Ujumbe kwa mtangazaji
Pakua na hariri taarifa hii kwa matumizi yako.
Maelezo kwa Mtangazaji
Makala hii ya matangazo. Ni makala ya maojiano kati ya Philip Chhinkhokwe, mtayarishaji wa matangazo ya redio katika Nkhotakota kituo cha redio nchini Malawi. Katika mahojiano Philip anaelezea jinsi kituo chake kinafanya utafiti wa wasikilizaji, na anatoa mfano wa utafiti uliofanywa katika programu za kilimo cha hifadhi. Sehemu ya pili ya makala hii ni hati kutoka programu ya redio juu ya kilimo cha hifadhi unaolenga utafiti wa wasikilizaji ulioelezwa katika mahojiano.
Soma kupitia kipande hiki na ona kama kuna kufanana kokote jinsi kituo chako kinafanya utafiti wa wasikilizaji na jinsi Nkhotakota inafanya utafiti wa wasikilizaji. Je, kuna mafunzo yeyote unayoweza kujifunza kutokana na utendaji wa Nkhotakota? Angalia jinsi sauti za wakulima zinavyoonekana katika vipengele kwenye programu ya Nkhotakota, na jinsi gani kituo kinatumia vema upatikanaji haba wa raslimali kwa kutegemea uwepo wa programu nyingine bajeti na programu za mashirika mengine.
Kama ilivyoelezwa katika kipengele namba moja, kwa kuunda programu za kilimo kwa ufanisi ambazo zinaendana na mahitaji ya wasikilizaji wako ni lazima ujue wasikilizaji wako ni wa aina gani, na ujue ni taarifa gani ya kilimo ni muhimu kwo. Baadhi ya shughuli za kilimo ambabazo Philipo anazielezea hapa chini ni njia nzuri za kujua wasikilizaji wako na kutafuta mahitaji yao
Script
Utangulizi.
Wakati vituo vya redio vinatangaazia wasikilizaji wake kuhusu nini wanataka kusikia redioni, kuandaa matangazo kwa njia ya stesheni kunaweza kutekeleza ………………….. Msikilizaji anaweza kujihusisha katika uandaaji kwa kukuambia nini wanachotaka kusikia na ni lini wanataka kukisikia na kufanya sauti zao zisikike hewani.
Maelezo ya Mtangazaji yafuatayo yamegawanywa katika sehemu mbili. Sehemu ya kwanza ni mahojiano kati ya Philipo Chinkhokwe, Mtagazji wa kituo cha redio jamii Nkhotakota ya Malawi. Katika mahojiano, Philip anaeleza jinsi kituo chake cha redio kinafanya utafiti kuunda programu za wakulima na wadau kama Wizara ya Kilimo na Mashirika yasiyo yasiyo ya kibiashara. Sehemu ya pili ni transcript ya sehemu ya programu ambayo Philip ameitengeneza ikihusisha utafiti yeye na wenzake walioufanya.
Sehemu ya kwanza: Mahojiano na mtegenezaji/mwandaa matangazo.
Zaidi ya kozi za programu, kwa mfano mahindi, tunatembelea wakulima mara kwa mara. Tunarekodi sauti zao na kuzitumia kama kumbukumbu katika programu zetu na tunaweka kumbukumbu ya hadithi za mafanikio. Wakulima pia hupata huduma ughani ya moja kwa moja. Wakulima hawa wanaitwa “Wakulima Hai.
Idara za Kilimo zinatuelekeza kwenye maeneo mengine ambapo pia wakulima wanalima mazao haya lakini hawajapata utendaji bora kwa mapana kama ‘Mkulma Hai.’ Wakulima hawa husikiliza kutoka katika programu na kutupa maoni. Mara nyingine tunawatembelea na kurekodi hadithi za mafanikio na kukadiria athari ya programu zetu kwa watu wanaosikiliza kwa muda huo. ‘hawa tunawaita wasikilizaji baridi/wasikilizaji wakimya kimya.
[Muhtasari wa mhariri: Kwa Mwongozo jinsi ya kupatataarifa, angalia kipengee cha kanza katika mfululizo huu]
Halafi tunaunda vikundi vya kusikiliza katika jamii ambazo zinataka Na mahali ambapo watu wanahisi programu inaweza kuwapatia. Mahitaji yao kwa njia ya taarifa.
Tunaanzisha vikundi kwa kusaidiwa. Na wafanyakazi ughani na kiongozi wa kijiji. kiongozi wa kijijii wanaitisha mkutano kijijini na tunahudhuria mkutano tukiambatana na wafanyakazi ughani. vikundi kwa kawaida vina watu karibu.
Tunawaambia kwa muhtasari wasikilizaji kuhusu programu zijazo.
Licha ya maeneo hai na yasiyo hai kuna wasikilizaji wengine ambao husikia kuhusu programu zetu kwa njia ya promosheni na kupigia stesheni kuelezea nia zao za kujiunga. Wasikilizaji hawa huunda vikundi na kama wasikilizaji hai na wasio hai tunazichukua shughuli zao na maboresho ya kozi ya programu na baada ya mradi kumalizika. Tunataka kujua ni jinsi gani shughuli za kilimo zinaendelea baada ya programu kufikia mwisho wake. Watangazaji wanatoa namba za simu ambazo wasikilizaji wanaweza kupiga kama wameshaunda vikundi na kusikiliza.
Baadhi ya wasikilizaji huandika barua pia. Tuna masanduku ya barua katikati ya kijiji. Mwanakijiji hukusanya barua mara moja au mbili kwa mwezi na mfanyakazi wetu wa idara ya masoko huzunguka kuzikusanya.
Niliguundua kwamba wakulima hawapati habari thabiti kutoka mashirika mbalimbali ya kiserikali na yasiyo ya kiserikali.
Mara nyingine wakulima hupuuzia ujumbe ambao si thabiti na hawafanyi lolote kuhusu mambo ya kilimo yaliyosisitizwa. Wakati mwingine mkulima hatekelezi wajibu anapopata ujumbe wa kutatanisha. Mkulima hajui amwamini nani, kwa hiyo hawawajibiki kabisa.
Kwa hiyo nilifanya tafiti katika ujumbe hizi ambazo si thabiti, hasa katika kilimo cha hifadhi. Nilikwenda katika eneo ambapo NASFAM -National Smallholder Farmers’Association of Malawi – kinatoa huduma za ughani. Nilikwenda pia mahali ambapo Shirika lisilo la kiserikali – NGO Concern Worldwide linatoa huduma za ughani. Nilitembelea eneo la tatu ambapo ughani unatolewa na Total Land Care, na sehemu ya nne amabapo wafanyakazi ughani wa serikali hutoa huduma.
Katika maeneo yote manne, niliona ni jinsi gani wakulima wanatumia kilimo hifadhi. Nilijikita zaidi katika kilimo cha kutumia mashimo, ambacho ni kuotesha mmea katika shimo na kuweka mabua juu ya udongo kuhifadhi unyevu. Nilitaka kuona kama kuna tofauti jinsi wakulima walikuwa wakilima kilimo cha hifadhi.
Nilitaka pia kujua ni watoaji huduma ughani wapi ambao wanaweza kunipa taarifa ambayo ni za hali ya juu na za kuaminika juu ya kilimo cha hifadhi iliniweze kutoa habari katika redio. Nilimwuliza mkulima mmoja kutoka kila eneo moja kati ya maeneo manne na kuwauliza kuhusu taarifa walizopata kutoka kwa wafanyakazi ughani.
Katika matukio mengine, niligundua kwamba wakulima wamelima kwa mashimo lakini wametandaza mabua pia. Kwa sababu wakulima waliambiwa pia kupanda mimea ya vetiver na kuweka alama za matuta, pia waliichukua. Walizifanyia kazi kila ujumbe walizosikia. Hawakutaka kuziachilia mbali shughuli walizotiwa nazo moyo kujaribu kwa hivyo waliamua kuzijaribu zote katika shamba moja.
Lakini shirika lingine lilipomfundisha kuhusu kupanda kwa mashimo aliachilia mbali kabisa utandazji wa mabua na kutizama kwenye upandaji wa mashimo.
Kuna wakulima wengine ambao wanapojifunza mazoea Fulani wanakwama kwa hayo kwamba hawataki kujifunza jambo jipya. Tabia yao ni hivi ndivyo nifanyavyo na hivi ndivyo nilivyofundishwa na ni njia bora. Wamekwisha mwamini mtu aliyewafundisha na hawawezi kumwamini mtu mwingine mbaye anakuja na taarifa nyingine kwa urahisi.
Kituo kina timu ya mpira ambayo imeundwa kwa ajili ya mahusiano ya kijamii. Tunapanga mechi na mechi za kijamii na zinatangazwa na wafanyabiashara wa kijamii wakiidhamini tukio. Hii insaidia wafanyakazi wa kituo kusafiri ndani ya wilaya na kukutana na wasikilizaji. Watu wanapopiga simu tunawauliza wanapiga simu kutoka wapi. Hii inatupa wazo ni umbali gani, kwa mapana gani mradi Tunaorekodi maoni kutoka katika programu ya kila shamba.
Tuna ujumbe wa simu za mbali za bure. Wakulima ambao ni wanachama wanaotumia mtandao wa airtel wanaweza kutuma ujumbe bure kwa mtandao huu. Wakulima ambao walikuwa wakifanya kwa njia hii iliyopendekezwa katika programu maalumu hueleza walichokifanya, walichojifunza na ni jinsi gani wamefaidika, vilevile matatizo ambayo wanayapata. Tunatumia maoni haya kujibu maswali ambayo watu huuliza wanapopiga simu au wanapotuma ujumbe. Kama maswali ni ya kiutaalamu zaidi, kama vile kuzuka kwa ugonjwa, tunamwona mtaalam wa kilimo. Mtaalamu pia ana imarisha baadhi ya jumbe tunazozipata kutoka kwa wakulima.
Shirika lisilo la kiserikali na idara ya kilimo wanapokuwa na shughuli vijijini, tunaalikwa kurekodi na kutoa tarifa juu ya shughuli. Hii pia ni fursa ya kusikia wakulima wanasema nini?
Licha ya hayo, Tunatembelea jamii kwa vikundi vinavyosikiliza redio karibu na Nkhotakota. Tunatumia safari hizi kusikia na kurekodi mawazo ya watu kuhusu programu yetu.
Tuna mahusiano mazuri na wafanyakazi ughani, ambao wako huru kutembelea kituo. Wakulima wanawambia pia wafanyakazi ughani kwamba wanataka mrusha matangazo kutembelea eneo lao, kurekodi uzoefu wao walioupata kwa njia hii. Idara ya kilimo inatoa pikipiki kutupeleka kwenye maeneo ambayo uhitajiwa huduma yetu.
Sehemuya pili Part II: Nakala ya maaendeleo ya programu kutoka katokana na utafiti
Kifuatacho ni dondoo za dakika nne kutokana na programu kuhusu kilimo cha kutumia mashimo kilichotangazwa kituo cha redio jamii cha Nkhotakota tarehe 1/8/2012 na kurudiwa tarehe 5/8/ 2012 Dondoo hizi zimetafsiriwa kutoka lugha ya Kichechewa Programu hii inahusu utafiti uliofanywa na Chinkhokwe, ambaye alimsaili mkulima kiongozi aliye jihusisha na upandaji kwa njia ya mashimo. Dondoo zilihusisha dhana ya mabadiliko ya hali ya hewana vilevile kuanzisha kilimo kwa njia ya mashimo kama njia ya kuyakinga mahindi wakati wa kiangazi. Wakulima wanaelezea jinsi ya kulima kilimo cha kutumia mashimona faida za kulima hivyo.
Mtangazaji akitangaza kwa sauti
Wakulima wenzangu mnafanya nini kukabiliana na mabadiliko ya tabia ya nchi? hali ya hewa? Mnafanya mambo gani kufuata uifadhi wa mali asili?
Tatizo moja linaloibuka kwa sababu ya mabadiliko ya hali ya tabia ya nchi ni ukame. Si hali ngeni kusikia matukio ya mvua kabla ya mazao kukomaana kuvunwa. Matokeo ya haya ni kuharibu mazao kama mahindi kwa sababu ya uhaba wa maji.
Leo tutajifunza jinsi ya kuweza kukinga mahindi yetu wakati wa kiangazi kwa kulima kilimo cha kupunguza ukame kama cha kulima kwa mashimo. Katika programu tuna msaili na bi Agnes Macheso kutoka kikundi kikuu cha Kijiji cha Nkhongo katika wilaya ya Nkhotakota.
Aina hii ya kilimo inayojikita kwenye matokeo ya utafiti uliofanywa inaonekana itawanufaisha Wamalawi, na kwamba mwaka ujao wakulima wengi watafuata kilimo cha mashimo. Kulingana na waliofanya utafiti juu ya kilimo cha kuotesha kwa mashimo mahindi huota vizuri kwa sababu ya maji na mvua inaelekezwa kwenye mashimo.
Acknowledgements
Imechangiwa na Vijay Cuddeford, Meneja Mhariri Redio ya wakulima ya kimatifa ikilenga kwenye mambo yaliyokusanywa na Tendai Banda na Philip Chinkhokwe.
Imepitiwa upya na: Doug Ward, Mwenyekiti na redio ya kimo ya kimataifa
Information sources
Msaili na Philip Chinkhokwe iliyofanywa na Tendai Banda, 17/9/2012.
Dondoo kutokana na programu zilizotangazwa katika Redio ya jamii ya Nkhotakota
Kwa maelezo zaidi juu ya kupanda mahindi katika mashimo: Soma Karen Sanje, 2011. Wakulima wa Malawi wachimba/walima ili kukabiliana na hali ya ukame. Alertnet, June 10, 2011. http://www.trust.org/alertnet/news/malawi-farmers-digging-in-to-combat-drier-conditions/
Mradi uliofanywa na kupewa msada wa kifedha na nchi ya Kanada uliotolwa kupitia wakala wa kimataifa wa mendeleo. (CIDA)