Maswali ya Mahojiano yaliyopendekezwa: Taarifa za chanjo ya COVID-19 na hatua za kuzuia Maambukizi

Afya

Ujumbe kwa mtangazaji

Save and edit this resource as a Word document

Maelezo kwa Watangazaji

Maswali haya yameundwa ili kusaidia watangazaji kufanya mahojiano na wataalam wa COVID-19 kama vile madaktari, wauguzi, wahudumu wa afya ya jamii na wawakilishi kutoka wizara za afya. Maswali haya yameundwa ili kusaidia watangazaji kupeperusha vipindi vya kuarifu kuhusu utengenezaji wa chanjo za COVID-19, ufanisi wa chanjo hizo, athari zake zinazoweza kutokea, na hatua za kufuata baada ya chanjo ili kuendelea kuzuia maambukizi ya COVID-19.

Wakati wa kupanga mahojiano yako, ni vizuri kuchagua mada tatu hadi tano kati ya mada zilizoorodheshwa ili kujadiliana na mhojiwa/wahojiwa wako. Uliza baadhi au maswali yote ya ufuatiliaji ili kuchunguza mada kikamilifu na kuwapa hadhira yako taarifa wanayohitaji.

Kupunguza muda wa mahojiano kutahakikisha kwamba si wasikilizaji wako wala wageni wako wanaolemewa na habari na kuacha kuwa makini.

Ikiwa ungependa kutoa maelezo zaidi kuhusu mada hii, panga mfululizo wa mahojiano na mgeni huyo huyo au na wengine wanaoweza kuzungumza kuhusu masuala haya. Na kumbuka kwamba mahojiano mazuri yanatokana na kusikiliza kwa makini na maswali mazuri ya kufuatilia. Tumia maswali haya kama mwongozo wa mjadala wako lakini uwe mnyumbufu vya kutosha kufuata mjadala unapoongoza.

Hadithi muhimu na habari potofu zinaweza kuja wakati wa majadiliano haya. Hakikisha kuwa umeshughulikia na kuyaondoa haya pamoja na mgeni wako, pamoja na simulizi nyinginezo ambazo ni maarufu katika jumuiya yako.

Hatimaye, maelezo yanayokuja wakati wa mjadala wako kuhusu chanjo za COVID-19 yanaweza kuwa ya kiufundi na ya kisayansi. Kila mara waulize mhojiwa/wahojiwa wako waeleze dhana za kiufundi kwa maneno ya wazi na rahisi ambayo msikilizaji yeyote anaweza kuelewa. Ikiwa mgeni yeyote anatumia neon tata au la kitaalamu, waambie walielezee—hata kama unaelewa, wasikilizaji wako hawawezi kuelewa.

Script

1. Kwa nini chanjo zilitengenezwa kuzuia COVID-19 badala ya tiba za kawaida kama vile dawa za kumeza?

a. Maswali ya kufuatilia:

a.i. Je, chanjo ni rahisi zaidi na haraka kutengeneza kuliko dawa?

a.i.1. Ni muda gani inachukua kutengeneza chanjo ya COVID-19?

a.i.1.a.Ni kwa namna gani chanjo ya COVID-19 ilitengenezwa kwa haraka?

a.ii. Je, kwa sasa kuna dawa zozote zinazoweza kutibu au kuzuia COVID-19?

a.ii.1. Kama jibu ni ndio, je, zinapatikana katika eneo hili?

a.ii.2. Kama jibu ni hapana, unadhani dawa hizo zitapatikana hivi karibuni?

2. Nini faida za kupata chanjo dhidi ya COVID-19?

a. Maswali ya kufuatilia:

a.i. Je, ni hatari zaidi kuambukizwa COVID-19 au kupata chanjo ya COVID-19? Eleza.

3. Ni kwa namna gani chanjo za COVID-19 zinawalinda watu zidi ya COVID-19?

a. Maswali ya kufuatilia:

a.i. Je, chanjo ina ufanisi gani katika kuzuia kulazwa hospitalini, kuugua au kifo kutokana na COVID-19?

a.ii. Je, chanjo ina ufanisi gani katika kuwalinda watu dhidi ya kuambukizwa COVID-19?

a.iii. Kinga dhidi ya chanjo ya COVID-19 hudumu kwa muda gani?

a.iv. Nimesikia kwamba baadhi ya watu wanaugua COVID-19 hata baada ya kupewa chanjo. Kwa nini hii?

a.v. Je, chanjo ya COVID-19 inafanya kazi dhidi ya aina zote za COVID-19—kwa mfano, aina ya virusi vya delta na omicron?

a.vi. Je, ninaweza kuchukua chanjo ya COVID-19 ikiwa kwa sasa nimeambukizwa COVID-19?

a.vi.1. Je, ninaweza kupata chanjo ya COVID-19 ikiwa nimekuwa na COVID-19 hapo awali na nimepona sasa?
a.vi.2. Baadhi ya watu wanajiuliza ikiwa kuambukizwa COVID-19 hapo awali kunawafanya wasipate COVID-19 katika siku zijazo. Ni kweli?

a.vi.2.a. Je, mtu ambaye amewahi kuwa na COVID-19 bado anafaa kupata chanjo?

a.vii. Je, dozi moja ya COVID-19 inatosha au ninapaswa kupata zaidi ya dozi moja?

a.vii.1. Kama ninahitaji zaidi ya dozi moja, ni muda gani baada ya dozi ya kwanza ninapaswa kupata dozi ya pili?
a.vii.2. Chanjo za nyongeza ni nini?

a.vii.2.a. Nani wanapaswa kupata chanjo ya nyongeza?

a.vii.2.b. Ni wakati gani ninapaswa kupata chanjo ya nyongeza?

a.vii.2.c. Je, chanjo za nyongeza zinapatikana katika eneo hili?

4. Kuna chanjo kadhaa tofauti za COVID-19 zinazopatikana, kila moja ikitolewa na kampuni tofauti. Je, mtu anapaswa kuchagua chanjo gani ya COVID-19 ili kuchanja?

a. Maswali ya kufuatilia:

a.i. Je, kupata chanjo ya COVID-19 kuna gharama yoyote?

a.ii. Wapi ambapo wasikilizaji wanaweza kupata vituo vya chanjo katika maeneo yao?

5. Je, kuna magonjwa au hali za kiafya zinazofanya iwe hatari kwa mtu kupata chanjo ya COVID-19?

a. Maswali ya kufuatilia:

a.i. Je, ni salama kwa mama mjamzito kupata chanjo ya COVID-19?

a.ii. Je, ni salama kwa mama anayenyonyesha kupata chanjo ya COVID-19?

a.iii. Je, ni madhara gani yanayoweza kutokea baada ya kupata chanjo ya COVID-19?

a.iii.1. Je, yoyote kati ya haya madhara ni ya kudumu?

a.iii.2. Ikiwa sina madhara yoyote, hiyo inamaanisha kuwa chanjo haikufanya kazi?
a.iii.3. Je, madhara hutofautiana kwa kila chanjo ya COVID-19?

a.iv. Kuna hadithi potofu zinazozunguka katika jamii yetu kuhusu chanjo ya COVID-19. Umesikia hadithi gani, na tafadhali unaweza kuziondoa kwa ajili yetu?

a.vi.1. Baadhi ya watu wana wasiwasi kuhusu chanjo za COVID-19 kwamba zinazoathiri uwezo wa kuzaa kwa wanaume, au uwezo wa wanawake kupata watoto. Je, kuna ukweli wowote kwa wasiwasi huu?

6. Je, chanjo ya COVID-19 itaniambukiza COVID-19?

a. Maswali ya kufuatilia:

a.i. Kuna ripoti za vifo vinavyotokea baada ya chanjo ya COVID-19. Nini maoni yako kuhusu vifo hivyo vinavyoripotiwa?

a.ii. Je, chanjo ya COVID-19 ni salama kwa makundi yote ya umri, wakiwemo watu walio na umri wa zaidi ya miaka 65?

a.iii. Je, ni salama kwa watoto na vijana kupata chanjo dhidi ya COVID-19?

a.iv. Je, chanjo ya COVID-19 inaweza kutumika kwa mtu anapotumia dawa au matibabu mengine kwa ajili ya hali ya kiafya?

7. Baadhi ya watu wana shaka kuhusu usalama wa chanjo za COVID-19, hasa kwa sababu ya jinsi zilivyotengenezwa haraka au kwa sababu ya ripoti za vyombo vya habari zinazotilia shaka ufanisi wao. Unawezaje kuwahakikishia kuhusu usalama wa chanjo za COVID-19?

8. Je, siku za mbeleni zinakuwaje kwa chanjo za COVID-19 na COVID-19?

a. Maswali ya kufuatilia:

a.i. Je, tutahitaji kuendelea kuwa na chanjo za COVID-19 hapo mbeleni?

a.ii. Je, kuna kipindi au miezi maalumu ambapo watu watahitajika kuchanjwa? Kwa mfano wakati ambapo kuna kipindi cha baridi na mafua?

9. Mbali na kupata chanjo, ni hatua gani za kivitendo ambazo watu binafsi na jamii wanaweza kuchukua ili kujilinda dhidi ya kuambukizwa COVID-19?

a. Maswali ya kufuatilia:

a.i. Ni aina gani ya barakoa zinafaa katika kuwalinda watu dhidi ya kuambukizwa COVID-19 na kuwaambukiza wengine?

a.ii. Ikiwa nitavaa barakoa za kuvaa na kutupa, je, ninaweza kuivaa kesho au kwa siku fulani, au ninaweza kuivaa mara moja tu?

a.iii. Je, ni umbali gani wa kimwili unapaswa kudumishwa kati ya watu walio katika nafasi zilizofungwa kama vile vyumba na ndani ya boma ili kuzuia kuenea kwa COVID-19?

a.iv. Je, watu wanapaswa kunawa mikono mara ngapi ili kuzuia maambukizi ya COVID-19?

a.v. Baada ya kupewa chanjo, je, bado ninahitaji kutekeleza tahadhari hizi? Ikiwa ndivyo, kwa nini?

a.v.1. Tutahitaji muda gani kuendelea kuvaa barakoa, kudumisha umbali wa kimwili, na kuzingatia tahadhari nyinginezo?

a.vi. Je, kula kwa Afya na kufanya mazoezi kunaweza kuzuia maambukizi ya COVID-19?

10. Je, kuna magonjwa au hali za kiafya zinazofanya watu kuwa katika hatari zaidi ya kuambukizwa COVID-19?

a. Maswali ya kufuatilia:

a.i. Ikiwa ndivyo, hali hizi za matibabu ni zipi?

a.ii. Kwanini zinawanafanya watu kuwa hatarini zaidi?

a.iii. Je, kuna hatua mahususi ambazo watu walio na magonjwa au hali hizi wanapaswa kuchukua ili kujikinga na ugonjwa wa COVID-19?

a.iv. Mtu aliye na mojawapo ya hali hizi anapougua COVID-19, inamuathiri vipi tofauti na mtu asiye na hali hii?

a.v. Tunawezaje kusaidia kuwalinda watu ambao wako hatarini zaidi kupata COVID-19?

a.vi. Je, ni salama kwa watu walio na hali hizi au magonjwa kupata chanjo dhidi ya COVID-19?

11. Kwanini ni muhimu kwa watu wengi iwezekanavyo kupata chanjo dhidi ya COVID-19?

a. Maswali ya kufuatilia:

a.i. Je, kuna lolote ungependa kuwaambia wasikilizaji ambao wanasitasita au wana wasiwasi kuhusu chanjo ya COVID-19?

Acknowledgements

Contributed by: James Karuga, journalist, Kenya.

This resource was developed thanks to funding by the Government of Canada through Global Affairs Canada as part of the Life-saving Public Health and Vaccine Communication at Scale in sub-Saharan Africa (or VACS) project.