Ujumbe kwa mtangazaji
Save and edit this resource as a Word document
Maelezo kwa watangazaji
Maswali haya yameundwa ili kukusaidia kufanya mahojiano kuhusu jinsi janga la COVID-19 limeathiri makundi sita tofauti ya watu walio hatarini au waliotengwa katika jamii yako: Wanawake na wasichana, vijana, wazee, watu walio na kinga dhaifu, wakimbizi na watu wasio na makazi, na watu wenye mahitaji maalum au ulemavu. Kwa kila moja ya makundi haya, tunatoa maswali manne hadi nane.
Utahitaji kuuliza maswali haya kwa watu ambao wana uzoefu wa kufanya kazi na makundi haya yaliyo hatarini moja kwa moja ili waweze kuzungumza kuhusu jinsi janga la COVID-19 limewaathiri. Unaweza kupata watu kama hao wanaofanya kazi na vikundi vya wanawake, ushirika wa vijana, ofisi za mashirika ya kimataifa kama vile Marie Stopes International, Plan International, na Girl Effect, au katika wizara za serikali za mitaa zinazoshughulika moja kwa moja na makundi haya sita. Utahitaji zaidi ya mhojiwa mmoja ili kupata uzoefu wa kila mmoja katika kufanya kazi na vikundi hivi.
Kumbuka kwamba baadhi au maswali yote unayouliza kikundi kimoja yanaweza kutumika kwa kikundi kingine. Kwa hivyo, unapojiandaa kwa mahojiano yako, hakikisha umekagua maswali yote katika waraka huu na uzingatie jinsi maswali yanayoelekezwa kwa wanawake na wasichana yanaweza pia kutumika, kwa mfano, kwa vijana au wazee.
Ikiwa ungependa kutoa maelezo zaidi kuhusu mada zinazoshughulikiwa katika rasilimali hii, panga mfululizo wa mahojiano na mgeni yuleyule, au na wengine wanaoweza kuzungumza kuhusu masuala haya. Kama sehemu ya mfululizo huu, unaweza pia kutaka kuzungumza na wanawake, vijana, wazee, watu wenye ulemavu, na watu walio na mifumo ya kinga ya mwili iliyoathiriwa ili waweze kushirikisha uzoefu wao wenyewe kuhusiana na janga la COVID-19.
Kumbuka kwamba mahojiano mazuri yanatokana na usikilizaji makini na maswali mazuri ya ufuatiliaji. Tumia maswali haya kama mwongozo wa mjadala wako lakini uwe mnyumbufu vya kutosha kufuata mjadala jinsi unavyokwenda.
Hadithi muhimu na habari potofu zinaweza kuja wakati wa majadiliano haya. Hakikisha kuwa umeshughulikia na kuyaondoa haya pamoja na mgeni wako, pamoja na simulizi nyinginezo ambazo ni maarufu katika jumuiya yako.
Hatimaye, dhana zinazojitokeza wakati wa mjadala wako zinaweza kuwa za kiufundi au za kisayansi. Kila mara waulize mhojiwa/wahojiwaji waeleze dhana kama hizi kwa maneno ya wazi na rahisi ambayo msikilizaji yeyote anaweza kuelewa. Ikiwa mgeni anatumia neno tata au la kitaalamu, waambie walielezee—hata kama unaelewa, wasikilizaji wako hawawezi kuelewa.
Script
Maswali yaliyopendekezwa kuhusu wanawake na wasichana
1. Je, janga la COVID-19 limeathiri hali ya kiuchumi ya wanawake?
a. Kama ndio, kivipi?
i. Je, ongezeko la bei za vyakula na vifaa vingine vya nyumbani linaathiri usalama wa chakula wa wanawake na familia zao? Ikiwa ndivyo, ni kwa jinsi gani?
ii. Kwa wanawake ambao walilazimika kufunga biashara zao wakati wa janga hili, ni changamoto gani wanakumbana nazo wanapojaribu kuanzisha tena biashara zao, au kufungua biashara mpya?
iii. Je, wanawake wanakabiliwa na changamoto za kupata fedha za kusaidia kurejesha biashara zao? Kama ndiyo, changamoto hizi ni zipi?
iv. Je, kwa wanawake ambao maeneo yao ya kazi yalifungwa wakati wa janga la COVID-19, nini imekuwa ni athari kwao na familia zao?
v. Wanawake wanafanya nini ili kuondokana na changamoto hizi za kiuchumi?
2. Je, janga la COVID-19 limeathiri vipi uwezo wa wanawake kukusanyika katika vikundi, kwa mfano, vikundi vya kuweka na kukopa, vikundi vya uuzaji na aina zingine za vikundi vya kijamii?
a. Je, ni kwa jinsi gani hii imeathiri maisha ya wanawake na maisha ya watu katika jamii zao?
3. Je, wanawake wanaathiriwa vipi na huduma za afya wakihama kutoka huduma za jumla na zinazolenga wanawake hadi huduma zinazohusiana na COVID-19?
a. Je, wanawake wajawazito wanakabiliwa na changamoto za kupata huduma ya kabla ya kujifungua wakati wa janga la COVID-19? Ikiwa ndivyo, tafadhali eleza.
i. Nini kinasababisha changamoto hizi?
ii. Wanawake wanakabiliana vipi na changamoto hizi?
iii. Je, kuna huduma au usaidizi unaopatikana kuwasaidia wanawake?
b. Ni changamoto zipi wanawake hukabiliana nazo wanapotafuta usaidizi wa kimatibabu ili kujifungua au kutoa mimba wakati wa janga la COVID-19?
i. Ni kitu gani kinasababisha changamoto hizi?
ii. Wanawake wanakabiliana vipi na changamoto hizi?
iii. Je, kuna huduma au usaidizi unaopatikana kuwasaidia wanawake?
c. Je, wanawake wana rasilimali wanazohitaji ili kubaki salama kutokana na COVID-19?
d. Je, janga hili linafanya kuwa vigumu kwa wanawake kupata maji ya kunawa mikono katika eneo lako?
i. Ikiwa ndivyo, ni nini athari?
e. Je, wanawake wanaweza kupata vitu wanavyohitaji kwa urahisi ili kuwalinda kutokana na COVID-19, kama vile barakoa, na visafisha mikono?
i. Kama sivyo, ni matatizo gani ambayo wanawake wanakumbana nayo katika kujaribu kupata vitu hivi?
f. Je, huduma nyingine za afya kwa wanawake zimeathiriwa vibaya? Ikiwa ndivyo, eleza.
4. Je, unyanyasaji wa kijinsia umeongezeka wakati wa janga la COVID-19?
a. Kama ndiyo, ni nini baadhi ya sababu za ongezeko hili la unyanyasaji?
b. Je, wanawake wanaripoti ukatili wa kijinsia unapotokea wakati wa janga hili?
c. Je, vyombo vya kutekeleza sheria vinapatikana kwa urahisi kushughulikia ripoti za unyanyasaji wa kijinsia?
i. Vinashughulikia ripoti hizi kwa ufanisi?
ii. Je, wanawake wanahisi usalama kuripoti matukio ya unyanyasaji wa kijinsia kwa watekelezaji wa sheria?
1. Kama sivyo, kwanini?
iii. Je, kumekuwa na ongezeko la ripoti za ubakaji au aina nyingine za unyanyasaji wa kingono na kijinsia?
iv. Je, waathirika wa unyanyasaji wa kijinsia wanapata usaidizi waliohitaji?
v. Ni huduma gani na mifumo ya usaidizi unaopatikana kwa wanawake walionusurika na unyanyasaji wa kijinsia?
5. Je, kazi za nyumbani za wanawake zimeongezeka wakati wa janga la COVID-19?
a. Je, hii inaathirije wanawake kihisia, kiakili, na kimwili?
b. Je, ni matokeo gani mengine ya ongezeko hili la mzigo wa kazi kwa wanawake na familia zao?
c. Waume, watoto, na wanafamilia wengine wanaweza kufanya nini ili kusaidia wanawake kwa mzigo wao wa kazi wakati wa janga la COVID-19 na zaidi?
6. Je, wanawake wana taarifa za kutosha kuhusu janga hili na jinsi ya kujikinga na magonjwa na kueneza COVID-19?
a. Ikiwa sivyo, ni nini sababu kuu ya ukosefu wa taarifa miongoni mwa wanawake?
b. Je, nini kifanyike ili kuwafikia wanawake kwa ufanisi zaidi na taarifa kuhusu uzuiaji wa COVID-19, ikiwa ni pamoja na chanjo za COVID-19?
c. Je, wanawake sasa wana ujuzi wa kutosha kuhusu upatikanaji wa chanjo za COVID-19?
7. Je, kufungwa kwa shule wakati wa janga la COVID-19 kuliathiri vipi wanawake na wasichana?
a. Je, ilikuwa vigumu zaidi kwa wasichana kuliko wavulana kufika shuleni? Ikiwa ndio, tafadhali eleza hali hiyo.
b. Je, kufungwa kwa shule kumekuwa na matokeo gani kwa madaraja ya ufaulu kwa wasichana na vipengele vingine vya masomo yao?
c. Je, ni matokeo gani mengine ya wasichana kukosa elimu wakati wa janga la COVID-19?
8. Je, janga la COVID-19 linaathiri vipi wanawake na wasichana kihisia, kiakili, na kimwili?
a. Watu wanapoanza kupata chanjo dhidi ya COVID-19, je, hali inaimarika kwa wanawake na wasichana?
b. Je, watu katika jamii wanaweza kufanya nini kusaidia wanawake wakati wa janga la COVID-19 na zaidi?
Maswali yaliyopendekezwa kuhusu vijana
1. Je, janga la COVID-19 linaathiri vipi vijana katika masuala ya elimu na taaluma zao?
a. Ni aina gani ya changamoto wanazokumbana nazo vijana katika masomo yao kutokana na janga la COVID-19?
i. Ikiwa elimu yao imekatizwa, je, vijana wameweza kuendelea na masomo yao? Ikiwa sivyo, tafadhali eleza hali hiyo.
b. Ni aina gani za changamoto za kijamii ambazo vijana wanakabiliana nazo sasa kutokana na janga la COVID-19? Kwa mfano, je, vijana wanakabiliwa na kutengwa na jamii, au masuala ya kisaikolojia kama vile msongo wa mawazo, au ujuzi wao wa kijamii umedidimizwa?
i. Ni nini athari za changamoto hizi za kijamii kwa vijana?
c. Je, ni mifumo gani ya usaidizi inapatikana kusaidia vijana wakati wa janga la COVID-19?
i. Je, vijana wanapata huduma za ushauri nasaha?
1. Ikiwa sivyo, matokeo yake ni yapi?
ii. Je, wanafamilia na jamii ya vijana ambao wamekuwa wakikabiliana na athari za janga hili wanaungwa mkono kiasi gani? Tafadhali eleza.
d. Je, vijana wanakabiliana vipi na changamoto za kijamii na kiuchumi kama vile kutengwa na ukosefu wa fursa za ajira kutokana na janga hili?
2. Je, vijana wanaathiriwa vipi na huduma za afya kuhama kutoka huduma za jumla hadi huduma zinazohusiana na COVID-19?
i. Je, huduma za afya ya uzazi wa mpango zimekatizwa?
1. Ikiwa ndivyo, hii inaathiri vipi vijana?
3. Je, vijana wana taarifa za kutosha kuhusu janga hili na jinsi ya kujikinga na magonjwa na kueneza COVID-19?
a. Ikiwa sivyo, ni nini sababu kuu ya ukosefu wa taarifa miongoni mwa vijana?
b. Je, nini kifanyike ili kuwafikia vijana kwa ufanisi zaidi na kuwapa taarifa kuhusu uzuiaji wa COVID-19, ikiwa ni pamoja na chanjo za COVID-19?
4. Je, janga la COVID-19 linaathiri vipi vijana kihisia, kiakili, na kimwili?
a. Je, watu katika jamii wanaweza kufanya nini kusaidia vijana wakati wa janga la COVID-19 na zaidi?
Maswali yaliyopendekezwa kuhusu wazee
1. Je, COVID 19 inaathiri vipi maisha ya kila siku ya wazee?
a. Ni shughuli gani imezuiwa au zimezuiwa kwa wazee kwa sababu ya janga la COVID-19?
i. Je, wazee wanaweza kupata kwa urahisi mahitaji ya kila siku kama vile chakula, maji na dawa?
1. Ikiwa sivyo, matokeo yake ni nini?
2. Je, COVID-19 ni hatari kwa wazee?
a. Je! wazee wanaugua COVID-19 kwa viwango kikubwa kuliko watu wengine?
b. Je, kuna idadi kubwa ya kulazwa hospitalini na vifo kutokana na COVID-19 kwa wazee?
i. Ikiwa ndivyo, kwa nini? Ni nini huwafanya wazee kuwa hatarini zaidi kwa COVID-19?.
3. Je, wazee wanaweza kupata taarifa muhimu kuhusu kuzuia na kuenea kwa COVID-19?
a. Je, ukosefu wa ujuzi wa mtandaoni na wa kidijitali unawazuia wazee kupata taarifa kuhusu COVID-19? Kama ndiyo, ni njia gani mbadala ya kupata taarifa ambayo wazee hutumia?
b. Je, nini kifanyike ili kuwafikia wazee kwa ufanisi zaidi na kuwapa taarifa kuhusu uzuiaji wa COVID-19, ikiwa ni pamoja na chanjo za COVID-19?
c. Je, wazee kwa sasa wana ujuzi wa kutosha kuhusu upatikanaji wa chanjo za COVID-19?
4. Je, wazee wanaathiriwa vipi na huduma za afya kuhama kutoka huduma za jumla hadi huduma zinazohusiana na COVID-19?
5. Je! Janga la COVID-19 linaathiri vipi maisha ya kijamii ya wazee?
a. Wazee wanakabiliana vipi na athari za kutokukaa karibu kati ya mtu na mtu katika maisha yao ya kijamii?
b. Ni nini matokeo ya kuongezeka kwa kutengwa kijamii kwa wazee?
6. Je, janga la COVID-19 linaathiri vipi wazee kihisia, kiakili, na kimwili?
a. Je, watu katika jamii wanaweza kufanya nini kusaidia wazee wakati wa janga la COVID-19 na zaidi?
Maswali yanayopendekezwa kuhusu watu walio na kinga dhaifu
1. Inamaanisha nini kwa mfumo wa kinga ya mtu kuathiriwa?
a. Ni magonjwa au hali gani zinaweza kusababisha mfumo wa kinga wa mtu kuathirika?
2. Je, COVID-19 ni hatari zaidi kwa watu walio na kinga dhaifu?
a. Je, watu walio na kinga dhaifu wanaugua zaidi COVID-19 kwa viwango vya juu kuliko watu wengine?
b. Je, kuna viwango vya juu vya kulazwa hospitalini na vifo kutokana na COVID-19 kwa watu walio na kinga dhaifu?
i. Ikiwa ndivyo, kwa nini? Ni nini huwafanya watu walio na kinga dhaifu kuwa katika hatari zaidi ya COVID-19?
3. Je, watu walio na mifumo ya kinga ya mwili iliyoathiriwa, ikiwa ni pamoja na watu walio na VVU, wanaathiriwa vipi na huduma za afya kuhama kutoka huduma za jumla hadi huduma zinazohusiana na COVID-19?
a. Je, upasuaji muhimu au matibabu yameahirishwa au kucheleweshwa?
b. Je, watu walio na kinga dhaifu wanaweza kupata dawa wanazohitaji?
c. Je, mabadiliko haya katika mfumo wa huduma ya afya yana athari gani kwa afya ya watu walio na kinga dhaifu?
d. Je, watu walio na kinga dhaifu wanaweza kupata chanjo za COVID kwa urahisi, ikiwa ni pamoja na chanjo za nyongeza?
4. Ni hatua gani maalum ambazo watu walio na mifumo ya kinga ya mwili iliyoathiriwa huchukua ili kujilinda kutokana na COVID-19?
5. Je, janga la COVID-19 linaathiri vipi watu walio na kinga dhaifu kihisia, kiakili, na kimwili?
a. Je, watu katika jamii wanaweza kufanya nini kusaidia watu walio na kinga dhaifu wakati wa janga la COVID-19 na zaidi?
Maswali yanayopendekezwa kuhusu wakimbizi na watu wasio na makazi
1. Je, watu wasio na makazi na wakimbizi wana hatari zaidi ya kuugua sana COVID-19?
a. Ikiwa ndivyo, kwa nini na kwa jinsi gani?
i. Je, wakimbizi na wasio na makazi wanaweza kujilinda kutokana na COVID-19? Ikiwa sivyo, tafadhali eleza matatizo yoyote wanayokumbana nayo wanapojaribu kupata barakoa, kusafisha mikono na kupata chanjo.
2. Je, wakimbizi na wasio na makazi wana taarifa za kutosha kuhusu janga hili na jinsi ya kujikinga na magonjwa na kueneza COVID-19?
a. Ikiwa sivyo, ni nini sababu kuu ya ukosefu huu wa taarifa?
b. Je, nini kifanyike ili kuwafikia wakimbizi na wasio na makazi kwa ufanisi zaidi na kuwapa taarifa kuhusu uzuiaji wa COVID-19, ikiwa ni pamoja na chanjo za COVID-19?
c. Je, wakimbizi na wasio na makazi sasa wana ujuzi wa kutosha kuhusu upatikanaji wa chanjo za COVID-19?
3. Je, janga hili linaathiri vipi wakimbizi na watu wasio na makazi kifedha?
a. Je! Wakimbizi wameweza kuendelea na biashara zao ndogo wakati wa janga hili?
i. Ikiwa sivyo, hiyo inaathiri vipi maisha yao?
ii. Je, wakimbizi wanakabiliana vipi na athari hizi?
4. Je, uhaba wa chakula kwa wakimbizi na wasio na makazi uliongezeka wakati wa janga la COVID-19?
a. Kama ndiyo, kuna huduma zinazopatikana kusaidia usalama wa chakula kwa wakimbizi na wasio na makazi? Kivipi?
b. Je, ni kwa namna gani tena wakimbizi na wasio na makazi wanakabiliana na uhaba wa chakula?
5. Je, gonjwa la COVID-19 linaathiri vipi wakimbizi na wasio na makazi kihisia, kiakili na kimwili?
a. Watu katika jumuiya wanaweza kufanya nini ili kusaidia wakimbizi na wasio na makazi wakati wa janga la COVID-19 na zaidi?
Maswali yanayopendekezwa kuhusu watu wenye mahitaji maalum au ulemavu
1. Inamaanisha nini kwa mtu kuwa na mahitaji maalum au ulemavu?
2. Je, COVID-19 inaathiri vipi maisha ya kila siku ya watu wenye mahitaji maalum au ulemavu?
a. Kwa sababu ya janga la COVID-19, ni shughuli gani imewekewa au zimewekewa vikwazo kwa watu wenye mahitaji maalum au ulemavu?
i. Je, watu wenye mahitaji maalum au ulemavu wanaweza kupata mahitaji ya kila siku kama vile chakula, maji na dawa?
1. Ikiwa sivyo, matokeo yake yamekuwa nini?
3. Je, watu wenye mahitaji maalum au ulemavu wana taarifa za kutosha kuhusu janga hili na jinsi ya kujikinga na magonjwa na kueneza COVID-19?
a. Ikiwa sivyo, ni nini sababu kuu ya ukosefu wa taarifa?
b. Je, nini kifanyike ili kufikia watu wenye mahitaji maalum au ulemavu kwa ufanisi zaidi na kuwapa taarifa kuhusu uzuiaji wa COVID-19, ikiwa ni pamoja na chanjo za COVID-19?
c. Je, watu wenye mahitaji maalum au ulemavu sasa wana ujuzi wa kutosha kuhusu upatikanaji wa chanjo za COVID-19?
4. Watu wenye mahitaji maalum au ulemavu wamechukua hatua gani maalum ili kujilinda kutokana na COVID-19?
5. Je, janga la COVID-19 linakatiza vipi huduma kwa watu wenye mahitaji maalum au ulemavu?
a. Je, watu wenye mahitaji maalum au ulemavu wanaweza kupata usaidizi na matunzo wanayohitaji?
i. Ikiwa sivyo, ni nini athari za usumbufu huu katika usaidizi na utunzaji wa watu wenye mahitaji maalumu?
6. Je! janga la COVID-19 linaathiri vipi maisha ya kijamii ya watu wenye mahitaji maalum au ulemavu?
a. Je, watu wenye mahitaji maalum au ulemavu wanakabiliana vipi na athari za kukaa kwa umbali kati ya mtu na mtu katika maisha yao ya kijamii?
b. Ni nini matokeo ya kuongezeka kwa utengano wa kijamii kwa watu wenye mahitaji maalum au ulemavu?
7. Je, COVID-19 ni hatari zaidi kwa watu wenye mahitaji maalum na ulemavu? Kwa nini au kwa sio hatari?
8. Je! Ugonjwa wa COVID-19 unaathiri vipi watu wenye mahitaji maalum, ulemavu, na magonjwa ya akili kiakili, kihisia na kimwili?
a. Watu katika jamii wanaweza kufanya nini ili kusaidia watu wenye mahitaji maalum au ulemavu wakati wa janga la COVID-19 na zaidi?
Acknowledgements
Contributed by: Neo Brown, freelance writer and communications expert, Addis Ababa, Ethiopia