English, Français

Script 105.13

Script

Pakua na hariri taarifa hii kwa matumizi yako

Nini maana ya mtangazaji bora wa programu au kipindi cha redio kwa ajili ya wakulima?

Mtayarishaji/mtangazaji wa programu za redio mwenye ufanisi hutumia ujuzi wake na stadi za utangazaji kwa njia ambayo husaidia wakulima kuboresha kazi zao, huzungumza juu ya kile ambacho ni muhimu kwao, na hatimaye ujumbe huo huchangia katika kuboresha maisha ya familia zao. Na wakati wote, mtangazaji huyo hufanya vipindi hivyo viwe vya kuvutia na vya kukumbukwa na wasikilizaji ambao ni wakulima.

Ikiwa wewe ndie mtangazaji wa programu au vipindi vya wakulima angalia hapa kwa mwongozo wetu: “Jinsi ya kuwa mtayarishaji na mtangazaji bora wa programu za redio za wakulima.”

Neno la tahadhari kwa mameneja au wasimamizi wa kituo cha redio: Katika vituo vingine, shughuli za usimamizi wa kituo hupewa kwa watangazaji tofauti tofauti. Utaratibu huu unaweza kuwa wa maana kwa sababu huruhusu watangazaji kua na uzoefu wa aina nyingi lakini ni mara chache utaratibu huo huwa wa maana kwa msikilizaji. Kiungo cha msingi kwa msikilizaji wa programu au vipindi vya redio ni mtangazaji wa programu au vipindi hivyo. Ikiwa mtangazaji wa programu hizo hufanya shughuli zake kwa ufanisi, msikilizaji atajenga uhusiano mzuri wa kihisia na mtangazaji huyo na atapendelea kusikiliza proramu au vipindi hivyo. Lakini kama mtangazaji atabadilishwa mara kwa mara, uhusiano kati yake na msikilizaji wa vipindi utadhoofika, na vipindi hivyo pamoja na kituo cha redio kwa ujumla kitakosa ubora.

Je, ni kwa namna gani utangazaji mahiri utaniwezesha mimi kama mtangazaji kuwahudumia wasikilizaji wangu kwa ubora zaidi?

– Nitawawezesha wakulima kuwa na mtazamo mzuri na matarajio mema kuhusu kazi zao.

– Nitawawezesha wakulima kua na uhuru wa kuzungumzia masuala yanayowakabili.

– Nitawawezesha wakulima kutekeleza masuala yote yanayowakabili.

Je, ni kwa namna gani utayarishaji mahiri wa programu za redio utawezesha mimi mtayarishaji kutayarisha vipindi bora zaidi?

 • Unanifundisha kusikiliza maoni mbalimbali pamoja na kuzungumza vizuri.
 • Unanihimiza kuona haja ya kuwasilisha mada kwa usahihi kabisa.
 • Unathibitisha kwamba ni lazima nipange mahojiano yangu na majopo husika kwa makini.
 • Inanisaidia niweze kuandaa vipindi vya redio vinayovutia na vitakayokumbukwa na wasikilizaji.

Mtangazaji anapaswa kuzingatia mambo muhimu kumi na mbili yafuatayo:

1) Heshimu sera au sheria za kituo chako.

2) Waelewe na kuwaheshimu wasikilizaji wako ambao ni wakulima.

3) Hakikisha unajenga uaminifu na wasikilizaji wako.

4) Wasilisha mada zako kwa uhalisi.

5) Kutoa mwongozo kwa wasikilizaji wako.

6) Kuwajengea wasikilizaji matarajio sahihi.

7) Wasaidie wakulima kuzungumza kwa uwazi.

8) Panga mahojiano yako na majopo husika.

9) Uwe msikilizaji mzuri.

10) Kuza hoja kutoka kwenye majadiliano na kuwawezesha wasikilizaji kuchukua hatua.

11) Fanya vipindi vyako kua vya kuvutia na kukumbukwa na wasikilizaji.

12) Boresha vipindi vyako kutokana na maoni au mrejesho unaoupata kutoka kwa wasikilizaji wako.

Maelezo ya kina:

1) Heshimu sera au sheria za kituo chako.

Bika shaka kituo chako kina sera na sheria zinazoongoza watangazaji kuhusu jinsi ya kutumia redio kwa ubora katika kuwahudumia wasikilizaji. Hivyo, unapaswa kuheshimu sera na sheria za kituo katika utekelezaji wa kazi zako, na kuhakikisha kuwa unazijua na kuzielewa sera na sheria zinazohusiana na kazi zako. (Angalia hapa chini kwa mfano wa sera zilizotengenezwa na shirika la kimataifa la Radio ya wakulima kwajili ya vituo vya redio. Ni pamoja na viwango vya programu ya VOICE, viwango vya uandishi wa habari vya FAIR, na tamko la kusudi la kipindi.)

Ikiwa utafikiri kwamba sera au sheria fulani inakwamisha utoaji wa huduma bora kwa wasikilizaji wako ambao ni wakulima, jadili suala hilo na meneja wako au msimamizi wa kituo. Pengine labda suala hilo linahitaji ufafanuzi fulani au labda kituo chako kitakubali kuiangalia sera au sheria hio kwa mara nyingine tena.

2) Waelewe na kuwaheshimu wasikilizaji wako ambao ni wakulima.

Wakulima wadogo wanakabiliwa na changamoto nyingi. Kwa mfano: Katika maeneo mengi, ubora wa udongo umeshuka, matukio ya hali mbaya ya hewa hutokea mara nyingi, na mavuno mengi ya mazao hupotea kabla ya kupata soko! Ikiwa unaweza kujifunza, na kisha kuelewa changamoto ambazo wasikilazi wako (ambao ni wakulima) wanakabiliana nazo, basi tayari utakua katika harakati za kuwasaidia wakulima hao kua wenye ufanisi zaidi katika kazi zao.

Tumia kila fursa ya kutembelea wakulima na mashamba au bustani zao, na kuwauliza maswali wakulima wake kwa waume. Kwa mfano:

– Je, ni kwa kiasi gani unaweza kulisha familia yako mwaka huu ukilinganisha na mwaka jana?

– Je, mavuno ya mazao sasa yakoje ukilinganisha na miaka iliyopita?

– Je, unafanya nini ili kuboresha uzalishaji?

– Je, bei ni nzuri kiasi gani katika soko la mazao yako?

– Je, ni changamoto zipi kubwa unazokabiliana nazo katika kilimo chako?

Na pia, heshimu wakulima unapokuwa ukitangaza. Kwa mfano, njia moja wapo unayoweza kutumia wakati wa kutambulisha jopo la mahojiano kuhusu upotevu wa mavuno kipindi cha uvunaji na baada ya kuvuna:

“Leo tuna Profesa John Zuma, ambae ni mkuu wa kitengo cha sayansi ya mazao katika Chuo Kikuu cha Abuja. Profesa John Zuma atajibu maswali kutoka kwa wakulima watatu wa eneo hili kuhusu uhifadhi wa mahindi.”

Na njia nyingine ni:

“Leo tutaweza kujadili kuhusu changamoto ya uhifadhi wa mahindi ili mavuno yako yote yaweze kufika sokoni. Susan Chako alipanda hekta mbili za mahindi karibu na kijiji cha Zonga. Mwaka jana, mazao yake yote ya mahindi yalipona na kuuzwa. Profesa John Zuma ni mkuu wa kiteno cha sayansi ya mazao katika Chuo Kikuu cha Abuja. William Bulawo alilima hekta moja ya mahindi, lakini mavuno yake ya mwisho yaliharibiwa sana na wadudu wala nafaka. Na Mary Gecho amekuwa akitazama miundo ya ghala mpya kwa ajili ya mazao yake ya mahindi huko Kwamalu. “

Tofauti kati ya mifano hio miwili ni kwamba, katika mfano wa pili, inaonyesha kua wakulima wana mengi ya kuchangia kwenye jopo la majadiliano sawa na profesa wa chuo kikuu. Hiyo inaonyesha heshima kwa wakulima!

Hatimaye, ni vizuri kua na majina ya wakulima na mahali pa sahihi walipo. Hakuna kitu kinachoonyesha kutokuheshimu mtu kama kukosea kutamka jina lake na kurudia rudia kosa hilo wakati wa utangazaji. Mfano: Kukosea jina la kijiji, au la mzee anaheshimika kijijini hapo. Inapotokea umekosea, hakikisha unarudia kutamka jina lake kwa usahihi, na uombe msamaha wakati unarekebishwa.

3) Hakikisha unajenga uaminifu na wasikilizaji wako.

Kwa kuwa wasikilizaji hujenga uhusiano na watangazaji wa redio, wewe kama mtangazaji utataka wasikilizaji wako wakuamini. Uaminifu hujengwa polepole, na unahitaji matendo mazuri kutoka upande wako.

Kwa mfano, unapomhoji afisa fulani au mtaalam, usiwaache tu wakaongea kwa muda mrefu kuhusu kazi nzuri wanayofanya. Bali, waulize maswali ambayo wakulima watapenda kusikia wakijibu. (Bofya hapa ili uone mwongozo kuhusu: “Jinsi ya kuwawajibisha wakuu.”) Kwa njia hii, wasikilizaji wako watakuja kutambua kuwa unawasemea.

Pia, kujenga uaminifu kunahitaji uwe ni mtu wa kuaminika. Je, uko tayari kwa wasikilizaji wako kila wiki? Je! unatoa ripoti ya hali ya hewa na ya masoko? Je! unafuatilia hadithi, simulizi au mada punde unaposema utafanya hivyo? Ikiwa utasema kua utatembelea kijiji fulani wiki ijayo, hakikisha unaenda!

Pia, kwenye kujenga uaminifu inamaanisha kuwepo na utayari wa kukubali makosa. Bila shaka, wakati wote unajaribu kuwa mkweli na kutoa taarifa sahihi, lakini wakati mwingine makosa yanatokea katika utangazaji. Uaminifu kati yako na wasikizaji wako utaimarika pale ambapo utaomba radhi kwenye kipindi kinachofuata kwa kusema: “Katika kipindi kilicopita, nilisema kazi ya kuboresha barabara kati ya Doula na Tangere bado haijaanza. Baada ya hapo nilitambua kua kazi hiyo ilianza tarehe 15 Juni na matengenezo yanatarajiwa kukamilika ifikapo Septemba.”

4) Wasilisha mada zako kwa uhalisi.

Kutokuwasiliana na wasikilizaji wako ili kujua kama kuna jambo halijaeleweka. Hii ni changamoto katika utangazaji wa vipindi vha mkulima kwa sababu vipindi vya wakulima huwa na maneno ya kitaaluma na kisayansi. Ikiwa mhojiwa anaanza kuzungumza juu ya aflatoxin, jiulize mara moja kwamba: “Hilo ni neno jipya kwangu. Kisha uuliza je, unaweza kueleza aflatoxin ni nini?” Na ikiwa majadiliano yametawaliwa na lugha ya kitaalamu, hakikisha unatoa muhtasari wa mambo muhimu yaliyoongelea au jadiliwa.

Baadhi ya wakulima ambao unataka uwape fursa ya kuchangia mada wanaweza kupata ugumu wa kufanya hivyo, labda kwa sababu ya aibu au kwasababu ya jinsi wanavyoongea. Inabidi uwawezesha wakulima hao kutoa maoni yao wakat huo huo ukiheshimu kabisa utu wao. Tumia vidokezo kama vile: “Ndugu Zomba, sikusikiavizuri ujumbe wako kamili. Je, ungependa tena kuurudia, tafadhali?” Au: “Ndugu Zomba, umetaja mapipa ya kuhifadhia mazao, lakini sikuelewa vizuri kama unafikiri mapipa ya udongo au mapipa ya chuma hufanya kazi nzuri zaidi.

Ikiwa unapata ugumu wowote na jopo la majadiliano, unaweza kurudisha nyuma mjadala kwa kusema hivi: “Hebu subiri kidogo! Umenipoteza mimi na labda baadhi ya wasikilizaji. Je, hii yote ina maana gani kwa mkulima wa mahindi katika kijiji cha Bamono?

Pia, kumbuka kuwa ni vigumu kuwasilisha namba au mahesabu kwa usahihi kwa njia ya redio. Namba au mahesabu hazigeuki kuwa picha ambazo mkulima anaweza kukumbuka. Kwa mfano, ni vigumu kwa msikilizaji kukumbuka mambo yafuatayo: “Weka safu zako pointi moja kwa umbali wa mita tano. Kisha piga mashimo yenye umbali wa sentimita thelathini kisha weka mbegu mbili katika kila shimo.” Ikiwa utalazimika kutoa nambari, basi unatakiwa kufanya hivyo kwa usahihi kwa kadiri iwezekanavyo. Unaweza ukatoa idadi hio au nambari hizo au mahesabu hayo angalau mara mbili wakati unawasilisha mada, na kuwasilisha au kutaja tena mwishoni mwa kipindi chako.

5) Kutoa mwongozo kwa wasikilizaji wako.

Unapoongoza kipindi, sio kua wewe tu ndie mwenye sifa, bali kiuhalisia, wewe ndie mtangazaji ulieamnika kufanya hivyo. Unatakiwa kuwaalika wasikilizaji kwenye kipindi chako, unawatembeza umo, unajadiliana nao, na kisha unawaruhusu waende zao.

Unafanya hivyo kwa:

– Kuwakaribisha mwanzoni kabisa kabla hujaanza kipindi,

– Kuwafahamisha yaliyomo katika kipindi,

– Kuwaonyesha walipo au watakapochangia kwenye mtiririko wa kipindi hicho,

– Kutoa muhtasari wa vipengele ambavyo havikueleweka vizuri,

– Kuwashukuru kwa kusikiliza, na

– Kuwajulisha kuhusu kipindi kinachufuatia na mada zake.

(Bofya hapa kwa mwongozo kuhusu “Jinsi ya kutayarisha ujumbe utakaochochea au kuvutia wasikilizaji, wakati wa ufunguzi na wakati wa kufunga kipindi”)

Pengine wasikilizaji wengi husikiliza vipindi wakiwa majumbani, au wakiwa na mtu mmoja au wawili. Kwahio unapoanza kuzungumza na wasikilizaji wa kipindi, kumbuka unaongea na mtu mmoja mmoja. Kwa mfano, unaweza kusema, “Najua kwamba unafikiri kuhusu wakati muafaka wa kuanza kupanda, na hivyo leo nimewaletea mtaalam wa ugani. Ana vidokezo muhimu kwa ajili yako.” Usiseme: “Huu ndio wakati wakulima wanafikiria kuanza kupanda. Mtalaamu wa ugani ana maoni mazuri kwa wakulima baadaye katika kipindi.”

6) Kuwajengea wasikilizaji matarajio au matumaini sahihi.

Kama ilivyoelezwa awali, kazi ya mkulima ina changamoto nyingi, na kuna nyakati ambazo hukatisha tamaa kabisa. Pamoja na kujua hivyo, inabidi uwasilishe kipindi chako kwa mkulima mmoja mmoja na hata kwa wakulima walioko kwenye kikundi kwa namna ambayo wanaweza kufanya mabadiliko mazuri yatakayoweza kuboresha maisha ya familia zao na jamii.

Vipindi vya redio ni kwaajili ya kuwezesha kilimo cha wakulima wadogo wadogo. Hii haina maana kwamba vipindi hivyo visitayarishwe na kutangazwa kwa umakini. Kwa kweli, ni muhimu kuibua mambo muhimu na kujadili changamoto ambazo zinawakabili wakulima, kama mabadiliko ya tabia nchi, udongo usio na ubora, mazao yanayoharibika, au ukosefu wa mikopo kwa wakulima wadogo. Lakini pia, unapaswa kuibua changamoto zilizopo kwenye ya mazingira ambayo mkulima anayaelewa ili aweze kuboresha kilimo chake na maisha kwa ujumla.

Hata wakati mambo ni ngumu, kuna njia za kuonyesha matumaini halisi. Kwa mfano, hebu tuseme barabara ya kwenda kwenye soko la jiji imeharibika sana kutokana na mvua kubwa iliyonyesha. Ingawa serikali imeahidi kuirekebisha, wewe ungependa kueleza jinsi ambavyo wakulima wanafedheheka na kukata tamaa wanaposindwa kupeleka mahindi yao kwenye sokoni. Pamoja na kusema hivyo, unaweza pia kutoa mada kuhusu jinsi ya kuhifadhi mahindi kwa usalama mpaka mkulima atakapoweza kusafirisha. Na kisha unaweza kutoa wito kila wiki kwa idara husika ya serikali kutoa kipaumbele katika utengenezaji wa barabara hio mpaka hapo serikali itakapowapatia wakulima tarehe au wakati ambapo matengenezo hayo yataanza.

Kuwapa wakulima matarajio au matumaini sahihi ni juu yako wewe, mwongozaji wa kipindi. Kuanzia unapoanza kipindi mpaka wakati wa majadiliano na hata wakati wa kutoa neno la mwisho wa kipindi, ni wewe ndie utakaefanya kipindi hicho kifanikiwe.

7) Wasaidie wakulima kujieleza kwa uwazi.

Kipindi kizuri cha wakulima kina malengo mawili muhimu. Kwanza kinawapa wakulima:

– taarifa wanayohitaji na kwa wakati muafaka

– fursa ya kuzungumzia juu ya mambo yenye umuhimu kwao.

Na lengo la pili ni muhimu tu kama la kwanza kwamba wakulima sio kama walimu au wanasheria au watangazaji ambao hutumia siku zao kuzungumza na watu kwenye mihadhara au taasisi mbalimbali za umma. Wakulima hutumia muda mrefu katika mashamba na bustani zao, pamoja na wanyama na mimea. Hivyo, kazi yako ni kuwasaidia ili waweze kuwa wazungumzaji wazuri kwenye redio.

Inapo wezekana, fanya mahojiano na wakulima wakati ambao wanaridhia kufanya hivyo labda katika nyumba zao, vijijini kwao, mashambni mwao, au hata sokoni. Anza kwa kutoa maoni mazuri juu ya hali fulani ya maisha yao. (Kwa mfano: “Kama sijakosea huyu binti yako ni msaada mkubwa katika shughuli za shambani,” au “Maoni yako juma lililopita kuhusu kutokuwepo kwa mtaalamu wa ugani kumeungwa mkono na watu wengi sana.”) Watu wanaojisikia kuthaminiwa au kuungwa mkono wana uwezekano wa kujieleza vizuri zaidi na kwa uwazi wanapouliza maswali.

(Bofya hapa kwa mwongozo kuhusu “Jinsi ya kuwawezesha wakulima kuzungumza juu ya mambo muhimu yanayowakabili (Kuwezesha kusikika kwa sauti za wakulima.”)

Inawezekana ikahitajika uchochezi katika kuwafanya wakulima wanawake waweze kuzungumza ukilinganisha na wanaume. Hivyo, unapotembelea kijiji, fanya mkutano na wanawake pekee (wakiwa kwenye kikundi mchanganyiko, wanaweza kuwaachia waume zao kufanya mazungumzo yote.) Ikiwa una simu hewani, ni vema kutoa laini moja kwaajili ya wanawake watakaopenda kupiga simu. Kwa jinsi hiyo, unaweza kuwezesha angalau nusu ya wapigaji simu wanaoingia hewani kuwa wanawake. Jinsi ambavyo wanawake wengi watawasikiliza wanawake wenzao wakizungumza hewani, ndivyo watakavyohamasika kuzungumza ili nao wasikike hewani.

(Bofya hapa kwa mwongozo kuhusu: “Jinsi ya kuwahudumia wakulima vizuri.”)

Ni muhimu kusherehekea matukio mbalimbali na wakulimu, kwa kujadiliana nao mbinu zitakazotatua matatizo yao na kuleta mabadiliko mazuri katika maisha yao. Sisi sote tunapenda kusifiwa, hivyo wakulima watakaposifiwa itawahamasisha kujiamini zaidi na kuzungumza kwa ujasiri na kuhamasika kutumia mbinu mpya za kilimo.

8. Panga mahojiano yako na majopo husika.

Kazi yako kubwa kama mtangazaji inahusiana na kuhoji wanawake na wanaume-wakulima, wazee, wataalamu, maafisa, na wanasiasa. Labda moja ya sababu kwanini wewe ni mtangazaji ni kwamba unapenda kufanya mazungumzo na watu. Vizuri! Lakini, kufurahia mazungumzo mazuri ni tofauti sana na kuwa mhojaji mzuri. Mazungumzo ni pamoja na gumzo za kirafiki kutoka mada moja kwenda nyingine kama mtakavyokubaliana. Hata hivyo, lengo la mahojiano ya kipindi cha mkulima ni kwa anaehoji kupata maelezo au taarifa muhimu kutoka kwa mhojiwa kama mada maalum itakayowavutia wasikilizaji. Wewe, kama mhojaji, unahitaji kudhibiti mahojiano, na kuhakikisha kwa manufaa ya wasikilizaji wako. Hii inamaanisha kwamba ni lazima upangilie jinsi utakavyoendesha mahojiano yako mapema, na uandike maswali na madodoso ambayo yatakusaidia kupata taarifa bora kutoka kwa mhojiwa. Pia, utahitaji kuandaa maswali ya nyongeza kwa wakati ambapo mhojiwa mwenye ujuzi anajaribu kutawala na kugeuza mahojiano kwa manufaa yake wenyewe. (Bofya hapa kwa mwongozo kuhusu “Jinsi ya kufanya mahojiano kwa ufanisi” na usome kipengele cha “Jifunze kuhusu aina tatu kuu za mahojiano.” Na bofya hapa kwa mwongozo kuhusu “Jinsi ya kufanya mahojiano na jopo la majadiliano kwa ufanisi.”)

9) Uwe msikilizaji mzuri.

Ingawa ni muhimu kupangilia jinsi utakavyofanya mahojiano na kuongoza mjadala, ni lazima usikilize kwa makini yale ambayo yanasemwa na mhojiwa. Huwezi tu kusoma orodha yako ya maswali na kua na matumaini kwamba mhojiwa anakupa majibu sahihi.

Hapa kuna mfano wa mtangazaji aliyefuatilia maswali yake kwa makini lakini hakusikiliza majibu ya maswali aliyouliza.

“Bi. Smith, ninaelewa kuwa mavuno yako ya mahindi yaliongezeka mara mbili mwaka huu. Je, hiyo ni sawa?”

“Ndiyo, lakini mume wangu alifariki na nimenyimwa kutumia shamba na familia yake.”

“Hongera! Na unafikiri ni kwa sababu gani ulipata mavuno bora?”

Unatakiwa kuwa msikilizaji mzuri wakati wote, sio tu wakati unapofanya mahojiano au au kuendesha mladala kwenye jopo fulani. Kuwa msikilizaji mzuri unapokuwa shambani ukizungumza na wakulima au unapozungumza nao sokoni. Kwa kufanya hivyo, utajifunza mambo ambayo huenda hakuyafikiria.

10) Kuza hoja kutoka kwenye majadiliano na kuwawezesha wasikilizaji kuchukua hatua.

Kua na mjadala mzuri ni jambo muhimu katika uendeshaji wa kipindi cha mkulima, lakini mjadala mzuri tu hautoshi kuwafanya wakulima kutekeleza mambo ambayo yataboresha kilimo chao. Kwakua kilimo bora kinahitajika ili kuwawezesha wakulima kupata mavuno bora kwaajili ya kujikimu kwenye maisha yao, wewe kama mtangazaji unaweza unae endesha mijadala mingi, unaweza kuwasaidia katika utekelezaji wa mapendekezo yatokanayo na mijadala hio. Kwa mfano, unaweza kuuliza maswali kama haya:

“Kila mtu anaonekana kukubali kwamba kupanda mahindi kwa safu utasababisha mavuno bora zaidi. Susan, wewe unapanda mahindi. Je, utafanya nini tofauti mwaka huu ili kuongeza mavuno?

“Ni nini kinaweza kufanyika na chama cha ushirika cha wakulima ili kuhakikisha kuwa wakulima wana mifuko sahihi ya hifadhi mavuno ya mwaka huu? Na je, ni kwa wakati gani chama cha ushirika kinapaswa kuchukua hatua?

“Kwa kuwa haionekani kama kurekebisha barabara kumepewa kipaumbele na serikali hii, ni nini kinachoweza kufanyika ili urekebishaji wa barabara upewe kipaumbele? Ni nani atakayehusika na hili?”

11) Fanya vipindi vyako kua vya kuvutia na kukumbukwa na wasikilizaji.

Hakuna mtu anayesikiliza kipindi cha redio kama hakimfurahishi. Unaweza ukatoa taarifa na kuwapa wakulima fursa ya kutoa maoni yao lakini kama kipindi hicho hakiwagusi au hakiwafurahishi wakulima, hawatakisikiliza. Wanaweza kuendelea kuwepo hewani kwaajili ya kupata taarifa za hali ya hewa na masoko tu na baada ya hapo wakasikiliza redio nyingine ambao inawagusa na kuwafurahisha. Ni muhimu sana kutambua hili kipindi hiki ambapo wakulima wana vituo vingi vya redio ambavyo wanaweza kusikiliza.

Kuna njia tofauti tofauti zinazoweza kutumika ili kufanya kipindi kua chenye mvuto na cha kukumbukwa na wasikilizaji kama zifuatazo:

 • Chagua muziki ambao unapendwa na wasikilizaj wako.
 • Andaa utangulizi unaoamsha hisia za wasikilizaji wako. Kwa mfano, usiseme tu, “Tunafurahi kuwa na Susan Alaro pamoja nasi leo kuzungumzia juu ya dawa zenye sumu au viatilifu.” Badala yake, unaweza kusema: “Juma lililopita tulipokua Bulawano, watoto wawili walikufa baada ya kuchanganya kinywaji chao na dawa yenye sumu. Je! Watoto wako ni salama? Leo, Susan Alaro atakusaidia kufanya nyumba yako-na watoto wako- wawe salama na dawa hizo.”
 • Tumia mashindano kusaidia wakulima kukumbuka taarifa muhimu (kwa mfano, “Hebu tutumie vina ambavyo vinataja vipimo vyote na hatua zinazohitajika kwa kupanda kwa safu.” Mshindi atapata T-shirt yetu ya ‘Wakulima Kwanza’!) Au uwe na mashindano kuhusu mapishi bora ya viazi vitamu ili watoto wapende kula viazi vitamu.
 • Uwe na kipengele ambacho kinaonyesha matukio ya kuchekesha yanayotokea wakati wa shughuli za kilimo. (Kwa mfano, fanya mahojiano na mwanamke ambaye alishambulia mnyama aliyekua akiiba mahindi kutoka kwenye ghala lake, na alichofanya baada ya tukio hilo.)
 • Unaweza kufanya utani juu ya moja ya mapungufu yako au udhaifu ulionao. Kwa mfano, kama wewe huna bustani nzuri au sio mtunzaji mzuri wa bustani, onyesha jinsi unavyoonekana kuua kila kitu unachojaribu kukuza au kupanda. Wasikilizaji wako watapata hisia na watafurahia hadithi zako.
 • Unaweza kuendesha kipindi chenye mada nzito kisha uhakikishe kipindi hicho kinafuatwa na kipindi chenye mada rahisi au nyepesi ili kuepuka kumchosha msikilizaji.
 • Onyesha alama mbalimbali ili wasikilizaji aweze kufahamu kuna kitu au mada ya kufurahisha inayokuja kwao hivi punde – hata kama hawapendi kipengele kilichopo hewani kwa wakati huo. Wakati ukiwa unasafiri na gari moshi, utaona ishara na vituo vya barabarani ambazo vinakuelekezea unakokwenda. Kadhalika, matumizi ya ishara au alama mbalimbali katika kipindi cha redio hufanya hivyo hivyo. Kwa mfano, unapofikia katikati ya kipindi chako unaweza kusema: “Huyo alikuwa Susan Quetcho akituelezea kuhusu mizinga yake mipya ya nyuki. Kinachokuja hivi punde ni: Jinsi ya kuwaondoa wadudu waharibifu kwenye nafaka zako.” Matumizi ya ishara na alama humfariji msikilizaji ambae amechelewa kufungulia kipindi cha redio.

Zaidi ya yote, kipindi chako kitakuwa cha kuvutia ikiwa untatoa sauti yenye kuonyesha udadisi, matumaini, heshima, na nguvu kwa wasikilazaji wako.

Bofya hapa kupata muongozo kuhusu: “Jinsi ya kufanya kipindi cha wakulima kuwa chenya kuvutia au kufurahisha na cha kukumbukwa.”

Hata kama unazungumzia mada ngumu usikwepe kujadili hoja yoyote ya muhmiu au itakayojitokeza eti kwa sababu ni mada ngumu. Unaweza ukaanza na hadithi ya kufurahisha inayoweza kukamata usikivu wa wasikilizaji wako na kuwavutia, ili waweze kusikiliza wakati unapojadili jambo gumu. (Bofya hapa kupata muongozo kuhusu “usimuliaji wa hadithi.”)

12) Boresha vipindi vyako kutokana na maoni au mrejesho unaoupata kutoka kwa wasikilizaji wako.

Mtangazaji wa kipindi cha redio mara nyingi huwa na wasifu wa juu kwenye jamii, na utakuwa na wapenzi ambao watakupa mrejesho wa kazi nzuri unayofanya. Ni furaha kupata maoni ya wasikilizaji wako, lakini yakupasa kufanya vizuri zaidi. Unahitaji kusikia kutoka kwa wasikilizaji ambao wanaelezea kwa kuunyambua ujuzi wako wa kuendesha vipindi, ili usifikiri unazungumzia mambo muhimu kwa uzuri sana na ukajisahau kufanya vizuri zaidi.

Hapa kuna njia mbalimbali zitakazokusaidia kupata maoni yenye manufaa:

 • Kuhimiza kituo chako kufanya majadiliano na kikundi cha wasikilizaji. Hakikisha unajumuisha maswali kama vile: “Unapenda nini kuhusu ‘muongoza vipindi vya wakulima wa kwanza’, William Bato? Je! Anawezaje kuboresha vipindi vyake? Je! kipindi cha ‘Wakulima Kwanza’ huzungumzia mambo ambayo ni muhimu kwako?”
 • Kuendeleza nidhamu yako katika utangazaji: unaweza kutumia orodha itakayokufanya ujiulize mara kwa mara ni kwa jinsi unatekeleza majukumu yako, na jinsi unavyoweza kuboresha.
 • Waulize watangazaji wengine kwenye kituo chako maoni yao kuhusu kipindi chako kimoja, na uwape orodha yako ya majukumu yako ili waweze kuota maoni yatakayo kusaidia. Unaweza kuitisha kikao ambacho wataweza kutoa maoni yao na kutoa mwongozo wa kuboresha. (Jitolee pia kuwafanyia hivyo na wao.)
 • Mshirikishe msimamizi wako kila mwaka katika kutathimini ni kwa jinsi gani umeweza kufikia malengo ya kipindi, kulingana na kazi za muongoza kipindi zilizoorodheshwa. Orodhesha maeneo ya kuboresha zaidi kwa mwaka ujao, na pia andika msaada wowote utakaohitajika (k.m., mafunzo, kufundisha) kufikia maboresho hayo

Kama ilivyoelezwa hapo mwanzo, kuwa mtangazaji bora wa kipindi ni jukumu kubwa linalohitaji ujuzi mwingi. Lakini unaweza kufanya hivyo ikiwa utaendelea kuboresha jinsi unavyofanya kazi zako kama ilivyo orodheshwa. Na unapoendelea kuboresha kazi zako, utasaidia wakulima wanaokusikiliza kuboresha mbinu za kilimo chao, na kuboresha maisha ya familia zao.

Nakutakia kila la kheri katika utekelezaji wa kazi hii muhimu.

 

Acknowledgements

Shukrani imetolewa na: Doug Ward, Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi, Farm Radio International, na kuhakikiwa na Shelagh Rogers, Mtangazaji wa Sura Ifuatayo, CBC Redio.

Information Sources

Vyanzo vya taarifa:

1) Viwango vya vilivyopo kwenye programu ya V.O.I.C.E.

2) Viwango vya utangazaji vilivopo kwenye programu ya wakulima ya F.A.I.R.

3) Andiko la kusudi la programu au kipindi lenye mambo matatu ambayo huelezea:

– Lengo la kipindi,

– Walengwa na

– Shughuli zitakazo fanyika ili kufikia lengo kuu.

Andiko la kusudi la kipindi linatakiwa kua fupi kwa kadri iwezekanavyo, ili kila mtu anayehusika na kipindi hicho kuweza kukumbuka na kutekeleza.

Hapa kuna andiko la programu ya wakulima kulingana na viwango vilivyoko kwenye programu ya wakulima ya VOICE :

“Wakulima hodari!” wanasaidia wakulima wke kwa waume wa Neruda kuwa wakulima wenye mafanikio.

Andiko hili:

– hutoa taarifa inayohitajika na wakulima na kwa wakati sahihi,

– huwapa wakulima fursa ya kujadili masuala muhimu kuhusu kilimo, na

– inasaidia wakulima ambao hutumia mbinu mpya wanazoamini zitaboresha kilimo chao.

gac-logoMradi uliofanyika kutokana na msaada wa kifedha kutoka Serikali ya Canada kupitia Global Affairs Canada (GAC)

Chanzo hiki cha taarifa kimefadhiliwa na Shirika la Rockefeller kupitia mradi wake wa YieldWise.