Tetea usawa wa jinsia na uwawezeshe wanawake

Ujumbe kwa mtangazaji

Ukosefu wa usawa wa jinsia unaendelea kuzua matatizo makuu barani Afrika na kwingineko. Wanawake wanapokosa udhibiti wa raslimali kama vile ardhi, wanashindwa kufanya maamuzi ambayo huboresha mapato ya jamii. Bila udhibiti wa mapato ya jamii, kwa mfano kwa kulima mazao ya biashara, wanawake huchangia muda wao na nguvu kazi yao kwa kudumisha aushi tu, na wanaathirika zaidi na umaskini kuliko wanaume. Na pia mila za kitamaduni, ambazo huenda zikawakataza wanawake kushiriki katika harakati kama vile kupanda miti, hupunguza uwezo wao wa kuhifadhi na kutetea uendelevu wa kimazingira.

Haki za ardhi na mali, ndizo hasa zinachukua nafasi muhimu katika karibu kila jukwaa la umma linaloandaliwa na maofisa wa serikali au mashirika ya kiraia, na wanawake wanachukua jukumu la uongozi katika vita dhidi ya ubaguzi. Usawa wa jinsia ni haki ya kibinadamu na iko katika kiini cha kufikia Malengo ya Maendeleo ya Milenia. Unakuwa wa lazima kabla kuangamiza njaa, umaskini na magonjwa. Usawa wa jinsia unamaanisha usawa katika viwango vyote vya elimu na maeneo yote ya kazi, udhibiti sawa wa raslimali, na uwakilishi sawa katika maisha ya umma na kisiasa.

Makala haya yanaangazia uondoaji wa tofauti za kijinsia katika sekta zote za maisha kwa sababu hatuwezi kufurahia maendeleo bila usalama, hatuwezi kufurahia usalama bila maendeleo na hatuwezi kufurahia moja ya hizo bila heshima kwa haki za binadamu. Njia moja ya kutayarisha makala haya kwa hadhira ya eneo lako ni kumhoji mtu mmoja kutoka jamii yako au hata eneo lako aliye mkereketwa wa usawa wa jinsia.

Makala haya yana misingi ya mahojiano halisi. Unaweza kutumia makala haya kama motisha kutafiti na kuandika makala juu ya mada sawia katika eneo lako. Ama unaweza kuchagua kutoa makala haya katika kituo chako ukitumia waigizaji wa sauti kuwakilisha wazungumzaji. Endapo utafanya hivyo, tafadhali hakikisha unaiambia hadhira yako mwanzoni mwa kipindi kuwa sauti hizo ni za waigizaji na wala si wazungumzaji asilia walioshiriki katika mahojiano.

Script

Wimbo wa kutambulisha kwa sekundi kumi halafu uondoe taratibu

Mwenyeji:
Karibu mpendwa msikilizaji, katika kipindi cha leo ambacho kinahusu wanawake na haki za mali. Hili sio suala la kitaifa tu bali pia ni jambo linalohusu dunia nzima. Mitamboni ni mwenyeji wako Rachel Adipo akikufikia kutoka Ugunja FM. Hapa katika studio nina mgeni wetu wa leo, Bi. Jessica Odima, mtetezi wa haki za wanawake nchini Kenya. Usiende mbali.

Wimbo wa kutambulisha kwa muda wa sekunde mbili kisha uondoe taratibu

Mwenyeji:
Karibu tena. Leo tutaangazia wanawake na haki za kumiliki mali kama njia ya kufikia Malengo ya Maendeleo ya Milenia ya kuinua usawa wa jinsia na kuwawezesha wanawake, hasa katika Wilaya ya Siaya. Karibu Bi. Jessica. Unaweza kugusia baadhi za haki ambazo wanawake wanastahili?

Jessica Odima:
Asante. Mwanzo, wanawake wanastahili kuweza kufikia ardhi, usalama wa umiliki, na haki ya umiliki wa mali. Wanawake kwa wanaume wametambua masuala haya kuwa hoja kuu za mjadala huu. Ingawa sheria za kitaifa nchini Kenya hazibagui dhidi ya haki ya wanawake kurithi mali, mila na tamaduni za jamii binafsi zinazidi kuwazuia wanawake kufikia mali hiyo.

Mwenyeji:
Ni kwa njia gani wewe na wanaharakati wenzako katika eneo la Siaya mnjaribu kuwasaidia wanawake kubadilisha sheria baguzi na njia za kimataduni kuhusu urithi, umiliki wa moja kwa moja wa wanawake na udhibiti wa ardhi, na umiliki wa pamoja wa wanawake wa ardhi ya familia?

Jessica Odima:
Kama wanaharakati wa Wilaya ya Siaya, tumesaidia wanawake kujua haki zao kupitia elimu pendwa, kliniki za msaada wa kisheria, kampeini za utangazaji kuhusu ufikiaji wa ardhi wa wanawake, na kusherehekea Siku ya Kimataifa ya Wanawake kila tarehe nane ya mwezi wa Machi.

Mwenyeji:
Nimesikia kuwa katika Wilaya ya Siaya, mkutano wa jamii huonekana kuwa na ila bila mtetezi wa haki za wanawake ama hata chifu mwenyewe kusisitiza haja ya kuwashirikisha wanawake na hata watoto katika masuala ya mali.

Jessica Odima:
Naam, na haya yote yameinua ari ya wanawake kupigania haki zao na kushughulikia ndugu zao walafi ambao wanawafanya wanawake kuteseka kwa kuwafurusha kutoka miji yao ya ndoa na kuchukua mali yao yote.

Wimbo wa kutambulisha kwa muda wa sekunde mbili kisha uondoe taratibu.

Mwenyeji:
Sasa Bi. Jessica, unaweza kuwaelezea wasikilizaji wetu baadhi ya hadithi za wanawake ambazo umesikia katika jamii?

Jessica Odima:
Ama kwa hakika, ndio. Hebu tusikilize hadithi ya Agnes Opiyo kutoka Wilaya ya Siaya.

Agnes Apiyo:
Baada tu ya kufanikiwa kupitia sherehe ya mpito ya kitamaduni ya Kiluo ambayo humhitaji mtu kung’olewa meno sita ya chini, nilifuatwa na mojawapo ya majirani zetu aliyekuwa anatafuta mke mwafaka wa mpwa wake. Muda mfupi baadaye, ilikuwa nilikutana na yule kijana mdogo, mwanamme mwenye sura nzuri ambaye aliishia kuwa mme wangu na baba wa wanangu watano, wavulana watatu na washichana wawili.

Niliishi kwa raha na mme wangu kwa takriban miaka kumi na minane ndipo mkasa ukatokea. Mme wangu Daniel Omollo alifariki kutokana na malaria. Ghafla, dunia yote ikaporomoka, na hata raha yangu ya kuwa mpendwa wa wakwe zangu. Kila mmoja aligeuka kuwa adui. Kuanzia ndugu zake mme wangu hadi wazazi wake, wote walidai sehemu ya mali ile.

Jessica Odima:
Agnes hayuko peke yake. Katika mikutano ya masomo inayoendeshwa na chama cha mitaani kiitwach Unguja Community Research Centre kwa ushirikiano na chama cha kitaifa kwa jina Kenya Land Alliance, hadithi za kusikitisha kuhusu jinsi wanawake mayatima walivyotimuliwa kutoka boma zao baada ya vifo vya mabwana zao zilitolewa.

Mwenyeji:
Kwa hivyo mikutano hii ya masomo ilifunguwa macho ya wengi?

Jessica Odima:
Ndio. Sasa wanawake wanataka kuwa usukani wa hatima yao wenyewe. Sasa wanataka kusema: “Hizi ndizo amali zetu na mipango ya maendeleo tuliyo nayo kwa maisha yetu ya siku za usoni,” wala siyo, “Hizi ndizo amali zetu na mipango ya maendeleo ambayo imeaandaliwa kwa ajili ya siku zetu za usoni.”

Mwenyeji:
Asante sana Binti Jessica. Sasa tunaona kuwa utofauti kati ya wanawake ni chanzo cha utajiri, nguvu, ujuzi na moyo.

(Sita) Leo tumejifunza mambo mengi: aina ya haki za wanawake, jinsi mila baguzi zinaweza kuondolewa, na vile wanaharakati katika Wilaya ya Siaya wanavyoinua uelewaji. Tumesikia kuwa hata waliodhulumiwa wanaweza kupata matumaini tena. (Sita) Msikilizaji, hapa ndipo tunafika mwisho wa kipindi chetu cha leo. Leo tumeangazia wanawake na haki ya kumiliki mali kama njia ya kufikia Malengo ya Maendeleo ya Milenia ya kuinua usawa wa jinsia na kuwawezesha wanawake. Tunatumai kwamba umejifunza jambo fulani. Hadi tutakapokutana tena, kwaheri.

Wimbo wa kitambulisho kwa sekunde 10 kisha ufifie na kumalizika

Acknowledgements

Yamechangiwa na: Rachael Adipo, Ugunja Community Resource Centre, Kenya.
Yamehaririwa na: Carole Houlihan, International Development Consultant, Canada

Information sources

Hakuna utaratibu mwafaka kuhusu aina za umiliki wa ardhi kwa wanawake. Hati miliki zilizosajiliwa huenda zikafaa katika miktatha kadhaa huku hati za kitamaduni zikifaa katika mingine. Utoaji wa uhakika wa kisheria na ufikiaji sawia wa ardhi na mali kwa wanawake unahitaji amali siyo kwa serikali tu, mbali pia kwa sekta zote za jamii, ikiwemo sekta ya kibinafsi, mashirika yasiyo ya kiserikali, jamii na utawala wa mitaani, na pia mashirika wenza na vyombo vya jamii ya kimataifa.

Wanawake wanahitaji sauti sawa katika maamuzi yanayoathiri maisha yao – kuanzia ndani ya familia hadi viwango vya juu zaidi vya serikali. Hii ni nguzo muhimu katika uwezeshaji wa wanawake. Kwa muda mrefu, wanaume wametawala ufanyaji wa maamuzi katika ngazi za juu. Hatua za kuzuia na zile za kurekebisha udhoofishaji unaotarajiwa dhidi ya haki za wanawake kuhusu ardhi na mali kwa sababu ya mikondo ya sasa ya sera za kiuchumi lazima zitayarishwe.

Marejeleo
Kofi Annan. Africa’s Green Revolution (A call to action).UN press release, July 6, 2004. http://www.un.org/News/Press/docs/2004/sgsm9405.doc.htm
UN Millennium Development Goals. United Nations Environment Program. United Nations Development Goals.
Phillip Onyango. Land and Property Rights. Ugunja Community Resource Centre, 2005.