Wakulima wanaweza kuwa na mapato kutokana na mbolea

Ujumbe kwa mtangazaji

Kuna wasiwasi mwingi kati ya wakulima wenye mashamba madogo kutokana na kupungua kwa rutuba katika udongo katika ardhi ya kilimo katika maeneo yanayopakana na Jangwa la Sahara. Upunguaji huu kwa kiasi fulani unatokana na ongezeko katika wingi wa kiasi cha mimea ya chakula, pale wakulima wadogo wanajaribu kukabiliana na tatizo la kuwa na mashamba ya chini ya ekari moja. Kwa kiasi fulani pia, hii inatokana na matumizi madogo ya mbolea ama za kimakaa (organic) au siziso za kimakaa (inorganic). Kulimwa mfululizo kwa muda mrefu hupunguza virutubisho vya udongo, hupelekea kupungua kwa bamba za kimakaa (organic matter), na kuharibu ubora wa udongo, na yote haya huchangia kupunguza mavuno.

Mifumo mingi ya kilimo cha mseto katika maeneo yanayopakana na Jangwa la Sahara hutumia bamba za kimakaa kutoka shambani kuhifadhi tija ya udongo. Aina nyingi za taka za shambani huwa na bamba za kimakaa za kutosha kuundia mbolea. Pembejeo za kuundia mbolea hujumlisha taka mango, taka za chakula, mabaki ya viwandani, kinyezi, mabaki ya kilimo, na taka za nyumbani. Kuhusu baadhi ya taka hizi, ni muhimu kutenganisha bamba za kimakaa na zile siziso za kimakaa kama vile vyoo, plastiki, na vyuma. Kwa vile sehemu za kimakaa katika taka hizi ni za aina nyingi, haitasaidia mimea sana taka hizi zikiongezwa katika udongo moja kwa moja bila kuozeshwa. Kuozesha hubadilisha bamba za kimakaa kuwa madini na misombo (compounds) ambayo inaweza kunyonywa kwa urahisi na mimea.

Mbolea ya kuozeshwa ina manufaa mengi kwa mkulima. Kwa mfano, ina gharama ndogo kutengeneza, inaweza kutengenezwa kwa kutumia bidhaa zinazopatikana tunakoishi, huboresha uzaaji wa udongo, ni rafiki kimazingira, haihitaji ujuzi mwingi ama hata ujuzi wa kiteknolojia, ni rahisi kununua, na huongeza mavuno. Vile vile, kama ilivyoonyeshwa katika makala haya, kutengeneza mbolea kunaweza kuwaletea mapato mazuri wakulima wadogo, hasa wakifanya kazi kwa ushirikiano.

Script

Mwenyeji:
Hamjambo asubuhi ya leo wasikilizaji. Kipindi cha leo kimelengwa moja kwa moja kwa wakulima wenye mashamba madogo. Kinazungumzia manufaa ya kiuchumi kutokana na matumizi ya mbolea ya kimakaa (compost). Kipindi chetu kina misingi ya mapendekezo na tajriba ya mkulima Mkenya na shirika la kimitaa la misaada liitwalo Rural Development Agriculture Program au ARDAP.

ARDAP ni shirika katika magharibi mwa Kenya ambalo hutetea usalama wa chakula na masuala mengine mengi muhimu. Utasikiliza mazungumzo ya wazi kati ya mkulima aitwaye Romano Afwande na mwakilishi mwendelezi kwa jina Boniface Omondi. Mkulima huyu anatoa mtazamo wa kiutendaji kuhusu kufanya kazi na mbolea ya kuozeshwa, huku mwakilishi mwendelezi akishiriki nasi baadhi ya vipengele vya kitaalam katika mada hii. Hebu tusikilize.

Weka muziki wa mandhari, kisha ufifie na kukoma.

Romano Afwande:
Habari ya asubuhi (mchana/jioni). Mimi ni Romano Afwande, Mkulima mdogo anayefanya kazi katika mradi wa kuozesha mbolea huko magharibi mwa Kenya.

Boniface Omondi:
Nami naitwa Boniface Omondi, dalali (afisa/ajenti) mwendelezi kutoka shirika liitwalo ARDAP. Tunatekeleza mradi wa kuozesha mbolea pamoja na kikundi cha wakulima wadogo huko magharibi mwa Kenya. Sote wawili tuko hapa kuzungumza nanyi kuhusu manufaa ya kuozesha mbolea, na hasa manufaa ya kutengeneza na kuuza mbolea hii.

Romano Afwande:
Kama ninavyoelewa, mbolea ya kimakaa ya kuozeshwa ni aina ya mbolea ambayo inatengenezewa shambani na ambayo ina kiasi kidogo kabisa cha uchafuzi wa kikemikali.

Boniface Omondi:
Hiyo ni kweli. Kuna aina kadhaa za mbolea za kimakaa. Kuna zile za kuozeshwa, lakini pia kuna aina nyinginezo za mbolea za kimakaa, zikiwemo zile majimaji au za kutokana na chai, konde na mbolea za kijani kibichi.

Romano Afwande:
Na kuna njia kadhaa za kutengeneza mbolea. Unaweza kutengeneza mbolea katika rundo la mbolea, au unaweza kutengeneza mbolea katika kikapu au ndoo. Unaweza pia kuongeza malighafi ya lishe za mimea siziso za kimakaa katika mbolea hii inapooza. Hii huimarisha au kuiongeza nguvu mbolea. Wakati watu wananiuliza kuhusu manufaa ya kutumia mbolea za kimakaa, nawaelezea mabadiliko yaliyofanyika shambani mwangu. Katika muda wa mwaka mmoja uliopita, nimeshiriki katika mradi wa kuozesha mbolea. Sehemu ya shamba yangu nilikotumia mbolea hii imeimarika katika muundo na sura ya udongo. Hii inamaanisha kuwa udongo unaweza kuhifadhi maji kwa muda mrefu zaidi. Inamaanisha pia kuwa mizizi inaingia chini zaidi katika udongo. Hii huongeza mavuno yangu na uvumilifu wa mimea yangu. Mimea yenye mizizi iliyoenda chini sana inastahimili vipindi vya kiangazi vyema zaidi

Boniface Omondi:
ARDAP huendesha mradi wa ufikiaji huko magharibi mwa Kenya. Katika mradi wetu, wakulima hujumuika pamoja kutengeneza viasi vikubwa vya mbolea, na pia kutumia mbolea hiyo ya kimakaa mashambani mwao. Kutengeneza mbolea ya kuuza kunaweza kuleta mapato mazuri. Mkulima anaweza kuongeza kiasi cha mbolea anachotengeza na kuuza mbolea asiyoihitaji shambani kwa wakulima wengine. Katika eneo letu, kuna boma za wakulima 10 ambazo zimeunda kikundi kutengeneza mbolea ya kuuza. Huwa wanatengeneza tani 80 kila mwaka. Tani 50 huuzwa na tani 30 huwekwa mashambani mwa wanakikundi.

Romano Afwande:
Kutengeneza mbolea ni kazi nzuri kwa vijana pia. Inahitaji nguvu ngazi nyingi, na inagharimu kazi ngumu na nyingi kutengeneza pahali pa kuozeshea! Kwa vijana katika boma za watu wenye mashamba madogo, inakuwa chanzo kizuri cha ajira mbadala.

Boniface Omondi:
Ili kupata faida zaidi, baadhi ya wakulima ambao wanatengeneza mbolea pia wanalima mazao ya cha chakula ya bei ya juu na muda mfupi kama vile nyanya, pilipili tamu na mboga za kitamaduni. Wananufaika sana kwa kutumia mbolea katika vijishamba vyao.

Romano Afwande:
Unaweza kuongeza nguvu mbolea za kimakaa kwa kuongeza malighafi iliyo na virutubisho katika mbolea. Mifano ya virutubisho hivi vya ziada ni madini ya rock phosphate, vyumbe wa kihadumini walio na nguvu na tope linalotokana na utengenezaji wa gesi ya samadi.

Boniface Omondi:
Ingawa soko la mbolea ya kimakaa haijaendelea kama ile ya mbolea za kutoka viwandani, wanaotoa mbolea ya kuozeshwa wameanza kufaulu. Hapa magharibi mwa Kenya, watengenezaji wa mbolea hii huuzia mtandao wa wateja. Wateja hawa hujumuisha wakulima wanaomiliki vitalu vya miche ya miti, wenye bustani za mitishamba na wanaolima mboga na maua. Wengi wa wateja hao ni wale wanaolima na kuuza miche.

Mwenyeji:
Ningependa kuwashukuru wageni wetu wote wawili wa leo kwa kushiriki nasi na kutugawia mambo mengi. Limekuwa jambo la kusisimua kuwa nao hapa katika studio. Tunatumai kuwa wasikilizaji wetu wapendwa wamesoma kuhusu manufaa ya kuwa mtengenezaji mdogo wa mbolea. Na kwa hayo, tumefika mwisho wa kipindi chetu. Asante sana kwa wageni wetu. Mnakaribishwa tena katika studio zetu wakati wo wote.

Romano Afwande and Boniface Omondi:
(Kwa Pamoja) Asante.
 

Host:
Kwaherini.

Wimbo wa mandhari wa kutamatisha kipindi, kisha ufifie na kuisha.

Acknowledgements

Yamechangiwa na: Macdonald Wesonga na Justus Makhulo kwa manufaa ya ARDAP Kenya, Afrika mashariki.
Yamehaririwa na: Anthony Anyia, Research Plant Physiologist, Alberta Research Council, Canada.

Information sources

Canon E.N. Savala, Musa N. Omare and Paul L. Woomer, editors, 2003. Organic Resource Management in Kenya: Perspectives and Guidelines. Forum for Organic Resource Management and Agricultural Technologies (FORMAT), P.O. Box 79, Village Market 00621, Nairobi, Kenya, East Africa, Tel. +254-20-6752866; Email: format@wananchi.com, website: www.formatkenya.org. Available at http://www.formatkenya.org/ormbook/Chapters/TOC.htm