Maswali ya mahojiano yaliyopendekezwa: Habari za Uwongo, Habari potofu na, COVID-19

Afya

Ujumbe kwa mtangazaji

Save and edit this resource as a Word document

Maelezo kwa Watangazaji

Maswali haya yameundwa ili kuwasaidia watangazaji kufanya mahojiano na wataalam wa vyombo vya habari na mawasiliano ambao wanaweza kuzungumzia masuala kama vile habari za uwongo, habari potofu, na taarifa zisizo sahihi, pamoja na suluhisho kama vile kuangalia kama habari ina ukweli. Unaweza kupata wataalam kama hao katika shirika la habari la eneo lako, au kikundi cha kijamii ambacho kinatoa mafunzo juu uandishi wa habari, kufikiria kwa kina, kuangalia ukweli wa habari, na masuala mengine yanayohusiana. Maswali haya yameundwa ili kukusaidia kuunda mijadala yenye taarifa kuhusu jinsi ya kutambua na kushughulikia habari feki, habari potofu na zisizo za kweli.

Ni muhimu kutambua kuwa habari za uongo, habari potofu, na habari za kughushi sio jambo geni. Zimekuwepo kwa kipindi chote cha dunia. Lakini, kwa kutumia vyombo vya habari vya leo vya utandawazi na intaneti, zinaweza kuenea zaidi na kwa urahisi zaidi—na hivyo kufanya uharibifu zaidi.

Wakati wa kupanga mahojiano yako, ni bora kuchagua mada tatu hadi tano kati ya zilizoorodheshwa ili kujadiliana na mhojiwa wako. Kuwekea kikomo mahojiano kwa idadi hii ya mada kutasaidia kuhakikisha kuwa mahojiano yanalenga zaidi, jambo ambalo litakuwa na manufaa zaidi kwa hadhira yako na kuepuka kuwajaza habari. Uliza baadhi au maswali yote ya ufuatiliaji ili kuchunguza mada kikamilifu na kuwapa hadhira yako taarifa wanayohitaji.

Ikiwa ungependa kutoa maelezo zaidi kuhusu mada hii, panga mfululizo wa mahojiano na mgeni huyo huyo au na wengine wanaoweza kuzungumza kuhusu masuala haya. Na kumbuka kwamba mahojiano mazuri yanatokana na kusikiliza kwa makini na maswali mazuri ya kufuatilia. Tumia maswali haya kama mwongozo wa mjadala wako lakini uwe mnyumbufu vya kutosha kufuata mjadala unapoongoza, na kuongeza au kuondoa maswali ya ufuatiliaji kama inavyotakiwa katika mahojiano yoyote.

Hadithi muhimu na habari potofu zinaweza kuja wakati wa majadiliano haya. Hakikisha kuwa umeshughulikia na kuyaondoa haya pamoja na mgeni wako, pamoja na simulizi nyinginezo ambazo ni maarufu katika jumuiya yako.

Hatimaye, dhana zinazojitokeza wakati wa mjadala wako zinaweza kuwa za kiufundi au za kisayansi. Kila mara waulize mhojiwa/wahojiwaji waeleze dhana kama hizi kwa maneno ya wazi na rahisi ambayo msikilizaji yeyote anaweza kuelewa. Ikiwa mgeni anatumia neno tata au la kitaalamu, waambie walielezee—hata kama unaelewa, wasikilizaji wako hawawezi kuelewa.

Script

1. Tafadhali eleza upotoshaji ni nini.

a. Maswali ya kufuatilia:

a.i. Wapi ambapo mtu anaweza akaona habari za kupotosha? Wanaweza wakaziona, kwa mfano kwenye mtandao wa intaneti, katika mitandao ya kijamii au WhatsApp? Wapi pengine wanaweza wakaona au kuzisikia?

a.ii. Habari za upotoshaji zinaonekanaje au zinasikikaje? Kwa mfano, zinakuja katika mfumo wa picha, video, makala zilizoandikwa, vipande vya sauti, n.k.?

a.ii.1. Tafadhali toa baadhi ya mifano ambayo wasikilizaji wetu wanaweza kuitambua.

2. Nini maana ya habari za uwongo?

a. Maswali ya kufuatilia:

a.i. Nini tofauti kati ya habari za upotoshaji na habari za uwongo?
a.ii. Tafadhali nipe mfano wa habari za uwongo.
a.iii. Ni aina gani ya habari hatarishi zaidi za uwongo na upotoshaji katika jamii yako?

3. Nini maana ya habari feki? Je, ni tofauti na habari za upotoshaji na habari za uwongo? Kama ndivyo, kivipi?

a. Maswali ya kufuatilia:

a.i. Wapi ambapo mtu anaweza akaona habari feki? Wanaweza wakaziona, kwa mfano kwenye mtandao wa intaneti, katika mitandao ya kijamii au WhatsApp? Wapi pengine wanaweza wakaona au kuzisikia?

a.ii. Je, kuna habari za uwongo katika vyombo vya habari vya kawaida kama vile TV, redio na magazeti—au ni mtandaoni pekee?

a.iii. Habari feki zinaonekanaje? Kwa mfano, zinakuja katika mfumo wa picha, video, makala zilizoandikwa, vipande vya sauti, n.k.?

a.iv. Je, ni rahisi kutambua habari za uwongo? Ikiwa ndivyo, unaitambuaje?

a.v. Tafadhali toa mifano ya habari feki.

a.vi. Je, kuna tofauti kati ya habari feki na makosa katika uwasilishaji? Kama ndio, nini tofauti?

a.vii.Tafadhali tupe mifano yoyote maarufu au ya hivi majuzi ya habari feki ambazo wasikilizaji wetu wanaweza kuzitambua.

a.vii.1. Nini ilikuwa ni madhara ya habari hizi feki?

4. Je, vipi ni baadhi ya vyanzo vya habari za upotoshaji, uwongo, na feki?

a. Maswali ya kufuatilia:

a.i. Yapi ni majukwaa maarufu ya kusambaza habari feki?
a.ii. Nani anaweza kusambaza habari feki?

5. Nini hatari ya habari za upotoshaji, uwongo na feki?

a. Maswali ya kufuatilia:

a.i. Tafadhali toa baadhi ya mifano ya jinsi habari potofu, habari za uwongo na habari feki zimesababisha madhara katika jamii au nchi yetu.

a.ii. Ni nani aliye hatarini zaidi kwa habari potofu, habari za uwongo, na habari feki?

a.iii. Je, ni hali gani mahususi ambapo habari potofu zinaweza kustawi na kuongezeka?

6. Je, kumekuwa na habari nyingi za uwongo, habari potofu, na habari feki wakati wa janga la COVID-19, na kuhusu chanjo za COVID-19?

a. Kama ndivyo, kwanini?
b. Kuna maswala mengine ambayo yanaonekana kutoa habari nyingi za uwongo na feki? Kwa nini?
c. Kwa nini habari za uwongo na habari feki zinatengenezwa?

c.i. Je, watu wanapata nini kwa kuunda na kushirikisha habari za uongo?

7. Hadithi nyingi za habari za uwongo zimeundwa ili kuleta “mshtuko.” “mshtuko” ni nini na inahusiana vipi na habari potofu, habari za uwongo na habari feki?

a. Maswali ya kufuatilia:

a.i. Tafadhali toa mifano ya habari zilizosambazwa “zenye kuleta mshtuko” ambazo wasikilizaji wetu wangetambua.

a.ii. Je, habari feki zinatengenezwa ili kuibua aina fulani za hisia kwa watu wanaoziona? Kwa nini?

8. “Fikra muhimu” ina maana gani katika muktadha wa vyombo vya habari, na inawezaje kutumiwa kutambua habari za uwongo, habari potofu na habari feki?

a. Maswali ya kufuatilia:

a.i. Je, watu wanawezaje kufikiri kwa kina kuhusu kile wanachosoma mtandaoni, kwenye mitandao ya kijamii, kwenye magazeti, kuona kwenye TV au kusikia kwenye redio?

a.ii. Je, kuna vidokezo na mbinu ambazo watu wanaweza kutumia ili kufikiria kwa kina kuhusu mambo wanayoona kwenye vyombo vya habari?

9. Mtu anawezaje kutambua habari potofu, habari za uwongo, au habari feki?

a. Maswali ya kufuatilia:

a.i. Je, kuna zana, ikiwa ni pamoja na zana za mtandaoni, ambazo watu wanaweza kutumia ili kutambua habari potofu au habari za uwongo?

a.ii. Inamaanisha nini “kuangalia chanzo”?

a.iii. Kwa nini ni muhimu kwamba kila mtu aweze kutambua habari potofu, habari za uwongo na habari feki?

a.iv. Uchunguzi wa ukweli ni nini?

a.iv.1. Ni aina gani ya zana ambazo watu wanapaswa kutumia ili kuangalia ukweli wa kile wanachokiona kwenye mitandao ya kijamii, kusikia kwenye redio, au kusoma kwenye gazeti?

a.iv.2. Je, mtu anapaswa kufanya nini mara tu anapogundua habari potofu, habari ya uwongo na habari feki?

10. Umeshirikisha habari za uwongo, unapaswa kufanya nini sasa?

a. Maswali ya kufuatilia:

a.i. Je, kuna adhabu za kisheria kwa kushirikisha au kuunda habari potofu, habari za uwongo na habari feki?

a.ii. Ikiwa mtu ataona picha, meme, au picha kwenye kikundi cha WhatsApp kwa mfano, na hafikirii kuwa ni ya kweli, anapaswa kufanya nini?

11. Wasikilizaji wanaweza kufanya nini ili kupambana na habari zisizo za kweli, habari za uwongo na habari feki katika jumii yao?

a. Maswali ya kufuatilia:

a.i. Je, ni rasilimali zipi za jamii au ushirikiano tunaoweza kutumia ili kupambana na taarifa potofu, habari za uwongo na habari feki?

Acknowledgements

Contributed by: Ted Phido, freelance writer, Lagos, Nigeria

This resource was created and translated thanks to funding by the Government of Canada through Global Affairs Canada as part of the Life-saving Public Health and Vaccine Communication at Scale in sub-Saharan Africa (or VACS) project.