{"id":4250,"date":"2012-04-26T20:10:30","date_gmt":"2012-04-26T17:10:30","guid":{"rendered":"http:\/\/frrp.wpengine.com\/?post_type=radio-resource-packs&#038;p=4250"},"modified":"2018-11-20T16:48:04","modified_gmt":"2018-11-20T13:48:04","slug":"zuia-malaria-wakati-wa-ujauzito","status":"publish","type":"radio-script","link":"https:\/\/scripts.farmradio.fm\/sw\/mwongozo-wa-redio\/zuia-malaria-wakati-wa-ujauzito\/","title":{"rendered":"Zuia malaria wakati wa ujauzito!"},"content":{"rendered":"<p>Fifiisha sauti za nyumbani &#8230; sufuria, maji yakimiminika, na kukifagiliwa<\/p>\n<p><strong>Bi. Chawila:<\/strong> Nancy, unaweza kuja kunisaidia kumaliza kusafisha madirisha tafadhali? Karibu nimalize. Lililobakia ni moja tu hili ya jikoni.<\/p>\n<p><strong>Nancy:<\/strong> Shangazi, naomba nimalize kusafisha vyombo vya jikoni \u2013 naja sasa hivi.<\/p>\n<p><strong>Bi. Chawila:<\/strong> EEEEEEhhhhyeeeee! Na Na Nanc \u2026!<\/p>\n<p><strong>Nancy:<\/strong> (Akipiga mayowe kwa hofu) Shangazi! Shangazi! Shangazi, kuna nini? Shangazi \u2026 Shangazi \u2026 Ongea! Saidieni! Saidieni jamani, \u2026 Shangazi yangu ameanguka kutoka juu ya stuli na kuzirai!<\/p>\n<p><strong>Bi. Bwalya:<\/strong> (Sauti za miguu ya watu wakikimbia kwenye mic) (Kwa hofu) Mungu wangu! Bi Chawila \u2026 Bi. Chawila, jirani, amka, jamani! Unanisikia Bi. Chawila? Tafadhali niambie! (Kimya kidogo, halafu sauti za watu wakiongea na kunong\u2019onezana chini kwa chini kuhusu kilichosababisha Bi Chawila kudondoka kutoka juu ya stuli. Sauti zinaendelea chini ya <em><strong>Bi. Bwalya:\u00a0<\/strong>\u00a0<\/em>Hakikisheni anapata hewa nyingi ili apate\u00a0<span style=\"text-decoration: underline\">fahamu haraka<em>.\u00a0\u00a0<\/em><\/span><\/p>\n<p><span style=\"text-decoration: underline\"><strong>Nancy:<\/strong>\u00a0<\/span>tafadhali fanya haraka ulete teksi\u00a0 tumpeleke kliniki mara moja.\u00a0 Inachukua muda kuleta teksi katika sehemu hii ya mtaa huu wa vibanda<\/p>\n<p><em>Sauti za miguu ya Nancy zinafifia kwenye mic.\u00a0 Kimya kwa sekunde mbili.\u00a0 Sauti ya gari ikikaribia na kisha kusimama.\u00a0\u00a0\u00a0<\/em><\/p>\n<p><strong>Bi. Bwalya:\u00a0<\/strong>(<em>Kwa sauti ya chini<\/em>) Haya Nancy, na tumwinue shangazi yako tumuweke ndani ya teksi.\u00a0 Lazima tumpeleke kwenye kliniki sasa hivi!\u00a0 Hali yake inaonekana kuwa baya sana.<\/p>\n<p><em>Sauti za Nancy na Bi. Bwalya wakijaribu kumuweka \u00a0Bi. Chawila ndani ya teksi, kisha mlango wa gari ukifungwa.\u00a0 Kimya, kisha sauti ya gari likiondoka, fifiisha kisha uihimili.\u00a0 Sauti ya gari likisimama katika chumba cha dharura, na mlango kufunguliwa.\u00a0 Sauti za wauguzi na daktari wakija kwa haraka ili kumchukua Bi. Chawila kwa machela.\u00a0 \u00a0\u00a0<\/em><\/p>\n<p><strong>Daktari Kamanga:<\/strong>\u00a0Alifanya nini?<\/p>\n<p><strong>Nancy:\u00a0<\/strong>(<em>Akieleza kwa hofu na woga<\/em>) Mimi sijui, daktari.\u00a0 Alikuwa akisafisha dirisha nje ya nyumba, halafu nikasikia akipiga mayowe na kuanguka chini kutoka kwenye stuli.\u00a0 Nilipofika pale nje, niliona kuwa amezirai na hangeweza kuzungumza name.<\/p>\n<p><strong>Daktari Kamanga:<\/strong>\u00a0Wewe unaitwaje na una uhusiano gani na mama huyu?\u00a0 Anaitwa nani?<\/p>\n<p><strong>Nancy:<\/strong>\u00a0Jina langu ni Nancy na mimi ni mpwa wake.\u00a0 Jina lake ni Bi. Mirriam Chawila.<\/p>\n<p><strong>Daktari Kamanga:<\/strong>\u00a0Mimba yake ni ya miezi mingapi?\u00a0 Amekuwa mgonjwa?\u00a0 Una habari kama amekuwa akiumwa na kichwa, homa au kizunguzungu?<\/p>\n<p><strong>Nancy:<\/strong>\u00a0Sina uhakika, lakini nafikiri mimba ni ya kama miezi saba hivi.\u00a0 Kwa ujumla, amekuwa na hali baya katika ujauzito huu.\u00a0 Ama kwa kweli, tunafikiri kuna mtu aliyemtupia jicho baya kwa vile amekuwa akipatwa na maumivu makali ya kichwa ya ghafla na pia kizunguzungu.<\/p>\n<p><strong>Daktari Kamanga:<\/strong>\u00a0Sawa, asante Nancy.\u00a0 Naomba mtoke\u00a0 msubiri hapo nje.\u00a0 Tutaona tutakavyosaidia.<\/p>\n<p><em>Fifiisha sauit, kisha upaandishe sauti za chumba cha matibabu ya dharura, sauti za vyombo vya matibabu vikiwekelewa mezani, watu wakiongea kwa sauti za chini na kadhalika.\u00a0 Simamisha kidogo chini ya onyesho hili.<\/em><\/p>\n<p><strong>Msimulizi:<\/strong>\u00a0Nancy anatoka kwenye chumba cha matibabu ambamo daktari na muuguzi wanamshughulikia Bi. Chawila.\u00a0 Daktari anampa vitu maji maji kupitia mishipa yaani IV, na kisha madawa ya kunusa ili arejeshe fahamu, huku naye muuguzi akipima malaria na kuangalia hali ya mtoto tumboni na kugundua kuwa mtoto yuatoka.<\/p>\n<p><strong>Daktari Kamanga:<\/strong>\u00a0Muuguzi, mama huyu ana malaria +++ na ukosefu mbaya wa damu.\u00a0 Yuko katika hali ya kujifungua sasa.\u00a0\u00a0<em>(Ujumbe wa mhariri.\u00a0 Nchini Zambia, wafanyikazi wa kiafya hutumia maelezo \u201c malaria +++\u201d kuelezea malaria iliyokithiri).\u00a0<\/em>Tunapaswa kumsaidia kujifungua.<\/p>\n<p><strong>Mwuguzi:<\/strong>\u00a0Naam daktari, nakubaliana nawe.\u00a0 Mpigo wa moyo wa mtoto tumboni pia unasikika kuwa hafifu.\u00a0 Angalia, nafikiri anarejeresha fahamu sasa.\u00a0 Bi Chawila, unanisikia?<\/p>\n<p><strong>Daktari Kamanga:<\/strong>\u00a0(<em>Akikatisha<\/em>) Ona, ana fahamu zake sasa, lakini hata usifikirie upasuaji wa \u2018caesarean\u2019!\u00a0 Hebu tuone.\u00a0\u00a0<em>(kimya kidogo anapomkagua)\u2026<\/em>Sawa, nafikiri anaweza kustahimili uchungu wa uzazi na pia kusukuma mtoto.\u00a0 Tusiwe na pupa kumtuma kwa mpasuaji.\u00a0 Tunaweza kumpoteza yeye au mtoto au hata wote wawili hasa kama yuko na upungufu wa damu.\u00a0 Bi. Chawila\u2026 Bi. Chawila, unanisikia?<\/p>\n<p><strong>Bi. Chawila:\u00a0<\/strong>Eeeesh! Eeeesh! Ndio, nakusikia.\u00a0 Lakini wewe ni nani?\u00a0 Niko wapi?<\/p>\n<p><strong>Daktari Kamanga:<\/strong>\u00a0Mimi ni daktari Kamanga, na uko katika kliniki ya dharura.\u00a0 Umepoteza fahamu kwa kuwa una maradhi ya malaria yaliyokithiri, na ambayo imekuletea ukosefu wa damu unaojulikana na baadhi ya watu kama \u2018damu hafifu\u2019<\/p>\n<p>Sikiza, hakuna muda wa kujibu maswali zaidi kwa sasa.\u00a0 Uko katika hali ya kujifungua na mtoto yuko njiani.\u00a0 Nataka ufuate maagizo yangu kwa makini\u2026 Nikisema sukuma, unasukuma, sawa?<\/p>\n<p><strong>Bi. Chawila:\u00a0<\/strong>Sawa.<\/p>\n<p><strong>Daktari Kamanga:<\/strong>\u00a0Sawa sasa! Sukuma! Tena! Sawa ng\u2026ngoja..ngoja\u2026ngoja! Sawa,\u00a0 sasa utasukuma mara nyingine moja kwa nguvu na tutamaliza mara moja.\u00a0 Sukuuuma! Daa (<em>Kimya)\u00a0<\/em>\u00a0\u00a0Ndiyo huyo hapo mtoto, ni msichana.\u00a0 Lakini kwa vile mtoto hakulia wala kupiga kelele yo yote, itabidi tumfanyie majaribio ya malaria pia.\u00a0 Muuguzi.\u00a0 Fanya majaribio hayo na kisha umweke mtoto\u00a0\u00a0 kwenye oksinjeni mara moja.\u00a0 Pia unganisha mpira kwa ajiri ya chakula cha mtoto.\u00a0 Naja sasa hivi.<\/p>\n<p><strong>Mwuguzi:<\/strong>\u00a0Sawa daktari, mtoto atakuwa kwenye kitanda nambari 37.<\/p>\n<p><em>Fifiisha sauti za kliniki.\u00a0 Sekunde mbili za kimya, kasha upaaze taratibu \u00a0sauti za kliniki.\u00a0 Sauti za nyayo za daktari akikaribia<\/em><\/p>\n<p><strong>Daktari Kamanga:<\/strong>\u00a0Bi Chawila, itabidi ulazwe hapa\u00a0 katika kliniki kwa muda kwa kuwa mtoto wako ana malaria pia.\u00a0 Itabidi tuwape matibabu nyote wawili hadi pale tutakapokuwa na uhakika kuwa mko wazima.\u00a0 Hapo ndipo tutawaachilia wewe na mtoto mwende nyumbani.<\/p>\n<p><strong>Bi. Chawila:\u00a0<\/strong>Sawa, naweza kumuona mtoto sasa?<\/p>\n<p><strong>Daktari Kamanga:<\/strong>\u00a0Hata! \u00a0Unahitaji kupumzika ili uwezeshe damu na sukari zilizo kwenye mipira kuisha.\u00a0 Hapo ndipo utaweza kutembea.\u00a0 Utajisikia nafuu sana, na mwenye nguvu.\u00a0 Wauguzi watashughulikia mtoto, usitie shaka.<\/p>\n<p><em>Kimya, kisha ufifiishe sauti za watu wakitembea na kuzungumza katika kliniki.<\/em><\/p>\n<p><strong>Msimulizi:<\/strong>\u00a0Imekuwa majuma mawili tangu Bi. Chawila alipokuja kwenye kliniki.\u00a0 Leo anaachiliwa kwenda nyumbani pamoja na mtoto wake msichana.\u00a0 Wote wawili ni wazima.\u00a0 Nancy amefika kumsaidia mizigo yake.\u00a0 Anaona kuwa shangaziye anaingia kwa daktari na hivyo anamsubiri nje.\u00a0 Daktari anamweleza Bi. Chawila kuwa imebidi ampe ushauri kuhusu jinsi ya kujikinga na kutibu malaria katika ujauzito kwa ajili ya usalama wake na wa mtoto ambaye hajazaliwa.\u00a0 Hebu tusikilize kwa maakini daktari anapoongea na Bi. Chawila ofisini mwake.<\/p>\n<p><strong>Daktari Kamanga:<\/strong>\u00a0Bi. Chawila, kulingana na kadi yako ya kliniki kabla ya kujifungua, naona kuwa ulitembelea kliniki hiyo mara tatu.\u00a0 Kuna wakati ulipatiwa madawa ya kuzuia malaria au kushauriwa ulale chini ya neti iliyotibiwa?<\/p>\n<p><strong>Bi. Chawila:\u00a0<\/strong>Ndiyo daktari, nilipewa madawa yale, lakini ni lazima nikiri kuwa sikuyatumia\u2026(<em>Kimya<\/em>)<\/p>\n<p><strong>Daktari Kamanga:<\/strong>\u00a0Naam, endelea.<\/p>\n<p><strong>Bi. Chawila:\u00a0<\/strong>Nyanyangu daima aliniambia kuwa mwanamke akiwa mjamzito, hapaswi kamwe kutumia madawa ya Kizungu kwa kuwa yanaweza kusababisha mimba kutoka au kuleta madhara kwa mtoto tumboni.\u00a0 Kuna jirani yangu ambaye amejifungua mtoto aliye na kasoro, jambo lililonitia wasiwasi.\u00a0 Kwa hivyo niliyatupa madawa yale.\u00a0\u00a0<\/p>\n<p><strong>Daktari Kamanga:<\/strong>\u00a0Na neti za kuzuia mbu je?\u00a0 Umekuwa ukitumia neti iliyotibiwa?<\/p>\n<p><a name=\"OLE_LINK2\"><\/a><a name=\"OLE_LINK1\"><\/a><strong>Bi. Chawila:\u00a0<\/strong>Sijawahi kulala chini ya neti ya kuzuia mbu kwa kuwa kuna rafiki yangu aliyenieleza kuwa dawa inayotumiwa kutibu neti husabababisha mizio<strong>.<\/strong><\/p>\n<p><strong>Daktari Kamanga:<\/strong>\u00a0Naona.\u00a0 Je ulijisikia mgonjwa wakati wa ujauzito?\u00a0 Mpwao alitaja kuwa ulikuwa na maumivu makali ya kichwa na kizungunguzungu.<\/p>\n<p><strong>Bi. Chawila:\u00a0<\/strong>Ndiyo, wakati nilikuwa mjamzito kwa muda wa miezi sita, nilianza kupata maumivu hayo makali ya kichwa, homa kali, na nikapoteza hamu ya chakula.\u00a0 Hali hii ilikuwa ikinijia jioni jioni, kwa hivyo nikaipuuza.\u00a0 Nilifikiria kuwa ni hali ya ujauzito tu.\u00a0 Lakini kadri siku zilivyoendelea, ilikuwa wazi kwangu kuwa haukuwa ugonjwa wa ujauzito pekee,\u00a0\u00a0 hatimaye, nilikuwa nyumbani kwangu nikisafisha madirisha, na punde si punde, nikaona kizunguzungu.\u00a0 Ninachokumbuka tangu hapo ni kuwa nilianguka.<\/p>\n<p><strong>Daktari Kamanga:<\/strong>\u00a0Bi. Chawila, kwanza nataka ujue kuwa malaria ndiyo muuaji nambari moja nchini Zambia, na hata kote barani Afrika.\u00a0 Watu walio na uwezekano mkubwa zaidi wa kuugua malaria ni wanawake wajawazito, watoto wa umri wa chini ya miaka mitano, na watu wanoishi na virusi vya ukimwi au wenye ukimwi.\u00a0 Ama kwa kweli, malaria ni hatari kuliko ukimwi.\u00a0 Malaria huweza kuua kwa muda wa masaa au siku chache.\u00a0 Ukimwi huchukua miezi au miaka kujitokeza au kuua mtu.<\/p>\n<p><strong>Bi. Chawila:\u00a0<\/strong>Kwa hivyo ugonjwa wa malaria ndio umenipelekea kujifungua mtoto kabla ya wakati uliofaa?\u00a0 Au kuna matatizo mengine ninayopaswa kujua?\u00a0\u00a0<\/p>\n<p><strong>Daktari Kamanga:<\/strong>\u00a0La hasha, hamkuwa na matatizo mengine. Malaria ndiyo umekupelekea kujifungua katika mwezi wa saba badala ya ule wa tisa.\u00a0 Unajua, wakati mbu jike anakuuma ukiwa mjamzito, anakuletea viini vya malaria.\u00a0 Viini hivi ndivyo vinasababisha malaria.\u00a0 Viini hivi huenda mara moja hadi kwenye chungu cha uzazi ambapo huzaana kwa kasi kuliko vikiwa ndani ya mwili wa mtu ambaye hana mimba.\u00a0 Chungu cha uzazi ni mahala pazuri sana kwa viini vya malaria kuzaana.\u00a0 Kwa hivyo, mtoto aliye mle anaambukizwa.\u00a0 Virusi huendelea kuzaana mtoto akiwa mchanga na huku akiwa hana nguvu za kutosha kustahimili maambukizi.\u00a0 Mwanamke mjamzito akiwa na malaria pia yuko katika hatari ya kujifungua mapema, hii ikiwa na maana kuwa unaweza kujifungua katika mwezi wa saba badala ya ule wa tisa. Mtoto anayezaliwa katika mwezi wa saba akiwa na malaria huweza kuwa mnyonge na mwenye mwili mdogo sana.\u00a0 Wengi hawaponi kwa kuwa hawana nguvu za kupigana na maambukizi.<\/p>\n<p><strong>Bi.Chawila:<\/strong>\u00a0(<em>Akimkatiza daktari)<\/em>Hivyo ndivyo mbu jike anaweza kuwa hatari.\u00a0 (<em>Kwa mshangao<\/em>) Mungu wangu!\u00a0 Lakini niulize, tunawezaje kutambua mbu kuwa jike au dume?<\/p>\n<p><strong>Daktari Kamanga:\u00a0<\/strong>Ni mbu jike anayeleta matatizo haya yote.\u00a0 Lakini kwa vile hatuwezi kwa macho yetu pekee kutambua aliye jike au dume, lazima tujikinge kutokana na aina yo yote ya mbu kwa kutumia mbinu ambazo nitazungumzia sasa hivi.\u00a0 Kama nilivyokuwa nasema, dalili za kwanza za malaria ni kuhisi homa, maumivu ya kichwa, na dalili nyinginezo.\u00a0 Katika hali hii, \u2018wanajeshi\u2019 walio mwilini mwako \u2013 na kwa hii nina maana chembechembe za damu zinazopigana na maambukizi \u2013 huwa wamevamiwa.\u00a0 Viini huanza kuwapiga na kuwaua, hivyo kuacha mtoto kuwa katika hali mbaya ya unyonge.\u00a0 Endapo wanawake wajawazito wenye malaria hawatatibiwa, ugonjwa huu huweza kusababisha kutoka mimba, kujifungua mapema, na ukosefu wa damu.\u00a0 Hapa nchini Zambia, tumechagua mikakati miwili ya kuzuia malaria katika ujauzito na hivyo kulinda maisha ya mtoto tumboni.\u00a0 Wa kwanza ni kutumia neti zilizotibiwa.\u00a0 Pili ni kuhakikisha wanawake wajawazito wanatumia madawa ya malaria.\u00a0 Kwa kawaida, madawa haya hugawa kupitia kliniki za kabla ya kujifungua.<\/p>\n<p><strong>Bi. Chawila:\u00a0<\/strong>Daktari, mambo hayo ni mengi sana kwangu.\u00a0 Huenda nisikumbuke maelezo haya yote, ingawa najua ni mambo muhimu sana.\u00a0 Ningependa wanawake kijijini mwangu waelewe mambo haya.<\/p>\n<p><strong>Daktari\u00a0Kamanga:\u00a0<\/strong> Sawa!\u00a0 Lakini tafadhali sikiliza hapa \u2013 ni muhimu sana endapo utakuwa mjamzito tena.\u00a0 Kliniki za kabla ya kujifungua ni muhimu sana.\u00a0 Kila nipatapo nafasi ya kuzungumza na akina mama katika kliniki, mimi huwasinikisha kuendelea kutembelea vituo vya afya vilivyo karibu nao wanapokuwa wajawazito.\u00a0 Hii si kwa ajili tu ya kumwona mkunga.\u00a0 Hii inahusiana na afya ya jumla kwa mama na mtoto anayekuwa tumboni.\u00a0 Unapokosa kuhudhuria kliniki hizi, unayaweka maisha yako na ya mtoto katika hatari kubwa kwa kuwa unaweza kukosa kugundua dalili za awali za malaria.\u00a0 Aidha, unaweza kupuuza dalili za maambukizi.\u00a0 Kama ulivyofanya Bi. Chawila.<strong>.<\/strong><\/p>\n<p><strong>Bi. Chawila:\u00a0<\/strong>Lakini nikuulize daktari, madawa ya malaria hayawezi kumfanya mtoto wangu azaliwe na kilema?<\/p>\n<p><strong>Daktari Kamanga:<\/strong>\u00a0Naelewa.\u00a0 Una wasiwasi kuwa dawa ya malaria inaweza kuwa na madhara kwa mtoto aliye tumboni.\u00a0 Madawa yanayozuia malaria wakati wa ujauzito ndiyo yale yale tunayowapa watu ambao hawana mimba.\u00a0 Tunapeana madawa hayo wakati tu ni salama kwa mama na mtoto \u2013 hivyo ni kusema baada miezi 16 ya ujauzito.\u00a0 Huu ndio wakati viungo vya mwili wa mtoto tayari vimekomaa, na hakuna hatari yo yote kwa mtoto.\u00a0 Kwa wingi, madawa ya kuzuia malaria hutolewa mara tatu kwa mama wakati wote wa ujauzito.<\/p>\n<p><strong>Bi. Chawila:\u00a0<\/strong>Naona daktari.\u00a0 Kwa hivyo unasema kuwa wanawake wasianze kutumia madawa ya malaria mara tu wagunduapo kuwa ni wajawazito?<\/p>\n<p><strong>Daktari Kamanga:<\/strong>\u00a0Hapana.\u00a0\u00a0 Kama nilivyosema, tunaepuka kuwapa wajawazito dawa hii wakati viungo vya mtoto vinajitunga tumboni au katika muda wa mienzi mitatu ya mwanzo wa ujauzito.\u00a0 Katika kipindi hiki, tunawashauri wanawake kulala chini ya neti iliyotibiwa na kuhakikisha mazingira ya karibu yamesafishwa na kupuliziwa dawa.\u00a0 Dawa inayotumiwa kutibu neti za kuzuia mbu haina madhara kwa mama na mtoto aliye tumboni.\u00a0 Neti iliyotibiwa hugharimu takriban Kwacha za Zambia 3000 (<em>Maelezo ya mhariri: chini ya dola moja ya Kimarekani<\/em>), na huwaweka mama na mtoto aliye tumboni salama kutokana na malaria.<\/p>\n<p><strong>Bi. Chawila:\u00a0<\/strong>(<em>Akitabasamu kwa kutosheka na kwa shukrani<\/em>) Daktari, asante sana kwa habari hii.\u00a0 Sikujua haya yote.\u00a0 Haya mambo yana uzito sana na yapaswa kujulikana na watu wengine.\u00a0 Wanawake wengi katika jamii hii hawajui mambo haya.\u00a0 Nafikiri napaswa kuandaa mkutano na wanawake wenzangu niwaambie yaliyonipata.\u00a0 Unaonaje daktari?<\/p>\n<p><strong>Daktari Kamanga:<\/strong>\u00a0Naam! Hilo ni wazo la busara. Bi.Chawila.\u00a0 Napendekeza ualike wale wanawake ambao hukataa kwenda hospitali na kliniki wakati wa ujauzito.<\/p>\n<p><em>Sauti za mlango ukibishwa<\/em><\/p>\n<p><strong>Daktari Kamanga:<\/strong>\u00a0Ingia.<\/p>\n<p><strong>Mwuguzi:<\/strong>\u00a0\u00a0\u00a0\u00a0\u00a0\u00a0 Daktari!\u00a0 Kuna mama ambaye ameingia katika chumba cha dharura na inaonekana kama anajifungua.\u00a0 Tafadhali njoo haraka.<\/p>\n<p><strong>Daktari Kamanga:<\/strong>\u00a0Naja, mwuguzi!\u00a0 Bi. Chawila, ikiwa una maswali zaidi kuhusu malaria au jinsi ya kujitunza, tafadhali zungumza na mwuguzi huyu.\u00a0 Anaweza kueleza kila kitu vizuri kama mimi tu.<\/p>\n<p><strong>Bi. Chawila:\u00a0<\/strong>Ndio daktari.\u00a0 Nitafanya hivyo.\u00a0 Lakini daktari, ngoja!\u00a0 Unaweza kufika mkutanoni ili unisaidie kujibu maswali yatakayonishinda katika mkutano wa wanawake?<\/p>\n<p><strong>Daktari Kamanga:<\/strong>\u00a0Bila shaka Bi. Chawila.\u00a0 Nitakuwa rai kufanya hivyo, na hata wafanyi kazi wenzangu wote.\u00a0 Tunachukua malaria kwa uzito mwingi hasa inapowahusu wanawake wajawazito.\u00a0 Naomba urejee na uniambie siku na saa za mkutano huo wa jamii, na mmoja wetu akuwa tayari kukusaidia.<br \/>\n.<br \/>\n<strong>Msimulizi:<\/strong>\u00a0Daktari anatoka chumba cha ushauri kwa haraka.\u00a0 Bi. Chawila anamwita Nancy ili ambembee mikoba waende nyumbani.\u00a0 Kabla hawajaondoka, Bi. Chawila anamwomba mpwae Nancy amsaidie.<\/p>\n<p><strong>Bi. Chawila:\u00a0<\/strong>Nancy, Nancy! Nitambeba mtoto.\u00a0 Twende zetu nyumbani.\u00a0 Utanisaidia kuandikia mwenyekiti wa chama cha wanawake barua?\u00a0 Ningependa kuandaa mkutano na wanawake ili niwaeleze hatari za malaria.<\/p>\n<p><strong>Nancy:<\/strong>\u00a0(<em>Akimkatiza<\/em>) Hatari za nini?\u00a0 Shangazi! \u2026 Unapaswa kuwa nyumbani ukimwangalia huyu mtoto mchanga na kupumzika.\u00a0 Unajua uliyoyapitia wakati wa ugonjwa huu.\u00a0 Hata hujui adui yako ni nani.\u00a0 Ni aina gani ya ambukizo la malaria, ehh?<\/p>\n<p><strong>Bi. Chawila:\u00a0<\/strong>Unataka kusema nini, Nancy?\u00a0 Kwamba nimeumwa kwa sababu ya uchawi?\u00a0 Hapana mpwa wangu.\u00a0 Nimekuja kuelewa kwamba ilikuwa malaria.\u00a0 Ninahitajika kuwaeleza wanawake vile ugonjwa malaria ulivyo hatari, na vile wanaweza kukingwa kwa kutumia neti zilizotibiwa na madawa ya kukinga malaria.\u00a0 Na jinsi ya kuutibu wapougua.<\/p>\n<p><strong>Nancy:<\/strong>\u00a0Shangazi, ni kama vile umetoka shuleni wala si kliniki.\u00a0 Utawezaje kumudu kuandaa mkutano na pia kuongea mbele ya umati wa watu?<\/p>\n<p><strong>Bi. Chawila:\u00a0<\/strong>(<em>Kwa utulivu<\/em>)Ndio maana nakuomba unisaidie kuandika barua kwa mwenyekiti wa kundi letu kuwaalika wanawake wote wasikose kuhudhuria.\u00a0 Daktari Kamanga amesema kuwa atakuja kusaidia kujibu maswali nikilemewa.\u00a0 Lakini nafikiri kuwa kisa cha tuliyoyapata mimi na mwanangu kwa sababu ya malaria kitatosha kabisa kukinga ugonjwa huu hatari katika jamii yetu.\u00a0\u00a0<em>(Kimya)<\/em>\u00a0Haya, na tuondoke.\u00a0 Muda umeyoyoma.<\/p>\n","protected":false},"excerpt":{"rendered":"<p>Fifiisha sauti za nyumbani &#8230; sufuria, maji yakimiminika, na kukifagiliwa Bi. Chawila: Nancy, unaweza kuja kunisaidia kumaliza kusafisha madirisha tafadhali? Karibu nimalize. Lililobakia ni moja tu hili ya jikoni. Nancy: Shangazi, naomba nimalize kusafisha vyombo vya jikoni \u2013 naja sasa hivi. Bi. Chawila: EEEEEEhhhhyeeeee! Na Na Nanc \u2026! Nancy: (Akipiga mayowe kwa hofu) Shangazi! Shangazi!&hellip;<\/p>\n","protected":false},"author":32,"featured_media":0,"parent":0,"menu_order":9,"template":"","meta":{"footnotes":"","beyondwords_generate_audio":"","beyondwords_integration_method":"","beyondwords_project_id":"","beyondwords_content_id":"","beyondwords_preview_token":"","beyondwords_player_content":"","beyondwords_player_style":"","beyondwords_language_code":"","beyondwords_language_id":"","beyondwords_title_voice_id":"","beyondwords_body_voice_id":"","beyondwords_summary_voice_id":"","beyondwords_error_message":"","beyondwords_disabled":"","beyondwords_delete_content":"","beyondwords_podcast_id":"","beyondwords_hash":"","publish_post_to_speechkit":"","speechkit_hash":"","speechkit_generate_audio":"","speechkit_project_id":"","speechkit_podcast_id":"","speechkit_error_message":"","speechkit_disabled":"","speechkit_access_key":"","speechkit_error":"","speechkit_info":"","speechkit_response":"","speechkit_retries":"","speechkit_status":"","speechkit_updated_at":"","_speechkit_link":"","_speechkit_text":""},"script-format":[537],"package":[637],"script-category":[],"class_list":["post-4250","radio-script","type-radio-script","status-publish","hentry","script-format-maigizo","package-637"],"acf":[],"yoast_head":"<!-- This site is optimized with the Yoast SEO plugin v27.6 - https:\/\/yoast.com\/product\/yoast-seo-wordpress\/ -->\n<title>Zuia malaria wakati wa ujauzito! - Farm Radio International<\/title>\n<meta name=\"robots\" content=\"index, follow, max-snippet:-1, max-image-preview:large, max-video-preview:-1\" \/>\n<link rel=\"canonical\" href=\"https:\/\/scripts.farmradio.fm\/sw\/mwongozo-wa-redio\/zuia-malaria-wakati-wa-ujauzito\/\" \/>\n<meta property=\"og:locale\" content=\"en_US\" \/>\n<meta property=\"og:type\" content=\"article\" \/>\n<meta property=\"og:title\" content=\"Zuia malaria wakati wa ujauzito! - Farm Radio International\" \/>\n<meta property=\"og:description\" content=\"Fifiisha sauti za nyumbani &#8230; sufuria, maji yakimiminika, na kukifagiliwa Bi. Chawila: Nancy, unaweza kuja kunisaidia kumaliza kusafisha madirisha tafadhali? Karibu nimalize. Lililobakia ni moja tu hili ya jikoni. Nancy: Shangazi, naomba nimalize kusafisha vyombo vya jikoni \u2013 naja sasa hivi. Bi. Chawila: EEEEEEhhhhyeeeee! Na Na Nanc \u2026! Nancy: (Akipiga mayowe kwa hofu) Shangazi! Shangazi!&hellip;\" \/>\n<meta property=\"og:url\" content=\"https:\/\/scripts.farmradio.fm\/sw\/mwongozo-wa-redio\/zuia-malaria-wakati-wa-ujauzito\/\" \/>\n<meta property=\"og:site_name\" content=\"Farm Radio International\" \/>\n<meta property=\"article:publisher\" content=\"https:\/\/www.facebook.com\/farmradio\/\" \/>\n<meta property=\"article:modified_time\" content=\"2018-11-20T13:48:04+00:00\" \/>\n<meta name=\"twitter:card\" content=\"summary_large_image\" \/>\n<meta name=\"twitter:site\" content=\"@farmradio\" \/>\n<meta name=\"twitter:label1\" content=\"Est. reading time\" \/>\n\t<meta name=\"twitter:data1\" content=\"12 minutes\" \/>\n<script type=\"application\/ld+json\" class=\"yoast-schema-graph\">{\"@context\":\"https:\\\/\\\/schema.org\",\"@graph\":[{\"@type\":\"Article\",\"@id\":\"https:\\\/\\\/scripts.farmradio.fm\\\/sw\\\/mwongozo-wa-redio\\\/zuia-malaria-wakati-wa-ujauzito\\\/#article\",\"isPartOf\":{\"@id\":\"https:\\\/\\\/scripts.farmradio.fm\\\/sw\\\/mwongozo-wa-redio\\\/zuia-malaria-wakati-wa-ujauzito\\\/\"},\"author\":{\"name\":\"alice.lungu\",\"@id\":\"http:\\\/\\\/scripts.farmradio.fm\\\/sw\\\/#\\\/schema\\\/person\\\/2a11cb1c0a6a2415436dae0f6ed1769a\"},\"headline\":\"Zuia malaria wakati wa ujauzito!\",\"datePublished\":\"2012-04-26T17:10:30+00:00\",\"dateModified\":\"2018-11-20T13:48:04+00:00\",\"mainEntityOfPage\":{\"@id\":\"https:\\\/\\\/scripts.farmradio.fm\\\/sw\\\/mwongozo-wa-redio\\\/zuia-malaria-wakati-wa-ujauzito\\\/\"},\"wordCount\":2307,\"publisher\":{\"@id\":\"http:\\\/\\\/scripts.farmradio.fm\\\/sw\\\/#organization\"},\"inLanguage\":\"sw-CG\"},{\"@type\":\"WebPage\",\"@id\":\"https:\\\/\\\/scripts.farmradio.fm\\\/sw\\\/mwongozo-wa-redio\\\/zuia-malaria-wakati-wa-ujauzito\\\/\",\"url\":\"https:\\\/\\\/scripts.farmradio.fm\\\/sw\\\/mwongozo-wa-redio\\\/zuia-malaria-wakati-wa-ujauzito\\\/\",\"name\":\"Zuia malaria wakati wa ujauzito! - Farm Radio International\",\"isPartOf\":{\"@id\":\"http:\\\/\\\/scripts.farmradio.fm\\\/sw\\\/#website\"},\"datePublished\":\"2012-04-26T17:10:30+00:00\",\"dateModified\":\"2018-11-20T13:48:04+00:00\",\"breadcrumb\":{\"@id\":\"https:\\\/\\\/scripts.farmradio.fm\\\/sw\\\/mwongozo-wa-redio\\\/zuia-malaria-wakati-wa-ujauzito\\\/#breadcrumb\"},\"inLanguage\":\"sw-CG\",\"potentialAction\":[{\"@type\":\"ReadAction\",\"target\":[\"https:\\\/\\\/scripts.farmradio.fm\\\/sw\\\/mwongozo-wa-redio\\\/zuia-malaria-wakati-wa-ujauzito\\\/\"]}]},{\"@type\":\"BreadcrumbList\",\"@id\":\"https:\\\/\\\/scripts.farmradio.fm\\\/sw\\\/mwongozo-wa-redio\\\/zuia-malaria-wakati-wa-ujauzito\\\/#breadcrumb\",\"itemListElement\":[{\"@type\":\"ListItem\",\"position\":1,\"name\":\"Nyumbani\",\"item\":\"http:\\\/\\\/scripts.farmradio.fm\\\/sw\\\/\"},{\"@type\":\"ListItem\",\"position\":2,\"name\":\"Maigizo\",\"item\":\"https:\\\/\\\/scripts.farmradio.fm\\\/sw\\\/mwongozo-wa-muundo\\\/maigizo\\\/\"},{\"@type\":\"ListItem\",\"position\":3,\"name\":\"Zuia malaria wakati wa ujauzito!\"}]},{\"@type\":\"WebSite\",\"@id\":\"http:\\\/\\\/scripts.farmradio.fm\\\/sw\\\/#website\",\"url\":\"http:\\\/\\\/scripts.farmradio.fm\\\/sw\\\/\",\"name\":\"Farm Radio International\",\"description\":\"Sharing knowledge, giving voice.\",\"publisher\":{\"@id\":\"http:\\\/\\\/scripts.farmradio.fm\\\/sw\\\/#organization\"},\"potentialAction\":[{\"@type\":\"SearchAction\",\"target\":{\"@type\":\"EntryPoint\",\"urlTemplate\":\"http:\\\/\\\/scripts.farmradio.fm\\\/sw\\\/?s={search_term_string}\"},\"query-input\":{\"@type\":\"PropertyValueSpecification\",\"valueRequired\":true,\"valueName\":\"search_term_string\"}}],\"inLanguage\":\"sw-CG\"},{\"@type\":\"Organization\",\"@id\":\"http:\\\/\\\/scripts.farmradio.fm\\\/sw\\\/#organization\",\"name\":\"Farm Radio International\",\"url\":\"http:\\\/\\\/scripts.farmradio.fm\\\/sw\\\/\",\"logo\":{\"@type\":\"ImageObject\",\"inLanguage\":\"sw-CG\",\"@id\":\"http:\\\/\\\/scripts.farmradio.fm\\\/sw\\\/#\\\/schema\\\/logo\\\/image\\\/\",\"url\":\"https:\\\/\\\/scripts.farmradio.fm\\\/wp-content\\\/uploads\\\/farmRadioLogo.jpg\",\"contentUrl\":\"https:\\\/\\\/scripts.farmradio.fm\\\/wp-content\\\/uploads\\\/farmRadioLogo.jpg\",\"width\":200,\"height\":75,\"caption\":\"Farm Radio International\"},\"image\":{\"@id\":\"http:\\\/\\\/scripts.farmradio.fm\\\/sw\\\/#\\\/schema\\\/logo\\\/image\\\/\"},\"sameAs\":[\"https:\\\/\\\/www.facebook.com\\\/farmradio\\\/\",\"https:\\\/\\\/x.com\\\/farmradio\",\"https:\\\/\\\/www.instagram.com\\\/farmradio\\\/\",\"https:\\\/\\\/www.youtube.com\\\/user\\\/FarmRadioInt\"]},{\"@type\":\"Person\",\"@id\":\"http:\\\/\\\/scripts.farmradio.fm\\\/sw\\\/#\\\/schema\\\/person\\\/2a11cb1c0a6a2415436dae0f6ed1769a\",\"name\":\"alice.lungu\",\"image\":{\"@type\":\"ImageObject\",\"inLanguage\":\"sw-CG\",\"@id\":\"https:\\\/\\\/secure.gravatar.com\\\/avatar\\\/abb05f561c29fbd3fb1fec94b50a6a0cbb5009e8ae2ba3ba7ee92d032645461f?s=96&d=mm&r=g\",\"url\":\"https:\\\/\\\/secure.gravatar.com\\\/avatar\\\/abb05f561c29fbd3fb1fec94b50a6a0cbb5009e8ae2ba3ba7ee92d032645461f?s=96&d=mm&r=g\",\"contentUrl\":\"https:\\\/\\\/secure.gravatar.com\\\/avatar\\\/abb05f561c29fbd3fb1fec94b50a6a0cbb5009e8ae2ba3ba7ee92d032645461f?s=96&d=mm&r=g\",\"caption\":\"alice.lungu\"}}]}<\/script>\n<!-- \/ Yoast SEO plugin. -->","yoast_head_json":{"title":"Zuia malaria wakati wa ujauzito! - Farm Radio International","robots":{"index":"index","follow":"follow","max-snippet":"max-snippet:-1","max-image-preview":"max-image-preview:large","max-video-preview":"max-video-preview:-1"},"canonical":"https:\/\/scripts.farmradio.fm\/sw\/mwongozo-wa-redio\/zuia-malaria-wakati-wa-ujauzito\/","og_locale":"en_US","og_type":"article","og_title":"Zuia malaria wakati wa ujauzito! - Farm Radio International","og_description":"Fifiisha sauti za nyumbani &#8230; sufuria, maji yakimiminika, na kukifagiliwa Bi. Chawila: Nancy, unaweza kuja kunisaidia kumaliza kusafisha madirisha tafadhali? Karibu nimalize. Lililobakia ni moja tu hili ya jikoni. Nancy: Shangazi, naomba nimalize kusafisha vyombo vya jikoni \u2013 naja sasa hivi. Bi. Chawila: EEEEEEhhhhyeeeee! Na Na Nanc \u2026! Nancy: (Akipiga mayowe kwa hofu) Shangazi! Shangazi!&hellip;","og_url":"https:\/\/scripts.farmradio.fm\/sw\/mwongozo-wa-redio\/zuia-malaria-wakati-wa-ujauzito\/","og_site_name":"Farm Radio International","article_publisher":"https:\/\/www.facebook.com\/farmradio\/","article_modified_time":"2018-11-20T13:48:04+00:00","twitter_card":"summary_large_image","twitter_site":"@farmradio","twitter_misc":{"Est. reading time":"12 minutes"},"schema":{"@context":"https:\/\/schema.org","@graph":[{"@type":"Article","@id":"https:\/\/scripts.farmradio.fm\/sw\/mwongozo-wa-redio\/zuia-malaria-wakati-wa-ujauzito\/#article","isPartOf":{"@id":"https:\/\/scripts.farmradio.fm\/sw\/mwongozo-wa-redio\/zuia-malaria-wakati-wa-ujauzito\/"},"author":{"name":"alice.lungu","@id":"http:\/\/scripts.farmradio.fm\/sw\/#\/schema\/person\/2a11cb1c0a6a2415436dae0f6ed1769a"},"headline":"Zuia malaria wakati wa ujauzito!","datePublished":"2012-04-26T17:10:30+00:00","dateModified":"2018-11-20T13:48:04+00:00","mainEntityOfPage":{"@id":"https:\/\/scripts.farmradio.fm\/sw\/mwongozo-wa-redio\/zuia-malaria-wakati-wa-ujauzito\/"},"wordCount":2307,"publisher":{"@id":"http:\/\/scripts.farmradio.fm\/sw\/#organization"},"inLanguage":"sw-CG"},{"@type":"WebPage","@id":"https:\/\/scripts.farmradio.fm\/sw\/mwongozo-wa-redio\/zuia-malaria-wakati-wa-ujauzito\/","url":"https:\/\/scripts.farmradio.fm\/sw\/mwongozo-wa-redio\/zuia-malaria-wakati-wa-ujauzito\/","name":"Zuia malaria wakati wa ujauzito! - Farm Radio International","isPartOf":{"@id":"http:\/\/scripts.farmradio.fm\/sw\/#website"},"datePublished":"2012-04-26T17:10:30+00:00","dateModified":"2018-11-20T13:48:04+00:00","breadcrumb":{"@id":"https:\/\/scripts.farmradio.fm\/sw\/mwongozo-wa-redio\/zuia-malaria-wakati-wa-ujauzito\/#breadcrumb"},"inLanguage":"sw-CG","potentialAction":[{"@type":"ReadAction","target":["https:\/\/scripts.farmradio.fm\/sw\/mwongozo-wa-redio\/zuia-malaria-wakati-wa-ujauzito\/"]}]},{"@type":"BreadcrumbList","@id":"https:\/\/scripts.farmradio.fm\/sw\/mwongozo-wa-redio\/zuia-malaria-wakati-wa-ujauzito\/#breadcrumb","itemListElement":[{"@type":"ListItem","position":1,"name":"Nyumbani","item":"http:\/\/scripts.farmradio.fm\/sw\/"},{"@type":"ListItem","position":2,"name":"Maigizo","item":"https:\/\/scripts.farmradio.fm\/sw\/mwongozo-wa-muundo\/maigizo\/"},{"@type":"ListItem","position":3,"name":"Zuia malaria wakati wa ujauzito!"}]},{"@type":"WebSite","@id":"http:\/\/scripts.farmradio.fm\/sw\/#website","url":"http:\/\/scripts.farmradio.fm\/sw\/","name":"Farm Radio International","description":"Sharing knowledge, giving voice.","publisher":{"@id":"http:\/\/scripts.farmradio.fm\/sw\/#organization"},"potentialAction":[{"@type":"SearchAction","target":{"@type":"EntryPoint","urlTemplate":"http:\/\/scripts.farmradio.fm\/sw\/?s={search_term_string}"},"query-input":{"@type":"PropertyValueSpecification","valueRequired":true,"valueName":"search_term_string"}}],"inLanguage":"sw-CG"},{"@type":"Organization","@id":"http:\/\/scripts.farmradio.fm\/sw\/#organization","name":"Farm Radio International","url":"http:\/\/scripts.farmradio.fm\/sw\/","logo":{"@type":"ImageObject","inLanguage":"sw-CG","@id":"http:\/\/scripts.farmradio.fm\/sw\/#\/schema\/logo\/image\/","url":"https:\/\/scripts.farmradio.fm\/wp-content\/uploads\/farmRadioLogo.jpg","contentUrl":"https:\/\/scripts.farmradio.fm\/wp-content\/uploads\/farmRadioLogo.jpg","width":200,"height":75,"caption":"Farm Radio International"},"image":{"@id":"http:\/\/scripts.farmradio.fm\/sw\/#\/schema\/logo\/image\/"},"sameAs":["https:\/\/www.facebook.com\/farmradio\/","https:\/\/x.com\/farmradio","https:\/\/www.instagram.com\/farmradio\/","https:\/\/www.youtube.com\/user\/FarmRadioInt"]},{"@type":"Person","@id":"http:\/\/scripts.farmradio.fm\/sw\/#\/schema\/person\/2a11cb1c0a6a2415436dae0f6ed1769a","name":"alice.lungu","image":{"@type":"ImageObject","inLanguage":"sw-CG","@id":"https:\/\/secure.gravatar.com\/avatar\/abb05f561c29fbd3fb1fec94b50a6a0cbb5009e8ae2ba3ba7ee92d032645461f?s=96&d=mm&r=g","url":"https:\/\/secure.gravatar.com\/avatar\/abb05f561c29fbd3fb1fec94b50a6a0cbb5009e8ae2ba3ba7ee92d032645461f?s=96&d=mm&r=g","contentUrl":"https:\/\/secure.gravatar.com\/avatar\/abb05f561c29fbd3fb1fec94b50a6a0cbb5009e8ae2ba3ba7ee92d032645461f?s=96&d=mm&r=g","caption":"alice.lungu"}}]}},"_links":{"self":[{"href":"https:\/\/scripts.farmradio.fm\/sw\/wp-json\/wp\/v2\/radio-script\/4250","targetHints":{"allow":["GET"]}}],"collection":[{"href":"https:\/\/scripts.farmradio.fm\/sw\/wp-json\/wp\/v2\/radio-script"}],"about":[{"href":"https:\/\/scripts.farmradio.fm\/sw\/wp-json\/wp\/v2\/types\/radio-script"}],"author":[{"embeddable":true,"href":"https:\/\/scripts.farmradio.fm\/sw\/wp-json\/wp\/v2\/users\/32"}],"version-history":[{"count":0,"href":"https:\/\/scripts.farmradio.fm\/sw\/wp-json\/wp\/v2\/radio-script\/4250\/revisions"}],"wp:attachment":[{"href":"https:\/\/scripts.farmradio.fm\/sw\/wp-json\/wp\/v2\/media?parent=4250"}],"wp:term":[{"taxonomy":"script-format","embeddable":true,"href":"https:\/\/scripts.farmradio.fm\/sw\/wp-json\/wp\/v2\/script-format?post=4250"},{"taxonomy":"package","embeddable":true,"href":"https:\/\/scripts.farmradio.fm\/sw\/wp-json\/wp\/v2\/package?post=4250"},{"taxonomy":"script-category","embeddable":true,"href":"https:\/\/scripts.farmradio.fm\/sw\/wp-json\/wp\/v2\/script-category?post=4250"}],"curies":[{"name":"wp","href":"https:\/\/api.w.org\/{rel}","templated":true}]}}