Mwongozo kwa watangazaji kwa magonjwa ya mifugo

Mifugo na ufugaji nyuki

Backgrounder

Kuna aina nyingi sana za magonjwa ya mifugo ambapo kwa mtu asiye mtaalam wa mifugo ni vigumu kufahamu. Makala hii hutoa mambo machache ya msingi mnamo kumi na mbili kuhusu magonjwa muhimu zaidi ya mifugo na yanayoenea. Maelezo haya ni ya msingi, lakini yanaweza kukusaidia kuamua magonjwa ya kuzingatia wakati wa kubuni kipindi cha redio. Kuandaa vipindi husika kwa wakulima wasikilizaji wako, utahitaji kufanya utafiti mdogo wa ndani. Kufahamu ni nini magonjwa makubwa sana ya mifugo katika eneo lako sasa na ambayo inaweza kuwa tatizo katika siku zijazo. Ongea na wafugaji, wanasayansi, madaktari wa mifugo na wafanyakazi wa ugani wa kilimo. Ikiwa unaweza ukapata mtandao, angalia tovuti zilizotajwa mwishoni mwa makala hii. Usisahau kwamba magonjwa mengi muhimu ya mifugo yanaweza kuambukizwa kwa wanadamu, ikiwa ni pamoja na homa ya Bonde la ufa, kichaa cha mbwa na kimeta. Kwa hiyo kumbuka kuingiza masuala ya afya ya binadamu wakati unapoandaa kipindi chako


Homa ya nguruwe wa Afrika:  Wanyama walioambukizwa na Virusi vya homa ya Nguruwe za kiafrika hujumuisha nguruwe, ngiri, nguruwe pori, na nguruwe ulaya. Ugonjwa huu unaweza kuambukizwa kwa njia nne tofauti. Kwanza, pale mnyama mgonjwa anapoweza kugusana moja kwa moja na mnyama mwenye afya. Pili, wanyama wanapoweza kula nyama iliyoambukizwa. Tatu, homa ya nguruwe za Afrika inaweza kuambukizwa na aina fulani za kupe. Nne, inaweza kusafirishwa na vitu vya kimwili kama vile magari, malori, zana na nguo.

Ambapo magonjwa hutokea: Kusini mwa Afrika Jangwa la Sahara na sehemu kadhaa za Ulaya Kusini.
Kuzuia na Matibabu: Hakuna chanjo au tiba.
Dalili: Homa, uwekundu wa ngozi, upungufu wa hamu ya kula, ulegevu, kuongezeka kwa mapigo ya moyo na kupumua haraka, kutapika, kuhara, kutokwa kwa machozi, utoaji mimba kwa wenye mimba.
Kiwango cha vifo: Katika nguruwe za kufugwa ndani, karibu ni 100%.


Kichaa cha ng’ombe (BSE)  BSE huathiri ng’ombe wa kufugwa ndani na aina nyingi za ng’ombe za mwitu kama vile nyala, zaidi kudu na swala aina ya choroa. Tofauti za ugonjwa huo pia unaweza kuwa katika wanyama jamii aina ya paka wa ndani na wa pori kama vile duma, puma, paka pori na simbamarara. Wanyama hawa wanapata ugonjwa wa kichaa BSE kwa kula nyama iliyoambukizwa au mlo wa mfupa. Inaaminika kwamba wanadamu pia wanaweza kuupata ugonjwa huo kwa kula nyama iliyoambukizwa.

Ambapo magonjwa hutokea: Uingereza na nchi zilizopokea bidhaa za nyama zilizoambukizwa kutoka Uingereza.
Kuzuia na matibabu: Hakuna chanjo au tiba.
Dalili: Wasiwasi, kuongezeka kwa mshutuko, au unyogovu. Usikivu wa ngozi kuongezeka na machozi ya ghafla. Kupatwa kwa mshutuko wa misuli, kutetemeka au kutenganishwa kwa ukandamizo wa misuli.


Kiwango cha kifo: Kipindi cha kuongezeka kwa ugonjwa huu kinaweza kufikia miaka miwili, lakini mara baada ya dalili kutokea, wanyama wote walioambukizwa watakufa kutokana na matatizo.
Nimonia ya ng’ombe inayoambukiza (CBP)

Ng’ombe, zebu na nyati zinaweza kuambukizwa na CBP. Inaambukizwa kwa njia ya mkojo, mate au kwa njia ya hewa kwa majimaji kutoka kwa wanyama wanaokohoa, wakati mwingine kwa umbali wa kilomita kadhaa. Mama pia anaweza kuwaambukiza watoto wake. Wanyama wanaweza kuwa wabebaji wa viini hivyo bila kuonyesha dalili.

Ambapo magonjwa hutokea: Yanaenea Afrika na huwasilisha kusini mwa Ulaya, Mashariki ya Kati na sehemu za Asia.
Uzuiaji na matibabu: Chanjo yenye ufanisi hutumika sana. Hakuna matibabu madhubuti. Kiuavijasumu haifai na haipaswi kutumiwa kabisa.
Dalili: Homa ya wastani na kupumua kwa kubanwa sana na mapafu. Kuhemahema, tabia ya muonekana na mkao (kisigino kugeuka, mgongo kupinda, kichwa kuwa kubwa), na kikohozi (wakati wa kwanza ni kavu, kidogo, na isiyofaa, kuwa na unyevunyevu). Wakati mnyama anaposimama au baada ya zoezi, hupumua kwa shida na utamsikia akihema kwa kukoroma. Ng’ombe anaweza kuwa na ugonjwa wa yabisi kavu na uvimbe katika viungo.


Ugonjwa wa miguu na mdomo (FMD)  Ugonjwa wa FMD huathiri wanyama mbalimbali ikiwa ni pamoja na ng’ombe, zebu, nyati wa kufugwa, yaki, kondoo, mbuzi, nguruwe, nguruwe pori, na popo. Ngamia, Ilama, na vikuna ni rahisi kuathiriki sana. Wanaweza kuambukizwa kwa kuwasiliana moja kwa moja na wanyama walioambukizwa, au kwa kugusana na pia kugusa nguo za binadamu, magari, zana za kilimo au vitu vingine visivyo hai vyenye kubeba virusi hivyo. Virusi hivyo vinaweza kusafiri hadi kilomita 60 juu ya ardhi na eneo la kilomita 300 katika bahari.

Ambapo ugonjwa hutokea: Katika Asia yote, Afrika, Mashariki ya Kati na Amerika ya Kusini, na kuzuka mara kwa mara katika maeneo mengine, k.m., Ulaya.
Kuzuia na matibabu: Wanyama wanaoambukizwa kirahisi wanapaswa kupewa chanjo. Chanjo mbili zilizotolewa kwa mwezi mmoja zinatoa angalau miezi 6 ya kinga. Katika maeneo magumu, chanjo inashauriwa kufanyika kila baada ya miezi sita. Kipaumbele na tahadhari lazima itolewe katika usahihi wa chanjo ya ugonjwa huo katika eneo husika.

Dalili:

Ngombe: Homa, kutetemeka, kupungua kwa maziwa, midomo kugongana, kutafuna meno, kutokwa mate mengi mdomoni, kupata ulemavu, kupigapiga chini kwa miguu au kupiga mateke ya miguu. Mnyama kwa ujumla huweza kupona ndani ya siku 8-15.
Mbuzi, kondoo na nguruwe: hupata vidonda au majeraha ya miguu.
Viwango vya kifo: kiwango ni kidogo kwa wanyama wenye umri mkubwa, lakini vifo ni vingi katika wanyama wenyeumri mdogo.


Ugonjwa wa kuhara, vidonda mdomoni na nimonia (PPR)  Mbuzi na kondoo ni wanyama wanaoathirika mara kwa mara na ugonjwa huu wa virusi, ingawa ng’ombe na nguruwe wanaweza kuambukizwa bila kuonyesha dalili za wazi. Inaambukizwa kwa njia ya maji maji ya mwili – mkojo, mate, nk – kutoka kwa wanyama walioambukizwa, na mara nyingi huzuka wakati wa mvua au msimu kame wa baridi.

Homa ya Bonde la Ufa  Wanyama wengi wanaweza kuambukizwa na ugonjwa huu wa virusi, ikiwa ni pamoja na ng’ombe, kondoo, mbuzi, ngamia, panya, wanyama wa porini, nyati, swala, na nyumbu. Wanadamu wanaweza pia kupata ugonjwa huu. Inaambukizwa na aina nyingi za mbu. Wanadamu wanaweza pia kuambukizwa kwa kuwashika na kuwahudumiaa wanyama walioambukizwa na pamoja na nyama zao.

Ambapo ugonjwa hutokea: Afrika Kusini mwa Jangwa la Sahara.
Kuzuia na matibabu: Kuna chanjo yenye ufanisi.

Dalili:

Ndama: Homa na unyong’ovu.
Ng’ombe wazima: Homa, mate nyingi, udhaifu, kuhara, kupunguza mavuno ya maziwa. Kiwango cha kuharibika mimba inaweza kufikia 85% katika mifugo.
Mwanakondoo: Homa, udhaifu, kifo ndani ya masaa 36.
Kondoo na mbuzi: Homa, kutokwa kwa damu puani, kutapika.
Watu: Dalili zinazofanana na mafua. Kupona ndani ya siku 4-7. Matatizo ni pamoja na ugonjwa wa jicho na upofu, na magonjwa kadhaa makubwa ambayo yanaweza kusababisha kifo.

Kiwango cha vifo:

Ng’ombe: Ni kiwango cha chini kwa ng’ombe wazima (chini ya 10%), kiwango cha juu kwa ndama (10-70%).
Ndama wa umri chini ya wiki moja: hadi 90%; zaidi ya wiki moja ya umri – hadi 20%.
Kondoo wazima: Katika kondoo jike wajawazito, mimba inaweza kufikia 100% na vifo vinaweza kufikia 20-30%.


Sotoka  Sotoka ni ugonjwa wa virusi unaoathiri ng’ombe, zebusi, nyati na aina nyingi za wanyama wa mwitu ikiwa ni pamoja na nyati wa Afrika, pofu, tandala, nyumbu, swala, paa, nguruwe pori, na twiga. Pia huathiri kondoo, mbuzi, na nguruwe (hususan nguruwe za Asia). Inaambukizwa kupitia mawasiliano ya moja kwa moja au kuwashika moja kwa moja au kuwa karibu na wanyama walioambukizwa.

Ambapo ugonjwa huu hutokea: Afrika ya Kati, Mashariki ya Kati, kusini magharibi na Asia ya kati.

Dalili:

Ng’ombe: Kwa siku ya kwanza hadi ya 2-3 kuna homa na unyong’ovu, kupunguzwa kwa kucheua, kuongezeka kwa kupumua na kiwango cha mapigo ya moyo kuongezeka, kujaa makohozi na kutokwa na mate mengi wakati wote. Wakati homa ikipungua, kuna kuhara kwa damu, kuishiwa maji mwilini, maumivu ya tumbo, udhaifu na kifo ndani ya siku 8-12. Katika baadhi ya wanyama wenye umri mdogo, homa kubwa na labda makamsi mengi ambayo hufuatwa na kifo baada ya muda mfupi.
Kwa kondoo na mbuzi: homa na kuhara.
Katika nguruwe: homa, ugonjwa wa macho wa kikope na kifo.
Kuzuia na matibabu: Chanjo hutoa kinga ya muda mrefu na labda ya maisha, lakini kupewa chanjo tena ya kila mwaka inapendekezwa ili kuhakikisha kuwa asilimia kubwa ya wanyama katika eneo fulani hupewa chanjo. Hakuna matibabu.
Kiwango cha kifo: Ni kikubwa na aina fulani ya ugonjwa huo, hutofautiana na mengine.


Kimeta  Kimeta ni ugonjwa wa bakteria ambao huathiri hasa ng’ombe, kondoo, mbuzi, farasi, nguruwe na wanadamu, ingawa jamii ya wanyama wote wanaweza kuupata kwa kiwango kikubwa zaidi. Inaambukizwa kwa njia ya maji maji, wadudu, wanyama wa mwitu na ndege, na vinyesi vya wanyama walioambukizwa. Wanyama huambukizwa wakati wanapokula chakula au maji yaliyokwisha ambukizwa. Mifugo nyingi huambukizwa mara nyingi wakati wa hali ya ukame au kavu wakati wanapaswa kula majani mafupi na kusababisha kula na udongo na hapo hula bacteria au kufuatia mafuriko wakati bacteria wanaposafirishwa na kubakia juu kwenye mashina ya majani. Ugonjwa unaweza pia kuambukizwa wakati wanyama wanapogusana na milo ya mifupa, mkojo na vinyesi zilizoambukizwa, na tishu na maji ya mwili wa mizoga iliyoambukizwa. Wanadamu wanaambukizwa hasa wakati bacteria kutoka kwa mnyama aliyeambukizwa anapowasiliana moja kwa moja na eneola wazi kwenye ngozi, kama vile sehemu iliyokatwa. (Kumbuka: aina ya kimeta ambayo imesababisha wasiwasi kwa ugaidi kwa kutumia silaha za kibayolojia ni aidha kimeta ya mapafu – maambukizi kwa njia ya kuvuta hewa au kimeta ya ngozi iliyowazi kupitia sehemu iliyokatwa au kidonda kwenye ngozi.)

Ambapo ugonjwa hutokea: Ulimwenguni kote.

Dalili:

Ng’ombe na kondoo: homa, kutetemeka kwa misuli, shida ya kupumua, na kuchanganyikiwa. Kifo hutokea ndani ya masaa 24 ya kuambukizwa.
Farasi na wanyama wanaohusiana: Kama kutokana na ulaji kwa njia ya mdomo, sawa na ng’ombe. Ikiwa kutokana na kung’atwa na wadudu, uvimbe wa moto, wenye maumivu makali chini ya ngozi kwenye eneo lililong’atwa ambalo huenea kwenye koo, shingo ya chini, tumbo, viungo vya mwili na vidonda vya katika tezi. Homa kali na maumivu makali au ugumu katika kupumua inawezekana.
Nguruwe, mbwa na paka: uvimbe wa shingo husababisha maumivu makali katika kupumua, na shida ya kumeza. Kunaweza kuwepo na uvimbe katika tumbo.
Kuzuia na matibabu: Kuna chanjo yenye ufanisi.
Kiwango cha kifo: Kutoka 2-80%, kulingana na aina za bakteria na njia ya maambukizo.


Kichaa cha Mbwa  Kichaa cha mbwa kinatokana na maambukizo ya virusi ambayo yanaweza kuathiri wanyama wote, ikiwa ni pamoja na wanadamu. Inaambukizwa kwa mawasiliano ya karibu na mate kutoka kwa wanyama walioambukizwa, kwa kung’atwa, mikwaruzo, kulambwa juu ya ngozi na utando telezi wa maji maji.

Ambapo ugonjwa hutokea: Ulimwenguni kote.

Dalili: Dalili za awali zinahusisha mifumo ya kupumua, tumbo na / au mfumo wa fahamu. Katika hatua ya dalili za baadaye, kunaweza kuwa na uchangamfu kupita kiasi (hasira ya ghadhabu kali) au kupooza (kuzubaa kwa ubongo). Katika aina za ukichaa zile za hasira na za ubongo, kuna maendeleo ya kukamilisha kupooza na kupelekea ulemavu ikifuatiwa na kupoteza fahamu na kifo. Bila kujali sana, kifo hutokea wakati wa siku saba za kwanza za ugonjwa kuonekana. Huduma lazima zitolewe haraka kwa wanyama wote wa mwitu, kama wengine wanaweza kuwa wanabeba virusi na hawaonyeshi dalili. Toa taarifa ya kuumwa na uwezekano wa kumwelezea daktari na uangalie kwa makini wanyama wote ambao walisababisha.

Kuzuia na matibabu:

Watu: Osha na ondoa uchafu katika jeraha au kwa kutumia sabuni na maji, sabuni au maji masafi, ikifuatiwa na matumizi ya ethanoli, na tincha au suluhisho la maji la iodini. Maafisa wa afya ya umma wanapaswa kutoa chanjo kwa aina fulani za uwazi. Tiba ya kupambana na tetanasi na madawa mengine wakati mwingine hutolewa kwa maambukizi ya pili. Mara nyingi mbwa na paka ni vyanzo vikubwa kwa maambukizi ya kichaa cha mbwa, mbwa wote na paka katika maeneo ambako kichaa kimeingia kwa wakati huo inapaswa kupatiwa matibabu haraka. (Kichaa hiki mara nyingi kwa kawaida huuwa wanyama.)


Malale (Maambukizi ya mbung’o)  Malale ni ugonjwa wa vimelea unaoathiri wanyama wengi wa mamalia, lakini ni mbaya zaidi kwa ng’ombe. Inaambukizwa na jamii ya inzi aina ya mbung’o, na kwa kiwango kidogo, na inzi wengine wanaouma. Wanadamu wanaweza pia kuathirika, kama kuumwa kwa aina fulani za nzi-mbung’o zinaweza kusababisha ugonjwa wa kulala yaani malale.

Ambapo ugonjwa hutokea: Afrika Kusini mwa Jangwa la Sahara, Amerika ya Kusini.
Dalili: joto kuwa juu, udhaifu, tezi kuvimba, utando wa kijivu, kupoteza hamu ya chakula, kupoteza uzito, utoaji mimba na utasa kwa wanyama wa kiume na wa kike.
Kuzuia na matibabu: Kuzuia ni kwa udhibiti wa kuruka kwa mbung’o. Dawa fulani pia hufanya kazi katika kupunguza dalili, lakini lazima itumike kwa makini kulingana na maelekezo.
Kiwango cha vifo: Katika matukio ya hali mbaya katika wanyama wanaocheua, kiwango cha vifo ni cha juu sana. Katika kesi chache mbaya sana ni ya chini lakini wanyama wanaweza kurudiwa tena.


Brusela  Brusela ni ugonjwa wa bakteria unaojulikana kama mimba ya kuambukiza. Inaathiri wanyama mbalimbali, ikiwa ni pamoja na kondoo, mbuzi, ng’ombe, nguruwe, elki, nguruwe pori, mbwa, na wanadamu. Inaambukizwa kwa kugusana moja kwa moja na wanyama walioambukizwa au kwa kuwasiliana na vijusi au viini tete zilizoharibiwa. Inakuja kutoka katika uzazi wa wanyama walioambukizwa, wakati wa kujamiiana, kwa njia ya maziwa ya uzazi na uwezekano kupitia maambukizi ya hewa. Wanadamu wanaweza kupata ugonjwa huo wakati wa kuwashika wanyama walioambukizwa au bidhaa za wanyama, ikiwa ni pamoja na maziwa. Aina ya ugonjwa wa mwanadamu inaitwa homa isiyofaa.

Ambapo ugonjwa hutokea: Ulaya ya Kusini na Mashariki, Afrika, Kusini na Amerika ya Kati, Asia, Caribbean, na Mashariki ya Kati.
Dalili:
Wanyama: Hakuna njia nzuri ya kuchunguza wanyama walioambukizwa kutokana na kuonekana kwao. Ishara zilizo wazi zaidi katika wanyama wajawazito ni utoaji mimba, kuzaliwa kwa ndama dhaifu, na utoaji wa ute ukeni. Ishara nyingine ni pamoja na kupungua kwa uzazi na viwango vya ubebaji wa mimba, kuhifadhiwa baada ya kuzaa na maambukizi ya kizazi, na viungo kushikwa na baridi yabisi.
Watu: Dalili ikiwa ni pamoja na homa, jasho, maumivu ya kichwa, maumivu ya mgongo, na udhaifu wa mwili. Inaweza pia kusababisha maambukizi makubwa ya mifumo ya ufahamu ya kati au ya kifua cha moyo, na homa ya muda mrefu, maumivu ya viungo, na uchovu.
Kuzuia na matibabu:
Wanyama: Hakuna matibabu madhubuti. Chanjo hutoa ulinzi zaidi.
Watu: Tiba ya madawa. Uwokozi inaweza kuchukua wiki chache kwa miezi kadhaa.
Kiwango cha vifo:
Wanyama: kiwango cha juu cha utoaji mimba. Kiwango cha kifo cha chini kwa wanyama waliokomaa.
Watu: chini ya 2%.


Ndigana  Huu ni ugonjwa wa vimelea unaoambukizwa na aina tatu za kupe. Na hasa huathiri ng’ombe.

Ambapo ugonjwa huu hutokea: Afrika ya Kati na Mashariki.
Dalili: homa, anemia, safura, kupoteza uzito, kupungua kwa maziwa, tezi za limfu, ugumu katika kupumua, utoaji mimba na kifo.
Kuzuia na Matibabu: Kuzuia ni kwa udhibiti wa kupe, kwa kawaida kwa matumizi ya dawa za kuua wadudu. Chanjo hutoa matibabu, ingawa wanyama walio chanjwa wanaweza kuwa wabebaji wa ugonjwa.
Kiwango cha kifo: Juu katika ng’ombe zisizopata chanjo.

Acknowledgements

Shukrani

Imetolewa na Vijay Cuddeford, Toronto, Kanada.

Imepitiwa na Terry S. Wollen, DVM, Mratibu wa Afya ya Wanyama, shirika la kimaifa la Heifer.

Anwani ya mahali: Heifer ya Nepal, Arun Tole, Satbobato, Lalitpur 15 Nepal.

URL yatovuti: www.hpinepal.org.np

Information sources

Chanzo cha habari

Rabies, World Health Organization Fact Sheet No. 99, June 2001. World Health Organization, Marketing and Dissemination, CH-1211 Geneva 27, Switzerland. Tel: +41 22 791 24 76, Fax: +41 22 791 48 57, URL: http://www.oms.ch/inf-fs/en/fact099.html

Anthrax, Veterinary Services Factsheet, October 2001. United States Department of Agriculture. For copies phone, (301) 734-7799. URL: http://www.aphis.usda.gov/oa/pubs/anthrax.html

Catalogue of diseases, Office International Des Epizooties, 12 rue de Prony 75017 Paris, France. Tel: +33 (0)1 44 15 18 88, Fax: +33 (0)1 42 67 09 87, E-mail: oie@oie.int, URL: www.oie.int/eng/maladies/en_alpha.htm

Manual of standards for diagnostic tests and vaccines, 4th edition, 2000. Office Internationale Des Epizooties, 12 rue de Prony 75017 Paris, France. Tel: +33 (0)1 44 15 18 88, Fax: +33 (0)1 42 67 09 87, E-mail: oie@oie.int Document available on-line at: http://www.oie.int/eng/normes/mmanual/A_summry.htm

Facts about brucellosis, United States Department of Agriculture, Animal and Plant Health Inspection Service, Veterinary Services, National Animal Health Programs, 4700 River Road, Unit 43, Riverdale, MD 20737-1231. Tel: (301) 734-6954, URL: http://www.aphis.usda.gov/oa/brufacts.html

Ticks and tick-borne diseases. Food and Agriculture Organization of the United Nations, Viale delle Terme di Caracalla, 00100 Rome, Italy. Tel: (39 6) 570 52267, Fax: (39 6) 570 56799, E-mail: Farming-Systems@fao.org, URL: http://www.fao.org/ag/AGA/AGAH/PD/pages/

Tafsiri ya hati hii inafadhiliwa na ELANCO ANIMAL HEALTH