa kuwa na mawazo ya nini wanachotakiwa kukizingatia kaatika mahojiano. Kutoka katika utafiti uliofanywa kwanza unapaswa kuwa na muhtasari usiokamilika wa hadithi, mawazo mazuri ya maswali unayotaka kuuliza na mawazo mazuri kuhusu mtazamo gani unafikiri utawaavutia wasikilizaaji wako.

Mahojiano ya shambani pia ni rahisi kufanaya. Ukichukulia kwamba kituo kina raslimali za kupeleka wafanyakazi shambani. Uhusishaji wa sauti ya shamba unaongeza vipengele vyenye mwonekano wa taarifa inayotangazwa. Hadhira bado haishiriki kikamilifu lakini sasa wasikilizaji wanaweza kuona onesho/eneo la tukio. Wataalamu wanaweza kuandaa maonesho wakitumia lugha ya wazi ambayo inajieleza na sauti za asili ilikuwawezesha hadhira kuona na kuelewa taarifa kwa uwazi. Mahojioano ya shambani na sauti asilia vinaweza kuwaunganisha hadhira kwa nguvu zaidi na hadithi inayosimuliwa, hisia zikielezewa. Kwa mfano, mahojiano ya shaambani na mkulima ambaye anamsubiri daktari wa mifugo kuangalia ng’ombe wa familia anaweza kuwa mwigizajina mwenye hsia nyingikuliko mahojino ya studo yaliyofanywa baada ya kutembelewa na daktari wa mifugo.

Mwenyeji anaweza kusaili watu wawili au zaidi kwa muda mmoja. Au mwenyeji anawesa kusaili mtu mmoja baada ya mwingine (na labda) kwa kuweka rekodi ya mtu akiongea kuhusu somo husika/mada husika.

Onesho la Upigaji Simu/uandikaji ujumbe: Mwenyeji anawaalika watazamaji kuelezea maoni yao juu ya mada maalum wakati mada ikiwa hewani. Miundo hii ni rahisi na rahisi kutengeneza na inaruhusu mtazamaji/hadhira kuwa sehemu ya programu, kwenye mazungumzo na kuuliza maswali.

Upigaji simu na utumaji ujumbe una ufanisi katika kushirikisha wasikilizaji. Mfumo huu unafanya kazi vizuri wakati mwenyeji anaiweka mada katika muunndo wa swaliambalo mpigajiau mtuma ujumbe ameulizwa kutoa maoni juu yake. Mataalam mgeni anapotumia njia ya maswali, muundo huu unaweza kuwa wa manufaa kwa kueneza ukweli kama kweli hizo zitakuwa misingi halisi ya hali ya maisha.

Kuzungumza na mwenyeji: Wasikilizaji wanataka kuwa na na mahusiano mazurin na mwendesha programu mwenyeji. Mwenyeji anaweza kufanya mambo mengi sana kupa moyo. Mwenyeji anayefanya kazi vizuri anaunda na kujenga uhusiano huu wa kirafiki kwa kuwaendea na kuwafikia na kushirikiana wasiwasi na furaha yake na kuwachukulia/kuwaheshimuwasikilizaji kama wako sawa. Mazungumzo ya mwenyeji kwa kawaida hutokea mwanzoni na mwishoni mwa programu. Lakini inaweza kutokea wakati wowote weye manufaa.

Jopo la majadilliano: Majopo hutofautiana kutoka usaili mmoja na mwingine kwa sababu wasikilizaji/hadhira husikia mitazamo mbalimbali katika maswala Fulani mahsusi. Tofauti hizi za mitazamo zinaweza kuchochea mjadala kamili, mkubwa na wenye kulazimisha. Katika jopo la wakulima wanawake, kwa mfano wakulima wanaweza kukusanya nguvu kutoka kwenyee maneno ya kila mmoja na kuyashirikisha zmajadiliano apana na marefu zaidi.

Kama majadiliano mengine ya studio, jopo la majadiliano njia ya haraka na y a ufanisi. Lakini pia yanawdza kuishia katika kuwa ni mfululizo wa mtu mmoja na mtu mmoja isipokuwa wanajopo wana mitazamo tofauti au pointi malumu ya kutokukubaliana. Jopo lenye ufanisi ni la majadiliano mengi sana kati ya washiriki kama mahojiano. Mhojaji ni zaidi kuliko msimamizi kuliko mwuliza maswali. Mazungumzo hai yanavutia kusikiliza zaidi na yanaweza kuwa ya ufanisi zaidi kwenye kupeleka taarifa ya mahojiano halisi ya moja kwa moja ya mtu mmoja na mtu mmoja.

Nyimbo za ujumbe: Redio ni njia kamilifu kwa nyimbo. Nyimbo zinaweza:

  • Kuongeza tofauti ktika programu yako kwa kuazhsaha aina nyinine ya sauti (tofauti na sauti rahisi)
  • Inaonesha na kuthibitisha utamaduni wa msikilizaji
  • Huamsha majibu ya kusismua juu ya mada
  • Husaidia asikilizaji kukumbuka taarifa tata/ngumu

Baadhiya programu yimine zinaunda au zinatumia nyimbo zilizorekodiwa katika mazingira zilipo kama sehemu ya kuanzisha. Katika sehemu nyingine wazalizaji hutumia nyimbo zilizopo na kuumia ujumbe uliopo amabao unaendana na ada ya programu. Uwe tu makini kwamba wimbo haumtoi msikilizaji nje ya ujumbe ambao unataka kuutoa.

Mchezo mfupi wa uigizaji: Redio inachukua na kusisimua fikra za msikilizaji… Kwa hiyo ni njia thabiti kwa mchezo wa kuigiza Mchezo wa kuigiza unaweza kuwa rahisi kama kurekodi mazungumzo ya simu ambayowafanyakazi wako wawili ni wigizaji wa sauti. Au inaweza kuwa ni ngumu kama kutangaza kifaa cha kiuizaji kilichozalishwa na watalamu wa utafiti, waandishi na waiizaji.

Redio ya uigizaji inaelezea hadithi, ama za kubuni zinazohusu matukio halisi ya mtu, ambayo yanaweza kuelimisha na kuwahamasisha wasikilizaji kuhusu maswala muhmu wakati wanaburudisha. Michezo ya kuigiza pia kinaweza kutungwa kimsingi kuhamasisha hadhira inayosikiliza kushiriki katika majadidiano ya umma.

Michezo miref ya kigiza inachukua muda na gharama na nara nyingine inahitaji waandishiwenye ufundistadi waigizaji wenye ufundi sana. Kwa ujumla mfuliulizo wa michezo ya kuigiza unahitaji wafadhili. Gharama ya hati/maandiko yenye ubora, waigizaji wataalamu na wataalamu wenye ufundi mkubwa untiliwa maanani. Hata hivyo mchezo mfupi wa kuigiza wenye waigizaji 2-5 unaweza kufanyika na ni rahisi na hutumikasana. Michezo ya kuigiza midogo midogo unaweza kuhusisha mfululizo mfupi wa matukio yaliyounganishwa. Michezo ya kuigiza ya rediohutegemea sana mazungumzo kuendesha vitendo vya kuigiza. Kwa sababu hadhira inayosikiliza wanaweza kusikia tu na wasione ni nini mhusika wa redioni anafanya, ni mazungumzo ambayo lazima yafanye tabia ya mhusika vitendo vyake kuwa wazi.

Sauti za kisasa (au sauti za Kijiji): A vox pop inahusisha mtangazaji kwenda mahali watu (watu wa muziki wa sasa) walipo na kuksanya maoni machache/mafupi (sauti inaanisha sauti) katika mada iliyoandaliwa kabla au maswali ya kabla. Haya maoni machache huhaririwa. Sauti za sasa ni njia nzuri ya kuandaa mahojiano. Zinanesha mtu ambaye atasailiwa kwamba kuna safu ya maoni ya umma ambayo anataka kuyashughulikia. Sauti za kisasa zinaweza kumhamasisha mhojiwa/ msailiwa kutoa majibu kamili nay a kiufafanuzi zaidi.

Kwa kutangaza kutoka njiani, vox pop inawapa wsikilizaji umiliki w programu za redio. Intambulisha maoni watu, n watu wnapenda kusikia sauti zao ktika redio.

Inaonekana rahisi sna kurekodi sauti za wapitaji, lakini kuna zaidi kwa Vox popping kuliko iapokutana na masikio.

  • Muziki wa ksasa lazima urekodiwe wazi wazi katika eneo lakini si utokane na kupitisha magari au muziki wa sauti kubwa sana. Angalia eneo lenye misingi ya kelele za kutosha si usambaaji wa jumla wa sauti zilizojipanga au muziki. Muziki bora wa kisasa ni wa harakaharaka, haraka na wenye kukumbukika.
  • Sauti ya mtoa habari kwa kawaida haitokei katika sauti za kisasa, isipokuwa labda kuuliza swali linalohusianaaaaaaa la swali la awali.
  • Swala la musiki wa sasa liwe kitu abacho watu wana uhakika wa kuhusu – mara nyingi ni kipengele/bidhaa iliyokatika habari. Epuka maswala/mada za utata kama ya ulimwengu wa baadaye.
  • Uliza swali rahisi ambalo litaeleweka kwa haraka na ambalo halitakuwa na majibu ya nfululizo wa wa ndiyo hapana.

Orodha yenye maandishi: Wakati wingine unahitaji kutoa taarifa ambayo ni ya kina, sahihi. Katika hili, kuwa na mwasilishaji ambaye anasoma maandishi yaliyoandikwa kwa kina inatoa maana sana. Kama ilivyoelezwa hapo juu, bei za masoko ziko katika orodha ya maandishi: Pia, kama programu yako inajadili uendeshaji wa kilimo kinachohusisha mfululizo wa hatua ni vizuri kutoa orodha ya maandishi ya hatua hizo mwishoni wa majadiliano. Hii itawasaidia wakulima kukumbuka taarifa muhimu. Orodha fupi ya maandishi inaweza kutengenezwa katika matangazo ya hapo kwa hapo anbayo yanaweza kutangazwa tena baadaye au wakati wa kutoa atangazo.

Mashairi, najaribio na mashindano mengine: (Kwa kawada na zawadi za kawaida) Hizi zinaweza kuwasaidia wasikilizaji kukunbuka taarifa maalum na zinaweza kuwa za kufurahisha/kuchekesha pia. Wakulima hukumbuka taarifa wanaposhiriki. Kwa mfano kutunga na kuwasilisha shairi, nyimbo au aina nyingine ya utugaji kuhusu mada maalumu ya kilimo. Kama mawaslisho mazuri ni kutangaza, hii inasaidia wakulima kukumuka baadaye. Njia nyingine ya kusaidia wakulima kukumbuka ni kuwapa moyo wa kupiga simu na kusoma pointi muhimu zilizosailiwa katika usaili.

Mahojiano ya maandishi/Usaili: Mashirika kama Farm Radio International yanatoa maandiko ya redio katika mada ambazo zinaweza kuwa ni za manufaa kwa wakulima wako. Kwa kufanya utafiti wa ndani, unawza kutumia maandiko haya kutoa habariza maswala muhimu ya ndani, ingawa kuna muda mwingine unaposoma maandishi mengine hewani kwa bei ndogo sana inakuwa sahihi.

Maandiko mengine yanaweza kuchukua muundo wa wenyeji wawili redioni wakijadili mada. Wenyeji si wataalamu wa mada lakini huzungumza vizuri kama wataalamu. Kati ya hawa wawili wanaanzisha na kutoa maoni ya jumla ya mada. Ni wazo zuri kwa kwa wenyeji kuwa na nyadhifa mbalimbaliau kuwa na haiba mbalimbali za utangazaji. Kwa mfano, wenyeji mojawapo anaweza kuuliza maswali (akijifanya msikilizaji) na mwingine anaweza kujibu maswali. Mwenyeji mmojwapo anaweza kutoa tarifa na mwingine akaburudisha. Kuwa na majukumu mawili au “hadhi” inaunda nguvu anayowafanya wasikilizaji/hadhira kushiriki. Mfumo huu unahitaji utafiti katika mada ambazo zinatosha kuamua ni taarifa ipi iwekwe kwenye maelezo ya jumla.

Maandiko megine ya (kutoka redio ya Kimataifa ya Mkulima na mashirika mengine) yanachukua mfumo wa maandiko ya mahojiano ya mtalamu mwenyeji. Mada hii inawasilisha mwenyeji akiongea na mtu mwenye utaalamu malumu wa mada. Kukabiliana/kuwza kutekeleza muundo huu wa mandiko kwa kutangaza, tafuta mtu mwingine katika stesheni yako anayeweza kuchukua jukumu la mtaalamu-mtangazaji mwingine au labda wakala ughani ambaye anafaanya kazi na stesheni yako. Pamoja na huyu mtu wa pili jarbuni kusoma maandiko ukitafsiri na uifanye katika lugha ya wakulima. Isome tena na tena mpaka uwe na imani kwamba haipo tena “kimaandishi” na kihiari nay a kufurahisha, na kumbuka: Usijaribu kuwadanganya wasikilizaji wako. Kama andiko linahusisha mwenyejina mwanasheria lakini huna mwanasheria, wambie wasikilizaji akio bayana/wziazi kwamba mahojiano ya mwanzo/awali yalifanywa na mwanasheria na kwa sababu jambo hili ni muhimu sana kwa wakulima unatengeneza upya mahojiano/usailikwa kuwa na mtu mwingine akiongea maneno ya mwaasheria.

Andlo la mazungumzo binafsi: Baadhiya sesheni/vituo wana mwenyeji au mtalamu wa kusoma anasoma andiko refu kuhusu jinsi ya kupanda au kuhfadhi mahindi. Hii kwa kawaida haitengenezi redio nzuri. Wasikilizaji huchoshwa na sauti moja ikiwaambia nii cha kufanya. Hata hivyo kuna muda unaokuwa na mantiki kwa mwenyeji kufanya mahojiano kidogo ya binafsi. Kwa mfano, unaweza kutaka:

  • Kutoa tarifa upya juu yataarifa/hadithi umekwishaimaliza kwa kina.
  • Kumalizia mada/jaambo ambalo hujawahi kuwa na muda nalo kulitolea taarifa juu yake na miundo miguu zaidi kama saili/mahojiano.
  • Kutoa uchunguzi wa kichekesho au dhihaka juu ya hali ya sasa.

Hata hivyo epuka muundo huu kama unavyoweahasa kwa taarifa ndefu/vipande virefu. Inaweza kuwa rahisi, lakini haitawasaidia waskilizaji vizuri, na inaweza kuwa na mwonekano wa wa kukosa jitihada za ubunifu au mawazo na kutokuwa na kiunganishi na wakulima.

Ukumbi wa mjini: Ukumbi wa mjini ni jopo kubwa ambalo ni mahali pa hadhira/wasikilizaji kama wahiriki. Mwenyeji ni nsimamizi, mara nyingi akiwa na na jopo la wataalamu yafanya majadiliano yaendelee. Ni juu ya yake mwenyeji kufanya majadiliano kuwa hai kwa kuhamasisha maswali yenye hamasa na maswali yenye kuoa najibu mzuri na maoni, majadiliano ya ukumbi wa mjini ni njia inayoonekana kutoa umiliki kwa hadhira inayosikiliza. Kwa kawaida huwa imerekodiwa na kuhaririwa kwa ajili ya kufanywa tena.

Shajara: Shajara ni taarifa isiyojitoshelezaya msimuliaji ambapo mwenye shajara kw kifupi huzungumzia kuhusu uzoefu wke. Kamainavyowsilisha hewani hakuna mwangalizi wa kubainisha/kuchunguza kati ya mwenye sahajara na hadhira. Mwenye shajara hutoa taaifa/hadithi yake kwa kifupi. Wenye shajara wamehamasishwa kuzunumza katika lugha yao ya ndani/wenyeji na kwa kawaida huzungumza kwa takribani dakika 5-7. Wenye shajara ni watu ambao hukabiliananahali ngumu sana kama vile watu wanaoshi na UKIMWI au wanaweza kuwa ni watu wa kawaida wenye haditi zao maalum za kusimulia kama vile watu waliojiriwa katika kazi ambazo watu wanakufa kwasabau ya mabadiliko ya utamaduni na teknolojia.

Sehemu za shajara kwa kawaida hutangazwa kama kipengele kimoja cha aina moja ya programu ya magazeti ya wiki. Lakini mahojiano ya kina yanahitajika kukusanya mambo yatakayoifanya sehemu ya shajra yenye umakini, kwa sababu watu wengi hawajui ni jinsi gani taaifa zao inafsi zinafurahisha auhatani jinsi gani hadithi/taarifa binafsi ilivyo. Muhimu nikuanzisha uhusiano kati ya msailina mwenye shajara ili matokeoyawe ya wazi ya uaminifu. Shajara zinahitaji ujuzi mkubwa wa kuhoji. Dodoso zinahaririwa, kwa hiyo ufundi wa wa usahili unahitjika kukwep mapengo ya uelewa au mabadilko ya kufedheesha katika makala ya mwisho.

Shajara za redio ni rahisi na gharama kuzitengeneza. Shajara zinawea baada ya muda kuzungumzia safu ya mamo mengi na inaweza kuwa yenye ufanisi katika kubadilisha tabia jamii kwa njia chanya.

Katika baadhi ya matukio, shajara ni nsingi wa prograu ya magazeti na vipengele vingine vya programu vinalenga katika mambosawa kama shajara.

Mazungumzo ya tepu: Hii ni nusu ya usaili, nusu ya, nusu ya hati/maandishi. Mwandishi anaenda kijijini anawasaili wakulima na halafu anahariri maoni yao. Halafu mwandishi anaandika andiko ambapo mwenyeji mwenyeji anamwuliza mwandishi wa habari katika sauti ya mazungumzo, na mwandishi wa habari anajibu kwa maneno yake mwenyewe ikifuatiwa na visehemu vya video kutoka kwenye eneo la wasaili. Visehemu vya video vinaelezea pointi,vinaeleazea hisia vinampeleka hadhira kwenye eneo jipya na kuwa mhusika. Mazungumzo ya tepu ni rahisi nay a haraka kuunda kuliko hati, lakini yanahitaji utendaji mzuri kutoka kwa wote mwenyeji na mwandishi wa habari.

Mazungumzo ya tepu yanaanzisha sauti mpya (ya mwandishi wa habari) kwa programu yako, na inakuruhusu kutangaza mahojianno ya eneo hata wakati mwenyeji hawezi kusafiri.

Hati ndogo ya maandishi: Hati ya maandishi ya redio au “makala maalumu” ni programu iliyotolewa kufanikisha mada fulani kwa undani, kwa kawaida mchanganyiko wa wasaili na watu waliohusika na ada, tafsiri ya andiko, aelezo na mijadala ikiongozana na na sauti sahihi. Mfumo huu unahitajimaana halisi ya habari, wataalamu waandishi na watekelezaji na ujuzi mzuri wa kurekodi na kufanya usaili/mahojiano. Unachukua muda mwingi kuutoa. Lakini hati fupi ya dakika tano hadi saba inaweza kuwahusisha watazamaji/hadhira, kuwapeleka katika safari kuwatanbulisha kwa watu wanaopenda kutoa taarifa muhimu.

Kwa kawaida ni wazo zuri kupata uzoefu na mazungumzo ya muundo wa tepu kabla ya kujaribu hati ya maandishi. Kumbuka kuwa hati ya mandishi ni rifa pia na hata kama ina sera na au wazo lingine la kufanya. Wahusika wazuri hupelekea hati nzuri ya maandishi.

Hapa kuna badhi ya vidokezo muhimu kwa ajili ya kundika hati ndogo yenye madhara.

Kama unaweza kuandika vizuri zaidi na fupi zaidi ya walivyosema, fanya hivyo.

Wakati wa kuhariri hakikisha kwanba unaweka iliyo bora sana. Dondoo nzuri/za dhahabu kutoka kwa wasaaaili wako wote. Mara kwa mara hizi zitakuwa ni dondoo ambazo zimeelezewa kwa hisia. Weka namba.

Weka nanba na idadi ya mambo magumu katika sehemuya andiko/mandishi yako.

Weka visehemu vinavyounganisha andikko lako vifupi kama inavyowezekana. Wasikilizaji wanapendelea kusikia kutoka kwa wageni wako.

Usiogope kucheza /kutumia vipengele/visehemu vya video pande zote nawageni tofauti tofauti wakitoa maoni yao katika mada moja iliyo sawa na au kujibu swali lililo sawa. Hakikisha uhakika wa kupata wageni kabla na baada ya kutumia visehemu ili wasikilizaji wasipotee/wasisindwe kufuatilia.

Muundo utumikao nje ya programu ya nagazeti.

Miundo miwili ifuatayo kwa kawaida hutangaza nje ya programu ya kawaida ya gazeti.

Matangazo ya redio: Matangazo ni mafupi (kwa kawaida hutumia sekunde 30-60) mawasilisho “ya kuvutia” au matangazo ambayo yanawasilisha ujumbe mmoja na ulio dhahiri/wazi. Yamekuwa yakitumikakwa mapana katika masoko ya jamii, kwa mfano kutangaza bidhaa za kondomu au vyandarua vilivyowkewa dawa. Hutumika sana katika kuwasilishaujumbe kuhusu muafaka wa tabia unaohitajika au afya ukianzia tabia ya kufanya ngono hadi ya usafi.

Mara nyingi matangazo huonesha watu wakifanya mambo ya usahihi nakuwa na matokeo ya kuboresha maisha ya watu. Wanatumia sauti ambazo ni wazi/sahihi, zikiifikiria jamii ya wasikilizaji, na/au kuwa na sauti ya kuaminika ya mamlaka.

Matangazo ya redio ni rahisi nay a gharama nafuu kutengeneza. Kwa sababu ni mafupi ni rahisi kuingizwa katika ratiba ambayo ni imefinywa na inaweza kuwekwa pamoja na programu ambayo tayari ina wasikilizaji/hadhira. Hakuna haja ya kufanya kampeni kujenga usilizaji/usikivu. Matangazo na jumbe yanaweza kubadilishwa kwa urahisi ni rahisi.
Matangazo yanaweza kuwa na aina/idadi ya mifumo. Michezo midogo/mifupi mifupi ya kigiza, matangazo, ridhaa kutokana na haiba au mamlaka, Sauti za kisasa, katuni au kuchukua filamu, mazungumzo, muziki, mfumo wa maswali na majibu au majaribio ya maswali/chemsha bongo.

Kumbuka kwamba matangazo yaliyotengenezwa vizuri yanaweza kutumiwa tena na tena kwa mara nyinine. Kwa hiyo ategeneze kwa utaratibu ili kuhakisha yanabaki yalivyo wakati wote/mara kwa mara na kutumiwa tena.

Maonesho: Maonesho ni visehemu vifupi vyenye wastni wa sekunde 10-30 zinazozalishwa kwa ajili ya kutangazwa nje ya njeya programu yako ya wakulima. Dhumuni la monesho ni:

  • Kufikia kila msikilizaji wote wa mara kwa mara na wenye uwezo, na
  • Kuwapa nafasi ya kusiiliza kwa wakati ujao-kwa onesho linalofuata kwa progrmu yako.
  • Onesho kwa kawaida lijibu swali la: Kwa nini nisikilize progrmu ijayo?

Watengeenezji/warushjiwengine wa mtangazo hawahangaiki kutenngeneza matangazo kwa kila programuna kwa badhi ya stesheni nyingine hazijishughulishi kutoa muda kwa kila tangazo. Wanakosea. Matamgazo ni sehemu muhimu y huduma ambayo programu na na stesheni ya redio intakiwa kutoa kwa wakulima. Nimuhimu kuliko shughuli zote za wahkuunda wahuska unazoweza kufanya, nje ya programu ya kawaida.

Kama kwa sababu nzuri tu huwezi kuanziha maonesho kwa onesho lako linalofuata, hakikisha una maonesho ya aina safu kwa programu yako ya redio unayoweza kurusha hewani kwa maonesho yanayofaa.

Hitimisho
Kama unavyoweza kuona, kuna uwezekano wa mifumo wa kutoa taarifa na kuwahusisha watazazanaji/hadhira yako. Majaribio na miundo mipya, labda maeneo machache, sauti za muziki wa sasa au jopo la majadiliano au mikutano ya ukumbi wa mjini. Usisahau kupata maoni kutoka khwa wasililizaji wakulima kuhusu ni jinsi gani watahitaji mifumo mipya. Zana nyingi za miundo ulizo nazo katika uwezo wako, na tofauti, moyo wa kupenda, kuhusisha, ulazima itkuwa ni mafanikio ya programu yako.

Acknowledgements

Imeandaliwa na: Vijay Cuddeford, Meneja mhariri, Redio ya kilimo ya kimataifa
Imepitiwa upya na: Doug Ward, Mwenyekiti, Redio ya kimataifa ya wakulima, na David Mowbray, Meneja wa mafunzo na viwango, redio ya kimataifa ya kilimo.

gac-logoMradi uliofanywa na kupewa msada wa kifedha na nchi ya uliotolwa kupitia wakala wa kimataifa wa mendeleo. (CIDA)