{"id":4248,"date":"2010-11-01T13:17:41","date_gmt":"2010-11-01T10:17:41","guid":{"rendered":"http:\/\/frrp.wpengine.com\/?post_type=radio-resource-packs&#038;p=4248"},"modified":"2016-02-22T02:29:57","modified_gmt":"2016-02-22T02:29:57","slug":"maji-ni-uhai-yagawe","status":"publish","type":"radio-script","link":"https:\/\/scripts.farmradio.fm\/sw\/mwongozo-wa-redio\/maji-ni-uhai-yagawe\/","title":{"rendered":"Maji ni uhai. Yagawe."},"content":{"rendered":"<p><strong>Wahusika\u00a0<\/strong><br \/>\n<strong>German:<\/strong> Mtu mwenye busara na moyo safi katika kijiji<br \/>\n<strong>Mkuu wa Kijiji:<\/strong> Mwenye busara lakini menye unyonge mara kwa mara.<br \/>\n<strong>Eda:<\/strong> Mwanamke mzee, mjane, anawalea mayatima walioachwa na mwanawe wa kiume\u00a0<a name=\"_GoBack\"><\/a>aliyefariki aliyefariki njaa.<br \/>\n<strong>Bimphi:<\/strong> Mlevi wa kawaida.\u00a0 Mwenye bidii, lakini anayetumia pesa zake nyingi kulewa pombe.<br \/>\n<strong>James:<\/strong>\u00a0 Mpwa wa Mkuu wa Kijiji, mgumu wa roho na mchoyo<br \/>\n<strong>Jacob:<\/strong> Rafiki mwema wa Bimphi, mwenye bidii na asiyeshiriki pombe<\/p>\n<p><strong>Msimulizi:<\/strong>\u00a0Kijiji cha Tiopaizi katika eneo linalosimamiwa na Chifu Msakambewa kilipoteza watu watano kwa ajili ya njaa mnamo 2001.\u00a0 Baada ya mkasa huu, waligundua kuwa kuna hazina fiche ambayo ilkuwa haitumiki: kulikuwa na mto wa kudumu katika kijiji kile. Walikutana baada ya kushinikizwa na mpendwa afisa kilimo wa eneo lao.\u00a0 Walikubaliana kuanzisha mradi wa kunyunyizia maji mashambani ili kuongezea mavuno ya kutokana na maji ya mvua.<\/p>\n<p>Lakini tatizo lilikuwa kuwa sehemu ilifaa zaidi kwa kilimo hiki cha unyunyiziaji maji ilikuwa sehemu ya eneo tengwa la msitu wa serikali.\u00a0 Walihitaji ruhusa kutoka kwa Idara ya Misitu kupitia kwa Mkuu wa Wilaya yao Bwana DC.\u00a0 Mkuu wa Kijiji aliamua kumwona Bwana DC.\u00a0 Je, Bwana DC atawapa ruhusa kutumia ardhi wanayohitaji?<\/p>\n<p><strong>FX:\u00a0<\/strong><em>Umati wa watu katika ua la mkuu wa kijiji.\u00a0<\/em><\/p>\n<p><strong>Bimphi:<\/strong>\u00a0(<em>Akiongea kwa sauti ya chini inayosikika chini ya kelele ya umati<\/em>) Jacob, ona vile mkuu wa kijiji anaoenekana mwenye huzuni\u2026..nilikwambia, Bwana DC hatakubali jambo hili.<\/p>\n<p><strong>Jacob:<\/strong>\u00a0Bimphi, hebu tusikilize anachotaka kutwambia\u2026.<\/p>\n<p><strong>Bimphi:<\/strong>\u00a0Lakini hii ndiyo ilikuwa nafasi yetu ya kupata pesa za kutosha kununulia bia<\/p>\n<p><strong>Jacob:<\/strong>\u00a0Wewe hufikiria bia pekee.\u00a0 Marafiki zako wanafikiria chakula.<\/p>\n<p><strong>Bimphi:<\/strong>\u00a0Mkuki kwa nguruwe, tamu kwa binadamu.\u00a0 Nazungumzia chakula changu bwana\u2026.Si watu walikufa njaa na kuniacha mie \u2013 mlevi \u2013 hai?<\/p>\n<p><strong>Jacob:<\/strong>\u00a0Koma wee!\u00a0 Hilo si jambo la mzaha.<\/p>\n<p><strong>Mkuu wa Kijiji:\u00a0<\/strong>Kimya tafadhali!\u00a0 Kimya!\u00a0 Nimewaita hapa nyote ili niwaeleze matokeo ya mazungumzo yangu na Bwana DC.<\/p>\n<p><strong>Bimphi:<\/strong>\u00a0(<em>Kwa sauti ya kilevi<\/em>) Mkuu wa kijiji, wewe tuambie moja kwa moja ulilotuitia.<\/p>\n<p><strong>James:<\/strong>\u00a0(<em>Akimkemea Bimphi<\/em>) Nyamaza wewe!\u00a0 Tunataka kusikia anachosema mkuu wa kijiji.<\/p>\n<p><strong>Bimphi:<\/strong>\u00a0Nani hataki kusikia sasa\u2026?\u00a0 Wewe James hujiona mwelevu sana.<\/p>\n<p><strong>Umati:<\/strong>\u00a0(<em>Kelele<\/em>) Aaaa wewe!<\/p>\n<p><strong>Sauti:<\/strong>\u00a0Bimphi daima huwa mlevi \u2013 yeye hupata wapi pesa?<\/p>\n<p><strong>Sauti nyingine:<\/strong>\u00a0Ni kweli.\u00a0 Kinachomnonesha nguruwe hakijulikani, au siyo?<\/p>\n<p><strong>Mkuu wa Kijiji:<\/strong>\u00a0Keti wewe Bimphi, na unyamaze\u2026 Bwana DC\u2026. amekubali ombi letu<\/p>\n<p><strong>Wote:\u00a0<\/strong>Ndio, ndio.<\/p>\n<p><em>Wanakijiji wanaimba wimbo wa kumsifu mkuu wa kijiji kwa ujasiri wake.<\/em><\/p>\n<p><strong>Kongwe:\u00a0<\/strong>Tiopaizi Ni samba \u2026.iiiii.<\/p>\n<p><strong>Wote:\u00a0<\/strong>Yeye ni simba.<\/p>\n<p><strong>Kongwe:\u00a0<\/strong>Yeye ni simba.<\/p>\n<p><strong>Wote:\u00a0<\/strong>Yeye ni simba ii\u2026ii\u2026ndio, yeye ni simba ii\u2026ii\u2026ndio.\u00a0 Yeye ni simba<\/p>\n<p><strong>Mkuu wa kijiji:\u00a0<\/strong>Asanteni, asanteni.\u00a0 Ketini.\u00a0 Bwana DC atatuma masoroveya kuweka mipaka mipya kesho.<\/p>\n<p><strong>Wote: (<\/strong><em>Wengine wakipiga mbinja<\/em> Ndio, mkuu wa kijiji. <\/p>\n<p><strong>Mkuu wa kijiji:\u00a0<\/strong>Yeye ana furaha kuwa hatujawahi kunyakua sehemu ya msitu.\u00a0 Hii ndiyo zawadi yetu.<\/p>\n<p><strong>Eda:\u00a0<\/strong>(<em>Analia kwa kwikwi<\/em>) Oh, mkuu wa kijiji, tazama.\u00a0 Haya yanafanyika wakati tayari nimepoteza mwanangu mpendwa kwa ajili ya njaa.\u00a0 Asante, mkuu wa kijiji!<\/p>\n<p><strong>Bimphi<\/strong>: Eda bibi yetu, hii si siku ya matanga bibie\u2026 tunaserehekea hapa.\u00a0 Usituharibie shangwe, mama.\u00a0 Tutakuwa na pesa za kutosha kulewa sasa.<\/p>\n<p><strong>Eda:<\/strong>\u00a0(<em>Akiongea pole pole<\/em>) Bimphi, inasitikisha kuwa mradi huu wa unyunyiziaji maji mashambani unakuja baada yangu kupotesha mtoto wa miaka ishirini na mitano kwa sababu ya njaa\u2026.\u00a0 Hebu angalia mayatima na mama yao alioniachia.<\/p>\n<p><strong>Mkuu wa kijiji: \u00a0<\/strong>Ama kwa kweli ni jambo la kusikitisha kuwa tulifiwa na watu watano kutokana na njaa mwaka uliopita\u2026Mungu na awarehemu.<\/p>\n<p><strong>Bimphi:\u00a0<\/strong>Ndio, mkuu wa kijiji.\u00a0 Ama kwa kweli Mungu awarehemu.<\/p>\n<p><strong>Mkuu wa kijiji:<\/strong>\u00a0Nina tangazo moja.\u00a0 Yule afisa wa ardhi atakuja kesho asubuhi kuhamisha mpaka wa eneo tengwa na kutuachia bonde\u2026Tukutane pale na tutie bidii kulima ardhi ile.<\/p>\n<p><strong>Wote:<\/strong>\u00a0Ndio.<\/p>\n<p><strong>James:<\/strong>\u00a0Huu utakuwa mwisho wa njaa kijijini mwetu.<\/p>\n<p><em>Mpito wa jukwaa<\/em><\/p>\n<p><strong>Msimulizi:\u00a0<\/strong>TWatu wa kijiji cha Tiopaizi walifanya kazi kwa bidii sana kulima ardhi waliopewa.\u00a0\u00a0 Walifanikiwa kugeuza mto na kuuelekeza kwenye ardhi hii huku wakisaidiwa na afisa kilimo wa eneo lao.\u00a0 Watu walipanda mahindi ili kuongezea chakula chao.\u00a0 Mahindi yalistawi.\u00a0 Lakini jambo fulani likatokea.\u00a0 Ni jambo gani hili?\u00a0 Je, njaa itasahaulika katika kijiji hiki?<\/p>\n<p><strong>FX:<\/strong>\u00a0<em>Jogoo anawika.\u00a0 Mlango unabishwa.<\/em><\/p>\n<p><strong>James:<\/strong>\u00a0Nani?<\/p>\n<p><strong>German:<\/strong>\u00a0Fungua mlango, James.\u00a0 Ni mimi.<\/p>\n<p><strong>James:<\/strong>\u00a0(<em>Akiwa na usingizi<\/em>) Nani?<br \/>\n<strong>German:<\/strong>\u00a0German\u2026. Amka.\u00a0 Kuja twende tukanyunyizie maji mimea yetu kabla yaw engine kuamka.<\/p>\n<p><strong>James:<\/strong>\u00a0Kwani ni saa ngapi hizi?<\/p>\n<p><strong>German:\u00a0<\/strong>Ni saa kumi asubuhi\u2026. Si tuliagana tuamke saa hizi?<\/p>\n<p><strong>FX:<\/strong>\u00a0<em>Mlango unafunguliwa.\u00a0 James anaenda miayo.<\/em><\/p>\n<p><strong>James:<\/strong>\u00a0\u00a0\u00a0\u00a0\u00a0\u00a0\u00a0\u00a0\u00a0\u00a0\u00a0 Usingizi ulikuwa mtamu huo.\u00a0 Unajua wakati wa baridi ya asubuhi, usingizi unakuwa mtamu.<\/p>\n<p><strong>German:<\/strong>\u00a0Mashamba yetu yako mbali na kitovu cha maji, hivyo hatuna bahati.\u00a0 Hii ndiyo maana lazima tuamke mapema namna hii.<\/p>\n<p><strong>James:\u00a0\u00a0\u00a0\u00a0\u00a0\u00a0\u00a0\u00a0\u00a0\u00a0\u00a0\u00a0<\/strong>Najua.\u00a0 Hebu tuanzie shamba langu kwa sababu liko mbali zaidi.\u00a0 Tutaenda kwenye shamba lako baadaye.<\/p>\n<p><strong>German:<\/strong>\u00a0Hamna shida rafiki yangu.<\/p>\n<p><em>Mpito wa jukwaa<\/em><\/p>\n<p><strong>FX:<\/strong>\u00a0<em>Maji yakitiririka na kufanya makelele chini kwa chini<\/em><\/p>\n<p><strong>James:<\/strong>\u00a0German, Angalia!\u00a0 Maji yanavunja mkondo huo.\u00a0 Funga mtaro huo.<\/p>\n<p><strong>German:<\/strong>\u00a0Huoni kuwa najaribu kuufunga?\u00a0 Lakini maji bado yanavunja\u2026 \u2026<\/p>\n<p><strong>James:\u00a0\u00a0\u00a0\u00a0\u00a0\u00a0\u00a0\u00a0\u00a0\u00a0\u00a0\u00a0<\/strong>Sawa, fungua mtaro wa kuelekea unakotaka yaende kwanza ili upunguze nguvu zake.\u00a0 Kisha ufunge ile ya usikotaka yaende.<\/p>\n<p><em>Wanacheka wote.<\/em><\/p>\n<p><strong>German:\u00a0<\/strong>Na kweli imefaa \u2026 ndio \u2026<\/p>\n<p><strong>FX:\u00a0<\/strong><em>Kelele za maji zinaisha.\u00a0<\/em><\/p>\n<p><strong>German:\u00a0<\/strong>Kuna nini sasa?\u00a0 Hebu ona, ni kiasi kidogo tu cha maji kinachokuja.\u00a0 Ni kitu gani kimetokea?&#8230;Kweli tutamaliza kunyunyizia maji leo kwa kutumia kiasi hiki kidogo kinachokuja?\u00a0 Dakika kumi kumaliza kijisehemu kimoja \u2013 haya mambo yamezidi!<\/p>\n<p><strong>James:<\/strong>\u00a0\u00a0\u00a0\u00a0\u00a0\u00a0\u00a0\u00a0\u00a0\u00a0\u00a0 Nafikiri kuna kitu kilichozimba ule mtaro mkuu<\/p>\n<p><strong>German:<\/strong>\u00a0Nafikiri hayo ni kweli.\u00a0 Huenda hiyo ndiyo sababu\u2026.Tufanye nini?<\/p>\n<p><strong>James:<\/strong>\u00a0\u00a0\u00a0\u00a0\u00a0\u00a0\u00a0\u00a0\u00a0\u00a0\u00a0 Hebu niende nikaone kinachoendelea\u2026Wewe endelea kuweka maji \u2013 naja..<br \/>\n<strong>German:<\/strong>\u00a0Twende wote.\u00a0 Endapo ni jiwe kubwa lililozimba mtaro, huenda ikabidi watu wawili washirikiane kuliondoa.<\/p>\n<p><em>Mpito wa jukwaa<\/em><\/p>\n<p><strong>FX:<\/strong><em>\u00a0Sauti ya maji\u00a0<\/em><\/p>\n<p><strong>German:<\/strong>\u00a0Hakuna kitu kilichozimba mto hapa.\u00a0 Kila kitu ni sawa.<\/p>\n<p><strong>James:\u00a0\u00a0\u00a0\u00a0\u00a0\u00a0\u00a0\u00a0\u00a0\u00a0\u00a0\u00a0<\/strong>Sawa, sasa ninajua.\u00a0 Naona kuwa Bimphi, Jacob na bibi Eda pia wanatumia maji, na mashamba yao yako karibu na kiini cha maji.<\/p>\n<p><strong>German:<\/strong>\u00a0Naam.\u00a0 Kwa hivyo tutafanya nini?<\/p>\n<p><strong>Bimphi:<\/strong>\u00a0(<em>Tayari amelewa<\/em>) Habari ya asubuhi German na James.\u00a0 Kwa nini mnaonekana wenye wasiwasi.\u00a0 Kuna nini?<\/p>\n<p><strong>James:<\/strong>\u00a0Bimphi, mlianza lini kunyunyizia maji?<\/p>\n<p><strong>Jacob:<\/strong>\u00a0James, hilo ni swali la aina gani?\u00a0 Una maana kuwa huoni kwamba tumeanza sasa hivi?<\/p>\n<p><strong>Bimphi:<\/strong>\u00a0Jacob, huwa sijibu maswali ya kijinga.\u00a0 Jibu langu kwa swali hilo litaleta tofauti gani?<\/p>\n<p><strong>James:\u00a0\u00a0\u00a0\u00a0\u00a0\u00a0\u00a0\u00a0\u00a0\u00a0\u00a0\u00a0<\/strong>Bimphi, tayari unanifahamu, na naomba tusigombane.\u00a0 Sisi ndio tulitangulia kufika hapa.\u00a0 Mlitupata hapa na mnaweza kunyunyizia pindi tukimaliza.<\/p>\n<p><strong>Bimphi:<\/strong>\u00a0Kwa nini tusubiri mmalize kwanza?\u00a0 Mradi huu ni wetu sote.<\/p>\n<p><strong>German:<\/strong>\u00a0Shinda ni kuwa maji yameacha kuenda kwenye mashamba yetu kwa kuwa mnayatumia.\u00a0 Yanayofika kule ni kidogo no.<\/p>\n<p><strong>Jacob:\u00a0<\/strong>Je, hilo ni tatizo letu?\u00a0 Fanyeni mtakalo, lakini kamwe hatuachi kunyunyizia mimea yetu maji.<\/p>\n<p><strong>James:\u00a0\u00a0<\/strong>Hivi ndivyo mambo yanavyofanyika: aliyetangulia anaanza yeye.\u00a0 Natoa amri uache.\u00a0 Kama huachi, nitakugonga.<\/p>\n<p><strong>Bimphi:<\/strong>\u00a0Sawa! sawa, Jacob, na tuyaache hayo.\u00a0 Mpwa wa mkuu wa kijiji anastahili kunyunyizia kabla ya wengine\u2026huyu ni mtu anayeweza kumchapa ye yote yule akitaka.<\/p>\n<p><strong>James:<\/strong>\u00a0Usiongee, acha tu.\u00a0 Enda nyumbani urejee baadaye, kwa\u00a0 kuwa hatutaki utuingilie tena.<\/p>\n<p><strong>Bimphi:<\/strong>\u00a0Ndiyo, Chifu.<\/p>\n<p><strong>James:\u00a0<\/strong>Bi kizee, koma kunyunyizia na uende nyumbani.<\/p>\n<p><strong>German:<\/strong>\u00a0Anaweza kunyunyizia.\u00a0 Mwache anyunyizie.<\/p>\n<p><strong>James:<\/strong>\u00a0Kuna tofauti gani?\u00a0 (Kwa Eda)\u00a0 Koma, nenda nyumbani, kisha urejee baadaye.<\/p>\n<p><em>Mpito wa jukwaa<\/em><\/p>\n<p><strong>Msimulizi:<\/strong>\u00a0Mzozano kuhusu maji umeanza.\u00a0 Je, tatizo hili litafika kikomo.\u00a0 Je, wanakijiji hawa watafikia malengo yao?<\/p>\n<p><strong>FX:<\/strong>\u00a0<em>Sauti za kimaumbile za usiku vichakani.\u00a0<\/em><\/p>\n<p><strong>James:<\/strong>\u00a0\u00a0\u00a0\u00a0\u00a0\u00a0\u00a0\u00a0\u00a0\u00a0\u00a0 Tazama uzuri wa mahindi tuliyo nayo mwaka huu.\u00a0 Hayakauki kwa ukosefu wa maji kama mashamba haya mengine.<\/p>\n<p><strong>German:<\/strong>\u00a0Ama kwa kweli ni mahindi mazuri sana.\u00a0 Lakini hii ni kwa sababu tunaamka mapema ili kunyunyizia mimea yetu.<\/p>\n<p><strong>James:<\/strong>\u00a0Si ndio! Unajua kuwa mgaagaa na upwa hali wali mkavu?<\/p>\n<p><strong>German:\u00a0<\/strong>Najua. \u00a0Lakini watu wanahoji kwamba hatuwapi nafasi kumwagia mimea yao maji..<\/p>\n<p><strong>James:\u00a0<\/strong>Je, unakubaliana nao?\u00a0 German, unakubaliana nao?<\/p>\n<p><strong>German:<\/strong>\u00a0Nimekuwa nikifikiria kuhusu suluhisho la kudumu kwa tatizo hili.\u00a0 Sipendi lile wazo la kuwahi huku tukiwa na watoto na wazee kati ya wanachama.<\/p>\n<p><strong>James:<\/strong>\u00a0\u00a0\u00a0\u00a0\u00a0\u00a0\u00a0\u00a0\u00a0\u00a0\u00a0 Usiongee kama mhubiri.\u00a0 Sote tunafanya inavyostahili.\u00a0 Je, tunawasimamisha wale tunaowakuta mashambani\u2026.?\u00a0 Wewe fikiria, maji yameacha kutufikia.\u00a0 Hii ni haki?\u00a0 Wamekuja tena.\u00a0 Unayataka haya, German?<\/p>\n<p><strong>German:<\/strong>\u00a0Utafanya nini?\u00a0 Ni yule mama mzee, Bimphi na Jacob.\u00a0 Tufanye nini?<\/p>\n<p><strong>James:\u00a0\u00a0\u00a0\u00a0\u00a0\u00a0\u00a0\u00a0\u00a0\u00a0\u00a0\u00a0<\/strong>Nitawakataza.\u00a0 Hawakutuelewa vizuri tulipowakataza jana.<\/p>\n<p><strong>German:\u00a0<\/strong>Hapana, mwache yule mama mzee amwagie maji.\u00a0 Yule bwana anaweza kuacha.<\/p>\n<p><strong>James:\u00a0\u00a0\u00a0\u00a0\u00a0\u00a0\u00a0\u00a0\u00a0\u00a0\u00a0\u00a0<\/strong>Mnafanya nini leo tena Bimphi, Jacob, na wewe bibi?<\/p>\n<p><strong>Bimphi:<\/strong>\u00a0Kwa nini unauliza swali kama hilo wakati unaona kuwa tunamwagia maji mimea?\u00a0 Na kwa nini unauliza ni lini tunamwagia maji?\u00a0 Hukutuuliza maswali kama hayo tulipokuwa tunatengeneza mitaro na kufyeka vichaka.<\/p>\n<p><strong>FX:<\/strong>\u00a0<em>Sauti ya kibao<\/em><\/p>\n<p><strong>Bimphi:<\/strong>\u00a0(<em>Kwa hasira)<\/em>\u00a0Umenichapa kibao!\u00a0 Umenichapa kibao!&#8230;kwa nini?\u00a0 Kwa nini?&#8230;Siendi ng\u2019o.<br \/>\n<strong>James:<\/strong>\u00a0\u00a0\u00a0\u00a0\u00a0\u00a0\u00a0\u00a0\u00a0\u00a0\u00a0 (<em>Kwa hasira<\/em>) Kwa nini wewe daima unakuwa mkorofi?\u00a0 Ndiyo sababu ya kukuzaba kibao\u2026. Sasa ondoka shambani.<\/p>\n<p><strong>Jacob:<\/strong>\u00a0Hapana James, usituchape \u2013 tutaondoka mara moja.\u00a0 Tunajua wewe ni hodari kwa vita.<\/p>\n<p><strong>Bimphi:<\/strong>\u00a0Mimi siondoki.<\/p>\n<p><strong>FX:<\/strong>\u00a0<em>Sauti ya vibao zaidi.\u00a0<\/em><\/p>\n<p><strong>Bimphi:<\/strong>\u00a0Basi! Basi!\u00a0 Tunaondoka.<\/p>\n<p><strong>James:\u00a0\u00a0\u00a0\u00a0\u00a0\u00a0\u00a0\u00a0\u00a0\u00a0\u00a0\u00a0<\/strong>Muna hiari kwenda kuripoti haya kwa mkuu wa kijiji &#8211;\u00a0 mimi sijali. Kama tunatangulia kufika hapa, na mpate tunamwagia mimea maji, kamwe msianze kumwagia yenu.\u00a0 La sivyo, nitawatia adabu.<\/p>\n<p><strong>German:<\/strong>\u00a0Kuna nini, James?<\/p>\n<p><strong>James:\u00a0\u00a0\u00a0\u00a0\u00a0\u00a0\u00a0\u00a0\u00a0\u00a0\u00a0\u00a0<\/strong>Kimya, German \u2026 Huenda nikasahau kuwa wewe ni rafiki yangu.\u00a0 (<em>Kwa Eda) \u00a0<\/em>Eda, ondoka. (<em>Kimya)\u00a0<\/em>Unafikiri ni mzaha?\u00a0 Ondokeni mrejee baadaye.\u00a0 Ama kunaye anayetaka kibao?<\/p>\n<p><strong>Eda:\u00a0<\/strong>Tafadhali niruhusu nimwagie maji mahindi yangu angalau kwa leo tu.\u00a0 Si unaona yanakauka?<\/p>\n<p><strong>James:\u00a0\u00a0\u00a0\u00a0\u00a0\u00a0\u00a0\u00a0\u00a0\u00a0\u00a0\u00a0<\/strong>Tuliwaambia jana kuwa inategemea anayetangulia.\u00a0 Ulikuwa wapi?\u00a0 Ama ulizidisha usingizi kwa kuwa wewe ni mchawi?<\/p>\n<p><strong>Eda:\u00a0<\/strong>(<em>Akilia<\/em>) Msiongee hivyo wanangu.<\/p>\n<p><strong>James:\u00a0\u00a0\u00a0\u00a0\u00a0\u00a0\u00a0\u00a0\u00a0\u00a0\u00a0\u00a0<\/strong>Mimi si mwanao..<\/p>\n<p><strong>Eda:\u00a0<\/strong>Wewe si wa rika langu.\u00a0 Unastahili kunipa heshima.\u00a0 Wewe ni rika la mjukuu wangu.<\/p>\n<p><strong>James:\u00a0\u00a0\u00a0\u00a0\u00a0\u00a0\u00a0\u00a0\u00a0\u00a0\u00a0\u00a0<\/strong>Sisemi usirudi.\u00a0 Nasema ungojee nimalize.\u00a0 Nina haki pia.<\/p>\n<p><strong>Eda:<\/strong>\u00a0(<em>Kwa kwikwi<\/em>) Jana ulinikataza, leo vile vile.\u00a0 Hata umempiga Bimphi leo.\u00a0 Ah, mwanangu, usifanye hivyo.<\/p>\n<p><strong>German:\u00a0<\/strong>James, mwache tu amwagie.\u00a0 Tutaendelea baadaye.<\/p>\n<p><strong>Eda:\u00a0<\/strong>Eee, mwanangu.\u00a0 Tafadhali msihi rafiki yako.\u00a0 Unajua kuwa nachelewa kuamka kwa kuwa mwili huniuma; si unaelewa kuwa mimi ni mzee?.<\/p>\n<p><strong>James:<\/strong>\u00a0\u00a0\u00a0\u00a0\u00a0\u00a0\u00a0\u00a0\u00a0\u00a0\u00a0 Hata, nina kazi nyingine, German\u2026.\u00a0 Kwa hivyo Eda, unajua kuwa nikisema acha, nina maana kuwa uache!\u00a0 Sitaki fujo yo yote hapa..<\/p>\n<p><strong>Eda:\u00a0<\/strong>(<em>Analia kwa kwikwi<\/em>) Mwanangu, kwa nini ulikufa mapema hivi na kuniacha hai?\u00a0 Kwa nini ulinipa chakula ukajinyima na kufa wewe, badala ya kuniacha mie mzee, nife njaa.<\/p>\n<p><strong>German:\u00a0<\/strong>Bibi, enda.\u00a0 Nitamwaga maji shambani mwako nikimaliza kwangu.<\/p>\n<p><strong>Eda:\u00a0<\/strong>Asante mwanangu.<\/p>\n<p><em>Mpito wa jukwaa<\/em><\/p>\n<p><strong>FX:<\/strong>\u00a0<em>Eda analia kwa kwikwi<\/em><\/p>\n<p><strong>Mkuu wa kijiji:\u00a0<\/strong>Eda, kwa nini unalia?<\/p>\n<p><strong>Eda:<\/strong>\u00a0Chifu, mpwao James alinikataza kumwagia maji mimea yangu, jana na hata leo.\u00a0 Hata amechapa Bimphi vibao.<\/p>\n<p><strong>Village headman:\u00a0<\/strong>James? \u00a0Kwa nini?<\/p>\n<p><strong>Eda:<\/strong>\u00a0Anasema alitangulia kufika.\u00a0 Tunapomwaga maji sote, hayafiki shambani mwake.<\/p>\n<p><strong>Mkuu wa kijiji:\u00a0<\/strong>Usiwe na wasiwasi.\u00a0 Mpwa wangu huyo ni kichaa.\u00a0 Wewe rejea baadaye umwagie mimea yako maji\u2026.German hakukusaidia?<\/p>\n<p><strong>Eda:\u00a0<\/strong>Tayari amenisaidia.\u00a0 Aliahidi kumwaga maji shamabani mwangu<\/p>\n<p><strong>Chief:<\/strong>\u00a0Sawa.<\/p>\n<p><em>Mpito wa jukwaa<\/em><\/p>\n<p><strong>Bimphi:\u00a0<\/strong>Mkuu wa kijiji, hebu tuambie ni kwa nini watu fulani pekee ndio wanamwagia maji mimea yao kila siku, ilhali sote tulishiriki kuchimba mitaro and kufyeka vichaka?<\/p>\n<p><strong>Mkuu wa kijiji:\u00a0<\/strong>Naomba usimulie yote.\u00a0 Nini kilitendeka?<\/p>\n<p><strong>Bimphi:<\/strong>\u00a0James anadai kuwa yeye huamka mapema na hivyo huwahi kufika shambani kila siku.\u00a0 Hii ndiyo sababu anataka tusubiri amalize kabla hatujamwaga maji kwetu.<\/p>\n<p><strong>Mkuu wa kijiji:<\/strong>\u00a0Ah, kumbe.\u00a0 Kama ni hivyo, ana haki.\u00a0 Kwa nini usiamke mapema, hata kabla yake?<\/p>\n<p><strong>Bimphi:<\/strong>\u00a0Mimi naweza, lakini Eda je, mwanamke mzee ambaye anakatazwa kumwaga maji kwa sababu hiyo hiyo ya aliyetangulia anufaike kwanza?<\/p>\n<p><strong>Mkuu wa kijiji:<\/strong>\u00a0Nifanye nini kama wanaamka mapema kila asubuhi?<\/p>\n<p><strong>Bimphi:\u00a0<\/strong>Kwa nini wanahitaji kumwagia mahindi kila siku?\u00a0 Hawawezi kutuachia nafasi na sisi tukamwagia mara kwa mara?<\/p>\n<p><strong>Mkuu wa kijiji:<\/strong>\u00a0Mbona usimuulize?<\/p>\n<p><strong>Bimphi:<\/strong>\u00a0Kwa nini usimuulize kwa niaba yetu?\u00a0 Tayari tumeshazambwa vibao na unasema\u2026. (<em>kwa hasira hivi kwamba anashindwa kusema vizuri)\u00a0<\/em>ni\u2026 mm ..wuu..lize?\u00a0 Kumbuka tulishiriki wote kuchimba mtaro na kufyeka vichaka.\u00a0 Haya mambo ya aliyetangulia anufaike kwanza yametokea lini?<\/p>\n<p><strong>Mkuu wa kijiji:\u00a0<\/strong>Huwa sijibu maswali ya kijinga mimi.<\/p>\n<p><strong>Bimphi:<\/strong>\u00a0(<em>Kwa hasira)<\/em>\u00a0Kama hakutakuwa na suluhisho ifikapo mwisho wa juma hili, nitatenda kitendo.\u00a0 Nitaharibu mtaro na itabidi uanze upya.\u00a0 Nilikuwa mshiriki katika mradi wote huo.\u00a0 Ukiwahi, utatangulia kitu gani?<\/p>\n<p><strong>Mkuu wa kijiji:\u00a0<\/strong>Usithubutu kuharibu mtaro.\u00a0 Ukifanya hivyo nitakufukuza kutoka kijijini mwangu.<\/p>\n<p><strong>Bimphi:\u00a0<\/strong>Hautathubutu.\u00a0 Nitakushtaki wewe kwa Mkuu wa Wilaya aliyetupatia ardhi ile.<\/p>\n<p><strong>Mkuu wa kijiji:\u00a0<\/strong>Wewe, usijaribu kufika huko.\u00a0 Unafikiri ninaweza kufanya nini kumkomesha James asiyakalie maji kwa kuwa yeye huwahi kuamka?<\/p>\n<p><strong>Bimphi:\u00a0<\/strong>Ita baraza ya kijiji kizima.\u00a0 Ulituita wakati wa kuanzisha mradi wa unyunyiziaji maji.\u00a0 Kwa nini usiite watu wote tena?\u00a0 Bwana DC atafikiwa na haya bila shaka.<\/p>\n<p><em>Wimbo wa mpito wa jukwaa<\/em><\/p>\n<p><strong>Msimulizi:\u00a0<\/strong>Mkuu wa kijiji anajua kuwa Bwana DC atamtimua kama mkuu wa kijiji.\u00a0 Mkuu wa kijiji atafanya nini kuzuia Bimphi kuharibu mitaro na kumshtaki kwa Bwana DC?<\/p>\n<p><strong>FX:<\/strong>\u00a0<em>Sauti ya kengele.<\/em><\/p>\n<p><strong>Boy:\u00a0<\/strong>(<em>Kwa sauti iliyopaazwa<\/em>) Mkuu wa kijiji anawaita nyote.\u00a0 Tukutane kwenye mradi wa kunyunyizia maji mashambani kesho asubuhi.\u00a0 Kaeni kwa utulivu.<\/p>\n<p><em>Sauti ya kengele<\/em><\/p>\n<p><em>Wimbo wa mpito wa jukwaa.<\/em><\/p>\n<p><strong>Msimulizi:<\/strong>\u00a0Mkuu wa kijiji atawaambiaje watu wale?\u00a0 Atawaambia vipi?\u00a0\u00a0 Je, kuna suluhisho rahisi hapa?<\/p>\n<p><strong>FX:\u00a0<\/strong><em>Umati wa watu ukiongea<\/em><\/p>\n<p><strong>German:\u00a0<\/strong>Kimya tafadhali!\u00a0 Kimya!\u00a0 Naomba tumsikilize mkuu wa kijiji Bwana Tiopazi, shujaa wetu.<\/p>\n<p><strong>Mkuu wa kijiji:\u00a0<\/strong>Jamani watu wetu.\u00a0 Naomba mwenyekiti wa mradi huu wa kunyunyizia maji aje asimame na mimi hapa.<\/p>\n<p><strong>Bimphi:\u00a0<\/strong>Tulidhani wewe ndiye mwenyekiti.<\/p>\n<p><strong>Mkuu wa kijiji:\u00a0<\/strong>Mimi! Nimeshawahi kusema hivyo?<\/p>\n<p><strong>Umati:\u00a0<\/strong>Hapana, hapana!<\/p>\n<p><strong>Mkuu wa kijiji:\u00a0<\/strong>Kwa hivyo, namtaka kiongozi wa mradi huu wa kunyunyizia maji.\u00a0 German, ni nani mwenyekiti?<\/p>\n<p><strong>German:\u00a0<\/strong>Hamna bwana.<\/p>\n<p><strong>Mkuu wa kijiji:\u00a0<\/strong>Itakuwaje kitu kisicho na kichwa kisonge mbele?\u00a0 Nitakuwa msimamizi.\u00a0 Hebu tumchague mwenyekiti leo.\u00a0 Nipeni majina manne, tafadhalini, ya watu wanaoweza kuwa mwenyekiti.<\/p>\n<p><strong>Umati:\u00a0<\/strong>German. German Banda, tafadhalini.<\/p>\n<p><strong>Mkuu wa kijiji:\u00a0<\/strong>Mnakubaliana nyote?<\/p>\n<p><strong>Umati:\u00a0<\/strong>Ndio.<\/p>\n<p><strong>Mkuu wa kijiji:\u00a0<\/strong>German, wewe sasa ndiye kiongozi wa mradi huu wa unyunyiziaji maji mashambani.\u00a0 Kabla hatujachagua maofisa wengine katika mradi huu, niambie jinsi utakavyogawa maji kwa njia ya haki kwa wote, wakiwemo watoto na wazee.<\/p>\n<p><strong>German:\u00a0<\/strong>Nitatoa tu mapendekezo, lakini mnaweza kunipa ushauri tofauti.\u00a0 Ikiwa hampendezwi na mapendekezo yangu, mniambie.<\/p>\n<p><strong>Umati:\u00a0<\/strong>Ndio.<\/p>\n<p><strong>Bimphi:\u00a0<\/strong>German, tunajua kuwa unatupenda sote, na huwezi kutudhuru.\u00a0 Unaonaje?<\/p>\n<p><strong>German:\u00a0<\/strong>Mwanzo, naomba msamaha kwa yote ambaye huenda nilimwuudhi.<\/p>\n<p><strong>Bimphi:\u00a0<\/strong>Wewe tuambie tu suluhisho ni nini.<\/p>\n<p><strong>German:<\/strong>\u00a0Suala la bibi yetu Eda linanisumbua\u2026 Lakini nafikiri tunapaswa kujigawa katika makundi na kutumia maji katika siku tofauti kulingana na makundi hayo.<\/p>\n<p><strong>Umati:\u00a0<\/strong>Ndio! German! German!<br \/>\n<strong>Mkuu wa kijiji:\u00a0<\/strong>Naam mwanangu.\u00a0 Sasa natuchague maofisa wengine ambao watakusaidia kutekeleza mpango huo.<\/p>\n<p><em>Mpito wa jukwaa<\/em><\/p>\n<p><strong>Msimulizi:\u00a0<\/strong>Je, unadhani matatizo ya ulafi katika matumizi ya maji yaliendelea?\u00a0 La, tatizo la ugavi wa maji lilifika hapo.\u00a0 Kila mtu alinufaika na akawa na usalama wa chakula.\u00a0 Umoja ni nguvu.\u00a0 Usingojee walevi kukushtua ili utekeleze yanayotakikana na kugawa maji kwa usawa.\u00a0 Maji ni uhai.<\/p>\n","protected":false},"excerpt":{"rendered":"<p>Wahusika\u00a0 German: Mtu mwenye busara na moyo safi katika kijiji Mkuu wa Kijiji: Mwenye busara lakini menye unyonge mara kwa mara. Eda: Mwanamke mzee, mjane, anawalea mayatima walioachwa na mwanawe wa kiume\u00a0aliyefariki aliyefariki njaa. Bimphi: Mlevi wa kawaida.\u00a0 Mwenye bidii, lakini anayetumia pesa zake nyingi kulewa pombe. James:\u00a0 Mpwa wa Mkuu wa Kijiji, mgumu wa&hellip;<\/p>\n","protected":false},"author":142,"featured_media":0,"parent":0,"menu_order":6,"template":"","meta":{"footnotes":"","beyondwords_generate_audio":"","beyondwords_project_id":"","beyondwords_content_id":"","beyondwords_integration_method":"","beyondwords_language_code":"","beyondwords_language_id":"","beyondwords_body_voice_id":"","beyondwords_delete_content":"","beyondwords_source":"","beyondwords_output":"","beyondwords_script_template_id":"","beyondwords_video_template_id":"","beyondwords_video_size":"","beyondwords_embed":"","beyondwords_podcast_id":"","speechkit_generate_audio":"","speechkit_project_id":"","speechkit_podcast_id":""},"script-format":[537],"package":[634],"script-category":[],"class_list":["post-4248","radio-script","type-radio-script","status-publish","hentry","script-format-maigizo","package-634"],"acf":[],"yoast_head":"<!-- This site is optimized with the Yoast SEO plugin v28.3 - https:\/\/yoast.com\/product\/yoast-seo-wordpress\/ -->\n<title>Maji ni uhai. Yagawe. - Farm Radio International<\/title>\n<meta name=\"robots\" content=\"index, follow, max-snippet:-1, max-image-preview:large, max-video-preview:-1\" \/>\n<link rel=\"canonical\" href=\"https:\/\/scripts.farmradio.fm\/sw\/mwongozo-wa-redio\/maji-ni-uhai-yagawe\/\" \/>\n<meta property=\"og:locale\" content=\"en_US\" \/>\n<meta property=\"og:type\" content=\"article\" \/>\n<meta property=\"og:title\" content=\"Maji ni uhai. Yagawe. - Farm Radio International\" \/>\n<meta property=\"og:description\" content=\"Wahusika\u00a0 German: Mtu mwenye busara na moyo safi katika kijiji Mkuu wa Kijiji: Mwenye busara lakini menye unyonge mara kwa mara. Eda: Mwanamke mzee, mjane, anawalea mayatima walioachwa na mwanawe wa kiume\u00a0aliyefariki aliyefariki njaa. Bimphi: Mlevi wa kawaida.\u00a0 Mwenye bidii, lakini anayetumia pesa zake nyingi kulewa pombe. James:\u00a0 Mpwa wa Mkuu wa Kijiji, mgumu wa&hellip;\" \/>\n<meta property=\"og:url\" content=\"https:\/\/scripts.farmradio.fm\/sw\/mwongozo-wa-redio\/maji-ni-uhai-yagawe\/\" \/>\n<meta property=\"og:site_name\" content=\"Farm Radio International\" \/>\n<meta property=\"article:publisher\" content=\"https:\/\/www.facebook.com\/farmradio\/\" \/>\n<meta property=\"article:modified_time\" content=\"2016-02-22T02:29:57+00:00\" \/>\n<meta name=\"twitter:card\" content=\"summary_large_image\" \/>\n<meta name=\"twitter:site\" content=\"@farmradio\" \/>\n<meta name=\"twitter:label1\" content=\"Est. reading time\" \/>\n\t<meta name=\"twitter:data1\" content=\"12 minutes\" \/>\n<script type=\"application\/ld+json\" class=\"yoast-schema-graph\">{\"@context\":\"https:\\\/\\\/schema.org\",\"@graph\":[{\"@type\":\"Article\",\"@id\":\"https:\\\/\\\/scripts.farmradio.fm\\\/sw\\\/mwongozo-wa-redio\\\/maji-ni-uhai-yagawe\\\/#article\",\"isPartOf\":{\"@id\":\"https:\\\/\\\/scripts.farmradio.fm\\\/sw\\\/mwongozo-wa-redio\\\/maji-ni-uhai-yagawe\\\/\"},\"author\":{\"name\":\"Farm Radio International\",\"@id\":\"http:\\\/\\\/scripts.farmradio.fm\\\/sw\\\/#\\\/schema\\\/person\\\/abc034e69b53cb6ac441ffa927f22648\"},\"headline\":\"Maji ni uhai. Yagawe.\",\"datePublished\":\"2010-11-01T10:17:41+00:00\",\"dateModified\":\"2016-02-22T02:29:57+00:00\",\"mainEntityOfPage\":{\"@id\":\"https:\\\/\\\/scripts.farmradio.fm\\\/sw\\\/mwongozo-wa-redio\\\/maji-ni-uhai-yagawe\\\/\"},\"wordCount\":2367,\"publisher\":{\"@id\":\"http:\\\/\\\/scripts.farmradio.fm\\\/sw\\\/#organization\"},\"inLanguage\":\"sw-CG\"},{\"@type\":\"WebPage\",\"@id\":\"https:\\\/\\\/scripts.farmradio.fm\\\/sw\\\/mwongozo-wa-redio\\\/maji-ni-uhai-yagawe\\\/\",\"url\":\"https:\\\/\\\/scripts.farmradio.fm\\\/sw\\\/mwongozo-wa-redio\\\/maji-ni-uhai-yagawe\\\/\",\"name\":\"Maji ni uhai. Yagawe. - Farm Radio International\",\"isPartOf\":{\"@id\":\"http:\\\/\\\/scripts.farmradio.fm\\\/sw\\\/#website\"},\"datePublished\":\"2010-11-01T10:17:41+00:00\",\"dateModified\":\"2016-02-22T02:29:57+00:00\",\"breadcrumb\":{\"@id\":\"https:\\\/\\\/scripts.farmradio.fm\\\/sw\\\/mwongozo-wa-redio\\\/maji-ni-uhai-yagawe\\\/#breadcrumb\"},\"inLanguage\":\"sw-CG\",\"potentialAction\":[{\"@type\":\"ReadAction\",\"target\":[\"https:\\\/\\\/scripts.farmradio.fm\\\/sw\\\/mwongozo-wa-redio\\\/maji-ni-uhai-yagawe\\\/\"]}]},{\"@type\":\"BreadcrumbList\",\"@id\":\"https:\\\/\\\/scripts.farmradio.fm\\\/sw\\\/mwongozo-wa-redio\\\/maji-ni-uhai-yagawe\\\/#breadcrumb\",\"itemListElement\":[{\"@type\":\"ListItem\",\"position\":1,\"name\":\"Nyumbani\",\"item\":\"http:\\\/\\\/scripts.farmradio.fm\\\/sw\\\/\"},{\"@type\":\"ListItem\",\"position\":2,\"name\":\"Maigizo\",\"item\":\"https:\\\/\\\/scripts.farmradio.fm\\\/sw\\\/mwongozo-wa-muundo\\\/maigizo\\\/\"},{\"@type\":\"ListItem\",\"position\":3,\"name\":\"Maji ni uhai. Yagawe.\"}]},{\"@type\":\"WebSite\",\"@id\":\"http:\\\/\\\/scripts.farmradio.fm\\\/sw\\\/#website\",\"url\":\"http:\\\/\\\/scripts.farmradio.fm\\\/sw\\\/\",\"name\":\"Farm Radio International\",\"description\":\"Sharing knowledge, giving voice.\",\"publisher\":{\"@id\":\"http:\\\/\\\/scripts.farmradio.fm\\\/sw\\\/#organization\"},\"potentialAction\":[{\"@type\":\"SearchAction\",\"target\":{\"@type\":\"EntryPoint\",\"urlTemplate\":\"http:\\\/\\\/scripts.farmradio.fm\\\/sw\\\/?s={search_term_string}\"},\"query-input\":{\"@type\":\"PropertyValueSpecification\",\"valueRequired\":true,\"valueName\":\"search_term_string\"}}],\"inLanguage\":\"sw-CG\"},{\"@type\":\"Organization\",\"@id\":\"http:\\\/\\\/scripts.farmradio.fm\\\/sw\\\/#organization\",\"name\":\"Farm Radio International\",\"url\":\"http:\\\/\\\/scripts.farmradio.fm\\\/sw\\\/\",\"logo\":{\"@type\":\"ImageObject\",\"inLanguage\":\"sw-CG\",\"@id\":\"http:\\\/\\\/scripts.farmradio.fm\\\/sw\\\/#\\\/schema\\\/logo\\\/image\\\/\",\"url\":\"https:\\\/\\\/scripts.farmradio.fm\\\/wp-content\\\/uploads\\\/farmRadioLogo.jpg\",\"contentUrl\":\"https:\\\/\\\/scripts.farmradio.fm\\\/wp-content\\\/uploads\\\/farmRadioLogo.jpg\",\"width\":200,\"height\":75,\"caption\":\"Farm Radio International\"},\"image\":{\"@id\":\"http:\\\/\\\/scripts.farmradio.fm\\\/sw\\\/#\\\/schema\\\/logo\\\/image\\\/\"},\"sameAs\":[\"https:\\\/\\\/www.facebook.com\\\/farmradio\\\/\",\"https:\\\/\\\/x.com\\\/farmradio\",\"https:\\\/\\\/www.instagram.com\\\/farmradio\\\/\",\"https:\\\/\\\/www.youtube.com\\\/user\\\/FarmRadioInt\"]},{\"@type\":\"Person\",\"@id\":\"http:\\\/\\\/scripts.farmradio.fm\\\/sw\\\/#\\\/schema\\\/person\\\/abc034e69b53cb6ac441ffa927f22648\",\"name\":\"Farm Radio International\",\"image\":{\"@type\":\"ImageObject\",\"inLanguage\":\"sw-CG\",\"@id\":\"https:\\\/\\\/secure.gravatar.com\\\/avatar\\\/493231adf65be6b99ae1dc0dfb13ccca3d412c29f85aa9727be6190faa6293cd?s=96&d=mm&r=g\",\"url\":\"https:\\\/\\\/secure.gravatar.com\\\/avatar\\\/493231adf65be6b99ae1dc0dfb13ccca3d412c29f85aa9727be6190faa6293cd?s=96&d=mm&r=g\",\"contentUrl\":\"https:\\\/\\\/secure.gravatar.com\\\/avatar\\\/493231adf65be6b99ae1dc0dfb13ccca3d412c29f85aa9727be6190faa6293cd?s=96&d=mm&r=g\",\"caption\":\"Farm Radio International\"},\"sameAs\":[\"http:\\\/\\\/frrp.wpengine.com\"]}]}<\/script>\n<!-- \/ Yoast SEO plugin. -->","yoast_head_json":{"title":"Maji ni uhai. Yagawe. - Farm Radio International","robots":{"index":"index","follow":"follow","max-snippet":"max-snippet:-1","max-image-preview":"max-image-preview:large","max-video-preview":"max-video-preview:-1"},"canonical":"https:\/\/scripts.farmradio.fm\/sw\/mwongozo-wa-redio\/maji-ni-uhai-yagawe\/","og_locale":"en_US","og_type":"article","og_title":"Maji ni uhai. Yagawe. - Farm Radio International","og_description":"Wahusika\u00a0 German: Mtu mwenye busara na moyo safi katika kijiji Mkuu wa Kijiji: Mwenye busara lakini menye unyonge mara kwa mara. Eda: Mwanamke mzee, mjane, anawalea mayatima walioachwa na mwanawe wa kiume\u00a0aliyefariki aliyefariki njaa. Bimphi: Mlevi wa kawaida.\u00a0 Mwenye bidii, lakini anayetumia pesa zake nyingi kulewa pombe. James:\u00a0 Mpwa wa Mkuu wa Kijiji, mgumu wa&hellip;","og_url":"https:\/\/scripts.farmradio.fm\/sw\/mwongozo-wa-redio\/maji-ni-uhai-yagawe\/","og_site_name":"Farm Radio International","article_publisher":"https:\/\/www.facebook.com\/farmradio\/","article_modified_time":"2016-02-22T02:29:57+00:00","twitter_card":"summary_large_image","twitter_site":"@farmradio","twitter_misc":{"Est. reading time":"12 minutes"},"schema":{"@context":"https:\/\/schema.org","@graph":[{"@type":"Article","@id":"https:\/\/scripts.farmradio.fm\/sw\/mwongozo-wa-redio\/maji-ni-uhai-yagawe\/#article","isPartOf":{"@id":"https:\/\/scripts.farmradio.fm\/sw\/mwongozo-wa-redio\/maji-ni-uhai-yagawe\/"},"author":{"name":"Farm Radio International","@id":"http:\/\/scripts.farmradio.fm\/sw\/#\/schema\/person\/abc034e69b53cb6ac441ffa927f22648"},"headline":"Maji ni uhai. Yagawe.","datePublished":"2010-11-01T10:17:41+00:00","dateModified":"2016-02-22T02:29:57+00:00","mainEntityOfPage":{"@id":"https:\/\/scripts.farmradio.fm\/sw\/mwongozo-wa-redio\/maji-ni-uhai-yagawe\/"},"wordCount":2367,"publisher":{"@id":"http:\/\/scripts.farmradio.fm\/sw\/#organization"},"inLanguage":"sw-CG"},{"@type":"WebPage","@id":"https:\/\/scripts.farmradio.fm\/sw\/mwongozo-wa-redio\/maji-ni-uhai-yagawe\/","url":"https:\/\/scripts.farmradio.fm\/sw\/mwongozo-wa-redio\/maji-ni-uhai-yagawe\/","name":"Maji ni uhai. Yagawe. - Farm Radio International","isPartOf":{"@id":"http:\/\/scripts.farmradio.fm\/sw\/#website"},"datePublished":"2010-11-01T10:17:41+00:00","dateModified":"2016-02-22T02:29:57+00:00","breadcrumb":{"@id":"https:\/\/scripts.farmradio.fm\/sw\/mwongozo-wa-redio\/maji-ni-uhai-yagawe\/#breadcrumb"},"inLanguage":"sw-CG","potentialAction":[{"@type":"ReadAction","target":["https:\/\/scripts.farmradio.fm\/sw\/mwongozo-wa-redio\/maji-ni-uhai-yagawe\/"]}]},{"@type":"BreadcrumbList","@id":"https:\/\/scripts.farmradio.fm\/sw\/mwongozo-wa-redio\/maji-ni-uhai-yagawe\/#breadcrumb","itemListElement":[{"@type":"ListItem","position":1,"name":"Nyumbani","item":"http:\/\/scripts.farmradio.fm\/sw\/"},{"@type":"ListItem","position":2,"name":"Maigizo","item":"https:\/\/scripts.farmradio.fm\/sw\/mwongozo-wa-muundo\/maigizo\/"},{"@type":"ListItem","position":3,"name":"Maji ni uhai. Yagawe."}]},{"@type":"WebSite","@id":"http:\/\/scripts.farmradio.fm\/sw\/#website","url":"http:\/\/scripts.farmradio.fm\/sw\/","name":"Farm Radio International","description":"Sharing knowledge, giving voice.","publisher":{"@id":"http:\/\/scripts.farmradio.fm\/sw\/#organization"},"potentialAction":[{"@type":"SearchAction","target":{"@type":"EntryPoint","urlTemplate":"http:\/\/scripts.farmradio.fm\/sw\/?s={search_term_string}"},"query-input":{"@type":"PropertyValueSpecification","valueRequired":true,"valueName":"search_term_string"}}],"inLanguage":"sw-CG"},{"@type":"Organization","@id":"http:\/\/scripts.farmradio.fm\/sw\/#organization","name":"Farm Radio International","url":"http:\/\/scripts.farmradio.fm\/sw\/","logo":{"@type":"ImageObject","inLanguage":"sw-CG","@id":"http:\/\/scripts.farmradio.fm\/sw\/#\/schema\/logo\/image\/","url":"https:\/\/scripts.farmradio.fm\/wp-content\/uploads\/farmRadioLogo.jpg","contentUrl":"https:\/\/scripts.farmradio.fm\/wp-content\/uploads\/farmRadioLogo.jpg","width":200,"height":75,"caption":"Farm Radio International"},"image":{"@id":"http:\/\/scripts.farmradio.fm\/sw\/#\/schema\/logo\/image\/"},"sameAs":["https:\/\/www.facebook.com\/farmradio\/","https:\/\/x.com\/farmradio","https:\/\/www.instagram.com\/farmradio\/","https:\/\/www.youtube.com\/user\/FarmRadioInt"]},{"@type":"Person","@id":"http:\/\/scripts.farmradio.fm\/sw\/#\/schema\/person\/abc034e69b53cb6ac441ffa927f22648","name":"Farm Radio International","image":{"@type":"ImageObject","inLanguage":"sw-CG","@id":"https:\/\/secure.gravatar.com\/avatar\/493231adf65be6b99ae1dc0dfb13ccca3d412c29f85aa9727be6190faa6293cd?s=96&d=mm&r=g","url":"https:\/\/secure.gravatar.com\/avatar\/493231adf65be6b99ae1dc0dfb13ccca3d412c29f85aa9727be6190faa6293cd?s=96&d=mm&r=g","contentUrl":"https:\/\/secure.gravatar.com\/avatar\/493231adf65be6b99ae1dc0dfb13ccca3d412c29f85aa9727be6190faa6293cd?s=96&d=mm&r=g","caption":"Farm Radio International"},"sameAs":["http:\/\/frrp.wpengine.com"]}]}},"_links":{"self":[{"href":"https:\/\/scripts.farmradio.fm\/sw\/wp-json\/wp\/v2\/radio-script\/4248","targetHints":{"allow":["GET"]}}],"collection":[{"href":"https:\/\/scripts.farmradio.fm\/sw\/wp-json\/wp\/v2\/radio-script"}],"about":[{"href":"https:\/\/scripts.farmradio.fm\/sw\/wp-json\/wp\/v2\/types\/radio-script"}],"author":[{"embeddable":true,"href":"https:\/\/scripts.farmradio.fm\/sw\/wp-json\/wp\/v2\/users\/142"}],"version-history":[{"count":0,"href":"https:\/\/scripts.farmradio.fm\/sw\/wp-json\/wp\/v2\/radio-script\/4248\/revisions"}],"wp:attachment":[{"href":"https:\/\/scripts.farmradio.fm\/sw\/wp-json\/wp\/v2\/media?parent=4248"}],"wp:term":[{"taxonomy":"script-format","embeddable":true,"href":"https:\/\/scripts.farmradio.fm\/sw\/wp-json\/wp\/v2\/script-format?post=4248"},{"taxonomy":"package","embeddable":true,"href":"https:\/\/scripts.farmradio.fm\/sw\/wp-json\/wp\/v2\/package?post=4248"},{"taxonomy":"script-category","embeddable":true,"href":"https:\/\/scripts.farmradio.fm\/sw\/wp-json\/wp\/v2\/script-category?post=4248"}],"curies":[{"name":"wp","href":"https:\/\/api.w.org\/{rel}","templated":true}]}}