{"id":9337,"date":"2012-04-26T20:29:25","date_gmt":"2012-04-26T17:29:25","guid":{"rendered":"http:\/\/frrp.wpengine.com\/sw\/?post_type=radio-resource-packs&#038;p=9337"},"modified":"2018-08-31T22:23:39","modified_gmt":"2018-08-31T19:23:39","slug":"maranda-ya-mbao-yaongeza-maisha-ya-ghala-kwa-viazi-batata","status":"publish","type":"radio-script","link":"https:\/\/scripts.farmradio.fm\/sw\/mwongozo-wa-redio\/maranda-ya-mbao-yaongeza-maisha-ya-ghala-kwa-viazi-batata\/","title":{"rendered":"Maranda ya mbao yaongeza maisha ya ghala kwa viazi batata"},"content":{"rendered":"<p><em>Wimbo wa Kitambulisho: Uendelee kwa hadi nukta tano kisha ufifie chini ya sauti ya mtangazaji.<\/em><\/p>\n<p><strong>Mtangazaji: <\/strong>Viazi batata ni zao la chakula muhimu nchini Kenya.\u00a0 Huwa vinakuzwa katika nyanda za juu za mikoa ya Kati, Bonde la Ufa na Magharibi.\u00a0 Hata hivyo, usalishaji na uuzaji wa viazi hutatizwa na hali duni ya uhifadhi ambayo hupunguza mapato ya wakulima pamoja na kuwavunja moyo.<\/p>\n<p>Katika kipindi chetu cha leo, tunakutana na mkulima mmoja wa viazi batata ambaye amegundua njia ya ajabu ya kuhifadhi viazi batata vyake katika hali nzuri kwa muda mrefu baada ya kuvuna.<\/p>\n<p><strong>SFX: <\/strong><em>Sauti za makelele ya sokoni.\u00a0 Zififie chini ya sauti ya mtangazaji.<\/em><\/p>\n<p><strong>Mtangazaji:\u00a0 <\/strong>Tuko katika kituo cha biashara cha Kinungi kilichoko katika barabara yenye shughuli nyingi ya Nakuru-Naivasha.\u00a0 Ni asubuhi na mapema and soko la ina shughuli nyingi.\u00a0 Leo, wakulima wana viazi batata vichache vya kuuza sokoni.\u00a0 Mavuno ya mwisho yalikuwa miezi mitatu iliyopita.\u00a0 Zao mpya bado linaendelea kukua shambani. <\/p>\n<p>Lakini mambo ni tofauti kwa Bw. Githenya Kariuki.\u00a0 Yeye amefika hapa kuuza viazi vyake kwa mnunuzi kutoka Nairobi, yapata kilomita 70 kutoka hapa.\u00a0 Yeye anasema kuwa ni msimu wa viazi batata kwake, haya yote yakitokana na mbinu yake mpya ya kuhifadhi viazi batata.<\/p>\n<p><strong>Githenya: <\/strong>Unajua, mimi nategemea viazi kukidhi mahitaji ya familia yangu.\u00a0 Mimi hulisha na kusomesha watoto, na bado hubaki na pesa kiasi fulani kushughulikia nyakati ngumu.\u00a0 Nina watoto watatu katika shule za upili, na huo si mzaha.\u00a0 Karo inakuwa nyingi sana, hasa kwa mtu kama mimi anayetegemea kilimo tu.<\/p>\n<p><strong>SFX:<\/strong> Sauti ya watu wanaotembea huku wakizungumza.\u00a0 Paaza na kuchanganya ukififiisha chini ya sauti ya mtangazaji na ile ya mtu anayelima.\u00a0\u00a0\u00a0<\/p>\n<p><strong>Mtangazaji: <\/strong>Tunatembea mita mia tatu kutoka barabara kuu na kufika katika shamba la Githenya.\u00a0 Bi. Githenya analima kisehemu cha ardhi ambacho bwana yake anasema kitapandwa viazi.<\/p>\n<p><strong>SFX:<\/strong><em> Sauti ya mlango ukifunguka.\u00a0\u00a0 <\/em><\/p>\n<p><strong>Githenya: <\/strong>Hili ni ghala langu ambamo naweka mengi ya mazao yangu.<\/p>\n<p><strong>Mhojaji:<\/strong> Ghala lenyewe ni kubwa.\u00a0 Lazima ulitumia kiasi kikubwa cha mbao kulijenga.\u00a0 Naona kitu kama rundo la nyasi kule pembeni.\u00a0 Je, kile ni chakula cha ng\u2019ombe wako?<\/p>\n<p><strong>Githenya: <\/strong>Hatimaye mimi huitumia kama chakula cha ng\u2019ombe.\u00a0 Lakini nyasi ile huzuia maranda ya mbao yasipeperushwe na upepo mkali wa asubuhi.\u00a0 Hilo likifanyika, viazi vyangu vitapata mwangaza na haitachukua muda mrefu kabla havijazaanza kubadilika rangi.\u00a0 Vinapoanza kubadilika rangi, basi vinakuwa havifai kama chakula cha binadamu.<\/p>\n<p><strong>Mhojaji: <\/strong>Je, umekuwa na tatizo hapo mbeleni?<\/p>\n<p><strong>Githenya:<\/strong> Nimekuwa nikitamani kuhifadhi viazi batata kwa muda mrefu zaidi.\u00a0 Kwa kawaida, niliviweka katika pembe moja ya ghala langu.\u00a0 Lakini baada ya muda, yalikuwa yakigeuka kijani kibichi na hivyo kuwa havifai kuuzwa.\u00a0 Kwa hivyo, nililazimika kuviuza vyote mara tu baada ya kuuza.\u00a0 Kwa vile soko huwa na viazi batata kwa wingi baada ya mavuno, bei yake\u00a0 huwa chini.\u00a0 Viazi vinapoharibika, naweza kuvitumia kama mbegu, lakini haiwezekani nikatumia vyote vilivyoharibika.<\/p>\n<p><strong>Mhojaji: <\/strong>Uligunduaje maranda ya mbao?<\/p>\n<p><strong>Githenya:\u00a0 <\/strong>Huwa natumia maranda ya mbao kama matandiko kwa kuku wangu.\u00a0 Siku moja, nilienda kwenye taka ambapo seremala hutupa machunjo ya mbao.\u00a0 Nilipokuwa naokota maranda, niliona viazi vilivyokuwa vimetupwa.\u00a0 Vilionekana kuwa katika hali nzuri.\u00a0 Jambo hili lilinipatia wazo la kutumia maranda ya mbao badala ya nyasi kufunikia viazi batata vyangu.\u00a0 Nilitumia safu mbadala za pumba na viazi, nikianza na kumalizia na safu ya maranda.<\/p>\n<p><strong>Mhojaji: <\/strong>Kiazi batata ni kama kitu kingine cho chote chenye uhai.\u00a0 Huishi na kupumua.\u00a0 Ukikiweka katika sehemu yenye joto, kitakua.\u00a0 Ukikifunga katika mfuko wa mpira, kitanyongwa.\u00a0 Kikiugua, kitaharibika.\u00a0 Na turejee kwa mahojiano na Bw. Githenya.<\/p>\n<p><strong>Mhojaji:<\/strong> Ulijifunza nini katika majaribio haya?<\/p>\n<p><strong>Githenya: <\/strong>Jambo moja nililojifunza ni kuwa maranda hayo ya mbao lazima yawe yamelowa kwa kiasi fulani.\u00a0 Ikiwa yamekauaka sana, basi ubora wa viazi vile utapungua kwa kasi kwa kuwa vitakauka na kuvamiwa na wadudu.\u00a0 Kwa upande mwingine, ikiwa yamelowa zaidi, basi viazi vitaoza baada ya muda mfupi.<\/p>\n<p><strong>SFX:<\/strong><em> Sauti ya nyasi ikigeuzwa na kuwekwa kando.<\/em><\/p>\n<p><strong>Mhojaji: <\/strong>Ni kilo ngapi za viazi batata vilivyoko katika rundo hili?<\/p>\n<p><strong>Githenya: <\/strong>Rundo hili lina kilo 400.\u00a0 Hili lingine lina kilo 300.\u00a0 Nilizipanga hivi kwamba nimetumia nafasi iliyoko kikamilifu.\u00a0 Kumbuka kuwa hili ni ghala ambamo mimi huweka vitu vingine pia.<\/p>\n<p><strong>Mhojaji: <\/strong>\u00a0Ni changamoto gani ulizokumbana nazo katika kujaribu mbinu hii?<\/p>\n<p><strong>Githenya:<\/strong> (<em>Akicheka<\/em>) Mara kwa mara watu hawaamini kitu mpaka waone kikifanikiwa.\u00a0 Nilipomwambia mke wangu kuwa nilitaka kujaribu njia mbadala ya uhifadhi, aliteta kuwa hii ingechukua nafasi kubwa sana katika ghala.\u00a0 Nilimwambia tungejaribu mara moja tu na kama haikufanikiwa, basi tungeiacha.\u00a0 Kwa hivyo, akakubali.<\/p>\n<p>Lakini nilikuwa na tatizo lingine.\u00a0 Mwanzoni, seremala walinipa maranda ya mbao bure.\u00a0 Lakini baada ya muda mfupi, wakanitaka kuilipia.\u00a0 Sikuwa na pesa kama hizo.\u00a0 Kwa hivyo, tukaafikiana kwamba wangenipa maranda nami niwape viazi vya thamani kama sawia.<\/p>\n<p><strong>Mhojaji: <\/strong>Githenya hakuachia hapo.\u00a0 Aliwaeleza wakulima katika kundi lake mafanikio ya mbinu hii mpya.<\/p>\n<p><strong>Githenya:<\/strong> Wakulima walipojaribu mbinu hii, walisema kuwa viazi batata vyao vilikaa vizima kwa muda mrefu zaidi kuliko kutumia mbinu nyinginezo.\u00a0 Hii ndiyo sababu kwa muda wa miaka mitatu iliyopita, wanachama wa kundi langu la kilimo wamekuwa wakitumia mbinu ya maranda ya mbao.\u00a0 Matumizi ya maranda ya mbao ni yenye ufanisi hivi kwamba sasa tunaweza kuhifadhi viazi batata vyetu kwa hadi miezi minne baada ya mavuno.<\/p>\n<p><strong>Mhojaji: <\/strong>Bw. Samuel Njiru ni Afisa Kilimo wa Wilaya katika wilaya ya Kinangop.\u00a0 Anasema kuwa njia duni za uvunaji zinaweza kusababisha hasara kubwa katika uhifadhi wa viazi batata.<\/p>\n<p><strong>Bw. Njiru: <\/strong>Uhifadhi bora huanza kwa uvunaji wenye uangalifu.\u00a0 Majira ya mavuno <em>ni suala nyeti<\/em>.\u00a0 Lazima wakulima wawe waangalifu sana ili wasivune mapema sana au wachelewe.\u00a0 Baadhi ya maambukizi yanayovamia viazi batata kwenye ghala huanza wakati wa kuvuna.\u00a0 Ili kuepukana na haya, inatakikana kuvuna viazi batata kama viazi vyenyewe vimekomaa kikamilifu.\u00a0 Hii hupunguza kuchunua ngozi yake ambako kunaweza kupelekea maambukizi.\u00a0 Kwa upande mwingine, iwapo viazi hivi vitachelewa kuvunwa, kuna uwezekano mkubwa kuwa vitakuwa <em>tayari <\/em>vimeambukizwa.<\/p>\n<p><strong>Mhojaji: <\/strong>Unazuiaje kuchunuliwa kwa viazi?<\/p>\n<p><strong>Bw. Njiru: <\/strong>Ili kuepuka uharibifu, ni vizuri kukata sehemu ya juu ya ardhi ya mimea hii siku 10 kabla ya kuvuna viazi batata.\u00a0 Jambo hili hupatia viazi muda wa kuunda ngozi iiyokomaa na ngumu.\u00a0 Lazima wakulima wahakikishe pia kuwa hawavuni wakati wa mvua.\u00a0 Ikiwa huwezi kuepuka kuvanya hivyo, lazima uviache viazi kukauka katika matuta kwa muda wa takriban siku 10 katika sehemu baridi.<\/p>\n<p><strong>Mtangazaji: <\/strong>Asante Bw. Njiru.\u00a0 Hebu tuwaeleze kwa kifupi wasikilizaji wetu mambo muhimu tuliyozungumzia.\u00a0 Kwanza, vuna viazi wakati ngozi yake imekuwa ngumu lakini usichelewe.\u00a0 Pili, chagua viazi ambavyo havina alama ya kudhulika.\u00a0 Tatu, tumia safu mbadala za maranda ya mbao katika uhifadhi.\u00a0 Na mwisho, chagua na uondoe viazi vyo vyote vilivyoharibika.<\/p>\n<p><strong>SFX:<\/strong><em> Sauti ya pikipiki ya magurudumu matatu inayoongezeka na kisha kulainika chini ya mtangazaji.<\/em><\/p>\n<p><strong>Mtangazaji: <\/strong>Naondoka huku nikiwaacha Kinungi na Githeya wakipakia mzigo wao wa mwisho wa viazi batata.\u00a0 Anaweza kufunga safari nyingine kuelekea sokoni kwa sababu ya mbinu yake mpya ya kutumia maranda ya mbao kuhifadhi viazi batata vyake. <\/p>\n<p><strong>SFX:<\/strong><em> Sauti ya pikipiki ya magurudumu matatu inayoongezeka na kisha kulainika chini ya mtangazaji.<\/em><\/p>\n<p><strong>Mtangazaji: <\/strong>Endapo una swali lo lote kuhusu mada ya leo ama hata wasiwasi kuhusu jambo lo lote katika shamba lako, tuma ujumbe mfupi kupitia nambari 0715 916 136. <em>The<\/em> <em>Organic Farmer<\/em> atakupigia simu au akutumie barua.\u00a0 Hadi wiki ijayo saa kama hizi, jina langu ni &#8230;&#8230;&#8230;.. nikikutakia usiku wenye baraka.<\/p>\n<p><em>Muziki wa kumalizia, hadi nukta nne kisha ufifie na kutoweka.<\/em><\/p>\n","protected":false},"excerpt":{"rendered":"<p>Wimbo wa Kitambulisho: Uendelee kwa hadi nukta tano kisha ufifie chini ya sauti ya mtangazaji. Mtangazaji: Viazi batata ni zao la chakula muhimu nchini Kenya.\u00a0 Huwa vinakuzwa katika nyanda za juu za mikoa ya Kati, Bonde la Ufa na Magharibi.\u00a0 Hata hivyo, usalishaji na uuzaji wa viazi hutatizwa na hali duni ya uhifadhi ambayo hupunguza&hellip;<\/p>\n","protected":false},"author":18,"featured_media":0,"parent":0,"menu_order":1,"template":"","meta":{"footnotes":"","beyondwords_generate_audio":"","beyondwords_integration_method":"","beyondwords_project_id":"","beyondwords_content_id":"","beyondwords_preview_token":"","beyondwords_player_content":"","beyondwords_player_style":"","beyondwords_language_code":"","beyondwords_language_id":"","beyondwords_title_voice_id":"","beyondwords_body_voice_id":"","beyondwords_summary_voice_id":"","beyondwords_error_message":"","beyondwords_disabled":"","beyondwords_delete_content":"","beyondwords_podcast_id":"","beyondwords_hash":"","publish_post_to_speechkit":"","speechkit_hash":"","speechkit_generate_audio":"","speechkit_project_id":"","speechkit_podcast_id":"","speechkit_error_message":"","speechkit_disabled":"","speechkit_access_key":"","speechkit_error":"","speechkit_info":"","speechkit_response":"","speechkit_retries":"","speechkit_status":"","speechkit_updated_at":"","_speechkit_link":"","_speechkit_text":""},"script-format":[517],"package":[640],"script-category":[843],"class_list":["post-9337","radio-script","type-radio-script","status-publish","hentry","script-format-mahojiano","package-640","script-category-shughuli-za-baada-ya-mavuno"],"acf":[],"yoast_head":"<!-- This site is optimized with the Yoast SEO plugin v27.3 - https:\/\/yoast.com\/product\/yoast-seo-wordpress\/ -->\n<title>Maranda ya mbao yaongeza maisha ya ghala kwa viazi batata - Farm Radio International<\/title>\n<meta name=\"robots\" content=\"index, follow, max-snippet:-1, max-image-preview:large, max-video-preview:-1\" \/>\n<link rel=\"canonical\" href=\"https:\/\/scripts.farmradio.fm\/sw\/mwongozo-wa-redio\/maranda-ya-mbao-yaongeza-maisha-ya-ghala-kwa-viazi-batata\/\" \/>\n<meta property=\"og:locale\" content=\"en_US\" \/>\n<meta property=\"og:type\" content=\"article\" \/>\n<meta property=\"og:title\" content=\"Maranda ya mbao yaongeza maisha ya ghala kwa viazi batata - Farm Radio International\" \/>\n<meta property=\"og:description\" content=\"Wimbo wa Kitambulisho: Uendelee kwa hadi nukta tano kisha ufifie chini ya sauti ya mtangazaji. Mtangazaji: Viazi batata ni zao la chakula muhimu nchini Kenya.\u00a0 Huwa vinakuzwa katika nyanda za juu za mikoa ya Kati, Bonde la Ufa na Magharibi.\u00a0 Hata hivyo, usalishaji na uuzaji wa viazi hutatizwa na hali duni ya uhifadhi ambayo hupunguza&hellip;\" \/>\n<meta property=\"og:url\" content=\"https:\/\/scripts.farmradio.fm\/sw\/mwongozo-wa-redio\/maranda-ya-mbao-yaongeza-maisha-ya-ghala-kwa-viazi-batata\/\" \/>\n<meta property=\"og:site_name\" content=\"Farm Radio International\" \/>\n<meta property=\"article:publisher\" content=\"https:\/\/www.facebook.com\/farmradio\/\" \/>\n<meta property=\"article:modified_time\" content=\"2018-08-31T19:23:39+00:00\" \/>\n<meta name=\"twitter:card\" content=\"summary_large_image\" \/>\n<meta name=\"twitter:site\" content=\"@farmradio\" \/>\n<meta name=\"twitter:label1\" content=\"Est. reading time\" \/>\n\t<meta name=\"twitter:data1\" content=\"6 minutes\" \/>\n<script type=\"application\/ld+json\" class=\"yoast-schema-graph\">{\"@context\":\"https:\\\/\\\/schema.org\",\"@graph\":[{\"@type\":\"Article\",\"@id\":\"https:\\\/\\\/scripts.farmradio.fm\\\/sw\\\/mwongozo-wa-redio\\\/maranda-ya-mbao-yaongeza-maisha-ya-ghala-kwa-viazi-batata\\\/#article\",\"isPartOf\":{\"@id\":\"https:\\\/\\\/scripts.farmradio.fm\\\/sw\\\/mwongozo-wa-redio\\\/maranda-ya-mbao-yaongeza-maisha-ya-ghala-kwa-viazi-batata\\\/\"},\"author\":{\"name\":\"john.cheburet\",\"@id\":\"http:\\\/\\\/scripts.farmradio.fm\\\/sw\\\/#\\\/schema\\\/person\\\/a8c983ec34913ec8d9039f021000e492\"},\"headline\":\"Maranda ya mbao yaongeza maisha ya ghala kwa viazi batata\",\"datePublished\":\"2012-04-26T17:29:25+00:00\",\"dateModified\":\"2018-08-31T19:23:39+00:00\",\"mainEntityOfPage\":{\"@id\":\"https:\\\/\\\/scripts.farmradio.fm\\\/sw\\\/mwongozo-wa-redio\\\/maranda-ya-mbao-yaongeza-maisha-ya-ghala-kwa-viazi-batata\\\/\"},\"wordCount\":1177,\"publisher\":{\"@id\":\"http:\\\/\\\/scripts.farmradio.fm\\\/sw\\\/#organization\"},\"inLanguage\":\"sw-CG\"},{\"@type\":\"WebPage\",\"@id\":\"https:\\\/\\\/scripts.farmradio.fm\\\/sw\\\/mwongozo-wa-redio\\\/maranda-ya-mbao-yaongeza-maisha-ya-ghala-kwa-viazi-batata\\\/\",\"url\":\"https:\\\/\\\/scripts.farmradio.fm\\\/sw\\\/mwongozo-wa-redio\\\/maranda-ya-mbao-yaongeza-maisha-ya-ghala-kwa-viazi-batata\\\/\",\"name\":\"Maranda ya mbao yaongeza maisha ya ghala kwa viazi batata - Farm Radio International\",\"isPartOf\":{\"@id\":\"http:\\\/\\\/scripts.farmradio.fm\\\/sw\\\/#website\"},\"datePublished\":\"2012-04-26T17:29:25+00:00\",\"dateModified\":\"2018-08-31T19:23:39+00:00\",\"breadcrumb\":{\"@id\":\"https:\\\/\\\/scripts.farmradio.fm\\\/sw\\\/mwongozo-wa-redio\\\/maranda-ya-mbao-yaongeza-maisha-ya-ghala-kwa-viazi-batata\\\/#breadcrumb\"},\"inLanguage\":\"sw-CG\",\"potentialAction\":[{\"@type\":\"ReadAction\",\"target\":[\"https:\\\/\\\/scripts.farmradio.fm\\\/sw\\\/mwongozo-wa-redio\\\/maranda-ya-mbao-yaongeza-maisha-ya-ghala-kwa-viazi-batata\\\/\"]}]},{\"@type\":\"BreadcrumbList\",\"@id\":\"https:\\\/\\\/scripts.farmradio.fm\\\/sw\\\/mwongozo-wa-redio\\\/maranda-ya-mbao-yaongeza-maisha-ya-ghala-kwa-viazi-batata\\\/#breadcrumb\",\"itemListElement\":[{\"@type\":\"ListItem\",\"position\":1,\"name\":\"Nyumbani\",\"item\":\"http:\\\/\\\/scripts.farmradio.fm\\\/sw\\\/\"},{\"@type\":\"ListItem\",\"position\":2,\"name\":\"Mahojiano\",\"item\":\"https:\\\/\\\/scripts.farmradio.fm\\\/sw\\\/mwongozo-wa-muundo\\\/mahojiano\\\/\"},{\"@type\":\"ListItem\",\"position\":3,\"name\":\"Maranda ya mbao yaongeza maisha ya ghala kwa viazi batata\"}]},{\"@type\":\"WebSite\",\"@id\":\"http:\\\/\\\/scripts.farmradio.fm\\\/sw\\\/#website\",\"url\":\"http:\\\/\\\/scripts.farmradio.fm\\\/sw\\\/\",\"name\":\"Farm Radio International\",\"description\":\"Sharing knowledge, giving voice.\",\"publisher\":{\"@id\":\"http:\\\/\\\/scripts.farmradio.fm\\\/sw\\\/#organization\"},\"potentialAction\":[{\"@type\":\"SearchAction\",\"target\":{\"@type\":\"EntryPoint\",\"urlTemplate\":\"http:\\\/\\\/scripts.farmradio.fm\\\/sw\\\/?s={search_term_string}\"},\"query-input\":{\"@type\":\"PropertyValueSpecification\",\"valueRequired\":true,\"valueName\":\"search_term_string\"}}],\"inLanguage\":\"sw-CG\"},{\"@type\":\"Organization\",\"@id\":\"http:\\\/\\\/scripts.farmradio.fm\\\/sw\\\/#organization\",\"name\":\"Farm Radio International\",\"url\":\"http:\\\/\\\/scripts.farmradio.fm\\\/sw\\\/\",\"logo\":{\"@type\":\"ImageObject\",\"inLanguage\":\"sw-CG\",\"@id\":\"http:\\\/\\\/scripts.farmradio.fm\\\/sw\\\/#\\\/schema\\\/logo\\\/image\\\/\",\"url\":\"https:\\\/\\\/scripts.farmradio.fm\\\/wp-content\\\/uploads\\\/farmRadioLogo.jpg\",\"contentUrl\":\"https:\\\/\\\/scripts.farmradio.fm\\\/wp-content\\\/uploads\\\/farmRadioLogo.jpg\",\"width\":200,\"height\":75,\"caption\":\"Farm Radio International\"},\"image\":{\"@id\":\"http:\\\/\\\/scripts.farmradio.fm\\\/sw\\\/#\\\/schema\\\/logo\\\/image\\\/\"},\"sameAs\":[\"https:\\\/\\\/www.facebook.com\\\/farmradio\\\/\",\"https:\\\/\\\/x.com\\\/farmradio\",\"https:\\\/\\\/www.instagram.com\\\/farmradio\\\/\",\"https:\\\/\\\/www.youtube.com\\\/user\\\/FarmRadioInt\"]},{\"@type\":\"Person\",\"@id\":\"http:\\\/\\\/scripts.farmradio.fm\\\/sw\\\/#\\\/schema\\\/person\\\/a8c983ec34913ec8d9039f021000e492\",\"name\":\"john.cheburet\",\"image\":{\"@type\":\"ImageObject\",\"inLanguage\":\"sw-CG\",\"@id\":\"https:\\\/\\\/secure.gravatar.com\\\/avatar\\\/78e885921cc16471b50889fa0bf634d5774e1c82ef80059705664dc6cfc4add9?s=96&d=mm&r=g\",\"url\":\"https:\\\/\\\/secure.gravatar.com\\\/avatar\\\/78e885921cc16471b50889fa0bf634d5774e1c82ef80059705664dc6cfc4add9?s=96&d=mm&r=g\",\"contentUrl\":\"https:\\\/\\\/secure.gravatar.com\\\/avatar\\\/78e885921cc16471b50889fa0bf634d5774e1c82ef80059705664dc6cfc4add9?s=96&d=mm&r=g\",\"caption\":\"john.cheburet\"}}]}<\/script>\n<!-- \/ Yoast SEO plugin. -->","yoast_head_json":{"title":"Maranda ya mbao yaongeza maisha ya ghala kwa viazi batata - Farm Radio International","robots":{"index":"index","follow":"follow","max-snippet":"max-snippet:-1","max-image-preview":"max-image-preview:large","max-video-preview":"max-video-preview:-1"},"canonical":"https:\/\/scripts.farmradio.fm\/sw\/mwongozo-wa-redio\/maranda-ya-mbao-yaongeza-maisha-ya-ghala-kwa-viazi-batata\/","og_locale":"en_US","og_type":"article","og_title":"Maranda ya mbao yaongeza maisha ya ghala kwa viazi batata - Farm Radio International","og_description":"Wimbo wa Kitambulisho: Uendelee kwa hadi nukta tano kisha ufifie chini ya sauti ya mtangazaji. Mtangazaji: Viazi batata ni zao la chakula muhimu nchini Kenya.\u00a0 Huwa vinakuzwa katika nyanda za juu za mikoa ya Kati, Bonde la Ufa na Magharibi.\u00a0 Hata hivyo, usalishaji na uuzaji wa viazi hutatizwa na hali duni ya uhifadhi ambayo hupunguza&hellip;","og_url":"https:\/\/scripts.farmradio.fm\/sw\/mwongozo-wa-redio\/maranda-ya-mbao-yaongeza-maisha-ya-ghala-kwa-viazi-batata\/","og_site_name":"Farm Radio International","article_publisher":"https:\/\/www.facebook.com\/farmradio\/","article_modified_time":"2018-08-31T19:23:39+00:00","twitter_card":"summary_large_image","twitter_site":"@farmradio","twitter_misc":{"Est. reading time":"6 minutes"},"schema":{"@context":"https:\/\/schema.org","@graph":[{"@type":"Article","@id":"https:\/\/scripts.farmradio.fm\/sw\/mwongozo-wa-redio\/maranda-ya-mbao-yaongeza-maisha-ya-ghala-kwa-viazi-batata\/#article","isPartOf":{"@id":"https:\/\/scripts.farmradio.fm\/sw\/mwongozo-wa-redio\/maranda-ya-mbao-yaongeza-maisha-ya-ghala-kwa-viazi-batata\/"},"author":{"name":"john.cheburet","@id":"http:\/\/scripts.farmradio.fm\/sw\/#\/schema\/person\/a8c983ec34913ec8d9039f021000e492"},"headline":"Maranda ya mbao yaongeza maisha ya ghala kwa viazi batata","datePublished":"2012-04-26T17:29:25+00:00","dateModified":"2018-08-31T19:23:39+00:00","mainEntityOfPage":{"@id":"https:\/\/scripts.farmradio.fm\/sw\/mwongozo-wa-redio\/maranda-ya-mbao-yaongeza-maisha-ya-ghala-kwa-viazi-batata\/"},"wordCount":1177,"publisher":{"@id":"http:\/\/scripts.farmradio.fm\/sw\/#organization"},"inLanguage":"sw-CG"},{"@type":"WebPage","@id":"https:\/\/scripts.farmradio.fm\/sw\/mwongozo-wa-redio\/maranda-ya-mbao-yaongeza-maisha-ya-ghala-kwa-viazi-batata\/","url":"https:\/\/scripts.farmradio.fm\/sw\/mwongozo-wa-redio\/maranda-ya-mbao-yaongeza-maisha-ya-ghala-kwa-viazi-batata\/","name":"Maranda ya mbao yaongeza maisha ya ghala kwa viazi batata - Farm Radio International","isPartOf":{"@id":"http:\/\/scripts.farmradio.fm\/sw\/#website"},"datePublished":"2012-04-26T17:29:25+00:00","dateModified":"2018-08-31T19:23:39+00:00","breadcrumb":{"@id":"https:\/\/scripts.farmradio.fm\/sw\/mwongozo-wa-redio\/maranda-ya-mbao-yaongeza-maisha-ya-ghala-kwa-viazi-batata\/#breadcrumb"},"inLanguage":"sw-CG","potentialAction":[{"@type":"ReadAction","target":["https:\/\/scripts.farmradio.fm\/sw\/mwongozo-wa-redio\/maranda-ya-mbao-yaongeza-maisha-ya-ghala-kwa-viazi-batata\/"]}]},{"@type":"BreadcrumbList","@id":"https:\/\/scripts.farmradio.fm\/sw\/mwongozo-wa-redio\/maranda-ya-mbao-yaongeza-maisha-ya-ghala-kwa-viazi-batata\/#breadcrumb","itemListElement":[{"@type":"ListItem","position":1,"name":"Nyumbani","item":"http:\/\/scripts.farmradio.fm\/sw\/"},{"@type":"ListItem","position":2,"name":"Mahojiano","item":"https:\/\/scripts.farmradio.fm\/sw\/mwongozo-wa-muundo\/mahojiano\/"},{"@type":"ListItem","position":3,"name":"Maranda ya mbao yaongeza maisha ya ghala kwa viazi batata"}]},{"@type":"WebSite","@id":"http:\/\/scripts.farmradio.fm\/sw\/#website","url":"http:\/\/scripts.farmradio.fm\/sw\/","name":"Farm Radio International","description":"Sharing knowledge, giving voice.","publisher":{"@id":"http:\/\/scripts.farmradio.fm\/sw\/#organization"},"potentialAction":[{"@type":"SearchAction","target":{"@type":"EntryPoint","urlTemplate":"http:\/\/scripts.farmradio.fm\/sw\/?s={search_term_string}"},"query-input":{"@type":"PropertyValueSpecification","valueRequired":true,"valueName":"search_term_string"}}],"inLanguage":"sw-CG"},{"@type":"Organization","@id":"http:\/\/scripts.farmradio.fm\/sw\/#organization","name":"Farm Radio International","url":"http:\/\/scripts.farmradio.fm\/sw\/","logo":{"@type":"ImageObject","inLanguage":"sw-CG","@id":"http:\/\/scripts.farmradio.fm\/sw\/#\/schema\/logo\/image\/","url":"https:\/\/scripts.farmradio.fm\/wp-content\/uploads\/farmRadioLogo.jpg","contentUrl":"https:\/\/scripts.farmradio.fm\/wp-content\/uploads\/farmRadioLogo.jpg","width":200,"height":75,"caption":"Farm Radio International"},"image":{"@id":"http:\/\/scripts.farmradio.fm\/sw\/#\/schema\/logo\/image\/"},"sameAs":["https:\/\/www.facebook.com\/farmradio\/","https:\/\/x.com\/farmradio","https:\/\/www.instagram.com\/farmradio\/","https:\/\/www.youtube.com\/user\/FarmRadioInt"]},{"@type":"Person","@id":"http:\/\/scripts.farmradio.fm\/sw\/#\/schema\/person\/a8c983ec34913ec8d9039f021000e492","name":"john.cheburet","image":{"@type":"ImageObject","inLanguage":"sw-CG","@id":"https:\/\/secure.gravatar.com\/avatar\/78e885921cc16471b50889fa0bf634d5774e1c82ef80059705664dc6cfc4add9?s=96&d=mm&r=g","url":"https:\/\/secure.gravatar.com\/avatar\/78e885921cc16471b50889fa0bf634d5774e1c82ef80059705664dc6cfc4add9?s=96&d=mm&r=g","contentUrl":"https:\/\/secure.gravatar.com\/avatar\/78e885921cc16471b50889fa0bf634d5774e1c82ef80059705664dc6cfc4add9?s=96&d=mm&r=g","caption":"john.cheburet"}}]}},"_links":{"self":[{"href":"https:\/\/scripts.farmradio.fm\/sw\/wp-json\/wp\/v2\/radio-script\/9337","targetHints":{"allow":["GET"]}}],"collection":[{"href":"https:\/\/scripts.farmradio.fm\/sw\/wp-json\/wp\/v2\/radio-script"}],"about":[{"href":"https:\/\/scripts.farmradio.fm\/sw\/wp-json\/wp\/v2\/types\/radio-script"}],"author":[{"embeddable":true,"href":"https:\/\/scripts.farmradio.fm\/sw\/wp-json\/wp\/v2\/users\/18"}],"version-history":[{"count":0,"href":"https:\/\/scripts.farmradio.fm\/sw\/wp-json\/wp\/v2\/radio-script\/9337\/revisions"}],"wp:attachment":[{"href":"https:\/\/scripts.farmradio.fm\/sw\/wp-json\/wp\/v2\/media?parent=9337"}],"wp:term":[{"taxonomy":"script-format","embeddable":true,"href":"https:\/\/scripts.farmradio.fm\/sw\/wp-json\/wp\/v2\/script-format?post=9337"},{"taxonomy":"package","embeddable":true,"href":"https:\/\/scripts.farmradio.fm\/sw\/wp-json\/wp\/v2\/package?post=9337"},{"taxonomy":"script-category","embeddable":true,"href":"https:\/\/scripts.farmradio.fm\/sw\/wp-json\/wp\/v2\/script-category?post=9337"}],"curies":[{"name":"wp","href":"https:\/\/api.w.org\/{rel}","templated":true}]}}