Ujumbe kwa mtangazaji
Pakua na hariri taarifa hii kwa matumizi yako
Maelezo kwa mtangaaji
Wanyama wote wana mahitaji ya msingi, kama chakula na maji na nyumba nzuri. Lakini wanyama pia wana haja ya kutibiwa vizuri. Hii ni pamoja na kuishi katika mazingira mazuri, kuwa pamoja na wanyama wengine, na kuepuka hali ambazo husababisha shida kwa mnyama.
Wakati wanyama wanapopata huduma nzuri, hii ina faida kubwa kwa mmiliki. Mifugo ya ndani iliyotibiwa vizuri hutoa maziwa zaidi, kuwa wakubwa, na kuwa na watoto wenye afya. Ubora wa nyama yao pia ni bora zaidi.
Muongozo huu unalenga baadhi ya dhana za msingi za ustawi wa wanyama, na hutumia hadithi rahisi ya mtu, mwanawe na ng'ombe wao ili kuonyesha dhana izi halisi.
Mawazo ya kujali juu ya umuhimu wa ustawi wa wanyama imekuwa ikipanuka haraka katika ngazi ya kimataifa. Shirika la Dunia la Afya ya Mifugo linajitahidi kuanzisha viwango vya kimataifa kwa ustawi wa wanyama. Maelezo zaidi yanaweza kupatikana kutoka kwenye tovuti yao katika http://www.oie.int/eng/bien_etre/en_introduction.htm
Muongozo huu ni mazungumzo ya wenyeji wawili. Mwenyeji alizungumza na kujadiliana juu ya ustawi wa wanyama na kuwaambia hadithi ya kutunga. Kuna njia kadhaa za kutumia muongozo huu. Unaweza kubadilisha tu muongozo huu kulingana na hali yako kwa kubadilisha maelezo ya hadithi. Unaweza ukaboresha muongozo huu, kisha uwe na mjadala wa mzunguko juu ya ustawi wa wanyama. Waongoza majadala wakuu wanaweza kuwahusisha wafugaji wa ndani, wataalam wa wanyama kutoka huduma za ughani, wafugaji wa mifugo, na wengine. Unaweza pia kuchagua kupanua hadithi na kuunda igizo
fupi, kulingana na masuala ya ustawi wa wanyama yaliyotajwa katika muongozo huu.
Script
MWENYEJI 1:
Habari za asubuhi na karibu katika (jina la kipindi au kituo cha redio). Jina langu ni ___.
MWENYEJI 2:
Na mimi ___. Karibu katika kipindi cha leo kuhusu ustawi wa wanyama.
MWENYEJI 1:
Tunaishi kwa kutegemea wanyama wa kufugwa – lakini wanatutegemea sisi pia. Hivyo, ni vema kuhakikisha maisha ya wanyama wetu inaleta maana nzuri kwa mmiliki.
MWENYEJI 2:
Hiyo ni kweli. Hebu tuzungumze kuhusu ustawi wa wanyama. Je! Wanyama wanahitaji nini ili kukua vizuri, kutoa maziwa au kuzalisha watoto wenye afya? Ni nini kinachoathiri ustawi wao? Je! Inawezekana kwamba wakati mwingine tunaweza kufanya mambo ambayo husababisha shida zaidi kuliko mnyama anayeweza kukabiliana nao?
MWENYEJI 1:
Ni swali zuri. Tunatumia wanyama kwa usafirishaji, kuvuta jembe au gari, kwa ajili ya maziwa, nyama na vitu vingine vingi. Kwa hiyo, ustawi wa wanyama ni muhimu kwa wamiliki wao. Ikiwa tutawatunza vibaya, mnyama atakuwa na mazao duni, thamani ya chini na kumgharimu mfugaji fedha zaidi.
MWENYEJI 2:
Kwa hiyo ustawi mzuri wa wanyama una faida kubwa. Wakati wanyama wanapotendewa vibaya, kutokuwajali au kuzingatia kuwaweka katika mazingira mazuri, inaweza kuwa na gharama kubwa kwa mmiliki. Lakini tunasikia hadithi ambazo zilitokea wakati wote. Kwa nini?
MWENYEJI 1:
Hebu tusikilize hadithi ya mkulima ambaye alikuwa na wanyama wachache, na labda tunaweza kujua ukweli zaidi.
MWENYEJI 2:
Mfugaji mmoja alikuwa na wanyama wachache kwenye sehemu yake ndogo ya ardhi. Kulikuwa na kondoo na mbuzi wachache, na ng’ombe mmoja aliyotumia kupata maziwa. Mwanawe wakati mwingine alisaidiana na babaye kuwatunza wanyama. Hata hivyo, huyo mtu aliona kwamba siku ambazo mtoto alisaidia, ng’ombe huyo alionekana kuwa na hofu zaidi. Hakula kwa urahisi na haikuwa rahisi kumshughulikia. Kisha siku moja ngombe alifungwa kitanzi.
MWENYEJI 1:
Unadhani nini kilikuwa kinatokea? Je! Una wazo lolote?
MWENYEJI 2:
Kabla ya kurudi kwenye hadithi yetu, hebu tuzungumze zaidi juu ya ustawi wa wanyama. Tunawezaje kuelezea ustawi wa wanyama maskini? Pengine, si tofauti sana na kile kinachotokea kwa wanadamu tunapokuwa chini ya shida kali.
MWENYEJI 1:
Hiyo ni sawa. Tunapokuwa na hofu au wasiwasi au labda hata kudhulumiwa na wengine, tunafanya tofauti. Tunapokula au kunywa vizuri, au afya yetu kuharibika. Tunapojeruhiwa, labda hatuwezi kufanya kazi kama kawaida, au tunaweza kuzalisha tabia nyingine ya maambukizi.
MWENYEJI 2:
Hiyo hutokea kwa wanyama. Ikiwa mnyama hawezi kukabili matatizo katika mazingira yake, hataweza kufanya vizuri pia. Anaweza kukua pole pole na kutofikia ukubwa sawa na wanyama wengine, kutoa maziwa kidogo, kuwa kipofu, au kupata magonjwa.
MWENYEJI 1:
Wanyama wengine pia wanahitaji umakini zaidi kuliko wengine. Hii haina maana tu kutaja kuwa zaidi ya matatizo ya kimwili na kuumia kimwili, lakini pia matatizo katika maeneo mengine kama vile afya, uzazi au hali ya akili ya wanyama.
MWENYEJI 2:
Lakini daima kuna dalili kwa ustawi wa wanyama. Fikiria juu ya ishara zifuatazo:
- mnyama hali au kunywa vya kutosha
- mnyama anaonekana kuwa dhaifu kiafya, labda kioo-macho, kupoteza nywele, na kutokwa kwa makamasi puani
- mnyama hawezi kuzaa au hupoteza uzao wake wakati wa kuzaliwa
- mnyama anafanya tabia ya kawaida ya kurudia rudia kama vile kung’ata vitu, au kujilamba mara kwa mara
- mnyama hakui vizuri kwa umri wake
- mnyama anakuwa mlemavu au haiwezi kuchangamka na huepuka kuingiliana na wanyama wengine
- mnyama anakuwa na hofu karibu anapokuwa na watu au wanyama wengine
MWENYEJI 1:
Hizi zinaweza kuwa dalili kwamba wanyama hawatendewi au hawakufanyiwa vizuri ama hawakuweza kuhukuliana na mazingira yake. Kuna mifano mingi ya dalili hizi. Huenda umeona baadhi ya dalili hizi, labda katika wanyama wa jirani, au hata wako mwenyewe. Lakini dalili nyingine zinaweza pia kuwa zimejificha sana na zinahitaji uchunguzi wa makini. Tunawezaje kufanya hivyo? Njia moja ni kwamba, badala ya kuelekeza tu mahali ambapo tunapotaka ng’ombe aende, labda itasaidia kuelewa kwa nini hawataki kwenda mahali hapo?
Usisahau kwamba wanyama wa ndani wanaishi katika mazingira ya kibinadamu. Ikiwa ustawi wao ni duni kwa sababu wanateswa, kwa sababu ya hali duni ya mazingira ambayo wanaishi, au kwa sababu ya mahitaji yao ya msingi hayakufikiwa vizuri, bado ni mmiliki au mhudumiaji ambaye anahitaji kujua jinsi ya kurekebisha tatizo. Huduma nzuri kwa mnyama matokeo yake itakusaidia wewe na familia yako.
MWENYEJI 2:
Hivyo, ustawi mzuri wa wanyama ni muhimu kwa wanyama yenyewe. Ustawi wa mifugo duni una matokeo mengine duni kwa mmiliki.
MWENYEJI 1:
Wakati wanyama wenye mshukutuko na shida wanapochinjwa, ubora wa nyama ni dhaifu sana, husababisha mazao ya nyama kuwa chini sana na uduni wakati inapopikwa. Mara nyingi, nyama haifai pia. Gharama nyingine ya ustawi wa mifugo ambayo ni kwamba wanyama wenye mshutuko na shida huwa na shida zaidi kwa ujauzito na wakati wa kuzaa, pia huwa na watoto wadogo na wachache.
Pia kuna utafiti wa kisayansi unaovutia sana ambao unaonyesha kwamba watu ambao huwatendea wanyama vibaya wana uwezekano mkubwa wa kuwatendea wanadamu wenzao kwa ukatili vile vile. Hatimaye, kuwanyanyasa wanyama mara nyingi ni kinyume na kanuni za kidini na matarajio ya wazee wa jamii.
MWENYEJI 2:
Kwa hiyo, ni nini wanyama wanahitaji ili kufanya vizuri? Njia moja ya kuelezea mahitaji ya msingi ya wanyama ni kwa kujua nini kiepukwe juu yao, au ni nini wanyama wanapaswa kutendewa wawe huru.
MWENYEJI 1:
Njia kuu tano za uhuru ni:
- Uhuru kutoka katika kiu, njaa na utapiamlo – kwa kuhakikisha upatikanaji wa maji safi na chakula ambayo ina afya kamili na nguvu.
- Uhuru kutoka katika usumbufu – kwa kutoa mazingira mazuri, ikiwa ni pamoja na makao na mahali pa kupumzika vizuri.
- Uhuru kutoka katika maumivu, kuumia na ugonjwa – kwa kuzuia au kuwafanyia uchunguzi wa haraka na kuwapa matibabu.
- Uhuru wa kudhihirisha tabia ya kawaida – kwa kutoa nafasi ya kutosha, vituo sahihi, na aina ya wanyama.
- Uhuru kutoka katika hofu na dhiki – kwa kuhakikisha hali zinazozuia mateso ya akili.
MWENYEJI 2:
Haya ni mahitaji ya msingi. Ikiwa hawatunzwi, hatuwezi kutarajia wanyama kufanya kama vile tulivyowatazamia. Na hilo sio zuri kwa mmiliki.
MWENYEJI 1:
Sasa hebu turudi katika hadithi yetu ya mtu na ng’ombe wake. Siku moja, mmiliki hakulazimika kwenda mjini. Kwa hivyo aliamua kuangalia alichokuwa akifanya mwana wake. Kila kitu kilionekana sawa. Kisha wakati wa kulisha, alimwona mwanawe akiweka vipandikizi vya nafaka na mboga katika kona ya mbali ya makazi ya ng’ombe, ambayo ilikuwa giza giza. Ng’ombe hakuenda mara moja huko, hivyo mtoto wake akachukua kipande cha mbao na kumpiga ng’ombe kwenye mguu kumlazimisha kuelekea katika ile kona ya giza yenye chakula.
MWENYEJI 2:
Kwa hekima, mmiliki aliingia ndani. Alimwambia mtoto wake kwa haraka kuwa ng’ombe huwa makini sana kwa kawaida huchukua tahadhari juu ya kuingia mahali pa giza ambapo hawezi kuona pia. Inaweza kuwa chaguo bora zaidi kuhamisha chakula, kutoa eneo lenye mwanga zaidi, au mpe ng’ombe ili kujilisha mwenyewe.
MWENYEJI 1:
Pia ikabadilika kuwa, katika kona ya giza, kulikuwa na vitu vyenye ncha kali kali toka nje ya ukuta ambao ilijeruhiwa mguu wa ng’ombe. Pamoja na mtu huyo na mwanawe ilibidi waweke ukuta na kuhamisha nafasi ya kulisha. Baadaye, ng’ombe alikaa vizuri.
MWENYEJI 2:
Kumbuka: ustawi mzuri wa wanyama hauna gharama ya pesa. Kwa kweli, mara nyingi huokoa pesa kwa kuzuia hasara za gharama kubwa. Mwishoni, mnyama aliyetunzwa vizuri atafanya vizuri, kukua kwa kasi, kuzalisha bidhaa bora zaidi, kuwa rahisi kushughulikia, na kuwa na kufurahia zaidi kummliki.
MWENYEJI 1:
Hii ni kweli kabisa. Mnyama aliye katika hali nzuri ya ustawi ni muhimu sana kwa faida yako. Ustawi wa wanyama ni wajibu wa kila mtu.
MWENYEJI 2:
Mimi ni (jina la mwenyeji), nikisema kwaheri kwa sasa.
MWENYEJI 1:
Na mimi ni (jina la mwenyeji). Kwaheri.
Acknowledgements
Shukrani
Imetolewa na: David Trus, Agrologist Mtaalamu, Taasisi ya Wakulima wa Ontario. Daudi pia huratibu masuala ya ustawi wa wanyama katika Idara ya Kilimo na Chakula Canada.
Tafsiri ya hati hii inafadhiliwa na ELANCO ANIMAL HEALTH