{"id":11957,"date":"2012-06-20T13:29:05","date_gmt":"2012-06-20T10:29:05","guid":{"rendered":"https:\/\/scripts.farmradio.fm\/sw\/?post_type=radio-resource-packs&#038;p=11957"},"modified":"2018-11-15T20:51:43","modified_gmt":"2018-11-15T17:51:43","slug":"11957-2","status":"publish","type":"radio-script","link":"https:\/\/scripts.farmradio.fm\/sw\/mwongozo-wa-redio\/11957-2\/","title":{"rendered":"Kupanda Viazi kunaongeza kipato kwa wakulima wa Kabale, nchini Uganda"},"content":{"rendered":"<p><i>Musiki kiashiria kwa sekunde moja, kasha shusha sauti ya muziki polepole.<br \/>\nJingo za kipindi (jogoo anawika).<\/i><\/p>\n<p><strong>MTANGAZAJI:<\/strong> Kwa mara nyingine ni muda wa \u201cSauti ya Mkulima.\u201d Kama umekaa baa unasubiria kugongwa kinywaji na rafiki yako, basi hauko mahali sahihi! Kama uko tayari kumeza haraka haraka gulp\u2026 gooooo na kurudi kazini!! Leo, tutaongea na mkulima wa viazi atakaye tuelezea jinsi yeye alivyopata mafanikio. Labda unaweza kujifunza kupitia mkulima huyu na ukawa na mafanikio pia! Tutaenda kuangalia ni wapi unaweza kupanda viazi vyako, na umuhimu wa kulimia mazao yako na kupanda mbegu safi na salama za viazi. (Kwa wageni wake). Karibu katika kipindi chetu, Bw. Unaweza kujitambulisha, waambie wasikilizaji wewe ni nani, unatoka wapi, na umekuaje mkulima mwenye mafanikio.<\/p>\n<p><strong>BW. BYARUGABA:<\/strong> Habari za asubuhi wasikilizaji, nina mafua kidogo asubuhi hii lakini nitajitahidi kuzungumza. (akakohoa kidogo kusafisha koo yake). Jina langu ni Byarugaba, ni katekisti wa kanisa na pia ni mkulima mwenye mafanikio mwanachama wa kikundi cha Nyabyumba cha Umoja wa wakulima.<\/p>\n<p>Mwanangu (akimwambia mtangazaji), kilimo sio kipande cha keki. Unahitaji kujitolea kama unahitaji kuendelea. Sikuenda shule kujifunza kingereza kama maprofesa, lakini, nina ona fahari kwani ninaweza kukaa chini na maprofesa nikawambia jambo na wakanisikiliza. Miaka ya nyuma mnamo 1999 nilikuwa masikini kama panya. Nilitegemea kabustani kadogo nilichokuwa nikilima hapo nyumbani. Hii haikutosha kulisha familia yangu achilia kupata mavuno ya ziada kuuza na kujipatia kipato ili niweze kupata ada ya watoto wa shule. Lakini sasa hivi hii imebaki kuwa historia tu.<\/p>\n<p><strong>MTANGAZAJI:<\/strong> \u201cKumbukumbu iliyopita muda Mrefu!\u201d Tafadahli tuelezee umepataje mafanikio na nani alikupa msaada, ulitumia vitu gani? na je, ulizipata wapi na mengineyo.<\/p>\n<p><strong>BW. BYARUGABA:<\/strong> Mwaka 1999 utabakia katika kumbukumbu zangu. Nilikuwa nina ploti mbili tu za shamba ambazo zilikuwa zinalimika kwasababu zilikuwa bondeni. Niliona kuwa ploti hizi ndio matumaini pekee kwa familia yangu. Ploti nyinginezo zilikuwa vipande vya shamba milimani zisizo limika, na sikuzitilia maanani kwasababu nilijua hazina manufaa.<\/p>\n<p>Nilialikwa katika kikao cha kijiji kilicho andaliwa na mashirika mawili yaitwayo, Shirika la taifa la Utafiti lijulikanalo kama NARO na Africare. Walitaka kufanyakazi na wakulima wazawa. Kushiriki katika kikao hiki mkulima alipaswa awe na shamba mlimani. Nilicheka na niliona kuwa hakuna chochote cha maana tutakachopata kutoka katika Bwadi huu. Lakini nilikuwa niko tayari kutoa shamba langu kwani tayari nililiona kuwa halina maana, na nilitaka kuona miujiza ambayo mashirika haya yangefanya.<\/p>\n<p><strong>MTANGAZAJI:<\/strong> Kwanini shirika lilitaka mkulima mwenye shamba mlimani?<\/p>\n<p><strong>BW. BYARUGABA:<\/strong> Walisema shamba la juu mlimani ndi shamba zuri kwasababu liko mbali na wadudu \u2013 kulinganisha na ardhi ya bondeni. Nilipanda viazi mabondeni kipindi cha nyuma, lakini sikuzote viazi vilishambuliwa na magonjwa kama backteria mkunjo na madoa doa mwishoni. Mtu anaweza kupanda gunia moja ya viazi na akavuna kiasi kidogo, kwasababu nusu ya mazao yataoza tu.<\/p>\n<p>Tuliambiwa na shirika la NARO na Africare kuwa viazi vinaoza kwasababu ya ugonjwa wa backteria mkunjo ambayo imekuwa katika udongo kwa miaka mingi. Mbegu dhaifu na zenye magonjwa yalikuwa ni matatizo mengine pia. Hatukuamini hiki mpaka tulipo hakikisha kwa mavuno yetu ya mwanzo.<\/p>\n<p><strong>MTANGAZAJI:<\/strong> Asante, Bw. Byarugaba, kwa taarifa hii. Baada ya mapumziko mafupi tutarudi na mgeni wetu ataendelea kutuambia Zaidi.<\/p>\n<p><em>Muziki<\/em><\/p>\n<p><strong>MTANGAZAJI:<\/strong> Tumerudi, unaweza kutuelezea zaidi ilikuwaje mlipo anza kufanya kilimo cha viazi kwa mara ya kwanza na shirika la NARO na Africare?<\/p>\n<p><strong>BW. BYARUGABA:<\/strong> Mashirika mawili haya yaliahidi kutupatia mbegu safi na salama hivyo tukaanza kuandaa shamba na vitalu vya kupandia mbegu katika mashamba ya milimani. Baada ya kumaliza maandalizi tulipatiwa mbegu salama za viazi. Tulipanda mbegu hizi na mbolea za madidni, na kwa nafasi ya sentimita 70 kutoka msatri na msatri na umbali wa sentimita 30. Tuliambiwa kunyunyuza dawa kwenye mbegu hizi za viazi kuepuka magonjwa kama bakteria baka, ili mmea uwe na majani ya kutosha kuwezesha kutengeneza chakula cha kutosha katika mizizi. Pia tulihakikisha mmea unapata jua la kutosha kwa kuondoa magugu isinyanganyane chakula na mme na kukinga jua, na kipindi cha ukuaji tukaendelea kukabiliana na wadudu. Baada ya siku 90, tulivuna viazi vingi. Huu ulikuwa ni mwanzo wa barabara ya mafanikio, mwanangu.<\/p>\n<p><strong>MTANGAZAJI:<\/strong> Unafikiri watu wengine wanaweza kupata maendeleo kama wewe?<\/p>\n<p><strong>BW. BYARUGABA:<\/strong> Waache wajaribu, na siku moja nitawasikia redioni wakisimiliz simulizi lao pia!<\/p>\n<p><strong>MTANGAZAJI:<\/strong> Asante, Bw. Byarugaba, kwa kushiriki katika \u201cSauti ya Wakulima\u201d Kachwekano FM 103.7. Tutapata mapumziko mafupi na tutakaporudi tutakwambia jinsi mradi unavyoweza kukunufaisha wewe or kikundi chenu?<\/p>\n<p><strong>BW. BYARUGABA:<\/strong> Ndio, kwa furaha.<\/p>\n<p><em>Jingo ya kipindi (jogoo anawika), ikifuatiwa na muziki wa kilimo<\/em><\/p>\n<p><strong>MTANGAZAJI:<\/strong> Akama tulivyo kuahidi kabla ya mapumziko, Bw. Byarugaba atatuelezea sasa juu ya kikundi chake. Bw. Byarugaba?<\/p>\n<p><strong>BW. BYARUGABA:<\/strong> Kikundi chetu cha Umoja wa wakulima Nyabyumba kimenufaika sana kwa kushiriki katika utafiti wa kisayansi. Sasa tunaweza kuzalisha aina tofauti za viazi \u2013 kwa kula ua kwa kuuza. Kwa pamoja tumeanzisha kituo ambacho wakulima wanaweza kukusanya viazi vyao na kuuza kwa pamoja. Lakini hatuja simama hapo! Nguvu yetu ya kufanya mapatano na madalali na masoko imekuwa kubwa, na sasa tunaweza kujua ni muda gani mzuri wa kulima, kuuza, na kuchukua masoko.<\/p>\n<p><strong>MTANGAZAJI:<\/strong> Hii ni nzuri, safi sana. Na ninaelewa kuwa umeanzisha shule ya kilimo, sahihi?<\/p>\n<p><strong>BW. BYARUGABA:<\/strong> Ndio. Tumetunukiwa na NARO na Africare kuwa sisi ni moja kati ya shamba darasa bora. Kwa matokeo haya tumweweza kunzisha huduma tunayoiita shamba shule. Kama kikundi tumeweza kununu gari ambalo tunatumia kupeleka viazi vyetu sokoni. Habari njea, Kituo cha utafiti wa viazi cha kanda hapa Uganda kijulikanacho kama PRAPACE imetusaidia sisi kupata mkataba na mgahawa mjini Kampala, kuwapelekea viazi kwaajili ya kutengeneza chipsi. Na bei wanayonunulia ni nzuri! Nini kingine nikwambie, mwanangu? Sasa tunaweza kulipa ada za watoto wetu na kuboresha lishe zetu kwasababu tuna pesa, na \u201ckuzungumza kama mwanaume yeyote.\u201d (<i>Ed. Nukuu: msemo huu unatumika kuelezea mtu mwenye hela<\/i>.)<\/p>\n<p><strong>MTANGAZAJI:<\/strong> Asante, Bw. Byarugaba. Natumaini wasikilizaji wetu wataona vitendo vyako na mafanikio yako kama chachu ya maendeleo na wao watafanya kama wewe! Kama nitaweza kurudi dondoo muhimu ulizo toa hap awali juu ya upandaji wa viazi, ulisema, Mkulima akumbuke kutumia mbegu bora na mbegu bora, na kukabiliana na wadudu na magonjwa. Ni muhimu pia kupambana na magugu ili kuepuka kunyonya chakula cha mmea na kupelekea kutengeneza makazi ya wadudu. Wakulima watafuta ushauri kwa mtaalamu wa kilimo ambao wanaujuzi wa kuzalisha viazi. Ni vyema pia kupanga katika vikundi na kuudhuria vikao vya vijijini. Na pia unatakiwa kufanya kazi kwa bidii!<\/p>\n<p><strong>BW. BYARUGABA:<\/strong> Ndio, Hivyo ni sahihi.<\/p>\n<p><strong>MTANGAZAJI:<\/strong> Nina kushukuru kwa ujumbe uliousambaza kwa wasikilizaji wetu leo wa kipindi cha \u201cSauti ya Wakulima.\u201d<\/p>\n<p><strong>BW. BYARUGABA:<\/strong> Asante kwa kunialika. Nina tumaini wakulima huko wako na majembe yao tayari kabisa kwenda kukifanya kile nilicho waambia! Wajarinu na kujionea. Tuna usemi kuwa \u201c<i>jarinu na amini<\/i>.\u201d Waache wajaribu, na wabarikiwe wale waaminio bila kuona. Asante na Mungu akubariki \u201cSauti ya Wakulima.\u201d<\/p>\n<p><strong>MTANGAZAJI:<\/strong> Wapenzi wasikilizaji asante kwa kuwa sehemu ya kipindi na ninatumaini mtafungulia redio zenu katika kipindi kijacho.<\/p>\n<p><em>Zima muziki kwa sekunde tano, kasha punguza sauti. <\/em><\/p>\n<p><strong>Shukrani<\/strong><br \/>\nImechangiwa na: Tumwebaze Baryamujura Adrian, Kachwekano Community Multi-Media Center, Kabale, Uganda, na taarifa kutoka Bw. Byarugaba (mwenyekiti wa umoja wa wakulima yabyumba), Rogers Kakuhenzire (daktari wa magonjwa ya mmea, NARO), Tibanyendera Deo (mtafiti msaidizi \/mwezishaji, Shamba Darasa, NARO), na Africare.<br \/>\nImehaririwa na: Daktari. Berga Lemaga, mwandamizi PRAPACE, na Dkt. William Wagoire, mkuu wa mradi wa viazi shirika la NARO Uganda. Shukrani ziwaendee CIAT pamoja na, walio wasaidia kuwaunganisha kikundi cha wakulima na soko, NANDOS masoko endelevu.<\/p>\n","protected":false},"excerpt":{"rendered":"<p>Musiki kiashiria kwa sekunde moja, kasha shusha sauti ya muziki polepole. Jingo za kipindi (jogoo anawika). MTANGAZAJI: Kwa mara nyingine ni muda wa \u201cSauti ya Mkulima.\u201d Kama umekaa baa unasubiria kugongwa kinywaji na rafiki yako, basi hauko mahali sahihi! Kama uko tayari kumeza haraka haraka gulp\u2026 gooooo na kurudi kazini!! Leo, tutaongea na mkulima wa&hellip;<\/p>\n","protected":false},"author":142,"featured_media":0,"parent":0,"menu_order":9,"template":"","meta":{"footnotes":"","beyondwords_generate_audio":"","beyondwords_integration_method":"","beyondwords_project_id":"","beyondwords_content_id":"","beyondwords_preview_token":"","beyondwords_player_content":"","beyondwords_player_style":"","beyondwords_language_code":"","beyondwords_language_id":"","beyondwords_title_voice_id":"","beyondwords_body_voice_id":"","beyondwords_summary_voice_id":"","beyondwords_error_message":"","beyondwords_disabled":"","beyondwords_delete_content":"","beyondwords_podcast_id":"","beyondwords_hash":"","publish_post_to_speechkit":"","speechkit_hash":"","speechkit_generate_audio":"","speechkit_project_id":"","speechkit_podcast_id":"","speechkit_error_message":"","speechkit_disabled":"","speechkit_access_key":"","speechkit_error":"","speechkit_info":"","speechkit_response":"","speechkit_retries":"","speechkit_status":"","speechkit_updated_at":"","_speechkit_link":"","_speechkit_text":""},"script-format":[517],"package":[664],"script-category":[844],"class_list":["post-11957","radio-script","type-radio-script","status-publish","hentry","script-format-mahojiano","package-664","script-category-uzalishaji-wa-mazao"],"acf":[],"yoast_head":"<!-- This site is optimized with the Yoast SEO plugin v28.2 - https:\/\/yoast.com\/product\/yoast-seo-wordpress\/ -->\n<title>Kupanda Viazi kunaongeza kipato kwa wakulima wa Kabale, nchini Uganda - Farm Radio International<\/title>\n<meta name=\"robots\" content=\"index, follow, max-snippet:-1, max-image-preview:large, max-video-preview:-1\" \/>\n<link rel=\"canonical\" href=\"https:\/\/scripts.farmradio.fm\/sw\/mwongozo-wa-redio\/11957-2\/\" \/>\n<meta property=\"og:locale\" content=\"en_US\" \/>\n<meta property=\"og:type\" content=\"article\" \/>\n<meta property=\"og:title\" content=\"Kupanda Viazi kunaongeza kipato kwa wakulima wa Kabale, nchini Uganda - Farm Radio International\" \/>\n<meta property=\"og:description\" content=\"Musiki kiashiria kwa sekunde moja, kasha shusha sauti ya muziki polepole. Jingo za kipindi (jogoo anawika). MTANGAZAJI: Kwa mara nyingine ni muda wa \u201cSauti ya Mkulima.\u201d Kama umekaa baa unasubiria kugongwa kinywaji na rafiki yako, basi hauko mahali sahihi! Kama uko tayari kumeza haraka haraka gulp\u2026 gooooo na kurudi kazini!! Leo, tutaongea na mkulima wa&hellip;\" \/>\n<meta property=\"og:url\" content=\"https:\/\/scripts.farmradio.fm\/sw\/mwongozo-wa-redio\/11957-2\/\" \/>\n<meta property=\"og:site_name\" content=\"Farm Radio International\" \/>\n<meta property=\"article:publisher\" content=\"https:\/\/www.facebook.com\/farmradio\/\" \/>\n<meta property=\"article:modified_time\" content=\"2018-11-15T17:51:43+00:00\" \/>\n<meta name=\"twitter:card\" content=\"summary_large_image\" \/>\n<meta name=\"twitter:site\" content=\"@farmradio\" \/>\n<meta name=\"twitter:label1\" content=\"Est. reading time\" \/>\n\t<meta name=\"twitter:data1\" content=\"6 minutes\" \/>\n<script type=\"application\/ld+json\" class=\"yoast-schema-graph\">{\"@context\":\"https:\\\/\\\/schema.org\",\"@graph\":[{\"@type\":\"Article\",\"@id\":\"https:\\\/\\\/scripts.farmradio.fm\\\/sw\\\/mwongozo-wa-redio\\\/11957-2\\\/#article\",\"isPartOf\":{\"@id\":\"https:\\\/\\\/scripts.farmradio.fm\\\/sw\\\/mwongozo-wa-redio\\\/11957-2\\\/\"},\"author\":{\"name\":\"Farm Radio International\",\"@id\":\"http:\\\/\\\/scripts.farmradio.fm\\\/sw\\\/#\\\/schema\\\/person\\\/69403b70932fd4f67bafd0d0da259786\"},\"headline\":\"Kupanda Viazi kunaongeza kipato kwa wakulima wa Kabale, nchini Uganda\",\"datePublished\":\"2012-06-20T10:29:05+00:00\",\"dateModified\":\"2018-11-15T17:51:43+00:00\",\"mainEntityOfPage\":{\"@id\":\"https:\\\/\\\/scripts.farmradio.fm\\\/sw\\\/mwongozo-wa-redio\\\/11957-2\\\/\"},\"wordCount\":1188,\"publisher\":{\"@id\":\"http:\\\/\\\/scripts.farmradio.fm\\\/sw\\\/#organization\"},\"inLanguage\":\"sw-CG\"},{\"@type\":\"WebPage\",\"@id\":\"https:\\\/\\\/scripts.farmradio.fm\\\/sw\\\/mwongozo-wa-redio\\\/11957-2\\\/\",\"url\":\"https:\\\/\\\/scripts.farmradio.fm\\\/sw\\\/mwongozo-wa-redio\\\/11957-2\\\/\",\"name\":\"Kupanda Viazi kunaongeza kipato kwa wakulima wa Kabale, nchini Uganda - Farm Radio International\",\"isPartOf\":{\"@id\":\"http:\\\/\\\/scripts.farmradio.fm\\\/sw\\\/#website\"},\"datePublished\":\"2012-06-20T10:29:05+00:00\",\"dateModified\":\"2018-11-15T17:51:43+00:00\",\"breadcrumb\":{\"@id\":\"https:\\\/\\\/scripts.farmradio.fm\\\/sw\\\/mwongozo-wa-redio\\\/11957-2\\\/#breadcrumb\"},\"inLanguage\":\"sw-CG\",\"potentialAction\":[{\"@type\":\"ReadAction\",\"target\":[\"https:\\\/\\\/scripts.farmradio.fm\\\/sw\\\/mwongozo-wa-redio\\\/11957-2\\\/\"]}]},{\"@type\":\"BreadcrumbList\",\"@id\":\"https:\\\/\\\/scripts.farmradio.fm\\\/sw\\\/mwongozo-wa-redio\\\/11957-2\\\/#breadcrumb\",\"itemListElement\":[{\"@type\":\"ListItem\",\"position\":1,\"name\":\"Nyumbani\",\"item\":\"http:\\\/\\\/scripts.farmradio.fm\\\/sw\\\/\"},{\"@type\":\"ListItem\",\"position\":2,\"name\":\"Mahojiano\",\"item\":\"https:\\\/\\\/scripts.farmradio.fm\\\/sw\\\/mwongozo-wa-muundo\\\/mahojiano\\\/\"},{\"@type\":\"ListItem\",\"position\":3,\"name\":\"Kupanda Viazi kunaongeza kipato kwa wakulima wa Kabale, nchini Uganda\"}]},{\"@type\":\"WebSite\",\"@id\":\"http:\\\/\\\/scripts.farmradio.fm\\\/sw\\\/#website\",\"url\":\"http:\\\/\\\/scripts.farmradio.fm\\\/sw\\\/\",\"name\":\"Farm Radio International\",\"description\":\"Sharing knowledge, giving voice.\",\"publisher\":{\"@id\":\"http:\\\/\\\/scripts.farmradio.fm\\\/sw\\\/#organization\"},\"potentialAction\":[{\"@type\":\"SearchAction\",\"target\":{\"@type\":\"EntryPoint\",\"urlTemplate\":\"http:\\\/\\\/scripts.farmradio.fm\\\/sw\\\/?s={search_term_string}\"},\"query-input\":{\"@type\":\"PropertyValueSpecification\",\"valueRequired\":true,\"valueName\":\"search_term_string\"}}],\"inLanguage\":\"sw-CG\"},{\"@type\":\"Organization\",\"@id\":\"http:\\\/\\\/scripts.farmradio.fm\\\/sw\\\/#organization\",\"name\":\"Farm Radio International\",\"url\":\"http:\\\/\\\/scripts.farmradio.fm\\\/sw\\\/\",\"logo\":{\"@type\":\"ImageObject\",\"inLanguage\":\"sw-CG\",\"@id\":\"http:\\\/\\\/scripts.farmradio.fm\\\/sw\\\/#\\\/schema\\\/logo\\\/image\\\/\",\"url\":\"https:\\\/\\\/scripts.farmradio.fm\\\/wp-content\\\/uploads\\\/farmRadioLogo.jpg\",\"contentUrl\":\"https:\\\/\\\/scripts.farmradio.fm\\\/wp-content\\\/uploads\\\/farmRadioLogo.jpg\",\"width\":200,\"height\":75,\"caption\":\"Farm Radio International\"},\"image\":{\"@id\":\"http:\\\/\\\/scripts.farmradio.fm\\\/sw\\\/#\\\/schema\\\/logo\\\/image\\\/\"},\"sameAs\":[\"https:\\\/\\\/www.facebook.com\\\/farmradio\\\/\",\"https:\\\/\\\/x.com\\\/farmradio\",\"https:\\\/\\\/www.instagram.com\\\/farmradio\\\/\",\"https:\\\/\\\/www.youtube.com\\\/user\\\/FarmRadioInt\"]},{\"@type\":\"Person\",\"@id\":\"http:\\\/\\\/scripts.farmradio.fm\\\/sw\\\/#\\\/schema\\\/person\\\/69403b70932fd4f67bafd0d0da259786\",\"name\":\"Farm Radio International\",\"image\":{\"@type\":\"ImageObject\",\"inLanguage\":\"sw-CG\",\"@id\":\"https:\\\/\\\/secure.gravatar.com\\\/avatar\\\/493231adf65be6b99ae1dc0dfb13ccca3d412c29f85aa9727be6190faa6293cd?s=96&d=mm&r=g\",\"url\":\"https:\\\/\\\/secure.gravatar.com\\\/avatar\\\/493231adf65be6b99ae1dc0dfb13ccca3d412c29f85aa9727be6190faa6293cd?s=96&d=mm&r=g\",\"contentUrl\":\"https:\\\/\\\/secure.gravatar.com\\\/avatar\\\/493231adf65be6b99ae1dc0dfb13ccca3d412c29f85aa9727be6190faa6293cd?s=96&d=mm&r=g\",\"caption\":\"Farm Radio International\"},\"sameAs\":[\"http:\\\/\\\/frrp.wpengine.com\"]}]}<\/script>\n<!-- \/ Yoast SEO plugin. -->","yoast_head_json":{"title":"Kupanda Viazi kunaongeza kipato kwa wakulima wa Kabale, nchini Uganda - Farm Radio International","robots":{"index":"index","follow":"follow","max-snippet":"max-snippet:-1","max-image-preview":"max-image-preview:large","max-video-preview":"max-video-preview:-1"},"canonical":"https:\/\/scripts.farmradio.fm\/sw\/mwongozo-wa-redio\/11957-2\/","og_locale":"en_US","og_type":"article","og_title":"Kupanda Viazi kunaongeza kipato kwa wakulima wa Kabale, nchini Uganda - Farm Radio International","og_description":"Musiki kiashiria kwa sekunde moja, kasha shusha sauti ya muziki polepole. Jingo za kipindi (jogoo anawika). MTANGAZAJI: Kwa mara nyingine ni muda wa \u201cSauti ya Mkulima.\u201d Kama umekaa baa unasubiria kugongwa kinywaji na rafiki yako, basi hauko mahali sahihi! Kama uko tayari kumeza haraka haraka gulp\u2026 gooooo na kurudi kazini!! Leo, tutaongea na mkulima wa&hellip;","og_url":"https:\/\/scripts.farmradio.fm\/sw\/mwongozo-wa-redio\/11957-2\/","og_site_name":"Farm Radio International","article_publisher":"https:\/\/www.facebook.com\/farmradio\/","article_modified_time":"2018-11-15T17:51:43+00:00","twitter_card":"summary_large_image","twitter_site":"@farmradio","twitter_misc":{"Est. reading time":"6 minutes"},"schema":{"@context":"https:\/\/schema.org","@graph":[{"@type":"Article","@id":"https:\/\/scripts.farmradio.fm\/sw\/mwongozo-wa-redio\/11957-2\/#article","isPartOf":{"@id":"https:\/\/scripts.farmradio.fm\/sw\/mwongozo-wa-redio\/11957-2\/"},"author":{"name":"Farm Radio International","@id":"http:\/\/scripts.farmradio.fm\/sw\/#\/schema\/person\/69403b70932fd4f67bafd0d0da259786"},"headline":"Kupanda Viazi kunaongeza kipato kwa wakulima wa Kabale, nchini Uganda","datePublished":"2012-06-20T10:29:05+00:00","dateModified":"2018-11-15T17:51:43+00:00","mainEntityOfPage":{"@id":"https:\/\/scripts.farmradio.fm\/sw\/mwongozo-wa-redio\/11957-2\/"},"wordCount":1188,"publisher":{"@id":"http:\/\/scripts.farmradio.fm\/sw\/#organization"},"inLanguage":"sw-CG"},{"@type":"WebPage","@id":"https:\/\/scripts.farmradio.fm\/sw\/mwongozo-wa-redio\/11957-2\/","url":"https:\/\/scripts.farmradio.fm\/sw\/mwongozo-wa-redio\/11957-2\/","name":"Kupanda Viazi kunaongeza kipato kwa wakulima wa Kabale, nchini Uganda - Farm Radio International","isPartOf":{"@id":"http:\/\/scripts.farmradio.fm\/sw\/#website"},"datePublished":"2012-06-20T10:29:05+00:00","dateModified":"2018-11-15T17:51:43+00:00","breadcrumb":{"@id":"https:\/\/scripts.farmradio.fm\/sw\/mwongozo-wa-redio\/11957-2\/#breadcrumb"},"inLanguage":"sw-CG","potentialAction":[{"@type":"ReadAction","target":["https:\/\/scripts.farmradio.fm\/sw\/mwongozo-wa-redio\/11957-2\/"]}]},{"@type":"BreadcrumbList","@id":"https:\/\/scripts.farmradio.fm\/sw\/mwongozo-wa-redio\/11957-2\/#breadcrumb","itemListElement":[{"@type":"ListItem","position":1,"name":"Nyumbani","item":"http:\/\/scripts.farmradio.fm\/sw\/"},{"@type":"ListItem","position":2,"name":"Mahojiano","item":"https:\/\/scripts.farmradio.fm\/sw\/mwongozo-wa-muundo\/mahojiano\/"},{"@type":"ListItem","position":3,"name":"Kupanda Viazi kunaongeza kipato kwa wakulima wa Kabale, nchini Uganda"}]},{"@type":"WebSite","@id":"http:\/\/scripts.farmradio.fm\/sw\/#website","url":"http:\/\/scripts.farmradio.fm\/sw\/","name":"Farm Radio International","description":"Sharing knowledge, giving voice.","publisher":{"@id":"http:\/\/scripts.farmradio.fm\/sw\/#organization"},"potentialAction":[{"@type":"SearchAction","target":{"@type":"EntryPoint","urlTemplate":"http:\/\/scripts.farmradio.fm\/sw\/?s={search_term_string}"},"query-input":{"@type":"PropertyValueSpecification","valueRequired":true,"valueName":"search_term_string"}}],"inLanguage":"sw-CG"},{"@type":"Organization","@id":"http:\/\/scripts.farmradio.fm\/sw\/#organization","name":"Farm Radio International","url":"http:\/\/scripts.farmradio.fm\/sw\/","logo":{"@type":"ImageObject","inLanguage":"sw-CG","@id":"http:\/\/scripts.farmradio.fm\/sw\/#\/schema\/logo\/image\/","url":"https:\/\/scripts.farmradio.fm\/wp-content\/uploads\/farmRadioLogo.jpg","contentUrl":"https:\/\/scripts.farmradio.fm\/wp-content\/uploads\/farmRadioLogo.jpg","width":200,"height":75,"caption":"Farm Radio International"},"image":{"@id":"http:\/\/scripts.farmradio.fm\/sw\/#\/schema\/logo\/image\/"},"sameAs":["https:\/\/www.facebook.com\/farmradio\/","https:\/\/x.com\/farmradio","https:\/\/www.instagram.com\/farmradio\/","https:\/\/www.youtube.com\/user\/FarmRadioInt"]},{"@type":"Person","@id":"http:\/\/scripts.farmradio.fm\/sw\/#\/schema\/person\/69403b70932fd4f67bafd0d0da259786","name":"Farm Radio International","image":{"@type":"ImageObject","inLanguage":"sw-CG","@id":"https:\/\/secure.gravatar.com\/avatar\/493231adf65be6b99ae1dc0dfb13ccca3d412c29f85aa9727be6190faa6293cd?s=96&d=mm&r=g","url":"https:\/\/secure.gravatar.com\/avatar\/493231adf65be6b99ae1dc0dfb13ccca3d412c29f85aa9727be6190faa6293cd?s=96&d=mm&r=g","contentUrl":"https:\/\/secure.gravatar.com\/avatar\/493231adf65be6b99ae1dc0dfb13ccca3d412c29f85aa9727be6190faa6293cd?s=96&d=mm&r=g","caption":"Farm Radio International"},"sameAs":["http:\/\/frrp.wpengine.com"]}]}},"_links":{"self":[{"href":"https:\/\/scripts.farmradio.fm\/sw\/wp-json\/wp\/v2\/radio-script\/11957","targetHints":{"allow":["GET"]}}],"collection":[{"href":"https:\/\/scripts.farmradio.fm\/sw\/wp-json\/wp\/v2\/radio-script"}],"about":[{"href":"https:\/\/scripts.farmradio.fm\/sw\/wp-json\/wp\/v2\/types\/radio-script"}],"author":[{"embeddable":true,"href":"https:\/\/scripts.farmradio.fm\/sw\/wp-json\/wp\/v2\/users\/142"}],"version-history":[{"count":0,"href":"https:\/\/scripts.farmradio.fm\/sw\/wp-json\/wp\/v2\/radio-script\/11957\/revisions"}],"wp:attachment":[{"href":"https:\/\/scripts.farmradio.fm\/sw\/wp-json\/wp\/v2\/media?parent=11957"}],"wp:term":[{"taxonomy":"script-format","embeddable":true,"href":"https:\/\/scripts.farmradio.fm\/sw\/wp-json\/wp\/v2\/script-format?post=11957"},{"taxonomy":"package","embeddable":true,"href":"https:\/\/scripts.farmradio.fm\/sw\/wp-json\/wp\/v2\/package?post=11957"},{"taxonomy":"script-category","embeddable":true,"href":"https:\/\/scripts.farmradio.fm\/sw\/wp-json\/wp\/v2\/script-category?post=11957"}],"curies":[{"name":"wp","href":"https:\/\/api.w.org\/{rel}","templated":true}]}}