{"id":39259,"date":"2022-10-13T17:12:00","date_gmt":"2022-10-13T14:12:00","guid":{"rendered":"https:\/\/scripts.farmradio.fm\/?post_type=radio-script&#038;p=39259"},"modified":"2023-08-28T21:51:00","modified_gmt":"2023-08-28T18:51:00","slug":"ukatili-majumbani-sababu-na-matokeo-yake","status":"publish","type":"radio-script","link":"https:\/\/scripts.farmradio.fm\/sw\/mwongozo-wa-redio\/ukatili-majumbani-sababu-na-matokeo-yake\/","title":{"rendered":"Ukatili Majumbani: Sababu na matokeo yake"},"content":{"rendered":"<p><strong>MTANGAZAJI:<\/strong> \u00a0\u00a0\u00a0\u00a0\u00a0\u00a0\u00a0\u00a0\u00a0\u00a0\u00a0\u00a0\u00a0\u00a0\u00a0\u00a0\u00a0\u00a0\u00a0\u00a0\u00a0\u00a0\u00a0\u00a0\u00a0\u00a0\u00a0\u00a0\u00a0 Hamjambo wapenzi wasikilizaji, karibuni katika kipindi chetu.<\/p>\n<p>Leo, pamoja na wageni wetu, tutazungumzia ukatili wa majumbani, aina ya ukatili wa kijinsia, unaojulikana pia kama GBV. Watazungumza kuhusu sababu na matokeo ya ukatili wa majumbani, pamoja na hatua zinazochukuliwa na mashirika na watu binafsi kukabiliana nayo. Pia watajadili hatua zinazochukuliwa na vyama na mashirika yasiyo ya kiserikali kuondokana na vikwazo vya utekelezaji wa sheria dhidi ya aina hii ya ukatili.<\/p>\n<p>Tutazungumza na watu watatu wa muhimu sana. Wa kwanza, Bi. Aminata Traor\u00e9, ni mwathirika wa ukatili wa nyumbani na mwalimu wa shule ya binafsi huko Djoro, katika eneo la Segou. Ataeleza jinsi alivyonusurika na ukatili huu.<\/p>\n<p>Kisha tutazungumza na Bi. Mariam Traor\u00e9, mwanasheria na mtaalamu wa maswala ya ukatili wa majumbani. Atatushirikisha uzoefu wake na mbinu zinazotumiwa kuwasaidia wanawake walionusurika. Mwisho, tutamkaribisha Bw. S\u00e9gn\u00e9 Sangar\u00e9. Yeye ni mwanasaikolojia, mshauri wa afya na mwanachama wa chama cha wanasaikolojia wa Mali. Atazungumza juu ya mada hii lakini katika kona ya mtazamo wa athari za kisaikolojia za ukatili wa majumbani kwa wanawake na watoto.<\/p>\n<p><strong>MTANGAZAJI:<\/strong>\u00a0\u00a0\u00a0\u00a0\u00a0\u00a0\u00a0\u00a0\u00a0\u00a0\u00a0\u00a0\u00a0\u00a0\u00a0\u00a0\u00a0\u00a0\u00a0\u00a0\u00a0\u00a0\u00a0\u00a0\u00a0\u00a0\u00a0\u00a0\u00a0\u00a0 Karibu, Bi. Aminata Traore!<br \/>\n<strong>AMINATA TRAORE: \u00a0\u00a0\u00a0<\/strong>\u00a0\u00a0\u00a0\u00a0\u00a0\u00a0\u00a0\u00a0\u00a0\u00a0\u00a0\u00a0\u00a0\u00a0\u00a0\u00a0 Asante kwa kuwa nami.<br \/>\n<strong>MTANGAZAJI<\/strong><strong>:<\/strong>\u00a0\u00a0\u00a0\u00a0\u00a0\u00a0\u00a0\u00a0\u00a0\u00a0\u00a0\u00a0\u00a0\u00a0\u00a0\u00a0\u00a0\u00a0\u00a0\u00a0\u00a0\u00a0\u00a0\u00a0\u00a0\u00a0\u00a0\u00a0\u00a0\u00a0 Kama mnusurika wa ukatili wa nyumbani, tuambie ilivyokuwa kwako.<\/p>\n<p><strong>AMINATA TRAORE:<\/strong>\u00a0\u00a0\u00a0\u00a0\u00a0\u00a0\u00a0\u00a0\u00a0\u00a0\u00a0\u00a0\u00a0\u00a0\u00a0\u00a0\u00a0\u00a0\u00a0\u00a0 Nilimjua mume wangu wa zamani karibu miaka ishirini iliyopita. Wakati huo tulikuwa wanafunzi. Nilioana naye bila ridhaa ya wazazi wangu ambao walimwona hana adabu sana. Tangu mwanzo, alikuwa na wivu pale aliponiona nikizungumza na wanaume wengine ikiwa ni pamoja na marafiki zangu. Hakuzungumza nami kwa siku kadhaa. Hali ilizidi kuwa mbaya tulipooana. Ili kuonyesha kutofurahishwa kwake, alinipiga kwa mkanda wake. Sikuweza kuinua sauti yangu alipozungumza, vinginevyo angenipiga. Ilikuwa ngumu zaidi alipopoteza kazi yake. Ilinibidi kuvumilia kwa sababu nilikuwa nimejifungua mtoto wa kiume aliyekuwa na umri wa miaka mitano wakati huo. Lakini sikuweza kuzungumzia jambo hilo na familia yangu, kwa kuwa tayari walikuwa wakipinga ndoa yetu.<\/p>\n<p>Siku moja alinipiga na kiti kidogo cha mbao kilichokuwa ndani ya nyumba. Nilikuwa na damu kila mahali na majeraha kichwani. Lakini licha ya majeraha yangu, hakuniruhusu nilale bila kukidhi hamu yake ya ngono. Nilihisi kwamba kuniona ninalia ilikuwa furaha yake. Nilipoteza mimba mara mbili kwa sababu ya ukatili huu. Nilitarajia angebadilika, lakini hali ilikuwa inazidi kuwa mbaya.<\/p>\n<p>Miaka michache baadaye, nilipata mimba ya binti yangu. Lakini hali haikuwa bora. Kwa miaka mingi, niliteseka kwa kila aina ya ukatili nyumbani kutoka kwa mume wangu. Hakunisaidia kifedha. Kwa mshahara wangu kama mwalimu, nililazimika kulipia dawa na chakula kwa ajili ya watoto wangu na yeye. Kwa ufupi, nilitekeleza jukumu ambalo sheria ya ndoa nchini Mali inamtaka yeye kufanya. Sheria inasema kwamba mwanamume lazima amlishe na kumlinda mke wake.<\/p>\n<p>Wakati huu, hakujaribu kufanya kazi. Na niliposhindwa kubeba mizigo hiyo, alininyanyasa kimwili na kunitukana. Ukatili wa kingono, wa matusi na kimwili ambao nilivumilia ulidhorotesha afya yangu ya akili na kuniacha katika hali ya mfadhaiko, huzuni, hasira, na chuki dhidi ya wanaume kwa ujumla.<\/p>\n<p><strong>MTANGAZAJI<\/strong><strong>:<\/strong>\u00a0\u00a0\u00a0\u00a0\u00a0\u00a0\u00a0\u00a0\u00a0\u00a0\u00a0\u00a0\u00a0\u00a0\u00a0\u00a0\u00a0\u00a0\u00a0\u00a0\u00a0\u00a0\u00a0\u00a0\u00a0\u00a0\u00a0\u00a0\u00a0\u00a0 Kwa nini ulivumilia mateso haya kwa muda mrefu?<\/p>\n<p><strong>AMINATA TRAORE:<\/strong>\u00a0\u00a0\u00a0\u00a0\u00a0\u00a0\u00a0\u00a0\u00a0\u00a0\u00a0\u00a0\u00a0\u00a0\u00a0\u00a0\u00a0\u00a0\u00a0\u00a0 Nilijilaumu kwa sehemu kwa sababu ya maonyo ya familia yangu kuhusu mume wangu wa zamani. Kwa hiyo, sikuweza kulalamika kwa wazazi wangu. Pia, nchini Mali, si rahisi kwa mwanamke kumwacha mume mwenye jeuri, hasa kwa uzito wa utamaduni unaopendekeza wanawake kuwa na subira na kuvumilia.<\/p>\n<p><strong>MTANGAZAJI:<\/strong> \u00a0\u00a0\u00a0\u00a0\u00a0\u00a0\u00a0\u00a0\u00a0\u00a0\u00a0\u00a0\u00a0\u00a0\u00a0\u00a0\u00a0\u00a0\u00a0\u00a0\u00a0\u00a0\u00a0\u00a0\u00a0\u00a0\u00a0\u00a0\u00a0 Je! watoto wako walipitiaje kipindi hiki?<\/p>\n<p><strong>AMINATA TRAORE:<\/strong> \u00a0\u00a0\u00a0\u00a0\u00a0\u00a0\u00a0\u00a0\u00a0\u00a0\u00a0\u00a0\u00a0\u00a0\u00a0\u00a0\u00a0\u00a0\u00a0 Kabla ya talaka, mwanangu mwenye umri wa miaka 16 alihisi matatizo yangu. Angesimama kati ya baba yake na mimi, akijaribu kumzuia asinitusi. Hili lilinitia hofu kwa sababu mwanangu alikuwa na uwezo wa kumpiga baba yake ili kunilinda, ingawa ni marufuku kabisa katika jamii yetu. Huku machozi yakinitoka, niliendelea kumwambia amruhusu baba yake anipige. Binti yangu angelia na kuingia chumbani. Shuleni, mwanangu angeshambulia marafiki zake. Alikuwa na hasira kila wakati juu ya vitu vidogo, na binti yangu alikuwa akiogopa kila wakati.<\/p>\n<p><strong>MTANGAZAJI:<\/strong> \u00a0\u00a0\u00a0\u00a0\u00a0\u00a0\u00a0\u00a0\u00a0\u00a0\u00a0\u00a0\u00a0\u00a0\u00a0\u00a0\u00a0\u00a0\u00a0\u00a0\u00a0\u00a0\u00a0\u00a0\u00a0\u00a0\u00a0\u00a0\u00a0 Uliwezaje kupata talaka?<\/p>\n<p><strong>AMINATA TRAORE:<\/strong> \u00a0\u00a0\u00a0\u00a0\u00a0\u00a0\u00a0\u00a0\u00a0\u00a0\u00a0\u00a0\u00a0\u00a0\u00a0\u00a0\u00a0\u00a0\u00a0 Kama tunavyosema mara nyingi, inatosha. Hatimaye, alianza kulala na wahudumu wa nyumba yangu na binti za majirani zetu. Nilipomtaka aache, alinipiga kofi na kunipiga na fimbo hadi akanivunja mkono. Wakati huo, nilichukua vitu vyangu vyote na kwenda nyumbani kwa wazazi wangu. Hapo ndipo nilipoamua kuachana naye kwa sababu nilimchukia. Nilizungumza kuhusu hilo na marafiki, ambao walinishauri kuwasiliana na vyama vya utetezi wa waathiriwa wa dhuluma ili kuwasilisha malalamiko na kuomba talaka. Haikuwa rahisi kwa sababu sikujua taratibu za kufuata mahakamani. Lakini kwa msaada wa NGOs kama vile WiLDAF na marafiki zangu, nilifanikiwa kupata talaka. Sasa ninaishi nyumbani kwa wazazi wangu na watoto wangu, nikingoja kupata mahali pangu mwenyewe.<\/p>\n<p><strong>MTANGAZAJI:<\/strong> \u00a0\u00a0\u00a0\u00a0\u00a0\u00a0\u00a0\u00a0\u00a0\u00a0\u00a0\u00a0\u00a0\u00a0\u00a0\u00a0\u00a0\u00a0\u00a0\u00a0\u00a0\u00a0\u00a0\u00a0\u00a0\u00a0\u00a0\u00a0\u00a0 Una ushauri gani kwa wanawake?<\/p>\n<p><strong>AMINATA TRAORE:<\/strong>\u00a0\u00a0\u00a0\u00a0\u00a0\u00a0\u00a0\u00a0\u00a0\u00a0\u00a0\u00a0\u00a0\u00a0\u00a0\u00a0\u00a0\u00a0\u00a0\u00a0 Ningependa kuwaambia wanawake kwamba watu wote ni sawa mbele ya sheria na kwamba hakuna mtu ana haki ya kumdhuru mwingine. Mtu anaoelewa ili kuwa na furaha, na si kuwa mtumwa wa mwenzi wake. Mwanamke anapopoteza maisha, watoto wake ndio wa kwanza kuteseka. Inabidi ufanye uamuzi kabla hujachelewa. Nilikuwa na bahati ya kutoka ndani yake. Lakini ni wanawake wangapi wamekufa? Fanya uamuzi haraka, au unaweza kuwa mwathirika mwingine.<\/p>\n<p><strong>MTANGAZAJI:<\/strong> \u00a0\u00a0\u00a0\u00a0\u00a0\u00a0\u00a0\u00a0\u00a0\u00a0\u00a0\u00a0\u00a0\u00a0\u00a0\u00a0\u00a0\u00a0\u00a0\u00a0\u00a0\u00a0\u00a0\u00a0\u00a0\u00a0\u00a0\u00a0\u00a0 Asante, Aminata Traor\u00e9. Hebu tumsikie sasa Bi. Mariam Traor\u00e9, mwanasheria na mtaalamu wa masuala ya ukatili majumbani wa WiLDAF. WiLDAF Mali ni mtandao wa takriban vyama ishirini na wanachama hamsini binafsi. Inalenga kulinda na kukuza haki za wanawake na watoto.<\/p>\n<p>Asante kwa kukubali mwaliko wetu. Hivi Mariam, ukatili wa majumbani ni nini?<\/p>\n<p><strong>MARIAMTRAORE:\u00a0\u00a0 <\/strong>Ukatili wa majumbani ni aina ya tabia, vitendo, na mitazamo ya mwenza au mwenza wa zamani ambayo inalenga kumdhibiti na kumtawala mwenza wake. Ukatili huu naweza kuchukua sura ya vitisho vya maneno, kimwili, kingono, au kiuchumi au kumlazimisha mwenza mwingine.<\/p>\n<p><strong>MTANGAZAJI:<\/strong> \u00a0\u00a0\u00a0\u00a0\u00a0\u00a0\u00a0\u00a0\u00a0\u00a0\u00a0\u00a0\u00a0\u00a0\u00a0\u00a0\u00a0\u00a0\u00a0\u00a0\u00a0\u00a0\u00a0\u00a0\u00a0\u00a0\u00a0\u00a0\u00a0 Je, hali ikoje na aina hii ya ukatili nchini Mali?<\/p>\n<p><strong>MARIAM TRAORE:<\/strong> \u00a0\u00a0\u00a0\u00a0\u00a0\u00a0\u00a0\u00a0\u00a0\u00a0\u00a0\u00a0\u00a0\u00a0\u00a0\u00a0\u00a0\u00a0\u00a0\u00a0\u00a0 Nchini Mali, kama sehemu nyingine yoyote, ukatili wa majumbani unaendelea kuwa suala la kutia wasiwasi. Tunaishi katika jamii yenye mfumo dume sana. Mume anaonekana kama mkuu wa kaya. Mzigo wa kaya unamwangukia yeye. Ama mke anatarajiwa kumtii mumewe. Ukosefu huu wa usawa mara nyingi husababisha ukatili wa ndani ya nyumba.<\/p>\n<p>Kwa mfano, tumeona kwamba baadhi ya wanawake wanaona vigumu kuendelea na masomo au taaluma zao baada ya kuolewa kwa sababu ya upinzani kutoka kwa waume zao. Kulingana na takwimu, mwanamke mmoja kati ya kila wanawake wawili wenye umri wa miaka 15 hadi 49 nchini Mali amekumbana na ukatili wa kimwili, kihisia, au kingono angalau mara moja katika maisha yake. Idadi sawa ya wanawake pia wanakabiliwa na ukatili wa kihisia au kimwili wakati wa kutengana.<\/p>\n<p>Kwa bahati mbaya, muktadha wa kijamii mara nyingi humlazimisha mwanamke kumvumilia na hata kumsamehe mwenzi wake kwa ukatili huu. Wale wanaoacha nyumba zao wananyanyapaliwa na jamii. Lakini jeuri, mateso anayowekewa mwenzi mwingine, huharibu upatano wa maisha ya ndoa na kuleta changamoto katika hatima ya watoto wa wanandoa hao.<\/p>\n<p>Mashirika ya kutetea haki za binadamu nchini Mali yanakashifu ukatili wa majumbani kwa namna zote. Lakini pamoja na wito wa mara kwa mara wa mageuzi, maendeleo kidogo yanafanywa katika kushughulikia aina hii ya ukatili kwa utaratibu na ufanisi.<\/p>\n<p><strong>MTANGAZAJI:<\/strong>\u00a0\u00a0\u00a0\u00a0\u00a0\u00a0\u00a0\u00a0\u00a0\u00a0\u00a0\u00a0\u00a0\u00a0\u00a0\u00a0\u00a0\u00a0\u00a0\u00a0\u00a0\u00a0\u00a0\u00a0\u00a0\u00a0\u00a0\u00a0\u00a0\u00a0 Je, ni sababu gani zinasababisha ukatili wa majumbani nchini Mali?<\/p>\n<p><strong>MARIAM\u00a0TRAORE: \u00a0\u00a0\u00a0\u00a0\u00a0\u00a0\u00a0\u00a0\u00a0\u00a0\u00a0\u00a0\u00a0\u00a0\u00a0\u00a0\u00a0\u00a0\u00a0\u00a0\u00a0 <\/strong>Ukatili wa nyumbani una sababu nyingi. Kuna sababu ya elimu. Watoto huiga tabia hii wanapolelewa katika mazingira ambayo matatizo yote hutatuliwa kwa nguvu, iwe shuleni au katika familia.<\/p>\n<p>Katika jamii ya Mali, dhana nyingi potofu zinahusishwa na mke ambazo si halali kwa mama, dada, na binti. Kwa mfano, nampenda mama yangu, nampenda dada yangu, nampenda binti yangu, lakini sipaswi kumuamini mke wangu.<\/p>\n<p>Hivi karibuni, ukatili hutokea wakati kuna upendeleo dhidi ya wanawake. Katika jamii ya Mali, kijadi mwanamume anachukuliwa kuwa muhimu zaidi kwa sababu ndiye anayeoa mwanamke, kulisha familia, na kuitunza. Hata katika kugawana mali ya familia, kwa mujibu wa desturi zetu, mwanamume hupokea sehemu mara mbili ya mwanamke. Kwa hivyo, ikiwa wanaume wanadhani kuwa wanawake wana hadhi ya chini, au kwamba wanawake hawana mamlaka sawa na wanaume, wanawake watatendewa kwa ukatili. Kimsingi, ukatili wa nyumbani ni matokeo ya ukosefu wa usawa wa kijamii.<\/p>\n<p><strong>MTANGAZAJI<\/strong><strong>:<\/strong>\u00a0\u00a0\u00a0\u00a0\u00a0\u00a0\u00a0\u00a0\u00a0\u00a0\u00a0\u00a0\u00a0\u00a0\u00a0\u00a0\u00a0\u00a0\u00a0\u00a0\u00a0\u00a0\u00a0\u00a0\u00a0\u00a0\u00a0\u00a0\u00a0\u00a0 Je, shirika lako linafanya nini kuwasaidia wanawake walionusurika na ukatili?<\/p>\n<p><strong>MARIAM\u00a0TRAORE:<\/strong>\u00a0\u00a0\u00a0\u00a0\u00a0\u00a0\u00a0\u00a0\u00a0\u00a0\u00a0\u00a0\u00a0\u00a0\u00a0\u00a0\u00a0\u00a0\u00a0\u00a0\u00a0\u00a0 Mashirika kadhaa ya haki za wanawake hutoa msaada wa kisheria na kijamii kwa wanawake walionusurika na ukatili wa majumbani. Sisi wenyewe tuna makazi ya wanawake na watoto walio katika dhiki. Wakati huo huo, kuna warsha za kisheria kusaidia wanawake kuwasilisha malalamiko. Waathirika wanaweza pia kufaidika na usaidizi wa wanasaikolojia, ambao huwasikiliza na kuwahakikishia usalama wao. Kisha tunapanga warsha kwa ajili ya mafunzo, uhamasishaji, na taarifa juu ya haki za wanawake na juu ya sheria zinazowalinda wanawake dhidi ya ukatili wa majumbani.<\/p>\n<p><strong>MTANGAZAJI:<\/strong> \u00a0\u00a0\u00a0\u00a0\u00a0\u00a0\u00a0\u00a0\u00a0\u00a0\u00a0\u00a0\u00a0\u00a0\u00a0\u00a0\u00a0\u00a0\u00a0\u00a0\u00a0\u00a0\u00a0\u00a0\u00a0\u00a0\u00a0\u00a0 Ni nini kinafanya iwe vigumu kutekeleza sheria dhidi ya ukatili wa majumbani nchini Mali?<\/p>\n<p><strong>MARIAM\u00a0TRAORE:<\/strong>\u00a0\u00a0\u00a0\u00a0\u00a0\u00a0\u00a0\u00a0\u00a0\u00a0\u00a0\u00a0\u00a0\u00a0\u00a0\u00a0\u00a0\u00a0\u00a0\u00a0 Wahalifu wengi wa ukatili wa majumbani wanaamini kwamba sheria haipaswi kuingilia maisha yao ya ndoa. Waathiriwa wa ukatili wa majumbani huhisi hatia kwa sababu wanasadiki kwamba wamefanya jambo baya. Kwa hiyo, wale wanaokumbana na ukatili kila siku huficha, hupunguza, au hufikiri kwamba ukatili huo ni wa muda tu kwa sababu wanaamini kwamba mtendaji atabadilika punde au baadaye.<\/p>\n<p>Manusura wa ukatili wa majumbani wanataka ukatili huo ukomeshwe, lakini mara nyingi hawataki kuchukua hatua za kisheria dhidi ya mhusika. Pia, shinikizo la kijamii kutoka kwa watoto au familia zote mbili linaweza kumzuia muathiriwa kuchukua hatua za kisheria dhidi ya mwenzi anayemwacha, kumtukana, au kumpiga. Wanawake wa Mali wanashikamana sana na maisha yao ya ndoa na mustakabali wa watoto wao na wanaweza kusadikishwa kwamba wanapaswa kuwavumilia kupita kiasi wenzi wao kwa muda mrefu kabla ya kuamua kuvunja ndoa zao.<\/p>\n<p><strong>MTANGAZAJI:<\/strong>\u00a0\u00a0\u00a0\u00a0\u00a0\u00a0\u00a0\u00a0\u00a0\u00a0\u00a0\u00a0\u00a0\u00a0\u00a0\u00a0\u00a0\u00a0\u00a0\u00a0\u00a0\u00a0\u00a0\u00a0\u00a0\u00a0\u00a0\u00a0\u00a0\u00a0 Je, itakuwaje kama sheria dhidi ya ukatili wa majumbani ikitekelezwa?<\/p>\n<p><strong>MARIAM TRAORE:<\/strong> \u00a0\u00a0\u00a0\u00a0\u00a0\u00a0\u00a0\u00a0\u00a0\u00a0\u00a0\u00a0\u00a0\u00a0\u00a0\u00a0\u00a0\u00a0\u00a0\u00a0\u00a0 Katiba yetu imeweka fursa sawa kati ya wanaume na wanawake. Baadhi ya aina za ukatili wa kimwili na kingono zinaadhibiwa na sheria. Kuna haja ya kutekeleza sheria kwa kuongeza shughuli zinazoongeza ufahamu kuhusu matokeo ya ukatili wa majumbani. Ni lazima pia tuunde mfumo wa kitaifa wa kuwalinda walionusurika na kuadhibu vikali ukatili wa majumbani.<\/p>\n<p>Kwa mfano, kuboreshwa kwa upatikanaji wa elimu kwa wasichana, fursa zaidi za kuzalisha kipato kwa wanawake, na uwakilishi bora wa wanawake katika maeneo yote ya sekta ya umma na binafsi, ikiwa ni pamoja na katika nafasi za uongozi, inaweza kuwa na manufaa. Chochote ambacho wanaume wanaweza kufanya, wanawake wanaweza pia kufanya mahali pa kazi. Wanawake na wanaume lazima washirikiane kwa maendeleo ya taifa.<\/p>\n<p><strong>MTANGAZAJI: <\/strong>\u00a0\u00a0\u00a0\u00a0\u00a0\u00a0\u00a0\u00a0\u00a0\u00a0\u00a0\u00a0\u00a0\u00a0\u00a0\u00a0\u00a0\u00a0\u00a0\u00a0\u00a0\u00a0\u00a0\u00a0\u00a0\u00a0\u00a0\u00a0\u00a0 Asante sana, Mariam. Sasa tunamgeukia S\u00e9gn\u00e9 Sangar\u00e9, mwanasaikolojia, mshauri wa afya, na mwanachama wa Chama cha Wanasaikolojia wa Mali.<\/p>\n<p>Bwana Sangar\u00e9, ni nini huwafanya baadhi ya wanaume kuwa wakatili dhidi ya wapenzi wao?<\/p>\n<p><strong>SANGARE\u00a0SEGNE: <\/strong>\u00a0\u00a0\u00a0\u00a0\u00a0\u00a0\u00a0\u00a0\u00a0\u00a0\u00a0\u00a0\u00a0\u00a0\u00a0\u00a0\u00a0\u00a0\u00a0\u00a0\u00a0 Wanaume wengine kwa asili wana hasira kali na wana uwezekano mkubwa wa kuwa na ukatili. Katika utamaduni wa Mali, mwanamume anaweza kufikiri kuwa ni &#8220;kawaida&#8221; kumtawala mke wake. Ikiwa hana utulivu, anamrudisha kwenye mstari. Wanaume hawa wanapowapiga wake zao, lengo ni kumfanya anyenyekee. Ikiwa mwanamke anakataa, inaweza kuwa ngumu, na hata mbaya kwa ajili yake. Lakini sababu za ukatili wa majumbani ni tofauti. Zinaweza kutokana na malezi yetu, kutokana na chuki za jamii dhidi ya wanawake, na kutokana na faida wanazopewa wanaume dhidi ya wanawake katika jamii yetu.<\/p>\n<p><strong>MTANGAZAJI: <\/strong>\u00a0\u00a0\u00a0\u00a0\u00a0\u00a0\u00a0\u00a0\u00a0\u00a0\u00a0\u00a0\u00a0\u00a0\u00a0\u00a0\u00a0\u00a0\u00a0\u00a0\u00a0\u00a0\u00a0\u00a0\u00a0\u00a0\u00a0\u00a0\u00a0 Kwa nini wanawake waliofanyiwa ukatili wanakataa kuwaacha wapenzi wao?<\/p>\n<p><strong>SANGARE\u00a0SEGNE:<\/strong>\u00a0\u00a0\u00a0\u00a0\u00a0\u00a0\u00a0\u00a0\u00a0\u00a0\u00a0\u00a0\u00a0\u00a0\u00a0\u00a0\u00a0\u00a0\u00a0\u00a0\u00a0\u00a0\u00a0 Kuna sababu kadhaa kwa nini wanawake walionusurika wanakataa kuondoka. Kwanza, jamii inaamini kwamba wanawake lazima wateseke ili watoto wao wafanikiwe katika maisha yao. Kuna sababu nyingine kadhaa. Waathirika mara nyingi huhisi aibu, hatia, na hawana nguvu. Wanaogopa kwamba wengine watawahukumu na wasiamini hadithi yao. Wanafikiri kwamba mtu huyo anaweza kubadilika, kwa sababu ameahidi.<\/p>\n<p>Wanaogopa vitisho vyake na mustakabali wa watoto wao. Wanaogopa matokeo ikiwa wangemwacha. Wanaogopa kupoteza kile ambacho wametumia miaka mingi kujenga. Wanaamini kuwa hawawezi kufanya hivyo peke yao. Wanahisi kuwajibika kwa &#8220;kuvunja&#8221; familia. Wanapuuza sheria zinazowalinda au wanaamini kwamba sheria haziwezi kuwalinda. Wanawapenda waume zao, lakini si tabia zao za ukatili.<\/p>\n<p>Kwa sababu hiyo, wananaswa, si kwa sababu ya imani yao tu bali pia kwa sababu ya mitazamo yao.<\/p>\n<p><strong>MTANGAZAJI:<\/strong>\u00a0\u00a0\u00a0\u00a0\u00a0\u00a0\u00a0\u00a0\u00a0\u00a0\u00a0\u00a0\u00a0\u00a0\u00a0\u00a0\u00a0\u00a0\u00a0\u00a0\u00a0\u00a0\u00a0\u00a0\u00a0\u00a0\u00a0\u00a0\u00a0\u00a0 Je, ni matokeo gani kwa wanawake walionusurika na ukatili wa majumbani na watoto wao?<\/p>\n<p><strong>SANGARE\u00a0SEGNE: <\/strong>\u00a0\u00a0\u00a0\u00a0\u00a0\u00a0\u00a0\u00a0\u00a0\u00a0\u00a0\u00a0\u00a0\u00a0\u00a0\u00a0\u00a0\u00a0\u00a0\u00a0\u00a0\u00a0 Ukatili wa majumbani unaweza kudhoofisha uwezo wa baadhi ya wanawake kujiamini. Wanawake hawa hawawezi tena kufanya chochote peke yao, na lazima waongozwe kila wakati. Wanahisi kudhalilishwa na kuchanganyikiwa. Wanateseka kwa kukosa usingizi na kuteseka sana kijamii kwa sababu ya shinikizo la waume zao.<\/p>\n<p>Mambo ni magumu zaidi kwa watoto. Wanaishi katika muktadha unaotegemea utawala na uchokozi. Wanakabiliwa na chaguo kati ya wazazi wao na wanaishi kwa uchungu. Pia, ukatili haizungumzwi sana ndani ya familia. Ukimya na mwiko unaozingira hali hizi kwa ujumla unamaanisha kwamba watoto hawapati maelezo ya vitendo wanavyoviona na kufanyiwa. Hivyo, hawana fursa ya kueleza hisia zao, au kuhakikishiwa. Wakiachwa katika hali ya dhiki na mshtuko, watoto hawa wanaweza kuendeleza matatizo ya kihisia na kitabia ambayo yataathiri ukuaji wao.<\/p>\n<p><strong>MTANGAZAJI:<\/strong>\u00a0\u00a0\u00a0\u00a0\u00a0\u00a0\u00a0\u00a0\u00a0\u00a0\u00a0\u00a0\u00a0\u00a0\u00a0\u00a0\u00a0\u00a0\u00a0\u00a0\u00a0\u00a0\u00a0\u00a0\u00a0\u00a0\u00a0\u00a0\u00a0\u00a0 Je, Waathirika wa ukatili wanaotafuta huduma zako wana umri gani?<\/p>\n<p><strong>SANGARE SEGNE:<\/strong> \u00a0\u00a0\u00a0\u00a0\u00a0\u00a0\u00a0\u00a0\u00a0\u00a0\u00a0\u00a0\u00a0\u00a0\u00a0\u00a0\u00a0\u00a0\u00a0\u00a0\u00a0\u00a0 Ni wanawake wa rika zote. Lakini kwa kawaida ni wanawake ambao wamekuwa kwenye uhusiano kwa zaidi ya miaka mitano. Mwanamke mkubwa zaidi niliyewahi kumsaidia alikuwa na umri wa miaka 63 na alikuwa katika uhusiano kwa miaka 45. Alikuwa mwathirika wa ukatili wa kimwili.<\/p>\n<p><strong>MTANGAZAJI: <\/strong>\u00a0\u00a0\u00a0\u00a0\u00a0\u00a0\u00a0\u00a0\u00a0\u00a0\u00a0\u00a0\u00a0\u00a0\u00a0\u00a0\u00a0\u00a0\u00a0\u00a0\u00a0\u00a0\u00a0\u00a0\u00a0\u00a0\u00a0\u00a0\u00a0 Je, unaweza kusema nini kuhitimisha mahojiano haya?<\/p>\n<p><strong>SANGARE SEGNE:\u00a0\u00a0\u00a0\u00a0\u00a0\u00a0\u00a0\u00a0\u00a0\u00a0\u00a0\u00a0\u00a0\u00a0\u00a0\u00a0\u00a0\u00a0\u00a0\u00a0\u00a0\u00a0\u00a0 <\/strong>Ningesema kwa wanawake ambao ni waathiriwa wa ukatili wa majumbani kwamba tuko pamoja nao mchana na usiku. Ingawa ni vigumu kutekeleza sheria nchini Mali, ingawa jamii tunamoishi haiwapendezi sana, bado kuna matumaini kwa sababu ya vyama na mashirika yasiyo ya kiserikali. Daima husikiliza na kufanya kila wawezalo kwa ajili ya wanawake na watoto.<\/p>\n<p><strong>MTANGAZAJI:\u00a0\u00a0\u00a0\u00a0\u00a0\u00a0\u00a0\u00a0\u00a0\u00a0\u00a0\u00a0\u00a0\u00a0\u00a0\u00a0\u00a0\u00a0\u00a0\u00a0\u00a0\u00a0\u00a0\u00a0\u00a0\u00a0\u00a0\u00a0\u00a0 <\/strong>Asante kwa maelezo yako, Bw. Sangar\u00e9. Asante pia Bi. Aminata Traor\u00e9 na Bi. Mariam Traor\u00e9 kwa michango yao.<\/p>\n<p>Ukatili dhidi ya wanawake ni pamoja na ukatili wa kimwili, lakini pia ukatili wa kiuchumi, kingono na kisaikolojia. Inaathiri jamii zote, zilizoendelea au zinazoendelea, na tabaka zote za kijamii. Matokeo yake ni mabaya kwa jamii kwa ujumla.<\/p>\n<p>Tumefika mwisho wa programu ya leo. Asante kwa wageni wetu wote na kwa kila mtu anayesikiliza. Tutarudi hivi karibuni kwa programu nyingine.<\/p>\n","protected":false},"excerpt":{"rendered":"<p>MTANGAZAJI: \u00a0\u00a0\u00a0\u00a0\u00a0\u00a0\u00a0\u00a0\u00a0\u00a0\u00a0\u00a0\u00a0\u00a0\u00a0\u00a0\u00a0\u00a0\u00a0\u00a0\u00a0\u00a0\u00a0\u00a0\u00a0\u00a0\u00a0\u00a0\u00a0 Hamjambo wapenzi wasikilizaji, karibuni katika kipindi chetu. Leo, pamoja na wageni wetu, tutazungumzia ukatili wa majumbani, aina ya ukatili wa kijinsia, unaojulikana pia kama GBV. Watazungumza kuhusu sababu na matokeo ya ukatili wa majumbani, pamoja na hatua zinazochukuliwa na mashirika na watu binafsi kukabiliana nayo. Pia watajadili hatua zinazochukuliwa na vyama na mashirika&hellip;<\/p>\n","protected":false},"author":185,"featured_media":0,"parent":0,"menu_order":0,"template":"","meta":{"footnotes":"","beyondwords_generate_audio":"","beyondwords_project_id":"","beyondwords_content_id":"","beyondwords_integration_method":"","beyondwords_language_code":"","beyondwords_language_id":"","beyondwords_body_voice_id":"","beyondwords_delete_content":"","beyondwords_source":"","beyondwords_output":"","beyondwords_script_template_id":"","beyondwords_video_template_id":"","beyondwords_video_size":"","beyondwords_embed":"","beyondwords_podcast_id":"","speechkit_generate_audio":"","speechkit_project_id":"","speechkit_podcast_id":""},"script-format":[],"package":[],"script-category":[],"class_list":["post-39259","radio-script","type-radio-script","status-publish","hentry"],"acf":[],"yoast_head":"<!-- This site is optimized with the Yoast SEO plugin v28.9 - https:\/\/yoast.com\/product\/yoast-seo-wordpress\/ -->\n<title>Ukatili Majumbani: Sababu na matokeo yake - Farm Radio International<\/title>\n<meta name=\"robots\" content=\"index, follow, max-snippet:-1, max-image-preview:large, max-video-preview:-1\" \/>\n<link rel=\"canonical\" href=\"https:\/\/scripts.farmradio.fm\/sw\/mwongozo-wa-redio\/ukatili-majumbani-sababu-na-matokeo-yake\/\" \/>\n<meta property=\"og:locale\" content=\"en_US\" \/>\n<meta property=\"og:type\" content=\"article\" \/>\n<meta property=\"og:title\" content=\"Ukatili Majumbani: Sababu na matokeo yake - Farm Radio International\" \/>\n<meta property=\"og:description\" content=\"MTANGAZAJI: \u00a0\u00a0\u00a0\u00a0\u00a0\u00a0\u00a0\u00a0\u00a0\u00a0\u00a0\u00a0\u00a0\u00a0\u00a0\u00a0\u00a0\u00a0\u00a0\u00a0\u00a0\u00a0\u00a0\u00a0\u00a0\u00a0\u00a0\u00a0\u00a0 Hamjambo wapenzi wasikilizaji, karibuni katika kipindi chetu. Leo, pamoja na wageni wetu, tutazungumzia ukatili wa majumbani, aina ya ukatili wa kijinsia, unaojulikana pia kama GBV. Watazungumza kuhusu sababu na matokeo ya ukatili wa majumbani, pamoja na hatua zinazochukuliwa na mashirika na watu binafsi kukabiliana nayo. Pia watajadili hatua zinazochukuliwa na vyama na mashirika&hellip;\" \/>\n<meta property=\"og:url\" content=\"https:\/\/scripts.farmradio.fm\/sw\/mwongozo-wa-redio\/ukatili-majumbani-sababu-na-matokeo-yake\/\" \/>\n<meta property=\"og:site_name\" content=\"Farm Radio International\" \/>\n<meta property=\"article:publisher\" content=\"https:\/\/www.facebook.com\/farmradio\/\" \/>\n<meta property=\"article:modified_time\" content=\"2023-08-28T18:51:00+00:00\" \/>\n<meta name=\"twitter:card\" content=\"summary_large_image\" \/>\n<meta name=\"twitter:site\" content=\"@farmradio\" \/>\n<meta name=\"twitter:label1\" content=\"Est. reading time\" \/>\n\t<meta name=\"twitter:data1\" content=\"11 minutes\" \/>\n<script type=\"application\/ld+json\" class=\"yoast-schema-graph\">{\"@context\":\"https:\\\/\\\/schema.org\",\"@graph\":[{\"@type\":\"Article\",\"@id\":\"https:\\\/\\\/scripts.farmradio.fm\\\/sw\\\/mwongozo-wa-redio\\\/ukatili-majumbani-sababu-na-matokeo-yake\\\/#article\",\"isPartOf\":{\"@id\":\"https:\\\/\\\/scripts.farmradio.fm\\\/sw\\\/mwongozo-wa-redio\\\/ukatili-majumbani-sababu-na-matokeo-yake\\\/\"},\"author\":{\"name\":\"Kathryn Burnham\",\"@id\":\"http:\\\/\\\/scripts.farmradio.fm\\\/sw\\\/#\\\/schema\\\/person\\\/03d3c3f4ee736655dd05a7e6d3d22ba5\"},\"headline\":\"Ukatili Majumbani: Sababu na matokeo yake\",\"datePublished\":\"2022-10-13T14:12:00+00:00\",\"dateModified\":\"2023-08-28T18:51:00+00:00\",\"mainEntityOfPage\":{\"@id\":\"https:\\\/\\\/scripts.farmradio.fm\\\/sw\\\/mwongozo-wa-redio\\\/ukatili-majumbani-sababu-na-matokeo-yake\\\/\"},\"wordCount\":2247,\"publisher\":{\"@id\":\"http:\\\/\\\/scripts.farmradio.fm\\\/sw\\\/#organization\"},\"inLanguage\":\"sw-CG\"},{\"@type\":\"WebPage\",\"@id\":\"https:\\\/\\\/scripts.farmradio.fm\\\/sw\\\/mwongozo-wa-redio\\\/ukatili-majumbani-sababu-na-matokeo-yake\\\/\",\"url\":\"https:\\\/\\\/scripts.farmradio.fm\\\/sw\\\/mwongozo-wa-redio\\\/ukatili-majumbani-sababu-na-matokeo-yake\\\/\",\"name\":\"Ukatili Majumbani: Sababu na matokeo yake - Farm Radio International\",\"isPartOf\":{\"@id\":\"http:\\\/\\\/scripts.farmradio.fm\\\/sw\\\/#website\"},\"datePublished\":\"2022-10-13T14:12:00+00:00\",\"dateModified\":\"2023-08-28T18:51:00+00:00\",\"breadcrumb\":{\"@id\":\"https:\\\/\\\/scripts.farmradio.fm\\\/sw\\\/mwongozo-wa-redio\\\/ukatili-majumbani-sababu-na-matokeo-yake\\\/#breadcrumb\"},\"inLanguage\":\"sw-CG\",\"potentialAction\":[{\"@type\":\"ReadAction\",\"target\":[\"https:\\\/\\\/scripts.farmradio.fm\\\/sw\\\/mwongozo-wa-redio\\\/ukatili-majumbani-sababu-na-matokeo-yake\\\/\"]}]},{\"@type\":\"BreadcrumbList\",\"@id\":\"https:\\\/\\\/scripts.farmradio.fm\\\/sw\\\/mwongozo-wa-redio\\\/ukatili-majumbani-sababu-na-matokeo-yake\\\/#breadcrumb\",\"itemListElement\":[{\"@type\":\"ListItem\",\"position\":1,\"name\":\"Nyumbani\",\"item\":\"http:\\\/\\\/scripts.farmradio.fm\\\/sw\\\/\"},{\"@type\":\"ListItem\",\"position\":2,\"name\":\"Ukatili Majumbani: Sababu na matokeo yake\"}]},{\"@type\":\"WebSite\",\"@id\":\"http:\\\/\\\/scripts.farmradio.fm\\\/sw\\\/#website\",\"url\":\"http:\\\/\\\/scripts.farmradio.fm\\\/sw\\\/\",\"name\":\"Farm Radio International\",\"description\":\"Sharing knowledge, giving voice.\",\"publisher\":{\"@id\":\"http:\\\/\\\/scripts.farmradio.fm\\\/sw\\\/#organization\"},\"potentialAction\":[{\"@type\":\"SearchAction\",\"target\":{\"@type\":\"EntryPoint\",\"urlTemplate\":\"http:\\\/\\\/scripts.farmradio.fm\\\/sw\\\/?s={search_term_string}\"},\"query-input\":{\"@type\":\"PropertyValueSpecification\",\"valueRequired\":true,\"valueName\":\"search_term_string\"}}],\"inLanguage\":\"sw-CG\"},{\"@type\":\"Organization\",\"@id\":\"http:\\\/\\\/scripts.farmradio.fm\\\/sw\\\/#organization\",\"name\":\"Farm Radio International\",\"url\":\"http:\\\/\\\/scripts.farmradio.fm\\\/sw\\\/\",\"logo\":{\"@type\":\"ImageObject\",\"inLanguage\":\"sw-CG\",\"@id\":\"http:\\\/\\\/scripts.farmradio.fm\\\/sw\\\/#\\\/schema\\\/logo\\\/image\\\/\",\"url\":\"https:\\\/\\\/scripts.farmradio.fm\\\/wp-content\\\/uploads\\\/farmRadioLogo.jpg\",\"contentUrl\":\"https:\\\/\\\/scripts.farmradio.fm\\\/wp-content\\\/uploads\\\/farmRadioLogo.jpg\",\"width\":200,\"height\":75,\"caption\":\"Farm Radio International\"},\"image\":{\"@id\":\"http:\\\/\\\/scripts.farmradio.fm\\\/sw\\\/#\\\/schema\\\/logo\\\/image\\\/\"},\"sameAs\":[\"https:\\\/\\\/www.facebook.com\\\/farmradio\\\/\",\"https:\\\/\\\/x.com\\\/farmradio\",\"https:\\\/\\\/www.instagram.com\\\/farmradio\\\/\",\"https:\\\/\\\/www.youtube.com\\\/user\\\/FarmRadioInt\"]},{\"@type\":\"Person\",\"@id\":\"http:\\\/\\\/scripts.farmradio.fm\\\/sw\\\/#\\\/schema\\\/person\\\/03d3c3f4ee736655dd05a7e6d3d22ba5\",\"name\":\"Kathryn Burnham\",\"image\":{\"@type\":\"ImageObject\",\"inLanguage\":\"sw-CG\",\"@id\":\"https:\\\/\\\/secure.gravatar.com\\\/avatar\\\/dbc5650c6499e1a82da60a08f70ed88bb2ad5dd756dd7367b88887d0839b5747?s=96&d=mm&r=g\",\"url\":\"https:\\\/\\\/secure.gravatar.com\\\/avatar\\\/dbc5650c6499e1a82da60a08f70ed88bb2ad5dd756dd7367b88887d0839b5747?s=96&d=mm&r=g\",\"contentUrl\":\"https:\\\/\\\/secure.gravatar.com\\\/avatar\\\/dbc5650c6499e1a82da60a08f70ed88bb2ad5dd756dd7367b88887d0839b5747?s=96&d=mm&r=g\",\"caption\":\"Kathryn Burnham\"}}]}<\/script>\n<!-- \/ Yoast SEO plugin. -->","yoast_head_json":{"title":"Ukatili Majumbani: Sababu na matokeo yake - Farm Radio International","robots":{"index":"index","follow":"follow","max-snippet":"max-snippet:-1","max-image-preview":"max-image-preview:large","max-video-preview":"max-video-preview:-1"},"canonical":"https:\/\/scripts.farmradio.fm\/sw\/mwongozo-wa-redio\/ukatili-majumbani-sababu-na-matokeo-yake\/","og_locale":"en_US","og_type":"article","og_title":"Ukatili Majumbani: Sababu na matokeo yake - Farm Radio International","og_description":"MTANGAZAJI: \u00a0\u00a0\u00a0\u00a0\u00a0\u00a0\u00a0\u00a0\u00a0\u00a0\u00a0\u00a0\u00a0\u00a0\u00a0\u00a0\u00a0\u00a0\u00a0\u00a0\u00a0\u00a0\u00a0\u00a0\u00a0\u00a0\u00a0\u00a0\u00a0 Hamjambo wapenzi wasikilizaji, karibuni katika kipindi chetu. Leo, pamoja na wageni wetu, tutazungumzia ukatili wa majumbani, aina ya ukatili wa kijinsia, unaojulikana pia kama GBV. Watazungumza kuhusu sababu na matokeo ya ukatili wa majumbani, pamoja na hatua zinazochukuliwa na mashirika na watu binafsi kukabiliana nayo. Pia watajadili hatua zinazochukuliwa na vyama na mashirika&hellip;","og_url":"https:\/\/scripts.farmradio.fm\/sw\/mwongozo-wa-redio\/ukatili-majumbani-sababu-na-matokeo-yake\/","og_site_name":"Farm Radio International","article_publisher":"https:\/\/www.facebook.com\/farmradio\/","article_modified_time":"2023-08-28T18:51:00+00:00","twitter_card":"summary_large_image","twitter_site":"@farmradio","twitter_misc":{"Est. reading time":"11 minutes"},"schema":{"@context":"https:\/\/schema.org","@graph":[{"@type":"Article","@id":"https:\/\/scripts.farmradio.fm\/sw\/mwongozo-wa-redio\/ukatili-majumbani-sababu-na-matokeo-yake\/#article","isPartOf":{"@id":"https:\/\/scripts.farmradio.fm\/sw\/mwongozo-wa-redio\/ukatili-majumbani-sababu-na-matokeo-yake\/"},"author":{"name":"Kathryn Burnham","@id":"http:\/\/scripts.farmradio.fm\/sw\/#\/schema\/person\/03d3c3f4ee736655dd05a7e6d3d22ba5"},"headline":"Ukatili Majumbani: Sababu na matokeo yake","datePublished":"2022-10-13T14:12:00+00:00","dateModified":"2023-08-28T18:51:00+00:00","mainEntityOfPage":{"@id":"https:\/\/scripts.farmradio.fm\/sw\/mwongozo-wa-redio\/ukatili-majumbani-sababu-na-matokeo-yake\/"},"wordCount":2247,"publisher":{"@id":"http:\/\/scripts.farmradio.fm\/sw\/#organization"},"inLanguage":"sw-CG"},{"@type":"WebPage","@id":"https:\/\/scripts.farmradio.fm\/sw\/mwongozo-wa-redio\/ukatili-majumbani-sababu-na-matokeo-yake\/","url":"https:\/\/scripts.farmradio.fm\/sw\/mwongozo-wa-redio\/ukatili-majumbani-sababu-na-matokeo-yake\/","name":"Ukatili Majumbani: Sababu na matokeo yake - Farm Radio International","isPartOf":{"@id":"http:\/\/scripts.farmradio.fm\/sw\/#website"},"datePublished":"2022-10-13T14:12:00+00:00","dateModified":"2023-08-28T18:51:00+00:00","breadcrumb":{"@id":"https:\/\/scripts.farmradio.fm\/sw\/mwongozo-wa-redio\/ukatili-majumbani-sababu-na-matokeo-yake\/#breadcrumb"},"inLanguage":"sw-CG","potentialAction":[{"@type":"ReadAction","target":["https:\/\/scripts.farmradio.fm\/sw\/mwongozo-wa-redio\/ukatili-majumbani-sababu-na-matokeo-yake\/"]}]},{"@type":"BreadcrumbList","@id":"https:\/\/scripts.farmradio.fm\/sw\/mwongozo-wa-redio\/ukatili-majumbani-sababu-na-matokeo-yake\/#breadcrumb","itemListElement":[{"@type":"ListItem","position":1,"name":"Nyumbani","item":"http:\/\/scripts.farmradio.fm\/sw\/"},{"@type":"ListItem","position":2,"name":"Ukatili Majumbani: Sababu na matokeo yake"}]},{"@type":"WebSite","@id":"http:\/\/scripts.farmradio.fm\/sw\/#website","url":"http:\/\/scripts.farmradio.fm\/sw\/","name":"Farm Radio International","description":"Sharing knowledge, giving voice.","publisher":{"@id":"http:\/\/scripts.farmradio.fm\/sw\/#organization"},"potentialAction":[{"@type":"SearchAction","target":{"@type":"EntryPoint","urlTemplate":"http:\/\/scripts.farmradio.fm\/sw\/?s={search_term_string}"},"query-input":{"@type":"PropertyValueSpecification","valueRequired":true,"valueName":"search_term_string"}}],"inLanguage":"sw-CG"},{"@type":"Organization","@id":"http:\/\/scripts.farmradio.fm\/sw\/#organization","name":"Farm Radio International","url":"http:\/\/scripts.farmradio.fm\/sw\/","logo":{"@type":"ImageObject","inLanguage":"sw-CG","@id":"http:\/\/scripts.farmradio.fm\/sw\/#\/schema\/logo\/image\/","url":"https:\/\/scripts.farmradio.fm\/wp-content\/uploads\/farmRadioLogo.jpg","contentUrl":"https:\/\/scripts.farmradio.fm\/wp-content\/uploads\/farmRadioLogo.jpg","width":200,"height":75,"caption":"Farm Radio International"},"image":{"@id":"http:\/\/scripts.farmradio.fm\/sw\/#\/schema\/logo\/image\/"},"sameAs":["https:\/\/www.facebook.com\/farmradio\/","https:\/\/x.com\/farmradio","https:\/\/www.instagram.com\/farmradio\/","https:\/\/www.youtube.com\/user\/FarmRadioInt"]},{"@type":"Person","@id":"http:\/\/scripts.farmradio.fm\/sw\/#\/schema\/person\/03d3c3f4ee736655dd05a7e6d3d22ba5","name":"Kathryn Burnham","image":{"@type":"ImageObject","inLanguage":"sw-CG","@id":"https:\/\/secure.gravatar.com\/avatar\/dbc5650c6499e1a82da60a08f70ed88bb2ad5dd756dd7367b88887d0839b5747?s=96&d=mm&r=g","url":"https:\/\/secure.gravatar.com\/avatar\/dbc5650c6499e1a82da60a08f70ed88bb2ad5dd756dd7367b88887d0839b5747?s=96&d=mm&r=g","contentUrl":"https:\/\/secure.gravatar.com\/avatar\/dbc5650c6499e1a82da60a08f70ed88bb2ad5dd756dd7367b88887d0839b5747?s=96&d=mm&r=g","caption":"Kathryn Burnham"}}]}},"_links":{"self":[{"href":"https:\/\/scripts.farmradio.fm\/sw\/wp-json\/wp\/v2\/radio-script\/39259","targetHints":{"allow":["GET"]}}],"collection":[{"href":"https:\/\/scripts.farmradio.fm\/sw\/wp-json\/wp\/v2\/radio-script"}],"about":[{"href":"https:\/\/scripts.farmradio.fm\/sw\/wp-json\/wp\/v2\/types\/radio-script"}],"author":[{"embeddable":true,"href":"https:\/\/scripts.farmradio.fm\/sw\/wp-json\/wp\/v2\/users\/185"}],"version-history":[{"count":0,"href":"https:\/\/scripts.farmradio.fm\/sw\/wp-json\/wp\/v2\/radio-script\/39259\/revisions"}],"wp:attachment":[{"href":"https:\/\/scripts.farmradio.fm\/sw\/wp-json\/wp\/v2\/media?parent=39259"}],"wp:term":[{"taxonomy":"script-format","embeddable":true,"href":"https:\/\/scripts.farmradio.fm\/sw\/wp-json\/wp\/v2\/script-format?post=39259"},{"taxonomy":"package","embeddable":true,"href":"https:\/\/scripts.farmradio.fm\/sw\/wp-json\/wp\/v2\/package?post=39259"},{"taxonomy":"script-category","embeddable":true,"href":"https:\/\/scripts.farmradio.fm\/sw\/wp-json\/wp\/v2\/script-category?post=39259"}],"curies":[{"name":"wp","href":"https:\/\/api.w.org\/{rel}","templated":true}]}}