{"id":41887,"date":"2024-01-11T19:47:52","date_gmt":"2024-01-11T16:47:52","guid":{"rendered":"https:\/\/scripts.farmradio.fm\/?post_type=radio-script&#038;p=41887"},"modified":"2024-12-02T18:29:21","modified_gmt":"2024-12-02T15:29:21","slug":"ufugaji-wa-nyuki-unawanufaisha-wakulima-huku-ukihifadhi-mazingira","status":"publish","type":"radio-script","link":"https:\/\/scripts.farmradio.fm\/sw\/mwongozo-wa-redio\/ufugaji-wa-nyuki-unawanufaisha-wakulima-huku-ukihifadhi-mazingira\/","title":{"rendered":"Ufugaji wa nyuki unawanufaisha wakulima huku ukihifadhi mazingira"},"content":{"rendered":"<p>SAUTI YA UTAMBULISHO Ipandishwe juu KISHA ISHUshe TARATIBU<\/p>\n<p><strong>MTANGAZAJI:<\/strong>\u00a0\u00a0\u00a0\u00a0\u00a0\u00a0\u00a0\u00a0\u00a0\u00a0\u00a0\u00a0\u00a0\u00a0\u00a0\u00a0\u00a0\u00a0\u00a0\u00a0\u00a0\u00a0\u00a0\u00a0\u00a0\u00a0\u00a0\u00a0\u00a0\u00a0 Habari, wasikilizaji wapendwa. Karibu kwenye programu yako. Jina langu ni Solange Bicaba.<\/p>\n<p>Leo, tutazungumzia kuhusu kazi ya ufugaji nyuki na manufaa yake kwa watu na mazingira huko Yabasso, kijiji kilichoko katika mkoa wa Hauts-Bassins magharibi mwa nchi ya Burkina Faso. Katika kijiji hiki, takriban watu thelathini katika ushirika wamekuwa wakifanya ufugaji nyuki wa kisasa tangu mwaka 2018 baada ya kupokea mafunzo kutoka kwa Fonds d&#8217;Intervention pour l&#8217;Environnement, au FIE.<\/p>\n<p>Hii imeleta mabadiliko katika hali zao za maisha. Ili kujua zaidi kuhusu manufaa yanayotokana na ufugaji nyuki, tulimhoji Yan Floran Millogo, mweka hazina wa Soci\u00e9t\u00e9 coop\u00e9rative simplifi\u00e9e des apiculteurs de Yabasso au Scoops-AY; Anselme Millogo, rais wa ushirika; pamoja na M\u00e8 Vincent Millogo na Sogodala P\u00e9lagie, wanachama wa ushirika huo. Pia tulizungumza na Naz\u00e9 Abdoulaye Konat\u00e9, Mkaguzi wa Maji na Misitu katika Kurugenzi ya Mazingira ya Mkoa wa Hauts-Bassins. Atazungumzia kuhusu mbinu bora za ufugaji nyuki zinazowanufaisha watu na bioanuwai.<\/p>\n<p>Sasa hebu tuwageukiwe wageni wetu.<\/p>\n<p>SAUTI YA UTAMBULISHO IPANDISHWE JUU KISHA ISHUSHE TARATIBU<\/p>\n<p><strong>MTANGAZAJI:<\/strong> \u00a0\u00a0\u00a0\u00a0\u00a0\u00a0\u00a0\u00a0\u00a0\u00a0\u00a0\u00a0\u00a0\u00a0\u00a0\u00a0\u00a0\u00a0\u00a0\u00a0\u00a0\u00a0\u00a0\u00a0\u00a0\u00a0\u00a0\u00a0\u00a0 Umekuwa ukifuga nyuki kwa miaka sita sasa, Bwana Millogo. Nini umefaidika nacho?<\/p>\n<p><strong>YAN FLORIAN MILLOGO: \u00a0\u00a0\u00a0\u00a0\u00a0\u00a0\u00a0\u00a0 <\/strong>Ufugaji wa nyuki si shughuli inayohitaji jitihada nyingi. Kinachohitajika ni kuweka mzinga na kuufuatilia. Nina mizinga 15 na huwa navuna mara tatu kwa mwaka. Uvunaji wa kwanza ni kutoka mwishoni mwa mwezi Februari hadi mwanzo wa mwezi Machi. Uvunaji wa pili ni kutoka mwishoni mwa mwezi Aprili hadi katikati ya mwezi Mei. Na uvunaji wa tatu, mara nyingi ni mwezi Novemba, inaitwa mavuno ya kusafisha kwa sababu inasafisha mzinga. Mavuno ya kwanza na ya pili huingiza kati ya elfu 200 na 300 za Cfaf (dola 320-390 za Marekani). Mapato kutoka mavuno ya tatu ni madogo sana ikilinganishwa na ya kwanza na ya pili kwasababu ubora wa asali sio mzuri. Mapato kutokana na ufugaji nyuki yameniwezesha kumaliza nyumba yangu na kuezeka kwa mabati 18. Kwa pesa hii, pia hununua pembejeo kwa ajili ya shughuli zangu za uzalishaji wangu wa kilimo.<\/p>\n<p><strong>MTANGAZAJI: <\/strong>\u00a0\u00a0\u00a0\u00a0\u00a0\u00a0\u00a0\u00a0\u00a0\u00a0\u00a0\u00a0\u00a0\u00a0\u00a0\u00a0\u00a0\u00a0\u00a0\u00a0\u00a0\u00a0\u00a0\u00a0\u00a0\u00a0\u00a0\u00a0\u00a0 Asante, Bw. Franck Xavier Millago. Bi. P\u00e9lagie Millago ana mizinga mitano yake mwenyewe. Karibu, na utuambie shughuli hii ina maana gani kwako.<\/p>\n<p><strong>PELAGIE MILLOGO: \u00a0\u00a0\u00a0\u00a0\u00a0\u00a0\u00a0\u00a0\u00a0\u00a0\u00a0\u00a0\u00a0\u00a0\u00a0\u00a0\u00a0\u00a0 <\/strong>Kwakuwa mimi ni mfugaji nyuki na mwanachama wa ushirika wa Scoops-AY, ninapokea sehemu yangu ya mapato ya ushirika, ambayo ni sawa na Cfaf 50 au 60 elfu Cfafa ($80-100 za Marekani) kwa kila mavuno. Kuhusu bidhaa za asali iliyosindikwa, kama vile nta na vinywaji, ninaweza kupokea Cfaf 30,000 ($50 za Marekani) kwa wiki, lakini ninaweza kupata zaidi au chini yah apo kwasababu soko si thabiti. Shukrani kwa ufugaji nyuki, tunaweza kuwalisha, kuwavisha na kuwasomesha watoto wetu. Sisi wanawake tunaweza kusherehekea hafla za kijamii kama ubatizo na harusi bila shida yoyote.<\/p>\n<p>Wanaume hutusaidia kuweka mizinga, kuitembelea, na kuvuna asali. Tunawaletea maji nyuki, tunatoa nta, kuchuja asali, na kuichakata kuwa katika hali ya kinywaji na juisi.<\/p>\n<p><strong>MTANGAZAJI: <\/strong>\u00a0\u00a0\u00a0\u00a0\u00a0\u00a0\u00a0\u00a0\u00a0\u00a0\u00a0\u00a0\u00a0\u00a0\u00a0\u00a0\u00a0\u00a0\u00a0\u00a0\u00a0\u00a0\u00a0\u00a0\u00a0\u00a0\u00a0\u00a0\u00a0 Faida nyingine ya ufugaji nyuki ni kwamba inatoa ajira kwa vijana na wanawake. Ili kuzungumzia hili, tunamkaribisha Bwana Vincent Millogo, ambaye si mfugaji wa nyuki tu bali pia ni mtunza kitalu.<\/p>\n<ol>\n<li><strong> VINCENT MILLOGO: <\/strong> Ndiyo, kama sehemu ya juhudi zetu za kukuza ufugaji nyuki, mradi wa FIE ulipendekeza tupande miche ya bustani kwa ajili ya upandaji wa miti. Mwaka huu, 2023, tulipanda miti 700 ya korosho. Hapo awali, baada ya mavuno ya kilimo, wakulima walikuwa hawana kazi ya kufanya kwa angalau miezi sita. Lakini sasa tupo bize na kuuza miche. Nina mizinga 18 ya nyuki ambayo inaniingizia takriban faranga 300,000 CFA (dola 500 za Marekani) kwa mwaka. Hii inaniwezesha kutunza familia yangu na kugharamia matibabu endapo kuna mgonjwa. Nimeweza kumpeleka kijana wangu wa kiume shule, na mwaka huu alifaulu mtihani wake wa shahada ya kwanza. Hii ni faida kwa familia nzima kwani barani Afrika, mtoto si mzaliwa wa wazazi wake tu, bali ni mali ya familia nzima.<\/li>\n<\/ol>\n<p><strong>MTANGAZAJI: \u00a0\u00a0\u00a0\u00a0\u00a0\u00a0\u00a0\u00a0\u00a0\u00a0\u00a0\u00a0\u00a0\u00a0\u00a0\u00a0\u00a0\u00a0\u00a0\u00a0\u00a0\u00a0\u00a0\u00a0\u00a0\u00a0\u00a0\u00a0\u00a0 <\/strong>Katika kijiji cha Yabasso, changamoto kadhaa zinakwamisha maendeleo ya ufugaji nyuki. Anselme Millogo, kama rais wa ushirika, ni zipi changamoto hizi?<\/p>\n<p><strong>ANSELME MILLOGO:<\/strong> \u00a0\u00a0\u00a0\u00a0\u00a0\u00a0\u00a0\u00a0\u00a0\u00a0\u00a0\u00a0\u00a0\u00a0\u00a0\u00a0 Kwanza kabisa, kijiji cha Yabasso kinazalisha angalau lita 1,600 za asali kila mwaka. Ushirika wetu una duka, lakini si kubwa na liko katika eneo ambalo sio zuri. Mkuu wa kijiji alitupatia kipande cha ardhi, lakini hatuna pesa za kujenga kwenye ardhi hiyo. Hatuna vifaa vinavyohitajika pia. Ukosefu wa vifaa unamaanisha, kwa mfano, kuwa nyuki mara nyingi huwaumiza sana wanawake wakati wa mchakato wa kuchuja asali. Shida nyingine ni kusimamia biashara ya asali. Watu hununua asali lakini huchukua muda mrefu kulipa wafugaji nyuki. Wafugaji wengine wanakutana na matatizo ya kifedha, lakini wanalazimika kusubiri.<\/p>\n<p><strong>MTANGAZAJI: \u00a0\u00a0\u00a0\u00a0\u00a0\u00a0\u00a0\u00a0\u00a0\u00a0\u00a0\u00a0\u00a0\u00a0\u00a0\u00a0\u00a0\u00a0\u00a0\u00a0\u00a0\u00a0\u00a0\u00a0\u00a0\u00a0\u00a0\u00a0\u00a0 <\/strong>Je, kuna changamoto nyingine, Bi. P\u00e9lagie Millogo?<\/p>\n<p><strong>PELAGIE MILLOGO: \u00a0\u00a0\u00a0\u00a0\u00a0\u00a0\u00a0\u00a0\u00a0\u00a0\u00a0\u00a0\u00a0\u00a0\u00a0\u00a0\u00a0\u00a0 <\/strong>Wanawake wanakutana na ugumu wa kupata maji kwa ajili ya nyuki. Tunapokwenda kisimani, tunalazimika kupoteza muda mrefu ili kupata kiasi kidogo cha maji, na mara nyingi maji hayo huwa na uchafu, hivyo yanahitaji kuchujwa kabla ya kutumika. Ikiwa tungemudu kupata visima vya maji, ingekuwa faraja kubwa kwetu.<\/p>\n<p><strong>MTANGAZAJI:<\/strong>\u00a0\u00a0\u00a0\u00a0\u00a0\u00a0\u00a0\u00a0\u00a0\u00a0\u00a0\u00a0\u00a0\u00a0\u00a0\u00a0\u00a0\u00a0\u00a0\u00a0\u00a0\u00a0\u00a0\u00a0\u00a0\u00a0\u00a0\u00a0\u00a0\u00a0 Asante kwa ufafanuzi wako. Mkaguzi Konat\u00e9, <em>Fonds d&#8217;Intervention pour l&#8217;Environnement<\/em> imeunga mkono ushirika wa Scoops-AY kwa mafunzo ya kujenga uwezo na vifaa vya ufugaji nyuki wa kisasa. Kama mtaalamu wa mafunzo ya ufugaji nyuki, ni nini kilichochochea mafunzo haya?<\/p>\n<p><strong>Naz\u00e9 Abdoulaye<\/strong><strong> KONATE: <\/strong> <em>Fonds d&#8217;Intervention pour l&#8217;Environnement au FIE<\/em> iliundwa mwaka 1994 katika sheria ya kwanza ya mazingira nchini Burkina Faso. Majukumu yake ni kupunguza mwelekeo wa sasa wa uharibifu wa mazingira, kupambana na athari mbaya za mabadiliko ya tabianchi, na kukuza maendeleo ya uchumi wa nchi kwa kutengeneza utajiri na kipato katika sekta ya mazingira na maliasili. Na, mwisho kabisa, kupunguza umaskini. Hatua yoyote ambayo inaambatana kikamilifu na malengo haya inaweza kufaidika na usaidizi wa kiufundi na kifedha wa FIE. Kwa kuwa ufugaji nyuki unachangia kwa kiasi kikubwa katika kulinda mazingira na kutengeneza kipato na ajira, ni kawaida kwamba ushirika huu unapaswa kuwa mnufaika.<\/p>\n<p><strong>MTANGAZAJI:\u00a0\u00a0\u00a0\u00a0\u00a0\u00a0\u00a0\u00a0\u00a0\u00a0\u00a0\u00a0\u00a0\u00a0\u00a0\u00a0\u00a0\u00a0\u00a0\u00a0\u00a0\u00a0\u00a0\u00a0\u00a0\u00a0\u00a0\u00a0\u00a0\u00a0 <\/strong>Na ni faida gani zinazotokana na ufugaji nyuki?<\/p>\n<p><strong>Naz\u00e9 Abdoulaye<\/strong><strong> KONATE: <\/strong> Sehemu muhimu ya ufugaji nyuki ni nyuki, kiumbe hai ambaye ni sehemu ya utofauti wa baionuwai na anahitaji kuhifadhiwa. Kazi yake kuu katika mfumo wa ikolojia ni uchavushaji, ambao ni muhimu kwa uzalishaji wa mimea mingi inayochanua duniani. Uchavushaji unahusisha uhamishaji wa chavua kutoka kwa kiungo cha uzazi cha kiume cha mmea, stameni, hadi kiungo cha kike cha ua, pistili. Uchavushaji unachangia takriban 80% ya uzalishaji wa mimea, na takriban 65-70% kwa mazao ya nafaka. Hivyo, nyuki ni rasilimali kubwa kwa kilimo na ukuaji wa miti na vichaka. Uhusiano huu kati ya mazingira na binadamu ni wa karibu sana, kwa sababu bila miti, hakuna maisha. Na bila nyuki, mimea ingetoweka kwa 70% kila mwaka.<\/p>\n<p>Hapo awali, ufugaji nyuki ulikuwa unafanywa na watu wenye rasilimali finyu za kifedha. Hata hivyo, leo hii, shughuli hii inavutia makundi yote ya kijamii. Inafanywa na wanaume, wanawake, vijana, na watu wenye ulemavu. Iwe ni shambani, katika kuchakata asali, au katika uuzaji, kila mtu anapata riziki. Ni shughuli inayotoa ajira na pia inazalisha kipato. Kwa mfano, wanawake wanaweza kutumia bidhaa za ziada za asali kutengeneza juisi, vinywaji vya pombe, au mafuta. Wafanyabiashara hutumia nta kutengeneza miundo wanapotengeneza shaba. Jeli ya kifalme hutumika kutengeneza bidhaa za dawa.<\/p>\n<p><strong>MTANGAZAJI: \u00a0\u00a0\u00a0\u00a0\u00a0\u00a0\u00a0\u00a0\u00a0\u00a0\u00a0\u00a0\u00a0\u00a0\u00a0\u00a0\u00a0\u00a0\u00a0\u00a0\u00a0\u00a0\u00a0\u00a0\u00a0\u00a0\u00a0\u00a0\u00a0 <\/strong>Asante, Mkaguzi. Sasa turudi kwa Yan Florian Millogo, mwanachama wa ushirika wa Scoops-AY ambaye chama chao kilinufaika na mafunzo ya ufugaji nyuki kwa njia ya kisasa mwaka 2018. Umejifunza nini?<\/p>\n<p><strong>YAN FLORIAN MILLOGO: \u00a0\u00a0\u00a0\u00a0\u00a0\u00a0\u00a0\u00a0 <\/strong>Tulijifunza kuhusu nyuki, ambao kwa kweli ni malighafi ya biashara yetu. Ni viumbe muhimu sana kwa binadamu na mazingira. Tunapaswa kuwapa umakini maalum nyuki pamoja na kuwakinga. Kabla ya hapo, tulijifunza kwamba kama wafugaji nyuki tunahitaji kuwa na sifa fulani, kama vile tabia ya utulivu na uvumilivu, kwa sababu nyuki ni wadudu wenye kuhitaji umakini sana.<\/p>\n<p>Tunapokwenda kuwatembelea, tunahitaji kuhakikisha kwamba hatuna msongo wa mawazo kwani hii inaweza kuwaathiri nyuki pia. Pia, ni wazi kwamba wafugaji nyuki wanahitaji kuwa wafuatiliaji wazuri ili kutambua tabia zisizo za kawaida kutoka kwa nyuki wao. Kuhusu nyuki mwenyewe, waalimu walitufundisha kuhusu tabia zake, mpangilio wake, na uzaaji wake. Tulijifunza jinsi ya kuweka mzinga katika maeneo yanayopendekezwa, vifaa muhimu vinavyohitajika kwa kazi hii, na jinsi ya kujilinda kutong\u2019atwa na nyuki.<\/p>\n<p><strong>MTANGAZAJI: <\/strong>\u00a0\u00a0\u00a0\u00a0\u00a0\u00a0\u00a0\u00a0\u00a0\u00a0\u00a0\u00a0\u00a0\u00a0\u00a0\u00a0\u00a0\u00a0\u00a0\u00a0\u00a0\u00a0\u00a0\u00a0\u00a0\u00a0\u00a0\u00a0\u00a0 Bwana Mkaguzi, kwa nini tunahitaji kujua kuhusu nyuki?<\/p>\n<p><strong>Naz\u00e9 Abdoulaye<\/strong><strong> KONATE: \u00a0<\/strong> Moja ya tafsiri za ufugaji nyuki inahusu kuwafuga nyuki kwa faida kubwa. Ikiwa unataka kufuga nyuki, ni lazima uwajue. Ikiwa hujui chochote kuhusu nyuki, ni wazi kwamba unaweza kuwafanyia mambo ambayo unadhani ni madogo, lakini yanaweza kuwa hatari kwao. Kwa mfano, katika kundi la nyuki, kuna aina tatu za nyuki: malkia mmoja, madume wachache wanaoitwa &#8220;drones,&#8221; wapatao 1,500 hadi 2,000, na wafanyakazi. Ikiwa humtambui malkia wakati wa mavuno, unaweza kujikuta umemuua. Matokeo yake, mzinga unaweza kukuchachia. Kwa hiyo, ni wazi kwamba lazima umtambue malkia kabla ya kuanza shughuli hiyo.<\/p>\n<p><strong>MTANGAZAJI: <\/strong>\u00a0\u00a0\u00a0\u00a0\u00a0\u00a0\u00a0\u00a0\u00a0\u00a0\u00a0\u00a0\u00a0\u00a0\u00a0\u00a0\u00a0\u00a0\u00a0\u00a0\u00a0\u00a0\u00a0\u00a0\u00a0\u00a0\u00a0\u00a0\u00a0 Ni kweli kwamba kuwajua nyuki ni jambo muhimu katika ufugaji wa nyuki. Lakini hilo pekee halitoshi. Kuna mbinu nyingine zinazohusika, sivyo Bwana Millogo?<\/p>\n<p><strong>YAN FLORIAN MILLOGO: \u00a0\u00a0\u00a0\u00a0\u00a0\u00a0\u00a0\u00a0 <\/strong>Mbali na kujifunza kuhusu nyuki, tulijifunza pia jinsi ya kuandaa mizinga ipasavyo. Mzinga unapaswa kuwekwa mbali na maeneo yenye kelele, kama vile sehemu za umma, nyumba, na barabara, na inapendekezwa uwe chini ya mti wenye kivuli kama mwembe, mti wa shea, au mkorosho. Hii ni miti ya matunda ambayo nyuki wanapenda kwa sababu maua yake huzalisha nekta na chavua kwa wingi. Aidha, nyuki wanapenda harufu kali na rangi angavu za maua ya miti hii, ambayo ni mingi katika kijiji cha Yabasso.<\/p>\n<p>Baada ya hatua hii, inayofuata ni ufuatiliaji au udhibiti. Hii inahusisha kuwapatia nyuki maji na kufuatilia maendeleo ya kundi la nyuki. Kwenye chombo cha maji, tunaweka kitu kinachoelea au kokoto ili kuzuia nyuki kuzama wanapojaribu kunywa. Mara asali inapokuwa tayari, tunahamia kwenye mavuno. Pia kuna mapendekezo kadhaa. Vaa mavazi maalum ya kazi, pamoja na buti na glavu. Inashauriwa watu wawili hadi watatu kushiriki katika kazi hii. Mtu mmoja huvuna, wa pili hushika kifuniko, na wa tatu huwafukizia moshi nyuki ili kuwatuliza. Vinginevyo, ikiwa kuna watu wawili tu, nani atashika ndoo ya kukusanya asali na nani atawafukizia moshi nyuki? Wakati ambapo hakuna watu wa kutosha kwenye mavuno, nyuki wengi hufa na kazi inakuwa ngumu sana.<\/p>\n<p><strong>MTANGAZAJI: <\/strong>\u00a0\u00a0\u00a0\u00a0\u00a0\u00a0\u00a0\u00a0\u00a0\u00a0\u00a0\u00a0\u00a0\u00a0\u00a0\u00a0\u00a0\u00a0\u00a0\u00a0\u00a0\u00a0\u00a0\u00a0\u00a0\u00a0\u00a0\u00a0\u00a0 Je, unaweza kuthibitisha mbinu hizi bora, Bwana Mkaguzi?<\/p>\n<p><strong>Naz\u00e9 Abdoulaye<\/strong><strong> KONATE: <\/strong>Ndio, wafugaji hawa wa nyuki wamefunzwa vizuri. Kama nyongeza ya alichosema Bwana Millogo, mzinga pia lazima utembelewe mara kwa mara ili kugundua matatizo yoyote, kama vile magonjwa ya nyuki, ili kuzuia yasije yakaharibu kundi la nyuki. Hapa Burkina Faso, nyuki wanakutana na changamoto kuu mbili: vimelea wanaojulikana kama &#8220;mchukuaji mdogo&#8221; (Ujumbe wa mhariri: jina la kisayansi ni Aethina tumida, na pia huitwa mdudu mdogo wa kwenye mzinga) na funza. Mchukuaji mdogo hauangamizi kundi la nyuki moja kwa moja, lakini funza ndie anayeweza kuharibu kundi. Utafiti unaendelea kutafuta tiba za magonjwa haya. Kwa sasa, wafugaji wa nyuki wanakabiliana nayo. Aidha, nyuki ni viumbe vinavyohitaji uangalizi. Kitendo cha kuwatembelea huwachochea kufanya uzalishaji.<\/p>\n<p>Kuhusu kuweka mzinga kwenye kivuli, unapoweka kwenye jua moja kwa moja, ukizingatia kwamba Burkina Faso mara nyingi huwa na joto kali, sega la asali litayeyuka, asali itamwagika, na hii husababisha uharibifu wa mayai na larva. Hii inamaanisha kwamba hautakuwa na uzalishaji mpya\u2014hutakuwa na nyuki wapya. Nyuki wataacha mzinga mwishowe. Joto linalopendekezwa ndani ya mzinga wa nyuki ni kati ya 33 hadi 36\u00b0C. Ikiwa kuna joto kali sana, hautapata asali ya kutosha kwa sababu nyuki wataweka nguvu zao kwenye kupoza mzinga badala ya kuzingatia uzalishaji wa asali.<\/p>\n<p>Mzinga pia unapaswa kuwekwa mbali na maeneo ya umma kama makanisa, shule, n.k. Nyuki hawapendi kelele. Ikiwa utawachanganya, watakushambulia. Hapo awali, mizinga ilikuwa inawekwa kwenye mti. Lakini sasa, mizinga iko chini ya mti kwenye nguzo za urefu wa kati ya 0.8 na 1.5 mita juu ya ardhi. Hapa Burkina Faso, upepo mkali na mvua kawaida hupita kutoka mashariki hadi magharibi. Kwa hivyo, mizinga inapaswa kuwekwa kwa namna ambayo shimo la kuingilia liko upande wa kaskazini au kusini, si mashariki wala magharibi. Pia, utahitaji kufunga vifaa vinavyolinda mzinga dhidi ya wanyama au wadudu waharibifu. Wengine hutumia mafuta ya injini, wengine hutumia maji ili kuzuia mchwa kupita kutoka chini ya nguzo hadi kwenye mzinga. Mizinga inayopendwa zaidi huko Yabasso ni mizinga ya Kikenya. Inatengenezwa kwa kutumia mbao na mafundi wa hapa. Inatoa harufu inayobadilika pindi inapoingia unyevu. Nyuki ni wanyama safi na wenye afya. Hawapendi harufu mbaya. Ndio maana hutaona nyuki wakitua sehemu iliyooza, na pia kwa nini hautakiwi kuweka mizinga maeneo yanayokumbwa na mafuriko.<\/p>\n<p><strong>MTANGAZAJI: <\/strong>\u00a0\u00a0\u00a0\u00a0\u00a0\u00a0\u00a0\u00a0\u00a0\u00a0\u00a0\u00a0\u00a0\u00a0\u00a0\u00a0\u00a0\u00a0\u00a0\u00a0\u00a0\u00a0\u00a0\u00a0\u00a0\u00a0\u00a0\u00a0\u00a0 Hatua ya mwisho ya uzalishaji ni kuvuna<\/p>\n<p><strong>Naz\u00e9 Abdoulaye<\/strong><strong> KONATE: <\/strong> Ndio, ni sahihi! Hapa Burkina Faso, kuna vipindi viwili vikuu vya uzalishaji wa asali, vinavyojulikana kama vipindi vya &#8220;mtiririko wa asali.&#8221; Kuanzia Februari hadi Juni, ni kipindi kikuu cha &#8220;mtiririko wa asali,&#8221; ambapo miti mingi ina maua. Mwishoni mwa msimu wa mvua au wa ukuaji wa mimea, bado kuna kile tunachokiita kipindi kidogo cha &#8220;mtiririko wa asali.&#8221; Hiki hudumu kuanzia katikati ya mwezi Agosti hadi mwezi Desemba, wakati kilimo cha nafaka kimekamilika na nekta ambayo nyuki wameweza kuvuna kutoka kwenye maua inaweza kutumika kutengeneza asali.<\/p>\n<p>Usafishaji: Haya ni mavuno ya mwisho, ambapo baadhi ya seli zinabaki kwenye mzinga, labda zikiwa na poleni au vibaragha vya nyuki. Zikikaa kwa muda, baadhi ya seli huganda na kuwa nyeusi. Hizi zinahitaji kusafishwa ili nyuki waweze kuzibadili. Usafishaji, kama jina linavyosema, hasa huandaa asali kuu ya mwezi Machi. Inahusisha kusafisha mzinga na kutoa mabaki yote. Wanavuna lakini unaweza kupata asali au hutapata chochote. Asali hii kwa kawaida huwa na maji mengi na haizingatiwi na ushirika. Mfugaji wa nyuki hufanya anavyotaka na asali hiyo.<\/p>\n<p>Mbinu zote hizi ni maalum kwa mizinga ya Kikenya au mizinga ya asili inayotengenezwa kwa mikono na inayotumika Yabasso.<\/p>\n<p>Ikiwa mbinu hizi zitatekelezwa ipasavyo, ubora na wingi wa asali utakuwa ni uhakika, hasa kwani asali haitavunwa kwa kutumia moto wa moja kwa moja, bali kwa kufusha moshi. Na sina shaka kuhusu hili linapohusu asali ya Yabasso. Niliweza kuonja asali hiyo wakati wa mkutano. Ladha na muonekano wa asali hii ni ya kipekee. Na inapokuwa hivyo, unafurahi kweli kwa faida zote za biashara yako.<\/p>\n<p><strong>MTANGAZAJI: <\/strong>\u00a0\u00a0\u00a0\u00a0\u00a0\u00a0\u00a0\u00a0\u00a0\u00a0\u00a0\u00a0\u00a0\u00a0\u00a0\u00a0\u00a0\u00a0\u00a0\u00a0\u00a0\u00a0\u00a0\u00a0\u00a0\u00a0\u00a0\u00a0\u00a0 Mbali na faida hizi, Bwana Konat\u00e9, ni zipi changamoto katika ufugaji wa nyuki?<\/p>\n<p><strong>Naz\u00e9 Abdoulaye<\/strong><strong> KONATE: <\/strong> Ufugaji wa nyuki hapa Burkina Faso unakutana na changamoto ambazo zinaweza kugawanywa katika makundi matatu: vifaa, masoko, na ushirika.<\/p>\n<p>Vifaa vya kisasa vya ufugaji nyuki ni ghali sana. Matumizi ya chuma katika ufugaji wa nyuki yanashauriwa kuepukwa kwa nguvu, ingawa chuma ndio malighafi inayopatikana zaidi nchini mwetu. Chuma kisichopata kutu ndicho kinachoshauriwa zaidi, ingawa zana zilizotengenezwa kwa nyenzo hii ni ghali sana. Kwa mfano, uvunaji wa mikono unagharimu takriban faranga 200,000 za CFA (dola 330 za Marekani), wakati mashine za chuma isiyoshika kutu zinagharimu kati ya faranga100,000 hadi 150,000 za CFA (dola 165 hadi 250 za Marekani). Si rahisi kwa wafugaji wa nyuki kuweza kumudu gharama hizi.<\/p>\n<p>Kuhusu mauzo, hakuna bei ya kawaida ya asali hapa Burkina Faso. Kila mfugaji wa nyuki huweka bei ya asali yao kulingana na vifaa wanavyotumia. Matokeo yake, bei zinatofautiana.<\/p>\n<p>Mwishowe, ingawa vyama vya wafugaji wa nyuki vimeanzishwa, havifanyi kazi vizuri. Kuhusu nyuki wenyewe, tatizo halisi ni mbinu za kilimo, ikiwemo kuvuna kupita kiasi mimea, ambayo hupunguza vyanzo vya nekta na poleni, na matumizi yasiyodhibitiwa ya vidhibiti vya wadudu. Asali inatokana na maua. Bila miti, hakuna maua na hivyo hakuna asali. Vidhibiti vya wadudu na moto wa msituni vinaua nyuki kwa wingi.<\/p>\n<p>&nbsp;<\/p>\n<p><strong>MTANGAZAJI: <\/strong>\u00a0\u00a0\u00a0\u00a0\u00a0\u00a0\u00a0\u00a0\u00a0\u00a0\u00a0\u00a0\u00a0\u00a0\u00a0\u00a0\u00a0\u00a0\u00a0\u00a0\u00a0\u00a0\u00a0\u00a0\u00a0\u00a0\u00a0\u00a0\u00a0 Je, unapendekeza nini ili kupunguza vikwazo hivi?<\/p>\n<p>&nbsp;<\/p>\n<p><strong>Naz\u00e9 Abdoulaye<\/strong><strong> KONATE: <\/strong> Tunahitaji kuanzisha na kuimarisha mashirika yaliyopo, na kuhamasisha mikutano ili kuboresha ujuzi na kushirikishana uzoefu. Serikali inapaswa kujumuisha vifaa vya ufugaji nyuki kwenye orodha yake ya vifaa vyenye bei zinazotambulika au kutoa ruzuku kwa vifaa vya ufugaji nyuki. Hii itatatua tatizo la bei zisizo sawa na, kwa upande mwingine, kuhamasisha usindikaji wa asali hapa Burkina Faso. Kwasababu ni katika usindikaji ambapo wafugaji wa nyuki wanaweza kupata faida kubwa zaidi.<\/p>\n<p><strong>MTANGAZAJI: \u00a0\u00a0\u00a0\u00a0\u00a0\u00a0\u00a0\u00a0\u00a0\u00a0\u00a0\u00a0\u00a0\u00a0\u00a0\u00a0\u00a0\u00a0\u00a0\u00a0\u00a0\u00a0\u00a0\u00a0\u00a0\u00a0\u00a0\u00a0\u00a0 <\/strong>Asante, Mkaguzi Konat\u00e9. Tumefika mwishoni mwa programu hii. Inaonyesha kwamba ufugaji nyuki unaongezeka katika kijiji cha Yabasso, Burkina Faso. Shukrani kwa Fonds d&#8217;Intervention pour l&#8217;Environnement, ushirika wa Scoops-AY wenye wanachama 30 una mizinga 300 ya Kikenya. Wanazalisha angalau lita 1,600 za asali kila mwaka. Uuzaji wa asali hii na usindikaji wa bidhaa zake husaidia wafugaji wa nyuki kujipatia riziki. Pia wana vitu vya kutosha vya kuwafanya kuwa bize wakati wa msimu wa kiangazi. Wakiwa na ufahamu wa faida za ufugaji nyuki kwa maisha yao na bioanuwai, wafugaji wa nyuki wanajitahidi sana kutekeleza mafunzo waliyoyapata.<\/p>\n<p>Natumai taarifa zilizotolewa katika programu hii zitakuwa na manufaa makubwa kwako. Asante kwa umakini wako. Na tutaonana hivi karibuni kwa programu nyingine mpya.<\/p>\n","protected":false},"excerpt":{"rendered":"<p>SAUTI YA UTAMBULISHO Ipandishwe juu KISHA ISHUshe TARATIBU MTANGAZAJI:\u00a0\u00a0\u00a0\u00a0\u00a0\u00a0\u00a0\u00a0\u00a0\u00a0\u00a0\u00a0\u00a0\u00a0\u00a0\u00a0\u00a0\u00a0\u00a0\u00a0\u00a0\u00a0\u00a0\u00a0\u00a0\u00a0\u00a0\u00a0\u00a0\u00a0 Habari, wasikilizaji wapendwa. Karibu kwenye programu yako. Jina langu ni Solange Bicaba. Leo, tutazungumzia kuhusu kazi ya ufugaji nyuki na manufaa yake kwa watu na mazingira huko Yabasso, kijiji kilichoko katika mkoa wa Hauts-Bassins magharibi mwa nchi ya Burkina Faso. Katika kijiji hiki, takriban watu thelathini&hellip;<\/p>\n","protected":false},"author":186,"featured_media":0,"parent":0,"menu_order":0,"template":"","meta":{"footnotes":"","beyondwords_generate_audio":"","beyondwords_integration_method":"","beyondwords_project_id":"","beyondwords_content_id":"","beyondwords_preview_token":"","beyondwords_player_content":"","beyondwords_player_style":"","beyondwords_language_code":"","beyondwords_language_id":"","beyondwords_title_voice_id":"","beyondwords_body_voice_id":"","beyondwords_summary_voice_id":"","beyondwords_error_message":"","beyondwords_disabled":"","beyondwords_delete_content":"","beyondwords_podcast_id":"","beyondwords_hash":"","publish_post_to_speechkit":"","speechkit_hash":"","speechkit_generate_audio":"","speechkit_project_id":"","speechkit_podcast_id":"","speechkit_error_message":"","speechkit_disabled":"","speechkit_access_key":"","speechkit_error":"","speechkit_info":"","speechkit_response":"","speechkit_retries":"","speechkit_status":"","speechkit_updated_at":"","_speechkit_link":"","_speechkit_text":""},"script-format":[517],"package":[961],"script-category":[866,882],"class_list":["post-41887","radio-script","type-radio-script","status-publish","hentry","script-format-mahojiano","package-124-sw","script-category-mazingira-na-mabadiliko-ya-tabianchi","script-category-mifugo-na-ufugaji-nyuki"],"acf":[],"yoast_head":"<!-- This site is optimized with the Yoast SEO plugin v28.1 - https:\/\/yoast.com\/product\/yoast-seo-wordpress\/ -->\n<title>Ufugaji wa nyuki unawanufaisha wakulima huku ukihifadhi mazingira - Farm Radio International<\/title>\n<meta name=\"robots\" content=\"index, follow, max-snippet:-1, max-image-preview:large, max-video-preview:-1\" \/>\n<link rel=\"canonical\" href=\"https:\/\/scripts.farmradio.fm\/sw\/mwongozo-wa-redio\/ufugaji-wa-nyuki-unawanufaisha-wakulima-huku-ukihifadhi-mazingira\/\" \/>\n<meta property=\"og:locale\" content=\"en_US\" \/>\n<meta property=\"og:type\" content=\"article\" \/>\n<meta property=\"og:title\" content=\"Ufugaji wa nyuki unawanufaisha wakulima huku ukihifadhi mazingira - Farm Radio International\" \/>\n<meta property=\"og:description\" content=\"SAUTI YA UTAMBULISHO Ipandishwe juu KISHA ISHUshe TARATIBU MTANGAZAJI:\u00a0\u00a0\u00a0\u00a0\u00a0\u00a0\u00a0\u00a0\u00a0\u00a0\u00a0\u00a0\u00a0\u00a0\u00a0\u00a0\u00a0\u00a0\u00a0\u00a0\u00a0\u00a0\u00a0\u00a0\u00a0\u00a0\u00a0\u00a0\u00a0\u00a0 Habari, wasikilizaji wapendwa. Karibu kwenye programu yako. Jina langu ni Solange Bicaba. Leo, tutazungumzia kuhusu kazi ya ufugaji nyuki na manufaa yake kwa watu na mazingira huko Yabasso, kijiji kilichoko katika mkoa wa Hauts-Bassins magharibi mwa nchi ya Burkina Faso. Katika kijiji hiki, takriban watu thelathini&hellip;\" \/>\n<meta property=\"og:url\" content=\"https:\/\/scripts.farmradio.fm\/sw\/mwongozo-wa-redio\/ufugaji-wa-nyuki-unawanufaisha-wakulima-huku-ukihifadhi-mazingira\/\" \/>\n<meta property=\"og:site_name\" content=\"Farm Radio International\" \/>\n<meta property=\"article:publisher\" content=\"https:\/\/www.facebook.com\/farmradio\/\" \/>\n<meta property=\"article:modified_time\" content=\"2024-12-02T15:29:21+00:00\" \/>\n<meta name=\"twitter:card\" content=\"summary_large_image\" \/>\n<meta name=\"twitter:site\" content=\"@farmradio\" \/>\n<meta name=\"twitter:label1\" content=\"Est. reading time\" \/>\n\t<meta name=\"twitter:data1\" content=\"13 minutes\" \/>\n<script type=\"application\/ld+json\" class=\"yoast-schema-graph\">{\"@context\":\"https:\\\/\\\/schema.org\",\"@graph\":[{\"@type\":\"Article\",\"@id\":\"https:\\\/\\\/scripts.farmradio.fm\\\/sw\\\/mwongozo-wa-redio\\\/ufugaji-wa-nyuki-unawanufaisha-wakulima-huku-ukihifadhi-mazingira\\\/#article\",\"isPartOf\":{\"@id\":\"https:\\\/\\\/scripts.farmradio.fm\\\/sw\\\/mwongozo-wa-redio\\\/ufugaji-wa-nyuki-unawanufaisha-wakulima-huku-ukihifadhi-mazingira\\\/\"},\"author\":{\"name\":\"Stephanie Coucopoulos\",\"@id\":\"http:\\\/\\\/scripts.farmradio.fm\\\/sw\\\/#\\\/schema\\\/person\\\/5408fc11331f1b60612ec51a0a96d37c\"},\"headline\":\"Ufugaji wa nyuki unawanufaisha wakulima huku ukihifadhi mazingira\",\"datePublished\":\"2024-01-11T16:47:52+00:00\",\"dateModified\":\"2024-12-02T15:29:21+00:00\",\"mainEntityOfPage\":{\"@id\":\"https:\\\/\\\/scripts.farmradio.fm\\\/sw\\\/mwongozo-wa-redio\\\/ufugaji-wa-nyuki-unawanufaisha-wakulima-huku-ukihifadhi-mazingira\\\/\"},\"wordCount\":2675,\"publisher\":{\"@id\":\"http:\\\/\\\/scripts.farmradio.fm\\\/sw\\\/#organization\"},\"inLanguage\":\"sw-CG\"},{\"@type\":\"WebPage\",\"@id\":\"https:\\\/\\\/scripts.farmradio.fm\\\/sw\\\/mwongozo-wa-redio\\\/ufugaji-wa-nyuki-unawanufaisha-wakulima-huku-ukihifadhi-mazingira\\\/\",\"url\":\"https:\\\/\\\/scripts.farmradio.fm\\\/sw\\\/mwongozo-wa-redio\\\/ufugaji-wa-nyuki-unawanufaisha-wakulima-huku-ukihifadhi-mazingira\\\/\",\"name\":\"Ufugaji wa nyuki unawanufaisha wakulima huku ukihifadhi mazingira - Farm Radio International\",\"isPartOf\":{\"@id\":\"http:\\\/\\\/scripts.farmradio.fm\\\/sw\\\/#website\"},\"datePublished\":\"2024-01-11T16:47:52+00:00\",\"dateModified\":\"2024-12-02T15:29:21+00:00\",\"breadcrumb\":{\"@id\":\"https:\\\/\\\/scripts.farmradio.fm\\\/sw\\\/mwongozo-wa-redio\\\/ufugaji-wa-nyuki-unawanufaisha-wakulima-huku-ukihifadhi-mazingira\\\/#breadcrumb\"},\"inLanguage\":\"sw-CG\",\"potentialAction\":[{\"@type\":\"ReadAction\",\"target\":[\"https:\\\/\\\/scripts.farmradio.fm\\\/sw\\\/mwongozo-wa-redio\\\/ufugaji-wa-nyuki-unawanufaisha-wakulima-huku-ukihifadhi-mazingira\\\/\"]}]},{\"@type\":\"BreadcrumbList\",\"@id\":\"https:\\\/\\\/scripts.farmradio.fm\\\/sw\\\/mwongozo-wa-redio\\\/ufugaji-wa-nyuki-unawanufaisha-wakulima-huku-ukihifadhi-mazingira\\\/#breadcrumb\",\"itemListElement\":[{\"@type\":\"ListItem\",\"position\":1,\"name\":\"Nyumbani\",\"item\":\"http:\\\/\\\/scripts.farmradio.fm\\\/sw\\\/\"},{\"@type\":\"ListItem\",\"position\":2,\"name\":\"Mahojiano\",\"item\":\"https:\\\/\\\/scripts.farmradio.fm\\\/sw\\\/mwongozo-wa-muundo\\\/mahojiano\\\/\"},{\"@type\":\"ListItem\",\"position\":3,\"name\":\"Ufugaji wa nyuki unawanufaisha wakulima huku ukihifadhi mazingira\"}]},{\"@type\":\"WebSite\",\"@id\":\"http:\\\/\\\/scripts.farmradio.fm\\\/sw\\\/#website\",\"url\":\"http:\\\/\\\/scripts.farmradio.fm\\\/sw\\\/\",\"name\":\"Farm Radio International\",\"description\":\"Sharing knowledge, giving voice.\",\"publisher\":{\"@id\":\"http:\\\/\\\/scripts.farmradio.fm\\\/sw\\\/#organization\"},\"potentialAction\":[{\"@type\":\"SearchAction\",\"target\":{\"@type\":\"EntryPoint\",\"urlTemplate\":\"http:\\\/\\\/scripts.farmradio.fm\\\/sw\\\/?s={search_term_string}\"},\"query-input\":{\"@type\":\"PropertyValueSpecification\",\"valueRequired\":true,\"valueName\":\"search_term_string\"}}],\"inLanguage\":\"sw-CG\"},{\"@type\":\"Organization\",\"@id\":\"http:\\\/\\\/scripts.farmradio.fm\\\/sw\\\/#organization\",\"name\":\"Farm Radio International\",\"url\":\"http:\\\/\\\/scripts.farmradio.fm\\\/sw\\\/\",\"logo\":{\"@type\":\"ImageObject\",\"inLanguage\":\"sw-CG\",\"@id\":\"http:\\\/\\\/scripts.farmradio.fm\\\/sw\\\/#\\\/schema\\\/logo\\\/image\\\/\",\"url\":\"https:\\\/\\\/scripts.farmradio.fm\\\/wp-content\\\/uploads\\\/farmRadioLogo.jpg\",\"contentUrl\":\"https:\\\/\\\/scripts.farmradio.fm\\\/wp-content\\\/uploads\\\/farmRadioLogo.jpg\",\"width\":200,\"height\":75,\"caption\":\"Farm Radio International\"},\"image\":{\"@id\":\"http:\\\/\\\/scripts.farmradio.fm\\\/sw\\\/#\\\/schema\\\/logo\\\/image\\\/\"},\"sameAs\":[\"https:\\\/\\\/www.facebook.com\\\/farmradio\\\/\",\"https:\\\/\\\/x.com\\\/farmradio\",\"https:\\\/\\\/www.instagram.com\\\/farmradio\\\/\",\"https:\\\/\\\/www.youtube.com\\\/user\\\/FarmRadioInt\"]},{\"@type\":\"Person\",\"@id\":\"http:\\\/\\\/scripts.farmradio.fm\\\/sw\\\/#\\\/schema\\\/person\\\/5408fc11331f1b60612ec51a0a96d37c\",\"name\":\"Stephanie Coucopoulos\",\"image\":{\"@type\":\"ImageObject\",\"inLanguage\":\"sw-CG\",\"@id\":\"https:\\\/\\\/secure.gravatar.com\\\/avatar\\\/6a106685b1a0c9e2132bb55a0acc6ca31d249d76feab716ffa33062ce0ee8c26?s=96&d=mm&r=g\",\"url\":\"https:\\\/\\\/secure.gravatar.com\\\/avatar\\\/6a106685b1a0c9e2132bb55a0acc6ca31d249d76feab716ffa33062ce0ee8c26?s=96&d=mm&r=g\",\"contentUrl\":\"https:\\\/\\\/secure.gravatar.com\\\/avatar\\\/6a106685b1a0c9e2132bb55a0acc6ca31d249d76feab716ffa33062ce0ee8c26?s=96&d=mm&r=g\",\"caption\":\"Stephanie Coucopoulos\"}}]}<\/script>\n<!-- \/ Yoast SEO plugin. -->","yoast_head_json":{"title":"Ufugaji wa nyuki unawanufaisha wakulima huku ukihifadhi mazingira - Farm Radio International","robots":{"index":"index","follow":"follow","max-snippet":"max-snippet:-1","max-image-preview":"max-image-preview:large","max-video-preview":"max-video-preview:-1"},"canonical":"https:\/\/scripts.farmradio.fm\/sw\/mwongozo-wa-redio\/ufugaji-wa-nyuki-unawanufaisha-wakulima-huku-ukihifadhi-mazingira\/","og_locale":"en_US","og_type":"article","og_title":"Ufugaji wa nyuki unawanufaisha wakulima huku ukihifadhi mazingira - Farm Radio International","og_description":"SAUTI YA UTAMBULISHO Ipandishwe juu KISHA ISHUshe TARATIBU MTANGAZAJI:\u00a0\u00a0\u00a0\u00a0\u00a0\u00a0\u00a0\u00a0\u00a0\u00a0\u00a0\u00a0\u00a0\u00a0\u00a0\u00a0\u00a0\u00a0\u00a0\u00a0\u00a0\u00a0\u00a0\u00a0\u00a0\u00a0\u00a0\u00a0\u00a0\u00a0 Habari, wasikilizaji wapendwa. Karibu kwenye programu yako. Jina langu ni Solange Bicaba. Leo, tutazungumzia kuhusu kazi ya ufugaji nyuki na manufaa yake kwa watu na mazingira huko Yabasso, kijiji kilichoko katika mkoa wa Hauts-Bassins magharibi mwa nchi ya Burkina Faso. Katika kijiji hiki, takriban watu thelathini&hellip;","og_url":"https:\/\/scripts.farmradio.fm\/sw\/mwongozo-wa-redio\/ufugaji-wa-nyuki-unawanufaisha-wakulima-huku-ukihifadhi-mazingira\/","og_site_name":"Farm Radio International","article_publisher":"https:\/\/www.facebook.com\/farmradio\/","article_modified_time":"2024-12-02T15:29:21+00:00","twitter_card":"summary_large_image","twitter_site":"@farmradio","twitter_misc":{"Est. reading time":"13 minutes"},"schema":{"@context":"https:\/\/schema.org","@graph":[{"@type":"Article","@id":"https:\/\/scripts.farmradio.fm\/sw\/mwongozo-wa-redio\/ufugaji-wa-nyuki-unawanufaisha-wakulima-huku-ukihifadhi-mazingira\/#article","isPartOf":{"@id":"https:\/\/scripts.farmradio.fm\/sw\/mwongozo-wa-redio\/ufugaji-wa-nyuki-unawanufaisha-wakulima-huku-ukihifadhi-mazingira\/"},"author":{"name":"Stephanie Coucopoulos","@id":"http:\/\/scripts.farmradio.fm\/sw\/#\/schema\/person\/5408fc11331f1b60612ec51a0a96d37c"},"headline":"Ufugaji wa nyuki unawanufaisha wakulima huku ukihifadhi mazingira","datePublished":"2024-01-11T16:47:52+00:00","dateModified":"2024-12-02T15:29:21+00:00","mainEntityOfPage":{"@id":"https:\/\/scripts.farmradio.fm\/sw\/mwongozo-wa-redio\/ufugaji-wa-nyuki-unawanufaisha-wakulima-huku-ukihifadhi-mazingira\/"},"wordCount":2675,"publisher":{"@id":"http:\/\/scripts.farmradio.fm\/sw\/#organization"},"inLanguage":"sw-CG"},{"@type":"WebPage","@id":"https:\/\/scripts.farmradio.fm\/sw\/mwongozo-wa-redio\/ufugaji-wa-nyuki-unawanufaisha-wakulima-huku-ukihifadhi-mazingira\/","url":"https:\/\/scripts.farmradio.fm\/sw\/mwongozo-wa-redio\/ufugaji-wa-nyuki-unawanufaisha-wakulima-huku-ukihifadhi-mazingira\/","name":"Ufugaji wa nyuki unawanufaisha wakulima huku ukihifadhi mazingira - Farm Radio International","isPartOf":{"@id":"http:\/\/scripts.farmradio.fm\/sw\/#website"},"datePublished":"2024-01-11T16:47:52+00:00","dateModified":"2024-12-02T15:29:21+00:00","breadcrumb":{"@id":"https:\/\/scripts.farmradio.fm\/sw\/mwongozo-wa-redio\/ufugaji-wa-nyuki-unawanufaisha-wakulima-huku-ukihifadhi-mazingira\/#breadcrumb"},"inLanguage":"sw-CG","potentialAction":[{"@type":"ReadAction","target":["https:\/\/scripts.farmradio.fm\/sw\/mwongozo-wa-redio\/ufugaji-wa-nyuki-unawanufaisha-wakulima-huku-ukihifadhi-mazingira\/"]}]},{"@type":"BreadcrumbList","@id":"https:\/\/scripts.farmradio.fm\/sw\/mwongozo-wa-redio\/ufugaji-wa-nyuki-unawanufaisha-wakulima-huku-ukihifadhi-mazingira\/#breadcrumb","itemListElement":[{"@type":"ListItem","position":1,"name":"Nyumbani","item":"http:\/\/scripts.farmradio.fm\/sw\/"},{"@type":"ListItem","position":2,"name":"Mahojiano","item":"https:\/\/scripts.farmradio.fm\/sw\/mwongozo-wa-muundo\/mahojiano\/"},{"@type":"ListItem","position":3,"name":"Ufugaji wa nyuki unawanufaisha wakulima huku ukihifadhi mazingira"}]},{"@type":"WebSite","@id":"http:\/\/scripts.farmradio.fm\/sw\/#website","url":"http:\/\/scripts.farmradio.fm\/sw\/","name":"Farm Radio International","description":"Sharing knowledge, giving voice.","publisher":{"@id":"http:\/\/scripts.farmradio.fm\/sw\/#organization"},"potentialAction":[{"@type":"SearchAction","target":{"@type":"EntryPoint","urlTemplate":"http:\/\/scripts.farmradio.fm\/sw\/?s={search_term_string}"},"query-input":{"@type":"PropertyValueSpecification","valueRequired":true,"valueName":"search_term_string"}}],"inLanguage":"sw-CG"},{"@type":"Organization","@id":"http:\/\/scripts.farmradio.fm\/sw\/#organization","name":"Farm Radio International","url":"http:\/\/scripts.farmradio.fm\/sw\/","logo":{"@type":"ImageObject","inLanguage":"sw-CG","@id":"http:\/\/scripts.farmradio.fm\/sw\/#\/schema\/logo\/image\/","url":"https:\/\/scripts.farmradio.fm\/wp-content\/uploads\/farmRadioLogo.jpg","contentUrl":"https:\/\/scripts.farmradio.fm\/wp-content\/uploads\/farmRadioLogo.jpg","width":200,"height":75,"caption":"Farm Radio International"},"image":{"@id":"http:\/\/scripts.farmradio.fm\/sw\/#\/schema\/logo\/image\/"},"sameAs":["https:\/\/www.facebook.com\/farmradio\/","https:\/\/x.com\/farmradio","https:\/\/www.instagram.com\/farmradio\/","https:\/\/www.youtube.com\/user\/FarmRadioInt"]},{"@type":"Person","@id":"http:\/\/scripts.farmradio.fm\/sw\/#\/schema\/person\/5408fc11331f1b60612ec51a0a96d37c","name":"Stephanie Coucopoulos","image":{"@type":"ImageObject","inLanguage":"sw-CG","@id":"https:\/\/secure.gravatar.com\/avatar\/6a106685b1a0c9e2132bb55a0acc6ca31d249d76feab716ffa33062ce0ee8c26?s=96&d=mm&r=g","url":"https:\/\/secure.gravatar.com\/avatar\/6a106685b1a0c9e2132bb55a0acc6ca31d249d76feab716ffa33062ce0ee8c26?s=96&d=mm&r=g","contentUrl":"https:\/\/secure.gravatar.com\/avatar\/6a106685b1a0c9e2132bb55a0acc6ca31d249d76feab716ffa33062ce0ee8c26?s=96&d=mm&r=g","caption":"Stephanie Coucopoulos"}}]}},"_links":{"self":[{"href":"https:\/\/scripts.farmradio.fm\/sw\/wp-json\/wp\/v2\/radio-script\/41887","targetHints":{"allow":["GET"]}}],"collection":[{"href":"https:\/\/scripts.farmradio.fm\/sw\/wp-json\/wp\/v2\/radio-script"}],"about":[{"href":"https:\/\/scripts.farmradio.fm\/sw\/wp-json\/wp\/v2\/types\/radio-script"}],"author":[{"embeddable":true,"href":"https:\/\/scripts.farmradio.fm\/sw\/wp-json\/wp\/v2\/users\/186"}],"version-history":[{"count":0,"href":"https:\/\/scripts.farmradio.fm\/sw\/wp-json\/wp\/v2\/radio-script\/41887\/revisions"}],"wp:attachment":[{"href":"https:\/\/scripts.farmradio.fm\/sw\/wp-json\/wp\/v2\/media?parent=41887"}],"wp:term":[{"taxonomy":"script-format","embeddable":true,"href":"https:\/\/scripts.farmradio.fm\/sw\/wp-json\/wp\/v2\/script-format?post=41887"},{"taxonomy":"package","embeddable":true,"href":"https:\/\/scripts.farmradio.fm\/sw\/wp-json\/wp\/v2\/package?post=41887"},{"taxonomy":"script-category","embeddable":true,"href":"https:\/\/scripts.farmradio.fm\/sw\/wp-json\/wp\/v2\/script-category?post=41887"}],"curies":[{"name":"wp","href":"https:\/\/api.w.org\/{rel}","templated":true}]}}